Maelezo zaidi - Kilimoznz.or.tz
Maelezo zaidi - Kilimoznz.or.tz
Maelezo zaidi - Kilimoznz.or.tz
- TAGS
- maelezo
- zaidi
- kilimoznz.or.tz
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
UZINDUZI WA KILIMO CHA MPUNGA KWA MSIMU

WA MWAKA 2011/2012 CHEJU

Mpunga ni miongoni mwa mazao yanayolimwa sana hapa visiwani, mpunga ukiwa tayari shamban,

huvunwa, huanikwa, hupigwa/hupukuchuliwa, hupetwa na kukubolewa ili kupatikana mchele ambao

tumika kwa mapishi ya vyakula aina mbali mbali kama vile wali, pilau, biriani, mikate na chila. Wakaazi

wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba hupoendelea kula wali ambao unatokana na mpunga.

Licha ya kua na mazao mengi ya kibiashara pamoja na chakula lakini moja ya chakula ambacho

kinawavutia wakaazi wengi wa visiwa hivi ni wali.

Wakulima wa visiwa vya Unguja na Pemba wanajishughulisha na kilimo cha mpunga kwa miaka mingi kwa

lengo la kujipatia chakula chao, ni dhana ambayo ilijengeka miongoni mwa wakulima wengi

waliojishughulisha na kilimo hicho.

Katika kukiinua kilimo hicho cha mpunga Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kufanya mabadiliko

makubwa kwa kukifanya kilimo cha mpunga

kiwe cha kibiashara kwa kuwaekea

miiundombinu bora katika maeneo ya

uzalishaji, kutoa ruzuku kwa pembejeo

muhimu za kilimo na kuwapatia wakulima

taaluma bora za uzalishaji ili kufikia lengo

lililokusudiwa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza

la Mapinduzi Mhe. Dr. ALI MOHAMMED

SHEIN aliyabainisha hayo huko Cheju,

Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja

wakati wa uzinduzi wa msimu wa mpunga

kwa mwaka 2011‐2012.

Shughuli ambayo ilihudhuriwa na viongozi

wengine wa Serikali wakiwemo Wakuu wa

Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Waziri wa

Miudombinu, Kaimu Waziri wa Kilimo,

Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Mkuu,

Wakurugenzi na maafisa kutoka Wizara ya

Kilimo pamoja na wakulima mbalimbali wa
kilimo cha Mpunga.

Amesema kuwa Serikali imeamua kufanya mabadiliko ya kilimo hicho kuwa cha kibiashara kutokana na

matumizi bora ya nyenzo za kilimo zitakazotumiwa na wakulima wake.

Amafahamisha kua kilimo ndio njia pekee ya kuwapatia wananchi chakula cha uhakika pia ndio jambo

ambalo Ulimwengu mzima hivi sasa unalitilia mkazo, hivyo hatuna budi kuongeza nguvu zaidi katika kilimo

chetu ili tuweze kulima kwa tija na kilimo chetu kiwe cha kisasa.

Amesema kupitia Shirika la Chakula Duniani (FAO) pamoja na mashirika mengine ya maendeleo likiwemo

IFAD yanaendelea kuzishajiisha nchi zote duniani ziweze kuzalisha mazao ya chakula kwa wingi na

kujitosheleza kwa chakula.

Dr. Shein alieleza kua hali ya dunia hivi sasa imebadilika kutokana na matatizo ya kiuchumi jambo ambalo

linasababisha kupanda kwa bei za vyakula mara kwa mara na kufanya hali ya thamani ya fedha

kutotabirika.

Dr. Shein alisema kua matarajio ya Serikali ni kukibadilisha kilimo cha mpunga na kulifanya bonde la

mpunga la Cheju kuwa la kisasa katika kilimo cha mpunga kwa kuzilima hekta zote 3000 zilizopo ili liweze

kuchangia upatikanaji wa chakula kwa Zanzibar yote. Hali ambayo itaweza kulibadilisha bonde hilo na

kuwa tofauti na ile ya zamani.

Amefahamisha kua kutokana na hatua hiyo lengo na matarajio kwa msimu wa 2011/1212 ni kupata tani

5000 za mpunga katika bonde hilo linaweza kufikiwa kutokana na juhudi zinazochukuliwa na Serikali

kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili kwani mipango yote ya kuwapatia wakulima wake huduma bora za

kilimo imeshapangwa.

Dr Shein amewataka wakulima wa bonde la Cheju kupanda mbegu ya aina moja ili iwe rahisi wakati wa

mavuno sambamba na utumiaji wa mbegu bora, mbolea na taaluma bora za uzalishaji.

Pamoja na uzinduzi huo Dr. Shein alitoa pongezi za dhati kutokana na juhudi kubwa zilizochukuliwa na

mafundi wa matrekta wa Unguja na Pemba za kufanya matengenezo kwa wakati. Jumla ya matrekta 21

yalifanyiwa matengenezo yakiwemo 14 Unguja na 7 Pemba.

DR. Shein pia alivipongeza vikundi vya wakulima vya bonde la Cheju kwa kuchangia asilimia 80 ya gharama

na kupelekea kuanza kulimiwa katika bonde lao kwa wakati.
Akielezea juu ya mikakati iliopo ya barabara ya Jendele‐Cheju‐Unguja ukuu kaibona, Waziri wa

Miundombinu na Mawasliano Mhe. Hamad Masoud alieleza kua utaratibu wa ujenzi huo unafanyiwa kazi

na hivi karibuni watapatikana makandarasi wa kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Nae Kaimu Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban aliwataka wakulima wa bonde

hilo kuiunga mkono Wizara ya Kilimo na Maliasili kutokana na jitihada zake inazozichukua katika kuwasidia

wakulima hao.

Akitoa ufafanuzi juu ya maendeleo ya kilimo kwa msimu huu Naibu Katibu Mkuu (Kilimo) ndugu Juma Ali

Juma alisema kuwa wizara imeshafanya maandalizi ya kuagiza mbegu ya kutosha kutoka Tanzania Bara

kwa msimu huu kwa ajili ya kugaiwa kwa wakulima kwa sasa tayari imeshanunua tani 141 za mbegu

sambamba na kufanya maandalizi ya mbegu ya NERICA.

Amaefahamisha kua kwa mwaka ujao 2012 eneo lote la bonde hilo litakua la kilimo cha umwagiliaji maji

ambapo tayari wataaalamu kutoka Korea washawasili.

Nd. Juma amesema kua

katika kukiimarisha kilmo

hicho Wizara imeamua

shughuli zote za kilimo

zitasimamiwa na wakulima

wakulima wenyewe kupitia

Jumuiya zao. Jumla ya vituo

20 vimetegwa Unguja na

Pemba. Aliendelea kueleza

kuwa Wizara imesamua

kuliteua bonde la cheju kuwa

eneo tengefu la mbegu ili

liweze kuleta tija na manufaa

kwa Taifa.

Nao wakulima wa Zanzibar

katika risala yao walieleza

kufarijika kwao na

kumpongeza Dr.Shein

kutokana na jitihada anazozichukua katika kukipa kipaumbele kilimo cha mpunga na kuweza kushiriki

katika shughuli mbalimbali za kilimo.

Aidha walitoa pongezi kutokana na bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka 2011/2012 ilivyowaona wakulima

kwa kuwapatia ruzuku ya pembejeo kwa asilimia 50.

Wakieleza changamoto zinazowakabili katika ukulima wa mpunga ni pamoja na tatizo la ujenzi kwenye

mabonde ya mpunga na wanaiomba Serikali kufuatilia kwa kina suala hilo ikiwa ni pamoja na kutunga

sheria itakoyozuia ujenzi katika mabonde ya mpunga.