13.07.2015 Views

Mkulima Mbunifu - Infonet-Biovision

Mkulima Mbunifu - Infonet-Biovision

Mkulima Mbunifu - Infonet-Biovision

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Jarida la kilimo endelevu Afrika MasharikiWakulima wanatumia taarifaToleo la 8 Septemba, 2012Malisho wakati wa kiangazi 2Pandikiza parachichi 4Mbinu ya mapambano 7Mwezi mmoja uliopita, tulitembeleasehemu mbali mbali nchini Tanzaniakuona wakulima wanafanya ninikutokana na taarifa tunazochapishakatika jarida hili. Ilikuwa ni maajabuna mshangao kwetu kuona namnaambavyo wakulima wamefaidika nataarifa hizi, na tayari wanazitumiakuboresha shughuli zao jambo ambalolimekuwa na manufaa makubwakwao.Moja ya taarifa tulizoandika nakujipatia umaarufu mkubwa miongonimwa wakulima kiasi cha kuanzakutekeleza mara moja, ni zile zinazohusianana ufugaji wa kuku, hasa wakienyeji, kilimo cha parachichi, ulishajiwa ng’ombe wa maziwa, utunzaji waudongo na matumizi ya mbolea namadawa ya asili. Kwenye toleo hilitunakuletea mbinu zaidi za kuboresharutuba kwenye udongo, malisho yang’ombe wa maziwa, utunzaji wamayai, na mengine mengi.Mradi wa ng’ombe, zingatia haya!bila kuvunjwa moyo na changamotozilizopo.Jambo la pili, mfugaji ataanzakuwaza kununua ng’ombe bora bilahata kufikiria atamlisha nini na niwapi atamfugia. Somo, kabla haujanunuang’ombe, jenga banda, kishaotesha majani kwa ajili ya malisho.Kumbuka, malisho utakayo oteshayatachukua muda kiasi mpaka kuwaMkM - Ufugaji wa ng’ombe wa maziwani mradi unaowavutia wafugaji vijanaambao wako tayari kuwekeza kwenyesekta hiyo. Hata hivyo, maandalizina uelewa wa kutosha, vitamuwekamfugaji kwenye barabara salama zaidikuelekea kwenye mafanikio. Chakwanza ni kuwa na moyo na utayariwa kuingia katika shughuli ya ufugajitayari. Vinginevyo, unaweza kuangaliakama unaweza kupata malishokutoka kwenye shamba la jirani. Jambomuhimu hapa ni kupata chakula chakutosha na bora wakati wote. Piataarifa ni muhimu. Soma sana kuhusianana ufugaji, hudhuria mikusanyikoya wafugaji na wakulima, na ujifunzekutokana na wafugaji wengine waliofanikiwa.Usiruhusu udongo uharibiweUtunzaji hafifu wa udongo unaofanywana wakulima unaweza kusababishakupata mavuno kidogo.Kila mara wakulima wanapolimamashamba yao tayari kwa ajili yakupanda, eneo moja wapo ambalohawatilii maanani ni kuzuia mmomonyokowa udongo. Mmomonyokounaosababishwa na maji na upepohuchukua tabaka la juu la udongo.Hii ni sehemu muhimu ya udongoambayo inafaa sana kwa ajili yakilimo kwa kuwa ina virutubishomuhimu vinavyosaidia mimeakukua vizuri. Tabaka la juu la udongolinapochukuliwa hufanya ufanisi waudongo kuwa hafifu, na pia uwezowa udongo unaobakia kuhifadhimaji hupungua. Hivyo, mkulima nilazima kuhakikisha kuwa udongoumefunikwa muda wote baada yakuvuna ili kuzuia mmomonyoko waudongo unaoweza kusabishwa naupepo.Mwanzoni mwa mwezi uliopita tuliwezakushuhudia shamra shamra katika maeneombalimbali nchini Tanzania kwa ajili yamaonesho ya kazi za wakulima na hatimayesikukuu ya wakulima maarufu kama NaneNane.Kwa wale ambao mliweza kuhudhuriamoja ya maonesho hayo, mliona ni jinsigani wanaoshughulika na kilimo walivyojitahidikujitokeza kwa wingi kuoneshambinu mbalimbali zinazoweza kumsaidiamkulima kusonga mbele katika shughulizake za kila siku.Ni ngumu kujua ni kiasi gani cha wakulimawadogo wadogo walioweza kujizatitina kuhudhuria maonesho hayo ambayoyalifanyika katika maeneo mbalimbalinchini Tanzani. Tangu kuzinduliwa jaridahili la Mkulima Mbunifu takribani mwakammoja sasa, tumekuwa tukitoa shime kwawakulima wadogo wadogo kuongeza juhudiili waweze kujikomboa, na ndiyo maanajarida hili ni kwa ajili yenu wakulimawadogo wadogo.Kwa kiasi kikubwa tumekuwa tukisikiasauti yenu juu ya yale mnayohitaji kujifunza,tukayafuatilia na kuwachapishiakatika jarida hili au kwenye machapishomengine yanayopatikana katika ofisi yetuya Mkulima Mbunifu.Tunashawishika kuwakumbusha wakulimana wafugaji wadogo kuitumia fursahii na habari muhumi tunazotoa ili kujiinuakiuchumi, na isiwe kama ambavyoidadi inayojitokeza kwa ajili ya maoneshoya nane nane haiendani na idadi yawakulima ambao ndio walengwa wakubwa.Tuna taarifa na mbinu mbalimbali zinazowezakukuongezea kipato, mfano machapishokwa ajili ya ufugaji wa kuku, mbuzi,kondoo, na hata ng’ombe. Pia namna yakuboresha kilimo na kuwa na tija zaidi.Tunafurahi kuona kuwa hata viongoziwa Serikali wana mtazamo sawa na sisiwa kuwasaidia na kuwahimiza wakulimawadogo kupigana kujikomboa kutoka katikalindi la umaskini.Pia ni muhimu kujiunga kwenye vikundiili iwe rahisi kupata usaidizi pale inapohitajika.Himiza wenzako na mjiunge kwenyevikundi muweze kufanya shughuli zenukwa mshikamano.Mk M, S.L.P 14402, Arusha, Simu 0717 266 007, 0785 133 005 Barua pepe info@mkulimambunifu.org, www.mkulimambunifu.org

Toleo la 8 Septemba, 2012Guatemala: Malisho wakati wa kiangaziMajani haya yanatumika kamachakula cha ziada kwa mifugo wakatiwa kiangazi, hayatakiwi kutumikakama malisho pekee.Neema MbisseMajani aina ya Guatemala (Tripsacumandersonii) imesambaa kwa kiasikikubwa katika ukanda wa tropiki.Aina hii ya majani inahitaji kiasikikubwa cha mvua, au udongo wenyeunyevu, lakini hata hivyo huwezakubaki yakiwa na kijani kibichi wakatiwote wa kipindi cha kiangazi.Nchini Tanzania, majani haya yanapatikanakwenye nyanda za kati, nasehemu zenye miinuko, hasa zenyerutuba ya kutosha kama vile kwenyesafu za mlima Kilimanjaro, mlimaMeru na Milima ya Usambara. Mimeahii inakuwa kwa wingi, na inafaa zaidikama chakula mbadala kinachotumikakwa ajili ya mifugo wakati wa kiangazi.Guatemala ina uvumilivu zaidiya matete (napier grass), lakini ni dhaifukatika uzalishaji na ina virutubishovichache sana.KupandaGuatemala hupandwa kutokana navipande vya mashina, na huwa tayarikuvunwa baada ya miezi. Hakikishakuwa unapata mapandikizi kutokakwenye chanzo kinachoaminika.Unaweza kupanda kipande cha shinachenye pingili 3, au sehemu ya shinailiyoanza kuota kwa kulaza chini,kwenye sehemu yenye nafasi ya ½mita x 1 mita. Inahitaji mbolea nyingikwa ajili ya ukuaji mzuri.MsetoGuatemala inaweza kupandwa msetona desmodium, leucaena, sesbania, au calliandraili kuongeza mavuno ya malishomakavu yenye protini kwa wingi.Mavuno na matumiziHekari moja ina uwezo wa kuzalishaGuatemala kiasi cha tani 9-22, yakiwayamekatwa kiasi cha sentimita 10-25kutoka kwenye usawa wa ardhi. Guatemalahasa hutumika kama akiba yamalisho ambayo hukatwa na kulishwamifugo wakati wa kiangazi yakiwamabichi. Majani haya hutengenezasileji yenye ubora wa wastani. Majanihaya yanaweza pia kutumika kamauzio sehemu ya kuishi, au kwenyeMkulima Mbunifu ni jarida huru kwa jamii ya wakulimaAfrika Mashariki. Jarida hili linaeneza habari zakilimo hai na kuruhusu majadilianokatika nyanja zote za kilimo endelevu.Jarida hili linatayarishwa kila mwezina The Organic Farmer, Nairobi, nimoja wapo ya mradi wa mawasilianoya wakulima unaotekelezwa na Biovision(www.organicfarmermagazine.org)kwa ushirikiano na Sustainable AgricultureTanzania (SAT), (www.kilimo.org),kontua kwa ajili ya kuzuia mmomonyokowa ardhi, matandazo shambani,au kwa ajili ya kukausha maji sehemuyenye tindiga. Inatumika pia kamakizuizi cha baadhi ya wadudu kwenyechai, kahawa na viazi.Guatemala haiwezi kuvumilia kuchungiamifugo au kukatwa marakwa mara. Haishauriwi kuchungiamifugo kwenye aina hii ya malisho.Inashauriwa kukata kwa uwiano wasiku 30 wakati wa mvua, na uwianowa siku 42-45 wakati wa kiangazi. Ilikuepuka kuvimbiwa, inashauriwakukata na kuacha majani haya yanyaukekabla ya kulishia mifugo.Ubora wa virutubishoKwa kiasi kikubwa hii inategemeanana ukataji wa mara kwa mara, mashinayakikomaa yanakuwa na nyuzi nyingina pia kuwa na kiasi kidogo cha protinina wanga kama hayakutunzwa nakuwekwa mbolea vizuri.Wakati wa hatua tofauti za matumizi,kiasi cha protini pia hutofautiana.Sehemu ya juu iliyokauka inakuwa naasilimia 6.4, sehemu ya juu ambayoni mbichi inakuwa na asilimia 8.8,sehemu ya majani ambayo ni mabichiinakuwa na asilimia 6.1, shina linakuwana asilimia 4.6. Kiwango chaprotini kinakuwa juu wakati wa wiki 3,na kuzidi kupungua kadri yanavyozidikukomaa na nyuzi nyuzi kuongezeka.Majani yanakuwa na kiasi kikubwa chamadini aina ya manganese, chuma, zinkna potashiamu.Kutokana na kiasi kidogo cha protinikwenye aina hii ya malisho, malishoMorogoro.Jarida hili linasambazwa kwa wakulimabila malipo.Mkulima Mbunifu linafadhiliwa na Biovision- www.biovision.ch, Swiss DevelopmentAgency (SDC) - www.swiss-corporation.admin.ch,na USAID-TAPP – www.fintrac.com.Wachapishaji African Insect Science for Foodand Health (icipe), S.L.P 30772 - 00100Nairobi, KENYA, Simu +254 20 863 2000,icipe@icipe.org, www.icipe.orgmbadala yenye kiasi kikubwa chawanga na protini inafaa kutumikakwa pamoja na Guatemala kwa ukuajimzuri wa mifugo. Miongoni mwavyanzo vya protini vilivyothibitishwani pamoja na vyakula vyenye mchanganyikowa samaki, soya, aina hii yamalisho huwa na matokeo mazurizaidi kuliko vyakula vinavyotokanana mashudu ya pamba, hasa kinapotolewakwa kiwango cha kutoshapamoja na majani ya Guatemala.Miti ya malishoGuatemala inaweza kupandwa msetona miti ya malisho. Kwa kufanyahivyo, mkulima anaweza kupunguzaau kuondokana kabisa na matumiziya virutubisho. Utafiti unaoneshakuwa kilo 3 za malisho yanayotokanana miti kama vile calliandra, leucaena,desmodium, viazi vitamu, haradali naaina nyingine za jamii ya mikundezina virutubisho sawa na pumbaaina ya diary meal. Mfugaji anawezakupunguza gharama kwa kutumiaaina hii ya malisho kwa ajili ya mifugowake.Ni muhimu kwa mkulima kufahamukuwa ng’ombe wa maziwa wanahitajimlo kamili wenye kutia nguvu,protini na vitamini. Mlo huo ni lazimauwe na wanga kiasi cha asilimia 75,Protini asilimia 24 na asilimia 1 yamadini.Taarifa hii imeandaliwa kujibu swali lililoulizwana kikundi cha wakulima chaMOWE kutoka Machame Mkoani Kilimanjaro.Mpangilio In-A-Vision Systems, +254 720419 584Wahariri Ayubu S. Nnko, John CheburetAnuani Mkulima MbunifuMakongoro Street,S.L.P 14402, Arusha, TanzaniaUjumbe Mfupi Pekee: 0785 496 036, 0753963 165Piga Simu 0717 266 007, 0785 133 005Barua pepe info@mkulimambunifu.org,www.mkulimambunifu.org

Toleo la 8 Septemba, 2012Mayai yanaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefuWakulima wanaowekeza kwenyemradi wa kuku, hupata hasara paleambapo hawatunzi mayai ipasavyo.Ayubu NnkoMayai ni bidhaa hafifu na inayoharibikakwa haraka. Hivyo, ni lazimaishikwe kwa uangalifu na kutunzwavizuri baada ya kutagwa ili yasivunjikeau kuharibika. Watu wengi wanaonunuamayai kutoka dukani watatambuamara moja kuwa mayai hayoyamevunjika au yameoza. Tatizo hililinaweza kutokana na utunzaji na uhifadhiwakati mayai bado yakiwa kwamfugaji.Ili kupunguza hasara, ni lazimamfugaji ahakikishe kuwa mayaiyanafika sokoni yakiwa bado mapya nasalama. Utunzaji sahihi wa mayai huyafanyayaepukane na madhara yanayowezakutokana na viumbe wadogowadogo kama vile bakteria, wanyamawalao mayai, upotevu wa unyevu, aujoto wakati wa uhifadhi na kusafirishakwenda sokoni, jambo linaloweza kuyafanyayavunjike. Mayai kama ilivyokwa viumbe hai wengine yanahitajikupumua. Trei za kuhifadhia mayaiziwekwe kwenye sehemu yenye hewainayozunguka, hasa hewa ya oxyjeni.Trei zote za kuhifadhia mayai nilazima ziwekwe katika hali ya usafi,zisiwe na harufu ili kuepuka kufishwaau kusababisha hali yoyote inayowezakusababisha uharibifu. Mayai nilazima pia yakingwe dhidi ya joto kalipamoja na unyevu.Weka sehemu yenye ubaridiMayai yanaweza kuharibika kwaharaka kutokana na joto kali. Labdayahifadhiwe kwenye jotoridi la chini,vinginevyo mfugaji atapoteza idadikubwa ya mayai kabla hayajafikasokoni. Ni lazima kuhakikisha kuwamayai yanahifadhiwa sehemu yenyeubaridi, ambayo siyo kavu sana,vinginevyo yatapoteza unyevu kwaharaka endapo yatawekwa sehemukavu. Hali ya mahali pa kuhifadhiainategemea na siku ambazo mfugajianahitaji kuhifadhi mayai.Wafugaji wenye uzoefu wamekuwana uwezo wa kuhifadhi mayai kwakipindi cha miezi 6-7 kwa kutumiajokofu. Wafugaji wadogo piawanaweza kuhifadhi mayai kwa sikukadhaa mpaka watakapopata mayaikwa ajili ya kuhatamiwa. Kamwe usihifadhimayai unayokusudia kutumiakwa ajili ya kuhatamiwa kwenyejokofu.Uhifadhi wa mayai kwa ajili yakuhatamiaWafugaji wadogo hutumia njia yakiasili kuhatamisha na kuanguamayai. Hii ni njia ya kutumia kukuau ndege mwingine ambaye hupewamayai na kuyahatamia hadi kuanguliwa.Kuku wa kienyeji ni wazurisana wanapotumiwa kwa ajili ya uzalishajiwa vifaranga. Hata hivyo kwauzalishaji mzuri ni lazima mfugajiahakikishe kuwa kuku anapewamayai yenye uwezekano mkubwa wakuanguliwa.Mbinu moja wapo ambayo mfugajianaweza kuitumia kutambua mayaiyenye uwezekano mkubwa wa kuanguliwani kwa kumulika kwa kutumiamshumaa. Mayai yanaweza kuwekwakwenye mwanga mkali ambao utakuwezeshakuona ndani ya yai. Kifaarahisi cha kumulika mayai kinawezakutengenezwa kutokana na kuwekabalbu ndani ya boksi dogo. Unakatatundu dogo kuruhusu mwanga.Hakikisha linakuwa na ukubwa wakuweza kuruhusu yai kukaa juu yake.Shika yai kwa kulisimamisha kwakutumia vidole vyako viwili, kishaliweke kwenye mwanga wa tochi aubalbu. Zoezi hili linakupa uhakikakuwa mayai yenye uwezekano wakuanguliwa ndiyo pekee yanayochaguliwa.Tengeneza sehemu ya kuhatamiamayaiMfugaji anaweza kuboresha uzalishajiwa kuku wa kienyeji kwa kuwajengeatabia ya kuhatamia mayai. Kukuwa kienyeji wakiwa wamelishwavizuri, wanaweza kuhatamia katiya mayai 10-14 kwenye mzungukommoja. Baada ya kuangua, mfugajiamruhusu kuku kukaa na vifarangawalau kwa wiki moja. Baada ya hapovifaranga wanaweza kutengwa.Kuku wakiwa bado katika haliya kuhatamia, anaweza kupewamayai ya bandia ambayo yanawezakutengenezwa kutokana na sabuni,huku kuku wengine wakiwa wamehatamiamayai halisi ya kutosha.Mayai bandia yanaweza kuondolewana kuku kuwekewa mayai halisiaendelee kuhatamia mpaka yatakapoanguliwa.Kuku wanaohatamia ni lazimawapatiwe chakula na maji ya kutosha.Kuku ambao hawahitajiki kwa ajili yakuendelea kutotoa, wanyang’anywevifaranga na kuachiliwa walipo kukuwengine. Ni vizuri kuweka alama kilayai kuonesha ni tarehe gani lilitagwa,hii itamsaidia mfugaji kutokuchanganyamayai ya zamani na mayaimapya. Badala yake, mfugaji anawezakuwatenga kuku ambao amewaandaakwa ajili ya kutotoa na waleambao ni kwa ajili ya kutaga tu iliasichanganye mayai yake.Jinsi ya kutunza vifaranga• Vifaranga wanapotengwa namama yao, wawekwe pahali safi.• Ni lazima wapatiwe joto kutokakwenye taa ya kandiri.• Vifaranga walishwe kwakutumia chakula maalumukwa ajili ya vifaranga, kishawaongezewe glukosi na maji safi.Hii itawawezesha kukua kwaharaka.• Sehemu wanapokuziwa vifarangani lazima kupima joto marakwa mara ili kuhakikisha kuwahawapati joto la kuwazidi au kwakiwango cha chini.

Toleo la 8 Septemba, 2012Vuna zaidi kwa kutumia mbinu ya tumbukizaTumbukiza ni mbinu inayofaa katikaeneo ambalo ni kame na lisilokuwakame. Ni mbinu ya kuhifadhi maji,na kutoa mavuno mengi zaidi. Nimbinu ambayo imepokelewa kwa kiasikikubwa na wafugaji wa ng’ombe wamaziwa kutoka sehemu ambazo wanaeneo dogo kwa ajili ya uzalishaji wamalisho. Ni ufumbuzi ambao umeonekanakuleta ongezeko la uzalishajiwa matete kwa asilimia 20 katika ekarimoja. Kama inavyo onekana kwenyepicha, mbinu hii inaweza kutumikakwa ajili ya aina mbalimbali za mazao.Kutengeneza shimo: Lima na usafisheshamba lako vizuri. Chimba shimolenye upana na urefu wa sentimita60 kwa 60, au 60 kwa 90, au 90 kwa90 kulingana na kiwango cha unyevukwenye eneo ulilopo. Changanya debe1 la udongo wa juu na debe mojala mbolea (mboji). Weka mchanganyikohuo kwenye shimo ukiacha kiasicha sentimita moja bila kujaza. Pandamimea/mapandikizi 5-10 kwenyeshimo moja.Kusanya mboleaMoja ya changamoto ambazo wakulimawanakabiliana nazo wanapotakakutumia mbolea mboji, ni kutopatambolea ya kutosha au yenye uboraunaotakiwa wanapohitaji kwa ajili yakupandia. Ili kuondokana na tatizo hiloni kukusanya mbolea. Njia sahihi yakupata mbolea nzuri ni kwa kurundikakinyesi na mkojo wa ng’ombe pamoja.Njia nzuri ya kuepuka upotevu wavirutubisho kwenye mbolea, inapendekezwambolea kutoka kwenye bandaikusanywe mara mbili kwa siku, kishakurundikwa kwenye shimo lililotengenezwamaalumu kwa ajili ya kukusanyiambolea. Hata hivyo ni rahisikukusanya kwa kuwa wafugaji waliowengi wanafungia ng’ombe kwenyebanda lenye sakafu.Mabua ya mahindi ni mazuri zaidi kwakukusanya madini (Nitrojeni) kutokakwenye samadi yanapotumika kamamatandiko kwenye zizi la ng’ombe.Wakulima ni lazima wawekezekwenye shimo la kukusanyia mboleaili kuhifadhi virutubisho. Ni muhimuMagonjwa huathiri uzalishaji wa ndiziNdizi ni mojawapo ya chakulamuhimu sana katika ukanda watropiki duniani kote. Hata hivyo, uzalishajiwake nchini Tanzania na AfrikaMashariki kwa ujumla unaathiriwana utunzaji hafifu pamoja na magonjwayanayosambazwa na bakteriana virusi. Matokeo yake, uzalishajiwa ndizi unapungua katika maeneoyote yanayozalisha ndizi. Wakulimawalio wengi hawafahamau magonjwayanayoshambulia migomba. Kamailivyo kwa mazao mengine, ndizi piazinahitaji utunzaji thabiti. Hii inaanziakwenye udongo ambao utapandamigomba.Migomba ni lazima ipandwekwenye sehemu ambayo imeachwaUsitumie mahindi yaliyoozaNi kweli wafugaji walio wengiwamekuwa wakitumia mahindi yaliyoozakulisha mifugo yao bila waokujua kama ni hatari kwa mifugo nawao wenyewe. Madhara ya kulishamifugo kwa kutumia mahindi yaliyooza,wanyama huathiriwa nasumu iliyopo kwenye mahindi yaliyoozainayojulikana kama mycotoxin.Madhara yanayosababishwana sumu hii ni pamoja na kupunguzahamu ya kula, mmeng’enyo wachakula, na kuathiri ukuaji. Baadhiya madhara haya yanaweza kupitiapia kupunguza muda wa kuhifadhi;kuongeza matumizi ya mboleashambani mara kwa mara huongezarutuba kwenye udongo.bila kulimwa angalau kwa mwakammoja. Usafi wa shamba ni muhimuili kufukuza wadudu. Kukata shinala mgomba na kuiacha shambaniinaweza kutumika kama mtego wakukamata wadudu waharibifu.Chukua tahadhari zaidi unapotumiasamadi kama mbolea kwa ajiliya migomba. Aina hii ya mboleainaweza kusababisha kuwepo vidukariwa migomba shambani.Ni hatari sana kuchukua mbegu yamigomba kutoka shamba la jiranikwa kuwa migomba yake inawezakuwa imeathirika, na kwa mantikihiyo shamba lako pia litaambukizwamagonjwa. Njia nzuri ya kupatambegu ambayo haijaathiriwa nikupata mbegu kutoka kwenye vituovya utafiti au kwa wazalishaji wambegu waliothibitishwa. Kamweusinunue mbegu za migomba zinazouzwakwenye vitalu vilivyomokando kando ya barabara.Katika toleo lijalotutashughulikiamagonjwa ya ndizi.kwenye bidhaa au ulaji wa bidhaayenyewe.Binadamu pia anaweza kuathirika.Hii inategemeana na kiasi cha sumukilichopo kwenye bidhaa husika, namadhara yanaweza kuonekana maramoja au ikachukua muda kuonekana.Hii inategemea kiasi hichocha sumu kimekaa kwenye mwili wamnyama kwa muda gani na uwezowa mnyama kukabiliana na sumu.Tabia hii ni lazima ikomeshwe katikanyanja zote, iwe kwa nguruwe, kukuau aina yoyote ya mifugo.

Zalisha mazao zaidi kwa kutumia ‘Mapambano’Ubunifu huu wa kutengeneza mboleamboji unafanikisha urutubishaji waudongo, na inawafaa wakulima wakilimo hai.Ayubu Nnko na INADESMapambano ni aina ya mbolea mbojiiliyobuniwa na kutafitiwa na SuzanaSilvesta, ambaye amebuni mbolea hiiya asili tangu mwaka 1960 na utafitiwake kukamilika ilipofika mwaka1985. Aliamua kuiita “Mapambano”kwa namna ilivyomkomboa toka lindila umaskini yeye na watoto wake alioachiwabaada ya mume wake kufariki.Mama huyu Alitambuliwa na Mradiwa kuendeleza Ubunifu wa Wakulima(PFI), uliotekelezwa na INADES nakusimamiwa na Wizara ya Kilimo naChakula mwaka 1998.Ubunifu wenyeweMwanzo alikuwa anavuna gunia 1 hadi2 za mahindi kwa eka moja. Maeneo yaWilaya ya Kondoa ni makame sana.Suzana alianza majaribio kwa kufukiamasalia ya mazao katikati ya matuta nakulima mahindi. Masalia hayakuwezakuoza yote. Hata hivyo, mavuno yakapandatoka gunia 2 hadi 4 za mahindikwa eka. Baadaye, akachimba mitaroya kina cha futi moja kwenda chinina upana futi 1 na kufukia masalia,mavuno yalipanda toka gunia 4 hadi6. Masalia hayo yalichukua miaka 3kuoza yote. Mwaka uliofuata alichimbamitaro ya kina cha futi 2 na upana futi2 na kujaza masalia ambayo yaliozabaada ya miaka 2 tu na mavunokuongezeka hadi gunia 8 kwa eka.Hapo ndipo akagundua kuwa kadrialivyoongeza kina na ndivyo masaliayalioza kwa haraka. Ndipo mwaka1980 alipochimba shimo kiasi cha mtumzima kutumbukia kabisa na kujazamasalia ya mazao, majani ya aina zote(hata ya katani) na samadi.Mchanganyiko huu ulioza baadaya mwaka 1 na nusu tu. Pia mavunoyalifikia gunia 15 kwa eka. Mafanikiomakubwa aliyapata mwaka 1985 alipogunduakuchanganya masalia yotehayo na majivu pamoja na mkojo wang’ombe. Hapo sasa yalioza kwa mudawa miezi 4 hadi 5 tu kulingana na kiasicha joto la jua na mavuno yake yaliongezekakutoka gunia 15 kwenda 20 nampaka sasa ni 24 kwa eka moja.Namna ya kutengeneza mboji yamapambano.1. Chimba shimo la kina cha mita 2 au3 na upana wa mita 2 au 3.2. Tanguliza majivu chini kama debe 6hadi 10 hivi.3. Weka juu ya majivu majani mabichiau makavu (yanyunyizie maji machafu)masalia ya mazao kama mahindi,karanga, maharagwe n.k juu ya samadiunene wa kama futi moja hivi.4. Weka samadi kama debe 6 – 10 juuToleo la 8 Septemba, 2012ya majani na masalia hayo.5. Kila masalia ya chakula cha binadamuyanapobaki, uchafu wa mifugo,uchafu wa ndani ya nyumba vinapopatikanabasi tupia ndani ya shimo hilo.6. Rudia mpangilio huu hadi shimolijae na yatokeze juu ya ardhi kamanusu mita.7. Likiisha jaa nyunyizia maji machafukama nusu ndoo hivi ama ya kuosheavyombo, nafaka, kufulia au kuoga juuya shimo.8. Uozaji ukiendelea huwa kunamvuke unotokeza juu ya shimo.Mvukeukiacha kutoka juu ya shimo basi huwaimeiva baada ya miezi 4 au 5.9. Kisha fukua mapambanoiliyoiva,iweke mahali pazuri na uifunikena majani laini ili isipoteze uborawake na anza kuitumia.10. Anza tena kujaza shimo kamaawali na kitakuwa kiwanda chako chambolea cha kudumu.Matumizi:Mboji ya mapambano hutumika kamasamadi itumikavyo. Unaweza kuwekakwenye mashimo au kuisambazashambani. Shamba lililokolea mapambanolinaweza kutumika miaka mitatukabla ya kuongeza mbolea nyingine.Mboji hii hurekebisha mchanganyikowa udongo, kuongeza rutuba na kukamatamaji yanayotaka kutiririka tokashambani wakati wa mvua.MafanikioShimo hilo linatoa mboji ya kuwezakutosha kati ya eka 5 hadi 7. MamaSuzana sasa ni mtaalamu na ametambuliwahata na taasisi ya Utafitiwa kilimo na mifugo kanda ya kati.Amekuwa mjumbe wa kamati yaushauri ya utafiti wa Maendeleo yaKilimo na Mifugo ya kanda ya kati(ZEC). Wakulima wengi na baadhiya wataalamu wa mikoa ya Dodoma,Singida, Morogoro, Mbeya na Iringawameanza kuitumia na wamepatamafanikio makubwa. Hivi sasaMama Suzana ni Mkulima Mbunifuna Mtaalamu na anatembelewa nawageni wengi toka ndani na nje yanchi kwa ajili ya kujifunza. Ubunifuwake tayari umeandikwa kwenyevitabu vingi kitaifa na kimataifa.ChangamotoWakati Suzan akibuni mbolea hiialipata shida sana, baadhi ya watuwalimuita kichaa kwani ilikuwaajabu kwa mwanamke kuchimbashimo kubwa na kukusanya majanikulijaza. Baadhi ya wataalamu walioionaau kuisikia hawaiungi mkonokwa sababu wao wanataka wakulimawatumie mbolea za viwandaniingawa zinaathiri mazingira, afyakwa walaji na zina gharama kwawakulima.Kwa maelezo zaidi wasiliana na MkurugenziMtendaji INADES Formation Tanzania,S.L.P: 203 Dodoma, Simu: 0262354230, Barua pepe: inadesfo@yahoo.com.Ungependa kupata jarida la Mkulima Mbunifu?Jarida la Mkulima Mbunifu linachapishwa na kutolewa kwa vikundi vyawakulima bure. Ili kikundi chako kipokee jarida hili basi jaza fomu hii:1. Jina la kikundi/taasisi.............................................................................2. Mahali ulipo............................................................................................3. Idadi ya wanakikundi: Wanaume………...……wanawake...………….4. Jina la kiongozi......................................................................................5. Nambari ya simu (rununu)....................................................................6. Anuani ya posta.....................................................................................ILANI: Tafadhali tumia taarifa za fomu hii na uambatanishe majina yawanakikundi kwenye karatasi tofauti na namba zao za simu.Tuma fomu uliojaza kwa S.L.P 14402, Arusha, Tanzania.Ujumbe Mfupi Pekee: 0785 496036, 0753 96 31 65.Barua pepe info@mkulimambunifu.org

Toleo la 8 Septemba, 2012Ni muhimu kuwa na njia za kuongeza kipatoAyubu NnkoKatika kipindi cha maonesho ya nanenane yaliyomalizika hivi karibuninchini Tanzania, Waziri mkuu waJamhuri ya Muungano wa TanzaniaMh. Mizengo Pinda, aliwataka wakulimakujijengea tabia ya kuwa na shughulimbalimbali zitakazowawezeshakukabiliana na ushindani wa soko napia kujiongezea kipato.Kuwa na shughuli mbalimbali ni mojaya mbinu muhimu inayotumiwa nawakulima vijijini katika kujiongezeakipato. Hapa uwiano wa hatari unagawanywakwenye miradi mbalimbalikiasi kwamba, endapo soko halitakuwazuri kwa bidhaa moja wapo, basinyingine itachukua nafasi na hivyomkulima kuwa kwenye usalama, bilahasara kubwa. Hii inatumika zaidikama njia ya kumuwezesha mkulimakuishi vizuri.Hii ni kusema kuwa uwekezaji mpyakwenye miradi mbalimbali ni njiaambayo imeonesha kuwa na mafanikiopale ambapo kunakuwa na matatizoya kiuchumi. Kwa mfano, wakulimawengine wanaweza kuamua kaujiriwakwenye shughuli nyingine tofauti nakilimo na ufugaji, huku shughuli zaoza kilimo na ufugaji zikiendelea. Hatahivyo, hali hii inaweza kusababishashughuli za shamba kutokuwa naufanisi mzuri kwa kuwa uangalifu piaunakuwa ni mdogo.Kwa upande mwingine, kuwa namiradi mbalimbali kunaweza kuwana manufaa kwenye mahusiano yawanyama na mimea, hivyo kumuwezeshamkulima kupunguza gharama zauzalishaji, pale ambapo upande mmojaunaweza kulisha mwingine, au kuwana uhusiano wa karibu. Kwa mfano,mkulima anayefuga kuku, anawezakutumia kinyesi cha kuku kama mboleakwenye shamba la mboga. Kwa halihiyo, anakuwa amepunguza gharamaza pembejeo, na hapo baadaye akawaameongeza faida kwenye mauzoya mboga. Wakati huo huo endapomboga ni nyingi sokoni, mfugaji huyuanaweza kutumia mboga hizo kwaajili ya kulishia kuku. Kwa kufanyahivyo, matumizi ya mbolea za viwandanishambani yanakuwa yamepunguakwa kiasi kikubwa.Ni lazima pia ieleweke wazi kuwauanzishaji wa miradi mbalimbaliunaweza kuwa changamoto kwawakulima kwa kuzingatia upatikanajiwa mtaji wa kuanzisha. Uanzishaji wamradi mpya shambani unahitaji pesa,ambazo kwa wakulima walio wengini shida. Na hili limeendelea kubakiakuwa tatizo kwa wakulima wengikufanya shughuli zao kibiashara nchiniTanzania. Mkulima Mbunifu, linapendakutoa changamoto kwa WaziriMkuu kufuatia kauli yake kwa wakulimawadogo kuanzisha miradi tofauti,kuangalia uwezekano wa kuwawezeshakupata mikopo kupitia vyama vyakuweka na kukopa, taasisi za kifedha,pamoja na kupunguza gharama zapembejeo, pamoja na kuwajengeauwezo wa kupata masoko kwa ajili yamazao yao ndani na nje ya nchi.Mwisho, tunaweza kusema kuwauanzishaji wa miradi mbalimbali kwawakulima wadogo wadogo ni jamboambalo linahitaji mtaji kidogo, jamboambalo linaweza kuleta unafuu kwawakulima. Miradi mbalimbali inasaidiakuimarisha kipato cha familia,na kutoa uhakika wa chakula, kiweni pamoja na uwezekano wa kupatachakula bora.Udhibiti wasiafu siyo rahisiNi vigumu sana kuwadhibiti siafupale wanapokuwa wamejenga makaziyao katika eneo fulani. Unaweza kunyunyiziamaji yenye magadi soda,au sabuni ya kuoshea vyombo.Unaweza kutumia kijiko kimoja chachai kwenye lita moja ya maji. Ukimwagamaji ya moto kwenye kiota chasiafu pia yanaweza kuwaangamiza.Mkojo pia huwafukuza siafu hasapale unapomwagwa kwenye kiotachao. Matandazo huwavutia siafukwa kuwa hula mimea inayo oza.Jaribu kuondoa aina hii ya mimeakatika eneo la kitalu ili kuwaondoasiafu.0717 266 007, 0785 133 005 0785 496036+255762001100 - Habari, ningependakujua kuhusu kilimo cha maua!naishiMbeya!nataka kujua kama hali ya hewaya Mbeya inaweza kufaa kwa kilimocha maua na pia ningependa kujuagharama za kuanzia kwa mkulimamdogo anayetaka kuanza biashara!Jibu: Tunashukuru kwa ujumbe wako,kwa sasa hatuna taarifa sahihi juu yakilimo cha maua, ila tutalifanyia kazina bila shaka utapata jibu lako.+255784838632 - Nimeona jarida lenu lamkulima mbunifu,mie ni mtaalam wamifugo toka wilaya ya iramba singida,je ninaweza kupata nakala zenu? EliasMbwambo, SLP 82 Kiomboi, Iramba,SINGIDAJibu: Bwana Elias hilo linawezekanakabisa, jaza fomu iliyopo kwenyenakala uliyopa, na ututumie taarifasahihi zinazohitajika, kisha utapatiwanakala kulingana na idadi ya wanakikundiwako.+255756468276 - Salaam sisi ni Kikundicha KIWAKAMA FOO tuliomba majaridatuka ahidiwa bado hatujapata.Jibu: Endapo mlitoa taarifa sahihi, basimfuatilie katika posta yenu kwa kuwakila wanao omba hutumiwa maramoja, vinginevyo muwe tu watulivukwa kuwa mara nyingine ni tatizo lamiundo mbinu katika nchi yetu.+255758221652 - Habari,mimi naitwaChrispin Mwamwezi,ninaishi UYOLE-MBEYA.Ni mfugaji wa kuku wa kienyeji.naitajivijalida vyenu.vyenyemaelekezo,dawa na kinga za kuku.Jibu: Bwana Chrispin unaweza kupatataarifa hizo katika toleo letu la 4.+255765914884 - Kunahitilafu ganiinapotokea sehemu fulani za shambamimeahufifia kukua baada ya yakuota vizuri licha ya kuweka mbolea.Jibu: Hali hiyo inaweza kutokana nasehemu hiyo kuwa na maji mengi,upungufu wa aina fulani ya virutubisho,au kuwepo kwa magonjwaambayo si rahisi mkulima kutambua.+255786883330 - Nashukuru kwa kuendeleakunitumia jarida la mkulimambunifu.kikundi chetu kinaendeleavyema nashukuru kwa kurekebishajina langu.Tunataka kujifunza zaidikuhusu ufugaji wa nguruwe na sokolake,Raphael B aluwa Nagawantu‘tunajali’ Mahenge.Jibu: Tunashukuru kwa taarifa hiyo,endelea kufuatilia matoleo ya MkulimaMbunifu yajayo pamoja na machapishomengine na utapata elimu zaidijuu ya ufugaji wa nguruwe. Kwa sasaunaweza kusoma tole la 4 la MkulimaMbunifu.+255753390755 - Habari ya kazi.Nimeona kwenye gazeti lenu kwambamnatoa CD je mnazo zinazo husianana ufugaji wa nyuki?Jibu: Naam CD hizo zina mada nataarifa mbalimbali, fuata maelekezoyaliyotolewa hapo, kisha utajipatianakala yako.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!