jamhuri ya muungano wa tanzania - Ministry of Livestock and ...

jamhuri ya muungano wa tanzania - Ministry of Livestock and ... jamhuri ya muungano wa tanzania - Ministry of Livestock and ...

15.01.2013 Views

Programu ya Usimamizi wa Bonde la Ziwa Tanganyika 128. Mheshimiwa Spika, Programu ya Usimamizi wa Bonde la Ziwa Tanganyika yenye vipengele vya mazingira, uvuvi na mfumo wa majisafi na majitaka chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kutekelezwa katika nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Tanzania na Zambia. Kwa upande wa Tanzania, programu hii inatekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za Kigoma, Kigoma - Ujiji, Mpanda, Nkasi na Sumbawanga. Katika mwaka 2010/2011, kazi zifuatazo zimetekelezwa kwa upande wa sekta ya uvuvi:- (i) Kuainisha vijiji 20 kwa ajili ya kuanzisha Kamati za Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi (Fisheries Management Committees); (ii) Kuainisha mialo 47 ya kupokelea samaki katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za Kigoma (10), Kigoma-Ujiji (4), Mpanda (3), Nkasi (27) na Sumbawanga (3) ambapo taratibu za ujenzi wa miundombinu kwenye mialo minne (4) katika Mikoa ya Kigoma miwili (2) na Rukwa miwili (2) zinaendelea; (iii) Kutoa mafunzo kwa watalaam 65 kutoka TAFIRI (Kigoma), vituo vya doria (Kasanga na Kipili) na Mamlaka za Serikali za Mitaa husika kuhusu uanzishaji na ufuatiliaji wa miradi midogo ya jamii za wavuvi; (iv) Kufanya sensa ya uvuvi katika Ziwa Tanganyika; (v) Kuanzisha BMUs 19 na kutoa mafunzo kwa viongozi wake katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za Kigoma-Ujiji (2), Kigoma Vijijini (5), Nkasi (4), Mpanda (4) na Sumbawanga (4); na (vi) Kuwezesha ujenzi unaoendelea wa ofisi za vituo vya doria vya Kipili na Kasanga. 129. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012, Programu ya Usimamizi wa Bonde la Ziwa Tanganyika kwa kushirikiana na wadau itaendelea kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi na kuboresha miundombinu. Mradi wa Utekelezaji wa Mpango wa Usimamizi wa Uvuvi katika Ziwa Victoria (Implementation of a Fisheries Management Plan Project for Lake Victoria - IFMP) 130. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Utekelezaji wa Mpango wa Usimamizi wa Uvuvi katika Ziwa Victoria (IFMP) umemaliza muda wake katika kipindi cha mwaka 2010/2011. Katika kipindi hicho, Mradi umewezesha kutoa mafunzo kuhusu madhara ya uvuvi haramu kwa wadau 9,552 kutoka Halmashauri 14 katika Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera. Pia, ujenzi wa mialo sita (6) ya Marehe (Missenyi), Kikumbaitare (Chato), Bwai (Musoma), Sota (Rorya), Kigangama (Magu) na Kahunda (Sengerema) umekamilika na kukabidhiwa 66

kwa Halmashauri husika. Vilevile, mradi umewezesha kufanyika kwa siku-kazi za doria 535 katika ukanda wa Ziwa Victoria ambapo makokoro 1,799, nyavu za makila 19,106, nyavu za dagaa 34, nyavu za Utali (monofillaments) 2,474, katuli 152, kamba za kokoro mita 125,210, magari 12 na mitumbwi 479 vilikamatwa. Aidha, sangara wachanga kilo 87,823, sato wachanga kilo 24,292 na watuhumiwa 388 walikamatwa. Pia, shilingi 14,706,537 zilikusanywa kutokana na faini. Mradi wa Usimamizi wa Uvuvi Unaojumuisha Ikolojia na Mazingira (Ecosystem Approach to Fisheries - EAF Nansen Project) 131. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Usimamizi wa Uvuvi Unaojumuisha Ikolojia na Mazingira unatekelezwa katika ukanda wa pwani kwa kipindi cha miezi 18 kuanzia mwezi Septemba, 2010 na unafadhiliwa na FAO. Katika mwaka 2010/2011, mradi umetekeleza yafuatayo:- (i) Kuwajengea uwezo watalaam 14 wa Sekta ya Uvuvi ili watoe mafunzo ya kuhamasisha usimamizi wa uvuvi kwa kutumia mbinu za kiikolojia kwa watekelezaji wa mradi; na (ii) Kutoa mafunzo kuhusu usimamizi wa uvuvi kwa kutumia mbinu za kiikolojia kwa wadau 98 wakiwemo watalaam (42) kutoka Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Maafisa Uvuvi nane (8) kutoka Halmashauri za Pangani, Muheza, Mkinga na Jiji la Tanga na Wavuvi (48) kutoka Jiji la Tanga; kuandaa na kusambaza vipeperushi 422 na mabango 300 kwa wadau. Katika mwaka 2011/2012 mradi utatekeleza yafuatayo:- (i) Kuandaa na kukamilisha Mpango wa Usimamizi wa Samaki Wanaopatikana katika Tabaka la Juu la Maji; (ii) Kutoa mafunzo ya uhamasishaji wa usimamizi wa uvuvi unaojumuisha ikolojia na mazingira kwa taasisi nyingine na wavuvi wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani; na (iii) Kuwezesha ziara ya mafunzo katika Jamhuri ya Shelisheli ili kujifunza namna nchi hiyo inavyosimamia samaki wanaopatikana katika matabaka mengine ya maji. Masuala Mtambuka Huduma za Utawala na Rasilimali Watu 132. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/2011, Wizara imewapandisha vyeo watumishi 380 na kuwathibitisha kazini 80. Pia, watumishi 200 wa kada mbalimbali wamepatiwa mafunzo ya muda mrefu (50) na ya muda mfupi (150). 67

kwa Halmashauri husika. Vilevile, mradi umewezesha kufanyika kwa siku-kazi

za doria 535 katika ukanda wa Ziwa Victoria ambapo makokoro 1,799, nyavu

za makila 19,106, nyavu za dagaa 34, nyavu za Utali (monofillaments)

2,474, katuli 152, kamba za kokoro mita 125,210, magari 12 na mitumbwi

479 vilikamatwa. Aidha, sangara wachanga kilo 87,823, sato wachanga kilo

24,292 na watuhumiwa 388 walikamatwa. Pia, shilingi 14,706,537

zilikusanywa kutokana na faini.

Mradi wa Usimamizi wa Uvuvi Unaojumuisha Ikolojia na Mazingira

(Ecosystem Approach to Fisheries - EAF Nansen Project)

131. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Usimamizi wa Uvuvi Unaojumuisha

Ikolojia na Mazingira unatekelezwa katika ukanda wa pwani kwa kipindi cha

miezi 18 kuanzia mwezi Septemba, 2010 na unafadhiliwa na FAO. Katika

mwaka 2010/2011, mradi umetekeleza yafuatayo:-

(i) Kuwajengea uwezo watalaam 14 wa Sekta ya Uvuvi ili watoe mafunzo

ya kuhamasisha usimamizi wa uvuvi kwa kutumia mbinu za kiikolojia

kwa watekelezaji wa mradi; na

(ii) Kutoa mafunzo kuhusu usimamizi wa uvuvi kwa kutumia mbinu za

kiikolojia kwa wadau 98 wakiwemo watalaam (42) kutoka Idara ya

Maendeleo ya Uvuvi, Maafisa Uvuvi nane (8) kutoka Halmashauri za

Pangani, Muheza, Mkinga na Jiji la Tanga na Wavuvi (48) kutoka Jiji la

Tanga; kuandaa na kusambaza vipeperushi 422 na mabango 300

kwa wadau.

Katika mwaka 2011/2012 mradi utatekeleza yafuatayo:-

(i) Kuandaa na kukamilisha Mpango wa Usimamizi wa Samaki

Wanaopatikana katika Tabaka la Juu la Maji;

(ii) Kutoa mafunzo ya uhamasishaji wa usimamizi wa uvuvi unaojumuisha

ikolojia na mazingira kwa taasisi nyingine na wavuvi wa mikoa ya Lindi,

Mtwara na Pwani; na

(iii) Kuwezesha ziara ya mafunzo katika Jamhuri ya Shelisheli ili kujifunza

namna nchi hiyo inavyosimamia samaki wanaopatikana katika matabaka

mengine ya maji.

Masuala Mtambuka

Huduma za Utawala na Rasilimali Watu

132. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/2011, Wizara imewapandisha

vyeo watumishi 380 na kuwathibitisha kazini 80. Pia, watumishi 200 wa kada

mbalimbali wamepatiwa mafunzo ya muda mrefu (50) na ya muda mfupi

(150).

67

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!