Aprili - Juni, 2011MISITU YA UKANDA WA PWANINa Rashid KhamisUzinduzi wa mradi wa Uhifadhi waMisitu ya Asili ya Ukanda wa Pwaniuliofanyika Bwawani Hoteli hapa Zanzibartarehe 30/05/2011 ambapo Shirika laUhifadhi wa Mazingira Duniani la GEF,kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa laMpango wa Maendeleo Duniani la UNDPlinasaidia uhifadhi wa Mazingira ya Misituya Asili ya Tanzania bara na Zanzibar.Hapa Zanzibar ipo misitu mitatu yahifadhi itakayofaidika na mradi huuambayo ni Jozani, Kiwengwa – Pongwe naMasingini kwa Unguja na msitu wa NgeziVumawimbi, Ras Kiuyu na Msitu Mkuukwa Pemba. Wizara ya Kilimo na Maliasiliinachukua juhudi za kunusuru kupoteakwa misitu ya asili ambayo imeshehenimiti ya asili na wanyamapori kutokanana maeneo ambayo yalikua yameshehenimisitu ya asili sasa yamebakia na vichakavitupu. Mfano halisi ni kuadimika kwamiti muhimu katika maeneo ya misituya kaskazini Unguja, ambapo hasara yakutokuwa na misitu imeonekana kutokanana kupungua kwa nishati ya kuni zakupikia majumbani.Misitu ni benki ya kuhifadhi miti na mimeatofauti yenye uhusiano wa moja kwa mojana maisha ya binaadamu, ustawi wamazingira tunayoishi na maendeleo yakiuchumi. Aidha, miti ya dawa, miti adimuaina ya mipapindi na wanyamapori kamavile Popo wa Pemba, Kimapunju na Paanunga huishi katika misitu ya asili nao nimuhimu kwa maisha yetu ambapo bilaya misitu maisha ya viumbe hawa huwamashakani.Misitu ya asili pia ni muhimu kwakinga dhidi ya majanga ya upepo mkalina urekebishaji wa hali ya hewa naupatikanaji wa mvua. Vile vile inachangiamaendeleo ya utalii, kutoa ajira kwawanavijiji wanaozunguka misitu ya hifadhi,kupatikana kwa vyanzo vya maji ambavyoni rasilimali kubwa kwa maisha yamwanadamu kwa matumizi ya majumbanina mahoteli (maji ni uhai). Misitu husaidiakujenga afya kwa uzalishaji wa matundamfano, mabungo na zambarau.Nje ya maeneo ya misitu ya hifadhi, ipomisitu iliyozunguka maeneo ya vijijiniambayo ni muhimu kwa kuhifadhiwa.Juhudi za uhifadhi ni vyema zihusishepande zote mbili, misitu iliyo chini yausimamizi wa taasisi za Kiserikali na iliyochini ya wanajamii.Kutokana na harakati za maendeleoya mwanadamu, baadhi ya maeneo yamisitu ya asili yameanza kupoteza uasiliwake kutokana na athari za kukatwa ovyokwa matumizi ya nishati ya kuni, makaa,kilimo, chokaa, majumba ya kuishi navitega uchumi.Daraja la mikoko la Jozani-Pete ni miongoni mwa kivutio cha watalii katikauhifadhi wa msitu wa ukanda wa pwani.Hivyo, kutokana na kutoweka kwa misituambayo ni muhimu katika maisha yaviumbe, Serikali kupitia Wizara ya Kilimona Maliasili kwa kushirikiana na washirikahao imezindua mradi huo kwa lengo lakuhifadhi misitu pamoja na rasilimaliziliomo kwa faida ya wanajamii na taifakwa jumla.Miongoni mwa changamotozinazosababisha uharibifu wa misitu nipamoja na kuendelea kupungua kiwangocha maji ardhini ambacho kimepelekeakupungua kwa maji katika visima,mito na kukauka kwa vyanzo vyengine.Kuongezeka kwa kiwango cha joto nakurundikana kwa hewa mkaa. Athari zachangamoto hizo husababisha ardhikukosa rutuba ya kustawisha mazao yakilimo kunakopelekea uzalishaji mdogo,ukame na njaa kwa binadamu, kufa kwamifugo, kupotea kwa wanyamapori nakutokea kwa mafuriko wakati wa mvua.i. Hatua za kuchukua ili kuimarishauhifadhi wa misitu na kuwa endelevuni:ii. Kutenga maeneo zaidi ya uhifadhi wamisitu ya asili na kuimarisha iliyopo,iii. Kuendeleza taaluma ya uhifadhi wamisitu kwa jamii,vi. Kufanya ukaguzi wa misitu na kuchukuahatua za kisheria kwa wanaoharibumisitu.v. Kushirikisha jamii katika uhifadhi kwakuwasaidia kuanzisha na kuendelezavitalu vya miti na kupanda miti mingimjini na vijijini.12vi. Kuacha kuwinda wanyama kiholelapamoja na,vii. Kuanzisha sheria ndogo ndogo.Jamii inashauriwa ipunguze kiwangokikubwa cha kuvuna misitu ya asili kwamatumizi ya nishati ya kupikia majumbani,mahotelini na katika mabekari nauchomaji wa chokaa na makaa. Aidha,wanajamii wanatakiwa waendeleze juhudiza kupanda miti ya misitu na matunda nawaachane na tabia ya kukata misitu yaasili ovyo, kwani tabia hiyo inasababishakutoweka miti mikubwa ambayo nimuhimu kwa uzalishaji wa mbegu.Ushirikishwaji wa wanavijiji katikakufanikisha utekelezaji wa mradi huuunahitajika ili waweze kutoa michangoyao katika kupanga na kutekeleza kaziza mradi kupitia kamati zao za uhifadhimisitu. Mradi unapaswa uwashirikisheuongozi wa Wilaya husika katikautekelezaji wake na kuwapatia taaluma yakupanga na kusimamia uhifadhi wa misitukatika ngazi za Shehia hadi Wilaya.Vile vile Taasisi za kiserikali chini yaWizara husika ziunganishe nguvu zaopamoja kupiga vita uharibifu wa misitu nakuhimiza upandaji miti na kuitunza iliyopoiweze kuimarika. Miongoni mwa taasisihizo ni zinazohusika na Maji, Mazingira,Ardhi na Utalii kushirikiana katika kupangautekelezaji wa mradi huu.Katika kuendeleza mradi huu ushirikianowa pamoja unahitajika baina ya Wizaraya Kilimo na Maliasili Zanzibar na Wizaraya Maliasili na Utalii ya Tanzania barakupitia Idara ya Misitu na Nyuki, Tanzaniaunahitajika ili kufanikisha mpango wautekelezaji wake.
UFUGAJI WA KUKU Aprili - Juni, 2011UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJINa Shauri HajiUfugaji wa kuku ni mradi ambaohufanywa na wanawake wengikaribu katika kila nyumba hasavijijini kwa lengo la kupata nyamana mayai kwa ajili ya kitoweleo,kuimarisha afya za familia nakujiongezea kipato. Kuku nilazima watunzwe vizuri ili watoemazao bora na kufi kia lengolililokusudiwa.Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni mojaya kazi zinazofanywa na kinamamaambao wameunda vikundi nakupatiwa taaluma za ufugaji borakupitia Programu za KuendelezaHuduma za Kilimo na Mifugo kwawakulima na wafugaji (ASSP/ASDP-L) ya Wizara ya Kilimo na Maliasilihapa Zanzibar. Taaluma hizi zaufugaji zinawasadia wafugaji wavisiwa hivi ambao wengi wao niwanawake kuongeza uzalishaji,pato na kupunguza umasikini.Bi. Zeyana Ali Saidi mwenye umri wamiaka 50 ambae ni mkaazi wa kijijicha Taifu Wilaya ya Wete Pemba,maarufu kwa jina la “Zeyana viponi”ni miongoni mwa wafugaji wa kukuwaliopatiwa mafunzo ya ufugajikupitia programu za ASSP/ASDP-L.Alisema; “Siku za nyuma ufugaji wakuku haukuwa na tija kutokana nakukosa taaluma ya ufugaji bora napia ulihitaji kutumia muda mwingiili kupata mafanikio”.Kuku wa kienyeji hukuwa vizuri na kutoa mazao mengi ikiwa watapatiwamatunzo boraMoja kati ya mambo anayojivunia nikutengeneza nyumba yake pamojana kuwasomesha watoto wakekutokana na mauzo ya kuku. Hivikaribuni aliuza kuku 80 ambao walimpatiajumla ya shilingi 400,000/=. Watu wengi wanafuga kukulakini hawaelewi kanuni na miikoya ufugaji hivyo bi. Zeyana Ali Saidiyuko mstari wa mbele katika kuwafundishawafugaji wenzake kulishachakula bora, kuweka usafi wamabanda ya kufugia kuku na vifaa,kuwapatia chanjo na matibabu vifarangana kuku ili kuzuia magonjwaya mripuko kama mahepe ambayoyanaua kuku wengi yanapotokea.Aidha, anasisitiza kuwa mfugajianapaswa kufanya usafi wa bandakila baada ya siku mbili kwani usafihupunguza uwezekano wa kutokeakwa maradhi.Mbali na uuzaji wa kuku bi. Zeyanapia ana mpango wa kuuza vifarangakwa wafugaji wenzake ili kuimarishasoko la kuku wake. Hii itawezekanakwa kutumia mpango maalumuwa utagaji (Program hatching).Njia hii inamfanya kuku mmojakutaga mara nne kwa mwaka nakuzalisha zaidi ya vifaranga 48ambapo mfugaji anapata faidazaidi badala ya njia ya kawaida yauzalishaji vifaranga 20 - 24 kwaufugaji usiozingatia utaalamu.13Vifaranga vinavyototolewa kwampango maalumu wa utagajihuingizwa kwenye sanduku lenyeuwezo wa kuchukua vifaranga 200au zaidi na kulelewa kwa muda wasiku saba ambapo hutoa fursa kwamakoo waliototoa kukutana tenana majogoo baada ya muda mfupi.Njia nyengine ni kutumia koolinalokubali kulea vifaranga hatakama sio wa kwake mradi tu wawena umri unaolingana.Miongoni mwa changamotoanazokabiliana nazo ni pamoja nabei kubwa ya madawa na vyakula.Ili kukabiliana na changanamotoya upatikanaji wa chakula, wfugajiwanashauriwa kutumia vyakulavinavyopatikana katika mazingirayao na kuchanganya wenyewemajumbani kwao kwa kutumiataaluma waliyapta katika mafunzo.