13.07.2015 Views

Jarida la Kilimo, Aprili

Jarida la Kilimo, Aprili

Jarida la Kilimo, Aprili

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Aprili - Juni, 2011Na Neema A. KhalfanMnazi una matumizi mengihapa visiwani na duniani kote,matumizi hayo ni kama madafu kwakinywaji, nazi kwa ajili ya kupata tui lakupikia na mbata kwa ajili mafuta yanazi, makumbi kwa ajili usumba nakamba, makuti hutengenezewa fagio,mapakacha na kuezekea majumba,kigogo cha mnazi pia hutumika kwambao, kuni na nguzo za kujengea napia una matumizi mengine mengi.MINAZI YA ASILITUHAMASISHANE KUPANDA MINAZI YA ASILIMnamo miaka ya 1970 zao la nazililikuwa na upungufu mkubwa ambapokila mnazi ulitoa wastani wa nazi 23tu kwa mwaka badala ya uzazi wakawaida wa nazi 40 kwa mwaka. Uzazihuo ni chini ya wastani wa kiwango chauzalishaji wa kawaida wa nazi 40 kwamwaka ambayo ilisababisha upungufumkubwa wa nazi kwa matumizi yamajumbani na viwandani.Utafi ti uliofanyika uligundua sababuza upungufu wa zao hilo ni kuzeekakwa minazi ya asili ambapo asilimia70 ya minazi ilikua ina umri zaidi yamiaka 100 na haikua na uzazi wenyetija, kuwepo kwa wadudu waharibifu,ukosefu wa mafunzo ya kilimo boracha minazi na uhaba wa ardhi kwa ajiliya utanuzi wa mashamba ya minazi.Kutokana na upungufu huo mnamomwaka 1979/1980 Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania ilianzishaMpango wa Taifa wa UendelezajiMinazi (NCDP).Wizara ya Kilimo Zanzibar nayo iliandaamikakati ya uhamasishaji wa upandajiminazi kwa kutoa mafunzo kwawakulima juu ya uchaguzi wa mbegubora, uoteshaji wa miche vitaluni,upimaji, ukaguzi wa mashambapamoja na usambazaji wa miche.Mpango huo ulifanikiwa kwa kufanyakampeni katika Wilaya za Magharibi,Kaskazini A, Kaskazini B, Kati naKusini kwa Unguja sambamba nakuwapa wakulima ushauri, mafunzoya kupanda miche chini ya minazimikongwe na kuwashauri kutumiavipimo vinavyotakiwa (mita 10 kwa15) kutoka mnazi hadi mnazi bila yakujali msongomano uliopo shambanimpando huu ulisaidia uendelezajiwa upatikanaji wa mavuno hukuikisubiriwa miche iendelee na ukuajiwake.Minazi iliyopandwa katika masafa yaliyopendekezwa na wataalamu hurahisishapalizi, kutoa mavuno bora na kumpa fursa mkulima kuchanganya na mazao mengineJumla ya wakulima 250 walihudhuriakatika kampeni hiyo na wakulima 102walikaguliwa mashamba yao ambapomashamba 47 yalikaguliwa, 22 kipindicha Vuli na 25 Masika, wakulima20 walipimiwa mashamba yao nakupatiwa miche.Katika kipindi cha Vuli 2010 na Masika2011 Wizara ya Kilimo na Maliasilikupitia vitengo vyake vya uzalishaji wamiche ya minazi imefanikiwa kuzalishana kuiuza kwa wakulima miche yaminazi ya asili 10,260.Upunguzaji wa Minazi MikongweWizara iliendelea na juhudi zakuwashajiisha wakulima kupunguzaminazi mikongwe katika mashambayao kwa kupanda minazi mipya chiniya minazi hiyo na baada ya miakamitatu ya ukuaji, walishauriwa kukataminazi mikongwe na kuondoa magogokwa lengo la kuzuia mazalia ya chonga.Aidha, wakulima walisisitizwa kuondoamagogo yote yaliyomo shambani nakuyatumia kwa kuchoma chokaa,kupasua mbao, kujengea daraja ndogondogo za kuvukia, vibao vya kukalia nakuni.Uchaguzi wa micheInashauriwa kuchagua miche iliyoborakwa ajili ya upandaji. Miche borahuwa na sifa ya kukua haraka nakutoa mazao bora. Miche bora ni ileambayo haikushambuliwa na wadudu14au magonjwa, yenye afya na majaniyake yasipungue sita (6) na yawe kijaniiliyokooza na imekaa kitaluni kwamuda usiopungua miezi tisa (9).Uchimbaji wa mashimoInashauriwa kuchimba mashimoyenye urefu, upana na kina chasentimita 60 (futi mbili), udongo wachini utenganishwe na wa juu ambaomara nyingi huwa na rutuba, baadaeuchanganywe na mbolea za kienyejikama vile samadi na mboji debe mojaau ndoo moja. mbolea hizi hupatikanakwa urahisi katika maeneo yetu.Upandaji wa micheWeka udongo wa juu uliochanganywana mbolea kiasi katika shimo, pandamche katikati ya shimo, endeleakufukia kwa udongo uliochanganywana mbolea na kumalizia na udogo wachini. Hakikisha unalishindilia vizurishimo lako ili kuzuia mche kung’okakwa urahisi.Zao la nazi ni muhimu hapa Zanzibar,hivyo Wizara ya Kilimo na Maliasiliinaendelea kuielimisha na kuishajiishajamii kupanda minazi ya asili ili zao hililiwe endelevu kwa faida ya wananchina Taifa kwa ujumla.Kwa maelezo zaidi ya uchaguzi wamiche ya minazi na upandaji wasilianana mhudumu wa kitalu, muone bwana/bibishamba wako au mtaalamu wakitengo cha minazi uliye karibu nae.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!