KILIMO CHA VITUNGUU MAJI - The 4-H Global Knowledge Center

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI - The 4-H Global Knowledge Center KILIMO CHA VITUNGUU MAJI - The 4-H Global Knowledge Center

4.hglobalknowledge.org
from 4.hglobalknowledge.org More from this publisher
17.12.2012 Views

Mbinu za kudhibiti ugonjwa huu ni kuendesha mzunguko (crop rotation) wa muda mrefu wa mazao pamoja na kuzuia kutuama kwa maji shambani. Kupunguza msongamano wa mazao shambani na matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine, matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu uongeza mlipuko wa magonjwa. Viatilifu kama vile Mancozeb hutumika kuzuia mashmbulizi ya ugonjwa huu. 2. Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) Magonjwa haya hushambulia majani ya mimea shamabani na hata miche michanga. Kwenye majani kunaonekana vidoa vyeupe hasa kwenye majani makuu ya mimea michanga. Ukungu mweupe unatokea na kuongezeka kwa haraka kwenye sehemu au nyakati za baridi. Viini huishi kwenye mabaki ya mimea ya vitunguu na huweza kupeperushwa mbali na upepo. Kwenye mimea michanga ugonjwa unaweza kudhibitiwa na madawa kama mancozeb. 3. Kuoza kwa vitunguu (bulb rots) Hali hii inaweza kutokea shambani au wakati wa hifadhi ghalani. Ugonjwa huu ni hatari zaidi kwenye sehemu za joto na zenye kutuamisha maji. Ni vyema kuhakikisha kwamba shambani hakuna hali ya kutuamisha maji na pia kwenye ghala kunakuwa na hali nzuri ya mzuunguko wa hewa. Udhibiti wa wadudu Utitiri wa vitunguu (Onion thrips), Funza wa vitunguu (Onion maggots) na Minyoo wa vitunguu (Onion wireworms) ni miongoni mwa wadudu wasumbufu kwenye zao la kitunguu. 1. Utitiri wa vitunguu (Onion thrips) Hawa ni wadudu wadogodogo sana ambao hula kwa kukwaruza juu ya jani na kunyonya majimaji ya kwenye mmea. Hali husababisha kutoka kwa mikwaruzo meupe kwenye majani ya vitunguu. Mashambulizi yakizidi majani huanguka na kunyauka. Ukubwa wa vitunguu hupungua. Hili ni tatizo kubwa zaidi hasa wakati wa ukame kuliko wakati wa unyevu. Utitiri wa vitunguu Madhara ya utitiri 2. Bungua weupe (White grub) Huyu ni aina ya funza mkubwa. Hutaga mayai yake kwenye uozo wa majani na samadi na hivyo mashamba ya vitunguu yaliyoko karibu au kwenye maeneo ya jinsi hiyo huwa kwenye hatari zaidi. Hushambulia mizizi na kusababisha kukauka kwa mimea. Kutifulia shamba na kuwaweka wazi wadudu hawa kunapunguza idadi yao.

Bungua mweupe Funza wa Kitunguu 3. Minyoo ya vitunguu (Onion wireworms) Hawa ni funza ambao mayai yao hutagwa kwenye maeneo yenye magugu. Wadudu hawa huwa ni tatizo kubwa kwenye sehemu zenye kutuamisha maji. Kutifulia udongo ili upitishe maji vizuri pamoja na udhibiti wa maguu ni njia nzuri ya kuwadhibiti wadudu hawa. Uvunaji Inapowezekana mwezi mmoja kabla ya kuvuna udongo uanze kuondolewa polepole ili kuviacha wazi vitunguu kwa ajili ya ukaukaji mzuri. Zoezi hili linalenga kufanya angalau theluthi moja ya sehemu ya kitunguu kiwe hakijafunikwa na udongo kwa siku kati ya 7 hadi kumi kabla ya kuvuna ili kuharikisha ukaukaji. Vuna wakati asilimia 75 ya shingo za vitunguu zimelala. Mara nyingi vitunguu hung’olewa na kurundikwa kwenye matuta na baadaye kukusanywa na kuwekwa kwa ajili ya kukata shingo. Mizizi pia inapunguzwa na vitunguu vinajazwa kwenye magunia tayari kwa kusafirishwa nyumbani kwa ukaushaji zaidi na kisha kuwekwa galani au kuuzwa. Ukaushaji Madhumuni ya kukausha ni kuvifanya vitunguu visiweze kuota kwa muda na pia kuvifanya visiharibike. Vitunguu vilivyokauka vizuri huwa na shingo iliyonywea vizuri na ganda kavu. Kama shingo ya kitunguu haikukauka sawasawa kutatokea hali ya uozo. Soko la vitunguu Ukubwa wa vitunguu ni sifa ingaliwayo na wanunuzi. Vitunguu vidogodogo sana au vinene sana huwa havipendwi. Vitunguu vinavyopendwa ni vile vyenye wastani wa unene wa sentimita nne. Vitunguu vilivyochubuka, mapacha na vyenye shingo ya chupa huwa havipendwi. Vitunguu vilivyooza na vile vilivyobabuka na jua pia havifai. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza vitunguu kwa vipimo vya magunia na ama ndoo za plastiki. Kwa miaka kadhaa vitunguu vimekuwa vikiuzwa kati ya shilingi 20,000/= hadi 30,000/= kwa gunia. Hifadhi ya vitunguu Vitunguu vipya vilivyovunwa huwa havioti upesi. Hifadhi sahihi hurefusha muda wa kutoota. Kwenye hifadhi ni vizuri vitunguu vipate hewa yenye mzunguuko mzuri na ndiyo maana maghala ya kuhifadhia vitunguu yanajengwa kama vichanja ili kuruhusu hewa kuzunguuka hata kwa kupitia sehemu za chini. Ndani ya ghala vitunguu humwagwa na kusambazwa kama inavyonyesha kwenye picha namba.. Vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi sita au zaidi bila kuharibika. Mavuno Mavuno ya vitunguu yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Vitunguu pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya kitunguu. Kwa wastani vitunguu vinaweza kutoa mavuno kati ya tani 10 hadi 18 kwa hekta moja.

Bungua mweupe Funza wa Kitunguu

3. Minyoo ya vitunguu (Onion wireworms)

Hawa ni funza ambao mayai yao hutagwa kwenye maeneo yenye

magugu. Wadudu hawa huwa ni tatizo kubwa kwenye sehemu zenye

kutuamisha maji. Kutifulia udongo ili upitishe maji vizuri pamoja na

udhibiti wa maguu ni njia nzuri ya kuwadhibiti wadudu hawa.

Uvunaji

Inapowezekana mwezi mmoja kabla ya kuvuna udongo uanze

kuondolewa polepole ili kuviacha wazi vitunguu kwa ajili ya

ukaukaji mzuri. Zoezi hili linalenga kufanya angalau theluthi moja ya

sehemu ya kitunguu kiwe hakijafunikwa na udongo kwa siku kati ya

7 hadi kumi kabla ya kuvuna ili kuharikisha ukaukaji. Vuna wakati

asilimia 75 ya shingo za vitunguu zimelala. Mara nyingi vitunguu

hung’olewa na kurundikwa kwenye matuta na baadaye kukusanywa

na kuwekwa kwa ajili ya kukata shingo. Mizizi pia inapunguzwa na

vitunguu vinajazwa kwenye magunia tayari kwa kusafirishwa

nyumbani kwa ukaushaji zaidi na kisha kuwekwa galani au kuuzwa.

Ukaushaji

Madhumuni ya kukausha ni kuvifanya vitunguu visiweze kuota kwa

muda na pia kuvifanya visiharibike. Vitunguu vilivyokauka vizuri

huwa na shingo iliyonywea vizuri na ganda kavu. Kama shingo ya

kitunguu haikukauka sawasawa kutatokea hali ya uozo.

Soko la vitunguu

Ukubwa wa vitunguu ni sifa ingaliwayo na wanunuzi. Vitunguu

vidogodogo sana au vinene sana huwa havipendwi. Vitunguu

vinavyopendwa ni vile vyenye wastani wa unene wa sentimita nne.

Vitunguu vilivyochubuka, mapacha na vyenye shingo ya chupa huwa

havipendwi. Vitunguu vilivyooza na vile vilivyobabuka na jua pia

havifai. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza vitunguu kwa

vipimo vya magunia na ama ndoo za plastiki. Kwa miaka kadhaa

vitunguu vimekuwa vikiuzwa kati ya shilingi 20,000/= hadi 30,000/=

kwa gunia.

Hifadhi ya vitunguu

Vitunguu vipya vilivyovunwa huwa havioti upesi. Hifadhi sahihi

hurefusha muda wa kutoota. Kwenye hifadhi ni vizuri vitunguu

vipate hewa yenye mzunguuko mzuri na ndiyo maana maghala ya

kuhifadhia vitunguu yanajengwa kama vichanja ili kuruhusu hewa

kuzunguuka hata kwa kupitia sehemu za chini. Ndani ya ghala

vitunguu humwagwa na kusambazwa kama inavyonyesha kwenye

picha namba.. Vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi sita au

zaidi bila kuharibika.

Mavuno

Mavuno ya vitunguu yanategeme huduma za shamba pamoja na hali

ya hewa. Vitunguu pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina

ya kitunguu. Kwa wastani vitunguu vinaweza kutoa mavuno kati ya

tani 10 hadi 18 kwa hekta moja.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!