hotuba ya waziri wa maendeleo ya mifugo na - Ministry of Livestock ...

hotuba ya waziri wa maendeleo ya mifugo na - Ministry of Livestock ... hotuba ya waziri wa maendeleo ya mifugo na - Ministry of Livestock ...

15.01.2013 Views

(ix) Kuendesha mafunzo kwa wataalam 28 kuhusu takwimu za uvuvi katika wilaya 14 zinazotekeleza mradi; (x) Kuwezesha kufanyika tafiti za samaki waishio kwenye matumbawe kwa lengo la uhifadhi wa samaki hao; na (xi) Kuwashirikisha wananchi na wadau wengine kuhusu uhifadhi wa samaki aina ya Silikanti kwenye eneo la Kigombe (Muheza). Mradi wa Kutekeleza Mpango wa Usimamizi wa Uvuvi wa Ziwa Victoria (Implementation of Fisheries Management Plan) 127. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kutekeleza Mpango wa Usimamizi wa Uvuvi wa Ziwa Victoria (Implementation of Fisheries Management Plan) unatekelezwa katika Ziwa Victoria na unahusisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambazo zinamiliki ziwa hilo na kusimamiwa na Taasisi ya Uvuvi katika Ziwa Victoria (Lake Victoria Fisheries Organization). Mradi huu unafadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) kwa gharama ya Euro milioni 29.9. Katika mwaka 2007/2008 kazi zifuatazo zimetekelezwa: (i) Kuandaa Mwongozo wa Kikanda na Kitaifa wa kuanzisha na kusimamia vikundi vya ulinzi wa rasilimali ya uvuvi (Regional and National BMU Guidelines); (ii) Kuhuisha taratibu za utoaji leseni na usajili wa mialo; (iii) Kuandaa Mpango wa Kikanda wa Kudhibiti Uvuvi haramu na Nguvu ya Uvuvi katika Ziwa Victoria (Regional Plan of Action to Deter and Control Illegal, Unreported and Unregulated Fishing); (iv) Kuandaa na kutekeleza Mpango wa Ki-kanda wa Kudhibiti Uvuvi Haramu na Kasi ya Uvunaji wa Samaki kwa kupunguza nguvu ya uvuvi - Regional Plan of Action for Reducing Fishing Capacity – RPOA – Capacity katika Ziwa Victoria; (v) Kuwezesha doria kufanyika dhidi ya uvuvi haramu ambapo watuhumiwa 558 walikamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Zana zilizokamatwa ni pamoja na makokoro 1,434, makokoro dagaa 141, nyavu chini ya inchi tano 6823, timba (monofilament nets) 742, mitumbwi isiyokuwa na leseni 60 na magari 3 yaliyokuwa yakisafirisha mazao ya samaki kinyume cha sheria; (vi) Kuwezesha uboreshaji wa mialo 12, miradi mitano ya huduma za jamii, ununuzi wa magari na vitendea kazi na kutoa elimu kwa umma na mafunzo kwa watalaam; na (vii) Kuwezesha kuandaa Viwango vya Utekelezaji “Standard Operating Procedures” (SOPs) na miongozo, “Code of Practices na Fish Inspectors’ Guide”, kwa matumizi ya nchi tatu za Afrika Mashariki. 128. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2008/2009, Wizara yangu kupitia Mpango wa Usimamizi wa Uvuvi wa Ziwa Victoria itatekeleza kazi zifuatazo: 48

(i) Ujenzi wa mialo sita ya Bwai (Musoma Vijijini), Sota (Rorya), Kigangama (Magu), Kahunda (Sengerema), Ikumbitare (Chato) na Marehe (Misenyi). (ii) Kukamilisha miradi mitatu ya huduma kwa jamii ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje katika zahanati ya Kijiji cha Lugata (Sengerema); na ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya kata ya Nyahongo (Rorya), ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Soswa (Sengerema). (iii) Kuendelea na ufuatiliaji na kutoa huduma za ushauri kwa wavuvi juu ya uvuvi endelevu na ulinzi wa rasilimali kupitia BMUs. (iv) Kuendelea kugharamia doria na mafunzo kwa wataalam. MASUALA MTAMBUKA Sensa ya Mifugo 129. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa sensa ya mifugo ili kupata takwimu sahihi kwa matumizi ya mipango ya maendeleo, Wizara yangu itaendesha sensa ya mifugo kwa njia ya sampuli (Sample Census Survey) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Taasisi ya Takwimu ya Taifa (National Bureau of Statistics). Sensa kwa njia ya kuhesabu mifugo kamili (total livestock count/ enumeration) itafanyika mwaka 2010 kwa mujibu wa Kalenda ya Sensa ya Kilimo Duniani (WCA-World Census of Agriculture) inayoratibiwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO). Hifadhi ya Mazingira 130. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2007/2008, Wizara iliendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Kuhifadhi Mazingira na Vyanzo vya Maji kwa kuhimiza matumizi bora ya maeneo ya malisho, matumizi ya fursa mbalimbali katika maeneo kame ya ufugaji na matumizi ya nishati itokanayo na samadi ya mifugo (biogas). Katika mwaka 2008/2009, Wizara itaendelea kuhamasisha hifadhi ya mazingira kwa kuhimiza matumizi bora ya ardhi ya malisho na nishati mbadala ya biogas. Jinsia 131. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2007/2008, Wizara yangu iliendelea kuboresha dawati la jinsia na kamati husika ziliundwa na mafunzo kutolewa. Katika mwaka 2008/2009, Wizara itaendelea kuimarisha dawati la 49

(ix) Kuendesha mafunzo kwa wataalam 28 kuhusu takwimu za uvuvi

katika wilaya 14 zinazotekeleza mradi;

(x) Kuwezesha kufanyika tafiti za samaki waishio kwenye matumbawe

kwa lengo la uhifadhi wa samaki hao; na

(xi) Kuwashirikisha wananchi na wadau wengine kuhusu uhifadhi wa

samaki aina ya Silikanti kwenye eneo la Kigombe (Muheza).

Mradi wa Kutekeleza Mpango wa Usimamizi wa Uvuvi wa Ziwa

Victoria (Implementation of Fisheries Management Plan)

127. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kutekeleza Mpango wa Usimamizi wa

Uvuvi wa Ziwa Victoria (Implementation of Fisheries Management Plan)

unatekelezwa katika Ziwa Victoria na unahusisha nchi za Tanzania, Kenya na

Uganda ambazo zinamiliki ziwa hilo na kusimamiwa na Taasisi ya Uvuvi katika

Ziwa Victoria (Lake Victoria Fisheries Organization). Mradi huu unafadhiliwa na

Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) kwa gharama ya Euro milioni 29.9. Katika

mwaka 2007/2008 kazi zifuatazo zimetekelezwa:

(i) Kuandaa Mwongozo wa Kikanda na Kitaifa wa kuanzisha na kusimamia

vikundi vya ulinzi wa rasilimali ya uvuvi (Regional and National BMU

Guidelines);

(ii) Kuhuisha taratibu za utoaji leseni na usajili wa mialo;

(iii) Kuandaa Mpango wa Kikanda wa Kudhibiti Uvuvi haramu na Nguvu ya

Uvuvi katika Ziwa Victoria (Regional Plan of Action to Deter and Control

Illegal, Unreported and Unregulated Fishing);

(iv) Kuandaa na kutekeleza Mpango wa Ki-kanda wa Kudhibiti Uvuvi

Haramu na Kasi ya Uvunaji wa Samaki kwa kupunguza nguvu ya uvuvi -

Regional Plan of Action for Reducing Fishing Capacity – RPOA –

Capacity katika Ziwa Victoria;

(v) Kuwezesha doria kufanyika dhidi ya uvuvi haramu ambapo watuhumiwa

558 walikamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Zana

zilizokamatwa ni pamoja na makokoro 1,434, makokoro dagaa 141,

nyavu chini ya inchi tano 6823, timba (monofilament nets) 742,

mitumbwi isiyokuwa na leseni 60 na magari 3 yaliyokuwa yakisafirisha

mazao ya samaki kinyume cha sheria;

(vi) Kuwezesha uboreshaji wa mialo 12, miradi mitano ya huduma za jamii,

ununuzi wa magari na vitendea kazi na kutoa elimu kwa umma na

mafunzo kwa watalaam; na

(vii) Kuwezesha kuandaa Viwango vya Utekelezaji “Standard Operating

Procedures” (SOPs) na miongozo, “Code of Practices na Fish

Inspectors’ Guide”, kwa matumizi ya nchi tatu za Afrika Mashariki.

128. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2008/2009, Wizara yangu kupitia

Mpango wa Usimamizi wa Uvuvi wa Ziwa Victoria itatekeleza kazi zifuatazo:

48

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!