12.12.2012 Views

1` 2` UBORA NA UPANGAJI WA KOROSHO KATIKA MADARAJA ...

1` 2` UBORA NA UPANGAJI WA KOROSHO KATIKA MADARAJA ...

1` 2` UBORA NA UPANGAJI WA KOROSHO KATIKA MADARAJA ...

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

1` 2`

UBORA NA UPANGAJI WA KOROSHO

KATIKA MADARAJA

Utangulizi

Kwa kipindi kirefu ubora wa zao la korosho

umekuwa ukididimia siku hadi siku kwa

sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu hizo ni

ndani ya uwezo wa wakulima na zingine

zimesababishwa na wanunuzi chini ya mfumo

wa soko.huria ulioanza msimu 1992/93.

Kipeperushi hiki kinaelezea namna ya kulinda

na kudumisha ubora wa korosho toka

shambani hadi gulioni ili kuinua kipato cha

mkulima.

Ubora wa Korosho.

Ubora wa korosho unaanza shambani. Ili

mkulima apate korosho nying na zilizo bora ni

budi azingatie kanuni za kilimo bora cha

korosho ikiwa ni pamoja na:-

• Kuweka shamba katika hali ya usafi ili

wadudu na magonjwa yasipate nafasi

ya kujificha na kuzaliana.\

Picha ya shamba

• Kupanda mazao ya msimu kama

mtama, mahindi na jamii ya kunde

katika shamba la korosho kama sehemu

ya matumizi bora ya ardhi na

kupunguza gharama za uendeshaji.

• Kutumia njia za asili ama madawa ili

kudhibiti Magonjwa yanayoathiri

ubora na uwingi wa korosho.

3`

• Kuokota korosho zilizoanguka

zenyewe na sio kuzitikisa pamoja na

kutoa kikonyo chake chote.

• Hakikisha kuwa nyama ya bibo

inayobakia kwenye korosho imetolewa

na kifaa kikali kuzuia uharibifu dhidi

ya maonjwa na wadudu.

• Kuanika korosho juani katika sehemu

iliyosafi na kavu kwa muda wa siku

mbili hadi tatu ili kuhakikisha kwamba

zimekauka inavyotakiwa. Korosho

zilizokauka vizuri hutoa mlio wa sauti

kali ukiziangusha chini.

• Sehemu ya kuanikia korosho sharti iwe

safi ili korosho zisipate uchafu.

• Kuzipanga korosho kimadaraja na

kuzihifadhi ndani ya magunia

kimadaraja.

• Kuhifadhi magunia ya korosho juu ya

chaga kwenye chumba kikavu na sio

sakafuni.

• Magunia ya mkonge au jute huruhusu

hewa kupita kwa urahisi wakati wa

kuhifadhi korosho.

• Kagua ghala lako ili kubaini kuwepo

kwa wadudu waharibifu kama mchwa.

KUPANGA MADARAJA YA KOROSHO.

Korosho zipangwe kwenye madaraja mawili.

Kwa kuzingatia sifa zifuatazo:-

Daraja la Kwanza (Standard Grade- SG)

• Korosho za daraja la kwanza zitakuwa

na sifa zifuatazo.

• Zitatoa mlio wa sauti kali ukiziangusha

chini.

• Zina rangi ya kijivu au kikahawia

kilichofifia.

• Hazina makunyanzi.

• Hazina madoadoa kwenye ganda la nje.

• Zina umbile safi.

• Zimekomaa vizuri, unyevu asilimia 12.

Picha ya korosho SG

Daraja la Pili (Under Grade – UG)

• Zimekomaa.

• Zimekauka unyevu asilimia 12, lakini

ganda lake la nje lina madoa doa.

• Zina makunyanzi.

Korosho za daraja la kwanza na la pili zote ni

budi ziwe na sifa za msingi za kukauka vizuri

na ujazo wa kutosha ndani karanga)

Picha ya korosho UG

Korosho zisizotakiwa.

• Hazikukomaa vizuri.

• Hazikauka au mbichi.

• Zimeota.

• Zina makunyazi.

Hazina rangi ya kijivu au kikahawia

kilichofifia.

Picha ya korosho Chafu

UTAFITI NA MAENDELEO

KANDA YA KUSINI

UBORA NA UPANGAJI WA

KOROSHO KATIKA MADARAJA

Imetolewa na

KITUO CHA UTAFITI,

NALIENDELE,

S. L. P. 509,

MTWARA

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!