HOTUBA RC MWANZA-BMU.pdf - karibu kwenye tovuti rasmi ya ...
HOTUBA RC MWANZA-BMU.pdf - karibu kwenye tovuti rasmi ya ...
HOTUBA RC MWANZA-BMU.pdf - karibu kwenye tovuti rasmi ya ...
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA MWANZA MHESHIMIWA

DR. JAMES ALEX MSEKELA (MB) KATIKA WARSHA YA VIONGOZI

WA SERIKALI ZA MITAA MKOA WA MWANZA JUU YA

USHIRIKISHWAJI WA JAMII KUPITIA VIKUNDI VYA ULINZI WA

RASLIMALI YA UVUVI (BMUs) KATIKA UKUMBI WA BENKI KUU

MWANZA TAREHE 17 MACHI 2006

MHESHIMIWA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LAMWANZA

WAHESHIMIWA WENYEVITI WA HALMASHAURI ZA WILAYA

WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI ZA WILAYA

MABIBI NA MABWANA

Awali ya yote ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa waandaaji wa

warsha hii kwa kunipa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa

warsha hii muhimu kuhusu Ushirikishwaji wa jamii katika ulinzi wa raslimali

ya Uvuvi hususani katika Ziwa Victoria. Nachukua nafasi hii kuwapa pole

ya safari wale wote waliotoka nje ya Jiji la Mwanza kuja kuhudhuria

warsha hii.

Ndugu Mwenyekiti, Nimejulishwa kuwa warsha hii imejumuisha Mstahiki

Meya wa Jiji la Mwanza, Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya,

Waheshimiwa Madiwani wa Kata zinazopakana na Ziwa Victoria na

Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya.Warsha ina lengo la

kujenga uelewa wa Waheshimiwa Madiwani juu ya dhana ya ushirikishwaji

wa jamii katika kupanga, kusimamia na kuendeleza raslimali ya Uvuvi

pamoja na mabadiliko ya muundo na utendaji wa vikundi vya ulinzi wa

raslimali ya uvuvi (Beach Management Units). Warsha hii imekuja wakati

mwafaka baada ya Halmashauri zetu katika Mkoa wa Mwanza kupata

Madiwani wapya baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Tarehe 14

Desemba 2005.

Ndugu Mwenyekiti, kama mnavyofahamu, mchango wa sekta ya uvuvi

katika uchumi wa taifa na wananchi katika halmashauri zetu

zinazozunguka Ziwa Victoria ni mkubwa sana.Ni ukweli uliowazi kwamba

maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Wananchi katika Mkoa wa Mwanza

1
yanategemea sana shughuli za Uvuvi.Sekta ya Uvuvi inatoa ajira kwa

Wananchi na hususani vijana ambao ni nguvu kazi inayopaswa kutumika

ipasavyo kuleta maendeleo ya taifa kiuchumi na kijamii katika taifa letu.

Takwimu zinaonyesha kuwa Sekta ya Uvuvi inatoa ajira kwa wavuvi

80,053 (Frame Survey 2002). Pia sekta ya uvuvi huongeza kipato na kutoa

lishe bora ya protini kwa wananchi na kuchangia pato la taifa la fedha za

ndani na fedha za kigeni. Kwa mfano mwaka 2005 mauzo ya tani

53392.20 za samaki nchi za nje yalilipatia Taifa Tsh. 182 bilioni sawa na

Dola za Marekani 16,561,981.46. Kupanuka kwa sekta ya uvuvi

kumechochea mzunguko mkubwa wa fedha na kusababisha upanukaji wa

shughuli zingine za kiuchumi na kijamii mfano upanukaji wa shughuli za

viwanda, ujenzi wa mahoteli, maduka, biashara na ujenzi wa nyumba bora

mijini na vijijini miongoni mwa jamii za wavuvi. Hivyo raslimali ya uvuvi ya

Ziwa Victoria inapaswa kulindwa,kuhifadhiwa, kuendelezwa na kuvunwa

kwa busara ili iendelee kutoa mchango endelevu wa maisha ya wananchi

kwa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.

Ndugu Mwenyekiti, licha ya manufaa niliyoyataja; raslimali ya Uvuvi

katika Ziwa Victoria inakabiliwa na matatizo kadhaa: uharibifu wa

mazingira unaotokana na uchafuzi wa maji taka toka viwandani na

majumbani, katika sehemu za mijini, kuendelea kuwepo kwa uvuvi usio

endelevu wa kutumia mbinu na zana haramu za uvuvi kama vile

• Makokoro ya kuvutia nchi kavu(beach seines)

• Makokoro ya dagaa chini ya milimita 10

• Nyavu za makila za chini ya inchi 5. kwa samaki aina ya

Sato(Tilapia) na inchi 6 kwa kuvulia samaki aina ya Sangara na

Katuli.

• Hali duni ya usafi wa mazingira ya mialo, pia kumekuwepo na

upotevu mkubwa wa samaki baada ya kuvuliwa kutokana na mbinu

duni za uchakataji(processing) na uhifadhi wa samaki baada ya

kuvuliwa.

Aidha ushirikiswaji duni wa wadau wa sekta ya Uvuvi na jamii ya wavuvi

katika Ziwa Victoria umechangia kwa kiasi kikubwa kwa jamii kutowajibika

2
katika kulinda raslimali ya uvuvi kutokana na jamii kufikiri kuwa raslimali ya

uvuvi ni mali ya Serikali na sio yao. Kutokana na matatizo niliyoyataja hapo

juu, ni wazi kuwa hivi sasa samaki wamepungua na aina nyingi za samaki

zimeelekea kutoweka katika Ziwa Victoria na kubakiwa na samaki aina

tatu tu zinazovuliwa kibiashara ambazo ni Sangara, Sato, Dagaa na Furu

katika baadhi ya maeneo.

Wote mnafahamu kuwa uwezo wa serikali pekee kusimamia raslimali ya

uvuvi ni mdogo kutokana na kuwa na watumishi wachache na uwezo

mdogo wa kugharamia usimamizi wa raslimali. Njia pekee ya kusimamia

kikamilifu raslimali hii ni kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta hii

hususan jamii ya wavuvi katika kupanga, kutekeleza, kusimamia na

kuendeleza raslimali ya uvuvi.

Ndugu Mwenyekiti, Kwa kutambua umuhimu wa jamii kushiriki katika

menejimenti ya uvuvi Serikali mwaka 1997 ilitunga sera ya uvuvi ambayo

inatamka bayana umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika kuhakikisha

usimamizi madhubuti wa raslimali za uvuvi katika nchi yetu.

Kulingana na sera hii ya sekta ya Uvuvi vikundi vya ulinzi wa

raslimali(BMUs) vipatavyo 511 vilianzishwa katika mialo ya Ziwa

Victoria.Kutokana na matatizo mbalimbali vikundi hivyo vimepungua sana.

Baadhi ya matatizo ni kutokuwa na nguvu ya kisheria ya uwepo wa

vikundi, kutoshirikishwa kwa makundi yote yaliyopo mialoni, kukosekana

kwa wajibu uliowazi wa vikundi hivi na kukosa ushirikiano wa kutosha na

msaada toka kwa viongozi katika ngazi za vijiji na wilaya katika kutekeleza

majukumu yao. Ili kutekeleza sera Serikali imetunga Sheria mpya ya Uvuvi

na. 22 ya Mwaka 2003 ambayo imefuta ile iliyokuwepo awali sheria Na.6

ya 1970.Hivi sasa ushirikishwaji wa jamii katika usimamizi wa raslimali ya

uvuvi una nguvu ya kisheria ukilinganisha na hali ilivyokuwa kabla ya

kutungwa kwa sheria mpya ambayo imeanza kutumika mwezi Agosti 2005.

Sheria hii pia inahalalisha uwepo wa vikundi vya ulinzi wa rasilimali ya

Uvuvi katika Ziwa Victoria (BMUs).

3
Ziwa Victoria linamilikiwa na nchi zote tatu za Afrika ya Mashariki, hivyo

usimamaizi wake unahitaji mtazamo na mbinu za pamoja.Kwa kutambua

hilo nchi hizi zimekubaliana kuwa ushirikishwaji wa jamii katika ulinzi wa

raslimali ya uvuvi ni njia pekee itakayowezesha kuwa na usimamizi

endelevu na mkamilifu wa sekta ya Uvuvi katika Ziwa Victoria. Nchi hizi

zimekubaliana juu ya mfumo wa uanzishaji na uendeshaji wa vikundi vya

Ulinzi wa raslimali(BMUs) ambao ni tofauti kidogo na mfumo tulioutumia

Tanzania katika kuanzisha vikundi hivi. Kutokana na mabadiliko hayo

inalazimu kufanya mabadiliko katika mfumo wa BMU tulionao. Hivyo

Tanzania imetoa muongozo wa kitaifa wa ushirikishwaji wa jamii katika

Menejimenti ya Uvuvi Ziwa Victoria (National BMU Guideline) ambao

umekidhi matakwa ya kikanda.

Nimeelezwa baadhi ya mabadiliko ni kuwa BMU katika mfumo mpya

zitajumuisha makundi yote ya wadau waliopo mwaloni, Uwakilishi

unaowiana wa makundi hayo katika Kamati ya Utendaji na kuwa ili mwalo

ustahili kuunda BMU unapaswa kuwa na mitumbwi kuanzia thelathini na

kuendelea.

Kwa kuzingatia mabadiliko hayo, nimefahamishwa kuwa katika warsha hii,

jumla ya mada sita zitatolewa ambazo zinalenga kuwaelewesha

Waheshimiwa madiwani kuhusu mradi wa IFMP unaofadhili utekelezaji wa

Mpango wa menejimenti ya Uvuvi katika Ziwa Victoria ambao

utajishughulisha na mambo yafuatayo:

• Kuimarisha usimamizi wa jamii wa raslimali;

• Hali ya uwingi na aina za samaki katika Ziwa Victoria;

• Sheria zinazohusu usimamizi wa raslimali ya uvuvi Tanzania

hususani Ziwa Victoria;

• Usimamizi wa serikali pekee na matatizo yake katika menejimenti ya

uvuvi na njia mbadala ya usimamizi shirikishi wa jamii;

• Ushirikishwaji wa jamii katika Menejimenti ya Uvuvi kupitia BMU;

• Mada juu ya Muundo, uanzishwaji na uendeshaji wa taasisi ya BMU

na

4
• Mada juu ya wajibu wa serikali za mitaa katika kusimamia raslimali

ya uvuvi hapa nchini.

Nimefahamishwa kuwa baada ya kila mada kutolewa majadiliano ya kina

yatafanyika, mikakati ya pamoja na maazimio yatawekwa yanayolenga

kuboresha ushiriki wa jamii katika menejimenti ya Uvuvi katika Ziwa

Victoria.

Napenda kusisitiza kuwa raslimali ya Ziwa Victoria ni muhimu kwa

maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wetu, kitaifa, kikanda na

kimataifa. Tumieni vizuri muda wa warsha hii katika kujadili matatizo ya

uvuvi usio endelevu na kupata uelewa juu ya umuhimu wa kushirikisha

jamii. Aidha kwa kuwa ninyi ni viongozi ni muhimu kupata uelewa wa kina

juu muundo mpya wajibu na utendaji wa BMUs ili muweze kutoa msukumo

katika kuziunda, kuratibu na kusimamia shughuli zake, kikamilifu kwa

lengo la kuwa na uvunaji endelevu wa raslimali ya samaki.

Mafanikio ya ushirikiswaji wa jamii katika ulinzi wa raslimali ya Uvuvi

yanahitaji sana msaada wa viongozi katika ngazi zote toka ngazi ya kijijini,

Wilaya(madiwani na uongozi wa wilaya) na Serikali kuu katika kujenga

uwezo wa jamii kushiriki kikamilifu katika menejimenti ya uvuvi. Pia jamii

inahitaji kujengewa uwezo katika katika uongozi, menejimenti ya uvuvi na

menejimenti ya fedha n.k. Nimeelezwa kuwa Mradi wa IFMP utagharamia

uundaji wa BMU katika mfumo mpya, kujenga uwezo wa vikundi katika

kusimamia raslimali kwa kutoa mafunzo kwa kamati za BMU katika nyanja

za uongozi, menejimenti ya uvuvi na menejimenti ya fedha. Pia Serikali ya

Tanzania imenunua injini 27 za boti ambazo zitagawiwa vikundi vya

jamii(BMU) vinavyohusika na ulinzi na usimamizi wa raslimali ya uvuvi.

Uendeshaji na usimamizi wa raslimali ya Uvuvi kupitia jamii(BMU) una

gharama zake. Jamii kupitia vikundi vya ulinzi wa raslimali inahitaji kuwa

na vyanzo vya mapato endelevu kugharamia usimamizi wa raslimali katika

ngazi ya jamii. Jambo muhimu na la msingi ambalo Halmashauri

zinapaswa kusaidia ni kuvipa upendeleo wa pekee vikundi hivi kwa kuvipa

uwakala wa kukusanya ushuru wa mapato ya samaki na mazao yake ili

5
mapato ya ziada baada ya kulipa kiwango kilichowekwa na halmashauri,

itumike katika kugharamia shughuli za usimamizi wa raslimali unaofanywa

na vikundi kwa manufaa yetu sote na pia kuwa motisha kwa ushiriki wao

katika usimamizi wa raslimali.

Ni mategemeo yangu kuwa baada ya warsha hii na mrudipo katika

halmashauri zenu mtakuwa katika mstari wa mbele kutekeleza na

kusimamia ushirikishwaji wa jamii kwa kuvipa vikundi vya BMU kila

msaada ili kuhakikisha jamii inatekeleza majukumu ya ulinzi wa raslimali

katika mialo wanayoisimamia. Mkumbuke kuwa ilani ya Chama Cha

Mapinduzi inatamka bayana kuhusu uvuvi endelevu hivyo hatuna budi

kuitekeleza kwa vitendo.

Baada ya kusema haya, sasa napenda kutamka kuwa warsha hii juu ya

ushirikishwaji wa jamii katika menejimenti ya Uvuvi katika Ziwa Victoria

kupitia vikundi vya jamii vya ulinzi wa raslimali(BMU) imefunguliwa rasmi.

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA

6