13.07.2015 Views

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINIMHESHIMIWA DKT. IBRAHIM MSABAHA (MB.),AKIWASILISHA KATIKA BUNGE MAKADIRIOYA MATUMIZI YA FEDHA ZA WIZARA YANISHATI NA MADINI KWAMWAKA 2006/2007i

ORODHA YA VIFUPISHOASAGBCDANIDAERTGSTGEFGTZIPTLIPPSIMFIAEAKIDTKVKfWKCPCMCIMSMWAlex Stewart Asseyers Government BusinessCorporation.Danish International Development AgencyEnergizing Rural TransformationGeological Survey of TanzaniaGlobal Environment FacilityGermany Tanzania technical cooperationIndependent Power Tanzania LimitedInternational Programme of Physical SciencesInternational Monetary FundInternational Atomic Energy AgencyKilimanjaro Industrial Development Trust FundKilovoltKreditanstalt fur WiederaufbauKiwira Coal and Power CompanyMining Cadastre Information Management SystemMegawattMKUKUTA Mkakati wa Kupunguza Umasikini na KukuzaUchumiNDFNORADOPRASProBECPSANordic Development FundNorwegian Agency for DevelopmentOpen Performance and Appraisal SystemProgramme for Biomass Energy ConservationProduction Sharing Agreementii

REAREFSADCSidaRural Energy AgencyRural Energy FundSouthern African Development CommunitySwedish International Development AgencyTANESCO Tanzania Electric Supply CompanyTPDCTanzania Petroleum Development CorporationTANSORT Tanzania Government Diamond Sorting OrganizationTPCUNDPUNIDOUNESCOUSAIDUKIMWITanzania Planting CompanyUnited Nations Development ProgrammeUnited Nations Industrial Development OrganisationUnited Nations Education and Science CommissionUnited States AidUpungufu wa Kinga Mwiliniiii

HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHESHIMIWADKT. IBRAHIM MSABAHA (MB.), AKIWASILISHA KATIKABUNGE MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA ZA WIZARA YANISHATI NA MADINI KWA MWAKA 2006/20071. Mheshimiwa Spika, baada ya kuzingatia taarifailiyowasilishwa mbele ya Bunge lako tukufu na Mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara,naomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako tukufu lijadili nakuidhinisha makadirio ya matumizi ya fedha za Wizara yaNishati na Madini kwa mwaka 2006/07.A: UTANGULIZI2. Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naombakumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivi karibunikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).Ninamshukuru kwa kuniteua kuiongoza Wizara hii na hivyokuweza kutoa hotuba yangu ya kwanza ya bajeti kwenye Bungehili tukufu. Napenda pia kutumia fursa hii kumpongezaMakamu wa Rais Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuwaMakamu wa Ris kwa mara nyingine na kumpongeza WaziriMkuu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kwa kuteuliwa kwakekushika wadhifa huo.3. Mheshimiwa Spika, pia nitumie fursa hii kuwapongezarasmi wewe na Naibu Spika kwa kuchaguliwa kwenu kuwaSpika na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania.4. Mheshimiwa Spika, nawapongeza WaheshimiwaWabunge wenzangu wote kwa kupata fursa. ya kuingia katikaBunge hili Ia Awamu ya Nne. Ninawaahidi WaheshimiwaWahunge ushirikiano wa bali va juu katika kutimiza majukumuvetu ya kitaifa.5. Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba kuchukua fursahii kuwashukuru sana wananchi wa Kibaha Vijijini kwakunichagua kwa kura nyingi kuwa Mbunge wao. Nawaahidikuwatumikia kwa uadilifu, kwa ari mpya, nguvu mpya na kasimpya.1

B: MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NABAJETI YA MWAKA 2005/06Mpango wa Utekelezaji6. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mpango na Bajetikwa mwaka 2005/06 ulizingatia Ilani ya Uchaguzi Mkuu yaChama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2000, Mpango waUtekelezaji wa Ilani hiyo, Mpango wa Kimkakati wa Wizara naProgramu ya Kazi ya Wizara. Kazi zilizopangwa kufanyikazilikuwa ni: kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini;kuanzisha Wakala na Mfuko wa Nishati Vijijini (REA na REFsawia); kusimamia, kufuatilia na kukagua utekelezaji wa miradiya maendeleo; kutangaza ndani na nje ya nchi fursa zilizopo zauwekezaji katika sekta za nishati na madini; kuimarishaukusanyaji wa mapato kutokana na sekta za nishati na madini;kuendeleza utafiti katika sekta za nishati na madini; kuboreshamazingira ya kuwasaidia wachimbaji wadogo ili kuongeza tija nauzalishaji; kuimarisha uwezo wa Wizara kutekeleza majukumuyake kwa kuwapatia watumishi mafunzo ya kazi na kujikinga naUKIMWI; kuajiri watumishi wapya; na kuboresha mazingira yakufanyia kazi kwa kujenga na kununua majengo ya ofisi navitendea kazi.Utekelezaji wa Mpango7. Mheshimiwa Spika, mafanikio yaliyopatikana katikautekelezaji wa mpango wa mwaka 2005/06 ni kuimarishwa kwauwezo wa utendaji kazi wa watumishi ambapo watumishi 55walipelekwa mafunzoni, kati yao 27 walishiriki katika mafunzoya muda mfupi na 28 katika mafunzo ya muda mrefu. Mchakatowa kupata Bodi ya Wakurugenzi wa REA na REF na MtendajiMkuu wa Wakala, ulianza. Ukarabati wa jengo la makao makuuya Wizara katika Mtaa wa Samora na ununuzi wa jengo la ofisiya madini Songea, ulifanyika. Aidha, warsha na semina kuhusunjia za kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWIzilifanyika kwa watumishi wa Wizara, wachimbaji wadogo nawadau wengine katika maeneo ya Mahenge, Masasi, Geita naSongea. Kazi ya ukaguzi wa migodi, kusimamia matumizi yabaruti, hifadhi ya mazingira na kuzingatiwa kwa sheria nakanuni za uchimbaji na biashara ya madini ilifanyika katikamaeneo mbalimbali nchini yakiwemo maeneo ya Merelani, Geita,Shinyanga, Kilindi, Handeni, Kigoma, Musoma naMbeya.Vilevile, katika kuimarisha uwezo wa utendaji kazi wawatumishi, mafunzo ya Upimaji wa Wazi wa Utendaji Kazi2

(OPRAS) yalifanyika kwa baadhi ya watumishi wa Wizara kwenyevituo vya Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro na Mbeya.8. Mheshimiwa Spika, mahitaji ya juu kwenye gridi yaTaifa ni Megawati (MW) 562, lakini kutokana na ukameulioikabili nchi yetu katika miaka mitatu mfululizo, uwezo wauzalishaji umeme unaotokana na maji katika mitambo ya Mtera,Kidatu, Nyumba ya Mungu, Pangani, Hale, na Kihansi, ulishuka.Uzaliahaji umeme katika mitambo hiyo ulikuwa na upungufu wawastani wa MW 120. Hali hii iliifanya TANESCO kutegemea zaidiumeme unaozalishwa na vituo vya IPTL na Songas. Upungufuhuo ulisababisha umeme utolewe kwa mgao nchini kote kuanziatarehe 5 Februari hadi tarehe 28 Machi, 2006 na kuanzia tarehe8 Juni, 2006 hadi sasa. Katika mgao unaoendelea, biashara naviwanda vikubwa vimelindwa ili visiathirike katika uzalishaji.9. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza miradi yakupeleka umeme vijijini, miji mikuu ya wilaya za Urambo,Serengeti na Ukerewe ilipata umeme kati ya Septemba naDesemba, 2005. Katika kuendeleza utafutaji mafuta, mikatabamitatu ya kugawana mapato (Production. Sharing Agreements -PSA) katika kina kirefu cha bahari Block 2, 6 na Block ya Tanga,ilisainiwa. Aidha, shughuli za utafutaji mafuta na gesi zilifanyikakatika maeneo ya Nyuni, Songo Songo Mashariki, Mandawa,Kisangire, Bigwa, Rufiji, Mafia, eneo jipya la Songo Songo naeneo la utafiti katika kina kirefu cha bahari, Block 1 na 5.10. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2005/06, kazizilizopewa kipaumbele kwenye eneo la nishati mbadala nikuendeleza na kuhamasisha matumizi ya majiko sanifu ya mkaana kuni, mabaki ya mimea, na vitofali vya makaa ya mawe(briquettes). Wizara iliendelea kukusanya taarifa za maporomokomadogo ya maji nchini kwa mikoa ya Ruvuma, Rukwa na Iringa.Taarifa za kasi ya upepo zilichukuliwa katika vituo vipya vyaMgagao (Mwanga), Makambako (Njombe) na Kitimo (Singida).Aidha, Serikali ilisimamia utekelezaji wa miradi ya umemenurukwa nia ya kuondoa vikwazo vya ukuaji wa soko la vifaavitumiavyo mionzi ya jua.11. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kujadiliana naKilimanjaro Industrial Development Trust (KIDT) ya Moshi juuya utafiti wa kuzalisha briquettes kwa kutumia vyanzo vinginevya tungamotaka kwa ajili ya kupikia. Kuhusu vitofali vyamakaa ya mawe, Serikali iliwezesha majadiliano kati ya KiwiraCoal Mines Limited na wadau kutoka Japan. Aidha, Wizara3

iliendelea kushirikiana na Kampuni ya Katani Ltd, pamoja naUNIDO na Common Fund for Commodity katika kutayarishamradi wa bayogesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kutokana namabaki ya mkonge. Sampuli za maji zilizokusanywa AmboniTanga na kwenye maziwa ya Manyara na Natron zilipelekwamaabara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni sehemu yautafiti wa jotoardhi. Matokeo ya uchunguzi yanasubiriwa.12. Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kusimamia nakuratibu programu ya tungamotaka (Programme for BiomassEnergy Conservation - ProBEC), inayotekelezwa na Shirika laKiufundi la Ujerumani GTZ. Mpango huu unatekelezwa nabaadhi ya nchi za SADC ikiwemo Tanzania kwa nia yakuhakikisha matumizi bora ya tungamotaka. Mradi huu umetoamafunzo katika mikoa ya Ruvuma na Mwanza ambapo mafundi20 wa kutengeneza majiko walifundishwa na vituo viwili vyenyeuwezo wa kuzalisha majiko sanifu 300 kwa mwezi, vilianzishwa.13. Mheshimiwa Spika, Wakala wa Serikali wa GeologicalSurvey of Tanzania (GST), ulikusanya takwimu za kijiolojia,kikemia na kijiofizikia kwenye maeneo ya wilaya za Kahama naBiharamulo. Aidha utayarishaji wa ramani za kijioiojia katikamaeneo ya Mpanda na Chunya, ulifanyika.14. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2005/06 katika Chuocha Madini, wanafunzi 15 walihitimu mafunzo ya miaka mitatu(3) ya cheti cha ufundi sanifu, wanafunzi 20 walikuwa katikamafunzo ya mwaka wa pili na wanafunzi 40 katika mafunzo yamwaka wa kwanza. Chuo kinafanyiwa ithibati (accreditation) naBaraza la Vyuo vya Kiufundi Nchini.15. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikioyaliyopatikana katika kipindi cha utekelezaji cha mwaka2005/06, sekta ya nishati ilikumbwa na vikwazo mbalimbaliikiwa ni pamoja na: ukosefu wa maji katika mabwawa yakuzalisha umeme; bei kubwa ya mafuta; na ukosefu wa fedhakwa ajili ya miradi ya maendeleo.C: MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2006/0716. Mheshimiwa Spika, Mpango na Bajeti kwa mwaka2006/07 imeandaliwa kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi Mkuuya CCM ya mwaka 2005; MKUKUTA; Mwongozo wa Utayarishajiwa Mpango na Bajeti wa mwaka 2006/07 - 2008/09; Sera zaJumla za Uchumi na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2006/07 -2008/09; Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa4

Tanzania aliyoyatoa alipoitembelea Wizara mwezi Januari, 2006;na Mpango wa Kimkakati wa Wizara.SEKTA YA NISHATIUkuaji wa Sekta ya Nishati17. Mheshimiwa Spika, mwaka 2005 mchango wa sekta yanishati ya umeme kwenye Pato la Taifa ulikuwa asilimia 1.4sawa na mwaka 2004. Ukuaji wa sekta ya nishati ya umemeulikuwa asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 4.5 mwaka 2004.Umeme uliozalishwa kwa mwaka 2005 ulifikia Gigawatt hours3,620.5 ikilinganishwa na Gigawatt hours 2,126.4 zilizozalishwamwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 58.7. Ongezeko hilolilitokana na kuanza kutumika kwa mitambo miwili ya SongasUbungo yenye jumla ya MW 75.Malengo ya Sekta ya Nishati18. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2006/07maengo ya sekta ya nishati ni pamoja na: kuimarisha nakuendeleza mfumo wa umeme nchini unaojumuisha uzalishaji,usafirishaji na usambazaji; kuratibu utekelezaji wa mpango wadharura, na mpango wa muda wa kati na mrefu wa kupunguzautegemezi wa umemeunaozalishwa kutokana na maji kwakutumia vyanzo vingine vya nishati vinavyopatikana nchinikama vile gesi na makaa ya mawe; kusimamia shughuli zautafutaji wa mafuta na gesi; kuratibu na kusimamia maendeleoya nishati mbadala; na kuhamasisha uwekezaji katika sekta yanishati.Kazi zilizopangwa kutekelezwa19. Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kutekelezwakatika mwaka 2006/07 ni: kupeleka umeme vijijini; kuendelezamiradi ya vyanzo mbadala katika uzalishaji umeme; kuboreshana kuipanua gridi ya Taifa ya umeme; kuboresha na kupanuamfumo wa usambazaji wa umeme; kupanua vyanzo vyaukusanyaji wa maduhuli kutoka katika sekta ya nishati;kuratibu utekelezaji wa miradi ya nishati; kuendeleza utafutajimafuta nchini; kuiwezesha TPDC kushiriki katika miradi yaSongo Songo na Mnazi Bay; kuitangaza sekta ya nishati nakushiriki katika majadiliario na wawekezaji.5

Ongezeko la Uzalishaji Umeme Usiotegemea Maji20. Mheshimiwa Spika, kutokana na ukame wa mudamrefu uliosababisha upungufu wa maji katika mabwawa yenyemitambo ya kuzalisha umeme, Serikali imechukua hatua zamuda mfupi na wa kati kukabiliana na tatizo hilo. Hatua zamuda mfupi zilizochukuliwa ni pamoja na kununia mitambo yaMW 100 itakayofungwa Ubungo na mingine ya MW 45itakayofungwa eneo la Tegeta. Mtambo wa Tegeta utatumiafedha za Serikali na msaada kutoka Serikali ya Uholanzi. Aidha,Serikali itakodi mitambo ya MW 100 na kuifunga Ubungo.Mitambo hii yote itazalisha umeme kwa kutumia gesi asilia yaSongo Songo na inatarajiwa kuanza kuzalisha umeme kati yamwezi Novemba, 2006 na Julai, 2007.21. Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha majadilianona Kampuni ya Kiwira Coal and Power Limited (KCP) iii kupanuauwezo wa kuzalisha umeme wa Kituo cha Kiwira kwa MW 200kwa kutumia makaa ya mawe yaliyopo Kiwira na Kabulo.Mkataba wa makusudio wa kuweka misingi ya uendelezaji wamradi huo (Agreement of Intent) kati ya Serikali, TANESCO naKCP ulisainiwa mwezi Machi, 2006. Mchakato wa kupata ridhaaya Serikali kwa ajili ya ujenzi wa mradi umeanza.22. Mheshimiwa Spika, mpango wa muda wa kati wakuongeza uzalishaji umeme katika gridi ya Taifa ni kufungamitambo ya gesi ya kati ya MW 200 hadi 300 eneo la Kinyereziifikapo mwaka 2010, pamoja na kutekeleza mradi wa Ruhudjiwenye uwezo wa kuzalisha MW 358 kwa kutumia nguvu ya majiifikapo mwaka 2012.Mradi wa Uunganishaji wa Gridi za Zambia – Tanzania- Kenya23. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Uunganishaji wa gridiza taifa za umeme za Zambia,Tanzania na Kenya umefikia hatuaya uendelezaji. Katika kikao cha Mawaziri wa nishatikilichofanyika Mei, 2006 Mombasa, Kenya, ratiba ya uendelezajiwa mradi iliidhinishwa. Aidha, mshauri mwelekezi atakamilishamchakato wa kutafuta fedha ifikapo mwezi Mei, 2007Uboreshaji wa Gridi ya Taifa ya Umeme24. Mheshimiwa Spika, vituo vingi vya uzalishaji umemekutokana na maji viko katika mikoa iliyo Kusini Magharibi yanchi. Ongezeko la uzalishaji wa umeme linatakiwa kwendapamoja na kuimarishwa kwa gridi ya Taifa ya umeme na6

kupanuliwa kwa gridi hiyo ili iifikie mikoa yote ya Tanzania.Mpango na Bajeti kwa mwaka 2006/07 umetenga fedha kwa ajiliya kuimarisha na kupanua mfumo wa gridi ya umeme nchini.Gridi ya kV 220 kutoka Iringa hadi Singida kupitia Dodomaitaimarishwa. Hatua za utekelezaji wa miradi ya upanuzi wagridi ya kV 220 kutoka Bulyanhulu kwenda Geita na kutokaShinyanga hadi Buzwagi na ya kV 132 kutoka Musoma hadiTarime, zitaanza. Aidha, hatua za awali za ujenzi wa gridi yamsongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi Kigoma na kutokaMakambako hadi Songea zitaanza katika mwaka 2006/07.25. Mheshimiwa Spika, mifumo ya usambazaji umemekatika miji ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam itaboreshwa ilikuimarisha upatikanaji na ubora wa umeme katika miji hiyo nakuondoa upotevu wa umeme (ulioongezeka kutoka asilimia 23mwaka 2004 hadi asilimia 27 mwaka 2005), matatizo ya umemekukatikakatika, na umeme hafifu.26. Mheshimiwa Spika, programu ya kuwezesha nakuongeza upatikanaji wa umeme vijijini (Energizing RuralTransformation - ERT) itaanza kutekelezwa. Miradi iliyofanyiwaupembuzi yakinifu ni ya Mtwara, Lindi, Njombe, Mufindi,Morogoro, Kilimanjaro, Manyara, na Kisiwa cha Mafia. Aidha,msisitizo katika programu hii unalenga kueneza matumizi yaumemenuru kwenye makazi yaliyo mbali na mtandao wa gridi yaTaifa, mashule na kwenye zahanati. Aidha, upeo wa programuutapanuliwa ili kujumuisha maeneo mengi zaidi.Mradi wa Gesi Asilia ya Songo Songo27. Mheshirniwa Spika, chini ya mradi wa Songo Songo,kituo cha MW 6 kinajengwa eneo la Somanga Funga, wilayaniKilwa kwa lengo kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kwaajili ya miji ya Kilwa Masoko, Utete, Ikwiriri na Kibiti. Pia, vijijikadhaa vilivyoko katika eneo la mradi vitapatiwa umeme namaji. Kazi ya ujenzi wa kituo hicho inatarajiwa kukamilikamwezi Mei, 2007. Kisiwa cha Songo Songo kimepewa upendeleomaalumu kwa kusambaziwa umeme na maji safi ya kunywakutoka kwenye kiwanda cha kusafisha gesi cha Songas,kuboresha zahanati na kujenga kituo kidogo cha Polisi. Piamaeneo ya Kinyerezi na Salasala mkoani Dar es Salaam,yaliyotengwa kwa ajili ya wananchi waliohamishwa kwenyemkuza wa bomba la gesi, yatajengewa miundombinu yabarabara, maji na umeme ili kuboresha maisha yao.7

Umeme Vijijini28. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali haina uwezowa kusambaza umeme nchi nzima kwa mara moja, iliamuakutekeleza jukumu hili kwa awamu. Mpango wa awali wausambazaji umeme ulikuwa kuanza na makao makuu ya mikoana wilaya. Hadi sasa makao makuu ya wilaya 18 hayajapatiwaumeme. Maeneo ambayo yangefuatia ni ya sehemu za uzalishajimkubwa, miradi mikubwa ya kijamii kama maji na hospitali namaeneo kando kando ya njia kuu za umeme. Serikali imetengafedha kwa ajili ya kupeleka umeme katika miji mikuu yaMbinga, Orkesmet, Ushirombo, Kilolo, Utete, na Ludewa.Maombi ya fedha kwa ajili ya makao makuu ya wilaya zilizobakiyamejumuishwa katika mpango wa Taifa uliowasilishwa kwenyeShirika la Marekani la Millennium Challenge Corporation (MCC).Aidha chini ya ufadhili wa UNDP/GEF Wizara itaendeleza mradiwa soko la umemenuru mkoani Mwanza kwa lengo la kuondoavikwazo vya matumizi ya umemenuru kama nishati mbadala.Wakala na Mfuko wa Nishati Vijijini29. Mheshimiwa Spika, baada ya mchakato wa kupatauongozi wa REA na REF kukamilika, utekelezaji wa majukumuyake utaanza baada ya Mtendaji Mkuu wa Wakala na wasaidiziwake kuajiriwa. Aidha, fedha za kuanzishia Mfuko huozimetengwa kwenye Bajeti hii.Mradi wa Umeme wa Mchuchuma30. Mheshimiwa Spika, Kamati Maalumu ya Wataalamuinayojumuisha wajumbe kutoka Wizara na taasisi mbalimbaliimeundwa ili kuharakisha utekelezaji wa mradi wa Mchuchuma.Hadidu za rejea za Kamati hiyo ni pamoja na kuratibu zoezi zimala kumpata mwekezaji wa mradi wa Mchuchuma na chuma chaLiganga; kufanya tathmini ya mapendekezo yaliyowasilishwa nawawekezaji; kutoa ushauri kuhusu njia bora ya kuendelezamiradi ya Mchuchuma na Liganga; na kuzingatia mkakati wautekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2005.Uendeshaji wa TANESCO31. Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba, 2005TANESCO iliondolewa katika orodha ya mashirikayaliyokusudiwa kubinafsishwa. Uamuzi huu ulifikiwa baada yaSerikali kutafakari upya unyeti na umuhimu wa huduma yaumeme kwa uchumi na maendeleo ya nchi. Aidha, mkataba8

uliopo wa uendeshaji wa TANESCO chini ya NetGroup Solutionsunaisha mwezi Desemba, 2006. Serikali kwa kushirikiana naBodi ya Wakurugenzi wa TANESCO inaandaa mkakati wakuendesha TANESCO utakaozingatia maslahi ya nchi baada yamuda wa mkataba Wa NetGroup Solutions kuisha.Utafutaji Mafuta32. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendeleza juhudi zakuwavutia wawekezaji kutafuta mafuta na gesi nchini. Wizaraitawasilisha mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Utafutajina Uzalishaji Petroli ya mwaka 1980 kwa lengo la kuiwianishana sheria nyingine ili kurahisisha utekelezaji wake. Aidha,majadiliano yanaendelea kati ya Serikali ya Muungano naSerikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya namna bora yakusimamia utafutaji mafuta kwa manufaa ya nchi yetu.33. Mheshimiwa Spika, kampuni zenye leseni na maeneoyanayoendelea kufanyiwa utafutaji ni: Petrobras ya Brazil (Block5); Dominion ya Uingereza (Kisangire, Mandawa na Selous);Maurel and Prom ya Ufaransa (Bigwa, Mafia); Ndovu Resources(eneo la Nyuni na Bonde la Ruvuma) na Ophir Energy zaAustralia (Block 1, 3 na 4). Aidha, leseni ya kampuni ya Antrimya Canada haijaanza kufanyiwa kazi katika maeneo ya Zanzibarna Pemba. Serikali inaendelea na majadiliano na kampunikadhaa ili zianze kutafuta mafuta. Kampuni hizo ni pamoja naPetrobras (Block 6); Statoil ya Norway (Block 2) na Petrodel yaUingereza (eneo la Tanga).Mradi wa Mnazi Bay34. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi wakuzalisha umeme kutokana na gesi asilia ya Mnazi Bayunaendelea. Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mradi ni pamojana uchorongaji wa kisima kingine kati ya viwili vinavyokusudiwaili kuhakikisha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwa ajili yamradi wa umeme na miradi mingine itakayobuniwa. Ujenzi wamtambo wa kusafisha gesi asilia uko katika hatua za mwisho.Ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Msimbati hadiMtwara unatarajiwa kukamilika hivi karibuni. Maandalizi yaujenzi wa msingi kwa ajili ya kituo cha kuzalisha umeme Mtwarayamekwishaanza. Majadiliano ya mikataba ya utekelezaji wamradi utakaosaidia kupatikana kwa umeme wa uhakika katikamikoa ya Lindi na Mtwara kati ya Serikali na Artumas Groupyamefikia hatua za mwisho. Aidha, makubaliano yamefikiwakwamba katika kipindi cha mpito Artumas watawauzia umeme9

TANESCO ili waendelee kuusambaza wakati wao wakiendeleakukamilisha ukarabati na ujenzi wa miundombinu yakuunganisha Mtwara, Lindi na Masasi. Hatua hii itawafanyawatumiaji wa umeme Mtwara kuanza kupata umeme kutokanana gesi asilia mapema.Bomba la Mafuta Dar es Salaam - Mwanza35. Mheshimiwa Spika, Serikali inafanya mazungumzona wawekezaji waliojitokeza kuwekeza katika kujenga kiwandacha kusafisha mafuta na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Dares Salaam hadi Mwanza. Ni matumaini yetu kuwa majadilianohayo yatakamilika katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.Ushiriki wa TPDC Katika Miradi36. Mheshimiwa Spika, ushiriki wa TPDC katika miradiya Songo Songo na Mnazi Bay utaongeza mgao wa Serikalikutokana na uwekezaji unaofanyika katika miradi hiyo. KatikaPSA, TPDC imepewa fursa ya kushiriki kwa kiasi cha hadiasilimia 20 katika uwekezaji wowote utakaofanyika kwenyemiradi ya gesi asilia ya Songo Songo na Mnazi Bay. Ushiriki waasilimia 20 utaifanya TPDC kupata gawio kubwa la faidaitakayopatikana kutokana na mradi husika na Serikali kupatagawio la kufidia gharama ilizochangia. Aidha, kutoshiriki kwaTPDC katika kuwekeza kwenye miradi hiyo kunawapa fursawawekezaji wengine kutumia fursa ya TPDC na hivyo kujipatiagawio kubwa kutokana na faida itakayopatikana kwenye mradihusika. Mwaka 2006/07 TPDC imetengewa fedha kidogo kwalengo hilo ingawa mahitaji yake ni makubwa.Uendelezaji wa Nishati Mbadala37. Mheshimiwa Spika, kutokana na kukua kwateknolojia za nishati mbadala Wizara itaendelea kuongeza kasiya kuwapatia wananchi walio wengi huduma bora za nishatimbadala, kutunza mazingira na kusimamia utekelezaji wamikataba ya kimataifa katika eneo hili kwa kuendeleza vyanzombadala vya nishati kama vile jua, upepo, tungamotaka,maporomoko ya maji, jotoarthi na makaa ya mawe. Aidha, baadaya Serikali kuondoa ushuru kwenye vifaa vya solar mwaka2005/06, bei ya vifaa hivyo imepungua kwa takriban asilimia 20ikilinganishwa na bei kabla ya Julai, 2005. Matokeo ya hatuahiyo ya Serikali ni ongezeko la kasi ya ununuzi wa vifaa hivyokama taarifa zilizopatikana kutoka kwa wadau, hususan, walewa mkoa wa Mwanza zinavyoonesha.10

38. Mheshimiwa Spika, mradi mwingine wa umemenuruunaofadhiliwa na Serikali ya Sweden kupitia Sida utaanzakutekelezwa katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Kigoma. Nimatarajio ya Serikali kuwa miradi hii itakapokamilika itaoneshamanufaa ya nishati hii kwa wananchi na hivyo kuchangia katikakufikisha huduma za umeme vijijini. Pamoja na miradi hiyo,asasi zisizo za kiserikali pamoja na sekta binafsi zinaendeleakuhamasisha matumizi ya umemenuru katika maeneombalimbali nchini.39. Mheshimiwa Spika, uendelezaji wa bayofueli ni eneojipya lililopewa kipaumbele katika bajeti hii. Mradi huu unalengo la kuzalisha mafuta ya mimea (dizeli na ethanol) kwa ajiliya kuendeshea mitambo. Pamoja na faida nyingine za bayofueli,mradi unalenga kuchangia katika kupunguza utegemezi wamafuta ya petroli katika kuendesha mitambo. Kamati Maalumuya Kitaifa ya Bayofueli (National Biofuel Task Force) imeundwaili kuandaa taratibu za kuwezesha maendeleo ya bayofuelinchini. Mimea inayoarigaliwa hapa ni pamoja na mbono kaburi(jatropha), moringa, miwa, michikichi, mtama, na alizeti.40. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2006/07Programme for Biomass Energy Conservation itaendeleza utafitiwajiko linalotumia mkaa, kuni, tungamotaka lijulikanalo kamarocket ili lizalishwe hapa nchini kwa kutumia malighafi za hapa.Pia, programu itaangalia uwezekano wa kutumia matanuri boraya kukaushia tumbaku ambayo yanatumika katika nchi yaMalawi. Aidha, jiko ambalo hutumia mafuta ya mimea liitwalobosch litafanyiwa majaribio.SEKTA YA MADINIUkuaji wa Sekta ya Madini41. Mheshimiwa Spika, mwaka 2005 mchango wa sektaya madini katika Pato la Taifa ulikuwa asilimia 3.5ikilinganishwa na asilimia 3.2 mwaka 2004. Ukuaji wa sekta hiirnwaka 2005 ulikuwa asilimia 1.7 ikilinganishwa na asilimia15.4 mwaka 2004 na hivyo kufanya sekta hii kuendelea kuwamojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi kubwa. Mauzo ya madininje kwa mwaka 2005 yalikuwa na hamani ya Dola za Marekanimilioni 711.3 ikilinganishwa na Dola milioni 680.2 mwaka2004. Ukuaji wa sekta hii ulichangiwa kwa kiasi kikubwa nakuanza kwa uzalishaji wa dhahabu katika mgodi wa Tulawakana ongezeko la bei ya dhahabu katika soko la dunia.11

Malengo ya Sekta ya Madini42. Mheshimiwa Spika, malengo ya sekta ya madini kwamwaka 2006/07 ni kutekeleza ahadi zilizomo ndani ya Ilani yaUchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 kuhusu kuwasaidiawachimbaji wadogo na kuongeza ajira; kuimarisha usimamizi wasekta; kuhamasisha na kusimamia uchenjuaji wa madini yetukwa lengo la kuyaongezea thamani; kusaidia wachimbaji wadogokupata masoko, mikopo, teknolojia na maarifa ya kisasa katikauchimbaji madini; kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli natakwimu; kuendeleza utafutaji wa madini; na kuvutia uwekezajikwenye sekta ya madini.Kazi Zilizopangwa Kutekelezwa43. Mheshimiwa Spika, katika sekta ya madini kazizitakazotekelezwa ni pamoja na: kuboresha mfumo wauwezeshaji wa uchimbaji mdogo wa madini; kuanza kutumiaMfumo Mpya wa Utoaji na Usimamizi wa Leseni za Madini(Mining Cadastral Information Manaqement System - MCIMS)lengo la kuboresha utoaji na usimamizi wa leseni na kupunguzamwingiliano katika utoaji leseni za viwanja; kuimarishaukusanyaji maduhuli katika sekta ya madini; na kuimarishausimamizi wa sekta ya madini kwa kuongeza kasi ya ukaguzi washughuli za madini migodini na maduka ya biashara za madini.Mradi Maalumu wa Kuboresha Utoaji naUsirnamizi wa Leseni za Madini44. Mheshimiwa Spika. Sekta ya Madini inakabiliwa namigogoro mingi kuhusu umiliki maeneo ya uchimbaji namahusiano mabaya kati va wachimbaji madini. Kwa upandemmoja, migogoro matokana na teknolojia duni katika mfumomzima wa utoaji leseni. Wizara kwa kushirikiana na NordicDevelopment Fund (NDF) ilianzisha mradi maalumu, MCIMS,ambao upo katika hatua za mwisho ili uanze kufanya kazi.Katika mfumo huo, ofisi 22 zilizoko mikoani zitaunganishwa nakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja yatakayoiwezesha kilaofisi kujua hatua zilizofikiwa na ofisi nyingine katika utoaji waleseni za madini na malipo ya kodi zinazostahili kwa kila leseni.Aidha, marekebisho ya baadhi ya vipengele vya Sheria ya Madiniyanahitajika ili iendane na mfumo mpya wa MCIMS. Serikaliinaandaa mapendekezo ya kuboresha vipengele vya sheriahusika.12

Uendelezaji wa Wachimbaji Wadogo45. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguziya CCM ya mwaka 2005, maelekezo ya Mheshimiwa Rais nataarifa zilizopo zinazoonesha kuwa kuna wachimbaji wadogotakriban milioni moja, Serikali iliunda Kamati ya KuandaaMikakati ya Kuendeeza Wachimbaji Wadogo.46. Mheshimiwa Spika, mikakati iliyoandaliwa ni pamojana: kufarinikisha upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya wachimbajiwadogo; kutoa mafunzo ya ufundi na ujasiriamali; kuhamasishana kueneza matumizi ya teknolojia bora na salama; kuanzishamfuko maalumu wa masharti nafuu; kutathmini kijiolojiamaeneo ya wachimbaji wadogo; kushawishi wachimbajiwakubwa watoe huduma za kitaalamu katika maeneo yauchimbaji mdogo; kuzielimisha taasisi za fedhajuu ya fursa zakiuchumi katika uchimbaji mdogo; uongezaji thamani nabiashara ya madini; kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vyaushirika katika maeneo ya uchimbaji; kujenga mazingira bora iiikushamirisha uongezaji wa thamani ya madini hapa nchini;kuweka mfumo wa masoko ya kushindanisha wanunuzi katikamaeneo ya uchimbaji; kuboresha usimamizi na uratibu washughuli za uchimbaji mdogo kwa kuziimarisha ofisi za madini;na kushughulikia kwa kasi mpya masuala mtambuka katikamaeneo ya uchimbaji yanayojumuisha UKIMWI, jinsia, ajira yawatoto na huduma za jamii.Aidha, Serikali itawasiliana na wawekezaji na makampuniyanayoweza kuingia katika makubaliano na wachimbaji wadogoili kuwawezesha kupata huduma za mikopo katika shughuli zaoza uchimbaji na masoko ya kuuza madini.Kupitia upya Mikataba ya Madini47. Mheshimiwa Spika, kufuatia hotuba ya MheshimiwaRais aliyoitoa Mei Mosi, 2006, Kamati Maalumu imeundwakudurusu mikataba ya madini kwa lengo la kuona uwezekanowa sekta ya madini kuongeza mchango wake kwenye Pato laTaifa. Kamati hiyo imekwishawasilisha taarifa ya awali ambayokwa sasa inafanyiwa kazi. Aidha, wakati zoezi la kudurusumikataba hiyo likiendelea, Wizara ilisimamisha utoaji leseni kwawawekezaji wakubwa waliotaka kuanza uzalishaji katika migodimipya. Mojawapo ya mafanikio yaliyofikiwa katika zoezi laupitiaji upya wa mikataba ya madini ni pamoja na makubalianoyaliyofikiwa baina ya Serikali na Kampuni za uchimbaji mkubwawa madini kukubali kuanza kulipa Dola za Marekani 200,00013

kwa mwaka kwa halmashauri husika kama kodi. Malipo ya kodihiyo kwa halmashauri yamekuwa hayafanyiki kwa kipindi kirefukutokana na utata wa kisheria uliosababishwa na kupinganakwa mikataba ya madini na Sheria ya Serikali za Mitaa yamwaka 1982. Majadiliano yaliyofikiwa baina ya Serikali yaAwamu ya Nne na kampuni hizo yalifanikisha kupatikana kwaufumbuzi wa utata wa kisheria uliokuwepo na hivyo kuruhusumalipo hayo ya kodi kwa halmashauri husika kuanza kufanyika.Hadi sasa, Kampuni ya Barrick Gold Tanzania inayomilikimigodi ya Bulyanhulu, Tulawaka na North Mara imelipa jumlaya shilingi 734,999,999 kwa wilaya za Kahama, Biharamulo naTarime. Kampuni ya Resolute itaanza kulipa kodi kwaHalmashauri ya Nzega kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.Aidha, mashauriano kati ya Serikali na kampuni za madiniyameanza katika zoezi la kudurusu mikataba ya madini kwalengo Ia kuhakikisha kuwa Taifa linanufaika ipasavyo.Kuboresha Sera na Sheria ya Madini48. Mheshimtwa Spika, baada ya Kamati ya KudurusuSera ya Madini kuwasilisha taarifa yake Serikalini, Wizaraimebainisha maeneo muhimu na vipengele vya sera na sheriavitakayofanyiwa marekebisho. Vipengele hivyo ni pamoja na:Kuongeza mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa Taifakwa kuongeza fungamanisho (linkage) la sekta ya madini nasekta nyingine; taratibu za uwekezaji na vivutio kwa utafutaji nauchimbaji madini; na ushiriki wa Serikali kimkakati katikaumiliki wa migodi. Aidha, Sheria ya Usonara itafanyiwamarekebisho kwa kufuta na kuongeza baadhi ya vipengele ilikukidhi mahitaji ya sasa ya kukuza uongezaji wa thamani yamadini.Uongezaji Thamani ya Madini49. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza uamuzi waSerikali wa kuhakikisha kwamba madini yanayozalishwa nchiniyanaongezewa thamani badala ya kuyauza nje ya nchi yakiwaghafi na kwa lengo la kuongeza mapato na ajira, Wizaraimekamilisha ufungaji wa mitambo ya uchongaji na usanifu wavito na mawe huko Arusha (Arusha Gemstone Carving Centre).Wizara inatathmini mfumo bora wa uendeshaji wa kituo hichoutakaohakikisha kinaendeshwa kibiashara na kuwezakuwasaidia wachimbaji wadogo kuongeza thamani ya madiniyao. Aidha, kituo hicho kitaendelea kutoa mafunzo ya awali yauchongaji na usanifu kwa wadau.14

Ukaguzi wa Gharama za Uwekezaji na Uendeshaji Migodi50. Mheshimiwa Spika, kazi hii inafanywa na kampuniya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation(ASAGBC). Ukaguzi wa uzalishaji na usafirishaji katika migodimikubwa ya dhahabu hapa nchini, unaendelea. Aidha, ukaguziwa gharama za uwekezaji kwenye migodi ya Geita, Golden Pridena North Mara umekamilika na ukaguzi katika mgodi waBulyanhulu, unaendelea. Taarifa kamilifu za ukaguzi kutokaASAGBC kujua hali halisi ya uendeshaji wa migodi hiyozinafanyiwa kazi. Mwaka 2006/07, Wizara itahakikisha inajengauwezo wa wataalamu wake kufanya kazi hiyo ya ukaguzi baadaya mkataba w ASAGBC kumalizika mwaka 2007 na hivyokutokuwa na ulazima wa kuendelea na mkataba huo.51. Mheshimiwa Spika, ili kujiridhisha zaidi kiutendaji,Wizara imeunda Kamati ya Wataalamu kupitia na kuchambuataarifa za Mkaguzi ili kubaini upungufu uliopo kwenye udhibitina usimamizi wa uzalishaji na usafirishaji wa madini yadhahabu hapa nchini. Kamati itatoa mapendekezoyatakayofanyiwa kazi ili kuboresha usimamizi na udhibiti wamadini ya dhahabu.Ukaguzi wa Migodi52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka2006/07 Idara ya Madini itafanya ukaguzi katika maeneo yoteya uchimbaji yakijumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar esSalaam, Tanga, Pwani na Morogoro.GEOLOGICAL SURVEY OF TANZANIARamani na Takwimu za Kijiolojia53. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka2006/07, GST itaendelea kuboresha shughuli zake za ugani;kufanya utafiti wa madini katika maeneo mbalimbali hapanchini; kukusanya, kuchambua na kutunza takwimu nasampuli za miamba; na kuboresha mazingira ya wafanyakaziwake kwa kuwapatia vitendea kazi na mafunzo ya muda mfupina mrefu. Kwa lengo la kuboresha utunzaji wa sampuli zamiamba, fedha zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa core shed. Pia,kazi ya uchoraji na uchapishaji wa ramani za Kahama naBiharamulo na block maps za Mpanda na Chunya itafanyika15

katika kipindi hiki. Aidha, GST itaendelea na shughuli zakukusanya takwimu za matetemeko ya ardhi na inategemeakufunga vituo vipya vitatu katika maeneo ya Kibaya, Kondoa naManyoni. Vituo hivyo vitapatikana kwa msaada wa InternationalProgramme for Physical Sciences (IPPS) ya Sweden.CHUO CHA MADINI54. Mheshimiwa Spika, Chuo cha Madini kilichokokatika Manispaa ya Dodoma, eneo la Mbwanga kinatoa mafunzoya muda mfupi na mrefu ya cheti na stashahada katika fanizajiolojia, uhandisi wa migodi, utafutaji, na uchenjuaji madinikwa wataalamu wa migodi mikubwa na midogo iliyopo nchini nawa Wizara iii kukuza uwezo wao katika kusimamia ukuaji wasekta ya madini.55. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka2006/07, Chuo kinatarajia kupata wakufunzi 17 kukiongezeauwezo wa ufundishaji na kuongezewa miundombinu yamaktaba, maabara, nyumba za kuishi, zahanati na viwanja vyamichezo.KITENGO CHA TANSORT56. Mheshimiwa Spika, Kitengo cha TanzaniaGovernment Diamond Sorting Organization (TANSORT)kitaendelea na majukumu yake ya kuthamini almasiinayoingizwa Uingereza kutoka Mwadui; na kukubaliana bei yaalmasi na mnunuzi (Diamond Trading Company, kampuni tanzuya Debeers). Aidha, katika kuimarisha utendaji kazi wa Kitengohicho, Wizara imetenga fedha kwa ajili ya kuwapeleka mafunzoniwatumishi wa Kitengo na kugharimia pango Ia ofisi. Mchakatowa kukihamishia Kitengo hiki nchini unaendelea ili kiwezekukagua na kuthibitisha usahihi wa almasi hapa hapa nchinikama inavyofanyika katika nchi za Botswana na Namibia.SHIRIKA LA MADINI LA TAIFA (STAMICO)57. Mheshimiwa Spika, Shirika la Madini la Taifalinawekeza katika utafutaji wa madini na linatoa huduma zauchorongaji wa miamba kwa malipo. Kwa sasa STAMICO maleseni saba za utafutaji wa madini ya dhahabu; leseni mbili zaplatinum group metals na leseni moja ya madini ya fluorite iliyokatika mkoa wa Mbeya. Katika eneo la Itetemia, karibu naBulyanhulu, linalomilikiwa kwa ubia kati ya STAMICO naTancan Mining Company Limited ya Canada, uchorongaji16

unafanyika ili kuthibitisha mashapo zaidi. Hadi sasa, mashapoyanayovuka wakia 900,000 za dhahabu yamegunduliwa. Utafitikatika maeneo mengine ya dhahabu unaendelea. Kwa upandewa uchorongaji miamba, STAMICO inazo mashine nne zazamani na iko katika hatua ya kununua mashine moja mpya ilikujiimarisha katika utoaji wa huduma hiyo. Aidha, STAMICOinaendelea na uchorongaji wa miamba eneo la Tanga Cement.D: AJIRA NA MAENDELEO YA WATUMISHI58. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2006/07 Wizarainatarajia kuajiri jumla ya watumishi 105 wa kada mbalimbali.Aidha, ili kuwaendeleza watumishi wake, katika bajeti hii Wizaraimetenga fedha kwa ajili ya mafunzo kwa kila idara/ kitengo.59. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2006/07, Mpangowa Kimkakati wa Wizara wa mwaka 2003- 2006 utafanyiwadurusu ili kuweza kukidhi mahitaji na mabadiliko yaliyojitokezakatika utekelezaji wa mkakati wa awali. Kukamilika kwa zoezihilo kutaiwezesha Wizara kutekeleza ipasavyo mfumo wa OPRASkwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi.Aidha, Wizara itaendelea kutoa semina na kuandaa mipango yakuwapatia mahitaji muhimu kiafya waliojitokeza kuwawaathirika wa UKIMWI.E: USHIRIKIANO WA KIMATAIFA60. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2005/06 sekta zanishati na madini zilinufaika kwa misaada ya wafadhilimbalimbali. Hivyo, kwa niaba ya Serikali napenda kutoashukrani kwa serikali za nchi na mashirika ya kimataifa kwaushirikiano na misaada waliyotoa kwa ajili ya kuendeleza sektahizo. Naomba nizishukuru serikali za Australia, Canada, China,Denmark, Finland, Hispania, India, Japan, Marekani, Norway,Sweden, Ubelgiji, Ufaransa, Uholanzi, Uingereza na Ujerumani.Aidha; natoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Nchiza Ulaya, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benkiya Rasilimali ya Ulaya, DANIDA, GEF, FMO, IAEA, IMF, JICA,KfW, NDF, NORAD, ORET, Sida, UNDP, UNESCO, UNIDO naUSAID.F: SHUKRANI61. Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hiikuwashukuru viongozi wenzangu ambao kwa pamoja tumewezakufanikisha shughuli za Wizara kwa mwaka 2005/06. Kwanza17

napenda kumshukuru Mhe shimiwa Lawrence Masha, NaibuWaziri kwa msaada wake mkubwa alionipa katika kusimamiashughuli za Wizara. Napenda piakuwashukuru Katibu Mkuu,Bwana Arthur Mwakapugi; Wakuu wa Idara na Vitengo; viongoziwa mashirika yaliyo chini ya Wizara wakiwemo Wenyeviti naWajumbe wa Bodi na Watendaji Wakuu; Kamati zinazosimamiwana Wizara; na wafanyakazi wote wa Wizara na Mashirika yake.G: MAJUMUISHO62. Mheshimiwa Spika, sasa naliomba Bunge lakolikubali na kuidhinisha mapendekezo ya bajeti ya Sh.465,202,173,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na mashirikayake kwa mwaka 2006/07. Mchanganuo wa bajeti hiyo ni kamaifuatavyo:(i)Bajeti ya Maendeleo ni Sh. 432,544,995,000 ambazokati yake Sh. 224,981,995,000 ni fedha za hapa naSh. 207,563,000,000 ni fedha za nje; na(ii) Bajeti ya Matumizi ya Kawaida ni Sh. 32,657,178,000ambapo Sh. 1,675,726,000 ni kwa ajili ya mishahara(PE) na Sh. 30,981,452,000 ni matumizi mengineyo(OC).63. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.18

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!