jamhuri ya muungano wa tanzania - Ministry of Livestock and ...

jamhuri ya muungano wa tanzania - Ministry of Livestock and ... jamhuri ya muungano wa tanzania - Ministry of Livestock and ...

15.01.2013 Views

kilimo cha mwani yanafanywa na vikundi vya Mkombozi kilichopo Kijiji cha Pande (Bagamoyo) na Mgoji kilichopo Mtwara Vijijini kwa kutumia chelezo 15 zenye wastani wa eneo la mita za mraba 16 kila moja katika maji yenye kina kirefu. Matokeo ya awali yanaonesha kuwa, kwa kutumia teknolojia hii, mbegu za mwani zinaweza kupatikana kwa mwaka mzima. Vilevile, uzalishaji wa kambamiti katika mabwawa ya Alphakrust (Mafia) umeongezeka kutoka tani 60 mwaka 2009/2010 hadi tani 231.5 mwaka 2010/2011. 120. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/2011, Wizara imetoa mafunzo kwa wadau 545 kuhusu ukuzaji na usimamizi wa chaza wa lulu, Mwatiko, unenepeshaji wa kaa na kilimo cha mwani katika Halmashauri sita (6) za Mtwara Vijijini, Lindi Vijijini, Bagamoyo, Mafia, Jiji la Tanga na Mkinga. Aidha, Wizara imewezesha maafisa watatu (3) kushiriki mafunzo ya muda mfupi kuhusu uzalishaji na usimamizi wa ukuzaji viumbe kwenye maji nchini Misri mmoja (1) na Israel wawili (2). 121. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012, Wizara itatekeleza kazi zifuatazo:- (i) Kuimarisha vituo saba (7) vya ufugaji wa samaki katika Mikoa ya Kilimanjaro, Mara, Kagera, Morogoro, Ruvuma, Tabora na Lindi ili kuzalisha vifaranga milioni 2.5 vya Perege na 500,000 vya Kambale kwa ajili ya kusambazwa kwa wafugaji; (ii) Kuimarisha Kituo cha Mbegani (Pwani) na kuanzisha vituo vya Machui (Tanga) na Chihiko (Mtwara) vya kuzalisha mbegu za viumbe wanaofugwa kwenye maji ya bahari; (iii) Kuhamasisha ufugaji bora wa viumbe kwenye maji kwa kutumia teknolojia sahihi za ufugaji samaki, ukuzaji wa lulu na ukulima wa mwani; (iv) Kupandikiza samaki kwenye mabwawa ya kuchimba na malambo ya asili; na (v) Kuwezesha mafunzo ya Shahada ya Uzamili kwa watumishi wawili (2). MIRADI YA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI Mradi wa Kuimarisha Uwezo Mifugo (SADC–TADs Project) wa Kudhibiti Magonjwa ya Mlipuko ya 122. Mheshimiwa Spika, Wizara inatekeleza Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kudhibiti Magonjwa ya Mlipuko ya Mifugo (SADC–TADs Project) unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika nchi tano (5) za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zikiwemo Angola, Malawi, Msumbiji, Tanzania na Zambia. Mradi unalenga katika kudhibiti magonjwa ya Homa ya Mapafu ya Ng’ombe na Ugonjwa wa Miguu na Midomo na magonjwa 62

mengine ya mlipuko yanayojitokeza. Katika mwaka 2010/2011, Wizara imetekeleza kazi zifuatazo:- (i) Kununua vitendea kazi kwa ajili ya uchunguzi wa Ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Ng’ombe (CBPP), Ugonjwa wa Miguu na Midomo (FMD), ugonjwa wa Sotoka ya Mbuzi na Kondoo na magonjwa mengine kwa ajili ya Maabara Kuu ya Mifugo - Temeke na vituo vya kanda vya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo; (ii) Kumpata mtalaam muelekezi wa kutathmini Maabara Kuu ya Mifugo – Temeke kwa ajili ya kupata ithibati; (iii) Kuwezesha kufanya uchunguzi wa Ugonjwa wa Miguu na Midomo kwenye nyati katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi na ng’ombe katika maeneo yanayozunguka Hifadhi hiyo na maeneo mengine nchini; (iv) Kuwezesha kufanya uchunguzi wa sampuli 6,000 kwa ajili ya Ugonjwa wa Sotoka ya mbuzi na kondoo katika wilaya za Sumbawanga vijijini, Mbozi, Ileje, Mtwara vijijini, Newala, Tandahimba, Masasi, Tunduru, Nanyumbu, Longido, Ngorongoro, Arusha, Arumeru, Karatu, Monduli, Tarime, Rorya na Serengeti; na (v) Kununua pikipiki 18 kwa ajili ya vituo vya mpakani na Vituo vya Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (VICs) nchini. 123. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012 mradi utaendelea kuwezesha mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wataalam na watafiti 120 ndani na nje ya nchi. Pia, kuendelea kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mlipuko (Homa ya Mapafu ya Ng’ombe, Ugonjwa wa Miguu na Midomo na Sotoka ya Mbuzi na Kondoo) na ununuzi wa vifaa vya maabara kwa ajili ya Maabara Kuu ya Mifugo na Vituo vya Kanda vya Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (VICs). Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani (Marine and Coastal Environment Management Project –MACEMP) 124. Mheshimiwa Spika, mradi wa MACEMP unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uratibu wa Wizara zenye dhamana ya uvuvi. Gharama ya mradi ni jumla ya Dola za Kimarekani milioni 61 na unatekelezwa kwa kipindi cha miaka sita, kuanzia Agosti 2005 hadi Agosti 2011, chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia (IDA) kwa mkopo nafuu (Dola milioni 51 za Kimarekani) na msaada wa Mfuko wa Kimataifa wa Mazingira (the Global Environment Facility - GEF) Dola milioni 10. Mgawanyo wa fedha za mkopo, ni Dola za Kimarekani milioni 30.6 (asilimia 60) kwa Tanzania Bara na Dola za Kimarekani milioni 20.4 (asilimia 40) kwa Tanzania Zanzibar. Aidha, mgawanyo wa fedha za msaada ni Dola za Kimarekani milioni 5 kwa kila upande wa muungano. 63

mengine ya mlipuko yanayojitokeza. Katika mwaka 2010/2011, Wizara

imetekeleza kazi zifuatazo:-

(i) Kununua vitendea kazi kwa ajili ya uchunguzi wa Ugonjwa wa Homa ya

Mapafu ya Ng’ombe (CBPP), Ugonjwa wa Miguu na Midomo (FMD),

ugonjwa wa Sotoka ya Mbuzi na Kondoo na magonjwa mengine kwa ajili

ya Maabara Kuu ya Mifugo - Temeke na vituo vya kanda vya uchunguzi

wa magonjwa ya mifugo;

(ii) Kumpata mtalaam muelekezi wa kutathmini Maabara Kuu ya Mifugo –

Temeke kwa ajili ya kupata ithibati;

(iii) Kuwezesha kufanya uchunguzi wa Ugonjwa wa Miguu na Midomo kwenye

nyati katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi na ng’ombe katika maeneo

yanayozunguka Hifadhi hiyo na maeneo mengine nchini;

(iv) Kuwezesha kufanya uchunguzi wa sampuli 6,000 kwa ajili ya Ugonjwa

wa Sotoka ya mbuzi na kondoo katika wilaya za Sumbawanga vijijini,

Mbozi, Ileje, Mtwara vijijini, Newala, Tandahimba, Masasi, Tunduru,

Nanyumbu, Longido, Ngorongoro, Arusha, Arumeru, Karatu, Monduli,

Tarime, Rorya na Serengeti; na

(v) Kununua pikipiki 18 kwa ajili ya vituo vya mpakani na Vituo vya

Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (VICs) nchini.

123. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012 mradi utaendelea

kuwezesha mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wataalam na watafiti 120

ndani na nje ya nchi. Pia, kuendelea kufanya uchunguzi wa magonjwa ya

mlipuko (Homa ya Mapafu ya Ng’ombe, Ugonjwa wa Miguu na Midomo na

Sotoka ya Mbuzi na Kondoo) na ununuzi wa vifaa vya maabara kwa ajili ya

Maabara Kuu ya Mifugo na Vituo vya Kanda vya Uchunguzi wa Magonjwa ya

Mifugo (VICs).

Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani

(Marine and Coastal Environment Management Project –MACEMP)

124. Mheshimiwa Spika, mradi wa MACEMP unatekelezwa na Serikali ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya

uratibu wa Wizara zenye dhamana ya uvuvi. Gharama ya mradi ni jumla ya

Dola za Kimarekani milioni 61 na unatekelezwa kwa kipindi cha miaka sita,

kuanzia Agosti 2005 hadi Agosti 2011, chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia

(IDA) kwa mkopo nafuu (Dola milioni 51 za Kimarekani) na msaada wa

Mfuko wa Kimataifa wa Mazingira (the Global Environment Facility - GEF) Dola

milioni 10. Mgawanyo wa fedha za mkopo, ni Dola za Kimarekani milioni

30.6 (asilimia 60) kwa Tanzania Bara na Dola za Kimarekani milioni 20.4

(asilimia 40) kwa Tanzania Zanzibar. Aidha, mgawanyo wa fedha za msaada

ni Dola za Kimarekani milioni 5 kwa kila upande wa muungano.

63

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!