20.01.2013 Views

Uk. 4 Uk. 18 Uk. 14 - MVIWATA

Uk. 4 Uk. 18 Uk. 14 - MVIWATA

Uk. 4 Uk. 18 Uk. 14 - MVIWATA

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Uk. 4

Toleo NO. 039 Julai –Septemba 2011 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937

Wakulima wapongeza MVIWATA kwa

kuhabarisha wakazi wa vijijini

Uk. 14

Maonesho ya NaneNane 2011

Uk. 18

Kijana mbunifu atengeneza mitambo ya radio

kunufaisha wanakijiji

Toleo NO. 039

Julai Septemba 2011

Bei Shs. 500/=

ISSN 0856-5937

WAHARIRI

Susuma Msikula Susuma

Stephen Ruvuga

BODI YA MVIWATA

Mwenyekiti – Yazid Makame

Makamu Mwenyekiti – Lydia Ruliho

Katibu - Stephen Ruvuga-

(Mkurugenzi Mtendaji)

Mweka Hazina - Grace Runkulatile

WAJUMBE

Cosma Bulu

Sylvester Yatuba

Joseph Kilowoko

Samweli Maseke

Julius Mbago

Habibu Simbamkuti

MSHAURI WA MVIWATA

Prof. Amon Mattee

LINATOLEWA NA

KUSAMBAZWA NA

Mtandao wa Vikundi vya

Wakulima Tanzania (MVIWATA)

S.L.P 3220 Morogoro, Tanzania

Simu: 023 261 41 84

Faksi: 023 261 41 84

Barua pepe: info@mviwata.org,

mviwata@morogoro.net

Tovuti: www.mviwata.org

MICHORO

Godwin Chipenya

USANIFU NA

UCHAPISHAJI

PENplus Ltd – 022 2182059

Uk. 4

Toleo NO. 039 Julai –Septemba 2011 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937

Wakulima wapongeza MVIWATA kwa

kuhabarisha wakazi wa vijijini

Uk. 14

Maonesho ya NaneNane 2011

Uk. 18

Kijana mbunifu atengeneza mitambo ya radio

kunufaisha wanakijiji

Picha ya Jalada:

Bw. Benjamini Nziku mkulima wa

kijiji cha Lusala kata ya Lupanga

wilayani Ludewa akipata habari

kupitia gazeti la wakulima la

Pambazuko. b

Tahariri

Habari za vijijini zipewe

kipaumbele

Ingawa juhudi na mchango wa jamii za vijijini nchini Tanzania

ndiyo vinavyoiendeleza Taifa, habari za vijijini haziandikwi kwa

umuhimu huo.

Mara nyingi, habari za vijijini zinazopewa nafasi kwenye

vyombo vya habari ni zinazohusu maafa, kesi, vimbwanga na hotuba

za viongozi wanapotembelea maeneo hayo.

Wanahabari wanafanya kazi kubwa ya kuuelimisha umma, hata

hivyo kwa sehemu kubwa habari hizo zimekuwa ni zile zinazohusu

watu wa mijini.

Toleo hili linalozungumzia habari za vijijini ni sehemu ya

utekelezaji wa ajenda ya upashanaji habari inayotekelezwa na

MVIWATA kwa muda mrefu sasa.

Tunafahamu kwamba pamoja haya umuhimu wa upatikanaji wa

habari kwa watu wa vijijini, ziko changamoto kadhaa zinazokwamisha

ufanisi wake.

Miongoni mwa changamoto hizo ni ukosefu wa vitendea

kazi ikiwemo usafiri, kamera na vinasa sauti ambapo hata

waandishi wachache wenye nia ya kwenda kukusanya habari vijijini

wameshindwa kufanya hivyo kwa kukosa usafiri na wengine kuishia

kutegemea usafiri wa viongozi wanapotembelea maeneo ya vijijini.

Kulingana na kubanwa na ratiba za viongozi hao, waandishi hawawezi

kukusanya habari nzuri zenye kuchochea maendeleo ya vijijini zaidi

ya kuishia kuandika hotuba na maagizo ya viongozi.

Changamoto nyingine ni ya waandishi wa habari kukosa

taaluma ya kutosha yenye kuwawezesha kudadisi na kuibua kero na

changamoto halisia za vijijini na siyo vimbwanga.

Tunaamini ziko changamoto nyingi na lengo letu siyo kuziainisha

zote isipokuwa tunawakumbusha wadau wa sekta ya habari kuwa

vijijini ndiko kwenye chimbuko la wazalishaji na kwamba hatupaswi

kuwatenga.

Tunashauri kuwepo na jitihada za makusudi za kutatua

changamoto hizi na vilevile kuwe na juhudi za kuhimiza vyombo

vya habari kuzipa kipaumbele habari za vijijini. Ni wakati muafaka

ambapo

Tunawakumbusha wana habari juu ya umuhimu wa kuzingatia

maadili ya taaluma ya uandishi wa habari kwa kuandika habari

zilizofanyiwa utafiti wa kina na kuhakikisha jamii zote vijijini na

mijini wananufaika na huduma hii muhimu.

Tusaidie kuchochea maendeleo vijijini kwa kuhakikisha

tunawapatia habari za kutosha na zilizofanyiwa utafiti.

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Upatikanaji wa habari vijijini,

kichocheo cha maendeleo?

Na Goodness Mrema, Morogoro

Kutokana na kupiga hatua

za kimaendeleo katika

teknolojia hasa ya habari,

wigo wa upatikanaji wa habari

hivi sasa umepanuka ukilinganisha

na miaka ya nyuma hasa wakati

tunapata uhuru.

Hivi sasa watu wanauwezo

wa kutumia kompyuta na

simu za mkononi zenye

huduma ya intaneti na

kuweza kupata taarifa

mbalimbali zinazotokea

ulimwenguni kwa wakati

huo huo ama kulipia huduma

mbalimbali kama vile matibabu,

maji na umeme. Lakini pia wanaweza

hata kufanya manunuzi ya bidhaa

mbalimbali kupitia intaneti na hivyo

kupunguza gharama na muda na

kurahisisha biashara.

Hata hivyo mbali na kukua kwa

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

teknolojia ya habari, nchi za Kusini

mwa Afrika bado zinakabiliwa na

tatizo kubwa la kukosekana kwa

habari za umma hasa kwenye maeneo

ya vijijini ambazo ni muhimu kwa

wananchi kutoa maamuzi mbalimbali

ambayo ni sahihi kwa maisha yao.

Hata

radio za kijamii

zilizoanzishwa kwa lengo

la kuhudumia wakazi wa vijijini,

zimeacha misingi ya kuanzishwa

kwake na kuegemea zaidi

kutangaza mambo ya

mijini.

Bado

kuna changamoto zinazoikumba

sekta hii ya habari ikiwemo uhaba

wa upatikanaji wa habari sahihi

na zenye manufaa kwa baadhi ya

MADA MAALUM

maeneo hasa ya vijijini. Mfumo wa

upashanaji habari uliopo sasa siyo

wa kuridhisha kwani haumfikii kila

mwananchi wa kijijini mahali alipo.

Kwa mfano magazeti yanayofika

kwa nadra vijijini ndani yake yanakuwa

yamejaa habari zinazohusu vuguvugu

la maisha ya mjini. Habari hizo nyingi

ni zile zinazohusu malumbano na

siasa za chuki baina ya viongozi

wa vyama, foleni za barabarani,

michezo ambayo pengine mtu

wa kijijini hajawahi kuiona na

burudani kama vile miziki

na picha kubwa kubwa za

wasanii ambazo ki uhalisia

hazimuongezei tija mtu wa

kijijini katika harakati zake za

kupambana na umasikini kupitia

kilimo, ufugaji ama uvuvi.

Tunashuhudia ongezeko la

vyombo vya habari vya kielektroniki

kama vile radio na televisheni na

ukuaji wake kutoka kwenye mfumo

Endelea Uk wa 2

Mwekahazina wa MVIWATA Ruvuma Bibi Immaculata John akitekeleza shughuli za MVIWATA za kusambaza habari za wakulima kwa

wadau

1

MADA MAALUM

Upatikanaji wa habari vijijini

Inatoka uk. wa 1

wa analogia kwenda digitali.

Ongezeko na ukuaji wa

teknolojia bado hauwanufaishi

vya kutosha wakazi wa vijijini.

Kilichobadilika ni kuwepo kwa

usikivu mzuri wa matangazo ya

radio kwenye baadhi ya vijiji tofauti

na ilivyokuwa awali. Habari zenye

mlengo wa kuchochea maendeleo

vijijini bado hazipewi kipaumbele.

Hata radio za kijamii

zilizoanzishwa kwa lengo la

kuhudumia wakazi wa vijijini,

zimeacha misingi ya kuanzishwa

kwake na kuegemea zaidi kutangaza

mambo ya mijini.

Japokuwa televisheni na redio

zinajitahidi kurusha matangazo

yake na kuwafikia kwa wakati watu

wa vijijini, lakini bado habari zake

zinakosa mguso kwao, ingawa serikali

inajinadi kuwa matumizi ya mfumo

wa digitali yameongeza upatikanaji

wa habari maeneo ya vijijini.

Kwa ujumla habari zinazohusu

mafundisho ama mafanikio ya

wananchi vijijini haziandikwi wala

kusikika vya kutosha na kwamba

kuna haja ya kubadili mfumo

ili waandishi wa habari wapate

msukumo wa kuwafikia wananchi

vijijini na kuandika habari zao.

Siku hizi umekuja utaratibu

mpya wa upashanaji habari kupitia

mitandao mbalimbali ya kijamii

(tovuti, blogs, facebook, twitter)

ambayo kwa hakika mkulima au

mfugaji mdogo anayeishi kijijini

hafahamu hata jinsi ya kuitumia na

wachache wenye uelewa hawawezi

kuitumia kwa kukosa nishati ya

umeme.

Changamoto ya

miundombinu

Ziko sababu nyingi zinazotajwa

kuchangia habari kutowafikia watu

wa vijijini. Sababu mojawapo ni ubovu

wa miundombinu ya barabara katika

maeneo mengi ya vijijini ambako

kuna asilimia 80 ya Watanzania

wazalishaji wanaochangia pato la

taifa.

Kulingana na miundombinu

duni ya barabara zetu hasa maeneo

2

ya vijijini, ni vigumu kwa mwananchi

wa kijijini kupata gazeti kwa wakati

na kulisoma.

Wauzaji na wasambazaji wa

magazeti ya kila siku wanajikuta

wakishindwa kuyafikia maeneo hayo

kwa wakati. Kwa mfano gazeti la

kila siku linalosambazwa asubuhi

katika maeneo ya mijini huchukua

wakati mwingine siku mbili kufika

eneo la Mrimba Kilombero mkoani

Morogoro kutokana na barabara ya

kuelekea sehemu hiyo kuwa mbaya.

Huu ni mfano wa sehemu moja

iliyo katika mkoa jirani na mji ambapo

magazeti mengi huchapishiwa, swali

ni je vipi kwa watu waishio Kigoma

vijijini, Karagwe ama Murugwanza

huko Ngara, wao hulipata gazeti hilo

siku ngapi baada ya kuchapishwa?

Ukosefu wa nishati nalo ni tatizo

kubwa kwa wakazi wa maeneo ya

vijijini ambalo linazuia wananchi

wa vijijini kununua televisheni

au radio kwa sababu ya kukosa

nishati itakayowawezesha kuvitumia

vyombo hivyo.

Maisha magumu ya vijijini

yanayosababishwa na ukosefu wa

huduma muhimu za kijamii pia

yanadhoofisha kasi ya upatikanaji

wa habari vijijini. Kwa mfano

mtu anayesumbuliwa

na maradhi kwa

kukosa huduma

sahihi za

matibabu,

hawezi kukaa

na kusikiliza

radio huku

a k i g u g u m i a

kwa maumivu

makali. Mtu huyu

pia hawezi kutenga

fedha ya kununua gazeti

linalomfikia baada ya siku mbili

Akina mama wengi vijijini

wanakosa muda wa kusikiliza taarifa

za habari ama matangazo mengine

muhimu kwa kuwa muda ambao

radio na televisheni zinatangaza

taarifa za habari wao wanakuwa

kwenye shughuli za kupika, kutafuta

maji na kuni na shughuli za shamba.

Ukiachana na tatizo la

miundombinu duni, iko sababu

nyingine ya baadhi ya wananchi kukosa

mwamko wa kutafuta ama kutoa

habari. Wananchi kwenye baadhi ya

maeneo ya vijijini hawajaelimishwa

vya kutosha juu ya umuhimu wa

kutoa na kupokea habari kuhusiana

na masuala mbalimbali hivyo baadhi

yao kuona kwamba kununua gazeti

ama kununua televisheni ni kuwa na

matumizi ya anasa.

Habari zinachochea

maendeleo?

Wakazi wa vijijini wengi wao wakiwa

ni wakulima waliopata fursa ya

kuzungumzia hoja hii, walikiri kuwa

upatikanaji wa habari sahihi vijijini

umesaidia kuchochea maendeleo,

japokuwa kiwango cha upatikanaji

wake siyo cha kuridhisha.

Walieleza kuwa habari chache

zilizowafikia ziliwasaidia kupata

elimu ya kilimo bora, taarifa za

upatikanaji wa pembejeo, masoko,

mwelekeo wa hali ya hewa na

mwenendo wa uchumi na hali ya

kisiasa nchini pamoja na kufahamu

jitihada za maendeleo zinazofanywa

na makundi mbalimbali.

Mbali na

vyombo vya habari,

ziko njia nyingine za asili

zinazotumika kufikisha habari kwa

jamii kwenye maeneo ya vijijini ikiwemo

mikutano ya vijiji, kwenye nyumba

za ibada na kwenye mikusanyiko

kama vile sokoni na kwenye

minada.

Walisema habari hizo pia

zinawapatia uwanja mpana wa

mjadala na kubadilishana uzoefu

kuhusiana na masuala mbalimbali

yanayowakabili ikiwemo uwezo wa

kudai haki zao za msingi. Wanafahamu

mahali pa kupata mahitaji muhimu na

fursa zinazopatikana kwa ajili yao na

Endelea Uk wa 3

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Inatoka uk. wa 2

njia muafaka za kufikia suluhu kwa

changamoto zinazowakabili katika

shughuli zao.

“Suala la upatikanaji wa habari

linahusika zaidi na maisha ya kila

siku ya mwananchi. Ni suala la

maendeleo ya kila mwanadamu hapa

ulimwenguni, endapo wananchi hawa

wa vijijini watapata habari sahihi na

kwa wakati zitachochea bidii katika

kujiletea maendeleo,” alisema Bw

Andrew Hepelwa, Katibu Mkuu

Mstaafu wa MVIWATA taifa.

Aliongeza kuwa maendeleo

ni jambo la muhimu ambalo kila

mwanadamu analitegemea katika

maisha yake kuanzia ngazi ya familia

hadi ngazi za kitaifa. Kama hupati

taarifa kamili kuhusu kitu fulani,

huwezi kujua uzito wake na huwezi

kuchukua hatua za kimaendeleo na

kwa upande mwingine jamii ikipata

taarifa na habari sahihi inaweza

kuchukua hatua ya kujikwamua

katika matatizo.

Matumizi ya habari

Kwa ujumla jamii ya vijijini kutokana

na kutengwa kwa muda mrefu na

mfumo wa habari, nayo kwa namna

fulani imekuwa kama imejiengua na

kuyaona masuala ya habari kama

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

siyo sehemu yao.

Jamii hii inahitaji kujengewa

ufahamu wa kutosha kuhusu

umuhimu wa kupashana habari

na matumizi sahihi ya vyombo vya

habari katika kujiletea maendeleo.

Vyombo vya habari katika hili vina

mchango mkubwa wa kuwafumbua

macho wakazi wa kijijini ili wafahamu

umuhimu wa matumizi sahihi ya

habari katika mchakato wa kujiletea

maendeleo.

Mbali na vyombo vya habari, ziko

njia nyingine za asili zinazotumika

kufikisha habari kwa jamii kwenye

maeneo ya vijijini ikiwemo mikutano

ya vijiji, kwenye nyumba za ibada

na kwenye mikusanyiko kama vile

sokoni na kwenye minada.

Hata hivyo taarifa nyingi muhimu

hutolewa katika mikutano ya vijiji,

lakini kutokana na kukosa mwamko

huko nako mahudhurio ni madogo

na hivyo kukosesha wananchi habari

muhimu.

Miongoni mwa wakulima

waliohojiwa wamekiri wazi kuwa

hawajawahi kuhudhuria mkutano

wa kijiji kwa zaidi ya miaka miwili.

Hili ni tatizo na ni tabia inayopaswa

kuachwa kwa sababu inadidimiza

maendeleo.

Miongoni mwa wakulima hao

pia wamekiri mapungufu kwamba

Upatikanaji wa habari sahihi unapanua wigo wa mijadala kama hii ya wakulima

MADA MAALUM

walipata habari lakini hawakuzitumia

ipasavyo jambo ambalo wamelijutia

na baadaye kujirekebisha. Kwa

mfano Bw. Charles Ndugulile

mkulima wa kijiji cha Mwamala Kata

ya Mwamala wilaya ya Shinyanga

Vijijini alisema “mwaka 2008 kupitia

matangazo ya radio nilipata taarifa za

kutokea mabadiliko ya tabia ambayo

yatasababisha ukame na mlipuko wa

wadudu lakini nilipuuzia na baadaye

msimu wa kilimo uliofuata nililima

shamba kubwa kama kawaida,

nikapata hasara baada ya mazao

kukauka kwa ukame.”

Bw. Ndugulile akafafanua

kwamba kutokana na hali hiyo

amekuwa mhamasishaji mkubwa

kwenye mkoa wa Shinyanga

akiwahimiza wakulima umuhimu

wa kutafuta habari na kuzitumia,

lakini pia wawe wamezipata kutoka

katika vyanzo vya uhakika na

vinavyoaminika ila wasipotoshwe

kwa kupata habari ambazo si sahihi.

Hitimisho

Ili kuboresha upatikanaji wa habari

vijijini, serikali na wadau wa habari

kwa ujumla wanapaswa kushirikiana

kuondoa kasoro zilizopo na kuweka

mfumo wa usawa wa utoaji taarifa

na upatikanaji wa habari kwenye

Endelea Uk wa 5

3

MADA MAALUM

4

Maoni ya wakulima na

Na Goodness Mrema

Changamoto kubwa

inayowakabili wakulima

vijijini kwa kukosa habari

ni kuachwa nyuma kimaendeleo,

kuibuka kwa migogoro mingi baina

yao na viongozi wao ama makundi

mengine katika jamii.

Baadhi ya wakulima na wataalam

wamekuwa na maoni tofauti

kuhusiana na suala hili la upatikanaji

wa habari vijijini. Wakulima kutoka

mikoa mbalimbali walieleza jinsi

wanavyokabiliwa na changamoto

katika kupokea na kutoa habari

katika maeneo mengi ya vijijini

kutokana na miundombinu mibovu.

Yafuatayo ni maoni waliyoyatoa

wataalam

baada ya kuulizwa swali lililosema

hali ya upatikanaji wa habari kijijini

ukoje?

Bibi. Mariam Mmanga

kutoka kijiji cha Kivulini wilayani

Mwanga mkoani Kilimanjaro alieleza

kwamba japokuwa kijijini kwake

hawatembelewi na waandishi wa

habari mara kwa mara wala kufikiwa

na magazeti, lakini wanawake

kijijini kwake wamejiunga katika

vikundi wanavyovitumia kupashana

habari kupitia mikutano na vikao

mbalimbali na sasa wamehamasika

na wanaelewa umuhimu wa kupata

habari, jambo ambalo linawatia moyo

na wanaimani kwamba hawataweza

kubaki nyuma kwani wanafahamu na

wanaelewa nini kinaendelea katika

nchi yao. Hata hivyo akaongeza

kuwa wanaomba kutembelewa na

wanahaabari ili habari za vikundi

vyao pia zitangazwe.

Bibi. Mariam Hassan

kutoka kijiji cha Magamba, wilayani

Kibondo mkoani Kigoma anaeleza

kwamba magazeti kijijini Magamba

yanawafikia baada ya siku tatu ama

nne, tena lazima awepo mtu ametoka

mjini siku hiyo. Kwa upande wa radio

wanakamata zaidi radio za Burundi

na kwamba hupokea matangazo ya

radio moja tu ya Tanzania ambayo

nayo husikika usiku tu, jambo ambalo

linawafanya washindwe kupiga hatua

kimaendeleo.

Ameiomba serikali kuwakumbuka

Endelea Uk wa 5

Miongoni mwa machapisho yanayotolewa na MVIWATA ambayo yamewanufaisha wakulima wengi kwa kuwapata habari sahihi za kilimo

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Inatoka uk. wa 4

na kuhakikisha kwamba nao pia

wanapata huduma hii muhimu kwani

wanaonekana wamesahaulika kama

vile wako nje ya Tanzania kutokana

na kijiji chao kuwa mpakani mwa

nchi ya Burundi. “Kuhusu habari za

kijijini kwetu zinaandikwa pale tu

kiongozi anapokuja kututembelea

ama wakati mwingine waandishi

hufika kijijini hapo kunapokuwa

na matukio ya maafa kama vile

mauaji. Tatizo hili linatuathiri zaidi

sisi wanawake kwani muda mwingi

tuko ndani, afadhali wenzetu

wanaume wanakutana kwenye

vikao na kuhabarishana na wengine

wanamiliki simu za mkononi.”

Bw. Hamad Abdallah

Salimin kutoka Zanzibar yeye

alieleza kukerwa na waandishi wa

habari wanaokurupuka na kutangaza

mambo yasiyo sahihi na kuupotosha

umma. Akashauri ni vyema

wanataaluma hawa kuthibitisha

habari wanazozikusanya kabla ya

kuzitangaza kwa umma.

Hata hivyo aliwashauri wakulima

wenzake wakabiliane na changamoto

ya upatikanaji wa habari katika

maeneo ya vijijini kwa kutosubiri

tu hadi magazeti yawafikie ndipo

wajue wamepata habari kumili kujua

nini kinaendelea, bali wanaweza pia

kupata habari zinazowahusu kwa

kupitia majarida yanayochapishwa

na mashirika yanayojihusisha

na shughuli za kilimo kama vile

MVIWATA ili kutambua fursa walizo

nazo.

Lakini akasema kwamba wakulima

wasiishie kusoma habari na kuziacha

tu katika makaratasi bali wazifanyie

kazi na pia wasiogope kutumia

vyombo vya habari kuwasilisha kero

na kufichua maovu.

Bw. Joseph Msagama kutoka

Tanga alikiri kuwa changamoto

kubwa ipo katika upokeaji wa habari

kutokana na uhaba wa rasilimali

fedha ambayo inamwathiri kila

mkulima.

“Jambo la kusikitisha ni kwamba

wananchi wa vijijini wanaonekana

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

kuwa tabaka la watu waliosahaulika

katika kila kitu kuanzia kipato, elimu

na hata haki zao mbalimbali ikiwemo

hii ya kupata habari” alisema Bw.

Msagama.

Alishauri Halmashauri za wilaya

ziweke utaratibu wa kutenga

mafungu ya kuwawezesha usafiri

maaalum waandishi wa habari

ili wafike maeneo ya vijijini na

kuwasaidia wananchi kufahamu

nini kinaendelea na kwa kiasi gani

kinaathiri uchumi wa wakulima.

Kwa upande wake Bw. Abdala

Ramadhani kutoka wilaya ya

Misungwi, Mwanza alisema wakulima

wengi vijijini wanakabiliwa na uhaba

wa habari na kushauri vituo vya

taarifa vijijini viimarishwe ili kuziba

pengo lililopo.

“Kupitia vituo hivyo vichache

vilivyopo sasa wakulima na

wajasiriamali wanapata habari

kuhusiana na bei za mazao na wapi

wanaweza kuuza lakini habari hizo

haziwafikii wengi kutokana na uhaba

wa rasilimali fedha unaozikabili,”

alisema Ramadhani.

“Tunashukuru kuwapo kwa

gazeti letu wakulima la Pambazuko,

linatuwezesha kufahamu wenzetu

katika maeneo mengine wanafanya

nini na ni njia gani wanazozitumia

kutatua changamoto zao, jambo

ambalo linatupa ari ya kufanya kazi

kwa bidii ili kuzalisha kwa tija.”

Bw. Ramadhani alisema kupitia

mtandao wa wakulima wanajipanga

ili kuweka utaratibu mzuri wa

kuwezesha habari za wakulima

wa Mwanza zinamfikia mhariri wa

Pambazuko kwa wakati.

Bw. Paul Mossama kutoka

Serengeti mkoani Mara, anaeleza

kuwa mfumo wa upashanaji habari

uliopo nchini hivi sasa ni mzuri

kuliko miaka ya nyuma, japokuwa una

kasoro ya kutotangaza habari nyingi

za kuwasaidia wakulima kuboresha

shughuli zao na akashauri vituo vya

radio na televisheni vinavyoanzishwa

na halmashauri za wilaya vitangaze

zaidi habari hizo badala ya kuwa na

Endelea Uk wa 6

Inatoka uk. wa 3

MADA MAALUM

Upatikanaji wa

habari vijijini

maeneo ya vijijini na mijini.

Kwa upande wa radio

matangazo yaboreshwe yasikike

vizuri vijijini ili wananchi wetu

walioko mipakani kama vile

Kigoma pia waweze kunufaika

na matangazo ya radio za nchini

mwao badala ya radio za nchi jirani

ya Burundi na Kongo ambazo

kila kukicha zinatangaza vita na

mauaji kutokana na mapigano

yanayoendelea nchini mwao.

Kadhalika waandishi

wenyewe wanakabiliwa na

changamoto ya kujiendeleza

kitaaluma ili kuweza kuwa

na upeo zaidi wa kuandika

na kuchanganua habari zao

kwa weledi hasa zinazohusu

maendeleo vijijini badala ya kuwa

mawakala ama mashabiki wa

siasa tu.

Kuna matatizo mengi vijijini

ambayo kimsingi yanahitaji nguvu

ya wanahabari kuyatatua. Kwa

mfano wanahabari wanapaswa

kuijengea uwezo jamii kuhusu

elimu ya afya vijijini, elimu ya

ukatili wa wanawake na vitendo

vya unyanyasaji, elimu juu ya

umiliki na matumizi bora ya ardhi,

elimu ya kilimo bora na ufugaji,

ujasiriamali, masoko na umuhimu

wa elimu kwa watoto wao.

Ipo haja kubwa ya tasnia

ya habari kutilia mkazo suala la

kuielimisha jamii ili iepukane na

imani potofu za kwenda kwa

waganga wa kienyeji kupiga ramli

badala ya kuwapeleka wagojwa

kutibiwa kwenye zahanati na

vituo vya afya.

Wanakijiji ambao kwa sehemu

kubwa ni wakulima wanapaswa

kujengewa uelewa wa masoko

ya mazao yao, taarifa za bei na

mbinu bora za kuongeza tija katika

uzalishaji na kuboresha uchumi.

Maendeleo vijijini

yanachelewa kwa sababu

wananchi hawapati habari sahihi

kwa wakati muafaka. Hivyo

yanapaswa kuchochewa kwa

kuwapatia habari za kina.

5

MADA MAALUM

Maoni ya wakulima...

Inatoka uk. wa 5

vipindi vingi vya miziki na salamu.

Akashauri pia magazeti kutenga

kurasa maalumu zitakazoandika

habari za wakulima wadogo angalau

mara moja kwa wiki. “Magazeti

mengi sasa yamefungua kurasa za

udaku, urembo na muziki, hivyo hata

kwa habari za wakulima jambo hili

linawezekana.”

Aliwashauri wakulima wadogo

kutumia mitandao ya wakulima

waliyonayo katika maeneo yao

kwa ajili ya kupashana habari

hadi pale wanapokuwa wanaona

wameshindwa kufanya hivyo

wenyewe ndipo waweze kumtafuta

mwandishi ambaye atawasaidia

kutangaza taarifa zao ili nao

wapate nafasi ya kupaza sauti zao

na kusaidiwa pale wanapohitaji

msaada.

Bw. Benardi Maiko kutoka

Kasanga, wilayani Sumbawanga

mkoani Rukwa alisema wakulima

wanayo mambo mengi ambayo ni

vyema wakayatangaza ikiwemo

mazao yao na bidhaa zingine

wanazozalisha, changamoto ya uhaba

wa pembejeo na zana bora za kilimo

pamoja na mahitaji ya masoko ya

kuuzia mazao yao.

Aliongeza pia, wakulima

wanahitaji kuwezeshwa kuwasiliana

wao kwa wao kupitia vyombo vya

habari ili kurahisisha mawasiliano

kwani badala ya wao kufunga

safari kwenda maeneo mengine

kuwatembelea wenzao wataweza

kusoma tu kwenye magazeti ama

kusikiliza radioni na kujifunza.

“Endapo habari zingekuwa zinafika

maeneo ya vijijini kama ilivyo kwa

maeneo ya mijini hakika wakulima

leo tungekuwa kundi lenye nguvu

kiuchumi na tusingekandamizwa

wala kunyanyaswa” alisema Bw.

Maiko

Bw. Charles Ndugulile

mkulima wa kijiji cha Mwamala

Kata ya Mwamala wilaya ya

Shinyanga Vijijini alieleza kwamba

6

upatikanaji wa habari unategemeana

na watafutaji wa habari kwamba

wanataka habari za namna gani na

zinazohusu nini na kutolea mfano

wa jarida la Pambazuko kwamba kila

anayetaka kupata habari kuhusiana

na wakulima anaweza kuzipata

kutoka ndani ya jarida hilo.

Akizungumzia matumizi sahihi

ya habari Bw. Ndugulile alisema

“mwaka 2008 kupitia matangazo

ya radio nilipata taarifa za kutokea

mabadiliko ya tabia ambayo

yatasababisha ukame na mlipuko wa

wadudu lakini nilipuuzia na baadaye

msimu wa kilimo uliofuata nililima

shamba kubwa kama kawaida,

nikapata hasara baada ya mazao

kukauka kwa ukame.”

Bw. Ndugulile alifafanua kwamba

kutokana na hali hiyo amekuwa

mhamasishaji mkubwa kwenye katika

mkoa wa Shinyanga akiwahimiza

wakulima umuhimu wa kutafuta

habari na kuzitumia, lakini pia wawe

wamezipata kutoka katika vyanzo

vya uhakika na vinavyoaminika ila

wasipotoshwe kwa kupata habari

ambazo si sahihi.

Alifafanua kwamba katika mkoa

wa Shinyanga wamewahamasisha

wakulima umuhimu wa kutafuta

habari kutoka katika vyanzo vya

uhakika na vinavyoaminika ili

wasipotoshwe kwa kupata habari

ambazo si sahihi.

Alisema kuwa wakulima wanaumia

waonapo habari mara kwa mara

zinazoeleza kuwa wameshindwa

kufanya jambo ama wana mgogoro

fulani wakati habari za mafanikio

waliyopata kupitia kilimo ikiwemo

kuongeza uzalishaji na kuweza

kulipa ada za watoto wao, kujenga

nyumba, kuongeza idadi ya mifugo

na hata kufanikiwa kununua zana za

kilimo, haziandikwi. “Kwa msingi huu

ndiyo maana mara nyingi nimekuwa

nikishauri kwamba ni muhimu

wakulima tuimarishe chombo

chetu cha habari kama Pambazuko

kinachoweza kutusemea habari

zetu.”

Bw. Ndugulile ambaye pia

ni mwenyekiti wa MVIWATA

Shinyanga, alisema vyombo vingi

vya habari nchini hivi sasa vinafanya

shughuli zake kibiashara na hivyo

kujikita katika matukio yenye

habari zinazouzika na kutupa kando

jukumu la kuwaelimisha wakulima

kilimo biashara ama ufugaji na uvuvi

wa kisasa.

Maoni ya wataalam

Bibi Mary Nsemwa, ni mkuu

wa Idara ya Ushawishi na Ujenzi wa

Nguvu za Pamoja katika Mtandao

wa Jinsia Tanzania (TGNP), anasema

asilimia kubwa ya wananchi wa

vijijini wanaoathirika na upatikanaji

wa habari ni wanawake.

Bibi Nsemwa alisema wanawake

wanahitaji kuhabarishwa kuhusiana

na kilimo, ujasiriamali, sheria

ya ardhi na mambo mbalimbali

yanayoendelea mijini na duniani,

lakini haki hiyo wanaikosa kutokana

na kutokuwepo kwa miundo mbinu

inayofika maeneo ya vijijini hususan

barabara kwa ajili ya magazeti.

“Hata kwa familia zenye radio

nyingi zinamilikiwa na wanaume,

hivyo wanawake kukosa taarifa

muhimu ndiyo maana wanazidi

kukandamizwa”.

Bw. Marcossy Albanie wa

Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki

za Binadamu yeye anasema “kwa

ujumla wakulima ni kundi lililoachwa

nyuma na hata wakizungumza watu

wanawapuuza na ndiyo maana hata

vyombo vingi vya habari vimeegemea

zaidi mjini, ingawa kisingizio kikubwa

kimekuwa ni miundombinu mibovu

vijijini.

“Suala hili linamfanya mkulima

mdogo abaki kwenye kiza na watu

wachache waendelee kunufaika na

rasilimali za nchi.

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

MAKALA

Soko huria lilivyoathiri upatikanaji

wa habari vijijini

Na Rashid Kejo

Tulikotoka

Nchi ya Tanzania tangu ilipopata

uhuru wake mwaka 1961, ilikuwa

ikitumia mfumo wa vyama vingi hadi

mwaka 1965 ilipoamua kuachana

nao. Hata hivyo mwaka 1992,

Tanzania iliridhia mageuzi makubwa

ya kurejea katika mfumo wa vyama

vingi vya siasa.

Sababu iliyotolewa mwaka 1965

wakati wa kuachana na vyama vingi

ni kwamba pamoja na mambo

mengine, vyama vya upinzani

ambavyo vilikuwapo kama vile

African Independence Movement

(AIM) na People’s Democratic

(PDP), havikuwa na nguvu.

Lakini pia wakati ule, kulikuwa na

vuguvugu kubwa la mataifa mengi

ya Afrika kuendeshwa chini ya

utawala wa chama kimoja kutokana

na kile kilichoelezwa kwamba ni

kuleta umoja wa kitaifa na kuondoa

mifarakano na migogoro kwa lengo

la kujiletea maendeleo.

Licha ya kuwa na chama kimoja

kilichokuwa kimeshika hatamu, hata

nyanja nyingine kuu na muhimu za

kiuchumi na kijamii, kwa kiwango

kikubwa zilikuwa chini ya umma.

Vyombo vya habari kadhalika,

vilikuwa katika mfumo dola. Redio,

televisheni (kwa Zanzibar) na

magazeti, ama vilimilikiwa moja

kwa moja na Serikali, taasisi zake au

chama na jumuiya zake.

Tunakumbuka vyombo kama

Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD),

Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ),

Magazeti ya Daily News/Sunday

News, Uhuru/Mzalendo, Mfanyakazi

na Mkulima wa Kisasa.

Kutokana na uchache na umiliki

wake, maudhui ya vyombo hivi

yaliratibiwa na dola yakilenga

masuala kadhaa ambayo Serikali

ilikuwa imeyapa kipaumbele.

Pamoja na changamoto zake,

habari za wakulima zilipata fursa

katika vyombo hivyo. Achilia mbali

gazeti, kulikuwa na vipindi vya redio

vya Mkulima wa Kisasa ambavyo

vilitoa mafunzo na maelekezo

mbalimbali ya kilimo bora.

Kulikuwa pia na mkakati maalumu

kupitia Taasisi ya Vielelezo wa

kupeleka sinema vijijini kuelimisha

wakulima juu ya ukulima na

ufugaji bora. Kimsingi, kulikuwa na

upatikanaji wa taarifa hasa zile za

msingi kwa umma wa vijijini.

Wahenga walisema, kila masika

yana mbu wake. Katika mabadiliko

ya mwaka 1992 yaliyoruhusu mfumo

wa vyama vingi na soko huria,

Serikali ilijitoa katika biashara na

kulegeza masharti hivyo kuiwezesha

sekta binafsi kushiriki moja kwa

moja katika masuala ya kiuchumi

na kijamii. Mabadiliko yalichochea

kuanzishwa kwa Sera ya Habari na

Utangazaji ya mwaka 1993.

Hata hivyo, haikujitoa katika

usimamizi na uendeshaji wa vyombo

vyake vya habari, bali iliruhusu sekta

binafsi nayo kuingia katika biashara

hiyo. Hivyo, kuanzia mwaka 1992,

magazeti, vituo vya televisheni

na redio na baadaye mitandao ya

mawasiliano vilianza kwa kasi.

Tofauti na awali ambako

mwelekeo wa habari ulilenga zaidi

propaganda, safari hii mtazamo

ulikuwa wa kibiashara zaidi na hali

hiyo imekuwa na athari kubwa katika

upatikanaji wa habari za vijijini.

Kutokana na msukumo huo wa

nguvu ya soko, vyombo ambavyo

vilishindwa kujiendesha kibiashara

vilikufa na hivyo ndivyo ilivyotokea

kwa Gazeti la Mkulima wa Kisasa.

Vipindi vingi vilivyoanzishwa katika

redio na televisheni vililenga zaidi

kuwavutia watangazaji (advertisers).

Kwa upande mwingine, asilimia

kubwa ya magazeti na machapisho

husomwa zaidi mijini ambako

usambazaji ni rahisi na kiwango cha

kujua kusoma na kuandika ni kikubwa

na hilo likawa na athari kubwa kwa

upatikanaji wa habari za vijijini.

Hiyo ilimaanisha kwamba

wakulima na wananchi wengine

waishio vijijini walianza kupewa

habari ambazo hazikuwa na uwiano

wa moja kwa moja na matatizo au

vipaumbele vyao.

Kwa mfano, mwaka 1995

wakati taifa likiwa katika kampeni

za kwanza tangu kurejeshwa kwa

mfumo wa vyama vingi, baadhi ya

vituo vya televisheni vilitumia fursa

hiyo vibaya kwa kuonyesha picha za

mauaji hivyo kuwatishia wananchi.

Mabadiliko makubwa

Hata hivyo, kadri miaka inavyosonga

kumekuwa na mabadiliko makubwa.

Kukua kwa teknolojia ya mawasiliano

na dhana ileile ya soko kumevifanya

vyombo vya habari kuanza kubaini

umuhimu wa kulitazama soko la vijijini

waliko asilimia 80 ya Watanzania.

Halmashauri za wilaya na

wawekezaji wengine wa ndani

wameanzisha redio za jamii

(community radio) ambazo zinatoa

huduma ya habari katika maeneo

yao. Hili limekuwa na mchango

mkubwa kwa wananchi wa vijijini

kwani taarifa, kero na shida zao

zimekuwa zikipata fursa ya kusikika.

Lakini siyo kusikika tu, kumekuwa

na fursa kubwa zaidi ya kupata

habari zinazokidhi mahitaji yao

kwa kiwango kikubwa na hivyo

kuchochea maendeleo yao.

Ingawa wilaya zilizoanzisha radio

hizi za jamii ni chache mno, lakini

wilaya zilizobahatika kuwa na redio

hizi, zimekuwa zikitumia fursa hiyo

kufikisha ujumbe muhimu katika

maeneo husika kama vile bei ya

bidhaa na huduma nyingine muhimu.

Endelea Uk wa 11

7

ANA KWA MFUMO ANA/MAKALA WA TAARIFA ZA MASOKO WA MVIWATA

(MAMIS)

PATA BEI ZA MAZAO KWENYE SIMU YAKO POPOTE ULIPO!!

Jinsi ya kupata taarifa kwenye simu yako:

Masoko yaliyopo mpaka sasa:

MOROGORO, TAWA, TANDAI, NYANDIRA, KIBAIGWA, DODOMA, IGUNGA, TABORA, SHINYANGA,

MASWA, BARIADI, BUKOMBE, KAHAMA, KILOMBERO (ARUSHA), KARIAKOO, BUGURUNI, TEMEKE,

IGURUSI (MBEYA), MKURANGA, MAKAMBAKO, SIMANJIRO, TAVETA, MKATA, IGAGALA, MATAI

(RUKWA), KASANGA, HIMO, HOLILI, n.k

Mazao yaliyo kwenye mfumo huu:

MAHINDI, MCHELE, MAHARAGE, CHOROKO, KUNDE, MBAAZI, NJEGERE, MTAMA, UWELE, ULEZI,

UFUTA, ALIZETI, NDIZI MBIVU, NDIZI MBICHI, MAGIMBI, MUHOGO, NANASI, CHUNGWA, PAPAI,

EMBE, PARACHICHI, NYANYA, VITUNGUU MAJI, VITUNGUU SAUMU, TANGO, KAROTI, KABICHI,

HOHO, LUBABU, SELELI, BITRUTI, ZUKINI, SALADI, KOLIFLAWA, TANGAWIZI, PILIPILI MTAMA,

MDALASINI, ILIKI.

...meseji moja kwa kila zao moja

8

imedhaminiwa na;

Taarifa ya BEI ZA MAZAO

1. Andika neno BEI acha nafasi

2. Andika zao unalotaka bei yake mfano; MAHINDI

3. Kisha tuma kwenda namba 0654 555 884

Taarifa ya WAUZAJI

1. Andika neno NANUNUA acha nafasi

2. Andika zao unalotaka kununua mfano; MAHINDI

3. Kisha tuma kwenda namba 0654 555 884

Taarifa ya WANUNUZI:

1. Andika neno NAUZA acha nafasi

2. Andika zao unalotaka kuuza mfano; MAHINDI

3. Kisha tuma kwenda namba 0654 555 884

Kwa Mawasiliano zaidi piga SIMU NAMBA 0659250317

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

MAKALA

Taaluma ya habari ni wito

Na Susuma Susuma

Vyombo vya habari ni jina

la jumla la mfumo wa

mawasiliano unaojumuisha

utangazaji wa redio, televisheni,

majarida na magazeti. Vyombo

hivi vina wajibu mkubwa wa

kuhudumia matakwa ya jamii katika

maisha yao ya kila siku. Vyombo

vya habari vinaelimisha, vinatoa

burudani na kutoa changamoto

kwa wananchi na viongozi kuhusu

mambo mbalimbali.

Kadhalika taaluma ya habari ni

tasnia nyeti inayoheshimika katika

jamii yoyote inayothamini ustaarabu,

umoja na utangamano wa kitaifa.

Kuandika makala kwenye

magazeti, kusoma taarifa ya habari

au utayarishaji wa vipindi vya siasa,

jamii, utamaduni, dini, burudani ama

matukio yanayohitaji jamii kupewa

taarifa, ni shughuli zinazohitaji

ushirikiano wa kutosha baina ya

wadau yaani waandishi, watoa habari

na walaji (wasikilizaji/wasomaji).

Kwa mantiki hiyo, ushirikiano

madhubuti kati ya wadau wa habari

na waandishi wa habari ni nguzo ya

maendeleo katika jamii.

Aidha, kufanikisha masuala

haya kunahitaji umakini, weledi,

mazingatio ya kufuata miiko, maadili

na heshima kwa mwandishi ama

mtangazaji husika.

Utendaji kazi wa vyombo

vya habari

Ukilinganisha miaka 50 iliyopita hali

ya utendaji kazi wa vyombo vya

habari na hali ilivyo hivi sasa nchini

kwetu ni tofauti kabisa.

Uandikaji wa habari, makala,

utangazaji na utayarishaji wa vipindi

hivi sasa hauzingatii ujuzi, taaluma na

kuheshimu miiko, kama ilivyokuwa

miaka ya awali.

Fani hii imeshuhudia watu

wanahitimu uandishi wa habari ngazi

ya shahada ya kwanza au ya uzamili,

lakini bado wakashindwa kuandika

habari kwa usahihi.

Kwa mfano eneo moja

linalowashinda ni jinsi ya kufahamu

mahitaji halisi ya wasomaji,

wasikilizaji ama watazamaji wao,

kushindwa kufahamu habari ilipo

ama kushindwa kutofautisha habari,

uzushi na fitina.

Wapo wanaosema fani hii ni

rahisi kuliko zote na hawa ndiyo

wanaovamia fani hii na kudhani

kwamba wanafanya vizuri bila

kufahamu kuwa wanachangia kuua

taaluma.

Fani hii siyo rahisi kama

inavyodhaniwa na wengi, na pengine

ndiyo maana kila kukicha vyombo

vya habari vinalaumiwa kwa kukiuka

miiko na maadili kwa kuwa wengi

wanaamua kujiunga wakidhani

ni kuandika tu, matokeo yake

wanafanya upotoshaji.

Tumeshuhudia pia utitiri wa

vyombo vya habari vinavyoanzishwa

kila leo, lakini cha kushangaza vingi

vinaanzishwa mijini na kuhudumia

watu wa mijini tu na kuwaacha

kando watu waishio vijijini.

Kwa mujibu wa takwimu za

Msajili wa Magazeti mpaka sasa

amekwishasajili zaidi ya magazeti

na majarida 350 ingawa ni asilimia

15 tu ya machapisho hayo ambayo

yanaonekana mitaani kwa wakati huu

na asilimia kubwa yakiwa mijini. Idadi

kubwa ya magazeti yaliyosajiliwa

yanamilikiwa na watu au makampuni

binafsi isipokuwa magazeti ya ”Daily

News, Sunday News na Habari leo”

ambayo yanamilikiwa na Serikali na

gazeti la Uhuru linalomilikiwa na

chama tawala CCM. Ukipekuwa

kwa undani utendaji kazi wa

magazeti haya sasa yako kibiashara

zaidi kinyume na matarajio ya kutoa

huduma ya kuhabarisha umma.

Vyombo vya habari

vinapoanzishwa vikiwa na mlengo

wa kibiashara zaidi, ni moja ya

sababu inayochangia vyombo vingi

virundikane mjini ambako wamiliki

wanaamini watauza na kupata

matangazo ya kutosha. Na hoja hapa

ni Je, jamii ya huko vijijini ambako

biashara ya radio, televisheni na

magazeti hazilipi, itafikiwaje na habari

zenye kuchochea maendeleo?

Kufanya hivi vyombo vya habari

vinakiuka sheria na kuwanyima haki

Endelea Uk wa 10

MVIWATA katika kusaidia wakulima kupaza sauti zao, imekuwa ikiwawezesha wanahabari

kuyafikia maeneo ya vijijini na kuchukua habari za kero zao

9

MAKALA

Taaluma ya habari ni wito...

Inatoka uk. wa 9

ya msingi wananchi wa vijijini.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania (1977) ambayo ilifanyiwa

marekebisho mwaka 1984, imeweka

kifungu maalum kinachotaja wazi

kuwa habari ni haki ya msingi ya raia.

Kifungu hicho cha 18 cha Katiba

kinasema:

(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila

mtu yuko huru kuwa na maoni

yoyote na kutoa nje mawazo

yake, na kutafuta, kupokea na

kutoa habari na dhana zozote

kupitia chombo chochote bila

ya kujali mipaka ya nchi, na

pia uhuru wa mawasiliano yake

kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa

taarifa wakati wowote kuhusu

matukio mbalimbali nchini na

duniani kote, ambayo ni muhimu

kwa maisha na shughuli za

wananchi; na pia juu ya masuala

muhimu kwa jamii.

Wajibu wa vyombo vya

habari

Njia muhimu za kuwezesha

wananchi kufurahia haki ya kupasha

na kupashwa habari na kujieleza

kwa kutoa maoni hadharani bila

bughudha,vitisho na ukandamizwaji

ni kupitia vyombo vya habari.

Kutokana na umuhimu wa kipekee

wa haki hii ya msingi, nafasi ya

vyombo vya habari katika utekelezaji

wake pia ni ya kipekee. Kwa kuwa

vyombo vya habari vinawawezesha

wananchi kutumia haki hii ili isibaki

nadharia au kwenye maandishi tu,

hakuna budi wamiliki wa vyombo vya

habari pamoja na serikali, watambue

na kukiri kwamba nafasi yao ni ya

kutoa huduma au mahitaji ya lazima

kwa jamii, huduma kwa umma.

Hadhi ya huduma ya kijamii

inazidi sana ile ya bidhaa ambazo

huuzwa kuingiza faida. Ndiyo maana

wajibu wa wamiliki wa vyombo vya

habari kwa jamii ni mkubwa kuliko

wa mfanyabiashara ama mwekezaji

ambao msukumo wao mkubwa ni

10

kutengeneza faida.

Hata vyombo vya habari vya

serikali vinapaswa kuwajibika kwa

umma na sio utashi wa kisiasa wa

wanasiasa na watawala.

Wanahabari pamoja na kwamba

huajiriwa na wamiliki wa vyombo,

bado huwajibika kwa umma. Na

ndiyo maana ili vyombo vya habari

viweze kutekeleza majukumu

yao, hakuna budi kwa wahariri na

wanahabari kuwa na uhuru wa

kutosha kukusanya, kuchambua

na kusambaza habari bila woga,

shinikizo au ushawishi wa wamiliki

na washiriki wao kibiashara.

Habari ni huduma

Kazi ya uandishi wa habari ni fani

ambayo pamoja na kuwa na ujuzi

lakini inahitaji zaidi wito. Ni fani

ambayo inahitaji zaidi mtu kutanguliza

utu na upendo ama dhana ya kutoa

huduma kuliko malipo ama kufanya

biashara. Ni fani isiyojali sana malipo

yenye kulingana na kadhia, ugumu

wala masuala mengine kwa kuwa

kuna wakati unakuwa unashughulikia

tatizo la kijamii iliyo masikini ambayo

malipo yake ni asante.

Kinachosikitisha zaidi ni kuona

baadhi ya waandishi wa habari

wakishabikia zaidi kuandika habari

za migogoro na kuwachafua watu,

wakati mwingine wakiishia kudai

posho bila hata kuandika chochote.

Hali hii inaonesha walivyokosa

ushirikiano na jamii.

Pia zipo sheria ambazo

zinaonekana kukandamiza uhuru wa

vyombo vya habari nchini, ambazo

wanahabari wamekuwa wakizipigia

kelele kwa kuitaka serikali

kuzirekebisha ama kuzifuta kabisa.

Hizi ni pamoja na sheria ya magazeti

ya Tanzania ya mwaka 1976 ambayo

inampatia uwezo waziri anayehusika

na habari wa kulifungia gazeti lolote

lile kama ataridhika kuwa limekiuka

kwa kiasi kikubwa matakwa ya sheria

hiyo. Sheria hizi pia zinakwamisha

upatikanaji wa habari sahihi zenye

maslahi umma.

Mfano halisi ni wa taarifa

zinazohusiana na kashfa kwenye

migodi ya madini na kwenye sekta ya

uwindaji wanyama kwenye mbuga za

wanyama ambazo zinaakisi uchumi

wa nchi.

Serikali inapaswa kupitisha sheria

rafiki kwa vyombo vya habari na

ambazo zinaweka mazingira huru ya

upatikanaji wa habari, kwani kuvifunga

minyororo vyombo vya habari ni

kuwafunga minyororo wananchi.

Kwa upande mwingine wapo

waandishi wa habari wanaotishiwa

maisha pale wanapofuatilia ili kupata

habari za kina kuhusiana na jambo

fulani lenye maslahi kwa jamii. Lakini

hiyo siyo sababu ya wao kufanya

shughuli zao kinyume cha sheria na

maadili ya taaluma yao kama vile

kutoa na kupokea rushwa, upotoshaji

na udanyanyifu, uchochezi, ushabiki,

kutunga ama kutia chumvi habari.

Hata hivyo changamoto ni sehemu

ya maisha, ni chachu kwa maendeleo

yoyote, wanahabari ni vyema

tukajenga tamaduni ya kwenda

vijijini kuzungumza na kutangaza

habari za mafanikio, ubunifu, uzoefu

na mbinu wanazotumia wanavijiji

kutatua changamoto za maisha yao

ya kila siku.

Kwa kuwa tumeamua

kuwatumikia wananchi wenye

uhitaji wa huduma yetu, hatuna

budi kuzikabili changamoto zote

za kutafuta, kuandaa na kuzifikisha

habari kwa wadau bila kujali

zinapatikana kutoka mazingira yenye

changamoto nyingi.

Kwa upande mwingine liko kundi

dogo la wanahabari nchini ambao

wamepungukiwa utu na upendo,

wametanguliza zaidi maslahi binafsi,

ndiyo maana wameigeuza fani hii

kuwa biashara badala ya huduma

kwa jamii. Kundi hili japokuwa ni

dogo lakini laweza kuwa na madhara

makubwa kwa jamii hasa kipindi hiki

ambao vitendo vya ufisadi vinazidi

kushika kasi ndani ya nchi yetu.

Wakialikwa kwenda kuchukua habari

Endelea Uk wa 11

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Soko huria lilivyoathiri...

Inatoka uk. wa 7

Inawezekana bado kuna vikwazo

vya hapa na pale katika kuwafikia

wananchi wa vijijini walio wengi, lakini

muhimu ni kuviimarisha zaidi vyombo

hivi ili walau viweze kuziba pengo

lililosababishwa na kutoweka kwa

majarida kama ya mkulima wa kisasa.

Mamlaka za miji na wilaya nchini

ni mali ya wananchi kupitia mabaraza

ya madiwani ambao wanatokana na

kura za watu katika ngazi za kata.

Kwa maana hiyo basi ni fursa kwa

viongozi hawa wawakilishi wa umma

(madiwani), kuimarisha usimamizi

wa vituo vya redio na televisheni

vinavyomilikiwa na halmashauri zao

ili viweze kukidhi matakwa ya jamii

husika, ziwe za wakulima, wafugaji,

wavuvi, wachuuzi au wengineo.

Hii ni moja ya hatua muhimu

zinazoweza kuwarejesha wazalishaji

wadogo wa sekta mbalimbali nchini

katika dunia ya mawasiliano.

Intaneti na simu za mkononi

Tunapozungumzia habari, hatuwezi

kuacha kuzungumzia njia nyingine

za kisasa za mawasiliano kama vile

intaneti na simu za mkononi. Hizi kwa

ujumla wake zimekuwa na mchango

mkubwa kwa wananchi wa vijijini

katika mambo mbalimbali.

Intaneti kwa mfano, imewawezesha

wananchi kutafuta masoko, masomo

na kuwasiliana kwa sababu mbalimbali

na taasisi, ndugu, jamaa na marafiki zao

walio mbali.

Zamani ilikuwa ni gharama kubwa

na usumbufu kuwasiliana kwa njia ya

barua na ndugu walio mbali. Lakini

sasa, katika baadhi ya maeneo ya

vijijini kuna vituo vya mawasiliano

ambako wananchi huenda na kupata

huduma hizo za mtandao (simu/

intaneti) na hivyo kupata taarifa

mbalimbali za shughuli zao na pia

kuwasiliana na watu mbalimbali.

Magazeti mengi ya ndani na

nje na hata redio zimeunganishwa

pia katika mitandao hii ya intaneti,

hivyo wananchi popote walipo

wanaweza kusoma habari za leoleo

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya

kuujua ulimwengu na yanayoendelea

na kutumia taarifa hizo kujiongezea

maarifa na kujiendeleza.

Njia hii ya simu ndiyo imekuwa

na athari chanya kubwa. Idadi kubwa

ya Watanzania mijini na vijijini hivi

sasa wanafaidika kwa huduma hii

iwe moja kwa moja au kupitia kwa

ndugu na jamaa zao.

Upashanaji wa habari ulikwaza

mambo mengi ya watu waishio

vijijini lakini baada ya mapinduzi ya

teknolojia hii, si ajabu hivi sasa kwa

mfano, mtu aliye kijijini kumweleza

au kumpa taarifa aliye mjini juu ya

tukio lililotokea huko huko mjini.

Mara ngapi tumesikia watu

waishio Dar es Salaam wakipewa

taarifa za msiba uliotokea hukohuko

Dar es Salaam na mtu aishie

kijijini? Kimsingi mawasiliano

hayo yamevunja umbali baina ya

watu wa maeneo haya. Japokuwa

haya yanatokea kwenye maeneo

machache mno ya vijijini ambayo

yamebahatika kuunganishwa na

huduma za simu za mkononi.

Mapinduzi mengine chanya

yaliyotokana na uwepo wa mawasiliano

haya ya simu ni utumaji na upokeaji wa

fedha kupitia mitandao ya simu.

Usumbufu wa kuwatumia wazazi

kijijini fedha au kuwalazimu wakulima

na wafanyabiashara kusafiri kwenda

mjini au kijijini kununua au kuuza

bidhaa siku hizi hauna ulazima. Baada

ya kuingia makubaliano, mkulima

anaweza kufungasha mazao yake na

kuyatuma mjini na kutumiwa fedha

kwa njia ya simu na hayo hufanyika

ndani ya muda mfupi mno. Zaidi ya

hayo huduma za mawasiliano ya simu

zimepanua wigo wa ajira kwa vijana

vijijini na kuongeza kipato, hivyo

basi wananchi wanapaswa kuitumia

vyema fursa hiyo kwa kuifanya kuwa

kichochocheo cha maendeleo yao.

Mwandishi wa Makala hii ni

Mhariri wa Habari wa Gazeti

la Mwananchi

Taaluma ya habari

ni wito...

Inatoka uk. wa 10

MAKALA

kijijini, swali la kwanza wanalouliza ni

watalipwa? nani atawalipa? kiasi gani

watalipwa? Wakishapewa majibu

kuwa hakuna malipo kwa kuwa

kazi hiyo ni sehemu ya utekelezaji

wa majukumu yao, wanaishia kutoa

visingizio vya kutoenda kufanya kazi

hiyo.

Wanahabari tunapaswa

kujitambua kuwa sisi ni nguzo

muhimu ya maendeleo katika

jamii hivyo tunatakiwa kujenga

ushirikiano madhubuti baina yetu

na wadau wa habari wakati wa

kutekeleza majukumu ya kuipasha

habari jamii kwa uaminifu na

kudhihirisha kuwa tulioko kwenye

taaluma hii tuna wito.

Aidha ni muhimu kwa umma

kuwa na imani na wanahabari

kuwa wanachofanya ni sehemu

ya utekelezaji wa majukumu

kama ilivyo kwa watumishi

wa sekta nyingine na kwamba

hawana sababu ya kuwaogopa,

kujenga chuki ama kuwapa taarifa

za uongo na uchochezi, bali

washirikiane nao kwa ukaribu.

Ni vyema kila kundi likajali na

kuheshimu uhuru wa kutoa na

kupata habari kama ilivyo ndani

ya katiba ya nchi.

Jihadhari na

maambukizo ya

UKIMWI

jikinga na umlinde

mwenzako

11

KAMERA

12

KAMERA YA MVIWATA MITANDAONI

Wakulima wa kata ya Mlangali wilayani Ludewa wakioneshana

jambo lililowavutia kwenye gazeti la Pambazuko linaloandika habari

za wakulima na kusambazwa vijijini

Moja ya mikutano ya mitandao ya wakulima ambayo imekuwa

ikitumika kupashana habari vijijini

Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi na watumishi wa MVIWATA

na wawakilishi wa ubalozi wa Ireland nchini Bibi Aileen D’donovan,

Dkt Sizya Lugeye na Bw. Vicent Akuluyuka (wa nne hadi wa sita

kutoka kushoto waliosimama), baada ya ujumbe huo kutembelea

makao makuu ya MVIWATA yaliyoko Morogoro Julai 5, 2011.

Bibi HotensiaThomas, mwenyekiti wa Bodi ya Soko la Wakulima

Nyandira akisikiliza swali kwa mmoja wa wadau wa masoko ya

Igurusi, Matai na Kasanga walipofanya ziara sokoni hapo Julai 21,

2011

Wana-MVIWATA walioshiriki Tamasha la Jinsia Septemba 2011

wakimsikiliza mwenzao wakati wa majadiliano

Wana-MVIWATA Kiteto Manyara walioshiriki mafunzo ya kujengea

uwezo viongozi Julai 28-29, 2011, wakiwa na baadhi ya watumishi

wa MVIWATA taifa waliowezesha mafunzo hayo

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

KAMERA YA MVIWATA MITANDAONI

Ukosefu wa habari sahihi za masoko vijijini unasababisha bidhaa za

wajasiliamali kama hawa wa Kwekanga Lushoto kukosa soko

Wakulima wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kushiriki

Jukwaa la Wakulima mkoani Ruvuma

Wanawake jamii ya wafugaji wilayani Monduli, wakishiriki kazi ya

kuchimba msingi na kuweka mawe ya msingi ya jengo la kukusanyia

la kituo cha kibiashara

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

KAMERA

‘Natangaza kazi za mikono’, ndivyo anavyoelekea kusema mama

huyu mkazi wa kijiji cha Kwalei wilayani Lushoto

Bibi Elizabeth Lagwen (kulia) Mwenyekiti wa mtandao wa msingi

Mamire Babati Vijijini akiwasikiliza wageni kutoka shirika la TRIAS

Ubeligiji waliomtembelea kujifunza shughuli anazozifanya

Licha ya kuwa na historia ya ufugaji pekee, jamii ya Wamasai sasa

wamebadlika na kuanza kushiriki kilimo kama wanawake hawa

walivyokutwa na kamera yetu wakipanda mazao shambani

13

KUTOKA MITANDAONI

Maonesho ya NaneNane 2011

Wakulima wazungumzia matumizi na faida

za bidhaa walizoonesha

Na Goodness Mrema, Morogoro

Mtandao wa vikundi

vya wakulima Tanzania

(MVIWATA) katika

kuhakikisha kwamba unatekeleza

vyema majukumu yake umekuwa

na utaratibu wa kuwawezesha

wakulima toka mikoa mbalimbali

kushiriki kuonesha bidhaa zao

kwenye maonesho ya kilimo

maarufu kama NaneNane.

Mwaka 2011 katika maonesho

hayo ya wakulima MVIWATA

iliwawezesha wakulima zaidi ya 40

kushiriki maonesho hayo kwenye

viwanja vya Mwalimu Nyerere

Morogoro na Themi Arusha, kwa

lengo la kuwapatia fursa ya kujifunza,

kubadilishana uzoefu na kutangaza

bidhaa zao. Katika maonesho hayo

MVIWATA ilipata ushindi wa kwanza

kwa upande wa vyama na mashirika

yasiyo ya kiserikali kwenye uwanja

wa maonesho ya NaneNane kanda

ya Mashariki wa Mwalimu Nyerere

Morogoro na katika kanda ya

Kaskazini kwenye viwanja vya Themi

14

Arusha na kukabidhiwa zawadi ya

Kombe na Cheti vilivyotolewa na

Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda.

Aidha kwenye viwanja vya Themi

Arusha mkulima Bw. Richard Kipara

ambaye ni katibu wa Mtandao wa

Vikundi vya Wakulima Ekenywa

(MVIWAEKE) alishinda kuwa

‘Mkulima Bora’ wa wilaya mpya ya

Arusha Vijijini.

Katika maonesho hayo mfugaji

Bw. Moses Ndoipo kutoka wilaya ya

Longido, alileta mbuzi bora aina ya

Isiolo wa uzito wa kilo 240 aliyekuwa

anauzwa Sh. 300,000 na kuwa

kivutio kwa wageni waliotembelea

maonesho.

Miongoni mwa wakulima waliopata

fursa ya kushiriki maonesho haya

ya NaneNane kwenye viwanja

vya Mwalimu Nyerere Morogoro,

walielezea umuhimu wa bidhaa

walizoonesha na faida ya maonesho

kwa ujumla.

Kakao na Mawese

Bibi Lain Mwakatundu kutoka

Kyela, Mbeya alikuwa na zao la

mawese na kakao ambapo

alisema usindikaji wa mawese

unawezesha utengenezaji wa bidhaa

mbalimbali muhimu kama vile sabuni

ya kufulia na kuogea.

Lain Mwakatundu

“Vile vile kutokana na mawese

unaweza kupata mbosa ambayo

hutengeneza mafuta ya kupikia

na kupaka. Mafuta haya ya kupaka

yanafaida kubwa ikiwemo ya

kuponya mba wa ngozi katika mwili

wa binadamu. Aidha magamba ya

mawese hutumika kwa ajili ya kuni.

Kwa upande wa zao la kakao

alisema lina matumizi mengi

ingawaje matumizi yanayofahamika

zaidi kwa watu ni utengenezaji

Endelea Uk wa 15

Mwenyekiti wa MVIWATA Morogoro Bw. Stanford Chabonga aliyenyanyua juu kikombe, akiungwa mkono na wana-MVIWATA wenzake

kusherehekea ushindi

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Inatoka uk. wa 14

wa kinywaji na kitafunwa aina ya

chocolate. Akaongeza kuwa “ndani

ya tunda la kakao kuna mbegu zenye

ladha ya sukari ambazo hutumika

kutengeneza juisi lakini pia juisi hiyo

waweza kuichachusha na kupata

kilevi baada ya kuiweka kwa muda

wa siku tatu hadi nne.”

“Mbegu hizi za kakao pia

zikikaushwa na kusagwa hupatikana

unga laini ambao unafaa kwa

matumizi mengi ikiwemo kuweka

kama kiungo kwenye mboga na

wengine hutafuna unga pekee maan

unaradha nzuri,” anafafanua.

Bibi. Mwakatundu anafafanua zaidi

kuwa zao la kakao ni dawa nzuri

ya kupunguza kasi ya ugonjwa wa

kisukari mwilini na pia hupunguza

mafuta ndani ya mwili wa binadamu,

hivyo anawahimiza watanzania

kulitumia zaidi.

Anaeleza kuwa katika mkoa wa

Mbeya hususan wilaya ya Kyela mazao

ya Kakao na Mawese hulimwa kwa

ajili ya chakula na biashara japokuwa

soko lake kwa sasa siyo zuri. Hata

hivyo anaongeza kuwa maonesho ya

mwaka huu yamemsaidia kupanua

wigo wa soko kwani hivi sasa

amepokea maombi ya wateja wengi

wanaohitaji bidhaa na wengine

wameomba aende kuwafundisha

kilimo cha mazao hayo.

Tiba asili

Mzee Hassan Nundu kutoka

kijiji cha Chamkoroma wilaya ya

Kongwa - Dodoma, yeye alionesha

dawa za asili zinazotokana na

magome na mizizi ya miti ambazo

zinaaminika kutibu magonjwa

mbalimbali ya binadamu kama vile

meno, tumbo, athma pamoja na

kideri cha kuku.

Akielezea matibabu ya ugonjwa

wa vidonda vya tumbo, anasema

mgonjwa anayetumia dawa hiyo

anapona kwa muda mfupi hata kama

vidonda ni vya muda mrefu. “Dawa

hii ambayo ni mchanganyiko wa

mizizi ya miti mbalimbali, mtumiaji

huchanganya na maziwa mabichi

kwa kuweka kijiko kimoja cha

dawa katika kikombe cha maziwa

na kunywa mara tatu kwa siku kwa

muda wa siku kumi na tano tu.”

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

“Dawa nyingine ni ya fangasi

ambapo fangasi hawa huwa tumboni

na kwenye mapacha ya vidole vya

miguu kutokana na joto linalokuwepo

ndani ya kiatu kufuatia msuguano

wa miguu ya mtu anapotembea.

Dawa hii ya unga inampasa mgonjwa

kuiweka kwenye maji baridi na kisha

kuichuja ili kupata mabaki ambayo

atayapaka sehemu zilizoathirika na

baadaye kunywa dawa iliyochujwa

mara tatu kwa siku kwa muda wa

siku tatu na atapona kabisa.”

Bw. Nundu anafafanua kuwa

athma ni ugonjwa ambao hauna tiba

hospitalini bali hutulizwa lakini yeye

anayo dawa ya kutibu ugonjwa huu

ambayo inapatikana kwenye vipaketi

vitatu. Mgonjwa anapaswa kuiloweka

na kuichuja kisha kunywa mara mbili

kwa siku asubuhi na jioni.

“Ninawashauri Watanzania

kurudia dawa zao za asili

zinazotokana na mizizi na magome

ya miti kwani hazina kemikali

zitakazowadhuru kiafya tofauti na

dawa za hospitalini ambazo nyingi

sasa ni bandia na kuongeza kuwa

anazo dawa nyingi za asili zinazotibu

maradhi ambayo hayawezi kutibiwa

hospitalini kama vile kukojoa

kitandani pamoja na meno ambayo

mara nyingi hung’olewa badala ya

kutibiwa.

Mzee Nundu anasema maonesho

ya NaneNane ambayo amekuwa

akishiriki yanamsaidia kupata wateja

wapya na kukutana na wagonjwa

aliowatibu miaka ya nyuma ambao

wanashuhudia kuponywa na dawa

zake.

Bibi Hortenzia Thomas kutoka

kijiji cha Nyandira Mvomero, mkoani

Morogoro alifika katika maonesho

hayo kutangaza tiba asili itokanayo

na matunda na mbogamboga

zikiwemo njegere, sereri, cornflower,

maharagwe, redishi, boga, nzukini,

pasili na kabichi.

Anaeleza kuwa kabichi huponya

ugonjwa wa kisukari. Hii ni baada ya

mgonjwa kuchukua mti wa katikati ya

kabichi kuukatakata na kuuchemsha,

kisha kunywa maji yake mara tatu

kwa siku. Pia mboga mboga kama

Radishi na tenepsi hutumika kutibu

vidonda vya tumbo na shinikizo la

damu.

KUTOKA MITANDAONI

Bibi Mwajuma Mwiyoha,

ni mkulima kutoka Chamkoroma

ambaye alifika kwenye maonesho

haya akiwa na zao la Alizeti ambalo

ni maarufu kwa kutengeneza mafuta

ya kupikia. Hata hivyo, kwa mkulima

huyo zao la Alizeti siyo kwa ajili

ya kukamua mafuta pekee bali pia

hulitumia kutengeneza dawa ya

kuhifadhia mazao galán, dawa ambayo

haina madhara kwa watumiaji.

Mwajuma Mwiyoha

“Dawa hii ya kuhifadhia mazao

hutokana na masuke ya alzeti

hutengenezwa kwa teknolojia

rahisi tu ambayo mkulima yeyote

anaweza kumudu kwani cha kufanya

ni kuyachoma masuke ya alizeti

kwenye chombo kisafi, yakishaungua

vizuri hutwangwa na kuchekechwa

ili kupata majivu laini ambayo

ndio dawa yenyewe. Dawa hii

hunyunyizwa juu ya magunia yenye

mazao na ina uwezo wa kuzuia

mazao yasishambiliwe na wadudu

kwa muda wa miaka miwili hadi

mitatu.

Bibi. Mwiyoha anasema dawa hii

ni nafuu kwani haimwingizii mkulima

gharama na ni salama kwa afya ya

binadamu.

Ufugaji wa nyuki wadogo

Bw. Hassan Haji kutoka Zanzíbar

ni mkulima mdogo anayefuga nyuki

wadogo wasiouma.

Mkulima huyu ameanza ufugaji wa

nyuki wasiouma miaka 15 iliyopita.

Alianza ufugaji wa nyuki hao kama

mradi wa kiuchumi lakini pia kwa

lengo la kuwahifadhi baada ya kuona

kwamba wako hatarini kutoweka

kutokana ukataji wa miti katika

maeneo ya misitu vitendo ambavyo

vinawafanya viumbe hao kukimbia

na hivyo kizazi hicho kupotea.

Endelea Uk wa 17

15

KUTOKA MITANDAONI

16

Ludewa wahimizwa kuwekeza

kwenye kilimo cha miti

Na Susuma Susuma, Ludewa

Wakulima wilayani

Ludewa na nchini kote

wametakiwa kuwekeza

zaidi katika upandaji wa miti

kibiashara ili kuhifadhi mazingira

na kujiongezea kipato kutokana

na soko la miti kuongezeka kila

mwaka.

Wito huo umetolewa na Naibu

Mkurugenzi wa Shirika la Swedish

Cooperative Center (SCC) Kanda

ya Mashariki mwa Afrika Bw. George

Onyango alipokuwa akizungumza na

wakulima wa kata za Mlangali na

Milo wilayani Ludewa katika mkoa

mpya wa Njombe.

Bw. Onyango alikuwa kwenye

ziara ya kukagua maendeleo ya

mradi wenye lengo la kuwawezesha

wakulima wadogo kuwa na uzalishaji

wenye kukuza na kuongeza kipato

na uhifadhi wa mazingira na bioanuai

Uharibifu

huu tuliufanya sisi katika

harakati za kujitafutia riziki, na

tunaoathirika na uharibifu huu ni sisi, hivyo

ni sisi wenyewe ndiyo tunapaswa kurejesha

uhai wa mazingira yetu kwa kuwekeza kwenye

upandaji miti na kwa kufanya hivi tutasaidia

kupunguza athari za mabadiliko ya

tabia ya nchi

k a t i k a

Ziwa Nyasa unaotekelezwa na

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima

Wadogo Tanzania (MVIWATA) kwa

kushirikiana na SCC.

Bw. Onyango alisema biashara ya

miti na mazao yake, inakuwa kila siku

na kupanda bei, hivyo kwa kuwekeza

zaidi kwenye upandaji miti wakulima

hao watapata mapato mazuri kuliko

hata wanayoyapata kwenye mazao

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Swedish Cooperative Center (SCC) Kanda ya Mashariki mwa

Afrika Bw. George Onyango (aliyenyosha mkono) akizungumza na wakulima wa kata ya Mlangali

ya chakula wanayolima.

Aidha aliwataka wakulima hao

kuunda mitandao imara itakayofanya

kazi ya kutafuta na kusimamia soko

la mazao ya miti ili kuondokana na

walanguzi ambao sasa wananeemeka

kwenye biashara ya mazao ya chakula

ya wakulima.

Naibu mkurugenzi

huyo alisema licha ya

kuwaingizia utajiri,

kilimo cha miti

kitasaidia kwa

kiwango kikubwa

katika utunzaji

wa mazingira ya

wilaya hiyo ambayo

yameharibiwa kutokana

na shughuli za kibinadamu

zikiwemo ukataji miti kwa ajili ya

kupata nishati ya mkaa na kuni.

“Uharibifu huu tuliufanya sisi

katika harakati za kujitafutia riziki,

na tunaoathirika na uharibifu

huu ni sisi, hivyo ni sisi wenyewe

ndiyo tunapaswa kurejesha uhai

wa mazingira yetu kwa kuwekeza

kwenye upandaji miti na kwa kufanya

hivi tutasaidia kupunguza athari za

mabadiliko ya tabia ya nchi,” alisema

Bw. Onyango.

Aliwahimiza wakulima hao

kutumia vyema elimu ya uhifadhi wa

mazingira, ujasiriamali na usimamizi

wa vikundi inayotolewa kupitia

mradi huo.

Kwa upande wake afisa

anayesimamia mradi huo wilayani

Ludewa Bw.Remmy Urio alisema

matokeo ya mafunzo yaliyotolewa

kwa wakulima yameanza kuonekana

baada ya wengi wao kuanza kupanda

miti kwenye maeneo ya wazi na

wameimarisha usimamizi wa sheria

zinazolinda mazingira.

Bw. Urio alisema wakulima wengi

pia wameibua miradi ya kiuchumi

ikiwemo uanzishaji wa SACCOS

ili kuwawezesha kuboresha kipato

badala ya kutegemea kipato kutoka

kwenye kazi zinazochangia uharibifu

wa mazingira.

Afisa Programu wa MVIWATA

Bw. Laurent Kaburire alisema, utafiti

uliofanywa na MVIWATA kwenye

wilaya zinazounganishwa na Ziwa

Nyasa kwa upande wa Tanzania,

umebaini kwa shughuli nyingi

zinazoathiri ziwa zinatekelezwa

na wavuvi, wafugaji na wakulima

Endelea Uk wa 17

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Maonesho ya NaneNane 201...

Inatoka uk. wa 15

Miongoni mwa faida anazozipata

Bw. Haji ni pamoja na kujipatia kipato

kwa ajili ya familia yake kwani kwa

sasa anao wateja wengi wanaotumia

asali ya nyuki hawa wasiouma na

kwamba asali yake ina soko zuri. Kwa

sasa ana jumla ya mizinga 20 ya nyuki

ingawaje changamoto anayokutana

nayo katika kupanua ufugaji huo ni

ugumu kuwapata kutoka msituni

kwani huwa wanajificha sana.

“Ninawashauri watanzania

kupenda kutumia zaidi asali kwani ni

kinga ya maradhi mengi kwenye mwili

wa binadamu. Hiki ni chakula kizuri

mno hasa kwa watoto, nawaambia

wazazi wasiwape watoto pia badala

yake wawape asali,” anasisitiza.

Ukaushaji matunda na

mbogamboga

Bw. Zuberi Sultani kutoka

Korogwe Tanga kwenye maonesho

haya yeye alionesha utaalamu

wa kuhifadhi matunda na

mboga mboga kwa njia

ya ukaushaji. Miongoni mwa

matunda yanayosindikwa ndizi,

mananasi, maembe pamoja na

zikiwemo mbogamboga kama vile

mchunga na kisamvu.

Anafafanua kuwa usindikaji wa

matunda na mboga unafanyika ili

kuyahifadhi na kutumika kwa msimu

wote wa mwaka, wakulima wengi

wa matunda hawanufaiki na kilimo

hicho kwa sababu msimu wa mavuno

matunda hushuka bei na mengine

kuoza kwa kuwa wakulima hawana

ujuzi wa kuyahifadhi.

Anasema ukaushaji huu hutumia

teknolojia rahisi, ambayo yeye

amekuwa akiwafundisha wakulima

wenzake bure ili nao wanufaike.

“Tunakausha kwa kutumia chombo

maalum ambacho hufunikwa na

turubali jeusi juu kwa lengo la

kupunguza ukali wa mionzi ya jua

na kuhakikisha kwamba haileti

madhara kwa watumiaji. Matunda

haya yanapokaushwa huzidishiwa

ubora kwani sukari yake huongezeka

mara dufu ukilinganisha na tunda

linavyokuwa katika hali ya kawaida.”

“Mtanzania yeyote anaweza

kusindika matunda na hata mboga

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

kwani si kazi ngumu bali inahitaji

usafi na uangalifu wa karibu ili

kuhakikisha bidhaa inakuwa katika

kiwango cha juu cha ubora ili isilete

madhara kwa binadamu,” anaeleza.

Bw. Sultani anasema kwamba

utaratibu wa kusindika matunda

huanzia katika utafutaji wa matunda

mazuri yaliyoiva kiasi, unayaosha

kuyakata vipande vidogo vinavyoweza

kukauka upesi, kisha kuyaweka

kwenye chombo kinachotumia

mwanga wa jua kukaushia na

baada ya hapo huhifadhiwa kwenye

vifungashio maalum tayari kwa

kuuzwa.

Utaratibu huu unafanana vile vile

katika mboga za majani ambapo

huoshwa na kuchemshwa kidogo

jikoni kisha huanikwa katika

chombo kinachotumia mwanga wa

jua kukaushia mazao na baada ya

kukauka huwa tayari kufangashwa

kwa ajili ya kuuzwa ama kuliwa.

Usindikaji zao la Muhogo

Bw. Juma Nyamgunda kutoka

Mkuranga Pwani anasema katika

kuhakikisha kwamba zao hili la

muhogo linaongezewa thamani

wakulima wa Mkuranga wameanza

kusindika muhogo na kupata unga

ambao huutumia katika kutengeneza

Watazamaji wakitoka kwenye banda la MVIWATA

KUTOKA MITANDAONI

vitu mbalimbali ikiwemo keki, biscuti,

tambi, chinchin, chapati na maandazi

kazi ambayo hufanywa kwa wingi na

kina mama kwa lengo la kuongeza

kipato cha familia.

Bw. Nyamgunda anasema

usindikaji unawapa faida kubwa

wakulima ukilinganisha na

walivyokuwa wakiuza muhogo ghafi

kwa walanguzi na katika maonesho

ya NaneNane amepata wateja wengi

wanaohitaji kiwango kikubwa cha

unga wa muhogo.

Ludewa

wahimizwa...

Inatoka uk. wa 16

wadogo ambao kipato chao ni

kidogo ama cha wastani.

Alisema katika hatua ya awali ya

miaka mitatu ya majaribio, mradi

unatekelezwa kwenye wilaya mbili

ambazo ni Kyela mkoani Mbeya na

Ludewa mkoani Njombe. Katika

hatua ya pili ya mradi utajumuisha

wilaya za Mbinga mkoani Ruvuma

na Makete mkoani Njombe.

Kwa ujumla mradi unalenga

kuwafikia na kuwanufaisha

wakulima,wafugaji na wavuvi

wapatao 15,000 wa hapa nchini.

17

MAKALA

Mtweve: Ubunifu wangu wa redio

umenufaisha wengi

Anamiliki Mlangali Coconut FM

Hatimaye ndoto ya siku

nyingi ya Bw. Ditrick

Mtweve (18) mkazi wa

Kata ya Mlangali wilayani Ludewa

mkoa mpya wa Njombe imeweza

kutimia baada ya kutumia ubunifu

wake kutengeneza mtambo wa

redio unaowanufaisha wakazi

wengi wa wilaya hiyo.

Mtambo huo uliotokana na

kuunganishwa kwa vifaa mbalimbali

kutoka katika redio mbovu na vifaa

vinginevyo kama miti ya mianzi,

boksi na vyuma vya baiskeli, ulianza

kurusha matangazo yake mwaka jana

katika kijiji cha Lufumbu na kwa sasa

matangazo hayo yanawafikia wakazi

wa vijiji sita katika Kata ya Mlangali.

Kwa sasa redio hii ambayo ameipa

jina la ‘Mlangali Coconut FM’ imekuwa

ikitumiwa na viongozi wa vijiji vya

kata ya Mlangali kutangaza taarifa

muhimu kama vile mikutano ya

vijiji, kampeni ya chanjo pia shughuli

muhimu za kijamii.

Vile vile imekuwa kichocheo

kikubwa cha biashara na burudani

kwani watu binafsi hutumia redio

hiyo kutangaza biashara na huduma

wanazotoa bila kusahau wapenzi wa

muziki wa kisasa na nyimbo za injili

ambao pia hupata fursa ya kupiga simu

Mwanachama na mhamasishaji wa MVIWATA Mlangali akizungumza kwenye kipindi cha

karibu mgeni

18

na kuchagua wimbo waupendao.

Bw. Mtweve ambaye ni mtoto

pekee kwenye familia na yatima

(aliyefiwa na baba) alisema kuwa

alitamani siku moja katika maisha

yake awe mtangazaji maarufu

wa redio kubwa hapa nchini na

ikiwezekana aweze kumiliki redio

yake mwenyewe na mapema mwaka

2009 akiwa kidato cha tatu katika

Shule ya Sekondari ya Lufumbu

ndoto yake ilianza kutimia ambapo

kwa kutumia maarifa madogo

aliyoyapata shuleni alianza kubuni na

kutengeneza mtambo huo wa redio.

“Wakati naanza ilikuwa kama

mchezo, kwanza nilichukua muda

nikitafakari kwanini ‘Microphone’

zisizo na waya zinasafirisha sauti

na kuupeleka katika mitambo.

Baadaye nilichukua kifaa ‘transistor’

kilichotumika katika ‘Microphone’

hizo na vifaa vingine nilivichukua

katika redio mbovu na kuviunganisha,”

alisema Bw. Mtweve.

Baada ya kukusanya vifaa

mbalimbali kutoka kwenye redio

mbovu na maeneo mengine pia

alitumia betri za kawaida hatimaye

kufanikiwa kuwasha mtambo wake

na redio yake kuanza kusikilizwa na

wananchi waishio jirani.

Uwezo huu wa redio kusikilizwa

na watu wa jirani ulianza baada ya

kuboresha baadhi ya vifaa vyenye

uwezo mkubwa zaidi ili kuwezesha

mawimbi ya sauti kufika mbali zaidi na

hatimaye alifanikiwa kufunga mnara

wa mlingoti wa miti iliyounganishwa

wenye antena ya waya wa kawaida

juu yake na kuutundika juu ya

kilele cha mlima uliokuwa jirani na

nyumbani kwao.

“Haikuwa kazi ndogo kwani

mwanzoni niliweka mtambo huu

nyumbani kwetu ambako ni bondeni

ikawa inasikika nyumba kadhaa za

jirani tu. Ilibidi kutumia muda mwingi

na kuumiza akili ili kuweza kufikia

mafanikio, baadaye nikapata wazo

la kuhamia hapa mlimani kwenye

nyumba ya rafiki yangu ambaye

amenipangishia chumba kimoja,”

alisema Bw. Mtweve alipozungumza

na Pambazuko ndani ya studio yake

kijijini Lufumbu.

Bw. Mtweve alisema anafurahia

ubunifu wake lakini bado anakabiliwa

na changamoto nyingi sana ikiwemo

kutokujua sheria “mpaka sasa redio

hii naimiliki kienyeji kwa lengo la

kukuza kipaji changu na kuiwezesha

jamii inayonizunguka kunufaika na

kipaji hicho, sijui taratibu za kuisajili

zikoje,” alisema Bw. Mtweve.

Tatizo jingine ni kukosa mtaji wa

kuweza kununua vifaa vya kisasa na

kuwa na jengo maalumu la studio ya

utangazaji.

Kwa hivi sasa Bw. Mtweve anaishi

na mama yake baada ya baba yake

kufariki wakati yeyé akiwa na umri

wa miaka 10 na alikuwa akisoma

darasa la tatu wakati huo.

Endelea Uk wa 19

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Inatoka uk. wa 18

Alisema hali hiyo ya kubakia na

mzazi mmoja imechangia kwa kiasi

kikubwa umasikini katika familia

yao baada ya mama yake kutokuwa

na uwezo wa kifedha na hata afya

yake kutokuwa thabiti kutokana

na maradhi yanayomsumbua na

hivyo wakati mwingine hulazimika

kusimamisha kazi za redio ili

kumsaidia mama yake shughuli za

shamba.

“Redio hii huwa hewani kwa

masaa 24 kila siku kwa kurusha

muziki hewani na salamu, short

time za muziki wa bongo flava na

chaguo la msikilizaji, na inapofika

4.00 usiku hurudi nyumbani na

kuuacha mtambo ukipiga muziki

mpaka alfajiri ninapoingia kuendelea

na vipindi,” alisema Bw. Mtweve.

Awali kabla ya kufikia kiwango

cha kurusha matangazo saa 24,

alikuwa akitumia redio inayotumia

kanda za kawaida na baadaye alipata

redio yenye kutumia ‘memory card’

ambayo imekuwa ikimwezesha

kupiga muziki muda wote.

Hata hivyo eneo hili la Mlangali

bado halijafikwia na huduma ya

umeme wa Tanesco hali inayomlazimu

kutumia betri za kawaida za

redio kuendeshea mtambo wake.

“Nimekuwa nikiwategemea watu

mmoja mmoja ambao wanavutiwa

na huduma hii, kuninunulia betri,

kuna wakati zinapoisha na hakuna

mtu wa kununua ninalazimika kuzima

matangazo kwa siku kadhaa, hadi

ninapoenda kufanya kibarua mahali

Afisa programu wa MVIWATA Bw. Laurent Kaburire akimtambulisha Bw.Ditrick Mtweve kwa

wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 16 wa MVIWATA Oktoba 24, 2011 mjini Morogoro

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Hii ndiyo mitambo ya kurusha matangazo

ya COCONUT FM

na kupata fedha, nitafurahi kama

kijijini kwetu tutapata umeme.”

Wakazi wa vijiji vya kata hiyo

ambao hawakuwa wakimiliki

redio majumbani mwao kwa sasa

wameanza kumiliki redio na kusikia

matangazo na burudani kutoka

katika mtambo wa redio ya kijana

huyo.

Wafanyabiashara wa Mlangali nao

kwa uchache wameanza kuitumia

fursa ya redio hii kujitangaza na

humlipa kati ya Sh 500 na 1,000 ili

kuweza kurushiwa matangazo yao

redioni kwa siku kiwango ambacho

kijana huyo anasema kuwa kimekuwa

kikimsaidia kwa mahitaji binafsi yeye

na mama yake.

Anasema hata hivyo kuwa kwa

sasa yeye ndiye mtangazaji na fundi

mitambo wa redio hiyo. Anawaomba

wananchi wenye uwezo na ambao

wanaguswa na kipaji chake kumsaidia

kuweza kwenda kusoma katika chuo

cha ufundi stadi (Veta) ili kuongeza

maarifa.

Sambamba na hilo, kijana huyu

anaeleza kuwa kamwe ndoto zake

MAKALA

hazitaishia hapo, bali ataendelea

kubuni mbinu mbalimbali na

kuboresha kazi yake hiyo na kiu

yake ni kuona siku moja redio hiyo

inasikika katika wilaya nzima ya

Ludewa.

Bw. Mtweve anaishukuru jamii

inayomzunguka kwani pamoja na

kukosa fedha sambamba na ufinyu wa

elimu ya ufundi alionayo, bado jamii

hiyo imekuwa msaada mkubwa sana

kwake kwani wameweza kutambua

umuhimu wake katika jamii kwa

kumpati redio mbovu ili aweze kutoa

vifaa muhimu kwa kazi yake.

Hii ndiyo studio ya COCONUT FM

Kwa kutambua mchango mkubwa

anaoutoa katika kuhakikisha jamii ya

vijijini inafikiwa na habari, Mtandao

wa Vikundi vya Wakulima Tanzania

(MVIWATA), ulimwalika Bw. Mtweve

na kuwezesha kushiriki kwenye

Warsha ya Kitaifa na Mkutano Mkuu

wa 16 wa MVIWATA uliofanyika

Oktoba 24 na 25, 2011 mjini

Morogoro.

Mojawapo ya mada iliyojadiliwa

kwenye warsha hiyo na kugusa hisia

ni “haki ya upatikanaji wa

habari vijijini” ambapo wakulima

kutoka vijiji mbalimbali walieleza

jinsi ambavyo wanakabiliwa na

changamoto katika kupokea na

kutoa habari katika kutokana na

vyombo vingi vya habari kuegemea

zaidi mijini.

Hivyo washiriki hao walipongeza

ubunifu wa kijana huyo na kuomba

MVIWATA kama taasisi kuendelea

kumuunga mkono na kumtumia

kutangaza zaidi habari za wakulima.

Jambo hilo limetekeleza na hivi sasa

baadhi ya vipindi vya SAUTI YA

MVIWATA vinarushwa kupitia redio

hiyo Mlangali Coconut FM.

19

KUTOKA MITANDAONI

Viongozi wa masoko ya wakulima

wapewa ushauri

Na Susuma Susuma, Morogoro

Viongozi wa masoko ya

wakulima wametakiwa

kutojenga uhasama na

viongozi wa awamu zilizopita bali

wawatumie kujifunza na kupata

mbinu za kuyafanya masoko hayo

kuwa endelevu.

Wito huo umetolewa Julai

30,2011 mjini Morogoro na

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi

wa Soko la Wakulima la Kibaigwa

Kongwa mkoani Dodoma Bw.

Richard Kapinye kwenye kikao cha

pamoja cha wakurugenzi wa bodi

za masoko sita yaliyojengwa na

MVIWATA kwenye vijiji mbalimbali

hapa nchini.

Bw. Kapinye alisema “tuepuke

uhasama unaofanywa na wanasiasa

kwamba akishamuondoa mwenzake

madarakani wanakuwa maadui

wanaotafuta kuharibiana kila wakati,

sisi tuwe tofauti tuwatumieni

wenzetu waliotutangulia ili tuweze

kufanikiwa.”

Kadhalika Bw. Kapinye ambaye

pia ni mkulima mdogo na Diwani

wa Kata ya Kibaigwa, aliwataka

wajumbe wenzake kutumie

vyema dhamana waliyopewa kwa

20

kusimamia haki na maslahi ya

wakulima huku akitahadharisha

tabia inayojitokeza ya baadhi ya

wakulima wanaopata nyadhifa za

kisiasa, kusahau walikotoka na

kuanza kuwakandamiza wenzao.

Akawahimiza pia wakulima ili

kupanua uelewa wawe na hamasa

ya kujifunza mambo mapya kwa

kusoma magazeti na machapisho

mengine likiwemo jarida la wakulima

la Pambazuko (Sauti ya Wakulima)

linalochapishwa na MVIWATA.

Kwa upande wake mratibu wa

kikao hicho ambaye pia ni Afisa

Masoko wa MVIWATA Bw. Jimmy

Mongi aliwahimiza wakurugenzi hao

wa bodi, wawatumie wajumbe wenye

uzoefu walioko masoko ya jirani ili

kuwafundisha na kuwajengea uwezo

wajumbe wapya wanaochaguliwa.

“Tunaamini kuwa wajumbe

wa mwanzo kwenye bodi hizi,

walijengewa uwezo mkubwa kielimu

kwa kupelekwa ziara mbalimbali

za mafunzo, hivyo tunapofikiria

kupata mafunzo kwa wajumbe

wapya tuwafikirie kwanza hawa,

ni wenzetu watatupatia elimu

hiyo kwa gharama ndogo na pale

panapohitajika utaalamu zaidi ndipo

tuombe msaada wa MVIWATA ofisi

Kufunga mipaka ya kuuza mazao nje ya nchi

kunamsababishia hasara mkulima

Na Martin Pius, Babati

Serikali imetakiwa kutotoa

amri za kuzuia mazao ya

chakula yakiwamo mahindi

kuuzwa nje ya nchi kwani kufanya

hivyo inawasababishia hasara

wakulima na kuwakatisha tamaa

ya kuongeza uzalishaji.

Rai hiyo imetolewa Julai

13, 2011 na Mjumbe wa Bodi

ya Mtandao wa Jinsia Tanzania

(TGNP), Bibi Rehema Mwateba

wakati akifungua Mkutano Mkuu

wa nne wa MVIWATA Manyara

uliowashirikisha wanachama wa

wilaya tano za mkoani Manyara.

Bibi Mwateba alisema Serikali

itambue kwamba inatumia mfumo

kandamizi kwa mkulima kwa kufunga

mipaka ya kuuza mazao ndani na nje

ya nchi bila ya kujali kuwa hilo ni

hitaji la mkulima la kuendesha maisha

yake yanayotegemea hasa bei nzuri

ya mazao. Alisema kuzuia biashara

ya mazao kwa kutumia kisingizio cha

kinga ya njaa hakitavumilika kwani

wakati utafika wakulima watachukua

kuu,” alisema Bw. Mongi

Kwa upande wake Bibi.

Honolata Blass, mjumbe wa bodi

ya Soko la Nyandira alisema bodi

za wakurugenzi zinapaswa kuwa

na ubunifu ili kuongeza ufanisi wa

masoko. “Kwa upande wetu ubunifu

wa bodi umesaidia kuongeza mapato

ya soko kila mwaka na kulifanya soko

kuwanufaisha wakulima wengi,”

alisema Bibi Blass.

Bodi hizo za wakurugenzi wa

masoko hukutana mara kwa mara

kwa lengo la kuwapa wadau hao

fursa ya kushirikishana uzoefu wa

mafanikio, changamoto na kuweka

mikakati ya uendelevu wa masoko

hayo ya wakulima.

Kikao hiki kilikutanisha

wakurugenzi 25 wa bodi za masoko

ya Kibaigwa wilaya ya Kongwa,

Nyandira wilayani Mvomero, Tandai

na Tawa Morogoro Vijijini, Mkata

wilaya ya Handeni na Igagala wilayani

Njombe.

Masoko hayo yalijengwa na

MVIWATA tangu mwaka 2004 na

kukabidhiwa kwa halmashauri za

wilaya na uendeshaji wake kubakia

mikononi mwa bodi za wakurugenzi

ambazo zinaundwa na wakulima na

wawakilishi wa halmashauri.

hatua ambazo huenda zikawa na

madhara makubwa kwa taifa.

“Serikali inatakiwa kufanya

utafiti wa haraka kubaini maeneo

yaliyoathirika na njaa na kupeleka

chakula cha msaada na kwa maeneo

mengine yasiyokuwa na uhaba wa

chakula wakulima waruhusiwe

kuuza mazao yao nje ya nchi ili

kuweza kupata faida,” alisema.

Makamu Mwenyekiti wa

MVIWATA Manyara, Bibi Fatuma

Kimolo, akizungumza kwenye

mkutano huo alisema kama serikali

Endelea Uk wa 21

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Wakulima washauriwa wasidai

posho za mafunzo

Na Ledis Kigala, Kyela

Baadhi ya wakulima wilayani

Kyela mkoani Mbeya

wamewaasa wenzao

kutanguliza mbele manufaa ya

elimu wanayopata katika kshiriki

kwao kwenye mafunzo badala ya

kudai posho.

Wamesema mtindo wa kudai

posho kwanza, unawafanya wakulima

kushindwa kupata elimu muhimu

kwa ustawi wa maisha yao.

Walitoa wito huo wakati wa

kufunga mafunzo ya kuwajengea

uwezo katika uzalishaji bora wa

mazao ya mpunga, mahindi, kokoa

na ufugaji wa wanyama.

Mmoja wa wakulima hao Bw.

Goden Mwantimwa wa kijiji cha

Lutusyo kata ya Muungano wilayani

Kyela alieleza kufurahishwa na

elimu na mafunzo yanayoendelea

kutolewa na Mtandao wa Vikundi

vya Wakulima Tanzania (MVIWATA)

na kuahidi kuwa ataendelea kushiriki

kwa sababu kwake elimu ni muhimu

kuliko posho.

“Mimi niko tayari kujitolea

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

kushiriki mafunzo mengine hata kama

itakuwa nje ya hapa, nawaombeni

wenzangu tuithamini sana elimu hii

ili itusaidie katika kuboresha kilimo

chetu,” alisema Bw. Mwantimwa.

Kwa upande wake Bw. Musa

Mwangongolo mkulima wa kijiji

cha Makwale kata ya Makwale,

alisema tabia ya kudai posho

kutoka kwa waandaaji wa mafunzo

imesababbisha wadau mbalimbali wa

maendeleo kuwakimbia wakulima

wa eneo hilo.

Alisema matokeo yake ni

waandaaji kuhamishia mafunzo hayo

katika maeneo mengine na kuwaacha

wakulima wa Kyela wakiwa hawana

la kufanya.

Alisema kimsingi wakulima siyo

masikini wa kipato, na kwamba

umasikini wao ni maarifa ambayo

MVIWATA imeonyesha njia ili

kufikia azma ya kuboresha kilimo ili

kiwe chenye tija zaidi.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia

tarehe Septemba 21 hadi Oktoba 11,

2011 kwenye vijiji 18 vilivyoko kwenye

kata 10 za wilaya ya Kyela yalilenga

kuwapa elimu wakulima ya kuongeza

Bibi Edina Mwakipesile mkulima wa kijiji cha Mwiyonde wilayani Kyela akielezea dhana

ya MVIWATA kwa wakulima wenzake walioshiriki mafunzo ya kujengea uwezo vikundi,

yaliyoandaliwa na MVIWATA mjini Kyela.

KUTOKA MITANDAONI

uzalishaji pamoja na ubora wa mazao

na mifugo.

Mafunzo hayo ni sehemu ya

utekelezaji wa mradi wa Uhifadhi

Mazingira na Kukuza kipato

kwa wakulima wadogo waishio

kandokando ya ziwa Nyasa,

unaotekelezwa na MVIWATA

kwa ufadhili wa Shirika la Swedish

Cooperative Center (SCC).

Afisa Mradi huo Bw. Ledis Kigala,

alisema, mradi huo unatekelezwa

kwenye kata 10 kati ya kata 20

za wilaya ya Kyela ambazo ni

Bujonde, Ikolo, Ngonga, Ikimba,

Katumbasongwe, Ipande, Mwaya,

Ipinda, Muungano na Makwale.

Kufunga mipaka ya kuuza

mazao nje ya nchi...

Inatoka uk. wa 20

imeamua kufunga mipaka ya kuuza

chakula inatakiwa sasa ijipange

kununua mazao hayo ya wakulima

kwa bei yenye tija badala ya

kupanga bei yake isiyokuwa na

maslahi kwa mkulima.

Bibi Kimolo alisema kufungwa

mipaka kipindi hiki kumesababisha

bei ya mahindi kushuka kutoka

Sh. 45,000 na kufikia Sh 30,000

kwa gunia, hali ambayo inarudisha

nyuma maendeleo ya mkulima.

Alihoji kuwa iweje watumishi

wa Serikali wapandishiwe

mishahara kila mwaka kutokana

na kupanda kwa gharama ya

maisha, huku mkulima akiwekewa

masharti ya kupata ujira stahiki ili

aweze kukabiliana na hali ngumu ya

maisha magumu kwa kuuza mazao

kwenye soko lenye bei nzuri?

Alisema umefika wakati sasa,

serikali iache kutumia raslimali

nyingi kwenye kutoa na kusimamia

matamko ambayo hayana tija kwa

ustawi wa wakulima badala yake

nguvu na raslimali hizo zitumike

kuimarisha miundombinu ya

kilimo ili kiweze kuwa na uzalishaji

wa kutosheleza mahitaji ya chakula

na ziada ya biashara.

21

KATUNI

MUDA

MREFU NAONA

UNASOMA HILO

GAZETI LINA

HABARI GANI?

WEWE UTAZI-

PATA VIPI HABARI ZA

MJINI WAKATI GAZETI

LINACHUKUA SIKU 4

KUFIKA HAPA

22

OH! KWELI NDIO

SABABU

AHA

HAHA SIO HIVYO,

NI MFUMO WA TAARIFA

YA MASOKO MVIWATA.

NAPATA TAARIFA KUPI-

TIA SIMU YANGU YA

MKONONI TU.

AH! GAZETI

LENYEWE LINA

HABARI ZA MJINI TU,

SIONI HATA HABARI

INAYOGUSIA KERO

ZETU.

WAANDISHI

WENGI WANAJI-

SHUGHULISHA NA

MAMBO YA MJINI

TU.

SI

NINATUMIA

SIMU YANGU YA

MKONONI

ONA

SASA MIMI

SIJUI HATA KUTUMIA

HUO MTANDAO, HEBU

FIKIRIA NI WATU WAN-

GAPI HAWAPATI HIZO

HABARI?

HIVI KWANINI SISI

WATU WA VIJIJNI

HABARI ZETU

HAZIANDIKWI?

NDIO MAANA

HAKUNA HABARI ZA

KILIMO KWENYE

MAGAZETI

MENGI!

YAANI

UNAWAULIZA

WATU WA MJINI KWA

SIMU!?

LAKINI MIMI NAONA BADO

HIZO HABARI UNAZOPATA

KWENYE SIMU HAZIZUN-

GUMZII KILIMO

NANI ATAKUJUA

HUKU KIJIJINI

HUKU

HABARI ZI-

TAFIKAJE

HAPANA

NATUMIA

MTANDAO

AH!

MBONA

MWAKA JANA

WAANDISHI WALI-

KUJA WENGI TU

LAKINI

MIMI NAPATA

TAARIFA NYINGI ZA

MASOKO YA MJINI

KILA SIKU.

HAWA

WAANDISHI

WANAUPENDELEO

BWANA!

WE UM-

ESAHAU!? SI KWA

SABABU WALILETWA

NA WAHESHIMIWA

KWENYE KAMPE-

NI

MTANDAO

WA WAKULIMA

MVIWATA?

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

HUKU

HABARI ZA

KILIMO HAZIANDIKWI

NA WAKIANDIKA GAZETI

LINACHELEWA KUFIKA

AU LISIFIKE KABISA.

SASA HUKU KWETU

BARABARA NI TATIZO

LABDA TUTAPATA HIZO

HABARI KWENYE RA-

DIO NA TV

KWELI TUTAPATAJE

MAENDELEO KAMA HATUJUI

TAARIFA YA KILA SIKU YA

MASOKO, UCHUMI NA

SIASA?!

WATU WENGI WANAKUFA KWA KUKOSA

ELIMU YA AFYA NA KUAMINI IMANI PO-

TOFU ZA KWENDA KWA WAGANGA.

LAKINI TUSIWALAUMU SANA

WAANDISHI, MIMI NAFIKIRI

SERIKALI YETU IANGALIE NA

MIUNDO MBINU YETU

HATA KAMA ZIPO KU-

TOKANA NA HALI YA UCHU-

MI JE, TUTAWEZA KUNUNUA

HIZI TV NA UMEME

TUTAPATA WAPI?

HAPO

MAENDELEO

YATACHELEWA

SANA

EH

HAYO YOTE

YANATOKEA SABABU

HATUPATI HABARI

SAHIHI!

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

ACHA UCHUMI

TU, IDADI KUBWA YA

WATANZANIA WANAISHI

VIJIJINI NA UMEME

HAKUNA HAYO MATAN-

GAZO WATAYAONA

VIPI?

WANAHABARI

WANA NAFASI KUBWA

SANA YA KUELIMISHA

WATU KUHUSU MATUMIZI

BORA YA ARDHI, UFU-

GAJI BORA, BEI KATIKA

MASOKO

KWA-

HERINI

NDIO, BARABARA SIYO

NZURI KUWEZA KUSA-

FIRISHA MAGAZETI

YAFIKE HARAKA

SASA

NAFIKIRI MUDA

MUAFAKA KWA WAHUSIKA KU-

LIANGALIA HILI, SABABU VYOMBO

VYA HABARI NDIO VINAWEZA KU-

WAELIMISHA WATU NA KULETA

MAENDELEO HARAKA.

ITA-

TUSAIDIA KUPA-

TA ELIMU SAHIHI YA

AFYA, UKATILI DHIDI

YA WANAWAKE

HILI TATIZO LIFANYIWE KAZI, SABABU HATA RADIO ZENYEWE

HAZIFIKI VIJIJINI NA ZINATANGAZA UDHAIFU TU WA WATU WA

KIJIJINI INGAWA KUNA MAFANIKIO NA UBUNIFU WANAOUFANYA.

KATUNI

KWELI

BARABARA NI

TATIZO KWA SABABU

HATA MTOTO WA MZEE

KIPARA ALIFARIKI KWENYE

GARI KWA UBOVU WA

BARABARA.

WASAL-

IMIE RAFIKI

ZANGU’

JUZI NILIKUWA MJINI

NIMEONA MATANGAZO MENGI

YANAYOONESHA UDHAIFU

WA WATU WA KIJIJINI TU

INA MAANA HUKU HATUNA

MAMBO MAZURI YA KU-

TANGAZA NA TV?

23

KUTOKA MITANDAONI

Mfumo shirikishi unaharakisha

maendeleo

Na Gratian Cronery, MUCCoBS

Shinyanga

Maendeleo na ustawi

wa miradi ya kijamii

yanategemea zaidi

ushirikishwaji wa jamii husika

katika hatua zote.

Katika nchi yetu hali ni

tofauti ambapo miradi mingi

wanayopelekewa wananchi

hawakushirikishwa kikamilifu na

kwamba kinachofanyika ni wao

kupokea amri ya bwana mkubwa na

kutekeleza wasichokijua.

Hali hii ya kuwapelekea

wananchi maamuzi badala ya wao

kushiriki kuibua wazo na kuamua,

imesababisha miradi mingi kutotoa

matokeo chanya licha ya kugharimu

fedha nyingi.

Serikali katika kuwasaidia

wananchi kutekeleza mipango ya

maendeleo imekuwa ikianzisha

miradi ikiwemo ya kujenga majengo

kwa lengo la kuwasaidia wananchi, ila

ukweli ni kwamba fedha na raslimali

nyingi zimekuwa zikipotea bure.

Iko mifano mingi ya miradi ya

aina hii ambayo wananchi wanaipa

jina la ‘miradi ya serikali’ kwa kuwa

hawakushirikishwa na haikuwa

kipaumbele chao. Miradi hii ni kama

vile ya majengo ya masoko kwenye

vijiji vya Ruvu Darajani mkoani

Pwani, Buigiri wilaya ya Chamwino,

Ruaha mkoa wa Iringa na kwingineko

ambayo yametelekezwa na kuwa

vichaka vya wezi ama nyumba ya

wanyama na wadudu, baada ya

wananchi kususa kuyatumia kwa

kuwa haikuwa kipaumbele chao

na kwingineko uchaguzi wa eneo

haukuwa sahihi.

Huu ni mmoja wa mifano ya

24

miradi mingi ambayo imeanzishwa

na serikali pasipo kuwashirikisha

wananchi katika kutoa mawazo yao

na kupendekeza nini wanahitaji na ni

kwa matumizi gani, na kama ni jengo

likae sehemu gani.

Mfumo uliotumika kuanzisha

na kutekeleza kauli mbiu ya “kilimo

kwanza” ni ule ule wa amri kutoka

kwa bwana mkubwa, mkulima hana

hiari cha kuchagua kukataa hata

kama kilicholetwa ni mwiba kwake.

Vile vile serikali imekuja na

mpango wa zana bora za kilimo

ikiwemo matrekta madogo (power

tiller) na ambapo kwenye maeneo

mengi hazihitajiki kutokana na

aina ya udongo na mazingira.

Baada ya wakulima kulazimishwa

kuzinunua wamezigeuza matumizi

na kuwa mashine za kufua umeme,

kusukuma maji, kulanda mbao na

kusaga unga.

Hii ni changamoto kwa serikali na

wadau wengine ambao wanatazamia

kupeleka miradi kwa wananchi,

kwamba ni vyema kuzingatia

ushirikishwaji wa wananchi na

mawazo yao yakaheshimiwa

ili baadaye wakithamini

wanachopelekewa.

Watanzania wanakabiliwa na kero

nyingi ambazo wangetarajia serikali

kuwekeza nguvu zake zaidi kwa

kutumia mfumo wa ushirikishwaji

katika kuzitatua. Kwa mfano

kuondoa kero ya ushuru mkubwa

wa mazao unaotozwa kwenye

vizuizi vya kila barabara ya nchi hii

inayoelekea mjini. Kuna maana gani

kumpa ruzuku ya pembejeo mkulima

na baadaye kumkamua faida yote

inayotokana na mavuno hayo?

Kama ushuru unatozwa ili kufidia

fedha za ruzuku, ni bora ruzuku

hiyo ifutwe wakulima wajitafutie

pembejeo na wawe huru kusafirisha

mazao yao. Hili linaweza kutatuliwa

kwa njia shirikishi ya majadiliano.

Kwa kufanya hivyo tunaweza

kutengeneza mipango na miradi

endelevu kwa vizazi na vizazi ambayo

italeta tija katika nyanja zote za

maisha kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kwa upande mwingine tumeona

mfano wa miradi ya ujenzi wa masoko

inayotekelezwa na MVIWATA

kwa mfumo shirikishi imefanya

vyema na wakulima wanathibitisha

matokeo yake. Mwenyekiti wa

MVIWATA Shinyanga Bw. Charles

Ndugulile anasema siri kubwa ya

mafanikio ya masoko ya MVIWATA

ni kuzingatiwa kwa dhana ya

ushirikishwaji.

“MVIWATA imefanikiwa kufanya

hivyo kwa hutoa mafunzo mazuri

ya jinsi ya kushirikisha jamii kuanzia

ngazi ya kaya hadi taifa ambayo

huambatana na mafunzo ya andiko

la mradi, uendeshaji na usimamizi

wa miradi, uhasibu wa vikundi na

mashirika pamoja na taasisi pamoja

na mifumo ya masoko na biashara,”

anasema Bw. Ndugulile.

Endapo serikali na wadau

wengine wa maendeleo watatumia

dhana hii ya ushirikishwaji wa jamii

kwa mapana na kuiona kama fursa

ya kuleta mabadiliko chanya kwa

jamii ya Watanzania, hakika taifa

litapiga hatua ya ukuaji wa kasi wa

maendeleo.

Jamii kwa upande wao pia

wanapaswa kujipanga vyema

kushiriki katika mradi kwa kuibua

wazo, kupanga, kutekeleza na

kusimamia na baadaye kujipima

kiwango cha uwajibikaji wao kwenye

miradi husika.

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Jipatie nakala ya Jarida la Pambazuko katika ofisi

za MVIWATA ngazi za kati zifuatazo

Mratibu

MVIWATA Morogoro

S.L.P 3220 Morogoro

Mahali: Uwanja wa Maonyesho NaneNane mkabala na

ofisi za TASO

Simu/Faksi: 023 261 41 84

Barua Pepe: morogoro@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Rukwa

S.L.P 468 Sumbawanga

Mahali: Jengo la Bethlehem Center – Barabara ya Msakila

Faksi: +255 25 280 25 58

Simu: +255 764 232 747, +255 784 940 606

Barua pepe: rukwa@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Mbeya

S.L.P 3015 Mbeya

Mahali: Jengo la Bima na CRDB Bank (Ghorofa ya

mwisho

Simu: +255 784 979 397, +255 652 835 568

Barua pepe: mbeya@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Chunya

Mahali: Jengo la Halmashauri, chumba Na.3

Barua pepe: chunya@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Iringa

S.L.P 918 Njombe

Mahali: Jengo la Njoluma, Njombe mjini

Simu: 0782 241 224, +255 767 241 224

Barua pepe: iringa@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Kilimanjaro

S.L.P 7389 Moshi

Mahali: Mbuyuni sokoni- ghorofa ya GOLDEN GROWN

LODGE

Simu: +255 27 275 16 39, +255 784 720 320

Barua pepe: kilimanjaro@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Kagera

S.L.P 1753 Bukoba Mjini

Mahali: Ofisi za Mayawa-Mtaa wa Rwamishenyi, Barabara

ya Uganda

Simu: +255 788 685818, +255 782 154961, +255 755 522 447

Barua pepe: kagera@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Dodoma

S.L.P 3293 Dodoma

Mahali:Area C Dodoma eneo la INADES Formation

Tz,mkabala na msikiti wa Area C

Simu:255-26-2350013, +255 782 257 783,

+255 767 881 352

Faksi: +255 26 2350744

Barua pepe: dodoma@mviwata.org

Pambazuko Na. 39 Toleo la Julai – Septemba 2011

Mwenyekiti

MVIWATA Monduli (MVIWAMO)

S.L.P 47 Monduli

Mahali: Barabara ya Boma-Moringe Sekondari, Monduli

Mjini

Simu: 255-27-253 8029, +255 27 253 8337

Faksi: +255 27 253 8338

Barua pepe: monduli@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Manyara

S. L. P. 446,

Babati Manyara

Mahali: Barabara ya Nyerere

SIMU: +255 27 253 0385 Faksi: +255 27 253 0707

Baruapepe: manyara@mviwata.org

Mwenyekiti

MVIWATA Tabora

S.L.P 175 Igunga

Mahali: Mtaa wa Uarabuni

Simu: +255 784 398 414, +255 782 219 551

Barua pepe: tabora@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Zanzibar

S.L.P 149 Zanzibar

Mahali: Mwana kwerekwe- mkabala na shule ya sekondari

M’kwerekwe A

Simu: +255 773 926 955, +255 777 470 518

+255 783 651 135

Barua pepe: zanzibar@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Ruvuma

S.L.P 696 Songea Manispaa

Mahali: Jengo la TTCL ghorofa ya 2

Simu: +255-25-2600626, +255 756 096 291

Barua pepe: ruvuma@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Mkuranga

S.L.P 56 Mkuranga

Mahali: Karibu na Stendi ya Kimanzichana

Simu: 0786 158 646

Barua pepe: mkuranga@mviwata.org

MAWAKALA

Mwenyekiti:

MVIWATA Shinyanga

S.L.P 1024 Shinyanga

Mahali: Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Shinyanga

(Kizumbi)

Simu: +255 763 740 675, +255 755 546 311

Barua Pepe: shinyanga@mviwata.org

Mwenyekiti

MVIWATA Kigoma

S.L.P 1144 Kigoma

Mahali: Ndani ya ofisi ya KIKANGONET, Lumumba road

jengo la NHC chumba 205

Simu: 0713 565 252, 0762 565 252

Barua pepe: aisimba@yahoo.co.uk

25

IJUE MVIWATA

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania- MVIWATA

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) ni chombo cha kuunganisha wakulima wadogo ili kuwa na sauti moja katika utetezi wa

maslahi yao ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa.

Mtandao huu ulianzishwa mwaka 1993 na wakulima wadogo. Kauli mbiu ya MVIWATA ni ‘Mtetezi wa Mkulima ni Mkulima

Mwenyewe’.

Falsafa, utume na dira ya MVIWATA

Falsafa ya MVIWATA inajengwa katika ya misingi ya ushawishi na utetezi wa maendeleo ya wakulima wadogo katika nyanja za kiuchumi na

kijamii; kuwezesha mawasiliano na kujifunza kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wakulima.

Utume wetu:

Kuimarisha mawasiliano na kuwaunganisha wakulima wadogo kupitia vikundi na mitandao yao katika ngazi mbali mbali ili kujenga mtandao wa

kitaifa wenye nguvu ya kuwezesha ushiriki na uwakilishi wa kweli wa maslahi ya wakulima wadogo katika ngazi zote za maamuzi.

Dira yetu:

MVIWATA ni kuwa chombo imara chenye nguvu za ushiriki na uwakilishi wa mawazo ya mkulima katika mchakato wa maamuzi ya kiuchumi,

kijamii na kisiasa. Kuwa na uwezo wa kutekeleza na kufuatilia michakato na shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayogusa maslahi ya

wakulima wadogo.

Malengo ya MVIWATA

1. Kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wakulima wadogo ili kujenga kwa pamoja mbinu na mikakati ya ushawishi na utetezi kwa maslahi ya

wakulima wadogo, kiuchumi na kijamii.

2. Kubadilishana mawazo, ujuzi na uzoefu juu ya kilimo na shughuli mbalimbali za wakulima ili kuboresha maisha na kuinua hali yao kiuchumi na

kijamii.

3. Kuwakilisha wakulima wadogo katika mashauriano na serikali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu au yanayoathiri ufanisi na maslahi ya

wakulima wadogo wa Tanzania.

Maeneo makuu ya mpango mkakati

1. Ushawishi na Utetezi: Kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kutetea maslahi yao.

2. Uwezo wa kiuchumi: kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kiuchumi kupitia njia za akiba na mikopo, kuunganisha wakulima na

masoko na elimu ya ujasiliamali

3. Kuimarisha vikundi na mitandao ya wakulima kwa lengo la kujipanga na kujitetea.

4. Masuala mtambuka: Kujenga uelewa wa wakulima juu ya Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya Tabia ya nchi.

5. Ujenzi wa kitaaasisi kwa lengo la kuimarisha shirika

Muundo

Muundo wa MVIWATA una ngazi tatu ambazo ni Ngazi ya Taifa, Ngazi ya Kati na Ngazi ya Msingi. Ngazi ya Kati inaundwa na mitandao ya

kimkoa na kiwilaya wakati Ngazi ya Msingi inaundwa na mitandao ya Kata na Vijiji.

Shughuli kuu

1. Kujenga uwezo wa wakulima wadogo kwa kupitia mafunzo shirikishi juu ya mbinu za ushawishi na utetezi, mbinu za kuimarisha uchumi wa

wakulima wadogo na uendelevu wa rasilimali kwa njia za warsha, mafunzo, mikutano na ziara za mafunzo.

2.

3.

4.

Kuhamasisha wakulima wadogo kujiunga katika vikundi vya kijamii na kiuchumi, mitandao ya msingi (kata na vijiji) na mitandao ya kati (mikoa

na wilaya). Mpaka sasa MVIWATA imeanzisha mitandao ya kimkoa katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,

Morogoro, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Tabora na Tanga kwa Tanzania Bara. MVIWATA pia imeanzisha mitandao ya kiwilaya katika Wilaya

za Monduli (Arusha) na Chunya (Mbeya). Tanzania Visiwani, MVIWATA Zanzibar imeanzishwa na kusajiliwa (Usajili namba 401). Mkakati

unaendelea wa kuimarisha mitandao iliyopo na kuanzisha mitandao mipya.

Kukusanya, kuweka katika kumbukumbu na kusambaza habari zinazohusu ujuzi na uzoefu wa wakulima, sera za kitaifa na kimataifa kwa

kupitia jarida la Pambazuko Sauti ya Wakulima, vipindi vya radio, vipeperushi, vijitabu na machapisho mengine.

Kuhamasisha na kuwezesha wakulima kubuni na kuendesha miradi shirikishi ya kiuchumi na uzalishaji kwa lengo la kuboresha uchumi wa

wakulima wadogo kama vile vyama vya mazao, vyama vya kuweka na kukopa na masoko ya mazao.

5. Kuandaa mikutano na warsha kuhusiana na mada zinazowagusa au kuathiri maslahi ya wakulima wadogo.

Uanachama na jinsi ya kujiunga na shirika

MVIWATA ina wanachama wa aina tatu (3).

Aina ya kwanza ni Wanachama wa Kawaida ambao wamegawanyika katika makundi mawili;

a) Kikundi cha wakulima wadogo au

b)

Mkulima mdogo binafsi aliye mwanachama katika Kikundi au Mtandao. Mkulima atakuwa mwanachama wa kawaida wa MVIWATA mara

tu Kikundi au Mtandao wake utakapokubaliwa kuwa mwanachama. Atapewa kadi ya uanachama na kikundi au mtandao utapewa cheti cha

utambulisho.

Aina ya pili ni Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo.

Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo vinavyojishughulisha na utetezi na ushawishi wa maslahi ya wakulima wadogo vilivyosajiliwa

chini ya sheria yoyote ya Tanzania katika Ngazi za Wilaya, Mkoa au Taifa vinaweza kuomba kuwa mwanachama wa MVIWATA iwapo vinakubaliana

kwa dhati na malengo na madhumuni ya Shirika.

Aina ya tatu ni Wanachama Washiriki

Ni mtu yeyote, taasisi au kikundi cha watu ambacho kinaunga mkono malengo na madhumuni ya Shirika. Mwanachama mshiriki anatamkwa na

Mkutano Mkuu wa MVIWATA.

Kila mwanachama, isipokuwa mwanachama mshiriki atalipa kiingilio na ada ya kila mwaka. Maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kujiunga na ada

yanapatikana kutoka kwa kiongozi au ofisi ya MVIWATA.

Kwa mawasiliano zaidi

Ofisi Kuu ya MVIWATA

Mkurugenzi Mtendaji

MVIWATA

S.L.P 3220 Morogoro

Simu: 023 261 41 84

Faksi: 023 261 41 84

Barua pepe: info@mviwata.org, mviwata@morogoro.net

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!