You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Toleo NO. 040 Oktoba – Disemba 2011 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937

Uk. 1

Je wakulima wadogo wamefaidi

matunda ya uhuru

Uk. 17

Bodi mpya ya MVIWATA

yachaguliwa

Uk. 20

Wakulima, matrekta waandamana

kupinga uporwaji ardhi
Toleo NO. 040

Oktoba Disemba 2011

Bei Shs. 500/=

ISSN 0856-5937

WAHARIRI

Susuma Msikula Susuma

Stephen Ruvuga

MHARIRI MSAIDIZI

TOLEO NO.040

BODI YA MVIWATA

Mwenyekiti – Habibu Simbamkuti

Makamu Mwenyekiti –

Veronica Sophu

Katibu - Stephen Ruvuga-

(Mkurugenzi Mtendaji)

Mweka Hazina – Esther Mallya

WAJUMBE

Joseph Kilowoko

Prisca John

Amina Kazibure

Projestus Ishekanyoro

Haji Ussi Haji

Paul Joseph

MSHAURI WA MVIWATA

Prof. Amon Mattee

LINATOLEWA NA

KUSAMBAZWA NA

Mtandao wa Vikundi vya

Wakulima Tanzania (MVIWATA)

S.L.P 3220 Morogoro, Tanzania

Simu: 023 261 41 84

Faksi: 023 261 41 84

Barua pepe: info@mviwata.org,

mviwata@morogoro.net

Tovuti: www.mviwata.org

MICHORO

Godwin Chipenya

USANIFU NA

UCHAPISHAJI

PENplus Ltd – 022 2182059

Toleo NO. 040 Oktoba – Disemba 2011 Bei Shs. 500/= ISSN 0856-5937

Je wakulima wadogo wamefaidi

matunda ya uhuru

Picha ya Jalada:

Mkazi wa kijiji cha Msowero wilayani

Kilosa mkoani Morogoro akiwa na

uso wenye tafakari nzito, Je, baada

ya miaka 50 amefaidi matunda ya

uhuru? b

Uk. 1

Uk. 17

Bodi mpya ya MVIWATA

yachaguliwa

Uk. 20

Wakulima, matrekta waandamana

kupinga uporwaji ardhi

Tahariri

Serikali iwasaidie wakulima

kujikwamua na umasikini

Moja ya kauli iliyotolewa

na mkulima aliyechangia

mawazo kwenye toleo hili

ni ile isemayo “Kuna maana gani ya

kusheherekea uhuru ili hali umasikini

kama adui namba moja wa uhuru

huo ametamalaki na kushamiri ndani

ya familia za watanzania?”

Kila msomaji wetu ana uhuru wa

kuipa tafsiri na uzito tofauti kauli hii

kadri ya mtizamo wake.

Kwetu sisi kauli hii inaibua

tafakari na msukumo wa kutafuta

kuona kuna mafanikio gani ya msingi

katika kupambana na umasikini

nchini tokea tupate uhuru ambayo

yanaweza kutufariji na kusheherekea

miaka 50 ya uhuru?

Ripoti ya Shirika la

Maendeleo la Umoja wa Mataifa

(UNDP) iliyozinduliwa mwaka jana

jijini Dar es salaam inonyesha jinsi

umasikini ulivyozidi kushika kasi

kwa mtu mmoja mmoja na taifa

kwa ujumla. Kwa mujibu wa ripoti

hiyo, katika kila watanzania 100,

watanzania 97 wanaishi kwenye

umasikini wa kipato cha chini ya

dola 2 kwa siku huku kila watanzania

89 kati ya 100 wakiishi chini ya dola

moja kwa siku. Kwa taswira hii na

katika ulimwengu huu ambapo kila

kitu kinapatikana kwa pesa, ni wazi

kuwa wimbi la watanzania wengi

hawamudu maisha yao kwa kukosa

kipato cha kufanya hivyo.

Kwa kukosa kipato, watanzania

hasa vijijini bado wanaishi kwenye

nyumba za nyasi na tembe mpaka hivi

leo kwa kuwa hawamudu kununua

bati, saruji na vifaa vingine vya ujenzi

kutokana na kukosa kipato, pia

watanzania wengi hususani vijijini

hawamudu gharama hafifu za afya

zilizopo na hivyo kuishia kufa au

kujikita zaidi katika kupiga ramli na

imani za kishirikina.

Inasikitisha kuona kuwa ndani ya

miaka 50 bado tunaishi kwa wasiwasi

wa kukumbwa na njaa kila mwaka.

Tokea uhuru mpaka sasa, watanzania

zaidi ya asilimia 89 wanaishi kwa

mwanga wa vibatari kwa kukosa

nishati ya umeme, ingawa tuna mito,

mabwawa na maziwa kila upande

wa nchi.

Ni vigumu wakulima kufurahia

kuwa wana uhuru wakati ujinga

miongoni mwao umeota mizizi

huku kukiwa na porojo nyingi za

kisiasa za kuwapumbaza hasa wakati

wa kupiga kura. Ni wakulima hao

hao wanaoliingizia kipato taifa hili,

watoto wao wanasoma wakiwa

wamekaa kwenye vumbi chini ya

vivuli vya miti. Je, ndani ya mika 50

ya uhuru na katika mazingira haya,

wakulima wanaelimika ama idadi

ya wajinga inaongezeka miongoni

mwao?

Kuwa huru maana yake ni

kukomboka kifikra kunatokana

na misingi ya elimu ambayo taifa

limejiwekea kwa watu wake.

Elimu ya kumkomboa mtanzania

ni ile ya kumfanya mtanzania

huyu ajisimamie mwenyewe na

kuendesha maisha yake kwa

umakini na ufanisi wa hali ya juu

bila kuwepo na utofauti wowote na

binadamu wengine wanaosemekana

kupiga hatua kimaisha. Je, jamii yetu

wakulima tunayo elimu kweli au

ni ile elimu ya kuzalisha manamba

wanaopaswa kuwahudumia wageni

wanaomiminika nchini kwa kivuli

cha uwekezaji. Ni uhuru upi huo

tunaousherehekea katika hali kama

hii?

Uko wapi uhuru wa mkulima

kijijini wakati bado maelfu ya

wanawake wanajifugulia nyumbani

kwa sababu katika vijiji wanavyoishi

hakuna zahanati, vituo vya afya wala

hospitali? Hii ni huduma ya msingi

inayopaswa kupatikana kiurahisi

na kwa ubora wa hali ya juu kwa

wananchi ndani ya taifa linalojinasibu

kuwa huru kwa takribani miaka 50

sasa. Katika hali halisi ya kitanzania,

je, uhuru maana yake ni kutembea

kilometa zaidi ya 50 kufuata huduma

muhimu? Kwa ujumla serikali

inapaswa kuwekeza nguvu nyingi

katika hili.

Umasikini umeota mizizi kwa

kuwa rushwa nayo imeota mizizi.

Endelea Uk wa 3

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania

Bara; Je, Wakulima Wadogo

wamefaidi matunda ya Uhuru?

Na Susuma Susuma, Morogoro

Tanzania Bara imeadhimisha

miaka 50 ya uhuru wake

tangu mkoloni Mwingereza

alipokabidhi utawala mnamo

tarehe 9 Disemba 1961. Uhuru

huu ulipatikana baada ya juhudi

za dhati za vijana wa wakati huo

wakiongozwa na Hayati Baba wa

Taifa Mwalimu Julius Kambarage

Nyerere kupambana kwa njia

ya amani pasipo umwagaji damu

kama yalivyofanya mataifa mengine

Mafanikio

yangekuwa ni uzalishaji

kwa mashamba ya wakulima

umeongezeka kwa kiasi gani, watu

wanaolala njaa wamepungua kwa kiasi

gani, watu wanaoishi chini ya dola

moja kwa siku wamepungua kwa

kiasi gani?

ya Afrika.

Miaka 50 ya kujitawala,

tumeshuhudia awamu nne za

uongozi wa Taifa letu, huku awamu ya

kwanza ikiongozwa na Baba wa Taifa,

Mwalimu Nyerere, awamu ya pili

Mzee Ali Hassan Mwinyi, awamu ya

tatu iliongozwa na Mzee Benjamini

Mkapa na awamu hii ya nne usukani

umeshikwa na Rais Jakaya Mrisho

Kikwete. Katika awamu zote nne,

serikali imepambana na changamoto

nyingi za maendeleo, pia imetumia

fursa nyingi za maendeleo ili

kuwezesha maendeleo ya kiuchumi,

kisiasa na ustawi wa jamii. Makala

hii ambayo imejumuisha maoni na

mitizamo ya makundi mbalimbali,

itaangalia yatokanayo na jitihada za

kuendeleza kilimo na changamoto

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

zake katika awamu zote hizo

Miongoni mwa maswali ya tafakari

yaliyochochea kuandaa makala hii,

ni:- Je ndani ya miaka 50 ya uhuru,

wakulima wadogo wamefaidi

matunda ya uhuru, nini mustakabali

wao kwa miaka 50 ijayo? Na Jitihada

zilizofanywa na awamu zote nne

za serikali, zimefanikiwa kiasi gani

kutatua matatizo yanayokabili ustawi

wa jamii ya wakulima wadogo?

Je wakulima wadogo wamefaidi

matunda ya uhuru?

Baadhi ya wadau wa kilimo,

walipokuwa wakijibu swali hili, wengi

wao majibu yao yalikuwa ni HAPANA

na kusema kuna kila sababu

ya msingi ya wakulima

kuwa na maombolezo

yanayoashiria kudai

uhuru wa kweli na

kuacha kudanganyika

na uhuru wa bandia

kutokana na dosari

nyingi walizoziainisha.

Msomi wa Chuo

Kikuu cha Kilimo cha

Sokoine (SUA) kilichopo

mkoani Morogoro Dkt Damian

Gabagambi aliyebobea katika

masuala ya Uchumi Kilimo katika

mada aliyoitoa kwenye Kongamano

la miaka 50 ya Uhuru lililoandaliwa

na MVIWATA Disemba 6, 2011

mjini Morogoro alisema tunatakiwa

kujitathmini kwa kina ili kujua

tumekosea wapi na tujipange vipi ili

kukwepa kurudia makosa tuliyofanya

huko nyuma na tunayofanya sasa.

“Kwa haraka haraka wananchi

wanaweza kushawishika na kuridhika

kuwa nchi yetu imeendelea sana

tangu tupate uhuru. Ukweli ambao

wananchi hawaelezwi ni kwamba,

tutoke ndani ya boksi kabisa, tuache

tabia ya kujilinganisha na wachovu

ambao hawana hata robo ya utajiri

wa maliasili za Tanzania, tujilinganishe

na walio mbele yetu kama vile

MADA MAALUM

Malaysia” alisema Dkt Gabagambi.

Alisema serikali inatumia fedha

nyingi kwenye sekta ya kilimo bila

mafanikio ya maana, zaidi ya yale

yanayoripotiwa kwenye makaratasi;

tena kwa kiwango cha raslimali

fedha zilizoingizwa kwenye sekta

na wala sio mabadiliko chanya kwa

mkulima.

Alisema mafanikio yanayotajwa

na serikali siyo mafanikio halisi bali

ni maandalizi ya kwenda kwenye

mafanikio. Mafanikio yangekuwa ni

uzalishaji kwa mashamba ya wakulima

umeongezeka kwa kiasi gani, watu

wanaolala njaa wamepungua kwa

kiasi gani, watu wanaoishi chini ya

dola moja kwa siku wamepungua

kwa kiasi gani?

“Kwa ufupi, kinachofanyika nchi

hii katika kuhudumia kilimo ni kwa

miradi kufukuzana na milestones

zilizo katika maandiko ya miradi

basi,” alisema na kuitaka serikali iteue

maeneo machache na kuwekeza kwa

tija badala ya kutawanya raslimali

kwenye miradi mingi isiyoleta tija.

Aliongeza kuwa pamoja na bidii

zote hizi sekta ya kilimo bado

inakabiliwa na matatizo yale yale

ya miaka yote ambayo ni tija duni,

ukosefu wa mikopo, miundo mbinu

duni, kilimo cha kutegemea mvua,

ukosefu wa masoko, usindikaji

mdogo, teknolojia duni, kutotumia

matokeo ya tafiti katika mipango na

huduma duni za ughani.

Mtaalamu huyu anaitaka serikali

iache kujilinganisha na nchi masikini

zenye raslimali chache kuliko Tanzania.

“Tulenge kupata mafanikio makubwa

bila kujali jirani zetu wamefanikiwa

kiasi gani. Kulenga mbali kuna maana

kubwa sana katika saikolojia ya

matumizi ya raslimali za mtu au nchi.

Nchi ikijiwekea malengo makubwa

italazimika kuwa mwangalifu sana

katika kila senti inayopatikana, na

haitakuwa na mchezo kwa yeyote

Endelea Uk wa 2

1
MADA MAALUM

Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara...

Inatoka uk. wa 1

anayekwamisha mipango kwa

kusimamia vibaya rasilimali za nchi.

Kinyume chake, nchi isipokuwa

na malengo ya juu sana inaweza

kujikuta ikiwa na matumizi ya anasa

kama tunavyoshuhudia hapa nchini.”

Anasema katika miaka hamsini

ijayo Tanzania inatakiwa ilenge mbali.

Ikilenga kuwa kama Afrika Kusini

inaweza kuishia kuwa kama Kenya.

Lakini ikilenga kuwa kama Marekani,

inaweza kuishia kuwa kama Malaysia

au Singapore, ambapo tayari

yatakuwa ni mafanikio makubwa.

Akamalizia ameshauri kwamba ni

vyema itumike kauli mbiu mpya

yenye ujumbe usemao “Miaka

50: Tumethubutu, Tumeshindwa,

Tujipange Upya”.

Mwalimu Nyerere aliposhika

madaraka alibainisha maradhi, ujinga

na umasikini kama matatizo ya msingi

ya nchi yaliyopaswa kushughulikiwa,

ambayo kwa mtizamo wa Bibi

Marcelina Charles Kibena

mkulima kutoka tarafa ya Mgeta

wilayani Mvomero, anahoji “kuna

maana gani ya kusheherekea uhuru

ili hali umasikini kama adui namba

moja wa uhuru huo ametamalaki

na kushamiri ndani ya familia zetu?

Kuna mafanikio gani ya msingi katika

kupambana na umasikini katika

kipindi hiki ambacho wakulima

tunyanyaswa na kunyimwa haki za

msingi?”

Bibi Marcelina Charles Kibena

Bibi Kibena aliyekuwa akiwasilisha

mada ya uzoefu wa mkulima mdogo

kwenye Kongamano la miaka

hamsini ya maendeleo ya kilimo

lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha

Sokoine cha Kilimo (SUA), alisema

tunapoangalia uzoefu wa miaka

50 iliyopita ni lazima kulinganisha

2

maisha ya mkulima mdogo kijijini

na shughuli zake za kilimo kama

mhimili wa maisha yake na wananchi

wengine ambao wanategemea aina

nyingine ya kipato, na hasa watu

waishio mijini.

“Kwa kipindi cha miaka hamsini

ya uhuru kumekuwepo na

matamko mbalimbali

yenye nia thabiti ya

kuboresha kilimo na

wakulima wadogo

kama Siasa ni Kilimo,

Kilimo ni uti wa mgongo

wa nchi, Chakula ni uhai,

Kilimo cha kufa na kupona na sasa

Kilimo Kwanza. Pamoja na matamko

yote hayo, kwa ujumla tunaweza

kusema kuwa katika kipindi hiki

cha miaka hamsini ya uhuru kundi

hili la wazalishaji wadogo limebaki

katika hali duni ya maisha. Hali hii

imetokana na sera ambazo kwa kiasi

kikubwa hazimjali mkulima mdogo.”

Alisema katika miaka 50 hii,

wakulima wadogo wanaishi kwa

hofu kubwa ya kuporwa ardhi na

akakumbuka maneno ya hayati

baba wa Taifa mwaka 1958 ambayo

sasa yanatimia, nukuu: “Katika

nchi kama yetu ambayo

Waafrika ni maskini na

wageni ni matajiri, kuna

uwezekano mkubwa kwamba

Mwafrika akiruhusiwa

kuuza ardhi, katika miaka

themanini au miaka ijayo,

ardhi yote ya Watanganyika

itamilikiwa na matajiri

wageni, na wenyeji watakuwa

watwana. Lakini hata

kama wageni wasingekuwa

matajiri, litaibuka tabaka

la watanganyika matajiri

wajanja. Tukiiruhusu ardhi

iuzwe kama kanzu, katika

muda mchache, kutakuwa

na kundi dogo la waafrika

wakiwa na ardhi na walio

wengi watakuwa watwana.”

Uwezeshaji na Uzalishaji

Akizungumzia kiwango cha uzalishaji,

Bibi Kibena alisema, wakulima

wamekuwa wakitumia kwa kiasi

kikubwa mbegu za asili na ndizo

ambazo zimewezesha kulisha taifa

kwa kipindi chote cha miaka hamsini

ya uhuru. Hata hivyo akasema

wameibuka watu wachache wa

kuzibeza wakishinikiza kuleta mbegu

za viini tete (GMOs) ili kutupotezea

“Sisi

tunaona kuwa hali

hii itamfanya mkulima mdogo

kuwa mtumwa wa mbegu na

kumzidishia umaskini.”

mbegu zetu za asili na wao kumiliki

soko lote la mbegu. “Sisi tunaona

kuwa hali hii itamfanya mkulima

mdogo kuwa mtumwa wa mbegu na

kumzidishia umaskini.”

Mkulima huyo, anashangazwa

na kitendo cha serikali kushindwa

kumuwezesha mkulima mdogo kuwa

mwekezaji ambaye anawezeshwa

kwa kila hali ili azalishe na mazao

yake yanunuliwe kwa bei nzuri

ambayo itamuwezesha kurudisha

gharama zote na akapata faida

stahiki, kwani hii ingekuwa ndiyo

njia pekee ya kuboresha maisha

ya wananchi wa vijijini badala ya

kuwaachia wajitafutie kama kuku

wa kienyeji.

Alisema changamoto nyingine

inayowakabili wakulima ni ushuru

na kodi. Akasema pamoja na

serikali kuondoa kodi ndogo ndogo

zilizokuwa kero kwa wananchi,

lakini bado Halmashauri nyingi

zimezirudisha kodi hizi ambazo

hatima yake ni kumbebesha mzigo

mkulima na kuzidi kumpunja mapato

yake. “Kwenye maeneo mengi

hivi sasa kusafirisha mazao kutoka

kijiji au kata moja kwenda nyingine

inabidi kulipa ushuru kwenye mageti.

Kadri unavyosafirisha mbali ndivyo

unavyokutana na mageti mengi

ambayo inabidi kulipa ushuru. Pamoja

ya kwamba ushuru unalipwa na

msafirishaji, lakini hatimaye mkulima

atapewa bei ndogo ili kufidia ushuru

anaotozwa msafirishaji, na hivyo

mkulima kuzidi kudidimia.”

Endelea Uk wa 3

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Inatoka uk. wa 2

“Kodi hizi haziishii kwenye

mazao peke yake. Hata pale ambapo

wakulima wadogo tumejitahidi

kuanzisha vyombo vyetu vya

fedha kama SACCOS, Mamlaka ya

Mapato Tanzania (TRA) wanakuja

na kuchukua kodi kutoka katika

vyombo hivyo japokuwa SACCOS

hulipa ada kwenye mamlaka

zinazosimamia ushirika nchini. Kwa

nini vyombo vyetu hivi visipewe

msamaha wa kodi kama tunavyosikia

na kushuhudia wawekezaji wa

nje wakipewa misamaha ya kodi

kwa vipindi maalumu?” alihoji Bibi

Kibena.

Kilimo na Muundo wa

Uchumi

Mhadhiri Msaidizi katika Chuo

Kikuu cha Dar es Salaam katika

Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala

wa Umma Bw. Bashiru Ally

anasema kwa asilimia kubwa kilimo

kimechangia maendeleo makubwa

nchini.

“Mambo mengi ya maendeleo

yaliyofanyika hapa nchini ndani ya

miaka 50 ni matunda ya kilimo

kwa sababu nchi yetu ni ya kilimo

na kilimo ndio kinachochangia

maendeleo kwa asilimia kubwa

kwani kinatupatia chakula pamoja

na fedha za kigeni.”

Hata hivyo akichambua historia ya

kilimo hapa nchini Bw. Ally anasema

kuanzia miaka ya 1961-1985 dola

ilimiliki shughuli zote ikiwemo Vyama

vya Ushirika vilivyoanzishwa kwa

malengo ya kuwasaidia wakulima

ambavyo vilimilikishwa kwenye dola

na hivyo kupoteza nguvu yake na

kufanya hali ya mkulima kuendelea

kuwa duni.

Anataja kuwa jambo ambalo

halikutokea katika miaka hii 25 ya

mwanzo ni kutovamiwa kwa ardhi

ya wakulima ingawaje kilimo chetu

kiliendelea kuwa cha kawaida. “Katika

kipindi hicho serikali haikufungua

milango kwa wawekezaji wakubwa

badala yake yenyewe ilianzisha

mashamba na kuyaendesha,

lakini kutokana na kukosa ufanisi

wa kuyatunza mashamba hayo

yalipoteza thamani yake.”

Amesema katika muundo wa

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

uchumi wa sasa, msukumo mkubwa

upo katika uwekezaji, ambapo ardhi

inayomilikiwa na wakulima wadogo

serikali imeigawa kwa wawekezaji

wakubwa kitendo ambacho kimeleta

athari kubwa kwa wakulima wadogo

kutokana na mfumo wao wa

uzalishaji kuvurugwa.

Bw. Ally akazungumzia jinsi

ambavyo katika miaka ya hivi

karibuni serikali imeshindwa

kuweka muunganiko baina ya

sekta ya uzalishaji (kilimo) na

sekta ya viwanda, kwani wakulima

wanazalisha malighafi lakini viwanda

vya kumalizia kutengeneza bidhaa

za kupeleka sokoni havipo. Viwanda

vingi vilivyokuwepo awali vimefia

mikononi mwa walafi wachache,

mfano kiwanda cha magunia, ngozi

na nguo.

Anasema mwelekeo wa uzalishaji

umekuwa ni wa kuuza nje na si

ndani ya nchi kwani bidhaa nyingi

zinazopatikana katika maduka mengi

nchini si mazao yanayolimwa hapa

nchini bali yanayotoka nje kitendo

ambacho kinachangia kuua soko la

ndani na kuacha mazao ya wakulima

wadogo yakiozea shambani na

kushuka thamani.

“Hivi sasa tunajiandaa kuruhusu

wakulima wakubwa kutoka nje

kuzalisha mazao ya chakula ili

kukidhi mahitaji ya ndani na nje

ya nchi badala ya kuwawezesha

wakulima wetu kuzalisha mazao

hayo ili waweze kuwa na kilimo

endelevu, jambo ambalo linaweka

hatarini mustakabali wa wakulima

wadogo. Mfano halisi ni wa maeneo

makubwa ambayo ni vyanzo vizuri

vya uzalishaji kama vile bonde la

Rufiji na mikoa ya Rukwa na Kigoma,

huku kote ni kwamba sauti za

wakulima wadogo hazisikiki na wala

hazionekani kuwa ni za muhimu.

Suala la sauti za wakulima

kutosikika lilimgusa pia Mtendaji

Mkuu wa Mfuko wa Mwalimu

Nyerere Bw. Joseph Butiku

wakati akifungua Kongamano la

Miaka 50 ya Uhuru na Mustakabali

wa Wakulima Wadogo lililoandaliwa

na MVIWATA Disemba 6, 2011 mjini

Morogoro, alisema wakulima sauti

zao hazisikiki kwa sababu ya uoga

na ujinga walionao. Alisema ujinga ni

MADA MAALUM

kigezo kikubwa kinachowakwamisha

wasifanikiwe. Akashauri chombo cha

MVIWATA kilenge kuwapa wakulima

nguvu ili waew na vitendo vya pamoja

na si sauti ya pamoja tu. “MVIWATA

muwajengee wakulima uwezo wawe

na nguvu na vitendo vya pamoja

vitakavyowezesha kuwaita viongozi

wa Serikali ili kuongea nao na kutoa

mapendekezo yao na wakulima

msiwe waoga wala wanyonge kwani

huwezi kuwa mwoga na ukatafuta

ukweli au kutoa ushauri na kujenga

taifa linalojiamini.”

Aliwahimiza wakulima kwamba

watafanikiwa tu iwapo wataunda

umoja na mshikamano thabiti ili

kwamba wakisema jambo linasikika

na serikali inajibu haraka.

Aliwasihi wajumbe wa kongamano

hilo wanapotafakari miaka 50 ya

uhuru na mustakabali wa mkulima

warejee historia ambapo alisema

kuwa nchi ya Tanzania ni ya makundi

makuu mawili yaani wakulima na

wafugaji na kundi la wafanyakazi,

ambapo kundi la wakulima na

wafugaji linabeba idadi kubwa ya

Inatoka uk. wa Tahariri

Endelea Uk wa 4

Serikali iwasaidie

wakulima...

Kwa sababu hakuna juhudi zenye

dhamira ya kweli za kupambana

na rushwa zaidi ya maigizo

tunayoyaona sasa basi ni dhahiri

kuwa kuna juhudi hafifu mno za

kupambana na maadui wa uhuru

wa kweli ambao ni umasikini,

maradhi na ujinga.

Kwa kuwa rushwa imekua injini

ya kuchochea ujinga na maradhi

ambayo nayo yamechangia

kukuza umasikini kwa taifa hili,

basi ni ukweli ulio wazi kuwa

rushwa pia ni kihunzi cha uhuru

wa kweli na maendeleo ya kweli

kwa Tanzania.

Wakati tunasherehekea

miaka 50 ya uhuru wa Tanzania

Bara, tunaitaka serikali ionyeshe

dhamira kubwa ya kusukuma

zaidi maedeleo ya kilimo nchini ili

kwenda sambamba na matarajio ya

kujikwamua kiuchumi na kuliletea

taifa maendeleo ya kweli.

3
MADA MAALUM

Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara...

Inatoka uk. wa 3

wananchi wanaolijenga Taifa la

Tanzania. “Serikali inatoka miongoni

mwa makundi hayo mawili kwa hiyo

inabidi kupanga pamoja ili kujua

tuendako baada ya miaka hii 50 ya

uhuru.”

Bw. Butiku alienda mbali zaidi

na kushauri wakulima watumie

mamlaka waliyonayo kwa kuinyima

kura kwenye uchaguzi mkuu ujao

wa 2015 serikali ya chama tawala

kilichopo madarakani iwapo

itaendelea kutowasikiliza.

“Ninyi nyote ni wapiga kura,

madaraka na mamlaka ya nchi hii

yanatoka kwenu, iambieni CCM

chama changu mimi kwamba kama

sheria ya vijiji na mambo mengine

yanayotukera hayatekelezwi, 2015

hatuwapigii kura,… mimi sitaki kufa

katika fujo tumekulia katika amani…

kauli yangu ni kauli ya demokrasi na

si uchochezi, ” alisisitiza Bw. Butiku.

Je bado wakulima ni sehemu

ya wamiliki wa uchumi wa

taifa letu?

Akizungumza kwenye Kongamano

hilo lililoandaliwa na MVIWATA Dkt.

Azavieli Lwaitama wa Chuo Kikuu

cha Dar Es Saalam, alisema kuwa

katika kipindi cha mwaka 1961 hadi

1985 ni kweli tulithubutu, tuliweza

na kusonga mbele kwa kuwasaidia

wakulima kwa kuanzisha Azimio

la Arusha na viwanda mbalimbali

vilivyotumia malighafi za wakulima.

Lakini kuanzia mwaka 1985 hadi

2011 nchi imekuwa na juhudi kubwa

katika kuwakaba koo wakulima na

kuwapora ardhi yao.

Alisema wakulima wadogo

wametupwa kando katika kumiliki

uchumi na kuonekana kama ni

wasumbufu. “Kwa kipindi hiki

kauli mbiu inatakiwa isomeke

“tumethubutu, tumeweza

na tunasonga mbele katika

kuwakaba koo wakulima.”

Alieleza kuwa Uhuru wa nchi yoyote

unatokana na umiliki wa ardhi na

ndio maana watu wanapigana kila

siku kudai ardhi na kuongeza kuwa

kwa sasa wakulima ndio wanapaswa

kujitafakari Je, wamethubutu,

wameweza na kusonga mbele katika

4

kutetea haki zao?

Alishauri kuwa ili kuweza

kukabiliana na hali hii na kuzidi

kusonga mbele inabidi wakulima

waimarishe umoja wao, wapate

elimu ya kujitegemea na sera za ardhi

zifundishwe kuanzia mashuleni.

Kwa upande wake Kanali

(Mst) Anatory Tarimo, Mkuu

wa mkoa mstaafu aliwaambia

washiriki wa Kongamano hilo

kuwa Katiba ya nchi haifuatwi

ndiyo maana hawafaidi matunda ya

uhuru na ni jukumu la wakulima

kuhakikisha inafuatwa na hatua hizo

zinaweza kuwa hata za kisheria.

Aliwashauri wakulima kujiendeleza,

kuwa wabunifu na kujenga uwezo

wa kujiamini huku akisisitiza kuwa

jukumu la kumuendeleza mkulima

mdogo ni la mkulima mwenyewe

na wasitegemee watu kutoka nje au

viongozi waliopo madarakani.

Alisema wakulima wanapaswa

kujipanga katika vikundi na mitandao,

kuwa wabunifu, wazifahamu sheria za

ardhi na wawe na mfumo imara wa

masoko utakaowezesha kumuuzia

mlaji wa mwisho na kuwaondoa

madalali ambao ndio wamekuwa

wakifaidi jasho la wakulima.

Bibi Veronica Sophu ni

Makamu Mwenyekiti wa MVIWATA

taifa na mkulima mdogo kutoka kijiji

cha Madibila wilaya ya Mbarali yeye

anasema pamoja na kubaki masikini

na kutotambuliwa na serikali katika

kipindi cha miaka hii 50 ya uhuru

wakulima wameendelea kulisha nchi

yetu.

Katika mawasilisho yake kwenye

kongamano hilo Bibi Sophu alisema

anasikitishwa na jinsi ambavyo

wakulima hawathaminiwi na

wanadharauliwa wakati wao ndio

wanalisha taifa. Alisema wakulima

hivi sasa wananyanyasika wanaishi

kwa hofu katika nchi yao kama

wakimbizi kutokana na vitendo

wanavyofanyiwa na serikali.

Bw.Thomas Laizer ambaye

ni Afisa Ushawishi na Utetezi wa

MVIWATA yeye anasema kutokana

na historia ya nchi yetu wakulima

wamenufaika kwa uchache sana na

matunda ya uhuru.

Anasema kufa kwa viwanda

vilivyojengwa katika awamu ya

kwanza ya utawala, kumepoteza

fursa nzuri ya masoko kwa mazao

ya wakulima. Jambo jingine anasema

ni kushuka kwa suala la elimu na

huduma muhimu za kijamii. “Kila

mahali wananchi wanashuhudia hilo

na ni vigumu kwa mkulima mdogo

kuakisi faida za uhuru huo katika

maisha yake ya kawaida.”

Bw. Ladslaus Bigambo,

Mratibu wa MVIWATA Ruvuma

anasema “kuna ukweli usiopingika

sasa kuwa Tanzania imepoteza

mwelekeo wa karama ya uongozi

wenye utashi wa kisiasa unaoweza

kuwaelekeza watu kwenye

mafanikio.

Kwa upande mwingine watanzania

wengi hawaoni uchungu wa dhuluma

wanayofanyiwa katika nchi yao,

hawapo tayari kuuliza ama kufuatilia

jambo lolote, hata kama lina athiri

maisha yao. Mfano wakazi Loborsoit

na Ngage wilaya ya Simanjiro mkoani

Manyara wamezungukwa na mbuga

ya wanyama inayotumiwa kwa

uwindaji wa kitalii, lakini wakazi wa

vijiji hivyo hawafuatilii kudai mapato

ambayo yangestahili kurejeshwa

kwao ili wao kama walinzi wa

wanyama hao wafaidi matunda.”

Bibi. Mary Nsemwa, mkuu

wa Idara ya Ushawishi na Ujenzi wa

Nguvu za Pamoja katika Mtandao

wa Jinsia Tanzania (TGNP), anasema

asilimia kubwa ya wananchi

wanaojishughulisha na kilimo hiki

ni wanawake ambao hawashirikishi

katika maamuzi ngazi ya kaya

hususani kiasi gani kizalishwe, kiasi

gani kiuzwe, na kwa bei gani na kiasi

gani kinaitosha familia kwa chakula,

vitendo ambavyo vinamfanya

mwanamke huyu kukosa thamani

katika jamii.

Katika miaka hii 50 baada ya uhuru

wanawake wakulima hawawezi

kujivunia kuwa wamenufaika na

lolote kutokana na kasoro mbalimbali

zinazojitokeza katika utaratibu wa

uongozi uliopo kwani hawashiriki

katika kutunga sera na sheria za

nchi, kushiriki katika vyombo vya

maamuzi na kupewa uhuru wa kutoa

maoni na mapendekezo yao katika

Endelea Uk wa 5

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Inatoka uk. wa 4

kupanga mikakati ya maendeleo

itakayowasaidia.

Ametaja mambo kadhaa ya

kufanyiwa marekebisho kuwa ni

pamoja na kuongeza ushiriki wa

wanawake katika vikao vya maamuzi

“wanaume waliobadilika na kuelewa

vyema suala hili la usawa huwasaidia

wanawake katika kutekeleza

majukumu yao.”

Akizungumzia suala la Bajaji

kutumika kusafirisha wajawazito

katika kipindi hiki huku kukiwa

hakuna miundombinu ni kuwafanyia

dhihaka kundi hili la wanawake.

Bw. Marcossy Albanie wa

Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki

za Binadamu na pia mchambuzi

wa masuala ya kisiasa na uchumi

yeye alianza kwa kushangazwa na

kitendo cha mkulima kuwekewa

masharti lakini biashara na viwanda

vimeendelea kuwa huru vitendo

ambavyo vimezuia wakulima wadogo

kuwa washindani katika soko huria.

Kwa sasa wakulima wanawekewa

vizingiti kuhusu nini cha kuzalisha, na

wauze wapi na cha kushangaza zaidi

ni kwamba wakuu wa wilaya wana

sauti ya kuwaamrisha wakulima

kuzalisha kwa kiwango fulani lakini

hawasemi kiwanda gani kiwekwe

hapo kitumie mazao yanayozalishwa

kitendo ambacho kinampa hasara

mkulima. Kwa ujumla wakulima ni

kundi lililoachwa nyuma na hata

akizungumza watu wanampuuzia.

Anasema ili wakulima wafaidi

matunda ya uhuru wanahitaji uhuru

wa pili ambao utamkomboa mkulima

na changamoto hizi zinazomkabili

na haya yote yanawezekana endapo

tutabadilisha mfumo wa uongozi

uliopo hapa nchini ambao utatoa

fursa sawa, utalenga huduma sawa

na kutambua kwamba kuishi vijijini

ni changamoto kubwa.

Anasema “Mkulima anapaswa

kupewa kiinua mgongo kama

mfanyakazi wa kawaida kwani hata

yeye anachangia katika maendeleo

ya taifa na mfumo huu uliopo ni

kandamizi, ni sawa na wizi wa nguvu

za wakulima.”

Nini kifanyike kumrejesha

mkulima mdogo katikati ya

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

mfumo wa uzalisaji

Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Morogoro

Bw. Stephen Mashishanga,

yeye alipendekeza kilimo cha

mkataba kipigwe marufuku nchini

kwa kuwa ni utumwa mpya na

ukoloni mambo leo unaotunyemelea

watanzania.

Akapendekeza pia kila mwananchi

amilikishwe ardhi kisheria, kuongeza

uzalishaji katika kila maeneo na

kuimarisha soko la ndani na nje

ya nchi, kuimarisha huduma za

ugani vijijini na wakulima washiriki

kikamilifu katika kuandaa katiba

mpya na MVIWATA iendelee kuwa

mtetezi wa kweli wa mkulima

mdogo.

Mwanasiasa Mkongwe nchini

Dkt Chrisant Mzindakaya

yeye anashauri serikali kuweka

kipaumbele katika kufanya utafiti

wa kilimo na mifugo na kuzitumia

tafiti hizo na akasisitiza watumie

wataalamu walioko vyuoni ili

kuhakikisha wanafanikisha tafiti hizo

zinazochochea maendeleo.

Kwa upande wake Profesa

Dominic Kambarage wa Chuo

Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)

anasema ili sekta ya kilimo na mifugo

iendelee lazima turudishe mifumo

ya uwajibikaji na serikali iandae

mikakati ya kudhibiti magonjwa

kwa mifugo na mimea. “Kwenye

tasnia ya ugani, ugani umeharibika

inabidi serikali ijiulize tufanye nini

ili kuwe na tasnia nzuri, njia pekee

ni kuajiri wataalamu toka vyuoni

na kutumia rasilimali vizuri waende

vijijini kufanya kazi bila hivyo kilimo

kwanza hakitafanikiwa.”

Profesa Dominic Kambarage - SUA

“Sekta ya mifugo itakwenda

kama kutakuwa na programu

MADA MAALUM

zinazoonyesha sera na nini

kimefanyika pia ndani yake kuwe

na mgawanyiko wa programu

ndogondogo kwa kila tasinia ya

mifugo kama za kuku, ngombe,

maziwa, kwani hivi sasa serikali

ukiiuliza kuhusu programu za

mifugo wanasema bado ziko jikoni

zinapikwa, huu si mwenendo mzuri,”

alisema Profesa Kambarage kwenye

Kongamano la Maendeleo ya Kilimo

chuoni hapo.

Akizungumzia mwelekeo wa

Chuo Kikuu pekee cha Kilimo (SUA)

juu ya kuleta maendeleo ya kilimo

katika miaka 50 ijayo Profesa

Amon Mattee anasema ni lazima

kuangalia mitaala na mbinu za

ufundishaji ili mafunzo yashabihiane

na uhalisia wa watakachokifanya

wahitimu wamalizapo masomo ili

kuweza kutoa mchango wa haraka

na wa moja kwa moja katika

maendeleo ya sekta ya kilimo.

Pili akashauri utafiti ulenge wadau

katika ngazi mbalimbali za maamuzi

toka kwa mkulima hadi ngazi za

juu kabisa za watunga sera kwani

maendeleo ya kilimo ni matokeo ya

maamuzi katika ngazi mbalimbali.

Dkt. Gabagambi wa SUA

anashauri iwepo programu kabambe

ya kitaifa ya kupima ardhi yote ya

nchi ili kuwa na ramani ya kanda za

matumizi bora ya ardhi. Ramani hiyo

ionyeshe eneo gani litatumika kwa

kazi gani hususan katika shughuli za

binadamu kwa uhai wa nchi hii.

Kadhalika anashauri iundwe

bodi ya nafaka (National Cereal

Board) kushughulikia mazao hayo

nchini. Jukumu kuu la bodi liwe

ni kuhamasisha uzalishaji wa

mazao haya kwa lengo la kuwa na

mlipuko wa nafaka (cereal boom)

utakaosaidia taifa kujitosheleza kwa

chakula (Tanzania kuwa ghala la

nafaka la nchi za mashariki na kusini

mwa Afrika), kupata fedha ya kigeni,

na kuchochea kasi ya kukua kwa

uchumi. Na akashauri pia liundwe

baraza la ushauri la kitaifa katika

sekta ya kilimo lenye jukumu la

kufanya tafakuri ya kina juu ya nini

kifanyike, kwanini kifanyike, wapi

kifanyike, namna gani kifanyike, lini

na kwa muda gani kifanyike, na kwa

matokeo gani.

5
MADA MAALUM

6

Maoni ya wakulima

Kwa sehemu kubwa maoni

yaliyotolewa na wakulima

kuhusiana na mustakabali

wao kwenye miaka 50 ijayo

yameakisi hofu kubwa waliyonayo

ya kusukumwa kando kwa

kuporwa ardhi na changamoto ya

masoko ya mazao.

Wengi wao wameonyesha jinsi

ambavyo mifumo ya uzalishaji

inavurugwa pale wakulima

wanapoondolewa kwenye ardhi

waliyokuwa wakilima tangu enzi

za mababu zao na kugawiwa kwa

wawekezaji. Baadhi ya wakulima

wamepigwa, kujeruwiwa na hata

kufungwa gerezani pale walipoendelea

kudai haki yao. Wakati mwingine mazao

ya wakulima kung’olewa shambani,

mifugo kuuawa, kuchomwa moto

nyumba zao au mifereji ya maji hasa

maeneo ya umwagiliaji kufukiwa na

hivyo wakulima kushindwa kuendelea

na kilimo. Wakulima wafuatao

wanashuhudia haya kuhusiana na hali

halisi ya mkulima kiuchumi, kielimu,

kisiasa na hata kijamii.

Bibi.Lydia Ruliho ni mkulima

mdogo kutoka mkoani Rukwa

anasema kuwa katika miaka 50 ya

uhuru elimu vijijini bado ni kitendawili

kutokana na serikali kutotilia mkazo

katika suala la elimu kwa wananchi wa

maeneo ya pembezoni, huku akitolea

mfano wa mkoa wa Rukwa kwamba

mwaka huu wa 2011 wanafunzi

wa darasa la saba katika vijiji 14

vya mwambao wa ziwa Tanganyika

hawakufanya mitihani ya darasa la

saba kutokana na miundombinu

ya maeneo hayo kuwa mibovu

na wakati mwingine kutokuwepo

kabisa, miundombinu hiyo ni pamoja

na ukosefu wa madaraja ambao

uliwafanya wasimamizi wa mitihani

hiyo kuogopa kuvuka ziwani kwa

kutumia mitumbwi kuelekea katika

vijiji hivyo kutokana na jografia ya

maeneo hayo ilivyo.

“Tatizo hili tumeliona hapa

Rukwa kwa viijiji hivyo lakini Je hali

ikoje kwa mikoa yote ya Tanzania, na

ni vijijii vingapi vinakosa elimu nchini

kila mwaka? Hii bado ni changamoto

kubwa inayoikabili nchi yetu, hivyo

mkulima mdogo bado hajafaidika na

uhuru uliopo kwani yeye anaonekana

kama vile si Mtanzania na wala hana

haki yoyote,” anasema Bibi Ruliho

ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti

Mstaafu wa MVIWATA.

Bibi. Kesia Laiser kutoka

Monduli anasema kwamba pamoja na

wao kuwa miongoni mwa Watanzania

ambao wako huru, wakulima wadogo

bado wanakabiliwa na changamoto

zinazowakwamisha katika harakati

zao za kujikomboa na umasikini na

miongoni mwa changamoto hizo ni

suala la gharama kubwa za pembejeo

ambazo ni vigumu kwa mkulima

mdogo kuzimudu.

Bibi. Kesia Laiser

Akizungumzia suala la elimu

Bibi. Laiser amesema kuwa watoto

wa wakulima ndio wanaosoma

katika shule za kata ambazo bado

ni duni kutokana na shule hizo

kukosa walimu wa kutosha na zana

za kufundishia ikiwemo vitabu na

maabara. “Kinachotuumiza zaidi ni

kuona watoto wa viongozi na matajiri

hawasomeshwi katika shule hizi hali

ambayo inawafanya wakulima wadogo

wahisi kuwa bado wako katika utawala

wa kikoloni kwani bado hawajafaidi

matunda ya uhuru wa nchi hii”.

Bibi. Fatuma Kimolo toka

kijiji cha Gidoma, kata ya Galapo,

Babati mkoa wa Manyara anasema

Wakulima wadogo hawajapata bado

matunda ya uhuru wa nchi hii kwa

sababu linapokuja suala la uwekezaji

wakulima wadogo hatushirikishwi

na wawekezaji huongea na serikali

kuu na kisha utekelezaji unafanyika

ambapo mara nyingi wakulima

wadogo huhamishwa bila ya kuwa na

uhakika wa mahali wanapopelekwa.

Kutoka Arusha Bibi. Ruth

Paul anaeleza kwamba katika

miaka 50 ya uhuru wakulima na

wafugaji wanazidi kunyanyasika

badala ya kusaidiwa, mifugo yao

haina dhamana na hakuna masoko

yanayoeleweka ya kuuzia mifugo

hiyo jambo linalozidi kuzorotesha

hali zao kiuchumi.

Ameeleza kwamba ili wakulima

wafaidi matunda ya uhuru ni

lazima katiba ya nchi iwatambue

na kuwalinda wakulima wadogo na

maslahi yao ndipo hata wawekezaji

watawaheshimu wakulima na wafugaji

wadogo tofauti na sasa ambapo

wanawaona kama vile manamba.

Ameongeza kuwa wazawa

wanaoishi jirani na hifadhi za taifa

za wanyama hawafaidiki na raslimali

hizo licha ya kuwalinda wanyama hao

ambao huliingizia pato kubwa taifa.

Bibi. Anna Mesoloi ni mfugaji

kutoka Monduli na anaeleza kwamba

wakulima wadogo hawajafaidi kitu

chochote zaidi ya kusikiliza kauli

mbiu mbalimbali zinazotangazwa

kila siku kwenye vyombo vya habari

ikiwemo hii ya Kilimo kwanza

ambayo hawaielewi na hawafahamu

inafanya nini licha ya kwamba wao

ndio walengwa wakuu wa kauli hiyo.

Amesema haya ni matokeo ya

mfumo wa uongozi uliopo kuanzia

ngazi za chini hadi za juu ambao siyo

shirikishi. Kwa kipindi hiki anasema

anachojivunia yeye ni kubahatika

kuwa mwanachama wa MVIWATA

ambayo imemwezesha kupata elimu

na mwanga wa kudai haki.

Amesema hali ya upatikanaji

wa mikopo ya elimu ya juu kwa

mtoto wa mkulima ni tatizo kwani

wengi wao huwa hawalewi nini cha

kufanya ili waweze kupata nafasi

hiyo ambayo kwao ni nafasi kubwa

na ya kipekee ya kujiendeleza

kielimu lakini cha kusikitisha ni

kwamba wakati mwingine fomu

zao huwa hazihangaikiwi kitendo

kinachowafanya wazidi kurudi nyyma

kielimu na kuachwa kimaendeleo.

Bibi. Mwanaidi Ally kutoka

Endelea Uk wa 7

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Inatoka uk. wa 6

wilaya ya Uyui mkoani Tabora

aneleza kwamba katika kipindi hiki

wakulima wadogo bado wana uhuru

bandia unaowanufaisha wachache

ambao hufaidi jasho la wakulima

na kuwaacha wenyewe bila kitu.

Amefafanua kwamba umasikini

unaowakabili wakulima wengi ndiyo

chanzo cha watoto wao kupata

elimu duni na kukuza kundi la

wajinga miongoni mwao.

Bibi. Hidaya Chikawe kutoka

Lindi anasema wakulima katika

miaka hamsini iliyopita wamepata

maendeleo kidogo ingawaje bado

wanakabiliwa na changamoto

mbalimbali katika shughuli yao

ya kilimo. Changamoto kubwa

inayowakabili wakulima ni ukiritimba

wa baadhi ya viongozi katika vyama

vya ushirika hasa vya zao la korosho

huko kwao ambao hukwamisha

maendeleo ya wakulima kwa sababu

wao pia hufanya kazi zao kama

madalali na hivyo kunufaika na jasho

la wakulima badala ya kuwasaidia

kuuza mazao yao kwa bei nzuri ili

waweze kupata faida.

Bw. Ponsian Ngaiza kutoka

Kagera anasema katika kipindi

cha miaka 50 ya Uhuru maisha ya

wakulima wengi yamezidi kuwa duni

kutokana na hali halisi ya uchumi

ilivyo hivi sasa ambapo bidhaa nyingi

zinapanda bei siku hadi siku huku

uchumi wa wakulima wengi ukizidi

kudorora kutokana na wao kukosa

masoko ya uhakika ya mazao yao

huku akitolea mfano wa bei ya kilo

ya kahawa katika mkoa wa Kagera

kuwa shilingi 1300 ukilinganisha na

kilo moja ya sukari shilingi 2000.

“Katika miaka hii 50 wananchi

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

wengi wa vijijini hawakupata fursa

ya elimu kuhusu masuala mbalimbali

yanayogusa maisha yao kila siku

kama vile siasa, uchumi na hata haki

zao, nashauri katika awamu ijayo

mambo haya yapewe kipaumbele,”

anasema Bw. Ngaiza ambaye pia ni

Mwenyekiti wa MVIWATA Kagera.

Bw. Paulo Mossama

kutoka Tarime mkoani Mara

anasema anachoweza kujivunia ni

kwamba katika miaka 50 wakulima

wamenufaika kwa kujifunza mambo

mbalimbali kama vile kilimo cha

kisasa lakini ni kwa asilimia ndogo

sana ukilinganisha na idadi ya

wakulima waliopo hapa nchini.

Bw. Paul Mossama

Bw. Andrew Chalangwa

kutoka Kasulu, Kigoma anasema

kuwa mkulima amenufaika kidogo

sana kwani bado anatumia nyenzo

duni ya jembe la mkono ilihali katika

nchi nyingine wakulima wanatumia

mitambo ya kisasa ya kilimo.

Changamoto nyingine inayowakabili

ni mabadiliko ya hali ya hewa

ambayo katika miaka 50 ijayo serikali

inapaswa kuweka mikakati madhubuti

kukabiliana na mabadiliko hayo.

Bibi. Deodata Katunga

toka Ruvuma anasema “mkulima

mdogo yuko katikati bado kwani

MADA MAALUM

hajapata faida ya kuridhisha ingawaje

amefunguka macho tatizo kubwa ni

watendaji na viongozi wa serikali

wanaoshindwa kutimiza wajibu wao

na kutaka kujinufaisha kwa jasho la

wakulima.

Bw. Hamad Abdalah

Salimini toka Zanzibar anasema

mkulima mdogo katika kipindi

cha miaka 50 kwa kiasi amefaidika

kwani kwa sasa ana sauti ya kusema

matatizo yake kupitia vyombo kama

MVIWATA, ingawa bado anakabiliwa

na changamoto nyingi kama vile

kutokushirikishwa katika vyombo

vya maamuzi.

Miongoni mwa maswali

tuliyokuwa tukijadili kwenye makala

hii ni Je ndani ya miaka 50 ya uhuru,

wakulima wadogo wamefaidi

matunda ya uhuru?

Kimsingi kusema kwamba

hakuna kilichofanyika katika miaka

50 ya uhuru si sawa, kwa sababu

yapo mengi ya maana yaliyofanyika.

Itoshe tu kusema kwamba kwa

yale tuliyopiga hatua tunashukuru

tumefanikiwa kufika hapo. Lakini

ziko changamoto kadhaa ambazo

wadau wameziainisha ambazo

zinadhihirisha ukweli kwamba

hawajafaidi matunda.

Kwa bahati mbaya sana

tunapoadhimisha miaka 50 baada

ya uhuru, taifa letu linashuhudia

matumizi ya ujuzi na utaalamu wa

baadhi ya viongozi na watendaji

wenye tamaa, ulafi na ubinafsi

vikitumika kuzidisha umaskini

miongoni mwa jamii kubwa ya

watanzania ambao ni wakulima.

Katika awamu ya kwanza,

Mwalimu Nyerere hakuishia

Endelea Uk wa 8

Hawa ndiyo watoto wa wakulima ambao kwa miaka 50 ya uhuru bado wanasoma kwenye mazingira duni na ya dhiki kama ambavyo wengi

wao wanaonekana hawana viatu, hivyo kuhatarisha afya zao

7
MAKALA

MAAZIMIO YA KONGAMANO

Miaka 50 ya Uhuru: Nini Mstakabali

Utangulizi

Ili kuwawezesha wakulima

kutafakari kwa pamoja mabadiliko

katika shughuli za kilimo kwa

kipindi cha miaka 50 tangu uhuru,

MVIWATA iliandaa Kongamano

lililowakusanya pamoja wajumbe

zaidi ya 170 wakiwemo wakulima

wadogo kutoka mikoa mbalimbali

ya Tanzania, viongozi wa serikali na

wakuu wa mikoa wastaafu, wataalam,

wachambuzi wa sera na wanahabari.

Kongamano hilo lilifanyika

Disemba 6, 2011 mjini Morogoro,

likiwa na ujumbe usemao “Miaka

50 ya Uhuru: Nini mstakabali wa

wakulima wadogo?”

Malengo ya Kongamano

Malengo yalikuwa yafuatayo:

· Kutafakari mabadiliko katika

kipindi cha miaka 50 tangu

Uhuru na Mustakabali wa

mzalishaji mdogo.

· Kuishauri serikali yetu njia

ya kuendelea kiuchumi bila

kuwasukuma kando wazalishaji

wadogo.

Akizungumza kwenye kongamano

hilo Mkurugenzi Mtendaji wa

MVIWATA Bw. Stephen Ruvuga,

alisisitiza kuwa tunapoangalia

mstakabali wa wakulima wadogo

baada ya miaka 50 tusiangalie mbegu,

pembejeo na soko la mazao ya kilimo

tu , bali tuzungumzie mstakabali wa

taifa ikiwemo upatikanaji wa elimu,

huduma za afya, haki ya mkulima,

umiliki wa ardhi pamoja na suala

zima la ulinzi wa mkulima.

Bw. Ruvuga alisema shuhuda

zilizotolewa na washiriki wa kongamano

zinadhihirisha kuwa mfumo wa serikali

unaotumika hivi sasa kuhudumia jamii

kiuchumi umefeli.

Alisema “ni ajabu sana kuona

kuwa ndio aina ya mfumo

tunaoukimbilia, kuushangilia na

kuupigia vigelegele, kwa mfano

tunashangilia na kutunga nyimbo

kuhusu Kilimo Kwanza, wakati ni

mfumo ulioletwa kutubomoa sisi

wakulima, tunashangilia kwa kutojua

na ndiyo maana naunga mkono kauli

ya Mzee Butiku kwamba ujinga ni

8

wa wakulima wadogo?

adui yetu nambari moja.”

Alisema ni wajibu wa wakulima

kutumia fursa ya kusanyiko kama

hilo kujifunza, kutafakari na kuchukua

hatua na kuongeza kuwa MVIWATA

isingependa kuendelea kusikia

wakulima wakisubiri ama kutegemea

zaidi nguvu za nje kuliko kuthamini

nguvu na uwezo walio nao wenyewe

kwanza katika kupigania haki zao.

Alisema kuwepo kwa watu

mashuhuri kama mgeni rasmi Bw.

Maoni ya wakulima...

Inatoka uk. wa 7

kukemea mataifa makubwa pekee

yaliyotunyonya, bali alikemea pia

viongozi wa ndani ya Tanganyika

ambao nia zao binafsi zilikuwa

zinakinzana na maendeleo ya nchi

yetu. Mwalimu hakusita kuanika

udhaifu, uchafu na tamaa za viongozi

wasio waadilifu na akasisitiza kuwa

watu hawa wasipewe uongozi.

Mwalimu alipata kusema kwamba

wasomi wachache waliobahatika

kupata fursa hiyo kwa kutumia kodi

za wananchi ni lazima wajue wana

wajibu wa kwenda kuwatumikia

wananchi kwa moyo.

Mwalimu Nyerere pia alikuwa

mtu wa mfano, alikuwa na shamba

lake kule Butiama, shamba la

Mwalimu lilikuwa mfano kwa

wanakijiji wenzake, ukubwa wa

shamba hili la mwalimu haukuwa

nusu ya ardhi ya kijiji, bali alichukua

sehemu kidogo ili kila mwanakijiji

mwenye nia ya kufanya kilimo naye

apate ardhi.

Hapa utaona fahari ya Mwalimu

Nyerere haikuwa kujilimbikizia

mali, ndio maana uwepo wa

Tanzania ulimhitaji sana Baba wa

Taifa Mwalimu Nyerere.

Kila tunapotazama tulipotoka,

hasa baada ya miaka 50 ya uhuru wa

Tanzania Bara, vema tukijua kuwa

mambo yaliyofanywa na waasisi

wa Taifa letu ni mfano hai wa hiki

kinachotokea. Serikali imeshindwa

kusimamia sheria zake ili wajanja

wachache wasitumie maarifa

Joseph Butiku kwenye kongamano

hilo ni kudhihirisha ni jinsi gani

wanawathamini na kuwaunga

mkono wakulima wadogo na hivyo

kuwataka wakulima kujiona kuwa

hawako pekee bali kuna wasomi na

viongozi wa kuwaunga mkono.

Maazimio ya Kongamano

Baada ya mawasilisho na majadiliano

ya kina washiriki kwa kauli moja

Endelea Uk wa 19

waliyoyapata kuihujumu serikali.

Wataalamu hawa waliofaidi matunda

ya uhuru kwa kusomeshwa, hivi sasa

wanatumika kukandamiza uhuru wa

watanzania wenzao.

Swali linabakia, je baadhi ya

viongozi tulionao ambao fahari

yao ni kujilimbikizia ardhi na

mali wanazowapora wakulima,

wanawatumikia wananchi kwa

moyo?

Bw. Lohay Langay, mkulima

wa Babati mkoani Manyara

anasema “tunaadhimisha miaka

hamsini ya uhuru wa Tanganyika,

tukiwa na matatizo makubwa ya

kiuchumi. Nchi ikiwa haina umeme

wa uhakika, gharama za maisha

zikipanda kila uchao, huku viongozi

tulionao wakiwa wamefumba

macho na masikio, kwa ufupi

wananchi wametelekezwa.”

“Tabia hii ya viongozi wetu

kuishi maisha ya kifahari, bila kujali

kuwa kuna watoto wa wapiga

kura wao hawana madawati,

wazazi wao wanaishi kwa mlo

moja tu, wakulima hawana soko la

mazao yao, wafugaji na wakulima

wanauana kwa kugombea ardhi

ya malisho inasikitisha mno. Binfsi

niseme huku ambako viongozi

wetu wanataka kutupeleka siko

tulikokusudia kwenda, na hii

itakuwa ni hatari tupu tunaifumbia

macho, lakini naamini itatugharimu

sana,” anaonya Bw Langay.

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

MAKALA

Wanawake wasifanywe wahanga

wa kila tatizo kwenye jamii

Na Gratian Cronery, MUCCoBS

Shinyanga

Asilimia 80 ya watanzania

waishio vijijini, maisha yao

hutegemea shughuli za

kilimo, ufugaji, uvuvi na uwindaji.

Shughuli hizo hufanywa kwa lengo

la kupata pato la kujikimu kwenye

kaya na kwa sehemu kidogo sana

hutumika kwa biashara.

Idadi kubwa ya kundi linalotekeleza

shughuli hizo katika maeneo mengi

ni la wanawake, ingawa mpaka sasa

kundi hili halinufaiki na matokeo ya

shughuli hizo.

Hali hii ya kazi nyingi kuachwa

mikononi mwa wanawake na

manufaa yake kusimamiwa na

wanaume, inatokana na mifumo

iliyopo ambayo imejengwa miaka

ya hivi karibuni licha ya kuwa kuna

watu wanaodai kuwa chimbuko lake

ni mila na desturi zilizorithiwa enzi

za mababu.

Hata hivyo, wanaojenga hoja

kuwa utumikishwaji wa wanawake

vijijini umerithiwa enzi za mababu

wanashindwa kubainisha kuwa enzi

hizo wanawake walifanya kazi zote

za nyumbani na mashambani lakini

wanaume nao walitimiza wajibu

wa kulinda na kutunza familia kwa

mahitaji yote tofauti na ilivyo sasa.

Historia inatuelekeza kuwa babu

zetu walikwenda porini kuwinda na

kuwaletea bibi zetu vitoweo vya

wanyamapori, lakini pia walihakikisha

maghala yanahifadhi chakula cha

kutosha na hifadhi hiyo inalindwa na

kutumika kwa nidhamu.

Bibi zetu majukumu yao yaliishia

kwenye kuchota maji, kukusanya kuni

(ambazo zilikuwa karibu) na kupika

tu huku mahitaji mengine kama ya

unga, mboga yakiwa yametekelezwa

na wazee.

Lakini leo ni wanaume wangapi

wanaoshinda vilabuni na baadaye

kurejea nyumbani kudai chakula

na wanapokikosa wanawadhalilisha

wanawake kwa matusi na vipigo?

Ni wanaume wangapi wanaoshiriki

kuwabaka watoto wa kike wengine

wakiwa ni mabinti zao wa kuwazaa?

Babu zetu hao ambao leo

tunawasingizia kuwa walituachia

mfumo kandamizi kwa wanawake,

hawakuruhusu bibi zetu

wadhalilishwe kwa vitendo vya

ubakaji kama inavyotokea kwenye

jamii yetu leo na yeyote aliyepatikana

na kosa hilo aliadhibiwa vikali.

Tunapoliangalia kundi hili la

wanawake hivi sasa, jambo la

kusikitisha ni kuona lilivyoachwa

nyuma kimaendeleo na kwamba

katika baadhi ya maeneo hata

mchango wao wanaoutoa katika

kuleta maendeleo, jamii haiutambui

kutokana na mifumo mibovu iliyopo

hasa ya kutothamini kazi zao.

Mwanamke anachukuliwa kuwa

ni mtu dhaifu wa kufikiri asiyeweza

kutoa mchango makini hata wa

mawazo katika shughuli yoyote

ile ya maendeleo na kwamba yeye

kazi yake ni kutekeleza tu masuala

yaliyojadiliwa na kuamuliwa.

Hali hiyo ya wanawake kupuuzwa

iko kwenye kila sekta ikiwemo hii ya

kilimo ambapo mwanamke hapewi

fursa ya kutoa ushauri nini kilimwe,

lini na kwa kiasi gani na hata mapato

ya familia yanayotokana na kilimo

matumizi yake yanaamuliwa na

wanaume.

Kutokana na kuwepo kwa

ukandamizwaji huu mwanamke

amejikuta akiwa ni mhanga kwenye

familia na jamii inayoishi kijijini.

Tunapoangalia matatizo kama

ya njaa kwenye familia, anayeteseka

zaidi ni mwanamke ambaye ni mlezi

mkuu wa watoto. Matatizo mengine

yanayoikabili jamii kama vile ukosefu

wa huduma bora za afya, maji, nishati,

elimu na miundombinu hususan

ya barabara mwathirika mkuu ni

mwanamke.

Licha ya serikali kutangaza

kuwa imeboresha huduma za afya

vijijini, lakini bado tunasikia na

kushuhudia matukio ya wajawazito

wakisafirishwa kwenye mikokoteni

ya ng’ombe na baiskeli na serikali

nayo kwa kuwapuuza ikawaletea

usafiri wa bajaji.

Suala la uhaba wa pembejeo za

kilimo, kadhalika nalo ni mzigo kwa

wazalishaji hawa ambao ni wanawake

na wengi wao wanashindwa kumudu

gharama za nyongeza ili waweze

kupata pembejeo hizo.

Hata hivyo, kwa upande mwingine

zipo taasisi na mashirika ambayo

kwa kutambua nafasi ya mwanamke

kwenye jamii yameanza kampeni

kuielimisha jamii, juu ya umuhimu

wa makundi yote kwenye jamii

kushirikiana na kuthaminiana.

Jamii nyingi vijijini zimewaachia wanawake kazi za kulima,kuhudumia mifugo, watoto, kupika,

kuchota maji, kukusanya kuni (ambazo zinapatikana umbali mrefu), afya zao kudhoofu.

9
MAKALA

Kilimo kina nafasi ya kimkakati

ya kukuza uchumi

Na Susuma Susuma

Miaka hamsini ni kipindi

kirefu kwa hali na

mazingira yoyote yale

hasa tunapoihusisha na maendeleo

ya binadamu, jamii viumbe au

jambo lolote lile linaloendelea

kuendana na wakati.

Mwaka huu wa 2011

tunaposherehekea na kufurahia

kufikia miongo mitano tangu taifa letu

la Tanzania Bara lijipatie Uhuru wake

kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza

mwaka 1961, tuna kila sababu ya

kujipima katika nyanja tofauti hasa

zile zinazohusisha maendeleo ya

kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa

taifa letu. Yatupasa kujiuliza na

kujitathmini wapi tumetoka, wapi

tulipo na ni wapi tunaelekea.

Kwa

wastani wakulima bado

wanalima vishamba vidogo vidogo, pia

bado wakulima wetu wanatumia zana duni

za jadi kama vile jembe la mkono.

Msingi mkubwa k a t i k a

hili ni kuyaangalia mafanikio

yetu katika harakati za kujiletea

maendeleo tangu tumepata Uhuru

na kuweza kuwa na sababu nzuri ya

kujipongeza kwa hilo. Halikadhalika

ili tuzitendee haki dhamira zetu ni

vyema tukaziangalia changamoto

zilizotukwaza katika kipindi chote

hiki cha miaka hamsini ya Uhuru,

ili basi, tuweze kupangilia mikakati

ya kukabiliana na changamoto hizo

na kuzifanya kuwa ndio sehemu ya

chachu ya kutuletea mafanikio kwa

ukubwa na kiwango cha hali ya juu

zaidi kwa kipindi kijacho cha miaka

hamsini.

Kilimo ndio msingi wa uchumi

wetu na kina nafasi ya kimkakati

katika kuboresha uchumi wa

Tanzania. Sekta ya kilimo ndiyo

10

inayotegemewa na asilimia kubwa

ya Watanzania katika harakati za

kujiletea maendeleo ya kiuchumi na

kijamii na kwa maendeleo ya taifa

letu. Kwa maana hiyo kilimo ndiyo

mhimili wa maisha ya watanzania

wengi.

Lakini kilimo cha Tanzania ndani

ya miaka 50 ya uhuru bado ni duni

na wakulima wenyewe wamesongwa

na matatizo mengi. Walio wengi

hawazijui na hawazitekelezi Kanuni za

Kilimo Bora kwa mazao wanayolima,

hivyo kilimo chao hakina tija na

mavuno yao ni kidogo. Kwa wastani

wakulima bado wanalima vishamba

vidogo vidogo, pia bado wakulima

wetu wanatumia zana duni za jadi

kama vile jembe la mkono. Hapa

mwelekeo chanya ni kwamba kilimo

cha kisasa kinapaswa kuwa sharti

muhimu katika kuchangia ujenzi wa

uchumi wa kisasa.

Heshima ya mkulima/mfugaji

mdogo

Toka wakati wa uhuru

hadi miaka ya 70 na 80

mwanzoni, wakulima

wadogo walikuwa

wanaheshimiwa na kazi yao

ilikuwa inathaminiwa na makundi

mbalimbali katika jamii. Hata wasanii

wa muziki walitunga na kuimba

nyimbo mbalimbali zilizowasifu,

kuwapongeza na kuwatia moyo

wakulima wadogo ili waweze

kuendelea na kazi ya kulisha taifa na

kuongeza pato la taifa kupitia katika

kilimo.

Kwa sasa hali imebadilika

kabisa, miaka hamsini ya uhuru

tunashuhudia kilimo kinaonekana

kama mbadala wa mwisho. Mambo

yote yakikushinda unaenda kwenye

kilimo na ukimaliza muda wako wa

kutumikia taifa kwa njia ya ajira rasmi

ndipo unarudi katika kilimo ukafie

huko. Ingawa kauli mbiu ya Kilimo

ni Uti wa Mgongo bado inatumika

sana na makundi mbalimbali katika

jamii yetu, lakini uhalisia ni kwamba

kilimo kinaonekana kuwa ni mateso

au adhabu au shughuli isiyokuwa na

heshima mbele ya jamii. Ni jambo

la kawaida kusikia mtu akisema:

‘Kama mjini pamekushinda rudi kijijini

ukalime’; ‘Kama sanaa imekushinda,

nenda ukalime’; Kama huwezi siasa

nenda kalime’; sio lazima kuwa na

digrii, ukiona unashindwa, rudi kijijini

ukawasaidie wazazi kulima’.

Kejeli hizi zinachangia vijana

wetu wengi kukimbia kilimo na

kwenda mjini kwani kuwa mkulima

ni aibu mbele za watu. Hata

mkulima akivaaa vizuri, akinawiri

au akitoa maoni yake ya maana,

utasikia minong’ono inayoonesha

mashaka kama hayo ni mawazo ya

mkulima. Hapo ndipo wakulima

wadogo wanajiuliza, hivi kweli sifa

zetu ni kuwa mchafu, mchovu, mtu

asiyeweza kutoa mawazo na maoni

ya maana mbele ya jamii au asiye na

mbele wala nyuma?

Kwa ujumla unaweza kuipa

tafsiri Sekta ya Kilimo kwa semi

mbalimbali, mojawapo ikiwa ni

‘sekta iliyotelekezwa ama sekta ya

watu wanaoganga maisha.’ Hata

hivyo, upana na unyeti wa shughuli

zinazofanywa na Sekta ya kilimo ndio

kigezo dhahiri kinachoipa umuhimu

kuweza kuingizwa katika mchakato

huu wa kujitathmini na kuelezea

mafanikio yake katika mwaka huu

2011.

Watanzania tunapoadhimisha

na kusherehekea kwa shangwe na

nderemo kutimiza miaka hamsini ya

Uhuru, tunapaswa kujiuliza je, kilimo

ambacho kinaelezwa kuwa kinatoa

mchango mkubwa katika pato la

taifa, kinatoa tafsiri ama mchango

gani wa maendeleo ya mkulima

mmoja mmoja?

Ni ukweli ulio wazi kuwa

wakulima wadogo ni wachangiaji

wakubwa katika pato na maendeleo

ya taifa, ingawa wao wenyewe

hawanufaiki na pato hilo.

Kodi zinazotozwa na

kukusanywa na serikali kwa njia

mbalimbali zinalipwa na kundi

Endelea Uk wa 11

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Inatoka uk. wa 10

kubwa la wale walio katika Sekta ya

Kilimo (wakulima ama wazalishaji

wadogo). Hawa ndiyo tunaambiwa

wanachangia pato la taifa kwa kuwa

shughuli zao kuu ni kilimo. Wanalipa

kodi hizo ama kupitia shughuli

zao za uzalishaji na biashara, ama

kupitia bidhaa wanazonunua kama

vile mafuta ya taa, sukari na nguo.

Lakini hoja inayoweza kuibuka hapa

Hifadhi

ya chakula ni eneo ambalo

linapaswa kuchukuliwa kwa uzito ili

mazao yasiendelee kupungua bali Tanzania

igeuke kuwa ghala ya chakula katika kanda

huu wa Afrika Mashariki.

ni je, kodi

hizo zimetumikaje kusaidia kutatua

kero na matatizo mengi yanayogusa

maisha yao ya kila siku?

Zipo changamoto nyingi

zinazowakabili wakulima nchini

kwetu hivi sasa ambazo zingeweza

kutatuliwa kwa kodi wanazolipa na

nyingine zingetatuliwa na uwepo

wa sera zinazomwezesha mkulima

kupiga hatua za maendeleo.

Kwa mfano changamoto za

masoko na bei nzuri ya mazao ni

suala la kisera, changamoto ya mitaji

inaweza tatuliwa na sera nzuri na

changamoto ya matumizi ya zana

duni, ubaha wa pembejeo na umiliki

wa ardhi ni masuala ya kimkakati

ambayo kama juhudi za makusudi

zikichukuliwa na kutekelezwa kwa

ushirikiano thabiti kati Serikali na

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

Sekta Binafsi, shughuli ya kilimo

itawanufaisha wakulima na wao

kuona wanafaidi matunda ya uhuru

sawa na wazalishaji kwenye sekta

nyingine. Tukifanya hivi tutaifanya

nchi yetu kufikia mafanikio ya

nchi kama vile Malaysia, Indonesia,

Singapore na Vietnam ambazo katika

miaka ya mwanzo wa sitini sekta za

kilimo zilikuwa katika viwango sawa

na nchi yetu.

Jambo jingine tunalopaswa

kulitumia vyema ni

kiwango kikubwa cha

rasilimali ambazo

Mungu ameijalia

ardhi yetu ya

Tanzania iliyojaa

rutuba na hali ya

hewa inayoruhusu

mazao aina mbalimbali

kustawi, jambo la msingi ni

kuwa na utashi wa kisiasa.

Juhudi kubwa inabidi zielekezwe

kwenye Kilimo cha Kibiashara na

hapa ushirikiano wa serikali na sekta

binafsi ndio utakaofanikisha azma hii.

Mbali na kuongeza wigo katika sekta

ya kilimo, mkazo inabidi uwekwe

kwenye uongezaji thamani kwa

kutilia mkazo usindikaji wa mazao.

Hifadhi ya chakula ni eneo ambalo

linapaswa kuchukuliwa kwa uzito

ili mazao yasiendelee kupungua

bali Tanzania igeuke kuwa ghala ya

chakula katika kanda huu wa Afrika

Mashariki.

Taarifa za ushindani katika uchumi

wa soko huria na urahisi wa kufanya

biashara zinahitajika ili kuchochea

juhudi za kujikwamua kiuchumi.

Vyombo husika vinapaswa kutoa

uwanja sawa na mazingira wezeshi

Kilimo ni Uti wa Mgongo?

MAKALA

kwa wadau wote. Haipendezi

kuendelea kuwabagua wakulima

kwa kuwazuia kuuza mazao huku

nchi ikinadi sera za soko huria.

Mafanikio makubwa ya maendeleo

katika sekta zote yanategemea

sana uwekezaji katika sayansi na

teknolojia. Matumizi ya teknolojia ya

habari (ICT) yatasaidia sana harakati

za biashara ya ushindani, kwa hiyo

uwekezaji katika eneo hili upewe

kipaumbele. Teknolojia hii ya habari

hivi sasa imeonyesha mafanikio

kwenye baadhi ya maeneo, mfano

dhahiri ukiwa ni Mfumo wa Taarifa za

Masoko (MAMIS) unaotekelezwa na

MVIWATA, ambao umepongezwa

na wadau wengi kwamba umesaidia

kuimarisha biashara ya mazao.

Kero kubwa katika utendaji wa

biashara ni miundombinu mibovu

hususan barabara ambazo ni

vyema zikaboreshwa ili kurahisisha

usafirishaji wa mazao toka vijijini

ambako ndipo uzalishaji unapofanyika

hadi maeneo ya masoko ya walaji

ambao mara zote ni wakazi wa

mijini.

Tuimarishe na kuwa na mfumo

wa uhakika wa upatikanaji wa

mbegu bora na mbolea na kueneza

matumizi yake kwa wakulima wengi

zaidi.

Uwezeshwaji wa wananchi kwa

ujumla ni jukumu ambalo serikali

inapaswa kulitekeleza kwa dhati. Sera

hii imebuniwa ili kuwapa mamilioni

ya Watanzania fursa ya kujikwamua

kiuchumi. Kilimo kina nafasi ya

kimkakati ya kukuza uchumi, ikiwa

juhudi zaidi zitawekwa kwenye

kupanua uwigo wa utekelezaji wa

mipango inayowekwa.

11
KAMERA

12

KAMERA YA MVIWATA MITANDAONI

Wana-MVIWATA Zanzibar walioshiriki mkutano mkuu oktoba 2011

mjini Morogoro

Wana-MVIWATA Chunya wakiwa katika ziara ya mafunzo kwa

wakulima wenzao wa wilaya ya Mkuranga Pwani

Bw. Hasira Zahoro Mwezeshaji wa MVIWATA akizungumza na wadau

wa soko la Matai Sumbawanga Vijijini, linalojengwa na MVIWATA

Wana-MVIWATA Mara walioshiriki mkutano mkuu Oktoba 2011

Viongozi wa MVIWATA Shinyanga kutoka kulia ni Bw. Masumbuko

Bunzali (Mwenyekiti MVIWATA Bariadi), Bw. Charles Ndugulile

(Mwenyekiti Mkoa) Bibi. Justa Charles (Mjumbe kamati ya uongozi

MVIWATA Kahama), Bw. Goma Boya (Katibu MVIWATA Shinyanga

Vijijini) na Bw. Yusuph Mboje (Katibu MVIWATA Kishapu) wakiwa

wameshika majarida ya Pambazuko baada ya kuyapokea kupitia

mfumo wa malipo kabla.

Bibi Atufuage Mgimba mkulima toka kikundi cha Amani, kijiji cha

Mapogoro kata ya Milo wilayani Ludewa, akizungumza kwenye

mafunzo ya uimarishaji vikundi, yaliyofanyika Mlangali

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
KAMERA YA MVIWATA MITANDAONI

Picha ya pamoja ya wakazi wa kijiji cha Itwangi Shinyanga Vijijini, baada

ya kikao cha ufuatiliaji wa Mradi wa Chukua Hatua unaotekelezwa na

MVIWATA kwa ushirikiano na shirika la Oxfam.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku

akisisitiza jambo kwenye Kongamano la MVIWATA la Kuadhimisha

Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Disemba 6, 2011 Morogoro mjini

Picha ya pamoja ya washiriki wa Kongamano la MVIWATA la Miaka

50 ya Uhuru lililofanyika Morogoro Disemba 6, 2011

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

KAMERA

Picha ya pamoja ya wana-MVIWATA Shinyanga Vijijini na waheshimiwa

madiwani wa halsmahauri ya wilaya hiyo, baadaya kikao chenye lengo

la kuimarisha mahusiano

Washiriki wa Kongamano la miaka 50 wakimsikiliza mgeni rasmi

Mzee Joseph Butiku anayeonekana picha ya kushoto

Bw.Anno Lwilo mkulima wa kijiji cha Mangalanyene wilaya ya Ludewa

mkoa wa Njombe akichangia mada kwenye Kongamano la MVIWATA

la miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania

13
KUTOKA MITANDAONI

WARSHA YA KITAIFA

Soko la uhakika kichocheo cha uzalishaji

kwa wakulima Tanzania

Na Jacueline Massawe, Morogoro

Ukosefu wa soko la uhakika

kwa mazao ya wakulima

ni miongoni mwa

changamoto zinazomkwamisha

mkulima mdogo kunufaika na

shughuli hiyo ya kilimo na hivyo

kuendelea kuwa masikini.

Kwa kuiona changamoto hiyo,

MVIWATA ambayo ni chombo

kinachowaunganisha wakulima

wadogo iliandaa warsha ya kitaifa

iliyowakutanisha wakulima zaidi

250 kutoka mikoa yote ya Tanzania

bara na Visiwani. Warsha hiyo pia

ilihudhuriwa na viongozi wa serikali

na wataalamu kutoka taasisi za

kiserikali na zisizo za kiserikali,

wasomi na wachambuzi wa masuala

ya sera na siasa nchini.

Lengo la warsha hiyo ya siku

moja, ambayo ilibeba maudhui

yasemayo, Soko la Uhakika Kichocheo

cha Uzalishaji! lilikuwa ni kuwapa

fursa wadau wa kilimo kujadili na

kuzitafutia ufumbuzi changamoto za

masoko ya mazao ya wakulima.

Warsha hiyo ilifanyika Oktoba

14

24, 2011 katika ukumbi wa Kituo

cha Mafunzo ya Wanawake CCT cha

Mjini Morogoro ikiwa ni utangulizi

wa Mkutano Mkuu wa 16 wa shirika

la MVIWATA uliofanyika Oktoba 25,

2011.

Warsha hiyo ilifunguliwa na

Mkuu wa Mkoa Mstaafu Bw. Stephen

Mashishanga, ambaye katika hotuba

yake, alipongeza utaratibu shirikishi

unaotumiwa na MVIWATA kwa

kuwashirikisha wakulima kuibua

kero kwa kuwakutanisha na wadau

mbalimbali na kuhimiza utaratibu

huo uimarishwe kwenye ngazi zote

na siyo ngazi ya taifa tu.

Bw. Mashishanga aliwataka

wakulima kuungana kwa pamoja kwa

kupaza sauti za kukataa makandamizo

na manyanyaso wanayofanyiwa

na serikali na wahisani mbalimbali

wasio na mapenzi mema.

“Ni vizuri wakulima tukahakikisha

kuwa tunajitetea mwenyewe kwa

umoja na nguvu zote badala ya

kutegemea kutetewa na mashirika

yanayokuja kwa mgongo wa

uwekezaji kwa maslahi ya nchi zao,

ama serikali ambayo haituungu

mkono,” alisema Bw. Mashishanga

Washiriki wa warsha ya kitaifa ya MVIWATA 2011

Aidha alihimiza vyama vya

wakulima vijenge mahusiano

imara na halmashauri za wilaya

katika kutekeleza majukumu yake

na kuongeza kuwa kwa kufanya

kazi pamoja wataweza kutatua

changamoto za masoko na

nyinginezo ambazo ni kero kwa

wakulima.

Aliitaka serikali iache kuwapuuza

wakulima na badala yake isikilize

kilio chao na kuzitafutia ufumbuzi

changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wake Mwenyekiti

wa MVIWATA Taifa aliyemalizamuda

wake Bw. Yazid Makame alisema kuwa

wakulima bado wanakabiliwa na

changamoto nyingi hasa za masoko,

ambazo zinapaswa kutatuliwa ili

kuwezesha maendeleo ya haraka

kwa wakulima wadogo nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi

Mtendaji wa MVIWATA Bw. Stephen

Ruvuga alisema tatizo la vikwazo

vya kibiashara kwa wakulima

wadogo limekuwa likiwakatisha

tama na matokeo yake yamekuwa ni

uzalishaji mdogo na duni.

“Wakulima wadogo wakiwa

Endelea Uk wa 15

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Inatoka uk. wa 14

na uhakika wa soko itakuwa ni

motisha kwao klima kwa bidii na

kibishara zaidi. Wakulima wadogo

wakiuza, mapato yao yanarudi tena

mashambani kuimarisha kilimo na

kuongeza uzaishaji. Wakizalisha bila

soko wanakata tamaa ya kuzalisha,”

alisema Bw. Ruvuga.

Akitoa maoni yake juu ya mpango

huo wa uwekezaji, Bw. Ruvuga,

alitahadharisha kuwa kitendo cha

kuwabagua wakulima wadogo katika

umilikaji wa ardhi kinaweza kujenga

tabaka la chuki na kuibua migogoro

ya ardhi isiyokoma.

“Tumeshuhudia nchi nyingine

wakulima waliondolewa katika ardhi

yao kimabavu, baadaye wameungana

na kuifatuta haki yao kwa nguvu”

alisema Bw. Ruvuga.

Bw. Ruvuga alisema, nchi lazima

ihakikishe kunakuwa na usalama

wa chakula kwa tahadhari kwani

wawekezaji wanaweza kuzalisha

mazao ya chakula kwa soko la nje

na kuiacha nchi bila chakula na pia

kushindwa kununua mazao hayo

kwa kuwa mengi yanauzwa kwa bei

kubwa.

Alishauri kuwa ni vyema serikali

ikawekeza zaidi kwa wazalishaji

wadogo kwa kuwajengea uwezo ili

waendelee kulisha Taifa bila kuwa

na kikwazo chochote cha kuingiliwa

katika ardhi yao.

Michango iliyotolewa na

wakulima walioshiriki warsha hiyo,

kwa sehemu kubwa ilionyesha

mashaka makubwa juu ya mkakati

huo wa serikali wa kuwafanya

wakulima kulima kibiashara kutokana

na kero nyingi huku wakitolea

mfano wa kero wanayokumbana

nayo mipakani wanapotaka kuvusha

mazao kwenda nchi jirani na kuitaka

Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingilia

kati suala hilo.

“Tunahamasishwa kulima

kibiashara kwa sababu ya soko

huria na soko la pamoja la Afrika

Mashariki, lakini tunapofika mipakani

tunakumbana na vizuizi na kwa kweli

tunanyanyasika mno, tunadaiwa

malipo ambayo hayapo kisheria,”

alisema Bibi Fatuma Kimolo Makamu

Mwenyekiti wa MVIWATA Manyara.

Bibi. Kimolo alisema wanasikia

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

nchi hizo zimesaini Makubaliano ya

Soko la Pamoja la Kibiashara, lakini

akashangazwa na vikwazo hivyo

kuendelea kuwepo.

Mkulima mwingine Bw. Joseph

Mshangama kutoka mkoani Tanga

mbali na kutaka kuondolewa kwa

vikwazo vya kuuza mazao nje ya nchi,

alisema wakulima bado wanahitaji

kuelimishwa vya kutosha kuhusiana

makubaliano ya Soko la Pamoja ili

kuondoa mkanganyiko unaojitokeza

hivi sasa.

Bw. Joseph Mshangama

Bw. Hamad Salmin, mkulima

kutoka Zanzibar alisema

changamoto kubwa inayowakabili

wakulima visiwani humo ni suala

la usindikaji. Alisema wakulima

wengi wanazalisha mbogamboga

na matunda, lakini hawana vifaa

vya kuhifadhi na usindikaji na hivyo

wakulima kulazimika kuuza mazao

kwa bei ndogo kwa madalali.

Wakulima hao walisema licha

ya kuwawekea masharti ya kuuza

mazao yao nje ya nchi kwenye bei

nzuri, serikali hiyo hiyo imekuwa

ikishirikiana na wawekezaji kuwapora

wakulima ardhi.

Bw.Levi Mlengule kutoka wilaya

ya Mufindi alisema katika eneo lake

wawekezaji wanafaidi misitu kuliko

ilivyo kwa wenyeji. Alisema wakulima

wamenyimwa fursa ya kuvuna misitu

hiyo ambayo wao ndiyo watunzaji

wakuu.

Bw. Ahmedi Simba mkulima toka

wilaya ya Kigoma alilalamikia Serikali

wilayani humo kwa kuchukua ardhi

kubwa na kuwapa wawekezaji

na kushindwa kutoa ardhi hiyo

hiyo kwa makundi madogo ya

wakulima ambao kwa muda mrefu

wamewasilisha maombi ya ardhi

hiyo.

“Nahofia tutaishia kuwa

manamba katika mashamba

KUTOKA MITANDAONI

makubwa, tunajiuliza kwa nini

Serikali inawapendelea wawekezaji

wageni na kuwaacha wazawa?”

alihoji kwa uchungu Bw. Simba.

Afrika Mashariki watakiwa

kutekeleza soko huria kwa

vitendo

Mkurugenzi Msaidizi katikaWizara

ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

anayeshughulikia kitengo cha

Uzalishaji Dkt. Abdullah Makame,

akiwasilisha mada kwenye warsha

hiyo alisema Jumuiya ya nchi za

Afrika Mashariki inatakiwa kuchukua

hatua za makusudi za kuwasaidia

wakulima kunufaika na kilimo kwa

kuwaondolea vizuizi vya kusafirisha

mazao mpakani na vikwazo

vinginevyo kwenye soko la mazao.

Dkt. Makame ambaye mada

yake ilizungumzia Fursa na Vikwazo

katika Biashara ya Mazao ndani ya

Jumuiya ya Afrika Mashariki, alisema

vizuizi hivyo ni moja ya sababu

zinazochangia kudumaza uchumi wa

nchi hizo ambazo asilimia kubwa ya

wananchi wake wanajishughulisha

na kilimo. Jumuiya ya Afrika

Mashariki inaundwa na nchi tano za

Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na

Tanzania.

Akizungumzia maendeleo ya

sekta ya kilimo nchini, Dkt Makame

alisema tatizo kubwa linaloikabili

nchi yetu ni miundombinu mibovu

ambapo asilimia 80 ya usafirishaji

wa mizigo ikiwemo mazao ya kilimo,

inategemea barabara, ilihali katika

nchi zilizoendelea bidhaa nyingi

zinasafirishwa kwa reli, meli na

ndege na hivyo kufikisha mapema

sokoni bidhaa zikiwa na ubora na

thamani inayokidhi soko.

Alisema tatizo jingine

linalowakabili wazalishaji wadogo

nchini ni kukosa umiliki wa ardhi

jambo ambalo alisema serikali

inapaswa kulipa kipaumbele ili

kuchochea uzalishaji na maendeleo

ya kiuchumi kwa ujumla hasa wakati

huu tunapozungumzia kuwa na

shirikisho la Afrika Mashariki.

Aliitaka serikali kuangalia upya

iwapo sera zinazotungwa na zilizopo

kama zinakidhi mahitaji ya kumsaidia

mzalishaji kujiletea maendeleo

Endelea Uk wa 16

15
KUTOKA MITANDAONI

Inatoka uk. wa 15

badala ya kumkandamiza.

Akiwasilisha uzoefu wa MVIWATA

kuhusu Ubia wa vyama vya

wakulima na Halmashauri za

wilaya katika uendeshaji wa

masoko, Mratibu wa Kitengo cha

Masoko Bw. Nickson Elly MVIWATA

mpaka sasa imefanikiwa kujenga

masoko tisa ya mazao ya wakulima

vijijini.

Alisema masoko hayo yako

kwenye vijiji vya Kibaigwa

Kongwa, Nyandira Mvomero,

Tandai na Tawa Morogoro Vijijini,

Mkata Handeni,Igagala Njombe,

Igurusi Mbarali, Matai na Kasanga

Sumbawanga Vijijini.

Alisema masoko hayo

kwa kawaida huendeshwa na

kusimamiwa na bodi za masoko

ambazo mundo wake unajumuisha

uwakilishi wa wadau mbalimbali

wa soko wakiwemo wawakilishi wa

halmashauri za wilaya.

Hata hivyo katika siku za hivi

karibuni uendeshaji wa masoko

hayo umekuwa na changamoto

nyingi ikiwemo kiwango kikubwa

cha ushuru ambao halmashauri

za wilaya zinalazimisha kulipwa,

ambazo hakilingani na makusanyo

halisi ya ushuru wa sokoni kwa

mwezi. Aliongeza kuwa hali hiyo

inahatarisha uendelevu wa masoko

hayo ambayo yamechangia kwa

kiwango kikubwa ukuaji wa uchumi

wa wakulima wa maeneo husika.

Bw. Elly alisema hali hiyo ni

mojawapo ya sababu zilizoisukuma

MVIWATA kandaa warsha hiyo ili

kupata fursa ya kujadiliana na wadau

mbalimbali wanahusika kwenye

mfumo wa masoko ya mazao ya

wakulima. kiwangoambah

Umiliki wa ardhi

Akiwasilisha mada kuhusu Nafasi

ya Wazalishaji Wadogo kwenye

mchakato wa kuandikwa Katiba

Mpya, Mhadhiri Msaidizi Kitivo cha

Sayansi ya Siasa ya Jamii chuo kikuu

cha Dar es Salaam Bw. Bashiru

Ally alisema kwamba, mambo yote

yanayohusiana na ardhi ni lazima

yapewe kipaumbele kuzungumziwa

katika katiba mpya ili kuzuia uadui

unaoweza kutokea baina ya wamiliki

16

ardhi na watawala.

“Ni lazima kuangalia sheria

zetu za ardhi na kuziimarisha ili

ziweze kulinda haki za wazawa wa

Kitanzania” alisisitiza Bw. Ally

Alisema hadi mwaka 2010,

Serikali ilikwishagawa hekta

610,000 za ardhi kwa makampuni

13 ya uwekezaji ya kigeni na wengi

wamepewa na kuhodhi maeneo

hayo pasipo kuyaendeleza na

wengine wamelalamikiwa kwa

kujiingiza katika biashara ya mbao

na hivyo kuharibu mazingira badala

ya kuyatunza.

Alisema serikali imekuwa

ikitangaza kuwa, Tanzania ina hekta

milioni 44 za ardhi inayofaa ka kilimo

na kwamba kati yake ni hakta 10.8

milioni tu zinazotumika.

“Lakini baadhi ya wataalamu na

wanaharakati watetezi wa haki ya

ardhi wamesema huu ni udanganyifu

kwani ardhi ambayo haitumiki ni ile

iliyopo kwenye mbuga za wanyama,

hifadhi ya misitu na kwenye hifadhi

za asili. Wakulima na wafugaji wote

wanatumia ardhi waliyotengewa na

katika maeneo mengi haiwatoshi

ndiyo maana kunatokea migogoro

ya ardhi,” alisema msomi huyo.

Aliwashauri wakulima kushiriki

kikamilifu katika mchakato wa

uandikaji wa katiba mpya pindi

utakapoanza, ili washawishi kuingizwa

kwa vipengele muhimu vinavyotetea

umiliki wa ardhi kwa wazawa.

Alisema mataifa tajiri ambayo

sasa yanaongoza kwa kuvamia ardhi

katika bara la Afrika ni pamoja na

Korea ya Kusini, China Saudi Arabia na

Umoja wa Nchi za Kiarabu, ambapo

nchi za Afrika zilizokwishavamiwa ni

Zambia, Ethiopia, Kenya na Sudani.

“Uwekezaji huo unalenga kuzalisha

mazao ya nishati mmea pamoja

na mazao ya chakula ambacho

kinasafirishwa pasipo nchi husika

kunufaika.”

Ingawa wanaounga mkono

uwekezaji huo wanatetea kuwa

hoja kwa maelezo kuwa utasaidia

kuimarisha kilimo kwenye nchi

zinazoendelea, lakini ukweli unabaki

wazi kuwa uwekezaji huo unafanyika

kwa malengo ya faida binafsi za

kibiashara ama faida za mataifa hayo

tajiri.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji

wa wilaya ya Chunya, Bw. Maurice

Sapanjo katika maeneo aliyofanyakazi

na vikundi vya wakulima hasa vya

MVIWATA, vimekuwa msaada

mkubwa wakuchochea kazi ya

maendeleo vijijini.

Alishauri MVIWATA kujieneza

zaidi vijijini waliko wakulima wengi

ili waweze kunufaika na utetezi na

maarifa inayotolewa kupitia mtandao

huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Chunya, Bw. Maurice Sapanjo

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Bodi mpya ya MVIWATA

Na Goodness Mrema, Morogoro

Wajumbe wa Mkutano

Mkuu wa 16 wa

MVIWATA uliofanyika

Oktoba 25, 2011 mjini Morogoro

wamechagua Bodi mpya ya

wakurugenzi wa shirika hilo

watakaokaa madarakani kwa miaka

mitatu 2011-2014.

Bodi mpya iliyochaguliwa

inaongozwa na Bw. Habibu

Simbamkuti mkulima mdogo kutoka

Kikundi cha Sanje kijiji cha Msolwa

Ujamaa, tarafa ya Kidatu wilaya ya

Kilombero mkoani Morogoro. Bw.

Simbamkuti anawakilisha kanda

namba 2 (Morogoro,Pwani na Dar

es Salaam).

Msaidizi wake ni Bibi. Veronica

Sophu mkulima mdogo wa kijiji cha

Madibila wilaya ya Mbarali mkoani

Mbeya anayewakilisha kanda namba

7 (Mbeya, Rukwa na Kigoma). Bibi

Esther Mallya mkulima kutoka

wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro

amechaguliwa kuwa Mwekahazina

akiwakilisha kanda namba 3

(Kilimanjaro na Tanga).

Wajumbe wa bodi wengine ni Bw.

Bodi ya zamani 2008-11

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

Joseph Kilowoko kutoka Namtumbo

Ruvuma akiwakilisha kanda namba

8(Iringa na Ruvuma), Paulo Joseph

kutoka Babati Manyara akiwakilisha

kanda namba 4(Manyara, Arusha

na Mara), Haji Ussi Haji kutoka

Bodi mpya 2011-14

KUTOKA MITANDAONI

Zanzibar akiwakilisha kanda namba

1 (Zanzibar).

Wengine ni Bw. Projestus

Ishekanyoro kutoka Kagera

akiwakilisha kanda namba 6

(Mwanza, Kagera na Shinyanga),

Bibi Amina Kazibure kutoka Masasi

Mtwara akiwakilisha kanda namba 9

(Mtwara na Lindi) na Bibi Prisca John

kutoka Igunga Tabora akiwakilisha

kanda namba 5 (Tabora, Singida na

Dodoma).

Mkurugenzi Mtendaji wa

MVIWATA Bw. Stephen Ruvuga

anaingia kwenye vikao vya bodi

kama katibu.

Wajumbe wa bodi iliyomaliza

muda wake walikuwa ni Bw. Yazid

Makame (mwenyekiti), Bibi Lydia

Ruliho (makamu), Bibi Grace

Runkulatire (Mwekahazina).

Wajumbe wengine walikuwa

ni Bw. Julius Mbago, Bw. Joseph

Kilowoko, Bw. Samwel Maseke,

Bibi Cosma Bullu, Bw. Habibu

Simbamkuti, Bw. Sylivester Yatuba.

17
KUTOKA MITANDAONI

SIKU YA WANAMTANDAO MKURANGA

Mkuu wa wilaya ahimiza mahusiano

baina ya wadau wa kilimo

Na Abdalla Idd, Mkuranga

Mkuu wa wilaya ya Mkuranga

mkoani Pwani Bw. Henry

Clemence, amewahimiza

wadau wa sekta ya kilimo wilayani

humo kuimarisha mahusiano yenye

lengo la kumsaidia mkulima kupiga

hatua za kimaendeleo.

Wito huo aliutoa wakati

akifungua maadhimisho ya SIKU YA

WANAMTANDAO MKURANGA,

iliyofanyika Disemba 6, 2011

Mkuranga mjini.

Mkuu huyo wa wilaya alisema, hivi

sasa katika wilaya hiyo na maeneo

mengine nchini yapo mashirika na

taasisi zinazofanya kazi na wakulima,

lakini taasisi hizo hazifahamiani

ingawa zinatekeleza shughuli kwenye

eneo moja.

Alisema kuimarishwa kwa

mahusiano hayo kutasaidia

Wanawake wa kijiji cha Kizapala wilayani Mkuranga wakionyesha usindikaji wa muhogo kwa

wageni toka nje ya nchi waliowatembelea kujifunza shughuli zao

18

kuunganisha nguvu na kuondoa

mtawanyiko wa raslimali ambazo

zikitumika vyema zitaongeza ufanisi.

Siku ya Wanamtandao Mkuranga

ambayo imefanyika kwa mara ya

kwanza, iliandaliwa na MVIWATA

Mkuranga kwa lengo la kuwakutanisha

wadau mbalimbali kuimarisha

mahusiano na kubadilishana taarifa.

Aidha siku hiyo ilitoa fursa kwa

wakulima kuonesha matokeo ya

shughuli za uzalishaji wanazofanya

na kuhamasisha matumizi ya bidhaa

zitokanazo na zao la Mhogo kama

mbadala wa mazao mengine ya

chakula.

Wakizungumza kwenye

maadhimisho hayo, baadhi ya

wanachama wa MVIWATA

walisema miongoni mwa mafanikio

waliyoyapata kupitia mtandao wa

wakulima wilayani humo ni pamoja

na kuimarisha mahusiano baina ya

wakulima na wadau wengine wa

kilimo zikiwemo asasi za fedha na

kushirikiana na Jeshi la polisi kupitia

ulinzi wa Polisi Jamii.

Walitolea mfano wa mfumo wa

ulinzi shirikishi ulioanzishwa na

mtandao wa wakulima wa kijiji cha

Kolagwa ili kutatua changamoto

ya usalama wa mali na maisha

ya wananchi hasa baada ya tukio

la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa

wakulima waliokuwa wamepata

mkopo.

Wakielezea kuhusiana na

changamoto walizokabiliana

nazo katika kufanikisha siku hiyo

wamesema kuwa ni pamoja na

uhaba wa rasilimali fedha na kwa

kuwa tukio hili lilikuwa la linafanyika

kwa mara ya kwanza ilichukua muda

mrefu kuwashawishi wadau na

kukubali kushiriki.

Mojawapo ya dosari zilizojitokeza

kwenye maadhimisho hayo ni

pamoja na baadhi ya wakuu wa

idara za halmashauri ya wilaya

kutohuhiria na hivyo changamoto

kadhaa zilizoibuliwa na wakulima

zilikosa majibu sahihi.

Mfano kukosekana kwa wataalamu

wa idara ya Afya kulikuwa ni kikwazo

kwa shughuli muhimu ya upimaji

wa hiari wa VVU kwa washiriki

waliokuwa tayari kufanya hivyo.

Siku hii maalum ya wanamtandao

ilihudhuriwa na wadau kutoka asasi

mbalimbali yakiwemo mabenki,

kampuni za simu za mkonini, Jeshi

la polisi, viongozi wa halmashauri

ya wilaya ya Mkuranga, viongozi wa

mtandao wa wilaya na watumishi

wa MVIWATA pamoja na wakulima

kutoka vijiji 16 vya wilaya hiyo.

Na maadhimisho ya siku hiyo

yalisindikizwa na burudani za aina

mbalimbali ikiwemo vikundi vya

ngoma na baadaye mashindano

ya mpira wa kikapu kwa timu za

wanawake.

Wakati huo huo, Mtandao

wa kati wa MVIWATA Mkuranga

Endelea Uk wa 19

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Maazimio ya Kongamano...

Inatoka uk. wa 8

waliazimia mambo yafuatayo:

1. Sisi wakulima wadogo tunasikitika

kuona kwamba maadili na misingi

ya Azimio la Arusha vimewekwa

kando kama msingi wa mfumo

wa uzalishaji na hivyo kukuza

matabaka ambapo matajiri

wachache ndiyo wanothaminiwa

na watawala wakati sisi tulio

wengi tukiwa tunapuuzwa katika

mfumo wa uzalishaji.

2. Sisi wakulima wadogo tunapinga

kwa nguvu zote na kwa kauli moja

mifumo yote ambayo kwa namna

moja au nyingine inapelekea

kumkandamiza mkulima mdogo na

kumsukuma kando katika mfumo

wa umilikaji ardhi na uzalishaji.

Mifumo hiyo inahusisha uporaji

wa rasilimali za ardhi ili kupisha

wawekezaji wakubwa wa ndani

na nje kwa kisingizio kwamba

wakulima wadogo hawana ufanisi

wa kuendeleza kilimo.

3. Pamoja na kushukuru juhudi za

serikali za kutoa huduma kwa

wakulima, sisi wakulima wadogo

tumekubaliana kwamba kuna

kasi ndogo sana ya maendeleo

ya mkulima mdogo na maisha

ya mkulima mdogo kwa ujumla

yameendelea kuwa duni hata

baada ya miaka 50 ya uhuru.

Tunaazimia kujipanga kuhakikisha

kuwa katika miaka 50 ijayo

wakulima wadogo wawe mhimili

wa uchumi wetu.

4. Wakulima wadogo tumekerwa na

kuchoshwa na migogoro mingi ya

ardhi isiyo na kikomo kila kukicha

katika maeneo mbalimbali ya nchi

hii, ambayo inasababishwa na

usimamizi mbovu na utekelezaji

hafifu wa sheria zetu ikiwemo

sera ya Ardhi ya Taifa pamoja

na sheria za ardhi za 1999 na

kanuni zake. Aidha, tunaitaka

serikali ichukue hatua dhidi ya

wawekezaji ambao wamekiuka

masharti ya kupewa ardhi kwa

ajili ya matumizi waliyoombea.

Vile vile, tunaitaka serikali ichukue

hatua za haraka katika kutatua

migogoro inayohatarisha amani

katika maeneo mbalimbali ya nchi;

kwa mfano mgogoro wa ardhi

Kibaigwa, Mbalali, Kiteto n.k

5. Tunasikitishwa na kuhuzunishwa na

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

kukua kwa matabaka kati ya matajiri

na masikini wengi wao tukiwa

sisi wakulima wadogo ambapo

hatuna uhakika hata wa upatikanaji

wa huduma za msingi ikiwemo

upatikanaji wa huduma muhimu

za kijamii hususan elimu ya watoto

wetu, huduma za afya kwa familia

zetu, miundombinu ya barabara na

maji safi na salama. Kwa sababu hiyo

tunaitahadharisha serikali kuchukua

hatua thabiti za kupunguza pengo

kati ya walionacho na wasionacho

ili kulinda amani na mshikamano wa

nchi yetu

6. Sisi wakulima wadogo tunaazimia

kuwawajibisha viongozi wote

ambao hawasimamii maslahi

ya wakulima wadogo, ikiwemo

kujipanga kutowapigia kura viongozi

wanaosaliti wakulima wadogo

katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Wakulima wadogo tusiburuzwe

na wanasiasa: tunapaswa kujenga

uwezo wetu wa kutofautisha

kauli za wanasiasa na ahadi zao za

majukwaani ili kuwabaini wanasiasa

wenye dhamira thabiti na wale

ambao kauli zao ni za kutetea

maslahi yao binafsi.

7. Sisi wakulima wadogo tumeazimia

kujenga mshikamano miongoni

mwetu ili tuweze kudai haki zetu

kwa nguvu ya hoja na bila woga.

Tutatumia fursa ya mchakato

wa utungaji wa katiba ili katiba

itakayotungwa ilinde vyema zaidi

maslahi ya wakulima wadogo

8. Sisi wakulima wadogo tumegundua

kwamba kudai haki kwa kupiga

kelele tu haitoshi. Kwa mfano

serikali imeziba masikio kuhusu

kilio chetu cha kuwa na uhuru wa

kuuza mazao yetu kwa mnunuzi

tunayetaka ndani na nje ya nchi.

Kwa hiyo tumedhamiria kutumia

sera, sheria na kanuni zilizopo

kudai haki zetu bila woga katika

vyombo vya sheria vilivyopo na

njia nyinginezo halali.

9. Ili kuongeza nguvu ya MVIWATA,

sisi ambao ni wanachama takriban

elfu sabini (70,000), tunaazimia

kuongeza idadi ya wanachama

wetu nchi nzima na shughuli

zetu za kiharakati pamoja na

kuelimishana kuhusu haki na

wajibu wa mkulima mdogo.

KUTOKA MITANDAONI

Mkuu wa wilaya

ahimiza...

Inatoka uk. wa 18

umefanya mkutano wake Mkuu

wa mwaka Disemba 5,2011

huku ukitanguliwa na warsha ya

siku moja kwa ajili ya kujifunza

na kujadili changamoto kadhaa

zinazowakabili wakulima wilayani

humo.

Mada kuu iliyojadiliwa kwenye

warsha ni mafunzo ya hatua za

mchakato wa uanzishwaji wa

Chama cha Akiba na Mikopo

(SACCOS) cha wakulima wa

zao la muhogo somo ambalo

lilifundishwa na Afisa kutoka Ofisi

ya Ushirika wilayani hapo.

Washiriki walitafakari zaidi

faida za kuwa na chombo hicho

ambacho kitarahisisha upatikanaji

wa mitaji na kuwasaidia kupanua

shughuli zao.

Baada ya mafunzo hayo,

washiriki walichagua kamati ya

muda iliyopewa jukumu la kuandaa

rasimu ya katiba ya SACCOS

na kukusanya michango kama

kiingilio na hisa kutoka katika vijiji

16 ambavyo ni Dundani, Mkuranga,

Mwanambaya, Mwanadilatu,

Sotele, Mavunje, Njopeka, Misasa,

Kerezange, Kizapara, Tungi, Tunda,

Mamdimpela, Mamdikongo,

Lupondo na Kolangwa.

Aidha siku ya mkutano

mkuu wa mtandao, wajumbe

walijadiliana juu ya uendelevu

wa mitandao ikiwa ni pamoja na

kutafuta mbinu itakayotumika

katika kuongeza wanachama

ambapo viongozi walikumbushwa

kuwahamasisha wakulima

kujiunga na MVIWATA na kuwa

na kadi za uanachama, kuweka

mfumo mzuri wa ukusanyaji wa

michango na pia kuweka mfumo

wa utunzaji wa kumbukumbu za

wanachama.

Mkutano huo pia ulipokea

taarifa ya utekelezaji wa shughuli,

taarifa ya mapato na matumizi ya

shughuli za mtandao kwa mwaka

2011 na kujadili mpango mkakati

wa mwaka 2012.

19
MAKALA

Wakulima, matrekta 200 waandamana

kudai haki

Na Goodness Mrema, Kibaigwa

Wakulima wilayani

Kongwa mkoani

Dodoma wakiwa

na matrekta yao zaidi ya 200

mnamo Disemba 1, 2011, walifanya

maandamano makubwa na kufunga

kwa muda barabara kuu ya Dodoma

– Dar es Salaam katika eneo la

Kibaigwa wakipinga maamuzi ya

serikali ya kuwazuia kulima kwenye

mashamba yao yaliyoko wilaya jirani

ya Kiteto mkoani Manyara.

Wakulima hao wana mashamba

yao makubwa kwenye vijiji tisa

vya wilaya ya Kiteto ambavyo ni

Lendolai, Mlimahamba, Laitini, Mbigiri,

Kutelimeinyi, Seseni, Laipela, Kimarai

na Kisima, ambavyo vimeingizwa

kwenye eneo la hifadhi ya taifa na

kuzuia shughuli zozote za kilimo.

Maandamano hayo yalifanyika

katika mji mdogo wa Kibaigwa

wilayani Kongwa mahali ambako

kuna soko la kimataifa la Mahindi

ambalo zaidi ya asilimia 60 ya mazao

yanayopokelewa sokoni hapo,

yanatoka kwenye vijiji hivyo.

Wakizungumza kwa nyakati

tofauti wakulima hao walisema kuwa

walianza kulima mashamba hayo tangu

mwaka 1990 lakini cha kushangaza

mwaka 2006 walitaarifiwa kuwa

eneo hilo limegeuzwa kuwa hifadhi

ya mbuga ya wanyama.

Bw. Clement Petro, mmoja wa

wakulima walioathiriwa na maamuzi

hayo anaeleza kuwa baada ya

kuzuiwa walifungua kesi mahakama

20

Mmoja wa wakulima walionyang’anywa ardhi akizungumza siku ya maandamano ya

Kibaigwa Disemba 1, 2011

kuu kupinga uamzi huo na kushinda.

Hata hivyo halmashauri ya

Kiteto ilikata rufaa mahakama ya

rufaa kupinga hukumu hiyo ambapo

ilishinda na wakulima wakaamriwa

kuondoka katika eneo hilo.

Hata hivyo, wakulima hao

wanasikitishwa na maamuzi hayo

huku wakisema serikali haiwatakii

mema kwa kuwa ni hivi karibuni tu

serikali imewahamasisha kuchukua

mikopo ya matrekta na kwamba

wanatarajia mavuno kutoka kwenye

mashamba hayo ili kulipa mikopo.

“Ni hivi majuzi tu serikali

imetuhamasisha kuchukua mikopo

ya matrekta nasi tumeitikia kwa

wingi tukifahamu kuwa tunayo ardhi

ya kutosha na tukivuna tutarejesha

mkopo, sasa leo tunazuiwa kulima, huu

ni sawa na uuaji,” alisema Bw. Petro.

Bw. Omary Athuman ni mkulima

na anamiliki matrekta zaidi ya 10

wilayani humo na anasema “kutokana

na halmashauri kutufukuza kutoka

katika eneo hili nina wasiwasi kama

nitaweza kurejesha mkopo wa

matrekta niliyokopa kutoka katika

Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga

taifa(Suma JKT) tawi la Dodoma.”

“Mimi sijui hii dhana ya kilimo

kwanza inatekelezwaje kwani mwanzo

tulidhani kuwa ni sera nzuri lakini hivi

sasa tunaona haitekelezwi kwa vitendo

na kuongeza kuwa yeye anazo hekari

300 ambazo huwa analima mahindi na

kupata mavuno mengi.”

Naye mkulima Bw. Ali Khalifan

Said, alisema kuwa wakati amri hiyo

inaanza kutekelezwa tayari walikuwa

wameshaandaa mashamba na hivyo

kuondoka katika eneo hilo ni hasara

kubwa sana kwake.

“Wanataka tuondoke katika eneo

hili lakini cha ajabu hawatuambii

twende wapi wala nani atalipa madeni

ya matrekta yetu tuliyokopa na nyumba

tulizojenga kwa mkopo” alisema Said.

Wakulima hao walielekeza kilio

chao kwa Rais Jakaya Kikwete

wakimuomba kuingilia kati suala

hilo ili waweze kurudishiwa ardhi na

kuendelea na uzalishaji, kwa sababu

viongozi wengine ngazi ya wilaya na

mkoa wameshindwa kuwasaidia.

Kwa upande wake, meneja wa soko

la wakulima la Kibaigwa Bw. Kusekwa

Dalali alisema kuwa wamekuwa

wakipokea mazao kutoka katika

mikoa mitano ambayo ni Dodoma,

Morogoro, Manyara, Iringa na Tanga.

Endelea Uk wa 21

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

KUTOKA MITANDAONI

Nani mchawi wa maendeleo ya

wakulima nchini?

Na Goodness Mrema

Uchumi wa wakulima

wadogo kabla na baada

ya uhuru uliendelea kuwa

mikononi mwa wakulima wenyewe

kupitia vyama vya ushirika.

Chanzo cha kuanzishwa kwa

vyama vya ushirika, ilikuwa ni

baada ya serikali ya kikoloni kuanza

kudhibiti faida ya mauzo ya mazao

ya wakulima bila kuwashirikisha.

Ni kweli mkoloni ndiye alianzisha

kilimo cha mazao ya biashara ili

kupata fedha za kigeni. Kabla ya hapo

wakulima walijishughulisha na kilimo

cha mazao ya chakula tu na ilipobidi

walibadilishana bidhaa pasipo kutumia

fedha kama ilivyo sasa.

Madhumini ya wakoloni ya

kuanzisha kilimo cha mazao ya

biashara na kuwaingiza wenyeji

kwenye mfumo wa biashara yalikuwa

ni pamoja na kupata malighafi kwa ajili

ya viwanda huko ulaya, lakini pia kwa

minajili ya kupata fedha za kugharamia

uendeshaji wa makolini yao.

Kwa kuwaingiza wakulima

kwenye kilimo cha biashara mkoloni

aliweza kutoza kodi na makato

mengine ambayo ndiyo yaliyotumika

kuendesha serikali.

Ili kupata fedha zaidi mkoloni

aliwanyonya wakulima kwa njia

mbalimbali, kwanza kununua mazao

kwa bei ndogo kuliko gharama

za uzalishaji, na pili kwa kuwauzia

pembejeo za kilimo kwa bei

waliyojipangia mwenyewe.

Na kama hiyo haitoshi, akaanza

kuwalazimisha kulima mazao

aliyoyataka yeye kwa manufaa yake

kitu ambacho kilitafsiriwa kuwa ni

utumwa.

Mtindo huu wa manunuzi

kujipangia bei ya kuuzia pembejeo

na kisha kujipangia ile ya kununulia

mavuno pasipo majadiliano, ndiyo

uliwazindua wakulima na kuanzisha

vyama vya ushirika.

Vyama hivyo vilisaidia siyo tu kuwa

na sauti ya pamoja lakini pia katika

kupigania bei nzuri inayoendana na

gharama halisi za uzalishaji. Vyama

hivi pia vilijiingiza katika kusambaza

pembejeo na huduma nyingine kwa

mkulima.

Wakulima wakajihamasisha na

kuanzisha vyama vya ushirika katika

sehemu mbalimbali za nchi.

TANU ilivyoanzishwa haikusita

kuziunganisha nguvu za vyama vya

ushirika na vyama vya wafanyakazi

na makundi mengine katika harakati

za uhuru. Lakini uhuru ulipopatikana,

serikali ya TANU iliendelea na

staili ile ya mkoloni ya kuwapunja

wakulima kwa kudhibiti faida ya

mauzo bila kuwashirikisha ili ipate

fedha za kugharamia uendeshaji wa

kazi za serikali.

Na ili kuhakikisha wakulima

hawafurukuti, mwaka 1967 serikali

iliviunganisha vyama vyote vya

ushirika nchini chini ya mwavuli

ulioitwa Muungano wa Vyama vya

Ushirika Nchini.

Serikali pia ilianzisha Bodi za Mazao

mbalimbali kuisaidia kudhibiti faida ya

mauzo kwa lengo lile lile la kupata

fedha za uendeshaji wa serikali.

Hata hivyo ilipofika mwaka 1976,

serikali iliuvunjilia mbali ushirika

na badala yake kukaanzishwa bodi

mbalimbali za mazao hasa mazao ya

biashara.

Bodi zilizoanzishwa ni pamoja na

za kahawa, pareto, tumbaku, chai na

korosho bila kusahau mkonge kwani

lilikuwa ndilo zao lenye kuingiza

fedha nyingi za kigeni hadi wakati

huo.

Baadaye tena baadhi ya bodi za

mazao zikabadilishwa kwa sheria

ya bunge kuwa mamlaka za mazao.

Hivyo kuwa na mamlaka ya mkonge,

mamlaka ya pamba na kadhalika.

Kazi kubwa ya mamlaka hizi ikiwa

ni kuimarisha udhibiti wa mfumo wa

uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa

mazao ndani na nje ya nchi.

Na kwa kuwa mamlaka hizo

zilianzishwa kwa sheria ya bunge

kukawa na udhibiti zaidi wa mazao

husika katika kila hatua. Kwa lugha

nyingine, mamlaka hizi ziligeuka

polisi wa wakulima.

Ni bodi za mazao ndizo zilizopanga

kima cha chini ambacho mkulima

alitakuwa kulima, utunzaji wa mazao

shambani, utaratibu na hata tarehe

ya kuvuna na bila kusahau zikipanga

bei ya kununulia mazao kutoka kwa

wakulima na pia bei ya pembejeo

walizouziwa wakulima.

Chini ya mamlaka za mazao

mkulima akageuka kuwa mfungwa

anayepaswa tu kutekeleza kile

alichoambiwa. Uhuru na demokrasia

waliyokuwa wameizoea kwenye

vyama vya ushirika vikapotea.

Badala yake sheria za kikoloni

zinazolazimisha mkulima kulima zao

fulani pasipo hiari yake na ambazo

ndizo zilikuwa zimewakasirisha watu

hadi kuupigania uhuru zikaimarishwa

ndani ya Tanzania huru.

Wakulima, matrekta 200 waandamana...

Inatoka uk. wa 20

Alisema kwa mwaka soko linauza

zaidi ya tani 1000 za mazao. “Tunauza

zaidi kwenye maeneo ya Dar es

Salaam, Kilimanjaro, MorogoroTanga,

Iringa na Mbeya na mikoa ya kanda ya

ziwa katika mikoa ya Mara, Mwanza

na Shinyanga ambako tumeanza

mwaka jana, pia kabla ya kufungwa

kwa mipaka tulikuwa tunapata

wateja kutoka Mombasa na Nairobi

lakini pia Zanzíbar ni wanunuzi

wazuri wa mazao yetu.”

Mazao wanayoyapokea katika

soko hilo ni pamoja na mahindi,

mbaazi, tetere, alzeti, nyonyo na

maharagwe na kwamba asilimia 60

ya mazao hayo hutoka katika wilaya

ya Kiteto.

“Kitendo hiki cha wakulima

kuzuiwa kulima mashamba

yao kwenye vijiji hivyo tisa

kinaashiria kufa kwa soko letu

kwa sababu asilimia 60 ya mazao

yanayopokelewa hapa hutoka

wilayani Kiteto hasa kwenye vijiji

hivyo,” alisema Bw. Kusekwa.

21
KATUNI

22

SASA

AFANYAJE NA

MAISHA HAYA MAGUMU

TUNAZALISHA KWA

NGUVU ZOTE LAKINI

FAIDA NI KIDOGO.

LAKINI MAMA CHUNGU HATA NCHI ZA

WENZETU MAJIRANI HAWAJAPIGA

HATUA SANA KATIKA MIPANGO YA

KUWAWEZESHA WAKULIMA

WADOGO.

MIAKA 50 YOTE

TUMESHINDWA KUFIKIA

MALENGO YA KUMUINUA

MKULIMA MDOGO, MIMI NAONA

TUSEME MIAKA 50 YA UHURU

TUMETHUBUTU, TUMESHINDWA,

TUJIPANGE UPYA.

MZEE

KUJIKO HAKATI

TAMAA MWAKA WA

PILI AMEKOSA MAHINDI

LAKINI BADO ANAENDA

KUPANDA TENA.

LAKINI

BABA CHUNGU

SERIKALI SI NDIO

INATAKIWA KUMSIMAMIA

MKULIMA?

‘EHE, EHE EHE!

NDIO

LAKINI SI NDIO

TUNASHEHEREKEA

MIAKA 50 YA UHURU SASA

ANGALIA MIAKA YOTE SERIKALI

IMEMSAIDIA VIPI MKULIMA

KUJIKWAMUA na KILIMO CHA

JEMBE LA MKONO

MH

TUSIJILIN-

GANISHE NA NCHI

MASIKINI ZENYE

RASILIMALI CHACHE

KULIKO TANZANIA

AAH

JEMBE

LENYEWE LA

MKONO?

MIMI SIONI

SABABU YA KUSHEHEREKEA

MIAKA 50 YA UHURU KAMA

MATATIZO YA MSINGI YANA-

TAKIWA KUSHUGHULIKIWA

HAYAJASHUGHULIKWA

LAKINI

ACHA AJARIBU

TENA ANAWEZA

KUPATA.

WAKATI

MKULIMA HUYO

HUYO NDIO ANAZAL-

ISHA CHAKULA CHA

KULISHA TAIFA

TULENGE MA-

FANIKIO MAKUBWA BILA

KUJALI MAJIRANI ZETU, SISI

TUNA RASILIMALI NA ARDHI YA

KUTOSHA AMBAZO HATUTUMII

IPASAVYO MFANO ARDHI, MITO

NA MAZIWA.

MATATIZO

GANI HAYO?

MARADHI,

UJINGA NA UMASKINI,

NA UMASKINI NDIO ADUI

No. 1 NA BADO WAKULIMA

HATUPEWI KIPAUMBELE

JAMANI!

AAH

KILIMO

CHENYEWE

CHA MVUA ZA

KUBAHATISHA?

TENA

NA KIJEMBE

KIMOJA CHA

MKONO!?

ILA MANENO YAKO

MAMA CHUNGU NI YA

BUSARA

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
MWAKA

1961 - 1985 ILIWEZA

KUWASAIDIA WAKULIMA

KWA KUANZISHA AZIMIO LA

ARUSHA, VIWANDA VILITUMIA

MALI GHAFI ZA WAKULIMA LAKINI

BAADA YA 1985 - 2011 MKULIMA

HANA THAMANI TENA.

MIAKA 50 YA

UHURU WAKULIMA WENGI

WANAONDOLEWA KWENYE

ARDHI YA MABABU. WAKULIMA

WANAPIGWA WANAFUNGWA,

WAKITETEA ARDHI YAO

NA KUUWAWA.

KWELI

TUMEKUWA

TUKIISHI KWA MATAMKO

MBALIMBALI KAMA KILIMO

NI UTI WA MGONGO, CHAKULA

NI UHAI, NA SASA KILIMO

KWANZA PAMOJA NA HAYO

WAKULIMA WAMEBAKI

DUNI.

HOFU

GANI TENA?

WANAHOFU

KUPORWA ARDHI

YAO.

MIMI

NAFIKIRI IMEFI-

KA WAKATI WAKULIMA

WAUNGANE WAIMARISHE

UMOJA WAO.

NA ARDHI

YENYEWE WANA-

PEWA WAWEKEZAJI

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

SIO UMOJA TU SASA HIVI

TUNATAKIWA TUJIPANGE NA

KUZIFAHAMU SHERIA ZA

ARDHI ILI TUITETEE HAKI

YETU

SASA

HAPO THAMANI

YA MKULIMA

MDOGO IKO WAPI?

NDIO

MAANA BABA WA

TAIFA ALISEMA MWAF-

RIKA AKIRUHUSIWA KUUZA

ARDHI BAADAE ARDHI YOTE

ITAMILIKIWA NA WAGENI

SABABU YA UMASKINI.

HUWEZI

KUJIZUIA KUUZA

ARDHI WAKATI

WEWE NI MAS-

KINI

HII IMESABA-

BISHWA NA SERA

AMBAZO HAZIMJALI

SANA MKULIMA

MDOGO

SAWA

KABISA SISI

NDIO WAZALISHAJI

WAKUBWA WA CHAKULA

CHA NCHI SIO HAO

WAWEKEZAJI WA-

NAOPELEKA CHAKULA

NJE YA NCHI

NDIO

KATUNI

JAMANI EH TUACHE

KULALAMIKA SI MMESIKIA

KAMATI YA KUKUSANYA MAONI

TUITUMIE VIZURI FURSA HII TUTOE

MAONI ILI KATIBA MPYA IMLINDE

MKULIMA MDOGO JUU YA DHULUMA

TUNAZOFANYIWA BASI!!

EEH NDIO

MAANA MIAKA 50

WANAISHI KWA HOFU!

SASA

IMEFIKA WAKA-

TI SERIKALI IFANYIE

KAZI MADHAIFU YOTE

YANAYO MKANDAMIZA

MKULIMA

23
KUTOKA MITANDAONI

Wakulima 30 wahitimu mafunzo ya

uwezeshaji na usimamizi vikundi

Na Goodness Mrema, Nyandira

Mvomero

Wakulima nchini

wamehimizwa kutumia

vyema ujuzi na elimu

wanayopewa wanaposhiriki

mafunzo mbalimbali kwa ajili ya

maendeleo ya wakulima wote

nchini.

Wito huo umetolewa Novemba

7, 2011 na Afisa Ushawishi na

Utetezi wa MVIWATA Bw

Thomas Laiser, alipokuwa akifunga

mafunzo ya Wakulima Wawezeshaji

30 (Mapromota) waliokuwa

wakihudhuria mafunzo ya wiki

mbili ya usimamizi na uendeshaji wa

vikundi katika kituo cha mafunzo ya

Wakulima cha Nyandira wilaya ya

Mvomero mkoani Morogoro.

Wawezeshaji hao walitoka

kwenye masoko matatu

yanayojengwa na MVIWATA katika

vijiji vya Igurusi Mbarali Mbeya, Matai

24

na Kasanga wilaya ya Sumbawanga

Vijijini.

Bw. Laiser alisema MVIWATA

imekuwa ikitoa mafunzo ya aina

mbalimbali kwa lengo la kuwajengea

uwezo wakulima wachache

(wakulima wakufunzi) ambao

wanatarajiwa kwenda kusambaza

ujuzi huo kwa wakulima wengine.

Mbali na mafunzo hayo MVIWATA

imekuwa ikiwezesha wakulima

kushiriki semina, mikutano na ziara

za mafunzo nje ya nchi na kwamba

wahusika wanaporudi kwenye

maeneo yao wanapaswa kuwa

chachu ya mabadiliko ya kusaidia

kusukuma mbele maendeleo.

“Tusiwe wachoyo wa kuwagawia

wenzetu maarifa tuliyopewa,

tumieni vyema maarifa mliyoyapata,

mkawasaidie viongozi na wakulima

wenzenu kuleta mabadiliko ya

kiuchumi na kuondokana na maisha

ya kimasikini,” alisema Bw. Laiser.

Aidha aliwataka washiriki

wa mafunzo hayo kuimarisha

Wahitimu wa mafunzo wakifurahia baada ya kukabidhiwa vyeti vya mafunzo hayo

mshikamano na mawasiliano katika

vikundi na mitandao ya wakulima

nchini ili kuwa na sauti yenye nguvu

itakayotimiza lengo la utetezi wa

maslahi yao.

“Mnatakiwa kuwasaidia wakulima

waweze kujipanga,kujisimamia na

kutetea maslahi yao na kuwezesha

vikundi kushirikiana na wadau

wengine,” alisema Bw. Laiser.

Aliwahimiza wakulima hao pia

kujenga utamaduni wa kutafuta

habari mbalimbali kupitia vyombo

vya habari na kuzitumia vyema habari

wanazozipata kujiletea maendeleo.

Katika risala yao wahitimu wa

mafunzo hayo walisema watatumia

vyema elimu waliyoipata kwa

kuielimisha jamii na kuahidi kutimiza

wajibu wao na kufanya kazi kwa

kujituma.

Wawezeshaji hao waliohitimu

mafunzo pia waliomba kupewa

ushirikiano na viongozi wa serikali

ngazi za vijiji na kata ili kurahisisha

utekelezaji wa majukumu yao.

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011
Jipatie nakala ya Jarida la Pambazuko katika ofisi

za MVIWATA ngazi za kati zifuatazo

Mratibu

MVIWATA Morogoro

S.L.P 3220 Morogoro

Mahali: Uwanja wa Maonyesho NaneNane mkabala na

ofisi za TASO

Simu/Faksi: 023 261 41 84

Barua Pepe: morogoro@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Rukwa

S.L.P 468 Sumbawanga

Mahali: Jengo la Bethlehem Center – Barabara ya Msakila

Faksi: +255 25 280 25 58

Simu: +255 764 232 747, +255 784 940 606

Barua pepe: rukwa@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Mbeya

S.L.P 3015 Mbeya

Mahali: Jengo la Bima na CRDB Bank (Ghorofa ya

mwisho

Simu: +255 784 979 397, +255 652 835 568

Barua pepe: mbeya@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Chunya

Mahali: Jengo la Halmashauri, chumba Na.3

Barua pepe: chunya@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Iringa

S.L.P 918 Njombe

Mahali: Jengo la Njoluma, Njombe mjini

Simu: 0782 241 224, +255 767 241 224

Barua pepe: iringa@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Kilimanjaro

S.L.P 7389 Moshi

Mahali: Mbuyuni sokoni- ghorofa ya GOLDEN GROWN

LODGE

Simu: +255 27 275 16 39, +255 784 720 320

Barua pepe: kilimanjaro@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Kagera

S.L.P 1753 Bukoba Mjini

Mahali: Ofisi za Mayawa-Mtaa wa Rwamishenyi, Barabara

ya Uganda

Simu: +255 788 685818, +255 782 154961, +255 755 522 447

Barua pepe: kagera@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Dodoma

S.L.P 3293 Dodoma

Mahali:Area C Dodoma eneo la INADES Formation

Tz,mkabala na msikiti wa Area C

Simu:255-26-2350013, +255 782 257 783,

+255 767 881 352

Faksi: +255 26 2350744

Barua pepe: dodoma@mviwata.org

Pambazuko Na. 40 Toleo la Oktoba – Disemba 2011

Mwenyekiti

MVIWATA Monduli (MVIWAMO)

S.L.P 47 Monduli

Mahali: Barabara ya Boma-Moringe Sekondari, Monduli

Mjini

Simu: 255-27-253 8029, +255 27 253 8337

Faksi: +255 27 253 8338

Barua pepe: monduli@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Manyara

S. L. P. 446,

Babati Manyara

Mahali: Barabara ya Nyerere

SIMU: +255 27 253 0385 Faksi: +255 27 253 0707

Baruapepe: manyara@mviwata.org

Mwenyekiti

MVIWATA Tabora

S.L.P 175 Igunga

Mahali: Mtaa wa Uarabuni

Simu: +255 784 398 414, +255 782 219 551

Barua pepe: tabora@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Zanzibar

S.L.P 149 Zanzibar

Mahali: Mwana kwerekwe- mkabala na shule ya sekondari

M’kwerekwe A

Simu: +255 773 926 955, +255 777 470 518

+255 783 651 135

Barua pepe: zanzibar@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Ruvuma

S.L.P 696 Songea Manispaa

Mahali: Jengo la TTCL ghorofa ya 2

Simu: +255-25-2600626, +255 756 096 291

Barua pepe: ruvuma@mviwata.org

Mratibu

MVIWATA Mkuranga

S.L.P 56 Mkuranga

Mahali: Karibu na Stendi ya Kimanzichana

Simu: 0786 158 646

Barua pepe: mkuranga@mviwata.org

MAWAKALA

Mwenyekiti:

MVIWATA Shinyanga

S.L.P 1024 Shinyanga

Mahali: Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Shinyanga

(Kizumbi)

Simu: +255 763 740 675, +255 755 546 311

Barua Pepe: shinyanga@mviwata.org

Mwenyekiti

MVIWATA Kigoma

S.L.P 1144 Kigoma

Mahali: Ndani ya ofisi ya KIKANGONET, Lumumba road

jengo la NHC chumba 205

Simu: 0713 565 252, 0762 565 252

Barua pepe: aisimba@yahoo.co.uk

25
IJUE MVIWATA

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania- MVIWATA

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) ni chombo cha kuunganisha wakulima wadogo ili kuwa na sauti moja katika utetezi wa

maslahi yao ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa.

Mtandao huu ulianzishwa mwaka 1993 na wakulima wadogo. Kauli mbiu ya MVIWATA ni ‘Mtetezi wa Mkulima ni Mkulima

Mwenyewe’.

Falsafa, utume na dira ya MVIWATA

Falsafa ya MVIWATA inajengwa katika ya misingi ya ushawishi na utetezi wa maendeleo ya wakulima wadogo katika nyanja za kiuchumi na

kijamii; kuwezesha mawasiliano na kujifunza kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wakulima.

Utume wetu:

Kuimarisha mawasiliano na kuwaunganisha wakulima wadogo kupitia vikundi na mitandao yao katika ngazi mbali mbali ili kujenga mtandao wa

kitaifa wenye nguvu ya kuwezesha ushiriki na uwakilishi wa kweli wa maslahi ya wakulima wadogo katika ngazi zote za maamuzi.

Dira yetu:

MVIWATA ni kuwa chombo imara chenye nguvu za ushiriki na uwakilishi wa mawazo ya mkulima katika mchakato wa maamuzi ya kiuchumi,

kijamii na kisiasa. Kuwa na uwezo wa kutekeleza na kufuatilia michakato na shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayogusa maslahi ya

wakulima wadogo.

Malengo ya MVIWATA

1. Kuwezesha mawasiliano miongoni mwa wakulima wadogo ili kujenga kwa pamoja mbinu na mikakati ya ushawishi na utetezi kwa maslahi ya

wakulima wadogo, kiuchumi na kijamii.

2. Kubadilishana mawazo, ujuzi na uzoefu juu ya kilimo na shughuli mbalimbali za wakulima ili kuboresha maisha na kuinua hali yao kiuchumi na

kijamii.

3. Kuwakilisha wakulima wadogo katika mashauriano na serikali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu au yanayoathiri ufanisi na maslahi ya

wakulima wadogo wa Tanzania.

Maeneo makuu ya mpango mkakati

1. Ushawishi na Utetezi: Kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kutetea maslahi yao.

2. Uwezo wa kiuchumi: kuwezesha wakulima wadogo kuwa na uwezo wa kiuchumi kupitia njia za akiba na mikopo, kuunganisha wakulima na

masoko na elimu ya ujasiliamali

3. Kuimarisha vikundi na mitandao ya wakulima kwa lengo la kujipanga na kujitetea.

4. Masuala mtambuka: Kujenga uelewa wa wakulima juu ya Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya Tabia ya nchi.

5. Ujenzi wa kitaaasisi kwa lengo la kuimarisha shirika

Muundo

Muundo wa MVIWATA una ngazi tatu ambazo ni Ngazi ya Taifa, Ngazi ya Kati na Ngazi ya Msingi. Ngazi ya Kati inaundwa na mitandao ya

kimkoa na kiwilaya wakati Ngazi ya Msingi inaundwa na mitandao ya Kata na Vijiji.

Shughuli kuu

1. Kujenga uwezo wa wakulima wadogo kwa kupitia mafunzo shirikishi juu ya mbinu za ushawishi na utetezi, mbinu za kuimarisha uchumi wa

wakulima wadogo na uendelevu wa rasilimali kwa njia za warsha, mafunzo, mikutano na ziara za mafunzo.

2.

3.

4.

Kuhamasisha wakulima wadogo kujiunga katika vikundi vya kijamii na kiuchumi, mitandao ya msingi (kata na vijiji) na mitandao ya kati (mikoa

na wilaya). Mpaka sasa MVIWATA imeanzisha mitandao ya kimkoa katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,

Morogoro, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Tabora na Tanga kwa Tanzania Bara. MVIWATA pia imeanzisha mitandao ya kiwilaya katika Wilaya

za Monduli (Arusha) na Chunya (Mbeya). Tanzania Visiwani, MVIWATA Zanzibar imeanzishwa na kusajiliwa (Usajili namba 401). Mkakati

unaendelea wa kuimarisha mitandao iliyopo na kuanzisha mitandao mipya.

Kukusanya, kuweka katika kumbukumbu na kusambaza habari zinazohusu ujuzi na uzoefu wa wakulima, sera za kitaifa na kimataifa kwa

kupitia jarida la Pambazuko Sauti ya Wakulima, vipindi vya radio, vipeperushi, vijitabu na machapisho mengine.

Kuhamasisha na kuwezesha wakulima kubuni na kuendesha miradi shirikishi ya kiuchumi na uzalishaji kwa lengo la kuboresha uchumi wa

wakulima wadogo kama vile vyama vya mazao, vyama vya kuweka na kukopa na masoko ya mazao.

5. Kuandaa mikutano na warsha kuhusiana na mada zinazowagusa au kuathiri maslahi ya wakulima wadogo.

Uanachama na jinsi ya kujiunga na shirika

MVIWATA ina wanachama wa aina tatu (3).

Aina ya kwanza ni Wanachama wa Kawaida ambao wamegawanyika katika makundi mawili;

a) Kikundi cha wakulima wadogo au

b)

Mkulima mdogo binafsi aliye mwanachama katika Kikundi au Mtandao. Mkulima atakuwa mwanachama wa kawaida wa MVIWATA mara

tu Kikundi au Mtandao wake utakapokubaliwa kuwa mwanachama. Atapewa kadi ya uanachama na kikundi au mtandao utapewa cheti cha

utambulisho.

Aina ya pili ni Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo.

Vyama, Mashirika na Mitandao ya Wakulima Wadogo vinavyojishughulisha na utetezi na ushawishi wa maslahi ya wakulima wadogo vilivyosajiliwa

chini ya sheria yoyote ya Tanzania katika Ngazi za Wilaya, Mkoa au Taifa vinaweza kuomba kuwa mwanachama wa MVIWATA iwapo vinakubaliana

kwa dhati na malengo na madhumuni ya Shirika.

Aina ya tatu ni Wanachama Washiriki

Ni mtu yeyote, taasisi au kikundi cha watu ambacho kinaunga mkono malengo na madhumuni ya Shirika. Mwanachama mshiriki anatamkwa na

Mkutano Mkuu wa MVIWATA.

Kila mwanachama, isipokuwa mwanachama mshiriki atalipa kiingilio na ada ya kila mwaka. Maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kujiunga na ada

yanapatikana kutoka kwa kiongozi au ofisi ya MVIWATA.

Kwa mawasiliano zaidi

Ofisi Kuu ya MVIWATA

Mkurugenzi Mtendaji

MVIWATA

S.L.P 3220 Morogoro

Simu: 023 261 41 84

Faksi: 023 261 41 84

Barua pepe: info@mviwata.org, mviwata@morogoro.net