You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
MBINU BORA ZA UZALISHAJI MPUNGA

WA KUTEGEMEA MVUA

Utangulizi:

Mpunga ni zao maarufu sana duniani na hapa

Zanzibar. Ni la tatu kulimwa likitanguliwa na

muhogo na ndizi. Hata hivyo ni la kwanza

kupendwa kuliwa na wananchi wote wa hapa

Unguja na Pemba.

Wakulima wa visiwani hulima mpunga wa aina

mbili, wakutegemea mvua ambao hulimwa katika

msimu wa mwaka na wa umwagiliaji maji ambao

unalimwa mara mbili kutegemea na uwezo

pamoja na mbegu zinazotumika.

Katika Kilimo cha aina zote mbili hutumia mbegu

kubwa za miezi sita au mbegu ndogo za miezi

mitatu. Hata hivyo mpunga wakutegea mvua

hupitia katika hatua saba muhimu nazo ni:

1. Utayarishaji wa ardhi.

2. Uchaguzi wa mbegu, usiaji na utiaji wa mbolea

za kupandia.

3. Palizi kwa jembe, mkono au kwa dawa.

4. Udhibiti wa wadudu

5. Ukaguzi wa shamba

6. Upatikanaji wa wataalam.

7. Mavuno

Utayarishaji wa ardhi:

Matayarisho ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha

mpunga huanza kwa kufyekwa majani, na

kuwekwa pembeni kama mipaka katika shamba

kwani yanapooza hutoa mbolea nzuri kutokana

na kupelekwa na maji ya mvua shambani.

Kwa wakulima waliowengi huchoma moto majani,

mbinu hii kitaalam haikubaliki kwani ni chanzo

kikuu cha uharibifu wa mazingira kutokana na

moto kuua viumbe hai wa udongo.

Kabla ya kupanda ni vyema kuweka mbolea za

awali kama Samadi au TSP ili kupata mimea bora

na yenye afya inayokua vizuri. Hata hivyo mbolea

za asili zinapendekezwa zaidi kwani hizi ni nzuri

kwa kuhifadhi mazingira na kupunguza gharama

za ununuzi

Uchaguzi wa mbegu:

Mkulima inampasa kuwa makini katika kutafuta

mbegu zenye sifa nzuri ili ataposia ziweze kuota

na kukua vizuri. Mbegu hizo ziwe na uwezo wa

kustahamili wadudu, magonjwa, maradhi na

upepo, sambamba na mbegu bora, kusia kwa

wakati pamoja na kutumia mbolea za kupandia

ni jambo la msingi ili mpunga uchipue na ukue

vizuri.

Aina nne ya mbegu za mpunga

Palizi kwa kutumia mkono, jembe au dawa:

Wakati wa palizi utakapofika mkulima anatakiwa

asichelewe kuifanya kazi hiyo,

Kwa sababu magugu yaliyoota na mpunga mara

nyingi huhitaji virutubisho vingi zaidi ili kukua

vizuri na kuuacha mpunga kukosa virutubisho vya

kutosha kutokana na magugu ardhini. Hali hiyo

ikitokea mpunga hautakuwa vizuri.

Mpunga ukipaliliwa unakuwa vizuri

Baada ya palizi majani laini yote yanayoweza

kuoza kwa haraka yawachwe huko shambani na

yale magugu yawekwe kwenye mipaka kwani

nayo baada ya muda itakuwa mbolea ambayo

itasambazwa na maji ya mvua.

Baada ya palizi ya kwanza unatakiwa kuweka

mbolea ya pili ya kukuzia na mbolea ya tatu

huwekwa baada ya palizi ya pili au mpunga ukiwa

na mimba.

Udhibiti wa wadudu:

Mpunga huwa unashambuliwa sana na wadudu

mbalimbali ukiwa katika hatua tofauti za ukuaji,
lakini mashambulizi makubwa yanatokea mpunga

ukiwa mchanga. Wadudu wanaoshambulia sana

mpunga ni pamoja na kunguni mgunda na funza

wa kigogo. Ili kudhibiti uharibifu hou hapana budi

kutayarisha shamba

vizuri na kwa wakati

pamoja na ukaguzi

wa shamba mara

kwa mara, ni mbinu

bora ya kupunguza

maradhi na wadudu

kwa kiasi kikubwa

sambamba na

utumiaji wa dawa za

viwandani kama vile

Dawa ya unga aina

ya Marshal ambayo huchanganywa na mbegu

kabla ya kupandwa, Dawa za mafuta za Rogo,

Attakan, C344SE, na nyenginezo. Dawa hizi

hutumika zaidi mara tu mashambulizi yanapoanza

baada ya mpunga kuota/kuchipua.

Ukaguzi wa shamba:

Kwa kipindi chote hicho inashauriwa kukagua

shamba lako mara kwa mara ili kuweza kugundua

tatizo lolote mapema na kulichukulia hatua

inayofaa kwa haraka.

Upatikanaji wa Wataalam:

Wakulima ili wafanikiwe wanahitaji kupata ushauri

wa kitaalam na miongozo mbalimbali ili uzalishaji

uweze kukuwa. Ni vizuri kwa wakulima kuwa

karibu na mabwana shamba wa maeneo yao, ili

kubadilishana uzoefu na kupata taaluma zaidi.

Mavuno:

Uvunaji hufanyika mapema mpunga unapokauka

na kugeuka rangi ya kahawia kabla majani

hayajakauka kabisa. Unapochelewa kuvunwa

mpunga hukauka shambani na hupukutika na

kupungua uzito.

Baada ya kuvunwa mpunga husafishwa kwa

kupeta na huhifadhiwa kwenye mapolo na

magunia kwa matumizi ya baadae.

Kimetayarishwa na

Kamisheni ya Kilimo, Utafiti na Elimu kwaWakulima

(Kitengo cha habari na Vielelezo)

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Mazingira

S. L. P 159, ZANZIBAR

Juni, 2008

WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NA

MAZINGIRA - ZANZIBZAR

MBINU MBINU BORA BORA ZA

ZA

UZALISHAJI

UZALISHAJI

MPUNGA MPUNGA WA

KUTEGEMEA KUTEGEMEA MVU MVUA MVU