12.07.2015 Views

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

kwa maana ya kutaka kueleza kinachoendelea natunataka kufanya nini. Ndio maana nikasema aah!!,najua watanilaumu viongozi wa mhimili huo mwingine,lakini I think, I have got to say something.Sasa hiyo ofcourse imetafsiriwa na hata hapaniliona dada yangu Halima akajaribu kuhusisha najambo lingine nikasema ni bahati mbaya. Kwa sababuwakati ule hata habari hizo sikuwa nazo. Kwa hiyonilichokuwa nasema kilikuwa kinahusiana zaidi namgomo wa Madaktari na nikaahidi nitatoa kauliBungeni. Lakini jana kwa bahati nzuri, mpaka janausiku tumeshauriana pamoja na vyombo vingine vyamihimili ikaonekana bado hatuwezi sisi wakati jambohili limeahirishwa mpaka mwezi ujao sisi tukaendeleakutaka kulieleza mbele ya Bunge na mimi nika-respecthuo ushauri. Kwa hiyo, kama ilitafsiriwa vibaya lakiniangle yangu hasa nilikuwa naitaka kuizungumziailikuwa ni kwa sababu nilijua hilo liko mbele yangu.Lakini nikadhani pengine haitakuwa na madharamakubwa. Lakini nimeona ushauri ule mzito nimekubalina si ajabu hata kauli ile hatutaitoa itategemea Spikaatakavyoelekeza.Lakini la pili, ni hili la yaliyompata Dkt. Ulimboka.Kwanza nionyeshe masikitiko yangu juu ya jambo hili namimi namtakia kila la kheri apone haraka. It’sunfortunate kwa sababu process ilivyokuwa inakwendailikuwa ni nzuri kwa maana ya kwamba tuliaminitungefika mahali tungeelewana vizuri sana na nilikuwanimelenga juu ya mambo mengi.3

hili linaharakishwa sana. Kwa ufupi ninayowezakusema ndiyo maelezo niliyonayo. (Makofi)MHE. FREEMAN A. MBOWE – KIONGOZI WAUPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Waziri Mkuu, tumesikiatena hapa pengine Serikali inakusudia kutokutoa Kaulijuu ya tatizo hili.SPIKA: Tatizo lipi?MHE. FREEMAN A. MBOWE – KIONGOZI WAUPINZANI BUNGENI: Tatizo hili la mgomo wa Madaktarina tunavyozungumza hivi kuna taarifa kwenye vyombombalimbali vya habari kwamba Madaktari tayari katikaHospitali ya Muhimbili, Mbeya Referral Hospital,Bugando, KCMC na maeneo mengine mengiwameanza mgomo rasmi na hawaendi kazini leo.Kama Serikali inasubiri kutoa tamko kwa sababuya kusubiri pengine process ya Mahakama kuna hatuagani za makusudi, za ziada zinazochukuliwa na Serikalikutafuta angalau ufumbuzi temporary wa tatizo hilikwa sababu ni vifo vya watu vinakwenda kutokeakwa wingi sasa.Mheshimiwa Waziri Mkuu mnafanya interventiongani katika misingi ya dharura?WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, kwa maanapengine ya hatua ambazo Serikali inafikiria auimeamua kuchukua ni hatua ambazo ni za kawaida.Tulichofanya pale tumezungumza na vyombombalimbali ili tuone katika mazingira tuliyonayo ni5

kutekwa kwa Dkt. Ulimboka na majambazi nakuumizwa vibaya.Je, sasa Serikali inachukua hatua gani ilikuwaondolea wananchi hofu ambayo imeanzakupanda?WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwambayako matukio yamejitokeza ambayo kidogo yameanzakutupa wasiwasi hata upande wa Serikali. Hili laSerengeti ni mojawapo, lakini hata hilo uliloligusia lakusafirisha Waethiopia kupitia Tanzania nalo vilevilelimekuwa ni jambo kubwa.Lile la Ndugu yangu Ulimboka kama nilivyosemakwa sababu uchunguzi umeanza tutaona litakapoishia.Lakini kwa ujumla tu niseme hali ya uhalifu nchini nikweli kwamba yako matukio ya hapa na palemakubwa ambayo yanahitaji kutazamwa kwa harakasana. (Makofi)Kwa hiyo, uamuzi umeshafanywa na Serikali natulikuwa na Rais lakini ameona arudi Dar es Salaamkwa sababu ya kwenda kuzungumza mambo hayanadhani Baraza lile la Usalama la Taifa litajadili kwakina jambo hili ili liweze kutoa maelekezo sasa juu yahatua stahiki ambazo zinaweza zikachukuliwa ndani yakipindi hiki kifupi. (Makofi)MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika,ahsante. Mheshimiwa Waziri Mkuu suala la utafutajimafuta katika Visiwa vya Zanzibar ni moja kati ya kerokubwa katika kero za Muungano. Hivi karibuni Serikali7

ya Zanzibar kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya RaisMheshimiwa Mohamed Abood, alitoa kauli akisemakwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshatoataarifa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania kuhusu uchimbaji na utafiti wa mafuta katikaVisiwa vya Zanzibar akiweka wazi kwamba mafuta yaZanzibar yatachimbwa na Serikali ya Zanzibar.Huu ni msimamo mpya ambao umetolewa hivikaribuni. Je, Serikali ya Muungano inatoa msimamogani mpya juu ya suala hili la mafuta ya Zanzibar?WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, upatikanaji wamafuta una hatua nyingi, hatua ya msingi kabisa ni ileya mwanzo ya utafiti au uchunguzi. Ni kweli kwambakwa upande wa Tanzania Zanzibar hilo bado limekuwani eneo moja ambalo hata kwanza lilikuwa halijaanzakufanyiwa utafiti kutokana na sababu mbalimbali.(Makofi)Baada ya pale mkishapata ndio mnaingia katikahatua sasa yenyewe ya kuchimba mafuta. Lakini swalilako la msingi ni lile linalohusu hili hili eneo la mafuta napengine na gesi maana vyote vinakwenda pamoja.Kwamba Serikali ya Zanzibar imeamua jambo hililitasimamiwa na Serikali ya Zanzibar.Mheshimiwa Spika, ukiniuliza nasema wala sionitatizo hata kidogo, sina mgogoro na jambo hili.Nasema hili kwa moyo mkunjufu tu kwamba kwanguZanzibar ikipata mafuta sidhani kama Tanzaniatutakosa kitu chochote. Tutakachofaidi ni kwambatutayapata mafuta pua na mdomo. Kwa hiyo,8

itakuwa rahisi sana, gharama nafuu sana kuliko ikiwambali zaidi.Tatizo tu ni lile la kisheria na Kikatiba, lakini upandewa Tanzania na sisi kama unavyosema jambo hilitumekwishaanza kulifanyia kazi nadhani wakatiwowote litapelekwa kwenye cabinet kwa maana yakufanya uamuzi wa msingi ili turuhusu hili jamboliendelee wakati taratibu nyingine hizo za kuja kuondoaau kutokuondoa kwa sababu Katiba liko kwenyeschedule basi ikifika likute hilo jambo liko mikononi kwawahusika. Kwa hiyo, binafsi nadhani halina mgogoromkubwa sana. (Makofi)MHE. KHATIB SAIDI HAJI: Ahsante sanaMheshimiwa Spika na ahsante Mhesimiwa Waziri Mkuukwa jibu zuri lenye matumaini.Mheshimiwa Waziri Mkuu, je, suala hili la utafutajiwa mafuta Zanzibar unadhani kwa mawazo yakolitatupeleka mpaka kwenye Katiba mpya au ufumbuziwake unaweza ukapatikana katika siku za karibuni?WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Khatib ninachosema tuhapa ni kwamba nataka hili jambo litazamwe kwamaana ya hatua za sasa. Kwamba kutafuta mafutainachukua miaka 7 au 8 ni muda mrefu sana na kipindichote kile inakuwa ni uchunguzi.9

Mimi kimtazamo nasema kwa upande wa Serikaliya Muungano ni vizuri tukaliona kwa nia njemakwamba turuhusu ule uchunguzi angalau wa katikahatua za awali uanze tu sababu hatujuikitakachotokea pale ni nini.Suala la kuliondoa kwenye eneo lile bahati nzurituko katika mchakato wa Katiba Mpya linawezalikafika wakati ule na pengine tutakuwa hata mafutayenyewe hatujayaona bado, lakini ni vizuri tukaanzabila kuchelewa ili tuwape nafasi waweze kufanya hiyokazi.MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Spika, ahsantesana. Kwa muda mrefu tumekuwa tukigharamia Mbioza Mwenge ambazo zimekuwa zikihamasisha nakufungua miradi ya maendeleo.Mheshimiwa Waziri Mkuu, hadi sasa Serikaliinaweza kuliambia nini Taifa faida jumla na hasaraambazo zimekuwa zikipatikana katika mbio hizi zaMwenge? (Makofi)WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, kila Taifa linamambo ambayo ingependa yawasaidie wananchiwake kuwakumbusha mambo fulani fulani. Upandewetu sisi tuliona kwamba pengine suala hili la kukimbizaMwenge linaweza kuwa linatusaidia kuwakumbushaWatanzania mambo fulani fulani ya msingi. Ndiyomaana unakuta hata Olympic wanakimbiza Mwengena unazunguka mpaka huku nchi nyingine,tunakwenda tunaupokea, kuna vitu ambavyomnakuwa mmedhamiria kuvifanya.10

Hasa kwa upande wa Tanzania Mwengeunatukumbusha mambo mengi na hasa ni kauli yaBaba wa Taifa alipokuwa anawasha Mwenge alitoamaneno ambayo yalikuwa ni mazito sana “Kwambanataka uwekwe juu ya Mlima Kilimanjaro itoematumaini kwa watu, iendeleze amani tujaribukujenga.” Ile hisia za mshikamano na maendeleoilikuwa hasa ndio lengo la kutaka tukumbushane.Ndiyo maana tunapoukimbiza tunatumia fursa hiyomara nyingi kuwa na kauli mbiu fulani fulani.Sasa Mwenge una nguvu sana kwa sababuunavuta watu wengi, unapita maeneo mengi. Kwahiyo kaulimbiu zile SENSA, UKIMWI, MAENDELEO nakadhalika, unaufikisha kwa watu kwa namna ambayoni rahisi na haina tatizo. (Makofi)Lakini pili, tumetumia sana Mwenge hasa kwenyekuwafanya watu watumie muda zaidi kidogo katikaMiradi ya Maendeleo. Ndiyo maana katika Mwengeunakuta tunazindua miradi mingi sana, tunawekamawe ya msingi mengi sana na kadhalika. Kwa kwelikimsingi nasema ni jambo jema na ni vizuri tusiliachebila ya sababu. (Makofi)SPIKA: Ahsante sana. Kama hakuna haja ya swalila nyongeza sio lazima uulize.MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Waziri Mkuu,je, Serikali inatambua manung’uniko ya wananchi ya11

kwamba kunapokuwa na mkesha wa mbio hizo zaMwenge kunafanyika zinaa ambayo ni kicho cheocha UKIMWI? (Makofi)WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Haji zinaa inafanyikapopote tu na kila mahali. Ndio!! Kwa hiyo kusemakwamba wakati wa Mwenge ndio zinaa inafanyika,mimi nadhani hatuutendei haki Mwange hata kidogo.Maana binadamu tulivyo tukianza kutafutana hapakwenye eneo hilo sijui mtasema nini, nadhani ukwelindio huo.SPIKA: Night clubs zipo. (Makofi/Kicheko)MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana.Mheshimiwa Waziri Mkuu, moja kati ya sababuzilizosababisha mfumko wa bei nchini ni chakula.Serikali katika kukabiliana nalo imekuwa ikijaribu sanakutawanya chakula kwa gharama kubwa kutokamaeneo ya uzalishaji na kupeleka sehemu nyingine.Kwa kuwa Mkoa wa Rukwa na Katavi ina idadikubwa sana ya chakula, mwaka huu peke yake Mkoawa Rukwa unatarajiwa kuwa na akiba ziada ya tani229,777.Je, Serikali haioni kuunganisha eneo hili la uzalishajina reli ili kupunguza gharama hii ambayo imekuwaikiingia kwa kutumia usafiri wa malori ambayo nigharama sana.12

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, sikumpata vizuri.Amesema meli Reli.MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Reli Mheshimiwa.WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, maana manenohaya meli na reli ukiwa mbali kidogo tabu kutofautishalakini vyovyote vile ninachoweza kusema kwambakwanza nikiri kwamba Rukwa kwa ujumla pamoja naMkoa mpya wa Katavi ni kweli una wazalishajiwakubwa sana wa chakula na hasa mahindi na tatizoletu sisi ni namna ya kuondoa mahindi kwenye eneohilo kuyapeleka maeneo yenye mahitaji ama kwakutumia reli ama kwa kutumia barabara vyovyotetunavyofikiri ni njia ambazo zingeweza kusaidia. Sasakwanza nikubaliane na wewe kwamba hiyo nichangamoto kwa upande wetu.Lakini niamini kabisa kwa mpango wa maendeleoulivyowekwa reli hii ya kati itakavyoanzakukarabatiwa pamoja na ile ya Mpanda na kwendaKigoma tunaamini tunaweza kuboresha sana hudumahiyo kupeleka mahindi kwenye maeneo mengine.Lakini si hiyo tu, iko haja vilevile ya kufungua barabaraya kutoka Mpanda kwenda Tabora, kupitia Sikongekwa njia ya lami. Tukifanya hivyo hili nalo litakuwa ninjia nyingine rahisi sana ya kupeleka vyakula hasakwenye maeneo ya Kanda ya Ziwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini niongeze vilevile kwambahata kama tungepata usafiri wa meli ungeweza13

kutusaidia sana kufikisha angalau pale Kigoma,Kigoma mnaingiza kwenye treni nayo ingeweza kuwanjia nyingine. Kwa hiyo, tutajitahidi kuona kila njiaambayo tunafikiri inaweza kutusaidia kuboreshausafirishaji wa mazao haya.SPIKA: Ahsante sana. Sasa nitamwitaMheshimiwa Tundu Lissu.MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu mwezi wa piliMadaktari walipogoma hili suala ulilichukua wewemwenyewe na ukalishughulikia na baadaye taifalikatangaziwa kwamba Madaktari hawatagoma tena.Haijapita miezi mitatu Madaktari wamegoma nchinzima. Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwaniniusiwajibike kwa kujiuzulu kwa kushindwa kutatuamatatizo ya Madaktari wetu. (Makofi)SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu.WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, yapo mazingiraunayoweza ukawajibika kwa njia hiyo lakini si lazimayakawa yote. Mimi sioni kama hili ni moja kati yamaeneo ambayo unaweza ukasema kistahiki hivinaweza nikafikia hatua hiyo. Ninacho-appreciate nikwamba tatizo hili ni kweli ni la muda mrefu lakini I havedone my best kujaribu kulitatua kwa kiasi kikubwa sana.Ndiyo maana nasema ukinifikisha pale na miminitakuwa na maelezo vilevile kueleza ni nini nimefanyakatika jitihada za kujaribu kulimaliza.14

Lakini being what It is inabidi tukubali kwambabado linachangamoto nyingi kwa sababu ya mambomengi tu ambayo yameingiliana na mgogorowenyewe. (Makofi)SPIKA: Mheshimiwa Tundu Lissu swali la nyongeza.MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu if you havedone your very best and you have failed why don’t youresign? (Makofi/Kicheko)SPIKA: Hilo swali linarudia swali lilelile. Naombausijibu kwa sababu linarudia lilelile.WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Tundu Lissu hiyo si lughanzuri sana. Mimi nakuheshimu sana. Lakini sidhanikama that is the best approach ya kuzungumza nawakubwa. (Makofi)SPIKA: Tunaendelea na Mheshimiwa MarthaMlata.MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Waziri Mkuu,kwa kuwa ziko habari zinazosambaa katika jamiikwamba madhara haya makubwa yanayotokana namgomo wa Madaktari unasababishwa na baadhi yavikundi vya watu ambavyo vinawatumia baadhi yamadaktari kwa kuwapa fedha ili waendewakahamasishe mgomo na kulazimisha baadhi yaMadaktari kwa sababu wanataka eti nchi isitawalike.Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuwa mgomo wamadaktari una madhara makubwa sana katika taifa15

hili. Je, Serikali sasa iko tayari kuchunguza ukweli huu nauvumi huu ili kuona ukweli uko wapi tuweze kuokoamaisha ya Watanzania wanaokufa bila hatia?Ahsante sana. (Makofi)WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, mgogoro huuwa madaktari una maneno mengi sana. Hilounalolisema dada yangu Mlata na mimi vilevilenimelisikia lakini tulishaomba vyombo vyetu vya ulinzina usalama vijaribu kulifuatilia tuone kama lina ukweliwowote ndani yake. Kama tutapata maelezoyanayotosheleza kuonyesha kwamba kuna ukweli huobasi nadhani hatua zinazostahili zitachukuliwa.(Makofi)MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika, miminashukuru kwa majibu ya mazuri. Sasa MheshimiwaWaziri Mkuu kwa kuwa pamoja na kwamba Serikalihaina dini lakini watu wake wana dini. Je, uko tayarikuomba taasisi zote za dini zikafanya maombi kwa ajiliya kuwaombea watu hawa wabaya wanaotakakuharibu usalama wa taifa letu. (Makofi/Kicheko)WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, mimi siyomcha Mungu, lakini ni Muumini wa dini vilevile. Rai kwamaana ya rai na pengine usi-confine tu kwa hawawabaya. Mimi nadhani tuliombee taifa hili amani kwaujumla. Mimi nataka niwashukuru sana viongozi wamadhehebu ya dini ambao kila kukicha wanaliombeataifa hili amani. Kwa sababu the bottom line vyovyotevile itakavyokuwa bila amani nchi hii hakunakitakachofanyika. Kwa hiyo, mimi nadhani rai ni nzuri16

tutaendelea kuwaomba waendelee kuliombea taifakwa kadri itakavyowezekana.SPIKA: Wewe mbona hauko kwenye orodha.MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Spika, kuhusuutaratibu.SPIKA: Naomba tafadhali tuendelee. Kwenyekipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu hakuna Kanuniinayosema tutafanya mwongozo. TuendeleeMheshimiwa Hemed.MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Spika, siomwongozo ni kuhusu utaratibu.SPIKA: Mheshimiwa Wenje tusibishane.Mheshimiwa Salum Hemed Khamis. Pole sanatumefurahi kukuona.MHE SALUM HEMED KHAMIS: Mheshimiwa Spika,nakushukuru nilidhani umeshaniruka. Maana kwenyeorodha mimi ni mtu wa nne. Mheshimiwa Waziri Mkuutarehe 28 Agosti, 2008 nilikuuliza swali hapa katikakipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kuhusu ahadi yaSerikali ya Muungano juu ya kifuta machozi cha familiaza wahanga wa maandamano ya tarehe 26 na 27Januari 2001 kule Zanzibar ambapo watu 23 waliuawakwa kupigwa risasi na Polisi na taarifa hizo ni kwamujibu wa Serikali yenyewe. Lakini kwa sababu ulikuwabado ni Waziri Mkuu mpya ulimwomba Naibu Spikaambaye sasa hivi ndiye Spika mwenyewe akupe mudawa kufuatilia sakata lile. Januari mwaka huu tayari17

imetimia miaka 12 tangu mauaji yale yafanyike nanadhani karibu miaka minne toka ulipoahidi kulifuatilia.Wakati tunaongea sasa hivi familia za wahanga naWazanzibar kwa ujumla wanakuona na wanakusikiliza.Je, naomba uwaambie ni kwanini ahadi ileimechelewa hadi leo.WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nimjiburafiki yangu Salim kama ifuatavyo:-Ni kweli tukio hilo lilitokea na ni kweli jambo hilolilipewa ahadi ya namna fulani ya kifuta machozi namimi baada ya kuniuliza siku ile nilijaribu kulifuatilia lakinihalijapata ufumbuzi.SPIKA: Mheshimiwa Salim swali la nyongeza.MHE. SALIM HEMED KHAMIS: Mheshimiwa Spika,inasikitisha ikiwa wafugaji wa Loliondo, Monduli naNgorongoro wamepewa kifuta machozi karibu shilingibilioni 633 kwa sababu ya kupoteza mifugo yaokutokana na ukame. Leo watu ambao binadamuwamepoteza ama mke ama mume au mtoto naSerikali imeahidi lakini mpaka leo hakuna ufumbuzi. Je,hapa kuna nia thabiti ya kupeleka hiyo ahadi kamailivyotolewa au ni ubabaishaji?WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ahadi ni deni.Mimi naamin tuvute subira jambo hili lina mambomengi litakapokamilika nina hakika litatoa majibu yake.SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuumaswali yamekwisha na wewe tunakushukuru sana18

kwa majibu na nawashukuru Waheshimiwa Wabungekwa kuuliza maswali. Kwa kifupi na tumewezakumaliza wale wote waliomba kuzungumza.Tunaendelea na Order Papaer, Katibu.MASWALI NA MAJIBU YA KAWAIDASPIKA: Tunaendelea, Mheshimiwa Peter Kafumuatauliza swali la kwanza.Na. 94Ukubwa wa Jimbo la IgungaMHE. DKT. DALALY P. KAFUMU aliuliza:-Jimbo la Igunga lina eneo kubwa na wakazi zaidiya 500,000. Sasa je, ni lini Serikali italigawa Jimbo hilona kufanya Majimbo mawili ili kurahisisha uwakilishi nakutoa huduma nzuri zaidi?WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA,URATIBU NA BUNGE) alijibu:-Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.Dalaly Peter Kafumu, Mbunge wa Igunga, kamaifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, wakati wa kugawa Majimboya Uchaguzi mwaka 2010 kabla ya Uchaguzi Mkuu,Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliweka vigezo na utaratibuwa kupokea maombi ya kugawa majimbo kutoka19

Halmashauri mbalimbali. Tume ilipokea maombi 53yakiwemo maombi kutoka Jimbo la Igunga. Kati yamaombi hayo maombi 42 yalitimiza vigezo likiwemoJimbo la Igunga.Hata hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi haikuwezakuligawa kutokana na ufinyu wa Bajeti ya kuendeshaBunge lakini pia nafasi ya Ukumbi wa Bunge naongezeko la Wabunge wa Viti Maalum kutoka 75mpaka 102. Hivyo tume iliweza kugawa Majimbo sabatu kati ya Majimbo 42 yaliyokuwa yamefikia vigezo.Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Katiba ya Nchiinatoa mamlaka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzikuchunguza mipaka ya Majimbo kwa vipindi maalum,Tume wataendelea kutekeleza jukumu lake hilo napale ambapo zoezi hilo litafanyika tena Jimbo laIgunga litafikiriwa kugawanywa kwa kuzingatia vigezovitakavyowekwa. (Makofi)MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Spika,namshukuru sana Waziri kwa majibu yake mazuri nanategemea baadaye Igunga nayo itapendelewa iwekati ya yale yatakayogawanywa awamu inayokuja.Naomba sasa nimwulize swali moja la nyongeza. Kwakuwa ni dhahiri kuwa eneo la Jimbo la Igunga ni kubwana kwa kuwa Jimbo hili linapokea wananchi wenyemifugo kutoka maeneo mengine wanahamia.Idadi ya watu katika Jimbo hilo inaongeza sana.Je, Serikali itakuwa tayari baada ya Sensa ya mwezi wanane idadi ya watu itakapojulikana itakuwa tayarikuruhusu mchakato wa maombi yetu tutakayoleta ya20

kuligawa Jimbo la Igunga kuwa Wilaya mbili yenyeJimbo moja moja?WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA,URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, mimi naombaMheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wotetusubiri zoezi kubwa zaidi linalokuja la mapitio ya Katibakwa sababu kwanza hata utaratibu wa Tume wakufikiria huwa unaenda kila baada ya miaka kadhaa.Haiendi kila mwaka na sio kila kipindi kimoja Tumeinafanya jambo hilo. Kwa hiyo kimsingi ningeombatuvute subira kwa sababu mimi naamini yapo mambomengi sana ambayo yanahitaji kurekebishwakutokana na mwenendo wa uchaguzi.Jana tumeulizwa swali na Mheshimiwa Mbungewa Viti Maalum kupitia Mkoa wa Dodoma juu yauchaguzi mdogo. Watu wengine wanafikiri hata byelectionszisiwepo. Kwa sababu by-election moja kamaile ya Igunga au ya Arumeru ina-cost Serikali shilingibilioni 1.57. (Makofi)Sasa ukiacha fedha za vyama vilivyoshiriki,ukiacha na wapambe wengine, vyombo vya habarizinatumika fedha nyingi na hizi zote huwa hazikokwenye Bajeti. Ikitoka by-election basi Serikaliinakwenda kuchota Hazina ambazo hazikuwa kwenyeBajeti kwa sababu huwezi kubajeti kitu ambachohakipo na zinatumika 1.57 billion kwa ajili ya jambokama hilo.21

Kwa hiyo, yapo mambo mengi sana ambayotukitengeneza Katiba yetu vizuri inawezekana hatamfumo wa uchaguzi, idadi ya Majimbo na utaratibuwa uendeshaji wa uchaguzi ukabadilika.MHE. FELIX F. MKOSAMALI: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwainakosea katika ugawaji wa Madiwani wa Viti Maalumkatika maeneo mengi sana nchini. Je, Serikali iko tayarikulichunguza jambo hili?SPIKA: Mheshimiwa Mkosamali, unasema ugawajiwa nini? Majimbo ya Madiwani au what?MHE. FELIX F. MKOSAMALI: Mheshimiwa Spika, VitiMaalum vya Udiwani vinavyogawanywa kwenyeHalmashauri zetu nchini wamekuwa wanakosea katikakufanya mchakato huu katika maeneo mengi. Je,Serikali iko tayari kulifuatilia jambo hili ili kubaini ukwelina mimi niko tayari kutoa ushahidi wa makosa ambayowamekuwa wanayafanya?SPIKA: Tunalikubali tu lakini ilikuwa kugawaMajimbo, sasa kugawa Madiniwani tena. HayaMheshimiwa Waziri wa Nchi.WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA,URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, ikiwa kamaMheshimiwa Mkosamali ana tatizo kama hilo na linavielelezo na anaushauri namshauri mambo mawili.Anaweza kulifikisha jambo hilo kwenye Tume22

likachunguzwa au unaweza ukanipa mimi ambayendiye mwakilishi wao hapa nikapeleka likachunguzwa.Haina tabu.Na. 95Kurejesha Magari ya Wagonjwa yaliyohamishwaMHE. MARIA I. HEWA (K.n.y. MHE. DKT. TITUS M.KAMANI) aliuliza:-Magari mawili ya wagonjwa yaliyokabidhiwakatika kituo cha afya cha Nasa na Zahanati yaLukungu mnamo mwezi mei, 2010 yaliondolewa naHalmashauri ya Wilaya ya Magu na hivyo kutokufanyakazi katika vituo hivyo kama ilivyokusudiwa:-Je, Serikali itarejesha lini magari hayo ili yatumikekwa malengo yaliyokusudiwa?NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:-Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.Titus Mlengeya Kamani, Mbunge wa Busege, kamaifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Halmashauriya Wilaya ya Magu mwaka 2010 ilipata magari mawiliyenye namba za usajili T 848 BFP na T 854 BFP aina yaFiat Ducato Ambullance kwa ajili ya kusaidia huduma23

ya kubeba wagonjwa katika Halmashauri ya Wilaya yaMagu.Magari hayo yalitolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikaliijulikanayo kama Community Development ReliefAgency ya mjini Magu. Magari haya yalipokelewa naaliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Busega kwa wakatihuo, Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni naaliyakabidhi katika kituo cha Afya Nassa na Zahanatiya Lukungu mnamo mwezi Mei, 2010. Magari hayahayakuwa mapya yalikuwa yametumika huo nchi zaUlaya.Mheshimiwa Spika, magari haya yalifanya kazikwa takribani miezi mitatu tu baada ya kukabidhiwana kisha yalianza kusumbua, hivyo ilibidi yahamishiwekwa mhandisi wa Halmashauri ili mafundi wawezekuyafanyia uchunguzi wa kina. Ukaguzi ulibaini kuwamagari haya yalikuwa na matatizo makubwa ambayoyalihitaji matengenezo makubwa pamoja nakubadilishwa vipuri mbalimbali. Baada ya hatua hii,zoezi lililofuatia lilikuwa ni kuandaa vidadisi bei nakupelekwa kwa wazabuni. Wazabuni walishindwakujaza vidadisi bei kutokana na ugumu wa kupatikanavipuri vya aina ya magari hayo. Magari hayohayakuondolewa bali yalirudishwa Halmashauri kwaajili ya matengenezo ili yaendelee kutoa hudumakatika Zahanati ya Lukungu na kituo cha Afya Nassa.Mheshimiwa Spika, magari hayo yamehifadhiwakatika yadi ya Halmashauri yakisubiri utaratibu tijakama itakavyoamuliwa na uongozi wa Halmashauri.Halmashauri kwa sasa inaendelea kuwahudumia24

wananchi wake wote kwa kutumia magari matanoyaliyopo katika vituo vya Afya vya Kisesa, Nyanguge,Igalukilo, kabila na gari lililopo katika hospitali ya Wilayaikiwemo Zahanati ya Lukungu na Kituo cha Afya Nassa.(Makofi)MHE. MARIA I. HEWA: Mheshimiwa Spika,ninashukuru kwa majibu yaliyotolewa, ninachotakakuuliza baada ya wahandisi kushindwa kujaza mamboyanayoitwa vidadisi bei na sasa ni awamu tatu zaBajeti tangu mwaka 2010 mpaka leo tunajadili Bajetiya 2012/2013. Wizara kama Wizara inawasaidiajewatu hawa ambapo wanasubiri utaratibu ambaoutaleta tija ni utaratibu upi ili muwasaidie haya magari.Aidha yauzwe au kitu kingine kifanyike?Mheshimiwa Spika, la pili wakati process hiiinafanyika ilikuwa Magu moja sasa Busega imemegekaninaamini haina hili gari linalozungumzwa la wagonjwa.Mheshimiwa Waziri unaifikiriaje Busega kupata gari lakujitegemea?NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) :Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa WaziriMkuu ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Maria Hewa kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, hili jambo analolisemaMheshimiwa Maria Ibeshi Hewa ni kweli na hivitunavyozungumza hapa RAS yupo ananisikia hapa waMkoa huu wa Mwanza ambao kwa kipindi hiki champito bado anakaa pale. Tunayo barua25

nimezungumza na Kordeli Ngurudungi ambaye ndiyeMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yaMagu kuhusu jambo hili linalozungumzwa hapa naakaniambia kwenye barua ile ambayo wameandikiwakutoka kwenye ofisi ya RAS ilielekezwa kwambatuangalie uwezekano wa kuyauza haya magari nahapa nimeitaja hii Community Development and ReliefAgency ambayo ndiyo iliyotoa msaada huo, wakopale mpaka sasa hivi tunapozungumza hapa. Kwahiyo, ukitaka kuuza pale lazima urudi kwa yulealiyekupa gari ili kupata ridhaa yake kwamba ufanyehivyo au usifanye hivyo ndicho ambacho kimebakipale.Mheshimiwa Spika, sasa kuna tatizo hili la vipurikama nilivyoeleza hapo mwanzo ni tatizo kubwa sasawataangalia na wakishaafikiana na yule mtoaji wa huomsaada wanaweza wakaenda katika hatua hiyoinayozungumzwa.Pili, anazungumzia kuhusu hii Development mpyani kweli sasa tunazungumza hapa Busega ni Wilayampya utaratibu wa nchi wakati unapokuwaumegawanya mamlaka hizi na tawala hizi zinatakasasa Halmashauri ile ikae pamoja na ile nyingine wotekwa pamoja wagawane mali pale. Kwa hiyo, sasa hivitunapozungumza hapa huduma zote zinatoka kwenyeile Halmashauri Mama kwa maana ya Magu.Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, wakati utakapofikawataketi wale wa Magu na hawa wa Busega watakaavizuri. Cha kuchunga hapa ni ku - maintain uhusianomzuri kati ya hizi Wilaya mbili mpya kwa sababu Wilaya26

ile iliyoanzishwa mpya kwakuwa Wilaya mpyailiyoanzishwa ndiyo huwa ina- suffer. Kwa kawaidatukiangalia utaratibu unavyokuwa na ninatoamaelekezo hapa mpaka tutakapokuwa tumeundaHalmashauri ya Wilaya ya Busega huduma zotemuhimu pamoja na Ambulance na vile vingine vyotevinavyotolewa kule vitaendelea kutolewa naHalmshauri ya Wilaya mama. (Makofi)SPIKA: Mheshimiwa Richard Ndassa.MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika,kwa sababu Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kupitiakituo chake cha Afya cha Nyambiti hakina garitufanyeje ili tupate gari?SPIKA: Mheshimiwa Richard Ndassa yaani weweunauliza tu na mimi nataka gari sasa tutafanyaje?Naomba hilo swali walilete wakati wa Wizara ya Afya.Tunaenda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waKimataifa Mheshimiwa Haji Khatibu Kai atauliza swali.(Makofi)Na. 96Itifaki ya Viongozi NchiniMHE. HAJI KHATIB KAI aliuliza:-Kutokana na mabadiliko ya Katiba ya Tanzania,Zanzibar ya kuwa na Serikali yenye Muundo wa Umojawa Kitaifa kumesababisha ongezeko la viongozi huko27

Tanzania, Zanzibar hivyo kuchanganya itifaki yaviongozi wa kitaifa wa Tanzania?NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA (K.n.y. WAZIRIWA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA)alijibu:-Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifanapenda kujibu swali la nyongeza la Mbunge waMicheweni kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, ni kweli kutokana namabadiliko ya Katiba ya Zanzibar mwaka 1984, hasaSura ya nne inayozungumzia muundo wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar, imepelekea utaratibu waKiitifaki kwa viongozi wa kitaifa kubadilika, mabadilikohaya ya mwaka 2010, katika Katiba ya Zanzibaryameondoa kiti cha Waziri Kiongozi kama ilivyokuwaawali na kuanzisha utaratibu wa makamu wa kwanzana Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar. Kutokana nahali hii, itifaki ya sasa kwa viongozi wa Kitaifa ni kamaifuatavyo:-1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania;3. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi;28

4. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania;5. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar; na6. Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar.Mheshimiwa Spika, ni matumaini ya Wizarakwamba kwa maelezo haya, naamini kwamba kuanziasasa hakutakuwa na utata wa Itifaki ya Viongozi waKitaifa. (Makofi)MHE: HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Spika,ahsante SANAkwa kunipa nafasi kuuliza maswalimawili ya nyongeza yenye kifungu (a) na (b) kwakuwa, cheo cha Waziri Mkuu ni cha kuteuliwa na Raisna kwa kuwa, Rais wa Zanzibar amechaguliwa nawananchi. Je, kiitifaki Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibarni nani mkubwa kiutawala?SPIKA: Hili la ukubwa tena itifaki siyo ukubwa haya.Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA (K.n.y. WAZIRIWA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA):Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifanapenda kujibu swali la nyongeza la Mbunge waMicheweni, kama ifuatavyo:-Kwanza kabisa kwenye jibu langu la msinginimeeleza na iko dhahiri kabisa na masuala ya Itifikihayaonyeshi nani ni mkubwa. Lakini pia masuala29

haya yako kikatiba na nimeeleza dhahiri kabisakwamba anaanza Rais wa Jamhuri ya Muungano, wapili anafuata Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano, na wa tatu ni Rais wa Zanzibar, wa nne niWaziri Mkuu. ( Makofi).MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Spika, kwamajibu aliyotoa Naibu Waziri kwamba Serikaliinatambua protocol iliyopo kwa Makamu wa Raiswawili wa Zanzibar. Ukisoma Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania haitambui Makamu wa Raiswawili wa Zanzibar, bali inatambua Waziri Kiongozi.Je, hamwoni kwamba kwa protocol hiyomnavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania?NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA (K.n.y. WAZIRIWA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA):Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa napenda kujibu swali lanyongeza la Mheshimiwa Ezekiel Wenje, Mbunge waNyamagana.Kwanza kabisa wote mnatambua kwambamabadiliko haya ya Katiba ya Zanzibar yalikuja mwaka2010 na wote tunatambua kwamba na sisi katikaJamhuri ya Muungano tuko katika wa kuleta maoni yaKatiba mpya hivyo basi tusubiri yoyote mwenyemapendezo yake asubiri wakati huo aweze kutoamaoni na ninaamini suala hili litashughulikiwaipasavyo. (Makofi)30

Na. 97Matumizi ya Sheria ya Ununuzi wa Vifaa vyaSerikali Na. 21/2004MHE. DKT. MARTY M. MWANJELWA aliuliza:-(a) Je, ni kwa nini licha ya kuwa na Sheria Na. 21ya Mwaka 2004 ya Ununuzi wa vifaa vya Serikali zoezi lakutangaza zabuni zilizokwisha tangazwa na Wakala wahuduma ya ununuzi wa Serikali bado zinaendelea?(b) Je, ni hatua gani zitakazochukuliwa dhidi yaHalmashauri na Taasisi za Serikali zinazoendelea kukiukaSheria hiyo mpya na kuleta mkanganyiko miongonimwa Wazabuni?(c) Je, Serikali haioni kuwa jambo hilo linawezakuiingizia gharama kubwa na upotevu wa fedhazinazotokana na kodi za wananchi?NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa fedha,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. MaryMachuche Mwanjelwa, Mbunge viti Maalum, kamaifuatavyo:-(a) Ni kweli kabisa baadhi ya Taasisi za Ummazikiwemo Halmashauri zinaendelea kutangaza zabunizilizokwisha kutangazwa na Wakala wa Huduma yaununuzi Serikalini kwasababu zifuatazo:-31

(i) Uelewa mdogo juu ya mfumo wa ununuzi wapamoja wa vifaa na huduma mtambuka.(ii) Sheria ya ununuzi wa Umma Na. 21 ya 2004,kutotamka wazi kwamba, Taasisi za Umma shartizitumie utaratibu wa kununua kwa pamojautakaoandaliwa na Wakala wa Huduma ya UnunuziSerikalini.(b) Hatua zilizochukuliwa na Serikali baada yakugundua kuwa baadhi ya Taasisi za Ummazinaendelea kutangaza zabuni zilizokwisha tangazwana Wakala ni pamoja na:-(i)Serikali ilitoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu,Wakuu wa Idara zinazojitegemea, Watendaji Wakuuwa Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali TanzaniaBara, tarehe 18 Juni, 2010 waraka namba CFA/140/150/01/09 iliyozielekeza Taasisi za Umma kutumiamikataba iliyoandaliwa na Wakala kufanya Ununuzi waPamoja wa vifaa na huduma mtambuka.(ii) Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalinialiendesha mafunzo tarehe 5 Mpaka tarehe 15Machi, 2011 kwa nchi nzima kwa watumishi 4,016 kwaTaasisi za Umma wanaoshughulika na masuala yaununuzi pamoja na wafanya biashara. Aidha Serikaliimefanya mapitio ya Sheria ya ununuzi wa UmmaNamba 21 ya 2004 na kuweka vifungu vinavyoelekezaTaasisi za Umma kutumia mfumo huu.32

(c) Ni kweli kwamba Taasisi za Umma kuendeleakutangaza Zabuni kutaiingizia Serikali gharama kupitiaeneo la ununuzi wa Umma. Hivyo basi, Serikaliimeamua kurekebisha Sheria ya ununuzi wa umma nakuainisha wazi matumizi ya mfumo huu. (Makofi)MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA: MheshimiwaSpika, pamoja na majibu mazuri ya Waziri ningependakuuliza maswali mawili ya nyongeza yenye (a) na (b)kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mikataba mingiimekuwa kwa upande mmoja tu wa Serikali na adhabukutolewa kwa mkandarasi akishindwa kutekeleza.(a) Je, Serikali au Taasisi zinaposhindwa kumlipamkandarasi kwa uzembe akimaliza kazi kwa mudainakuwaje?(b) Sheria mpya ya manunuzi pamoja na kanunizake itaanza lini? Ningeomba Mheshimiwa NaibuWaziri atujulishe kuwa itaanza lini kutumika ili kuokoafedha za walipa kodi zinazopotea kutokana namatumizi mabovu, nashukuru. (Makofi)NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kwaniaba ya Waziri wa fedha, napenda kujibu swali laMheshimiwa Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa,Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, suala lake la mwanzo lilihusianana vipi Serikali ikiwa inashindwa kumlipa mkandarasi.Kwa kawaida mikataba inakuwa imeeleza wazi33

perlatus ambazo zimo katika mkataba ule kwa pandezote mbili. Kwa hiyo, mikataba ile inakuwa inaonyeshawazi vipi kama Serikali itakuwa inakiuka taratibu husaniwakati wa malipo mara nyingi tunakuwa tunalipainterest kwa kuchelewa kulipa mkandarasi.Lakini matumizi ya Sheria mpya kama nilivyoelezakatika suala langu la msingi kwamba kulikuwa namarekebisho hususani yanayohusiana manunuzi yajumla. Kwa hiyo, sheria hiyo inatumika lakini Sheria hiiikiwa itafanyiwa maboresho na tuko katika mchakatowa kuanza kukusanya maoni na Wabunge vilevilemtahusika once tukiwa tumemaliza na kusainiwa Sheriahiyo itaanza kutumika rasmi.MHE. SUSAN L. A. KIWANGA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwa kuwa, katikaHalmashauri nyingi nchini zimetunga Sheria zinazokiukaSheria ya ushuru wa mazao uliotangazwa mwaka 2002na aliyekuwa Waziri wa Serikali za mitaa Brigedia Gen.Hassan Ngwilizi.Je, Serikali inatueleza nini sasa ushuru huounaotozwa kwa Sheria zilitungwa katika Halmashauriambapo inakiuka Sheria mama tangazo la Waziri nahaijafutwa mpaka leo na wananchi wanataabikakatika Halmashauri mbalimbali?SPIKA: Mheshimiwa Susan huoni kuwa ilikuwaProcurement wewe umeenda kwenye mazao? HayaMheshimiwa Jitu Soni oh! umeshaondoa swali lakohaya tuendelee na sijaona mtu mwingine na34

tunaendelea na swali linalofuata Mheshimiwa ClaraMwatuka, swali linalofuata.Na. 98Riba Kubwa Kwa Mikopo ya SACOSS na VICOBAMHE. CLARA D. MWATUKAaliuliza:-Lengo la Serikali katika kuhamasisha wananchikuunda vikundi vya SACCOS na VICOBA ni kuwasaidiakujikwamua kiuchumi:-(a) Je, Serikali inasemaje kuhusu riba kubwawanayotozwa wananchi kutokana na fedha zaowanazoziweka benki?NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Clara Diana Mwatuka, Mbunge wa vitimaalum, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, viwango vya juu vya ribavinavyotozwa na Taasisi na asasi za fedha vinatokanana sababu mbalimbali ikiwemo sera yenyewe ya Taifaya Taasisi ndogondogo za fedha (Microfinance).Sera inatamka kwamba, viwango vya riba kwaajili ya mikopo vitapangwa na asasi husika bilakuingiliwa na Serikali, Benki Kuu wala wafadhilikwasababu asasi zinafahamu fika gharama za35

uendeshaji, hatari/ usalama wa mikopo na mbinu zabiashara.Gharama za uendeshaji, taarifa za mkopaji,hatari/usalama wa mikopo na mbinu za biashara, kwapamoja hujumuishwa katika kufanya maamuzi wakatiwa kupanga viwango vya riba.Mheshimiwa Spika, kwa kawaida, SACCOs naVICOBA hazitoi riba kubwa kama zinatumia fedha zaokukopesha, bali hukopa kwenye benki za biasharaambapo riba ni za juu na hivyo kufanya riba zao piakuwa za juu. SACCOS/VOCOBA hulazimika kuongezariba ili waweze kupata faida na kuweza kujiendesha.Hata hivyo, inatarajiwa kwamba kuongezeka kwaidadi kubwa ya asasi hizi na kuwepo kwa aina nyingi zabidhaa (mikopo) kutaleta ushindani ambao hatimayake ni kuteremka kwa viwango vya riba na kuongezaubora wa huduma.Mheshimiwa Spika, ni vema pia kugusia mikakatimbalimbali ambayo Serikali na Taasisi zake zimechukuakatika kushughulikia tatizo la riba kubwa inayotozwa nabenki na Taasisi nyingine za fedha zikiwemo SACCOSna VICOBA.Hii ni pamoja na kuweka mfumo wa upatikanajiwa taarifa za wakopaji wa taarifa za wakopaji yaanicredit reference system. Mfumo huu utarahisishaupatikananji wa taarifa za wakopaji na hivyokuziwezesha Taasisi zinazokopesha kufanya maamuzistahiki ikiwemo kiasi cha riba. Mfumo huu utatoa36

mzania mzuri wa usalama wa mikopo (safety credit vscredit risk).Mheshimiwa Spika, Serikali ipo katika hatua nzuri zakuboresha masijala ya Ardhi ( Land Registry) ilikurahisisha upatikanaji wa Hati za viwanja/Mashambazitakazoweza kutumiwa na wakopaji kama dhamanana hivyo kupunguza riba inayotozwa.Mkakati mwingine ni pamoja na kuweka mfumowa kusimamia Taasisi zinazokopesha kwa kutumiafedha zao wenyewe. Aidha, Serikali kupitia Benki kuuinaandaa mfumo wa kuelimisha jamii ya mamboyanayohusu fedha na mikopo. Elimu ya fedha namikopo itasaidia kuondoa hali ya wananchi kutozwariba kubwa kwa kukosa tu uelewa wa masuala yamikopo, riba ya mikopo. (Makofi)MHE. CLARA D. MWATUKA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri wa fedha.(a)Kwa kuwa, SACCOs na VICOBA hukopafedha zao benki na wao ndipo hukopeshawana vikundi jambo ambalo linawafanyawananchi hawa kutozwa riba mara mbili.Je, Serikali haioni ya kwamba inawapamzigo mkubwa na kuwafanya hawawanyanyasike?37

(b) Je, isingekuwa rahisi Serikali ikafanyampango wa kuwafanya hawawakopeshwe na benki moja kwa moja?NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM): Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali inaonamzigo mkubwa ambao unawapata wananchi hususanikutozwa riba mara mbili na ndiyo maana katika swali lamsingi nilieleza hatua ambazo Serikali inachukua kwaajili ya ku-address issue hii.Kwa hiyo, Serikali tayari inaona huu mzigo nakwamba tuko katika mwendelezo wa kufanya CreditReference System kwa ajili ya kuangalia hasa ile hatariama reference ya yule mkopaji hivyo itarudisha chinikiwango wa riba.Mheshimiwa Spika, lakini swali lake la pili lilisemaSerikali inahakikisha vipi kwamba mwananchi wakawaida kuweza kukopa benki moja kwa moja,nadhani katika hotuba ya Waziri wa Fedha imeelezawazi hatua ambazo Serikali inachukua katika kuingizamitaji katika mabenki ambao utasababisha wananchitu wa kawaida waende wakakope kule. Kwa hivyonaomba tu turejee katika ile hotuba na tujue Serikaliinafanya hatua gani katika kuelezea tatizo hili.Ahsante sana. (Makofi)MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipatia nafasi kuuliza swali lanyongeza.38

Kwa kuwa, SACCOS na VIKOBA imekuwamkombozi wa wananchi wa hali ya chini hasa katikasehemu za vijijini, ningeomba kuuliza ni lini VIKOBAitapewa nafasi kama ilivyo SACCOS ili iweze kupatamikopo kwa ajili ya kusaidia wananchi kamainavyofanyiwa SACCOS hasa katika lile eneo laMisenyi?SPIKA: Ahsante sana, VIKOBA kupata hadhi yaSACCOS Naibu Waziri majibu.NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM): Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali na wadauwote wengine wamegundua kwamba VIKOBA nimfumo ambao umeweza kuwatoa wananchi wengikatika dimbwi la umaskini. Kwa hiyo, nadhani ni ushaurimzuri na sisi tunauchukua tutakwenda kuufanyia kazi iliVIKOBA vyenyewe navyo vipate hadhi SACCOS ilikuweza kuwasaidia wananchi. Siwezi nikatoa tarehemaalum lakini hili ni suala zuri na Serikali italichukuatutalifanyia kazi. (Makofi)MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali lanyongeza.Kwa kuwa, nchi nyingi Duniani zina mfumo wakuwataka mabenki yanayowekeza ndani ya nchi yaokuchangia katika huduma za maendeleo. Je Serikaliyetu ina mpango gani wa kuhakikisha kwambamabenki yanayowekeza ndani ya nchi yetuyanachangia kwenye mifuko ya SACCOS na VIKOBA?39

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM): Mheshimiwa Spika, Serikali si tu kwenyeMabenki, lakini na makampuni mengine ya uwekezajiinayataka lazima watimize wajibu wao kwa jamii yaani(Cooperate social responsibility) kwa hiyo huo ni wajibuwao. Lakini Serikali haim-confine benki ama shirikakuweza kusaidia VIKOBA parse lakini inataka iweinahudumia jamii kama ni part yake ya cooperatesocial responsibility. Kwa hiyo hilo itakuwa ni wajibu wamwekezaji mwenyewe, ni wajibu wa kampuni yenyewena ni wajibu benki yenyewe lakini nalo si suala baya.(Makofi)SPIKA: VIKOBA na SACCOS isije ikaonekana nimambo ya akina mama tu, Mheshimiwa Mpina swali lamwisho la nyongeza.MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spikaahsante kwa kuniona. Kwa kuwa hivi sasa hapa nchinituna tatizo kubwa sana la riba za mabenki kwambariba hizi zipo juu sana, avarege ya riba sasa hivi katikaFinancial Institutions imefikia asilimia 33, wanatoza ribaya asilimia 33 ambayo ni kumbwa mno na kwambahaiwasaidii kabisa hawa wananchi wanaoendakukopa badala yake ni kufilisiwa mali zao.Kwa kuwa tatizo la riba kuwa kubwalinasababishwa na upatikanaji wa mitaji ambakoFinancial Institution pamoja na Commercial Bank kulewabakopata mitaji kwa ajili ya kukopesha wateja wao.Je Serikali ina mpango gani wa kuweka utaratibumahsusi wa zile Unit Cost ili waweze ku-regulate hiziriba za mabenki kwa sababu hakutakuwa na sababu40

tena ya kuwa na mabenki ya kukopesha wananchikwa sababu yanawafilisi badala ya kuwasaidia?WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa naomba kumpongeza Naibu Waziri wangu kwamajibu yake mazuri ambayo ameyatoa. (Makofi)Mheshimiwa Mpina anataka kujua ni namna ganiSerikali inaweza kuwa na strategies ya kupunguzagharama ya kukopesha (Cost of Lending).Mheshimiwa Spika, naomba kwa manufaa yaWabunge wote nitoe mambo manne ya msingiambapo mabenki yanafanya ili riba ile iweze kuwa ipo.Kwanza, ni gharama ya kuwa na pesa ile iliyo mkononi(cost of borrowing), wao wameipata kwa gharamagani, kwa hivi tunaanzia hapo.Pili ni gharama au athari au yule anayekopawanamtizama anaweza akawa na uwezo wakurudisha au namna gani (Borrowers risk) na katika hilowanatazama vigezo vitatu. Kigezo cha kwanza je huyuanayekopa biashara yake ina uwezo gani wakurudisha pesa, kigezo cha pili wanatizama uwezowake wa huyu anayetaka kukopa yaani (borrowerscapacity) na intergrity yake, na kigezo cha tatuwanatizama je ikiwa hatalipa hela ile itarudi namnagani (collateral au security).Mheshimiwa Spika, lakini jambo la tatukinachokuwa katika component ya interest rate ni costof doing business yaani ni gharama gani waowanaikabili katika kuendesha ile shughuli. Kwa hiyokazi ya benki ni sawa na kazi zingine katika41

kugharamia. Kwa hivyo kuna gharama ya umeme,kuna gharama ya mishahara, kuna gharama yauendeshaji kwa hivi nayo inaingia katika element yacosting ya ile interest rate.Mheshimiwa Spika, nne wanatizama kitu kinaitwa(profit margin au mark up), hiyo inakuwa katika namnagani wao wata-peg ili kiwango gani ili nao wawezekuwa na faida. Kwa hivyo wanapo-calculate interestrate wanatizama vyote vinne kwa mpigo. Sasa hali yaTanzania bado gharama ya kukopesha iko juu kwasababu ya vitu vya msingi ambavyo bado lazimatuvifanyie kazi katika uchumi kwa pamoja.Mheshimiwa Spika, kwanza from the supplies sideyaani upande wa wakopeshaji. Je, wapo wa kutoshaili wao wenyewe washindane ili gharama yakukopesha iweze ikapungua. Kwa hivi ni kazi ya Serikalitunatizama namna gani ya kuboresha hali ya financialinstitutions katika nchi hii ili kwanza ziweze kuwa nyingina zikishakuwa nyingi zinaposhindana ile riba yenyewenayo itaanza kuteremka. Kwa hivi kuna vitu vingitunatizama kisayansi ili viweze vikaja vikasaidia kwamuda mrefu katika hali halisi ya kuteremsha interestrate. Ahsante sana. (Makofi)SPIKA: Waheshimiwa Wabunge maswaliyamekwisha na majibu haya ya mwisho ni semina yabure, kwa hiyo, tunashukuru kwa elimu hiyo.Waheshimiwa Wabunge, wageni tulionao hapakwetu. Tunao Madiwani 35 kutoka Kata zote za Jimbola Handeni wakiongozwa na Mwenyekiti wa42

Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Ndugu RamadhaniDiliwa, naomba mahali walipo wasimame kama wapondani, karibuni sana kumbe ni watatu tu. (Makofi)Waheshimiwa Wabunge tunao wanafunzi hamsinikutoka shule ya sekondari ya Bihawana pamoja nawalimu wao, Walimu na wanafunzi naomba msimamemlipo, ahsante sana wengine wapo huku nyuma,karibuni sana tunaomba msomo kwa bidii. Siku hizikusoma ni kushindana, karibuni sana. Tuna wanafunzina walimu 55 kutoka Kanisa la Pentekoste Jimbo laDodoma wapo wapi ahsanteni sana. Tunashukuru sanana ninyi pia mkazane kusoma, msome vizuri. Halafutuna wanafunzi na walimu 85 kutoka shule ya msingi yaAmani ya Dr es Salaam wako wapi? Ahsanteni sanapoleni na safari karibuni sana nadhani mtajifunzamambo machache hapa kuhusu mwenendo waBunge ahsanteni sana. Kuna wanafunzi na walimu 52kutoka shule ya msingi Ignusius ya Dodoma wapobasement wamekosa nafasi labda baadayewatapanda huku juu.Waheshimiwa Wabunge kuna wanafunzi 30kutoka chuo Kikuu cha Dodoma ambao ni wageni waWaheshimiwa mbalimbali hapa Bungeni, wanafunziwote wa UDOM mahali walipo wasimame, karibunisana tunawatakia masomo mema. Ahsante sana.Waheshimiwa Wabunge, matangazo yanayohusushughuli za Kamati. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumuya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, MheshimiwaProfesa David Mwakyusa, anaomba niwatangazieWajumbe wa Kamati yake kwamba leo hii saa saba43

mchana kutakuwa na kikao cha Kamati katika ukumbiwa chumba Namba 231. Makamu Mwenyekiti waKamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala,Mheshimiwa John Lwanji, anaomba niwatangazieWajumbe wa Kamati hiyo kwamba leo saa sabamchana kutakuwa na kikao cha Kamati katika ukumbiNa. 227.Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda naBiashara, Mheshimiwa Mahamoud Mgimwa, anaombaniwatangazie Wajumeb wa Kamati yake hiyo kwambaleo saa saba kutakuwa na kikao katika Ukumbi Na.219.Waheshimiwa Wabunge nina tangazo linalotokakwa Katibu wa Wabunge wa CUF MheshimiwaMagdalena Sakaya anaomba niwatangazie Wabungewote wa CUF kuwa wanatakiwa kuhudhuria kikaokitakachofanyika leo saa nane mchana ukumbi waMsekwa C.Mheshimiwa Yahya Kassim Issa wale watu wakohawakukutana siku ile? Anaomba niwatangazieWabunge wote wanaoishi magorofa ya site moja,mbili, tatu na nyumba za kisasa wanaombwawakutane leo saa saba mchana baada ya kumalizakikao cha Buneg ukumbi wa Pius Msekwa, sijui siku ilehawakukutana basi mnaombwa tena mkutaneanasema ni muhimu sana kuhudhuria kwa wale wotewanaohusika, kuhudhuria kwenu ndiyo mafanikiomnayokwenda kuongea.44

Mheshimiwa Kiumbwa Makame Mbarak, Mbungewa Viti Maalum, amefiwa na mama yake mzazi usikuwa kuamkia leo na watakuwa na maziko huko Zanzibarsiku ya leo. Tunayo taarifa tena Mheshimiwa WaziriWassira naye amefiwa na mama yake mzazi ndiyomaana hamumwoni hapa amefariki kuamkia leo. Kwahiyo tuwaombee wazee wetu hawa Mwenyezi Munguapumzishe roho zao mahali pema peponi. Ahsantenisana, tunaendelea.WABUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.SPIKA: Unajua mimi matumizi ya mwongozo huwasielewi, kwa sababu toka tumeanza ni maswali yaWaziri Mkuu na maswli ya kawaida na mimi, sasamwongozo haya hebu tusikilize na kama siyo sahihinitawaambia siyo, Mheshimiwa Dkt. Mbassa.MHE. DKT. ANTONY G. MBASSA: Mheshimiwa Spika,naomba Mwongozo wako kupitia Kanuni ya 68 (7),mapema wakati wa kipindi cha maswali kwa WaziriMkuu kuna Mbunge mwenzetu ameliarifu Bunge hilikwamba kuna kikundi cha watu ambacho kinachangafedha kuwapa Madaktari kushinikiza mgomo na sualahili ni suala ambalo linagusa maisha ya watu na nisuala ambalo halipaswi kufanyiwa mzaha.Naomba mwongozo wako Mbunge huyu kwaniniasikitaje hicho kikundi ili kurahisisha kazi ya Serikalikusuluhisha mgomo huo, ahsante. (Makofi)45

SPIKA: Bahati nzuri wakati anajibu yule aliyeulizwaalisema na wao wamesikia sikia na utafiti unaendelea.WABUNGE: Kelele.SPIKA: Ndivyo alivyosema! Kwa hiyo tunaombahuo utafiti uendelee. Mnapiga kelele kwa sababugani?Mheshimiwa Mnyika Mwongozo mwingine.MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Naomba mwongozo wako kwa mujibu waKanuni ya 116 ambayo naomba niisome, Mbali namajukumu ya msingi ambayo yameorodheshwa kwakila Kamati ya Kudumu, Kamati yeyote inawezakupendekezwa kwa Spika ipewe majukumu yanyongeza ambayo yatatajwa katika pendekezo hilo,na vile vile Spika anaweza kukabidhi jambo linginelolote kwa Kamati yeyote kadri atakavyoona inafaakwa ajili ya kushughulikiwa na Kamati hiyo.Mheshimiwa Spika, naomba niweke mkazokwenye maneno. Vile vile Spika anaweza kukabidhijambo lingine lolote kwa Kamati yeyote kwa kadriatakavyoona inafaa kwa ajili ya kushughulikiwa naKamati hiyo.Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako naombaninukuu Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania inayosema sehemu ya pili yaBunge itakuwa ndiyo chombo kikuu cha Jamhuri ya46

Muungano wa Tanzania, ambacho kitakuwa naMadaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia nakuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kuna mambo yametokeamapema leo na jana. Mosi ni taarifa tulizoelezwa janana Naibu Spika kwamba Kamati ya Bunge ya Hudumaza Jamii ambayo ilipewa kazi mwezi Februari mwaka2012 kuhusu suala la madai ya madaktariilishakamilisha kazi yake na kwa taarifa tuliyoelezwajana Bungeni tayari taarifa hiyo imekwishapelekwaBungeni. Lakini mimi ni mbunge na sijawahi kupewanakala ya hiyo taarifa na hiyo taarifa haijawahi kujaBungeni.Lakini leo vile vile tumeelezwa hapa kwambaSerikali imeacha kutoa kauli leo ambayo ilikuwakwenye orodha za shughuli za leo kwa maelezokwamba kuna mambo bado inayafanyia kazi, haliambayo inaoonesha kwamba mpaka katika hatua yasasa na kwa kuwa mgomo unaendelea upo kwenyehali mbaya, Serikali imeshindwa kushughulikia tatizo hili.Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imeshindwakushughulikia tatizo hili, ningeomba mwongozo wako iliuweze kutumia madaraka yako kwa mujibu wa kifungucha 116 cha Kanuni ili kuweza kuelekeza Kamati yaBunge ya Huduma za Jamii, ifanye mambo mawilimuhimu. Moja itupatie sisi Wabunge nakala ya iletaarifa ambayo imetumia siku nyingi sana kufanyiwa47

kazi na imesikiliza pande zote mbili tofauti mbali nahizi taarifa za upande mmoja tunazopewa na Serikali.Lakini la pili, Kamati ya Bunge iweze kuingilia katikusuluhisha kwa sababu hapa mgogoro ni kati yaSerikali na Madaktari na Serikali imeshindwa kutatuamgogoro ili Bunge tusionekane na sisi Wabunge naBunge tunazembea kuchukua hatua. Kamati yaBunge iingilie kati ishughulikie maana yake maisha yawatu yanapotea. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako.(Makofi)SPIKA: Haya, na hiyo Kanuni ukisoma inasemaSpika anaweza kutoa majibu baadaye, sasa naombaKatibu endelea na Order Paper.KAULI ZA MAWAZIRIMgomo wa Madaktari NchiniSPIKA: Nimesema huyu nitamjibu baadaye, kwasababu majibu yake yanalingana na ninachotakakusema katika hatua inayofuata ya agenda ya siku yaleo. Kauli ya Waziri tuliyoambiwa kwamba itatolewa leohaitatolewa. Sababu zake ni kwamba, Mhimilimwingine umelalamika kwamba wao wanashughulikiamasuala yanayokuwa katika Mhimili wao. Sisi hapatunaendelea kuyazungumza, tunaendelea kudadisi natunaendelea kutoa taarifa. Kwa hiyo, hiki kipengelehakitakuwepo leo cha Kauli ya Mawaziri.48

Vivyo hivyo hiyo taarifa anayosema MheshimiwaMnyika, ile Kamati niliiagiza wakae na Serikaliwajadiliane kauli iliyotolewa hapa na Waziri aliyehusika.Walifanya hiyo kazi, walikwenda Dar es Salaam naKamati yangu ya Uongozi tulikutana na tuliwaleta nandege usiku kutoka Dar es Salaam ili waweze kuitoleabriefing Kamati ya Uongozi kuhusu kazi waliyokwendakufanya kule. Wakatoa taarifa yao, tulikaa mpaka saasaba usiku tukakubaliana kwamba taarifa ilehaitaletwa Bungeni hapa kwa sababu ipo katikamikono ya Executive. Sisi siyo wa kujibu mambo yaExecutive hapa tuna kazi yetu. Hivyo ndivyotulivyokubaliana.Kuna mengine ambayo walipendekeza usiku ule,tulikubaliana kwamba, mimi nitaenda kuwashauriwanaohusika wachukue hatua zinazostahili. Kwabahati hatua zile zilichukuliwa, hiyo taarifa imepelekwaExecutive na wamefanyia mambo mengiyanayoendelea. Kwa hiyo, haitakuja hapa kwasababu mimi ndiyo niliyewaagiza wafanye hiyo kazi naKamati ya Uongozi walipitia hiyo taarifa na wakatoataarifa inavyostahili. Hivi sasa suala hili lipoMahakamani, naomba lifungwe. Tunaendelea.(Makofi)HOJA ZA SERIKALIMakadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka2012/2013 – Ofisi ya Waziri Mkuuna Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Majadiliano yanaendelea)49

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nina orodha hapaya wachangiaji, kuna ambao hawajachangia hatamara moja wanafikia 55 na waliochangia mara mojawanafika 46. Kwa hiyo, kwa mujibu wa taratibu zetu,tunaanza na ambao hawajachangia hata mara mojaambapo yupo Mheshimiwa Abdalla Haji Ali naMheshimiwa Yusuph Haji Khamis.MHE. ABDALLA HAJI ALI: Mheshimiwa Spika,ahsante. Kwanza, sina budi kumshukuru MwenyeziMungu, aliyenijalia leo na mimi kunipa uwezo wakusimama hapa katika Bunge lako Tukufu. Pianakushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi hii.Ninakupongeza wewe binafsi na Watendaji wakokatika Kiti chako hicho, kwa kuhimili mikiki mizito yaBunge hili. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nilisikiliza Hotuba ya WaziriMkuu kwa umakini kabisa na mwisho nikagunduakwamba, katika Hotuba yake ya mwaka huu kunaupungufu. Kama kawaida yake, Mheshimiwa WaziriMkuu ametaja angalau kwa kifupi masuala ya elimu,umeme, kilimo, utalii, afya, uvuvi na mambo mengine.Upungufu niliougundua katika Hotuba yake hiihakutaja hata kipengele kimoja kuhusu suala lanyumba na maendeleo ya makazi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hii inakwenda kinyume naHotuba yake ya Bajeti ya mwaka uliopita, ambayoalizungumzia suala hili kwa kina na uthibitishoukapatikana katika Hotuba yake ya mwaka 2011/2012,ukurasa wa 28, naomba ninukuu: “Nyumba na50

maendeleo ya makazi: Mheshimiwa Spika, Serikaliimehamasisha mabenki na vyombo vingine vya fedhakutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba ya muda mrefu nayenye riba nafuu kupitia Sheria ya Mikopo ya NyumbaNamba 17 ya Mwaka 2018. Sheria hiyo, imewezeshabaadhi ya mabenki kutoa mikopo kwa ajili ya kununuana kujenga nyumba kwa masharti ya kurejesha mikopohiyo ndani ya miaka 15.” (Makofi)Mheshimiwa Spika, namwomba Waziri Mkuuatakapokuja kufanya majumuisho ya Hotuba yake hii,hili ni suala muhimu sana, kifungu hiki nacho akipenafasi akiweke katika Hotuba yake. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kutokana na hilo, nimeonaangalau kwa maneno machache kabisa nizungumziesuala la nyumba na maendeleo ya makazi. Sotetunafahamu kwamba, mwendelezaji mkuu wa ujenziwa nyumba katika nchi yetu ni Shirika la Nyumba laTaifa (NHC). Shirika hili ni la kupigiwa mfano; ni Shirikalenye kuleta maendeleo makubwa katika nchi hii na nivizuri mashirika mengine yakaiga mwenendo mzimawa Shirika hili. (Makofi)Mheshimiwa Spika, katika mafanikio yake Shirikahili, naomba kwa uchache nitaje Shirika la Nyumba,hatua yake ya mwanzo lina hazina ya ardhi eneo lakutosha, eneo lipatalo ekari 562.8 katika maeneombalimbali ya nchi, ambapo ekari 202.2 zipo eneo laKibada, Kingamboni - Dar es Salaam ambalowamekusudia kujenga nyumba zipatazo 223 za beinafuu kwa ajili ya wananchi. (Makofi)51

Mheshimiwa Spika, katika mafanikio yake, vile vileShirika lina Miradi kumi yenye nyumba 827, kati yakeMiradi mitatu imeshakamilika ya nyumba 86 kwa ajili yakuuzwa na nyumba 741 zinaendelea kujengwa.(Makofi)Mheshimiwa Spika, vile vile Shirika kwa mwaka huulimekusanya makusanyo ya pango yenye kuvukalengo kabisa. Shirika lilijipangia au lilikadiria kukusanyashilingi bilioni 43.1, lakini mpaka Mei, Shirika kwa ufanisikabisa limefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 47.2, sawana asilimia 146. (Makofi)Mheshimiwa Spika, Shirika hili linafanya kazi nawafanyakazi wake hawana miujuza kutoka Mbinguni,siri yao kubwa ni ushirikiano, wanashirikiana vizuri.Wakurugenzi wako huru kuendesha Idara zao bilakubughudhiwa. Shirika hili lina wabunifu mahiri kabisawaliokusudia kwa dhati kuweka historia katika nchi hiikupitia Shirika lao. Nachukua fursa ya makusudikuwapongeza Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba.Pongezi pekee zimwendee Mkurugenzi Mkuu wa Shirikala Nyumba, Ndugu Mchechu; kijana huyu ni mahiri, nimakini na ni mchapakazi mkubwa. Naiomba Serikaliimpe ushirikiano mkubwa na ana nia ya dhatikuipeleka nchi hii mbele. (Makofi)Mheshimiwa Spika, penye mafanikio hapakosichangamoto au matatizo; Shirika la Nyumbalinakabiliwa na changamoto mbalimbali. Changamotohizo miongoni mwao moja ni Kodi ya VAT kwa Serikali.Shirika hulazimika kuzipandisha nyumba bei ili kufidiatatizo hilo. Tulielezwa nyumba inaweza kuuzwa pengine52

kwa shilingi milioni 25 lakini kulinganisha na gharamanyingine zinazoingizwa pale za VAT, nyumba hufikiashilingi milioni 35 mpaka shilingi milioni 40. NaiombaSerikali iwaondolee Shirika la Nyumba Kodi ya VAT naiwapatie fursa ya kuwauzia bei mwafaka wananchi.(Makofi)Mheshimiwa Spika, changamoto nyingineinayowakumba watu wa Shirika la Nyumba ni palewanapokwenda kuwekeza katika maeneo mapyahulazimika kupeleka miundombinu ya maji, umeme nabarabara. Yote hii ni gharama ambayo hujumuishwakwenye manunuzi ya nyumba na nyumba ikawa nighali hainunuliki. Vile vile na nyumba ya Serikaliijiwekeze kwenye miundombinu katika maeneo hayamapya ili Shirika lipate nafuu ya kuwapunguziawananchi bei. (Makofi)MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa ruhusa yako. Nachukua nafasi hiikumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema,Mwenye Kurehemu, kwa kuniwezesha na mimi kushirikikatika Kikao hiki cha Bajeti. Pia nakushukuru weweMheshimiwa Spika, kwa kuniruhusu kusimamakuchangia Hotuba iliyopo mbele yetu. Siku kama yaleo tarehe 12 Aprili, 2012 katika Kipindi cha Maswali yaPapo kwa Papo, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba,alimwuliza Waziri Mkuu, naomba kunukuualivyomwuliza: “Ni kiasi gani kimerudi na MheshimiwaWaziri Mkuu hizo fedha zitapelekwa kwenda kunusuruSekta ya Elimu na zitagawanywa kwa utaratibu gani ilikuhakikisha kwamba zinatimiza kusudi lililokusudiwa.”(Makofi)53

Hizi zilikuwa fedha za ufisadi wa rada ambaotunazitakasa kwa ajili ya chenji za rada. Halafu katikaKitabu hiki cha Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,katika ukurasa huu unaoning’inia sijui ukurasa nambangapi huu hapa, umeelezea hivyo hivyo kuhusu fedhaza rada. Alivyojibu Waziri Mkuu na majibu yaliyopokatika ukurasa huu yanalingana. Kwa hiyo, hakunawasiwasi kwamba, Baraza la Mawaziri limekaa nakuzigawanya fedha hizi. Fedha hizi zimegawiwa katikashule za msingi Tanzania Bara peke yake na hizi fedhani za Jamhuri ya Muungano kwa kupitia Jeshi laWananchi wa Tanzania. (Makofi)Kinachonishangaza, katika Baraza la Mawaziri,tunao Mawaziri kutoka Zanzibar, ambao walikuwawana haki ya kuitetea haki hii kwenda Zanzibar, lakinimpaka leo sijasikia kauli yoyote waliyotamka naZanzibar hakukupelekwa kitu chochote. Nataka kujuakama kilikuwepo Kikao cha Baraza la Mawaziri na waohawakuchangia chochote na haki ya Zanzibarikapotea au kama walikaa Watanzania Bara peke yaowao hawakupata nafasi ya kuzungumzia kitu chochotebasi pia walitakiwa watoe kauli tuisikie kwamba nawao wametetea Zanzibar kuhusu fedha hizi. Kutokanana kwamba wao hawakuwajibika kuwatetea Zanzibar,nafikiria Zanzibar yapo matatizo chungu nzima ya shuleza msingi, madawati hakuna na vyoo hakuna, lakiniwameshindwa kutetea basi mimi naomba wawajibike.(Makofi)54

Mheshimiwa Spika, katika kuwajibika hawaMawaziri, nitanukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano,Ibara ya 54(1) inayosema kwamba: “Kutakuwa naBaraza la Mawaziri ambalo Wajumbe wake watakuwani Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar naMawaziri wote. Huyu Rais wa Zanzibar ninamvuahatakuwemo lakini Mawaziri wale walioteuliwa na RaisJakaya Mrisho Kikwete kutoka Zanzibar, naombawawajibike kwa sababu hawakuitendea haki Zanzibar.(Makofi)SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, hawa Mawaziriwanafanya kitu kimoja. Sasa unawatoaje wao katikaBaraza lao? Wewe dai hela ya chenji tu.MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Spika,mimi nimekuwa nikishangaa sana kuhusu hizi fedha zaufisadi wa rada huu, tumekuwa tunashabikia kamapamepita jambo la kawaida tu. Wabunge wamekuwakila mmoja anaziomba hizi fedha zikatumike katikaJimbo lake pasipo aibu, sijui pana matatizo chungunzima kana kwamba tumefanya biashara yenye faidakubwa sasa tunashangilia tumepata mapato kumbetunakwenda mahali pabaya sana. Kulikuwa kunamambo ya msingi ya kushughulikia, kwanza, watafutweakina nani walihusika wapelekwe katika vyombo vyasheria ili wawajibike. Ufisadi Tanzania unakua mkubwana unaimeza Tanzania kila siku. (Makofi)Mheshimiwa Spika, tuna ufisadi chungu nzima, leoTanzania imekuwa kama jambo la kawaida; marautasikia kuna ufisadi wa rada, kuna ufisadi wa EPA,ufisadi wa Richmond. Sasa hivi pia nimesoma gazeti55

jana au juzi, kuna matrilioni ya shilingi ambayoyanatajwa yamefanyiwa ufisadi ndani ya Tanzania.Mheshimiwa Spika, sasa Taifa hili halifiki mahalipazuri, tutakuwa tuna kazi kubwa sana za kupelekamahali pazuri halafu vizazi vinavyokuja vitatushtaki kwaMwenyezi Mungu. Neema ya Mungu kaiweka ndani yaTanzania nyingi juu na chini; chini tuna madini na juuardhini tuna miti na kila kitu lakini tunakwenda vibayasana. Tugeuze njia tuelekee mahali ambapotumekusudia. (Makofi)Mheshimiwa Spika, juzi wakati nikiwa katika Bungehili hili wamesimama Waheshimiwa Wabunge hapawamesema tumegundua gesi nyingi, imetajwa kwamatrilioni, kwa mapipa, tutauza. Kama hatunamwelekeo mzuri hata tuzalishe kitu gani tutabaki hapahapa. Watu wengine wanasonga mbele sisi tunabakianyuma. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa nini maneno ya MwalimuJulius Kambarage Nyerere tunakuwa tunayatamkandani ya mdomo hatuyatendei kazi? Hii ni aibu kwaTaifa hili; kila anayekaa utamsikia ana-quote manenoya Mwalimu, Mwalimu kasema kupanga ni kuchaguakumbe tunawanyima watu maendeleo,tunachelewesha maendeleo. Hebu tufanye juhudi yamakusudi kumuezi Mwalimu. Mwalimu alikuwa nauchungu wa nchi hii na mambo haya mabayahayakuwahi kutokea enzi za Mwalimu. Kwa ninihatuwezi kufuata nyayo za Mwalimu kwa vitendo?56

Mimi nina-quote usemi wa Mwalimu ambaoamesema ili tuendelee tunahitaji mambo manne;Ardhi, Watu, Siasa Safi na Uongozi Bora. InaonekanaUongozi wa CCM siyo bora na ndiyo unatupelekahapa. Kwa nini twende hivi? Lazima twende vizuri.(Makofi)Leo sisi tuna madini chungu nzima, nimetembeleaGeita kule na Kamati ya Nishati na Madini, kunamashimo makubwa ambayo hayafukuliki hata siku yakiama. Watu wanachukua mali, sisi tunabakia. Ukiendakule, watoto shule zao hafifu, hawana madawati,hawana dispensary, barabara chafu, maji ya kunywapia hamna, mali zinatoka katika ardhi yao. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hili ni tatizo kubwa kwa nchiyetu, lazima turudi nyuma tuangalie, nchi hii itakuwakila mwenye mikono mikubwa anakuja kuchota mali,sisi tunabaki kuangalia. Kitakachopatikana kitakuwakigumu na itabakia historia tu, mashimo yaliyokuwepoyanayochimbwa madini, yanabakia kama yalivyohalafu vizazi vyetu vitakuja kutulaani na tuna wajibu wakwenda kujibu hoja kwa sababu wengi tunaaminitutakufa, tutakwenda kujibu hoja juu ya urithi, maliMungu aliyowapa Watanzania halafu viongozitukashindwa kusimamia. (Makofi)Mheshimiwa Spika, wakati umefika…(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)SPIKA: Umefika kumaliza. (Kicheko)57

Ahsante Mheshimiwa. Sasa namwita MheshimiwaHussein Amar na Mheshimiwa Dkt. Antony Mbassaajiandae na Mheshimiwa Jenista Mhagama ajiandae.MHE. HUSSEIN NASSOR AMAR: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangiahoja hii ya Waziri Mkuu. Napenda kumshukuruMwenyezi Mungu, ambaye ameniwezesha kunipa afyanjema na kuweza kusimama tena kwenye Ukumbi huukutoa malalamiko ya Wananchi wa Jimbo laNyang’hwale. (Makofi)Mheshimiwa Spika, napenda kuipongeza Serikaliya Chama cha Mapinduzi, kwa kutusogezea hudumaya Kiwilaya, Jimbo la Nyang’hwale, sasa hivi ni Wilayana Makao Makuu yake ni Karumwa. Kwa hiyo,tunaipongeza sana Serikali ya Chama cha Mapinduzikwa kutusogezea huduma ya Kiwilaya. Baada yapongezi zangu, napenda pia nitoe taarifa kwamba,Jimbo hili la Nyang’hwale lina upungufu wa chakulakama ilivyotokea mwaka jana, lakini tunaishukuruSerikali iliweza kutuvusha mwaka jana kwa kutupachakula cha msaada na cha bei nafuu. TunaiombaSerikali ijipange tena kwa sababu upungufu wachakula katika Jimbo la Nyang’hwale ni mkubwa sana.Mheshimiwa Spika, sasa naanza kuchangia. Kunaahadi ambazo zilitolewa mwaka jana katika maswaliyangu ambayo niliuliza, hakuna hata moja ambayoimetekelezwa. Niliulizia Serikali ina mpango ganikutekeleza ahadi za Mheshimiwa Rais alipokujaJimboni, aliahidi mambo mengi; aliahidi58

kututengenezea barabara ya kutoka Busisi kwendaKahama kwa kiwango cha lami, alituahidi maji,utafufuliwa mtambo ambao ulikuwa umesimamatangu mwaka 1975 na Naibu Waziri wa Tawala zaMikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Mwanri alisemakwamba, tayari kuna pesa zimetengwa, shilingi milioni20 kwa ajili ya upembuzi lakini hakuna ambachokimefanyika mpaka hivi sasa!Mheshimiwa Rais aliahidi kupandisha Kituo chaAfya cha Karumwa na kuwa Hospitali ya Wilaya lakinimpaka sasa hakuna kinachoendelea wala dalili yaaina yoyote. Hizo ni ahadi za mwaka jana na piaaliahidi kwamba umeme utawashwa, mpaka leo hiiJimbo la Nyang’hwale tunausubiri umeme kwa hamusana, lakini tumeoneshwa kwamba sasa hivi umemeutawashwa kwa sababu nguzo zimetupwatupwa kilaeneo. Nguzo hizo hazijasimamishwa leo takriban zaidiya miezi minane. Naiomba Serikali isije ikawachukuliahatua Wananchi wangu wa Jimbo la Nyang’hwalewatakapoanza kuzichanja zile nguzo na kutumia kamakuni.Mheshimiwa Spika, masuala ya umeme; sasa hivitayari ni Wilaya. tunategemea umemeutakapowashwa Wilaya hiyo itakwenda kwa kasi.Tunaomba ahadi ambazo ziliahidiwa zitekelezwe namimi nitaunga mkono hoja hii baada ya kutolewatamko kwamba ahadi zote nilizoahidiwa mwaka janaangalau zitaanza kutekelezwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, suala la elimu; tunashukurukwamba sasa hivi walimu wameongezeka kwa kiasi59

fulani, lakini bado kuna changamoto nyingi; madawatihakuna, nyumba za walimu hakuna, hii change yarada ambayo inazungumzwa na sisi Jimbo laNyang’hwale basi hebu zituangukie kwakutengenezewa madawati na nyumba za walimu.(Makofi)Mheshimiwa Spika, nina masikitiko makubwa sana;sisi Wananchi wa Kanda ya Ziwa ukiangalia uchumitulionao na maisha yetu tuliyonayo inasikitisha sana.Msemaji aliyemaliza kuchangia sasa hivi amesematuna migodi zaidi ya saba katika Kanda ya ZiwaVictoria ikiwemo na Nyang’hwale, lakini ukiangalia sisituliozungukwa na migodi hiyo, kaangalie maisha yawananchi walioko pale ni ya kusikitisha sana; hali nimbaya, hakuna maji, hakuna barabara, ahadi nyingiwametuahidi watu wa migodi, tuliahidiwa kuchimbiwavisima saba na Mgodi wa Bulyanhulu, lakini tanguwametuahidi leo miaka minane visima sabahawajachimba hata kimoja. Hayo ni malalamiko nanasema kwamba, yachukuliwe kwa kina ili kujengamahusiano yaliyo mazuri kati ya wawekezaji nawananchi.Mheshimiwa Spika, masikitiko mengine kuhusu Zaola Pamba; Kanda ya Ziwa ni wakulima wazuri sana wapamba, lakini hebu jaribuni kuangalia hali ya wananchihao ilivyo mpaka hivi sasa. Wananyanyaswa na soko lapamba. Wananchi wangu wa Jimbo la Nyang’hwalemsiuze pamba hiyo chini ya shilingi 1,000 naikiwezekana iwe mara ya mwisho mwaka huu kulimapamba, limeni alizeti ambayo haina vikao. (Makofi)60

Mwaka jana msimu wa pamba ulipofika vilianzavikao bei ikashuka na mwaka huu msimu umefika beiimeshuka; mbona hatujasikia vikao vya msimu waalizeti? Ninawaomba wananchi msiuze pamba chini yashilingi 1000, limeni alizeti mwaka ujao nitawatafutienisoko la alizeti. (Makofi)Mheshimiwa Spika, angalieni maisha ya Wananchiwa Kanda ya Ziwa, mmetusahau. Nimezungumzia kunamigodi saba, Tarime, Geita, Kahama, migodi hiyo ipompaka Shinyanga kuna almasi. Migodi saba ambayonaifahamu lakini jaribuni kuangalia maisha yawananchi. Angalia hata kwenye Uchaguzi, CCMimepata kura nyingi sana Kanda ya Ziwa, lakiniangalieni maisha ya Wananchi wa Kanda ya Ziwammetusahau. Tunaiomba Serikali ijaribu kutuangalia,ardhi yetu imetobolewa na hawa wawekezaji namaisha yetu ni mabovu. Leo Kanda ya Ziwa inaletauchumi mkubwa sana katika nchi, lakini ndiyo imekuwaya nyuma. Mmetusahau hata kwenye uongozi, angaliaBaraza la Mawaziri, Kanda ya Kaskazini, angalia hatakwenye Vyama vya Upinzani, Viongozi wake wa ngaziya juu wanatoka Kaskazini. Kwa nini ina maana sisiWasukuma hatuna elimu? Tumekuwa daraja lakupandiwa. Uchumi Kanda ya Ziwa; leo angalia zao lasamaki, Kanda ya Ziwa tulikuwa na uchumi pamba nasamaki, lakini vyote vimeporomoka kwa nini? Jaribunikuiangalia Kanda ya Ziwa.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, siungimkono hoja mpaka mambo niliyoyataja ambayoyaliahidiwa mwaka jana yatakapotekelezwa. Siungimkono hoja mpaka nitakapojibiwa. (Makofi)61

SPIKA: Haya ahsante, mpaka apatikaneMwenyekiti wa CHADEMA huko Musoma. Haya,mtakuwa mbali mno. Tunaendelea na MheshimiwaDkt. Antony Mbassa, atafuatiwa na MheshimiwaJenista Mhagama, Mheshimiwa Riziki Omari Juma naMheshimiwa Al-Shymaa Kwegyir.MHE. DKT. ANTONY G. MBASSA: Mheshimiwa Spika,ninakushukuru. Mheshimiwa Mbunge, nafasi ipoCHADEMA aje tu atapata Uongozi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nianzekwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, ambaye amenijaliaafya njema ya kuwepo mahala hapa. Vile vilenawashukuru Wananchi wa Jimbo la BiharamuloMagharibi, ambao tumekuwa pamoja, wameshirikiananami hususan katika kipindi chote ambacho nilikuwanashughulikia kesi ya uchaguzi; ninawashukuru;Mwenyezi Mungu azidi kuwajalia na nimeshinda.(Makofi)Mheshimiwa Spika, nianze kuchangia kwa kulaanikitendo cha kijambazi ambacho amefanyiwa DaktariUlimboka, ambaye anatetea maslahi ya Madaktariwanaohudumia Wananchi wa Tanzania hii. Madaktariwanaofanya kazi katika mazingira magumu, ambaohawana vitendea kazi, posho duni, lakini kwa kulifanyahilo, ameonekana amekuwa mbuzi wa kafara;tunamwombea Mungu atamjalia kheri. (Makofi)Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Kagera tunatatizo la wahamiaji haramu. Wahamiaji hawa haramu62

sasa wamegeuza Burigi Game Reserve kama makao,wanasumbua sana wananchi, wamefuga kiholela kiasikwamba sasa inaonekana Mkoa wetu sasa umekuwani shamba la bibi ambalo halina mwenyewe.Inasikitisha sana watu hawa wanapokuja na kuwakutawananchi, wazalendo, wakaonekana wazalendohawana haki. Katika Jimbo langu la BiharamuloMagharibi imekuwa ni kero, mazingira yoteyamevamiwa, watu hawa wanafuga kiholela nawanaharibu mazingira. Mimi nashindwa kuelewaSerikali yetu jamani inatusaidia vipi? Watu hawawamekuwa na kiburi kweli, kila mahala wanaona nieneo lao la kufanya mambo yao wanayoyataka.(Makofi)Naomba Serikali tafadhali iliangalie hili kwa makinisana na ninaomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, taarifazetu nyingi tumezileta kama Wabunge wa Mkoa waKagera uzifanyie kazi, tumechoshwa na vitendo hivi.Leo hii inaonekana mzawa ndani ya nchi yake hanahaki ila mgeni ndiyo mwenye haki na mgeni ndiyoanathaminiwa zaidi kuliko mzawa; hii inatusikitishasana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ufugaji huu wa kiholelaumeharibu sana Burigi Game Reserve kiasi kwambahata wanyama wanatoka sasa kule porini kwendakushambulia wananchi kwa sababu wamefukuzwa nahawa wafugaji haramu na tumesikitika kwa hili, kwasababu kule kuna askari wa wanyamapori, wanafanyakazi ya kulinda wanyama wetu, lakini ajabuwanaruhusu hao wafugaji. Hivi ni sheria ipi63

inayowaruhusu wafugie ndani ya reserve? Je, Serikalihailioni hili? (Makofi)Mheshimiwa Spika, matokeo yake, mifugo ileinapita mle na mbaya zaidi sasa imefika mahala hatahatua nyingine imebadilika, hata maaskari wetuwanadiriki kuwaangalia au kuchukua mifugo yawafugaji wanaofugia karibu na Nora Reserve nakuifukuzia ndani ya reserve na matokeo yakewanaanza kuwatoza wale wenye ile mifugo pesaambazo haziingii kwenye Mfuko wowote ule waSerikali; inasikitisha sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ng’ombe wamekufa kule, watuwanatishiwa, ni maisha ya ajabu sana. Sasa huyumwananchi tutamwendelezaje? Imeonekana mfugajihana chake katika nchi hii. Ninaomba tafadhali Serikaliiangalie kwa makini sana na pindi inapotokea suala lanamna hiyo, tunapotoa malalamiko yetu mtusaidie.Mheshimiwa Spika, mwaka jana niliuliza swalikatika Bunge lako hili Tukufu na nikajibiwa kwa ahadiya matumaini mazuri. Wafugaji wangu wana tatizokubwa la kukosa sehemu za kufugia. NilimwombaMheshimiwa Waziri afanye mchakato ndani ya Wizarayake, najua ni suala mtambuka lakini wananchi hawawapewe eneo la kufugia, ahadi ikatolewa vizuri tu nakabla ya suala hilo kuna wafugaji walishakuja mpakahapa Dodoma wakamwona Mheshimiwa Waziri naakawaahidi kulitatua lakini mpaka leo hii imekuwa niahadi ya kiini macho. Ninaomba Mheshimiwa Waziriutekeleze suala hilo.64

Mheshimiwa Spika, katika Bunge hili tumeshuhudiakodi ya vijana wetu wanaoendesha pikipikiimeondolewa na tukaridhika kabisa kwamba, kwakuondoa kodi hii tumetengeneza nafasi za ajira lakinisiyo kweli. Hawa wanaoendesha hizi pikipiki ni asilimiangapi ya vijana walioko mtaani ambao hawana ajira?Hawa wachache wanaoendesha pikipiki wanasaidiajekuinua kipato cha wenzao ambao hawana ajira?Mheshimiwa Spika, mwaka jana Bunge lako hilililiidhinisha Mpango wa kujengwa Vyuo vya VETA lakiniajabu mpaka leo hii hatuoni hivyo vyuo vimejengwawapi. Ukisoma taarifa wanasema wamejenga kimoja.Suluhisho la ajira kwa vijana wetu ingekuwa ni kujengavyuo ambavyo vitawasaidia wapate ufundi, leo hiitumewahalalishia waendeshe pikipiki lakini naniatakayetengeneza hizo pikipiki kama hatuanzishi Vyuovya VETA na vya Ufundi?Mheshimiwa Spika, tukubaliane kabisa kwamba,hapa sasa kuna haja ya msingi ya kuangalia hili kundila vijana, tuwatafutie shughuli maalumitakayowawezesha kujiajiri wao wenyewe na si vinginebali ni kuwa na vyuo vya VETA. Leo hii ukihesabu Vyuovya VETA vilivyokuwepo ni vichache mno, vinachukuaidadi ndogo sana ya wanafunzi. Vyuo vilivyokuwepovya FDC leo hii vingine hata vimetelekezwa,vinachukua vijana kidogo sana. Tunaomba tafadhaliSerikali iwaangalie vijana kwa upana na ukubwa iliwaweze kupata ujuzi utakaowasaidia katika kujengamaisha yao ya baadaye. Kila siku tunaambiwa vijanaTaifa la kesho, hapana, kujenga Taifa la kesho unaanza65

leo hii, tuseme nguvu ya vijana sasa hivi ndiyoinayohitajika si vinginevyo.Mheshimiwa Spika, naomba niongelee kuhusuMabaraza ya Kata. Mabaraza haya ya Katayamekuwepo lakini sina uhakika wala sina imani kamayamejengewa uwezo. Leo hii Mabaraza hayayanafanya kazi kadiri yanavyojua. Ukiangalia mapatoyake yanapatikanaje au wanalipwaje hawa Wajumbewa Baraza hili ni tabu tupu. Leo hii inafika mahalaunajichukulia maamuzi ya kutoza faini au vifunguvingine vya sheria ambavyo havipo.Mtu ameshtakiwa kwenye Baraza la Kataanaambiwa hana haki ya kujieleza. Sasa kama hanahaki ya kujieleza kwa nini anapelekwa pale asipelekwekwenye vyombo vinavyohusika? Baraza la Katalinamwambia wewe hupaswi kujieleza hapa;inasikitisha sana. Inafika mahala wanatoza adhabu,bado wanampangia yule kwamba uende kwaMtendaji akakupangie kazi inayolingana na thamaniya shilingi fulani kama adhabu yako. Mimi nafikirihatuwatendei haki wananchi. Ninaomba tafadhaliMabaraza ya Kata yajengewe uwezo, wafahamumisingi inayowafanya wao kuwepo pale, wajuewanatumia taratibu zipi katika kutoa suluhu mbalimbalina wao watambuliwe wapewe posho, vinginevyondiyo tunakokuta ukiritimba wa rushwa zisizokuwa namwelekeo.Mheshimiwa Spika, kuhusu bei ya mazao yawakulima; inasikitisha sana wakati wakulima hawawanapoanza kilimo, wanapewa maneno mazuri sana66

ya ushawishi; walime, bei nzuri, lakini wakati wa kuuzani tabu. Nimeshuhudia wakulima wa Zao la Tumbakukatika Kata zote zinazolima tumbaku Jimbo laBiharamulo Magharibi, kuna mgogoro na Afisa Ushirika,wameletewa pembejeo, bei hawaambiwi, mwisho wasiku wanaenda kudai pesa yao wanaambiwawametumbukia, ndiyo neno wanalolitumia. Waowanasomesha watoto, wana familia, wana mahitajiyao, unakuwa mgogoro. Hesabu zinakokotolewa sikunne, lakini jibu halitoki. Tafadhali waambieni wakulimaukweli kwamba zao hili zamu hii bei haipo waelewe.Mheshimiwa Spika, hakuna elfu, hakuna kilo yapamba. Ahsante.MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika,kwanza, namshukuru Mwenyezi Mungu, kwakuniwezesha kusimama mbele ya Bunge hili leo ili namimi niweze kuwawakilisha Wananchi wa Jimbo laPeramiho katika kuzungumza machache kwenyeHotuba hii ya Bajeti.Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuwaombaWabunge wote waunge mkono hoja ya Bajeti hii.(Makofi)Mheshimiwa Spika, ninasema hivyo kwa sababunikianza hata na msemaji mwenzangu aliyekaa hivipunde, Mheshimiwa Dkt. Mbassa, ameeleza kero zawananchi katika Jimbo lake. Sisi Wabunge wote niMadiwani katika Mabaraza ya Halmashauri kwenyemaeneo yetu. Kwa hiyo, hakuna Bajeti ambayo nimsaada mkubwa kwetu kutatua kero za wananchi67

kama hii, inayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,ambapo TAMISEMI pia ipo humo ndani. Kwa hiyo,ninawaomba Wabunge wenzangu, kutokuungamkono Bajeti hii ni kushindwa kutekeleza Sera naMipango ya Serikali kwenye Halmashauri zetu kupitiaTAMISEMI na sisi tukiwa kama Madiwani ndani yaHalmashauri hizo na tunaona matatizo ya wananchikatika Halmashauri tunazoziongoza. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Halmashauriyangu, ambayo ndiyo inayosimamia maendeleo yaWananchi wa Jimbo la Peramiho, ninaunga mkonohoja hii kwa asilimia mia moja. NinampongezaMheshimiwa Waziri Mkuu na Mawaziri wote waliokokatika Wizara yake. (Makofi)Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaendelea,ninampongeza kwa dhati kabisa Mkuu wetu wa Mkoatuliyeletewa, ameanza kazi kwa speed ya ajabu.Ametambua ni nini mahitaji ya Wananchi wa Mkoa waRuvuma na amekuja na spirit ya kuturudisha kwenyeAgizo la Mlale ambalo lilisimamia Siasa ya Kilimo naUjenzi wa Nyumba Bora. Mheshimiwa Mwambungu,nakupongeza. Wabunge Wote wa Mkoa wa Ruvuma,tunakupa ahadi ya kushirikiana na wewe bega kwabega na tutafanya kazi kwa maslahi ya wananchiwetu na kwa kuwa wewe ni Kiongozi Bora, tunaaminiutatuendeleza zaidi katika Mkoa wetu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ninawapongeza DCs wetu.Karibu Mkoa mzima tumepatiwa DCs wapya, tutakuwanao bega kwa bega. Nimwombe Mkuu wangu waWilaya, aamini kabisa kwamba, mimi na Dokta68

Nchimbi, Wabunge wake katika Wilaya yake yaSongea, tutafanya nae kazi kwa maslahi ya Wananchiwa Wilaya ya Songea. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa ufupi niingie kwenyekupongeza zaidi na hasa ari yangu ya kuunga mkonoBajeti hii. Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninakushukuru sanakwa kupokea kilio cha Madiwani na kuwaongezeaposho. Ninaomba Ofisi yako iende mbele zaidikuhakikisha Madiwani hawapati shida ya mikopo yavyombo vya usafiri na mambo menginewanayoyahitaji ili waweze kutusimamia shughuli zetuvizuri. Nakupongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, hiloulilolifanya ni jema na ninaamini Mawaziri katika Ofisiyako, watatusaidia sana kuyasimamia hayo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali yangu kwakukubali Hospitali ya Peramiho kuingia kwenyeMpango wa DDH. Tumeungana na Serikali, Hospitali yaPeramiho sasa ni Hospitali ya Rufaa kwenye Mkoawetu. Ninamwomba sana Waziri wa Afya, tokaHopsitali hiyo imepanda hadhi hatujapata Madaktari.Kwa hiyo, ninaomba sana katika Bajeti ya Wizara yaAfya, nipate majibu ni Madaktari wangapi wataletwakwenye Hospitali ya Peramiho. Ninashukuru sanaMheshimiwa Waziri Mkuu, Ofisi yako imepokea ombi laMji Mdogo wa Madaba; Kijiji cha Madaba, kupandahadhi sasa kuwa Mji Mdogo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ninaamini kabla mwaka huuhaujaisha, Gazeti la Serikali litatangaza Madaba kuwaMji Mdogo. Namshukuru sana Waziri aliyepita,Mheshimiwa George Mkuchika, alitoa ushirikiano wa69

kutosha sana kwenye Halmashauri yetu. Ninaaminikabisa, dada yangu Mheshimiwa Hawa Ghasia nayeye ataongeza nguvu kuhakikisha Madaba sasainakuwa Mji Mdogo. Dada Hawa Ghasia, Waziri wetu,ninakutakia kila la heri ufanikishe hili, hitaji kubwa sanala Wananchi wa Madaba. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini pale Madaba bado tunahoja ya ujenzi wa chumba cha upasuaji kwenye Kituocha Afya. Dada Hawa Ghasia, utakuta faili letukwenye Ofisi yako, ninaomba pia tushirikiane katikahilo.Mheshimiwa Spika, haya ninayoyasema, yananipamoyo kuunga mkono Bajeti hii kwa sababu ni hivi juzi tuMheshimiwa Magufuli ametuletea Halmashauri yetushilingi milioni 500 na kitu kutekeleza Mradi Mkubwa waBarabara mbili. Barabara moja ikitoka Kijiji cha Matimilakwenda Mkongotema, nikiungana na ndugu yanguMheshimiwa Vita Kawawa. Barabara nyinginetuliyopata favour ni kutoka Ndongosi kwendaNambendo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, barabara hizo hazijawahikupitiwa na greda toka zimeanza, toka Uhuruumepatikana. Hivi leo nikisimama hapa nikasema siungimkono hoja hii, hata wale wananchi watanishangaa.Kwa hiyo, naomba niseme naunga mkono hoja hii.Namshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Magufulina naishukuru Serikali yangu. Bado tunasubiri ujenzi wabarabara kutoka Likuyufusi kwenda Mkenda, Serikaliimeshatoa fedha barabara ile imeshafanyiwaupembuzi yakinifu, inatuunganisha na mpaka wa70

Tanzania na Msumbiji. Ninadhani tupo kwenyemazungumzo mazuri, Serikali itapanga bajetikuendeleza Daraja la Mwekulu na kuendeleza kiporocha barabara kinachounganisha Jimbo lako na Jimbolangu na wewe unaufahamu Mradi wetu huo. Basinimwombe Mheshimiwa Hawa Ghasia, afungue mafailiaone ule Mradi wetu atusaidie uweze kukamilika naunazidi kuendelea kwa faida ya wananchi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nikiingia kwenye kilimo, suala lambolea; ninaomba niiambie Serikali, tafadhali sanatusirudie makosa tuliyoyafanya mwaka jana. Mboleailichelewa, mbegu zilichelewa, uzalishaji wa chakulaunategemea Mikoa ya Kusini kwa nchi nzima yaTanzania, sasa lile lisijitokeze, lakini tulipata tatizo kubwasana la soko. Ninamwomba sana Waziri wa Kilimo naWananchi wa Mkoa wa Ruvuma na hasa Jimbo laPeramiho, safari hii utaratibu wa soko la mahindi usiwena matatizo tena. Ajenda hii ni muhimu. Mhimilimkubwa wa uchumi wa Wananchi wa Jimbo laPeramiho na Mkoa wa Ruvuma, upo kwenye mazaoya chakula na hasa mahindi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ninaomba niungane naMheshimiwa Devotha Likokola, jana aliombatujengewe soko. Mheshimiwa Mary Naguanakumbuka, mama wa uwekezaji, Mheshimiwa Waziriwangu; nimekuomba sana soko mpakani mwaTanzania na Msumbiji, hebu wekeza pale uwasaidieWananchi wa Jimbo la Peramiho na Mkoa waRuvuma, kuongeza uchumi wao kupitia soko lamahindi, ndiyo zao tunalolitegemea. Mheshimiwa MaryNagu, ninaamini kabisa Waziri wangu, sasa twende71

kwenye ule mkakati ambao toka ukiwa enzi za Wizaraile mpaka sasa bado haujafanyiwa utekelezaji.Mheshimiwa Spika, ninaishukuru Serikali kwakutenga fedha kwa umeme wa gridi kutokaMakambako mpaka Songea. Nina haja ya kuishukuruSerikali, umeme utapita Igawisenga, Wino, Lilondo,Madaba, Gumbilo na Mchangimbole. Sasa ni kwa nininisiunge mkono Bajeti hii? (Makofi)Mheshimiwa Spika, ukiangalia pale Lilondo, mimina wananchi wangu, tumeshaanza kutengenezaumeme kwenye maporomoko. Tuna uwezo wa kuuzaumeme huo kwenye Gridi ya Taifa, lakini naiombaSerikali ipeleke umeme kwenye taasisi zilizoko palePeramiho, Mlale JKT na katika maeneo mengine.Mheshimiwa Spika, nimalize kwa kuzungumziasuala la ajira kwa vijana. Tatizo la ajira kwa vijana nikubwa sana. Mimi nilikuwa ninafikiri mambo hayanitakayosema yafanyike, Serikali ianze kuangalia jinsi yakuwekeza katika miundombinu. Kuna nchi zimefanikiwakwenye ajira kwa sababu ya kuwekeza kwenyemiundombinu.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,ninaunga mkono hoja hii kwa maslahi ya Wananchi waJimbo la Peramiho. (Makofi)SPIKA: Ahsante. Umesahau kwamba na kwanguunapita Kifanya pia. Unapita Kifanya kule kwangu.72

Sasa namwita Mheshimiwa Al-Shaymaa Kwegyir,Mheshimiwa Zaynab Vullu ajiandae, MheshimiwaMbaruk Salim ajiandae na Mheshimiwa Pindi HazaraChana ajiandae.MHE. AL-SHAYMAA J. KWEGYIR: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa,napenda kutoa pongezi zangu kwa Mheshimiwa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaWaziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda na wewepia Mheshimiwa Spika, kwa kujali masuala ya watuwenye ulemavu, mnajali na mnafuatilia.Nawapongezeni sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, napenda kuzungumziamasuala ya watu wenye ulemavu kuondoka kwenyeWizara ya Afya na wahamishiwe kwenye Wizara yaWaziri Mkuu. Ombi hilo tumeliomba sana, siyo pekeyangu ninazungumza leo, lakini limeshazungumzwasana. Kwa hiyo, leo naomba kutilia msisitizo nakuiomba Serikali iangalie masuala ya watu wenyeulemavu kwenye Wizara ya Afya, yahamishiwe Ofisi yaWaziri Mkuu, kwa sababu pale kwa Waziri Mkuu kunaKitengo Maalum kinashughulikia masuala hayo. Kwahiyo, tunaomba tuwepo pale, ombi hili nalileta tena nanimeshawahi kuomba, lakini naomba kurudia tena leokwamba, tunaomba masuala ya watu wenye ulemavuyaje kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, pili, naomba kuzungumziamasuala ya viziwi. Kwenye Katiba ya Jamhuri yaMuungano, Ibara ya 18, inazungumzia haki ya kupatahabari za jamii. Viziwi haki hiyo hawaipati73

wananyanyasika. Kunatoka taarifa kwenye vyombovya habari, wao habari hawapati, hawajui chochotekinachozungumzwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ombi langu, kwenye Vyombovya Television, kuwepo na watu wa lugha ya alama ilina wao wapate taarifa kinachoendelea. Sasa hiviBunge linaendelea, hakuna wanachokijua, hawaelewikinafanyika nini humu ndani. Hawajui kitu ganikinazungumzwa humu ndani kwa sababu ile hakihawaipati. Wananyanyasika kwenye nchi yaowenyewe kama wageni, kumbe wao ni raia wa nchihii. Wapewe haki hiyo na wao wapate kusikia nakuelewa kitu gani kinaendelea ndani ya Bunge, kitugani kinachoendelea kwenye masuala yote mengi.Kunakuja sasa hivi Tume ya Katiba, itapita kuzungukana wao wapate haki ya kutoa maoni yao. Hilonaomba lifanyiwe kazi.Mheshimiwa Spika, katika nchi yetu kumekuwahakuna chuo cha kujifunzia lugha ya alama. Natoaombi kwa Serikali, kuna Chuo cha Patandi kinawezakikageuzwa yakapelekwa mafunzo ya lugha ya alamayakaenda kwenye Chuo hicho. Naiomba ombi languhilo lisikilizwe na wao watendewe haki, wapate haki yakupata habari katika jamii wajue kinachoendelea.Mheshimiwa Spika, naomba kuingia kwenye sualala Baraza la Ushauri kwa watu wenye ulemavu. Sheriailipopitishwa ya watu wenye ulemavu kuna Barazatumeambiwa litaundwa; swali langu je, Baraza hililitaundwa lini?74

Mheshimiwa Spika, naomba kupata jibu kwenyeswali hilo kwamba, hili Baraza litaundwa maana naonasiku zinazidi kwenda. Sheria imeshapita; je, ni lini Barazahilo litaundwa kwa ajili ya kushughulikia masuala yawatu wenye ulemavu?Mheshimiwa Spika, lingine ninalopenda kuongeleani kuhusu miundombinu. Miundombinu kwa watuwenye ulemavu ni tatizo kubwa sana. Wanapofikakwenye majengo, watu wenye ulemavu wa viungowanapata matatizo, haki hawana. Unakuta jengo,haliko rafiki kwa mtu mwenye ulemavu wa viungo.(Makofi)Mheshimiwa Spika, nina mfano mzuri kwenyemajengo yanayojengwa sasa hivi na National Housing.Majengo mengi yanayojengwa sasa hivi siyo rafiki kwawatu wenye ulemavu wa viungo. Nina mfano mzuri; juzinimepata mgeni nyumbani ana ulemavu; ilibidikumbeba kumuweka kwenye lift, angalau pana lift, piailibidi kumbeba hakuweza kumudu mwenyewe.Hakukuwa na lile eneo la kupita kwa ile Wheel Chairyake, kwa hiyo, hiyo siyo haki.Mheshimiwa Spika, ninaomba suala hili, ninarudiatena kulisema na nimeshasema sana na nitaendeleakusema sitachoka. Narudia kuzungumza na Wizarahusika wananisikia; majengo yanayojengwayawekewe miundombinu rafiki kwa watu wenyeulemavu. Kwa sababu watu wenye ulemavuwanapigia kelele matatizo yao kila siku, lakini75

hayafanyiwi kazi; kuna tatizo gani? Wamekosa niniwatu wenye ulemavu? (Makofi)Mheshimiwa Spika, hali ya uchumi ni ngumu,maisha ni magumu, lakini watu wenye ulemavu ugumuhuu unakuwa mara mbili zaidi au mara tatu zaidi kwao.Basi tuangalie hata yanayowezekana yafanyike.Ninarudia kusema haya yanayowezekana yafanyike.Mheshimiwa Spika, hapo hapo kwenyemiundombinu, ninaingia kwenye alama za barabarani;suala la alama za barabarani nimeshazungumza 2010,wakati ule Waziri wa Miundombinu akiwa MheshimiwaKawambwa. Nilimkabidhi Mheshimiwa Spika, kitabukama hiki.Mheshimiwa Spika, nilimpa MheshimiwaKawambwa, kitabu hiki chenye alama za barabaranikwa ajili ya watu wenye ulemavu. Suala hililimeshindikana, kuna taasisi inaitwa Kamati ya UsalamaBarabarani kwa Watu Wenye Ulemavu, kunaMwenyekiti pale anaitwa Bwana Kabatele, hodari sanahuyo bwana; ameshughulika amepata mabango,mabango yanaota vumbi yako karibu sabini na kitu,yamewekwa ndani uwezekano wa kuwekwaumeshindikana mpaka leo.Mheshimiwa Spika, Mkuu wa Mkoa wa Dar esSalaam analijua hili. Walikwenda kwake kumwombayale mabango yawekwe, kibali kimetoka Manispaa yaKinondoni na Manispaa ya Temeke yale mabangoyawekwe kusaidia mlemavu wa viungo akipita kuwena tahadhari kwamba, hapa jamani anapita mlemavu76

wa viungo, hapa anapita mwenye ulemavu wa ngozi,ana uoni hafifu haoni, kwa hiyo, aonekane anapovukabarabara. Kuna viziwi hawasikii sauti yoyote,anapovuka barabara aonekane.Mheshimiwa Spika, ninamwomba Waziri Mkuu, hilisuala lifanyiwe kazi. Barua ilikuja kwako MheshimiwaWaziri Mkuu, kuomba suala hili litiliwe maanani. Kikikitabu ninacho, naweza nikamkabidhi MheshimiwaWaziri Mkuu akione na alama hizo zipo azione.Mheshimiwa Spika, naomba kuingia sasa kwenyesuala la mauaji ya walemavu wa ngozi (albino). Mauajiyanaendelea, juzi ameuwawa albino Arumeru, Arusha.Amekatwa mikono, amenyofolewa sehemu za siri,ametolewa koromeo, haya mauwaji yataisha lini katikanchi hii?Mheshimiwa Spika, viungo vinachukuliwavinaenda kuuzwa, hawa wanaochukua viungohawajulikani? Ina maana imeshindikana kuwajua watuwanaotumia viungo? Mbona faru ameuwawa juzi, sijuianaitwa George, wauwaji wameshakamatwa tayari?Kumetokea mauwaji juzi kwenye utalii huko, wauwajiwameshakamatwa. Inashindikana nini kwenyemauwaji ya walemavu wa ngozi? Idadi imekuwakubwa, wanakimbilia themanini na kitu, wanazidi kufa,kutishika na kukatwa mikono. (Makofi)Mheshimiwa Spika, tatizo hili limekuwa kubwa.Katika watetezi Mheshimiwa Spika na wewe umo,tutetee. Ulikuja Lindi tukasherehekea pamoja sherehe.Natamani hata kulia, najisikia kulia kwa sababu77

wanauwawa, wanakatwa mikono, wananyofolewasehemu za siri; tumekosa nini katika nchi hii? (Makofi)Mheshimiwa Spika, tumekosa nini? Naumia rohonimwangu. Siungi mkono hoja. (Makofi)MHE. SAID A. ARFI: Mheshimiwa Spika, nakushukurukwa kunipa nafasi na mimi nichangie katika hojailiyopo mbele yetu. Nianze na kulizungumzia Bunge.Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Katiba yaJamhuri ya Muungano, Bunge lina shughuli maalum namahususi na ni Mhimili ambao unajitegemea, lakiniBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niChombo cha Serikali. Kimekuwa kikitumika muda wotekwa ajili ya kuihudumia Serikali na kufanya kazi zaSerikali. Wabunge hawapati fursa ya kuwasilisha maonina hoja mbalimbali za wananchi.Mheshimiwa Spika, natolea mfano, nina hojaambayo nimeiwasilisha katika Ofisi ya Spika toka mweziNovemba, ambayo inagusa maslahi na matatizo yawananchi, lakini kila siku Huduma za Serikali, Shughuli zaSerikali na Hoja za Serikali, zimepewa kipaumbele kulikomatatizo ya wananchi. Vivyo hivyo, hata inapofikiamasuala ya kujadili Taarifa za Kamati za Bunge nazozinanyimwa muda, zinapewa muda mdogo; Kamatitatu kwa siku moja, jambo ambalo linatunyima uhuruwa kujadili masuala yanayowahusu wananchi. Jambohili linasikitisha. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hoja yangu ilikuwa ni suala laardhi. Mmesikia wenyewe, kila Mbunge aliyesimama78

hapa amezungumzia matatizo yanayogusa ardhi.Ninayo CD hapa ya matokeo yaliyotokana nakuzembea kutokuisikiliza hoja yangu, nitaiwasilishakwenye Meza yako.Mheshimiwa Spika, natoka kwenye Bunge, nakujakwenye Bajeti. Tutengeneze sasa Bajeti ambazozinatekelezeka. Tusiwape wananchi matumaini yatarakimu wakati bajeti hazitekelezeki. Nitatoa mfano,Halmashauri yangu ya Mji wa Mpanda katika Bajetiiliyopita ya Maendeleo, tulikuwa tumetengewa nakudhinishiwa na Bunge lako Tukufu shilingi bilioni 4.42,lakini mpaka mwisho wa mwaka tumepokea shilingibilioni 1.78, sawa na asilimia 43 tu. Wananchi walikuwana matarajio makubwa sana kutokana na bajetiiliyokuwa imeidhinishwa na Bunge lakini Serikalihaiteremshi fedha kwenye Halmashauri zetu ili Miradiiweze kutekelezeka. Maeneo mengine hatukupatafedha kabisa. (Makofi)Nyumba za watumishi hatukupata fedha, Mpangowa Maendeleo ya Elimu za Sekondari ambao tulikuwatumeidhinishwa shilingi 6,014 milioni hatukupata lakinikwenye taarifa ya majedwali yaliyoambatanishwakwenye Hotuba ya Waziri Mkuu, inasema kwamba,kuna madawati 1200 yametengenezwa yenyethamani ya shilingi milioni 97, kitu ambacho ninamashaka nacho na sina uhakika nacho kwa sababunafahamu hakuna fedha iliyoletwa katika Halmashauriyetu lakini kwenye taarifa inaonekana kwamba kunamadawati yametengenezwa. Kwa hiyo, nitahitajikupata maelezo katika hilo.79

Mheshimiwa Spika, juu ya Bajeti, tulikuwatumetengewa bilioni moja na milioni mia tatu kwa ajiliya Miradi ya Maji. Mpaka mwisho wa mwakatumepata milioni 422 ambayo ni sawasawa na asilimiakama 33 hivi. Tatizo la maji katika Mji wa Mpandalitaendelea kuwepo, tumeshindwa kukamilisha tenki lamaji, niombe sasa Serikali, fedha ambazozimeidhinishwa na Bunge zipelekwe ili wananchiwaweze kupata maendeleo yaliyokuwayamekusudiwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, Mpanda tunalima tumbaku,wakulima wa tumbaku wanalipwa wanauza tumbakuyao kwa dola, wanalipwa kwa Shilingi za Kitanzania,kama waliuza kwa dola walipe kwa dola. Nilipatamalalamiko, siku ambayo mkulima amekuja kulalamikakwangu dola ilikuwa shilingi 733 na yeye analipwashilingi 1,400 na Chama cha Msingi; huu wizimuuangalie, wakulima wa tumbaku walipwe fedhakutokana na bei ambayo wameuza kwenye masoko.Zaidi ya hapo, nimwombe Mheshimiwa Waziri Mkuu,mwaka 2010 wakati anafungua Soko la Tumbaku paleMajalila na mimi nikiwepo, aliwaahidi wakulimakuwatafutia soko Nchini China, wakulimawameongeza kilimo cha Zao la Tumbaku lisituleteetena mgogoro kama msimu uliopita.Mheshimiwa Spika, zaidi ya hapo ni kwamba,Ushirika ni hiari, kwa hiyo, wananchi wanapokuwawameungana wakaamua kuanzisha Ushirika waowaruhusiwe wasiweke urasimu na vikwazo. (Makofi)80

Chama cha Msingi cha Wakulima wa Tumbakucha Mpanda Kati ni kikubwa na ni lazima kigawanywena jitihada za kutaka kukigawa Chama hiki kilazinapofanyika wananchi ambao wanataka kujengaUshirika wanazuiliwa.Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala laMkurugenzi wa Mji wa Mpanda, ambaye aliwahi kuwaAfisa Utumishi pale, akawa Kaimu Mkurugenzi wa Mji,sasa amethibitishwa kuwa Mkurugenzi, namtakia kila laheri na baraka na mafanikio katika kazi yake mpya.Alipewa uhamisho kwenda Ileje kama Afisa Utumishiakazuiliwa na TAMISEMI asiondoke, amethibitishwakuwa Mkurugenzi amepelekwa Ngala amezuiliwa tenaasiondoke Mpanda tatizo ni nini? Je, analinda maslahiya nani? (Makofi)Mheshimiwa Spika, lipo tatizo kubwa juu yapensheni za walimu, wengi hawapati pensheni zaokwa wakati, aidha wapo ambao wamefariki penshenizinakuja na wapo ambao wako hai na hawapatipensheni zao. Jambo hili naomba liangaliwe ni namnagani wanaweza kulisimamia hilo. Nilipata bahati yakutembelea shule za msingi zilizopo katika Jimbo langu,kuna tatizo kubwa la uhaba wa vyumba vyamadarasa na madawati, watoto wengi wanakaa chinina si Mpanda tu pake yake limekuwa ni tatizo la nchinzima, watoto wengi wanakaa chini kutokana nauhaba wa madawati. Kibaya zaidi, hakuna mkakatiwa makusudi ambao umewekwa na Serikali kwa ajili yakuliondoa hili tatizo na kuhakikisha kwamba watotowetu wanapata elimu katika mazingira mazuri, salamana safi. Niombe nijue mkakati wa Serikali katika81

kukabiliana na tatizo la uhaba wa vyumba vyamadarasa na madawati hususan katika shule za msingi.Mheshimiwa Spika, nirejee Hotuba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, ukurasa wa 37, inayohusu umemekwamba, Wakala wa Umeme Vijijini umetekelezaProgramu Kabambe katika mikoa kadhaa ikiwemoMkoa wa Rukwa. Rukwa tuna tatizo kubwa sana laumeme achilia mbali vijijini, ambapo mimi sikubalianina taarifa hii, kwa sababu siamini kama kuna mpangowowote wa kufikisha umeme katika kijiji chochotekatika Mkoa wa Rukwa na Katavi. Iwapo katika MakaoMakuu yenyewe ya Wilaya za Mikoa ya Rukwa naKatavi umeme ni tatizo, Mpanda umeme ni tatizo,Sumbawanga ni tatizo, Nkasi hawana kabisa, kwa hiyo,ninaposoma kwamba kuna mpango wa kupelekaumeme vijijini, taarifa hii inanitia mashaka na sinauhakika kama Mheshimiwa Waziri aliisoma na kwasababu na yeye anatoka Rukwa, ana uhakika ni kijijigani ambacho kimepelekewa umeme. Nadhaniatakapohitimisha ataniambia ndugu yangu Arfi,tulishapeleka umeme katika vijiji kadhaa.Pia nizungumzie suala la barabara za kuunganishaMpanda, wamesema wenzangu waliotanguliakwamba, Mkoa wa Rukwa na Katavi tunazalishamazao ya kutosha hasa mahindi na tunapeleka katikamikoa ambayo inakuwa na upungufu wa chakula.Barabara za Mpanda – Tabora na Mpanda - Kigoma,zipewe kipaumbele kuhakikisha zinapitika wakati wotena zijengwe kwa kiwango cha lami kama itawezekana.82

Mwisho kabisa, kama sitazungumzia reli nitakuwasijakamilisha mchango wangu. Reli nayo tuitazamehususan Reli ya Mpanda. Hivi sasa tukienda Mpanda,tuondokane na zile fikra za zamani kwamba, Reli yaMpanda ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa huduma tu, Reli yaMpanda ipo kwa ajili ya biashara. Kuna biasharakubwa ambayo ipo Mpanda, Shirika la Relilimeshindwa kui-tape hiyo biashara ya kuhamisha nakusafirisha mizigo. Kuna shehena kubwa ya mahindi natumbaku inangojea kusafirishwa kutoka Mpanda.Nakushukuru. (Makofi)MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nianze kwa kusemanaunga mkono hoja hii na ninazo sababu za msingi.Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa Hotubanzuri, lakini pia namshukuru kwa uteuzi wa Mkuu waMkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe,ambaye sisi kule kwetu Kagera tumemwongezea jinaanaitwa Kanali Mstaafu Fabian Massawe Mlokozi.(Makofi)Mlokozi kule kwetu maana yake ni mkombozi.Kanali Massawe alitokea Wilaya ya Karagwe kablahajapandishwa kuwa Mkuu wa Mkoa, kwa hiyo,namfahamu vizuri sana. Kusema kweli Mkoa waKagera tumebahatika, kama ni karata tunasematumelamba dume. Tunamhakikishia ukishirikano wa haliya juu sana na sisi wote Wabunge wa Kageratumejipanga kuhakikisha kwamba tunamsahidia kadiriya uwezo wetu kuendeleza mkoa wetu.83

Mheshimiwa Spika, nianze na riba za mabenki; iliwananchi wetu waweze kuendelea ni lazimawachangie katika uchumi wa nchi hii kwa kukopa lakiniriba za mabenki ziko juu sana. Naomba Serikaliiwaangalie wananchi, wanaogopa benki kama kituocha polisi.Mheshimiwa Spika, ningetamani sana nione Tawila Benki ya Kilimo Kayanga katika Makao Makuu yaWilaya ya Karagwe kwa sababu hakuna Mwananchiwa Karagwe ambaye anaweza kwenda Dar esSalaam akapata mkopo katika benki hii. Vilevile Benkihii iende kwenye wilaya zote ili wananchi wetu wawezekufaidika kwa maana wakulima wako vijijini hawakoDar es Salaam. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lingine, Serikali imekuwa nautaratibu wa kutumia fedha za Serikali kupitia Benkimoja hapa nchini, ambayo ni Benki ya NMB, fedhazote za Serikali zinapitia Akaunti ya NMB. Fedha hizizinakaa kwenye benki bila kutoa riba hata senti tanona kawaida ya fedha ni kwamba, fedha zinachakaa.Sasa juzi hapa Serikali ilitoa zabuni ikatangaza mabenkiyashindane kwa ajili ya kutoa huduma katika Akauntiza Serikali. Jambo zuri sana, nilibahatika kuiona zabunihii, kigezo kimojawapo ni kwamba kila benki ambayoinashindana katika hili ni lazima iwe na tawi katikawilaya zote.Ukiangalia Benki ambayo ina Matawi katikaWilaya karibu zote ni Benki ya NMB. Sasa kigezo hikikimeondolea ushindani Benki kama Barclays, CRDB,84

Akiba Commercial Bank na Mabenki mengine. Kwamaana hiyo basi ni kwamba, tangazo ni kama lililengakuipatia nafasi Benki moja tu.Kwa hiyo, naishauri Serikali zabuni hii isiwe yakibaguzi. Naiomba Serikali iangalie na MheshimiwaWaziri Mkuu naamini kabisa utaliangalia kwa makini hili;tufute zabuni hii ili kigezo hiki kiondoke na Benki zetuzishindane. Pia nilikuwa napendekeza fedha za Serikaliziwekwe katika Mabenki, kwa mfano, TANROADS, waofedha zao wanaweka katika Benki na wanatengenezainterest wanapata faida kwa maana kwamba, fedhaya Serikali isikae kabla haijatumika, unawezaukatengeneza faida ndani ya siku tatu, saba, nimasuala ya makubaliano.Mheshimiwa Spika, fedha hizi hasa za Halmashauriza Wilaya zikiwekwa katika akaunti fulani ambazozinatoa interest kabla hazijatumika na kabla kandarasihazijfanyika, zitasaidia ku-generate profit, yaani faidaambayo itasaidia sana matatizo mengi ambayotunapata katika Halmashauri zetu za Wilaya.Mheshimiwa Spika, nimesimama hapa kuungamkono hoja kwa sababu nimefarijika na kazi yainayofanywa na Serikali hasa kupeleka umeme vijijini.Kule kwangu Jimbo la Karagwe, Serikali imesikia kiliochangu cha muda mrefu wanaanza kupeleka umemekatika Tarafa ya Nyaishozi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, angalizo langu katika Mradihuu na Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madininingeomba anisikilize kwa sababu nipo kwenye eneo85

lake ni kwamba, Mradi huu wa Umeme umerukabaadhi ya vijiji. Kuna Kijiji kinaitwa Lukale, wamekirukahawakupeleka hata nguvu. Pia wameruka Kijiji chaMisha, Kijiji cha Ruhita, Kijiji cha Rubare, Kijiji chaKibogoizi na Kijiji cha Omorusimbi. Sasa Mradi huu ndiyoni mzuri lakini usiwe wa kibaguzi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kuna ahadi ya MheshimiwaRais aliyoitoa wakati wa kampeni mwaka 2010 katikaMji Mdogo wa Nyakaiga, Tarafa ya Nyabionza.Wananchi walimwomba Mradi wa Umeme na aliahidina Mradi huu nilitegemea uwe umeanza katika kipindicha mwaka uliopita. Kwa maana ya kupeleka Mradiwa Umeme katika Vijiji vya Kamagambo, Kiruruma,Nyakaiga, Chamchuzi, Chabuora, Bukangara,Akishaka na tarafa nzima ya Nyabionza. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ninaomba Mradi huu ukianzaSerikali iache ile tabia ya kuruka kijiji fulani na kwendakingine. Mimi ningeomba waanzie Chamchuzi, kunaKijiji kinaitwa Chamchuzi Serikali ianzie hapo, ianzie Kijijikinachoitwa Kaiko na Kijiji cha Kanyomagana waendempaka Kamagambo, Mkangala, yaani kwa maanakwamba unapojenga Mradi wa Umeme basi eneo lotelile liwake siyo wengine wabaki wananuna.Kwa hiyo, naomba sana Tarafa ya Nyabionza.Katika bajeti hii sitaki kumtisha Mheshimiwa Waziri waNishati kwa sababu ni mgeni na ni mtani wangu, lakininilikuwa namwomba ajikite vizuri katika eneo hiliahakikishe kwamba bajeti ijayo ili nimuunge mkono,vijiji vyangu vyote hivi vya Tarafa vya Nyabionza86

viwepo kama ambavyo Serikali imekuwa ikiahidi tangumwaka 2006.Mheshimiwa Spika, tuna Mradi wa Umeme ambaoulianza tangu mwaka 2006, lakini nguzo zimelalaUkanda wa Kituntu mpaka Rwambezi. Mwaka 2006niliiomba Serikali ije iondoe nguzo hizo ipeleke sehemunyingine ambapo zitaonekana zina umuhimu. KwaMkoa wetu wa Kagera, amezungumza MheshimiwaMbassa, tuna tatizo la wahamiaji wasio rasmi, mimisiwezi kuwaita haramu; tunaiomba sana Serikaliituhakikishie kwamba ifikapo tarehe 1 Mei, watakuwawameondoka wao na mifugo yao. Naombba Serikalijambo hilo itueleze wakati Waziri Mkuu ana-wind upkwamba amefikia wapi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, tuna tatizo la vitalu vyawafugaji, nimezungumza humu nadhani inaweza kuwakama mara ya 20 kwa maana ya Kata ya Kihanga,Vitalu vya Wafugaji vya Ranchi ya NARCO viligawiwakwa wafugaji; sina tatizo nao, lakini kuna Kampunimoja ya Kagera Sugar ilipewa hekta karibu 45,000 lakinina vijiji vyangu sita vya Kishoju, Kihanga, Katanda,Kibwera, Mlamba na Bishabaigulu, ninaambiwakwamba navyo vimepewa hekta 2000 wakati mtummoja wa Kagera Sugar amepewa hekta 45,000.Naiomba Serikali iangalie uwezekano wa harakasana kutenga hekta zisizopungua 20,000 kwa ajili ya vijijihivi sita ili wananchi wangu waweze kufaidika.87

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kagera tunahitajiChuo cha VETA, hakuna Chuo cha VETA, tunakiombakwa ajili ya vijana wetu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sisi Kagera ni wakulima wakahawa, tunategemea kahawa, bei ya kahawainasuasua, ninamwomba Mheshimiwa Waziri Mkuuatoe bei elekezi isimamie kuanzia shilingi 1000 nakuendelea isiwe inashuka. Hatuwezi kukubali leowanunuzi wanakuja na bei ya kwanza shilingi 1500mwisho wanashuka mpaka shilingi 700. Kwa hiyo,nitafurahi sana wananchi wangu wakijua kwamba beihasa ambayo ni ya kununulia kahawa ni shilingi 1500na kuendelea siyo wale walanguzi wanakuja kutuibia.Mheshimiwa Spika, kwa heshima kubwa sana,naunga mkono hoja kama nilivyosema. (Makofi)MHE. ALI JUMA HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante.Kwanza, namshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kunijaliaafya njema na kusimama katika Bunge letu Tukufukuchangia Hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu.Mheshimiwa Spika, nianze na Mabaraza yaWatoto; Mabaraza ya Watoto ni sehemu mojaambayo ina changamoto kubwa na ina watoto wenyevipaji sana na upeo mzuri wa kutoa hoja na hataukiwauliza maswali wanavyojibu utafikiria labda huyumtoto ameshakuwa Waziri.Mheshimiwa Spika, watoto wanavyotetea haki zaohutodhani kwamba hawa ni watoto wa umri midogo;wanajenga hoja vizuri, wanatoa ushahidi mzuri88

mahakamani na inafika wakati hata wazazi wenginewenye roho za kikatilii wanaowakatili watoto wao wakuwazaa wanafungwa kwa ushahidi wa watoto nausimamizi mzuri wa watoto. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kupitia Wizarahii ya TAMISEMI, itenge fedha hizi kwa ajili ya Mabarazaya Watoto. Mimi ni shahidi niliyepita kuwaangaliawatoto na hata Waziri wa Fedha wa hivi sasa alikuwaMwenyekiti wa Kamati hiyo, naye namwombaasimamie hili kwa sababu ni Waziri wa Fedha.Kuzisimamia Halmashauri kutenga fedha kwa ajili yakuwawezesha watoto, watoto wana vipaji vizuri,tutapata viongozi wazuri sana wa baadaye.Hata Wabunge wakija kugombea watakuwawazuri, nadhani tukianza kule ni sawasawa timu zampira tukianza kuwaanzisha watoto wadogo tutapatatimu nzuri. Basi Serikali ikiwekeza kule kwa watotonadhani tutakuwa na Viongozi wazuri. Naiomba sanaSerikali iangalie Mabaraza ya Watoto ni mazuri kwakweli. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lingine nije katika Hotuba yaWaziri wa Nchi, TAMISEMI, ukurasa wa 12 kuhusuMuungano; Muungano ni Chombo muhimu sana nakwa kweli watu wengine wanatafsiri labda Wazanzibarihatuupendi.Mheshimiwa Spika, lakini kinachopelekeatuonekane hatuupendi Muungano ni kero zaMuungano kwamba hazitatuliwi. Haya siyasemi mimitu, nimesoma gazeti la Zanzibar Leo, wapo baadhi ya89

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, hotuba zaozimesema kwamba sisi tunaupenda Muungano, lakinikinachotupelekea liwe ni jambo ambalo linaonekanahatuupendi, ni kero za Muungano kwamba,zinachukua muda hazitatuliwi.Leo ukiangalia Mheshimiwa Waziri ameorodheshakero 13 halafu anaeeleza kwamba zilizopatiwaufumbuzi ni kero mbili, kKatika hizo mbili ikiwemo mfukowa Jimbo. Mfuko wa Jimbo kweli ni kero yaMuungano? Mimi naona hii bado hatujawa seriouskatika kutatua kero za Muungano, na hili ndilolinalopelekea matatizo yanayotukuta Zanzibar. Lakinikama kweli Serikali zetu mbili zitakaa kwa dhati kabisana kujadili mambo ya kero za Muungano nakuonyesha umahiri wa kutatua kero za Muungano,nadhani wananchi wengi tutaupenda Muungano.Kwa hiyo, naziomba Serikali zote mbili zikaeziharakishe kutatua kero za Muungano na pianingemwomba Waziri kwa sababu leo kaeleza kerombili tu, hebu hizo kero 11 zilizobaki akija hapa akifanyamajumuisho atuainishie ni kero gani zilizokuwahazijatatuliwa? Mimi nadhani hizo ndiyo zitakuwa kerohasa za Wazanzibar kuliko hizo zilizotatuliwa.Mheshimiwa Spika, nije kidogo katika suala lamgomo wa Madaktari, lakini siingilii hili lililopoMahakamani. Naomba nieleze kabisa, nataka kutoarai tu, lakini kwanza ni-declare interest kwamba niMjumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii. Nadhanitulipoleta maelezo yetu au taarifa yetu, wewe ulikuwani shahidi na mimi niliichangia hii kwamba Serikali90

imefika wakati sasa ijenge hospitali kubwa ya kijeshikwa sababu tumeshaona kwamba majeshi ni chombokimoja ambacho kinafanya kazi kwa nidhamu kubwasana na ninadhani hata tulipowahoji hawa Wanajeshitukawaambia kwa ninyi hamfanyi mgomo kwenyehospitali? Wakasema hili jambo kwetu ni mwiko na waohawafanyi kazi kwa kulipwa kulingana na mishahara yavyeo vya kidaktari, bali wao wanakwenda kwamishahara ya vyeo vya Kijeshi. Kwa hiyo, ni taabu sanakufanya mgomo katika chombo hiki cha majeshi.Kwa hiyo, naiomba Serikali, umefika wakati sasaione ipo haja kujengewa hospitali kubwa majeshi yetuna wanajeshi wasomeshwe vizuri ili tupate hospitalikubwa mbadala. Kama Muhimbili watagoma leo,tayari Serikali inasema watu wakatibiwe Lugalo, lakiniLugalo haiwezi kukidhi haya ya wananchi wote kamavile Muhimbili. Lakini itakapojengwa hospitali kubwakama ya Muhimbili au zaidi ya Muhimbili, mimi nadhaniitakidhi haja na matatizo ya migomo yataondoka.Mheshimiwa Spika, nije katika ujenzi wa reli. Lazimatukubali kwamba sasa hivi Serikali ipo haja ya kuhimizaujenzi wa reli. Wenzetu hapa Mawaziri wahimize sualahili kwa sababu barabara zetu kwa kweli zinakufa sanana ajali zinaongezeka kutokana na kufa kwa barabarakwa magari makubwa ya mizigo. Tayari Serikaliinatuambia imetenga fedha za kutosha, hebu sasatuwaombe Mawaziri walisimamie hili. MheshimiwaMwakyembe tunakuamini, tunaomba ulisimamie hili.Mheshimiwa Spika, Mawaziri wanapokuwa benchi,wenzetu kwa kweli ndiyo wachangiaji wazuri, wasemaji91

wazuri, lakini tunaomba mnapokuwa huko sasa naninyi muwe kwa kweli watekelezaji wazuri. Uzalendotunataka utumike sana. Wenzetu muujali uzalendo ilimambo haya yatekelezwe. Hebu safari hii tuanze,wananchi watapiga kelele wapi? Nadhani kutakuwahakuna kelele kubwa, reli hii inapigiwa kelele na kweliwanyonge watafaidika na uchumi utakua. Kwa kweliipo haja reli yetu ijengwe.Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia, nizungumziejambo moja ambalo kwa kweli nchi yetu hiiinasikitishwa sana na inatuambia sana hapa kwambaiwapo itapewa masharti ya misaada kwamba labdatuingie katika ndoa ya jinsia moja; juzi MheshimiwaMembe alisema hapa kwamba tutafunga mkandakwa dhati kabisa, lakini misaada hiyo hatutaipokea. Sisitunaipongeza Serikali kwa hilo. Lakini Serikali yetu kwanini haipigi vita kwa vitendo ambavyo vinaashiriaushoga? Kwa mfano, the Comedy, wale madumemazima yanaji-act kama wanawake, wanarembuamacho kwenye vyombo vya televisheni kulikomwanamke mwenyewe, kweli watu wale hawaashiriiushoga? Hawaitangazi nchi yetu kama kweli? Kwasababu dume na dume lina-act mtu na mkewe. Hetutuangalie kwani kitendo kama hiki naomba Serikaliipige vita na penye wanawake waweke wanawake,wapo wasanii wanawake.Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.(Makofi)92

SPIKA: Ahsante sana. Sasa nimwite MheshimiwaBahati Ali Abeid na Mheshimiwa Namelok Sokoineajiandae.MHE. BAHATI ALI ABEID: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipatia nafasi hii mchana huu wa leona mimi kuwa mchangiaji wa hotuba hii ya WaziriMkuu.Mheshimiwa Spika, kabla sijaanza kuchangia,naiunga mkono hotuba hii kwa asilimia mia moja.(Makofi)Mimi mchango wangu wa kwanza naanzaukurasa huu wa 28 kwenye kitabu hiki cha maelezo yakiutendaji ambacho kimewasilishwa na MheshimiwaHawa Ghasia.Mheshimiwa Spika, Wabunge wengi Wazanzibarwamechangia fedha hizi za chenji ya Rada, lakini miminataka nizigusie kidogo fedha za chenji ya Radakwamba, kama Rada yenyewe imenunuliwa kwafedha ambazo zimetoka kwenye mfuko waMuungano, basi namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuuatakapokuja kutoa majumuisho atuambie hii ni haki yakuleta mchanganuo huu wa fedha hizi za chenji yaRada kupelekwa katika sehemu moja ya Muunganona sehemu nyingine fedha hizi zisiende? Kama fedhahizi za ununuzi wa Rada hazikutoka kwenye mfuko huuwa fedha za Muungano, basi atueleze ili tuwezekuelewa. Ninavyomjua Mheshimiwa Waziri Mkuu, hanashida na hili atatueleza tu ili tuweze kufahamu.93

Mheshimiwa Spika, lakini pia nichangie kwenyefedha ambazo ziliitwa mabilioni ya Kikwete, kwaZanzibar fedha hizi zilitolewa na Mheshimiwa Rais wetuJakaya M. Kikwete na Mheshimiwa Aman Karume kwawakati ule na zilikuwa na madhumuni ya kukuza mitajiya wafanyabiashara wadogo wadodo, wajasiriamali,na fedha hizi zilikuwa zinatolewa kwa njia ya mkopo,siwezi kusema kwamba fedha hizi hazikutolewa. Fedhahizi zilitolewa na zilitolewa kwa njia hiyo hiyo ya mkopokwamba waliokopa warejeshe ili na wengine wawezekukopa.Mheshimiwa Spika, lakini cha kusikitisha, fedha hiziuendelevu wake hauonekani. Kwa kuwa, Wabungetuliokuwepo wakati ule tulimwomba sana MheshimiwaRais wetu Jakaya Kikwete fedha hizi ziende mpakaZanzibar na ombi letu likakubaliwa hapa Bungeni, kwahiyo, mimi leo namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuuafanye mawasiliano na Zanzibar kwa kuwa fedha hizituliziomba ndani ya Bunge lako Tukufu afanyemawasiliano na Zanzibar ili tuweze kujua fedha hizi zikowapi na zinafanya nini. Kama zipo kwenye utaratibumwingine, basi pia tuweze kuelezwa ili wananchi hawawafanyabiashara ndogo ndogo ambao wanaitwaWajasiriamali wakituuliza tuweze kuwajibu; tunakuwahatuna majibu ya uhakika juu ya fedha hizi. Maraiswetu wetu hawa walizitoa kwa nia ya dhati yakuwaendeleza Watanzani wajasiriamali, naomba sanaSerikali izisimamie fedha hizi ili ziweze kuwanufaishawafanyabiashara walio wengi.Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine ambalonataka kulizungumza kidogo ni kuhusu Muungano.94

Mimi binafsi yangu naupenda sana na Wanzibar wengitunaupenda Muungano. Kama alivyosemaMheshimiwa aliyepita kuzungumza hapa, lakini miminapata mshangao kidogo, tunapoweza kuongeza hizikero za Muungano. Mheshimiwa Waziri Mkuu miminaomba uwe mwisho sasa wa kuongezeka kwa kerohizi.Mheshimiwa Spika, ni wakati muafaka sasa kablahatujakwenda kwenye mchakato wa Katiba mpya,basi kero hizi ziwe zimetatuliwa ili tukifanya mchakatohuu wa kupata Katiba mpya tusiweze kuwa tena nakero zile za nyuma zikawa ndiyo vikwazo sasa vyakusababisha Katiba yetu hii mpya nzuri ikaingia dosariza hapa na pale juu ya kutatuliwa kwa kero hizi.Mimi nimepata mshangao mwingine kuona sualahili la ushauri ambalo wamelitoa WaheshimiwaWabunge wa Zanzibar wa Majimbo, kusema Mfuko waJimbo baada ya kumalizia kwenye Halmashauri na zileHalmashauri hazihusiani na masuala ya Muungano kuleZanzibar, masuala haya ya fedha hizi za Mfuko waJimbo ziishie kwenye Ofisi ndogo ya Bunge ya Zanzibarnalo limejumuishwa hapa. Nisingependa kumkosoaWaziri Mkuu, lakini suala hili halikutendewa haki, tusemesasa kero zilikuwa 12 na iliyotatuliwa ni moja nazimebakia kero 11.Mheshimiwa Spika, sasa kila ninapopata nafasi yakusimama hapa au nikichangia katika mchangowangu wa maandishi, huwa napenda sanakuwasemea wastaafu, hawa waliokuwa ni95

wafanyakazi wazalendo ndani ya nchi hii ambayoinaongozwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.Kuna baadhi ya wastaafu walio wengi sana,wakistaafu wanapata mafao yao mapema, lakiniwapo wachache bado wanaendelea kudhalilika.Nasema kudhalilika kwa sababu kama mstaafuanayetoka Wizara ya Muungano akiwa Zanzibar, wapowengine mpaka wavuke Bahari waje Tanzania Barakufuatilia mafao yao, hili siyo jambo zuri. Naomba watuhawa wapatiwe mafao yao haraka iwezekanavyo.Mheshimiwa Spika, lakini siyo hilo tu. Katika kitabuhiki cha hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu,amewasifu sana Askari wa Jeshi la Polisi wanavyofanyakazi kwa umahiri mkubwa na uzalendo mkubwa wakupenda nchi yao. Lakini anapotokea Askari huyu kufa,mjane na familia yake wanateseka. Naomba wapatemafao haya haraka. Watanzania tumezoea kufarijianakatika misiba mbalimbali inapotokea, ni vema, sasakwa makusudi mazima Serikali ihakikishe mfanyakaziyeyote anapofariki, basi familia yake inayobakiaifarijiwe kwa kupewa mafao yake harakaiwezekanavyo kuliko kuachwa kuhangaika kuteseka nakudhalilika.Mheshimiwa Spika, kwa kuwa sisi wenginetumekuwa wachangiaji wa mwisho mwisho,nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii na ninaendeleakuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Ahsantesana.96

SPIKA: Ahsante. Mwisho wapi? Wewe siyo wamwisho, kwani bado kuna wengine. MheshimiwaNamelok Sokoine!MHE. NAMELOK E. M. SOKOINE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipatia nafasi ili nami niwezekuchangia katika hotuba ya bajeti ya Ofisi yaMheshimiwa Waziri Mkuu.Napenda kuchukua nafasi hii kumpongezaMheshimiwa Waziri Mkuu kwa kusimamia Serikali kwaumakini katika kutekeleza dhana ya Chama chaMapinduzi. Vilevile nachukua nafasi hii kuwapongezaMawaziri na Watendaji wote waliosimamia utekelezajihuo.Mheshimiwa Spika, pamoja na misukosukoambayo bado inaendelea kuzikabili nchi mbalimbaliduniani kwa viwango tofauti na Tanzania tukiwawamojawapo, lakini bado tumeweza kupata mafanikokama tulivyooona katika hotuba ya Mheshimiwa WaziriMkuu.Mheshimiwa Spika, kama muda utanitosha,nitazungumzia mambo manne. Nitazungumzia tatizo laardhi, adha wanazokutana nazo wakazi wa jamii yaNgorongoro; nitazungumzia pia tatizo la maji na tatizowanalokumbana nalo wakazi wa Jiji la Arusha.Mheshimiwa Spika, matatizo ya ardhi ni mengimno, lakini mimi nitazungumzia mambo matatu tu.Nitazungumzia tatizo la ardhi wanalokumbana nalojamii ya wafugaji. Kuna tatizo kubwa sana kati ya97

wafugaji na wakulima, kuna tatizo kubwa sana kati yawafugaji na maeneo ya Hifadhi za Wanyamapori, lakinipia kuna tatizo la ardhi la mipaka kwenye Wilaya zetu.Mheshimiwa Spika, hivi karibuni Kamati yetu yaKilimo, Maji na Mifugo tulikwenda kutembelea eneo laIkwiriri. Kulikuwa na ugomvi mkubwa sana kati yawakulima na wafugaji katika eneo hilo ambao hataimepelekea mauaji. Lakini kitu cha kushangaza, Serikalihadi hivi sasa wameshindwa kutatua migogoro hiyo.Wafugaji waliokwenda katika eneo lile walikuwawamejitayarisha kwa ajili ya ng’ombe 50,000 lakini kitucha ajabu kuna ng’ombe zaidi ya 300,000 na hataSerikali hadi hivi sasa haijatoa tamko lolote.Tulipokwenda kukutana na jamii ile, walisemaitakapofika tarehe 30 mwezi huu wataamua kuchukuasheria mkononi, kwani hawataki tena kuwaonawafugaji wale katika eneo lile.Mheshimiwa Spika, zaidi ya hilo, pia lipo tatizokatika hifadhi za wanyamapori. Kuna hifadhi ambazozimepakana na jamii ya wafugaji. Hivi karibuni tukiwakatika Bunge hili, tarehe 12 Juni, kwenye Hifadhi yaMikumi Wilaya Kilosa wapo ng’ombe walipigwa risasi,walikwenda kunywa maji katika eneo lile na hiiimekuwa kawaida kabisa kwa Hifadhi za Wanyamapori(TANAPA) kupiga ng’ombe risasi au kuwachukuang’ombe wale na kuwadai watu fidia ya Sh. 10,000/=kwa ng’ombe mmoja. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hali kadhalika katika Wilaya yaMonduli kuna mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya yaMonduli na Arumeru, hali kadhalika Wilaya Longodo na98

Arumeru. Najua Serikali ina suluhisho ya matatizo yotehayo, lakini kitu cha kushangaza ni hadi sasa migogorohiyo inaendelea na Serikali haitoi tamko lolote.Mheshimiwa Spika, nafahamu nchi yetu inawataalamu wengi wa mifugo ambao wanawezakutuambia ng’ombe mmoja kwa mwaka mzimaanakula kilomita ngapi na baada ya kufanya hivyowakafanya sensa ya wanyama na kujua tuna mifugowangapi, kila watu wakabaki na mifugo yao katikaMikoa yao, wakapewa maeneo ambayo itakuwa kwavitalu na mifugo ile ikala kwa rotation, badala ya hivisasa ambapo wafugaji wanazunguka tu hawaelewiwana-belong in which society. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hata ukiangalia dhana yaKilimo Kwanza, haielezi mfugaji anafaidikaje. Wakulimawanapewa pembejeo, lakini mfugaji haelezewianafaidikaje na kuwa na dhana ya Kilimo Kwanza.Mheshimiwa Spika, jambo la pili nitakalozungumzani kuhusu Hifadhi ya Ngorongoro. Kuna jamii yawafugaji inaishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.Mwaka 2008 Serikali iliwasimamisha jamii ile kulimabustani, sote tunafahamu ni jamii ya wafugaji ambaohawafanyi biashara na hawana shughuli nyingineyoyote zaidi ya mifugo. Lakini wakati Serikaliinawasimamisha, haikuwaambia pia watapata wapichakula na wataishije.Mheshimiwa Spika, hivi sasa jamii ile wanatesekasana. Unapofika Karatu, Arusha na kila mahaliunakutana na akina mama wanakwenda kuuza ugoro,99

akina baba dawa za kienyeji, vijana wamekwendakuwa walinzi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, vijana wale wenginewanaweza kufanya kazi za ulinzi ndani ya hifadhi ile napia wanaweza kuajiriwa wakawa madereva nakufanya petty jobs, lakini kitu cha ajabu wameachwatu. Hakuna kipaumbele chochote kinachotolewa kwajamii ile. Nitafurahi sana wakati Mheshimiwa WaziriMkuu anahitimisha hotuba yake atueleze hili laNgorongoro. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nafahamu kuna Baraza laWafugaji ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro, lakinilimekaa kisiasa zaidi. Nilikuwa nashauri kama Serikaliinaweza, kungeundwa Mabaraza mengine mawili;Baraza la Wanawake na Baraza la Vijana; naMabaraza hayo yakawezeshwa na wakapata elimu yaujasiriamali.Bahati nzuri hili liko chini ya Mheshimiwa WaziriMkuu ambapo kuna Uwezeshaji na Uwekezaji.Mabaraza haya wakatafutiwa wawekezaji ambaowatawafundisha wakapata mbegu bora ya mifugo,lakini pia kutokana na mbegu hiyo ya mifugowakaweza ku-pack maziwa, cheese na kadhalikaambayo itauzwa katika hifadhi hiyo, wakaweza kupatapato lao kuliko hivi sasa wanavyoteseka. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lipo tatizo linalowakumbawakazi wa Jiji la Arusha kwamba hatuna soko, nahatuna stendi. Soko la Arusha Mjini lilijengwa mnamomiaka ya 1970 wakati ule population ya watu wa100

Arusha ilikuwa kama laki moja hivi, tofauti na hivi sasaambapo population ya Mji wa Arusha ni 590,000. Sokolile linatumiwa na watu wa Wilaya tatu za ArumeruMashariki, Magharibi na Arusha Mjini. Hata watu kutokaWilaya nyingine wanapokuja pale kuleta mazaowanauza kwa jumla na kuondoka. Kuna msongamanomkubwa sana katika Soko la Arusha Mjini kiasi kwamba,inafikia saa 10.00 jioni kuna barabara imefungwa, watuwame-pack bidhaa kila mahali.Mheshimiwa Spika, nilijaribu kuzungumza nawengine, wananiambia kwamba wana marejesho kilawiki, hawana namna ya kufanya marejeshowasipofanya biashara ya kuuza chakula, kwani hiyondiyo biashara ya uhakika ambayo wanaiamini. Lakinisasa nadhani ni wajibu wa Serikali kuwatafutia sehemunzuri ya kufanyia biashara kwa kuwajengea sokokubwa la kisasa. (Makofi)Siyo hilo tu, pia tuna tatizo la stendi. Arusha Mjinihakuna stendi. Tunaomba Serikali ifikirie ni kwa namnagani tunaweza tukajengewa stendi na soko la kisasa.Pale Arusha Mjini kuna eneo la wazi la NMC ambalo nimashuhuri kwa kufanyia mikutano ya dini na kisiasa nahata hivi sasa limepata umashuhuri mkubwa, linaitwaArusha Tariri Square kwa ajili ya mikutano ya kisiasa.Mheshimiwa Spika, nilikuwa nashauri, badala yabarabara hizo kuendelea kufungwa na watu kuwekavyakula njiani ambayo ni hatari, kwani kuna milipukoya magonjwa inayotokea kwa wingi sana wakati wamvua. Nilikuwa nashauri Serikali itukubalie eneo lilewatu waweze kuweka vitu kwa muda wakati tuko101

kwenye kipindi cha mpito tukisubiri kujengewa sokokubwa la kisasa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ukiacha hilo, lipo tatizo la majiambalo linatukabili wakazi wa Arusha Mjini na Wilayazote sita ndani ya Mkoa wa Arusha. Tatizo la maji nikubwa sana ndani ya Mkoa wa wetu wa Arusha.Wilaya zote sita hazina maji ya kudumu. MheshimiwaRais alipokuja Arusha mwaka 2010 alisema apelekeweArusha Water Plan. Lakini mpaka sasa master plan yamaji hajapelekewa, haijaandikwa na hatufahamu nikwanini. Tulikuwa tunaomba Serikali isimamie ili Wilayazote sita ndani ya Arusha Mjini ziweze kupata maji yakudumu.Mheshimiwa Spika, vilevile tarehe 24 Juni, 2011wakati wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu,Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassaaliomba Monduli tuingizwe kwenye list kama ilivyoMakondeko, Chalinze Water Basin. Nami leo kwa maraya pili nasimama kuendelea kuiomba Serikali ili tuwezekuingizwa katika list hiyo. (Makofi)(Hapa kengele ililia kuashiria muda wa Mzungumzajikwisha)MHE. NAMELOK E. M. SOKOINE: Kengele ya pilihiyo?SPIKA: Ya pili mama, ahsante.MHE. NAMELOK E. M. SOKOINE: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. (Makofi)102

MHE. MOHAMED H. MISSANGA: Mheshimiwa Spika,kwanza, namshukuru Mwenyezi Mungu Sub-hanahwataalakwa kunijalia afya na uzima na salama, nakuniwezesha kushiriki katika hotuba hii muhimu yaMheshimiwa Waziri Mkuu. Nakushukuru wewe kwakunipa nafasi ya kuchangia na pia nitumie nafasi hiikumshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete naSerikali yake kwa kututengea maeneo mapya yautawala.Mheshimiwa Spika, tumepata Wilaya mbili mpyajambo ambalo tumelilia kwa muda mrefu na hatimayelimefanikiwa. Hivyo, tuna kila sababu ya kutoa shukrani.Tumepata ma-DC wazuri, nawapongeza na hasa DCwangu wa Wilaya mpya ya Ikungi. Comrade ManjuMsambya ambaye ni mwenzetu tunamfahamu vizurisana. (Makofi)Nimpongeze sana Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa waSingida Dkt. Paseko Kone kwa kazi nzuri ambayoanaendelea kuifanya na kutupa ushirikiano sisiWabunge na wananchi kwa ujumla. Nimtakie kila lakheri na kuahidi kwamba tutaendelea kushirikiananaye vizuri. (Makofi)Mheshimiwa Spika, tarehe 26 Agosti, kutakuwa nasensa kama tulivyoarifiwa. Naikubali na tumeshafanyakazi ya kuwahamasisha wananchi kama tulivyotakiwa,na wako tayari kushiriki katika Sensa. Ombi langu nikwamba kwa muda mrefu Mheshimiwa Waziri Mkuuanajua kulikuwa na concern kwamba, sisi watu wa103

Mkoa wa Singida tunaitwa Mkoa wa mwisho, jamboambalo siyo haki na kwa kweli hatustahili kuitwa kuwaMkoa wa mwisho kutokana na maendeleo ambayoyamefikiwa katika Mkoa wa Singida. Haiwezekanikabisa! Ni takwimu mbovu za miaka mingi zilizotumikaambazo mimi nachelea, ni kwanini hazitakikurekebishwa? Ukiangalia Mkoa wa Singida na Mikoamingine ambayo sitaki kuitaja hapa nitawa-offendwatu. Haiwezekani Mkoa wa Singida kuambiwa kuwani wa mwisho. Haiwezekani!Mheshimiwa Spika, sasa naomba kupitia sensa hiikwa sababu katika madokezo, najua vigezo vyakimaendeleo ambavyo viko mle ndani vitatumika.Namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba sualahili sasa angalau limepata fursa hii ya sensa, sasaitumiwe ili kupata takwimu sahihi za kuweza kuuwekaMkoa wa Singida katika mahali pake. Hatuko tayarikuendelea kuambiwa kwamba sisi ni Mkoa wa mwishowakati Mheshimiwa Waziri Mkuu umekuja mara nyingina hata wewe huridhiki. Lakini sijui ni watu gani hawaambao wanaendelea kutunyanyasa kwa kutuwekaMkoa wa mwisho wakati sisi hatustahili kuwa wamwisho. (Makofi)Mheshimiwa Spika, moja ya kero ambazowapigakura wangu wamenituma na wamekuwawakinililia, ni suala la soko la zao la biashara la alizeti.Tulihangaika sana, muda mrefu hatukuwa na zao labiashara. Sasa tumepata zao la biashara la alizeti.Tatizo ni kwamba wako walanguzi ambaowanakwenda vijijini na mashambani kuwalanguawananchi kwa kuwapa bei duni kabla hata alizeti104

yenyewe bado ni mbichi na iko shambani. Sasaukienda kuwahamasisha, wanasema tunalima alizeti,lakini soko hatupati, mnawaachia walanguzi wanakuja.Tunatoa majibu kwamba sisi hatuwaachiiisipokuwa nyie wenyewe mnaridhika. Lakini ukweli nikwamba walanguzi wale wanawanyanyasa sana nakuwadhulumu wananchi wetu. Sasa hivi karibu Mkuuwa Mkoa wa Singida ametoa maelekezo kwambaalizeti inunuliwe na Vyama vya Ushirika na katikamagulio. Jambo hili linapingwa na baadhi ya watuambao wana maslahi binafsi. Mimi kama Mbunge waJimbo ambaye wananchi wangu wakulimawanalalamika kila siku, alizeti yao inapotea,wanadhulumiwa na walanguzi, hao watu wa katikati.Nitakuwa mtu wa ajabu sana kama nikipingana naazimio la Mkuu wa Mkoa ambaye nia yake nikumsaidia na kumkomboa mkulima apate bei sahihi nanzuri ya zao lake la biashara. Kwa maana hiyo,naliunga mkono azimio la Mkuu wa Mkoa kwamba,watu waende kwenye Vyama vya Ushirika au maguliokwenye ushindani. Wewe usiende kuwalangua watukule Kijiji wakati alizeti yenyewe bado, halafu unaanzakumdanganya gunia Sh. 15,000/= wakati sasa hivi beiya soko kwa gunia ni Sh. 40,000/= tayari Serikaliimeshatoa bei elekezi ya Sh. 600/= kwa kilo, jamboambalo hawa walanguzi hawawezi wakatoa kitu kamahicho hata siku moja.Mheshimiwa Spika, naomba sana tutoe ushirikianokwa Mkuu wa Mkoa na Serikali yake kwa sababu niayake ni kumsaidia mkulima ili asiendelee kunyonywa,kwani amenyonywa kwa muda mrefu sana, na sisi105

viongozi wengine tushiriki kutoa elimu inayostahili.Uamuzi wowote unaweza ukawa na pande mbili; unafaida na hasara zake. Hakuna maamuzi ambayoutafanya ambayo hayatakuwa na pande mbili. Kaziyako ni kuangalia uzuri uko wapi na yale machacheambayo unaona kwamba yana mapungufuunayafanyia kazi. Namwomba Mkuu wa Mkoa kamakuna matatizo yataonekana dhahiri kabisa, labdakuna hiyo contract farming na nini, lakiniwameshaahidi Serikali ya Mkoa iwe tayari kukaa nawale wafanyabiashara wenye viwanda, watatue yalematatizo. Tusi-generalise tukazuia mpango mzuri etikwa sababu ya watu ambao pengine wana maslahiyao.Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana hilolifanyike. Lakini kazi kubwa zaidi, sisi ni viongozi wa siasa,viongozi wa kuteuliwa, tuendelee kuwaelimishawananchi wetu umuhimu wa kuuza mazao yao katikaVyama vya Ushirika na kwenye magulio na waachanekabisa na hao walanguzi ambao wanakwendakuwadanganya katika maeneo yao mbalimbali. Hilondilo lingine ambalo nilitaka nilisemee. (Makofi)Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nilitakanilisemee ni suala zima la ndege waharibifu. Hakunahata siku moja hapa nimezungumza bila kugusiandege waharibifu na Serikali yote inajua, Waziri Mkuuanajua, Mawaziri wa TAMISEMI wote wanajua, kila mtuanajua pale mpaka Rais wa nchi nimemwambiaalipotembelea kule Singida, lakini hakuna utatuzi.Ndege waharibifu wanaharibu sana mazao yawananchi, mazao ya biashara na chakula. Watu106

wanafanya jitihada sana kulima, lakini maskini yaMungu at the end of the day ndege wanakula kilechakula. Sasa wananchi hawaelewi hivi ni mpaka liniSerikali itasikiliza kilio chao cha kutafuta njia nzuriambazo zinaweza zikawasaidia wananchi wetuwakaondokana na adha hii.Mheshimiwa Spika, hii ni kadhia kubwa.Namwomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu aliangaliehili. Naambiwa hii ndege ambayo tunaitumia yakuangamiza ndege inamilikiwa na nchi sita au saba.Ndege yenyewe ni ya miaka karibu thelathini, kuu kuu.Kwanza ni kuu kuu, halafu moja, na pia ni ya nchi sitaau saba. Tunazungumzia Kilimo Kwanza, huwezikufanikiwa Kilimo Kwanza kama ndege waharibifuwataendelea kumaliza chakula cha wananchi.(Makofi)Mheshimiwa Spika, sasa nishauri, it is high time sasaSerikali iangalie uwezekano wa kupata ndege zakekama siyo mbili, basi angalau moja ya kuanzia.Tuachane na hii ambayo wakati wewe unaitaka ikoMalawi, unaambiwa sijui iko Botswana, maraunaambiwa sijui iko Angola. Hivi kweli tunadhaniaKilimo Kwanza wakati tunategemea ndege moja tuambayo inatutesa kiasi hiki? (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba sana tununue ndegezetu, na zije kwa wakati. Mazao yanaanza Januari,Februari na Machi, muda unajulikana, kwanini Wizaraya Kilimo hailijui hili mpaka tuanze kuombaombandege? Sasa Wizara ya Kilimo iweke utaratibu, Serikaliinunue ndege moja au mbili na kadhalika. Lakini juzi107

Jumatatu saa 3.00 usiku TBC1 walirusha kipindiwakaonesha mgunduzi mmoja amegundua mashineambayo inafukuza ndege waharibifu na hawawanyama waharibifu. Hebu msaidieni yule mgunduzimwananchi, Mtanzania ili kusudi tupate suluhu juu yajambo hili ambalo linafanyika. (Makofi)Mheshimiwa Spika, mradi wa maji wa Benki yaDunia umefeli. Jina lake ni kubwa World Bank lakinihauna kitu. Mimi nadhani tusidanganyane hapa.Tutafute njia mbadala ya kuwapatia watu wa Singidamaji. Tusiendelee kusema kwamba, mna mradi waBenki ya Dunia, hakuna kitu ni bomu tupu hapa. Mradiuna miaka 10, una vijiji kumi. Wewe angalia, yaanimwaka mmoja kijiji kimoja, mwaka mmoja kijiji kimoja,ni mradi gani huo?Mheshimiwa Spika, namwomba sana MheshimiwaWaziri Mkuu atutafutie mradi mwingine ambao utakidhimahitaji ya maji hasa kwa maeneo ya vijijini. (Makofi)Mheshimiwa Spika, namwomba MheshimiwaWaziri Mkuu atupe progress report ya suala laMahakama ya Kadhi. Yeye amekuwa anasimamiamazungumzo kati ya Serikali na jopo la Mashehe kwaajili ya kupata ufumbuzi wa suala la Mahakama yaKadhi. Sasa mimi namwamini Mheshimiwa Pinda, ninahakika ameifanya kazi hiyo na anaendelea kuifanya.Ningependa sana wakati atakapokuwa anajumuisha,tupate progess report ya suala la Mahakama ya Kadhi.(Makofi)108

(Hapa kengele ya pili ililia kuashiria muda waMzungumzaji kwisha)SPIKA: Ahsante, tunashukuru sana kengele ya pili.MHE. MOHAMED H. MISSANGA: Eeh. MheshimiwaSpika, naunga mkono hoja. (Makofi)MHE. ABDULKARIM E. H. SHAH: Mheshimiwa Spika,nami nakushukuru kwa kunipa fursa hii adhimu yakuweza kuchangia hoja yetu ya chini ya Ofisi ya WaziriMkuu. Nami niungane na wenzangu kwanza kuungamkono hoja hii mia kwa mia. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie kwanininaunga mkono hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuumia kwa mia kama kiongozi wetu wa shughuli zaKiserikali hapa Bungeni, kwa maana ndiye kinara wausimamizi, utekelezaji wa kero za wananchi katika nchiyetu. Naomba niseme kwamba, tunasemwa sanawakati mwingine kwa kuwa sio wachangiaji sana,hatusemi sana, lakini naomba tu siku ya sikutuhukumiwe kwa kazi zetu tulizozifanya. Naaminiwananchi wa Mafia walionichagua hawataniuliza sikumoja kwanini hujatoa miongozo mingi hapa Bungeni,sijatoa taarifa nyingi wala kuomba nafasi za kuwezakusimama kila wakati. Lakini akili ni nywele, kila mtu anazake na tumekutana hapa Dodoma kwa niaba yawananchi wetu. Kwa hiyo, wakati mwingine kila mtuanakufa na lake.Mheshimiwa Spika, binafsi nasema naombaniipongeze sana na kutoa shukrani nyingi kwa Serikali109

yetu hasa kwa kazi nzuri ambayo ilikuwa kero sugu yaujenzi wa Gati la Mafia. Mheshimiwa Waziri Mkuunaomba upokee shukrani hizi za wananchi wa Mafia,Gati letu linaendelea na wakati wowote litakamilika.Mheshimiwa Rais pamoja na wewe na Wizara yote naikiwezekana kwa sababu ni kitu ambacho ni chakihistoria, basi Wizara ya Uchukuzi chini ya MheshimiwaDkt. Mwakyembe, hebu alika siku hiyo ya kuja kuzinduaBaraza lote la Mawaziri lije kule maana ni jambo lakihistoria kwa Wilaya yetu ya Mafia. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naishukuru tena Serikalikwamba Airport inajengwa na vifaa viliishafika na kaziinakwenda vizuri.Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya MheshimiwaMwakyembe nakuomba upokee shukrani zetu zaWizara yake na Idara zake zote kupitia MheshimiwaWaziri Mkuu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara katika ujenziwa uwanja wa ndege, kuna barabara na iliishafanyiwatathmini. Ninachokuomba kupitia Ofisi ya Waziri Mkuuna Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe anatusikia hapakwamba tutakuja kuelezewa mengine, maana yakehatuwezi kupata muda, muda wenyewe ni mchache,lakini tathmini tayari imefanyika zaidi ya miaka minneiliyopita. Naomba sana, ujenzi wakati wowoteunategemewa kufanyika, na ninaamini katika bajeti hii,inaelewa fedha ya kulipa fidia (compensation) walewatakaohamishwa itatolewa, lakini muangalie na haliya maisha ilivyo.110

Mheshimiwa Spika, lugha yetu ya kuongea ninyepesi, hatutoi ukali, tunataka kwa maana yakuiomba Serikali iangalie tathmini iliyofanya miakaminne iliyopita na hali ilivyo sasa hivi. Wakati ule mfukowa sementi kule Mafia ulikuwa Sh. 13,000/= lakini leo niSh. 20,000/= mpaka Sh. 22,000/=, na wakati mwinginekama pepo za bahari zinakuwa kali, usafiri unakuwamgumu.Mheshimiwa Spika, suala lingine nililokuwa natakakulizungumzia baada ya shukrani hizo, katika jambololote la heri na changamoto zinakuwepo. Kwa hiyo,naomba sana kutoa changamoto zangu kupitia Ofisiya Waziri Mkuu kwa sababu pengine sitaweza kupatabahati ya kuchangia Wizara zote. Naomba sanatuangalie, Mafia tumeanzisha Benki ya Watu wa Mafia.Tumejitahidi sana, leo tunakaribia mwaka mmoja nanusu. Hali yetu tumechemsha katika kukusanya mtajiwa Shilingi milioni 250 kwa ajili ya kupata licence yakuanzisha benki ile. Lakini tumejitahidi, tuna fedhachache Shilingi milioni kama 40 tulizoweza kufikia.Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana kupitiaOfisi ya Waziri Mkuu na bahati nzuri Mheshimiwa MamaNagu anatusikia kupitia Baraza lake la Uwezeshaji,atusaidie katika kuihuisha hii benki iweze kufanya kazi.Benki ya Watu wa Mafia itatusaidia sana kwa sababuwote tunalalamika na tunafahamu kwamba Mabenkihaya ya kibiashara shughuli zake zinakuwa nzito sanakatika ukopaji. Tukianzisha Benki yetu na mkituwezeshakama hamwezi kutupa grant, kama mlivyowezakuisaidia Benki ile ya Wanawake, basi tusaidieni naBenki ya Watu wa Mafia tuweze kuihuisha ifanye kazi.111

Naona Mheshimiwa Nagu anatikisa kichwa, nafikiriameelewa na atatusaidia. Nakushukuru sana.Mheshimiwa Spika, lingine ni kero ya watumishi wakawaida. Hili ni jambo la nchi nzima, watumishi hasawa kada ya afya. Tunajua tupo katika mtikisiko sasahivi wa huduma hii kupitia Madaktari wetu. Lakinijambo lolote lile linakuwa na mwisho, hakuna jambolisilokuwa na mwisho, yatakwisha, yatatulia na nafikiriSerikali kama alivyosema Mheshimiwa Waziri Mkuukwamba wako mbioni katika kumaliza kero zao, basilitakapomalizwa tuangalieni sana watumishi wa Idaraya Afya katika Wilaya ya Mafia.Mheshimiwa Spika, tuna kazi nzito. Ninapata mzigomzito, kila inapotokea dharura, basi huwa inabidinichangie katika kumsafirisha yule mgonjwa kutokaMafia kumleta Dar es Salaam. Gharama ni kubwa namimi niko mmoja, watu wanaougua ni wengi, wakatimwingine tunachemsha, inabidi tukusanye wagonjwawawili, watatu kuwasafirisha kwa njia ya bahari, uwezowa ndege hatuna. Lakini tukipata wataalamu hawa nabahati nzuri vifaa vipo sasa hivi Mafia X-Ray inafanyakazi, mtaalamu yupo na baadhi ya vifaa kamaultrasound na vingine vipo vitaweza kusaidia katikakuwatibu pale pale hawa wagonjwa wanaotokea kuleMafia. Naomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu nabahati nzuri kaka yangu Dkt. Hussein na Dkt. Seifwanatusikia, mpo pale mtuangalie sana mtuoneehuruma watu wa Mafia tunapata kazi nzito, aliyekuwaBara tofauti na sisi Visiwani. Hali ya Visiwa mnaifahamu,kwa hiyo, sina mengi ya kusema.112

Mheshimiwa Spika, lakini suala la Walimu pia nikero katika Wilaya yetu hasa Walimu wa Shule zaSekondari na Msingi kwa sababu tatizo tunalopataMafia kwa uchache wa wanafunzi waliokuwa katikashule zetu na vigezo vilivyowekwa na Wizara ya Elimukwamba Mwalimu mmoja kwa wanafunzi 40, matokeoyake Walimu wachache tunapata na Shule, inakuwana Walimu wawili hadi watatu. Kwa hiyo, naombasana suala hili na bahati mbaya miaka mitatu iliyopitaMafia hatukupata Walimu waliopangiwa kuja Mafia.Kwa hiyo, naomba mwaka huu tupangiwe Walimu natutajitahidi kuongea nao na bahati nzuri tunaboreshamazingira yao ya kuishi vijijini. Tunawawekea katikanyumba za Walimu umeme jua sasa hivi, kwa hiyo,hata akiwa pale ataweza kuwasiliana na wenzake kwamaana ya kuweza kupata huduma zile ambazo yeyeatazihitaji kama za kimawasiliano. Kwa hiyo, hili lipo nabahati nzuri kuna mengine tutakuja kuchangiatutakapokuwa katika Wizara ya Nishati na Madini,tutayasema mengi mazuri ambayo sasa hivi Mafiayanaelekezwa.Mheshimiwa Spika, jambo lingine na hili ndilojambo sugu ambalo nataka nilizungumzie, MheshimiwaRais alipokuja Mafia alitoa ahadi, tulimwomba naakasema itatekelezwa. Ahadi kubwa ambayoinatusumbua sasa hivi ni maji katika visiwa vidogovidogo vya Mafia. Tumejitahidi sana, lakini kamaWilaya kutokana na kigezo tunachopata cha fedha,fedha ndogo tunazozipata za ruzuku, basi tunaombasasa Wizara ya Maji na Umwagiliaji ilibebe hili, wajekutusaidia katika kuhakikisha kwamba ahadi yaMheshimiwa Rais inatekelezwa na yale maji yaliyokuwa113

na bahati nzuri, visima tumeshachimba, sasatunatafuta nguvu ya kuweza kununua pipe nakuzivusha na siyo mbali sana kama kilomita sita tu. Kwahiyo, tusaidieni Serikali na naomba Mheshimiwa WaziriMkuu alibebe hili suala awaambie Wizara itafute fungutuweze kuondoa kero hii ambayo ni ahadi yaMheshimiwa Rais. Ni aibu tutakapomaliza kipindi chetucha safari hii kwa maana awamu hii, basi ahadi ileisipotekelezwa itaonekana sijui hatusemi ukweli au kitugani. Kwa hiyo, naomba sana hii ahadi sasa hiviSerikali Kuu muibebe na iweze kutekelezwa.Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo natakakulizungumza ni suala la uvuvi. Mafia asilimia kati ya 70au 80 sisi ni wavuvi tunategemea bahari. Lakini kituambacho kinatusibu sasa hivi kupitia Wizara yaMaendeleo ya Mifugo na Uvuvi, naomba sanaMheshimiwa Waziri Mkuu atusaidie kuwaambia watuwa Wizara hiyo waunde Kamati Maalum ya kuwezakuchambua na kufahamu kwamba ni jinsi gani bahariyetu inaweza ikachangia pato la Taifa.Mheshimiwa Spika, ni aibu kuambiwa kwambanchi hii ya Tanzania uvuvi au bahari inachangia asilimiamoja. Hebu basi wawezesheni hawa wazunguke katikanchi jirani tu zilizokuwa katika nchi hii hii ya bahari yaHindi waone jinsi bahari wenzetu wanavyoitumia vizurikatika kuondoa umaskini au kuwezesha nchi yaokupata fedha, na hizi kero nyingine kwa mfano zaMadaktari fedha zao hata mishahara itapanda.Mheshimiwa Spika, leo naunga mkono, lakininaomba suala la uvuvi lizungumzwe sana kwa sababu114

wananchi wa Mafia na ukanda wa Pwaniwanawategemea. (Makofi)MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Spika, ahsante.Ama kweli mama ni mwenye huruma. Nianze kutoamchango wangu kwenye maafa. Katika ukurasa wa58 Na. 95 inasema: “Katika mwaka wa 2011/2012Serikali imeshughulikia matukio ya maafa katikamaeneo mbalimbali nchini.” Pia katika ukurasa wa 96imetaja waathirika wa Mabomu ya Gongolamboto.Hapa nitamtaka Mheshimiwa Waziri Mkuu,atakapokuja kufunga mjadala atuambie ni kwa ninihajaonyesha kwamba Zanzibar kulitokea maafamakubwa ambayo yaliwashtua Watanzania na duniakwa jumla?Mheshimiwa Spika, nianze kuchangia katikaMuungano. Kwa kawaida Muungano wowote dunianihutegemewa kuongeza nguvu kwa walioungana. Siyokupunguza nguvu zote za upande huo na kuelekezaupande mmoja ukabaki bufurutupu. Zanzibar inauwezo wa kupanga mipango yake ya kiuchumi,huduma za jamii na miundombinu. Lakini huwezikupanga haya bila kujua takwimu ya watu wako nakujua makisio ya wageni wako. Zanzibar haina uwezowa kudhibiti lolote.Tuangalie mfano wa Hong Kong na Mak Hou hivini visiwa vya China. China kwa kuvienzi nakuviendeleza visiwa vyake, basi pamoja na kwambaChina ni moja, lakini Mchina kutoka Bara hawezikuingia Hong Kong na Mak Hou kiholela bila udhibiti waaina yoyote.115

Mheshimiwa Spika, uingiaji wa Zanzibar ulikuwepoutaratibu kabla ya Muungano na hata baada yaMuungano, lakini ikafanywa nongwa vikaondolewa.Leo Zanzibar ni nchi pekee duniani ambayo hainauwezo wa kudhibiti uingiaji wa watu. Unaweza kutokaCongo ukapitia taratibu zote za kuingia Dar es Salaam,kwani kwa hilo mko makini, lakini ukishaingia Dar esSalaam, basi utaingia Zanzibar na utateremka kamashamba la bibi.Mheshimiwa Spika, hakuna ubishi kwambaMataifa mengi duniani yameungana, lakini tusiishiehapo twende mbali zaidi tuone huu Muungano wao niMuungano wa namna gani? Ni Muungano wakumezana au ni Muungano wa kudhoofishana kamavile ambavyo Muungano huu unaidhoofisha Zanzibarna kuifuta katika ramani ya dunia. (Makofi)Mheshimiwa Spika, napenda niseme jambo moja,mpaka unapomwona mtu mzima analia, basi anajambo kubwa, mwulize unalilia nini? Leo Zanzibarkusema hawataki Muungano huu, basi waulizwekulikoni? Wanautaka ama hawautaki? Vilevile tujiulizekama huu Muungano wetu ni mzuri au ni tunu yakuenziwa? Mbona umedumu miaka 50 hadi leohakuna hata mmoja aliyetamani kujiunga naMuungano huu?Mheshimiwa Spika, nitarudia. Nasema tujiulizeikiwa Muungano wetu ni mzuri ama ni tunu yakuenziwa, umedumu miaka 50, mbona hakuna hatammoja au hata nchi moja iliyotamani kujiunga na116

Muungano huu na hata wakati lilipokuja wazo lakuunda Afrika Mashariki hakuna aliyetamanikuuendeleza huu?Mheshimiwa Spika, hata Umoja wa Ulayaulipoundwa, walianza na wanachama sita, leotakribani ni 30. Huu ndiyo Muungano. Nimalizie kwakusema kama aliyosema Waziri Membe. MheshimiwaMembe alisema: “Watanzania tutakuwa tayarikujifunga mikanda tufe kwa njaa kuliko tusaidiwetuingie katika ndoa za jinsia moja.” Wazanzibar naowanasema tuko tayari tufe kwa njaa kuliko kubakiakatika Muungano huu dhalimu ambao haututendeimema, ambao ni Muungano wa kutudhoofisha na wakutudhalilisha na kutufuta katika ramani ya dunia.Mheshimiwa Spika,...TAARIFASPIKA: Taarifa, lakini kengele itagongwa sasa hivi.MHE. MOHAMED AMOUR CHOMBOH: MheshimiwaSpika, nataka kumpa taarifa ndugu yangu kutokaZanzibar, Wazanzibar wanaojua kwao ni Zanzibar,wenzangu kama mimi siwezi nikakataa Muunganohata siku moja. Kwa hiyo, hiyo ni yake yeyemwenyewe. (Makofi)SPIKA: Ahsante. Bahati nzuri wakati unamtoleataarifa kengele ilimekwishagongwa. Kwa hiyo,unathibitisha kwamba hawa Wazanzibar, hamkuwawote, basi.117

Tunaendelea, Mheshimiwa Magdalena Sakayahalafu Mheshimiwa John Lwanji atafuatiwa naMheshimiwa Susan Kiwanga kama kutakuwa na muda.MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kuweza kunipa nafasi hiimuhimu niweze kuchangia kwa ufupi kwenye bajeti yaWaziri Mkuu.Mheshimiwa Spika, kabla ya kuchangia, naombanitoe rai kwa Serikali iliyoko madarakani, nitoe rai kwaWaheshimiwa Wabunge wenzangu, nitoe rai kwaWatanzania wote tuweze kuilinda amani tuliyonayoTanzania. Tunu hii tuliyoachiwa na Marehemu MwalimuNyerere muasisi wa Taifa hili, tumeshaanza kuona kunadalili za maneno ya viongozi, maneno ya WaheshimiwaWabunge, maneno ya wanasiasa ya kugusia suala laudini na suala la ukabila.Mheshimiwa Spika, Serikali isikae kimya tukiachamaneno haya yakiendelea kutamkwatamkwa leo,kesho tutakuwa kama Burundi au kama nchi nyingineza Syria na maeneo mengine. Kwa hiyo, tunutulioachiwa tuishike, ni almasi, ni keki, hatuwezi kuipatapengine popote. (Makofi)Mheshimiwa Spika, pili, niende kwenye pongezi.Nachukua nafasi hii kwa moyo wa dhati kumpongezaMkuu wa Mkoa wa Tabora tuliyepewa, Mama FatumaMwassa. Kwa kweli tumepewa Mkuu wa Mkoamwenye dhamira ya dhati, mama mchapakazi, mamamwenye nia ya kusaidia maendeleo ya Mkoa wa118

Tabora. Naiomba Serikali im-support, wananchi wotewa Mkoa wa Tabora na viongozi tum-support kwamoyo wa dhati aweze kubadili maisha ya wananchiwa Mkoa wa Tabora.Mheshimiwa Spika, niende kwenye mchangowangu, nianze na suala la afya. Mkoa wa Taboraumekuwa na huduma duni za afya kwa miaka yote.Mwaka 2011 wakati nachangia bajeti kwa miakayangu yote saba sasa, kila mwaka nachangia suala laafya, na Serikali ilikuwa inatoa matumaini, lakini hakunakinachofanyika. Mwaka 2011 wakati nachangia Bungela Bajeti, Serikali ilisema kwamba kuna mpangokabambe kwa sababu walitoa taarifa hapa Bungenikwamba Mkoa wa Tabora ni wa pili kwa huduma duniTanzania za kiafya. Wakasema kuna mpangokabambe kwa kushirikiana na Benki ya Afrika kusaidiakuboresha huduma za afya Mkoa wa Tabora,wakianzia na hospitali kuu ya Kitete kuboreshamiundombinu, kuweka mazingira vizuri, hospitali zakinamama za kujifungulia na mambo mengine nakwenda kwenye hospitali zote. Kwa mwaka mzimasasa hakuna juhudi ambazo tumeziona kuwezakusaidia huduma za afya Mkoa wa Tabora.Mheshimiwa Spika, wananchi wa Mkoa waTabora, Wilaya karibu zote wamejenga dispensary kwanguvu zao miaka mingi. Dispensary zile zimekuwazinadondoka, zimeliwa na mchwa, hazipelekewihuduma, hawapeleki Watendaji, hakuna Waganga,mpaka leo bado hospitali kuanzia akiwa MheshimiwaProfesa Mwakyusa amekuja Dkt. Mponda, aliyetoka119

sasa hivi, tunaomba suala la afya Mkoa wa Taboraliangaliwe.Mheshimiwa Spika, sasa hivi tunashukuru kwambaSerikali imetupatia Wilaya mpya ya Kaliua. Nisemekwamba wananchi wa Wilaya ya Kaliua wamefurahina wanaishukuru sana Serikali na wanaomba Wilayampya ya Kaliua ibaki ndani ya Mkoa wa Tabora kwalengo la kusaidia huduma ziweze kuwa jirani na Mkoawa Tabora. Pia Wilaya hii mpya tayari tumeshapatahospitali iliyokuwa imeshajengwa, hospitali ndogo,lakini hospitali hii ina nyumba mbili za Madaktari nampaka sasa hivi haijafunguliwa, na hatuna mhudumuyeyote. Kwa hiyo, tunaomba Serikali itusaidie kwasababu sasa hivi ni Wilaya, tuletewe Madaktari hospitaliile ifunguliwe ili tuanze na speed mpya ya kuendelezaWilaya yetu mpya ya Kaliua.Mheshimiwa Spika, zipo hospitali ambazo Serikaliinasema kila siku hapa kwamba huduma za akinamama wajawazito ni bure kwa maeneo yote. Lakinikwa Wilaya ya Urambo bado zipo dispensary ambazozinawatoza akina mama fedha wanapojifungua.Mfano halisi dispensary ya Igagala, Tarafa ya Kaliua,mama akishajifungua kama hajatoa Sh. 6,000/= hatokipale hata siku mbili tatu haondoki. Lakini Serikali kila sikuBungeni inatangaza kwamba huduma ni bure. Kwahiyo, tunaomba Serikali isimamie maamuzi yake namatamko yake. Kama huduma kwa akina mama nibure zitolewe bure kwa watoto ni bure na wazee nibure zitolewe bure. Maagizo ambayo hayafuatiliwi naWatendaji hayaleti tija kwa Watanzania.120

Mheshimiwa Spika, niende kwenye suala la majikwenye mkoa wangu wa Tabora. Naishukuru Serikalikwamba ina mpango kabambe wa kuleta maji kutokaKahama. Lakini maji yale kama mradi uleutatekelezwa utazinufaisha Wilaya tatu tu ambayo niNzega, Igunga na Manispaa, bado Wilaya nyingineparticularly Urambo kuna tatizo kubwa la maji.Mheshimiwa Spika, mradi wa maji wa World Bankumefeli, hakuna hata Kijiji kimoja ambachokimefanikiwa kuwa na mradi wa World Bank. Kwa hiyo,tunaiomba Serikali ije na mpango mwingine, Wilayanyingine kama Urambo, Uyui na nyingine utaratibugani umeandaliwa kusaidia wananchi wale?Mheshimiwa Spika, kwa Wilaya ya Uramboambapo walipata maji kwa vijiji vitatu, wananchiwanayaangalia mpaka leo tangu mwaka janamwanzoni. Maji yamepatikana, wameziba kile kisima,hayajasambazwa, wananchi wanayaangalia,tunaambiwa kesi iko Mahakamani. Naiuliza Serikali,inakuwaje wananchi wanateseka kupata maji ambayoyameletwa mpaka wanayaona kwa macho yao kwakesi ambayo iko Mahakamani? Sasa imekuwa kama nitabia, inapotokea tatizo mtu anakimbilia Mahakamani,lakini wanaopata shida ni wananchi wa Urambo. Kwahiyo, naiomba Serikali iliingilie kati, visima ambavyo majiyamepatikana, yasambazwe wananchi wapate majina yale maeneo mengine ambayo hawajachimbawaende. Kwa sababu pesa ilishatolewa, lakini tatizo niufuatiliaji, wananchi wa Urambo wanapata shida sana,akina mama wanateseka kwa shida ya maji. (Makofi)121

Mheshimiwa Spika, niende kwenye suala la ardhi.Mkoa wetu wa Tabora ulikuwa unasifika kuwa na misitumingi, lakini kwa bahati mbaya misitu yote almostimeshavamiwa, yote imekwisha. Kila mahalikumeshakuwa nyang’anyang’a. Kwa sasa hivi kwamaeneo mengi kila wananchi wanapokaawanaambiwa wako hifadhini. Lakini ukifuatiliawananchi wamekaa kule kuanzia mwaka 1972 kablaya operesheni vijiji leo wanaambiwa wako hifadhini.Unataka kusema Serikali ilikuwa wapi? Mpaka sasa hivitunapiga kelele, hakuna hatua zinazochukuliwa na hivininavyoongea jana nimepigiwa simu kuna maeneo yavijiji vitatu kilometa 60, Kangeme na Uyumbuwameambiwa wako hifadhini na wamekaa pale tangumwaka 1972 mpaka leo, wamejenga kila kitu,dispensary zipo, nyumba zipo, wanaambiwa zikohifadhini. Sasa tatizo la Serikali kuona misitu inaingiliwawakanyamaza kimya halafu baada ya miaka 30wanasema wananchi wako hifadhini, hatupigi hatua,na haya siyo maendeleo. Naomba juhudi za dhati.Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Tabora ziko tumenyingi zimetumwa na zimefanya utafiti wa maeneo yahifadhi na wamegundua tatizo liko wapi. Maeneohayajaainishwa, matatizo yapo, mgongano upomkubwa, Serikali haifanyii kazi taarifa zile. Kwa hiyo,matatizo yanaendelea kuwepo, matokeo yakewananchi wapo mguu ndani, mguu nje, hawawezikufanya shughuli za maendeleo kwa sababu hawajuiwanastahili kuwepo pale au hawastahili.Mheshimiwa Spika, niende kwenye vyama vyamsingi. Vyama vyetu vya msingi vimeundwa kwa nia122

ya kuwasaidia wakulima na kusaidia kuinua kilimo. Kwabahati mbaya sana kwa Mkoa wa Tabora naparticularly Wilaya ya Urambo, vyama vingi vya msingivinaingiliwa na Madiwani. Madiwani wenginewamekuwa ni Makatibu na Meneja wa Vyama vyamsingi. Matokeo yake wanaingilia hata utendaji kaziwa Maafisa Ushirika, wanakosa nguvu. Kwa hiyo, vingivimekuwa dhaifu kwa sababu Madiwani wanaingiliautendaji kazi wa vyama vya msingi. Imefikia mahaliDiwani akiona kwamba aliyeko pale kwenye Chamacha msingi hamnufaishi yeye binafsi, anamtoa,anamweka mtu ambaye ni weak ili aweze kunufaikana kile Chama cha msingi. Kwa hiyo, matokeo yakevyama vimekuwa dhaifu vimekuwa na migogoro nahasa vile vinavyoendeshwa na Madiwani kama niMakatibu Meneja. Naomba sasa Mheshimiwa WaziriMkuu atoe agizo na mwongozo kwenye vyama vyamsingi, Madiwani wote wasiwe Makatibu Meneja.Wawaachie wakulima wachague mtu wao ambayewanajua ataweza kuendesha Chama chao kwa nia yakunusuru vyama hivi na viweze kuwa na tija kwasababu ndiyo nia ya msingi ya kuvianzisha. (Makofi)Mheshimiwa Spika, niende kwenye elimu. Suala laelimu imekuwa inashuka siku baada ya siku nchinikwetu na bado juhudi ambazo zinachukuliwa sionikama zinaleta tija kwa sababu kitendo cha kuwa nawanafunzi 5000 wasiojua kusoma na kuandika ndani yamwaka mmoja kwenye Taifa, ni aibu. Lakini pia lipotatizo la Walimu wapya kutokupewa mishahara yaokwa wakati, inakatisha tamaa. Kwa hiyo, nadhanitatizo la msingi ni maslahi na mahitaji ya Walimu. Hebutuwasaidie Walimu tuone wafanye kazi yao kwa moyo123

na dhati na tuone kama elimu haitainuka ndani yanchi yetu.Mheshimiwa Spika, kwa haraka haraka lipo sualala Wakurugenzi. Sasa umefika wakati tuwe naWakurugenzi wa Halmashauri ambao wanapatikanakwa njia ya usaili, wafanyiwe mitihani, tupate watumakini wanaofanya kazi vizuri na wanaoweza kuletamaendeleo kwa ajili ya Halmashauri zetu.Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)SPIKA: Ahsante. Sasa nimwite Mheshimiwa PaulLwanji, nafikiri Mheshimiwa Susan atapata nafasi jioni.MHE. PAUL J. LWANJI: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa nafasi. Mimi ni Mjumbe wa Kamati yaKatiba, Sheria na Utawala na pia ni MakamuMwenyekiti wa Kamati hiyo.Mheshimiwa Spika, mimi niliunga mkono hoja hiitoka kwenye Kamati, kwa hiyo, sina ugomvi kwasababu wenzetu itabidi tuwape muda. Tukumbuke hivikaribuni Mheshimiwa Rais alilisuka Baraza lake laMawaziri akateua Wakuu wa Mkoa, basi tuwape mudatuone hiki kipya walichokileta kama kinawezakutukwamua.Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hiikumpongeza sana Mheshimiwa William Mgimwa, Waziriwetu mpya wa Fedha kwa juhudi alizozionyesha naumahiri mkubwa aliouonyesha katika ku-present. Kwa124

hiyo, sina shaka kwamba tukiwapa muda huendawakatuletea matunda.Mheshimiwa Spika, siyo kwamba Serikalihaijafanya kitu kwa siku zote hizi, imefanya. Jimbonikwangu mengi yamefanywa, barabara zinajengwa,umeme unapelekwa na mambo mengi menginekadha wa kadha. Lakini tunachogomba hapa nikwamba tumechelewa katika kupiga hatua kwenyemasuala ya maendeleo, tumechelewa. Wakatitunapata uhuru, tulikuwa na matumaini makubwakwamba tungesonga mbele haraka zaidi pamoja namatatizo yaliyokwisha kutokea. Lakini wenzetuBotswana walipopata uhuru mwaka 1968 miaka sababaada ya sisi kupata uhuru, GDP per capita incomeyao ilikuwa Dola 70. Lakini leo hii 2012 per capitaincome yao ni Dola 14,000 ambazo ni sawa na Shilingimilioni 21. Sasa leo hii per capita income yetu ni Dola1,400. Sasa unaweza kuona.SPIKA: Wapo wangapi Botswana?MHE. PAUL J. LWANJI: Mheshimiwa Spika, watu niwachache kuliko sisi.SPIKA: Milioni moja na laki nane.MHE. PAUL J. LWANJI: Mheshimiwa Spika,tunaelewa hilo, lakini ninachozungumzia hapa ni jinsitunavyoweza kuzitumia vizuri rasilimali zetu. Ziko nchindogo, zina rasilimali za kutosha, lakini zimeshindwakutumia vizuri rasilimali zao. Kwa hiyo, mimi ndipo haponinapogomba kwamba hatujatumia vizuri rasilimali125

zetu. Pamoja na kwamba tunazo rasilimali za kutosha,lakini tungezitumia vizuri tungeweza kupiga hatuakama wenzetu wa Botswana, ambayo sasa hivi ni nchiya uchumi wa kati kama ilivyo Uturuki, Mexico na nchinyingine. Sasa hilo ndiyo wasiwasi wangu mkubwaambao unanipa tatizo kwenye eneo hili la kupigahatua za maendeleo.Mheshimiwa Spika, Itigi tumegundua uranium natumeambiwa hapa mara mbili, tatu na wataalam,kwamba maeneo hayo ya Wilaya ya Manyoni uraniumimepatikana. Sasa naomba sana tuandae vizuri watu.Wilaya ya Manyoni ni kubwa, tumekuwa tukiombasana kwamba tupewa kipaumbele kuigawa Wilaya hiiili Serikali iwe karibu zaidi ku-honest resources zake kwaajili ya maendeleo ya wananchi, lakini imekuwa ngumuna sababu zimetolewa nyingi.Mheshimiwa Spika, Mwenyezi Mungu ametujalia,ameshusha uranium na unaifahamu, ni madini muhimukatika kurutubisha silaha za nyuklia, na inasemekenakwamba sasa hivi kama itabainika kwamba watawezawakayachimba, tutasafirisha nje uranium ghafi. Sasakatika utaratibu ni kwamba ni yellow cake. Sasa hiinadhani itatusaidia sana katika kukuza uchumi wa nchihii. Lakini naomba Serikali, maeneo kama hayoambayo yana resources kama hizo, basi yapewekipaumbele katika kugawa keki ya Taifa hili vizuri.Mheshimiwa Spika, mpango wa D by D, sisi badotuna wasiwasi kwa sababu nchi hii imefanya majaribiomengi katika utaratibu huu wa D by D. Hii nadhaniitakuwa kwenye utaratibu wa D by D, itakuwa ni126

mpango wa nne kama sikosei ama wa tatu tangutumepata uhuru. Tulivunja hizi Halmashauri baada yakuzivunja, tukaja na utaratibu wa decentralization,madaraka Mikoani. Lakini utaratibu huu ukashindikana.Huu utaratibu wa D by D una maana kwamba,tunachukua pesa nyingi tunazipeleka kwenyeHalmashauri zetu. Lakini namna ya kuzisimamia hizifedha limekuwa tatizo kubwa. Wizi mkubwa ndiyoumekithiri na dada yangu mmoja hapa juzi,Mheshimiwa Lulida alitoa orodha ndefu ya watuwanaohujumu kwa makusudi na Serikali imekaa paleinawaangalia badala ya kuwachukulia hatuamadhubuti, wamekuwa wakihamishwa.Mheshimiwa Spika, hili lilinifanya mpaka niombemwongozo hapa kwa Mheshimiwa Waziri wa Nchi,nilidhani kwamba ametoa kauli yule ambaye ilimuudhiyule ambaye alitoa hiyo hoja, lakini hiyo ilikuwa ni jazbailiyonipata mimi, kwamba, kama wametajwa nawanafahamika, basi waanikwe badala ya kuhamishwamara kituo hiki, au kituo hiki. Haiwezekani!Mheshimiwa Spika, niliona kuna umuhimu wa haowatu, tatizo letu siyo mipango, hata katika Jumuiya yaAfrika Mashariki sasa hivi wanasema sisi Tanzania nimabingwa wa ku-drop ideas, halafu watu wa Kenyawana-plan, halafu watu wa Uganda waowanatengeneza action plan halafu wanawaachiaWanyarwanda wana-implement. Hapo ndipo tatizo,lakini tatizo letu tuna mipango mizuri na mikakati mizuri,lakini wizi na uhujumu umezidi. Sasa naomba, kamamhalifu anafungwa, atajwe na jina na eneo analotokana kabila, basi. Kwanini iwe aibu kutaja mtu127

anayehusika na kabila lake na eneo analotoka ilituweze kujua hawa watu wanaotuhujumu kiasi hikitufanye nini? Tuwaweke kwenye hizi nafasi au tujuekwamba sasa hii nchi maana yake tatizolinazungumzwa, umoja wa kitaifa; umoja wa kitaifaambao unaleta imbalance, katika hali hii, hatuwezikuuvumilia.Mheshimiwa Spika, naomba eneo hili lizingatiwe,vinginevyo tutaibiwa na mipango yetu haiwezikwenda. Nasema kwamba ikiwezekana kama kunaeneo lenye miradi mingi kwa mfano eneo fulani, hizi nirumours lakini huenda ikawa ni kweli, kwamba mtuanahamishwa kwa makusudi kwenda kusubiri pesa zahuo mradi, akishaiba basi anahamishwa anakwendasehemu nyingine. Hii hali ni ya kusikitisha.Mheshimiwa Spika, alikuwepo adui ujinga,umaskini na maradhi, tumeshindwa kuwatokomeza,wote na wameungana hawa watu na wana KamatiMaalum na wame-incorporate, wamezaa maaduiwengine, wizi, ubadhirifu na ufisadi. Sasa hatuwezikatika hali hii, hawa watu wamekuwa sugu! (Makofi)Mheshimiwa Spika, mimi niungana na kaka yanguMheshimiwa Missanga kwenye suala la maafa. Singidasafari hii tumelima sana mtama, lakini mtama huumwingi umeliwa na ndege. Tuliahidiwa kwambakutakuwa na ndege maalum ya kuweza kunyunyiziakuwaua hawa ndege, lakini imeshindakana. Safari hiimtama mwingi na mazao haya ya ukameyamepunguzwa kwa kiasi kikubwa na ndege hawa wakweleakwelia. Sasa tunaiomba Serikali pia kwamba128

ingalie uwezekano wa kuwa na ndege yake badala yakutegemea ndege kutoka sehemu nyingine.Mheshimiwa Spika, suala la njaa linafahamikasana na tumelizungumza sana kwenye Kamati. Hilisuala siyo la mchezo na Serikali inaonekana katikaeneo hili haijajipanga vizuri. Mimi sijaridhika nautaratibu wa kupeleka chakula katika maeneoambayo yanakumbwa na janga hili la njaa. Watuwanaingia kwenye utaratibu wa tender, hizi ofisi zaHalmashauri wakishaingia hizo tender inachukua hizotender na hakuna kitu kingine, maana ni ya kupatawatu wa kuja kuchukua chakula kama ni Dodoma ilikuweza kupeleka maeneo husika.(Hapa kengele ililia kushiria muda wa Mzungumzajikwisha)SPIKA: Basi, ahsante. Kengele ya pili.MHE. PAUL J. LWANJI: Mheshimiwa Spika, ahsante.SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nina matangazomachache. Asubuhi niliwataja Madiwani 35 kutokaKata zote za Jimbo la Handeni wakiongozwa naMwenyekiti wa Halmashauri ya Handani, MheshimiwaRamadhani Diriwa. Waheshimiwa Madiwani karibunisana. (Makofi)Wakati mwingine tunakuwa na wageni wengikatika ukumbi wetu, basi nafasi yetu inakuwa haitoshi,lakini karibuni sana nadhani mtajifunza mengi.129

Halafu nina tangazo lingine. Katibu wa Kamati waWabunge wote wa CCM, Mheshimiwa JenistaMhagama anaomba niwatangazie WaheshimiwaWabunge wote wa CCM kuwa leo saa 7.00 mchanahuu kutakuwa na kikao kitakachofanyika katika Ukumbiwa Pius Msekwa. Wote mnaombwa kuhudhuria.Asubuhi nilisema ukumbi ule ulikuwa unatumika nawatu wengine, nadhani wataelewana wenyewe hukohuko.Tangazo lingine, Wabunge ambao hawajajazaFomu za Vitambulisho vya Taifa wazijaze fomu hizo kwaMaafisa wa NIDA waliopo pale mapokezi kwenyejengo letu la Utawala. Tarehe ya mwisho kwa Maafisahao ni kesho tarehe 29 Juni, 2012. Hivyo ili kuepekausumbufu wa kuwafuata Maafisa hao NIDA, ni vyemaWabunge mkatumia nafasi mliyonayo. Kama kunawatu ambao wamejisahau, maana kuna wenginewanaweza kusema labda kesho, labda kesho. Keshondiyo deadline.Waheshimiwa Wabunge, kwa sababu ya wingi wawachangiaji kwa kweli asiyekuwepo na lake halipo. Niwale tu ambao wametoa taarifa, basi wale wataingia.Kwa sababu wachangiaji ni wengi, asiyekuwepo nalake halipo. Mimi nitaendelea na orodha nyingine.Waheshimiwa Wabunge, sina tangazo lingine.Naomba nisitishe shughuli hizi mpaka saa 11.00 jioni.(Saa 6.58 mchana Bunge lilisitishwa mpaka saa 11.00jioni)130

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tulipokuwatunaondoka nilikuwa nimemwita Mheshimiwa SusanKiwanga, atafuatiwa na Mheshimiwa Joyce Mukya,atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. David Mallole naatafuatia Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed.MHE. SUSAN L.A.KIWANGA: Mheshimiwa Spika,naenda moja kwa moja katika kuchangia hoja iliyokombele yetu ambayo ni Hotuba ya Waziri Mkuu.Mheshimiwa Spika, mimi natokea Mkoa waMorogoro na ni vizuri nikachangia kwa kujikita ndani yaMkoa ambao ninaufahamu, niliozaliwa, niliokulia naninaendelea kuishi. Mkoa wa Morogoro ni Mkoa uliomkubwa kuliko Mikoa yote hapa Tanzania ambapouna eneo la kilometa za mraba sabini na tatu elfu nathelathini na tisa lakini vilevile ni asilimia 8.2 ya nchiyetu. Kwa hiyo, ukiangalia Mkoa wa Morogoro, ni Mkoaambao ni mkubwa sana na unategemea kwambabajeti zake zitalingana na Mkoa wenyewe jinsi ulivyo.Mheshimiwa Spika, lakini Mkoa wa Morogoro niMkoa wa wakulima na wafugaji, vilevile kunawafanyabiashara na Mkoa wa Morogoro ni Mkoa waviwanda hapo zamani lakini sasa hivi ni marehemu.Mkoa wa Morogoro Rais wa Tanzania, MheshimiwaJakaya Mrisho Kikwete mwaka 2006 alitangaza kuleBagamoyo kwamba ni Mkoa ambao ameuitakwamba ni Ghala la Chakula na Mkoa huohuo kwatamko la Kunduchi kuhusu Kilimo Kwanza umepewa131

kwa maneno kipaumbele ambapo tutaendesha KilimoKwanza, ukiangalia Mkoa wenyewe barabara zake nimatatizo.Mheshimiwa Spika, lakini pia ukiangalia Mkoawenyewe na inasemekana kwamba ni Kilimo Kwanza,hela zinazopangwa katika hicho Kilimo Kwanza nivichekesho. Mwaka jana katika bajeti ya mwaka2010/2011 tuliahidiwa kwamba kwa mfano Bonde laKilombero litaanza uzalishaji mkubwa wa chakulakatika kilimo cha mpunga na kilimo cha miwa pamojana Wami lakini cha kushangaza hela iliyotengwa eti niya kufyeka tu. Kwa hiyo, mpaka sasa hata hiyo miradikatika mpango mzima wa kuzalisha chakula badoWilaya ya Kilombero au Mkoa wa Morogoro kwaujumla haujaonyesha picha halisi, haujaonyesha faidana haujaonyesha matokeo kwamba hili kweli ni Ghalala Chakula.Mheshimiwa Spika, ukiangalia katika majedwalituliyopewa, Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilomberoeti umepewa matrekta mawili makubwa (power tiller),hata moja hakuna jamani hicho ndicho KilimoKwanza? Hilo ndilo Ghala la Chakula? Hatuoni kamatunasema kwa maneno tu lakini kwa vitendohatutekelezi? Ndiyo maana mfumuko wa bei umekuwamkubwa ndani ya nchi yetu lakini Wilaya hiyohiyo yaKilombero ndani ya Mkoa wa Morogoro kuna kilimokikubwa sana cha mpunga. Katika Kata ya Mgetaambapo wanasema KPTL (Kilombero Planting TanzaniaLimited) ambapo inafanya kazi kubwa sana ya kulima,lakini katika Hotuba ya Waziri Mkuu inaonyesha katikaukurasa wa kumi na tisa, inasema kwamba hilo eneo132

wakulima wadogo wanafaidika, uzalishajiunaongezeka, wanapewa pembejeo lakini hali halisikatika Tarafa ya Mgeta yenye Kata tatu Chita, Mgetana Mchombe hali halisi iliyoko pale kweli mwekezajiyupo na anazalisha kiasi cha kutosha, ametoa elimukweli kwa vikundi mbalimbali katika hizo Kata lakini halihalisi mpaka sasa wakulima wanaambiwa mfukommoja wa mbolea ni shilingi laki moja na wakulimahawana uwezo wa kununua mbolea hiyo, matrektahamna. Kwa hiyo, wakulima wadogo wanaozungukaule mradi hawafaidiki, hali ni mbaya, vikundi vimepewaelimu kwani elimu ndiyo kulima? Zinatakiwa zana lakiniukiangalia hali halisi ya mgao wa mbolea katika nchiyetu, mwaka jana Mikoa mingi imelalamika mboleahazifiki kwa wakati, ile yenye ruzuku ya Serikali, kwahiyo, wakulima wanashindwa kulima. Kweli ardhi ni nzurilakini hakuna faida yoyote kwa wananchi wa kawaidakatika kukaa Mgeta, katika zile Kata elimu wamepewalakini uzalishaji haupo.Mheshimiwa Spika, hiyo haitoshi, angalia barabaraya kutoka Ifakara mpaka Mgeta, ni mashimo matupu,barabara ya vumbi siyo ya changarawe. Chakusikitisha katika Bunge hili, tarehe 11/7/2011, miminilimuuliza Waziri wa Ujenzi wa wakati huo kwambabarabara ya Kidatu- Ifakara na Ifakara - Mrimbampaka Madeke mpakani mwa Njombe itatengenezwalini kwa kiwango cha lami? Nikajibiwa vizuri kuwakilometa kumi na saba zimeshajengwa kiwango lamina hizo zilizobaki zitawekwa kwa kiwango kwachangarawe lakini mpaka leo ninavyozungumzahamna changarawe wala mawemawe, kuna vumbitupu wakati wa mvua zile barabara hazipitiki.133

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Tarafa ya Mgetayenye Kata tatu wanalima, umeme hakuna, yulemwekezaji pale ana umeme anashindwa kuwasaidiawale wanaomzunguka kupata umeme. Kwa hiyo,hakuna mashine za kukobolea mpunga matokeo yakewakulima wanalima ila wakitaka kupeleka mpungawao sokoni inabidi wakodi fuso kutoka Mgeta mpakaIfakara kwa shilingi laki tano wakati ni kilometathemanini tu lakini mfanyabiashata akitoka Ifakarampaka Dar es Salaam kwa fuso ambapo ni kilometamia tano ni shilingi laki tano hiyohiyo. Kwa hiyo, hatuonikuwa wananchi wa Wilaya ya Kilombero wanatesekasana, hawana faida na mpango mzima wa KilimoKwanza. Wananchi hawa hawawezi kuondoka katikaumaskini kama barabara hakuna. Ni muhimutunaposema kwa maneno tutekeleze kwa vitendo.Mwaka huu ningependa bajeti ionyeshe kwamba kweliSerikali ina nia ya kuboresha kilimo katika Bonde laKilombero la sivyo tutakuwa tunaandika manenovitabuni lakini hali halisi hakuna.Mheshimiwa Spika, vilevile kwenye huu ukurasa,sasa matokeo yake ni nini wanaposafirisha ule mpungakwenda kukoboa mashine za Ifakara, ushuru wa Kijijiwanalipa shilingi elfu moja na mia tano, gunia mojawanagharamia shilingi elfu kumi na Halmashauriwanawa–charge shilingi elfu tatu. Mkulima anakuwachargedkwenye geti la Idete, ndiyo maana geti laIdete ni maumivu sana kwa wakulima wa Wilaya yaKilombero hususani katika Tarafa ya Mgeta, jamani nikilio. Kuna Sheria ya mwaka 2002, Sheria Na.230, tamkolililotolewa na Brigedia Ngwilizi aliyekuwa Waziri wa134

Serikali za Mitaa kwamba ushuru wa mazao umefutwalakini leo mkulima anateseka kwa kulipia ushuru na siyomfanyabiashara, anazalisha mpunga mwingi, mashinehakuna, umeme hakuna, anapeleka Ifakara, anakuwacharged kwenye geti la Idete, hiki ni kilio kikubwa.Naomba Waziri aje na majibu atawasaidia vipiwananchi wa Kilombero katika ushuru ambaounawatesa kila kukicha, atoe ufafanuzi ni kwa niniSheria zinakiukwa?Mheshimiwa Spika, ukurasa huohuo wa kumi natisa kuhusu wananchi wa Kilombero sukari wanafaidika,ametuambia wanafaidika. Mheshimiwa Waziri Mkuuhawafaidiki hata leo na jana wakulimawadogowadogo mashamba yao yameungua kwabahati mbaya kwa uchomaji wa moto na yule wakiwandani hataki kuvuna miwa yao na miwa hiyoikikaa wiki moja inaharibika, wanapata hasara na hizihasara miaka yote wanazipata. Kibaya zaidi, kulekiwandani wanakoenda kupima miwa hakunamwakilishi yeyote yule, mwenye kiwanda ni jeuri hatakinini wala nini na haruhusu wakulima wawe namwakilishi kupima miwa yao kwamba miwainapatikana sukari kilo ngapi kwa hiyo, hiyo ni taabu.Mheshimiwa Spika, lakini Halmashauri inakosamapato, sukari ikizalishwa Kilombero inapelekwa Dar esSalaam halafu inarudi Kilombero, mtu wa Dar esSalaam ananunua bei ya chini na mtu wa Kilomberoananunua bei juu. Kwa hiyo, huyu mwananchi waKilombero anafaidika vipi na hicho killimo cha sukari?Kama tunataka kumnufaisha Mtanzania wa kawaida,ni bora tukaboresha miundombinu, tukaruhusu yule135

mwekezaji wa KPTL awaruhusu REA na REA wako tayarikupeleka umeme kwa wananchi lakini yeye ni mjeuri,umeme wenyewe ni wa maji na maji ni yetu, hivi kiburihiki anapata wapi? Hapa wananchi wa kawaidawataonaje kama uwekezaji una faida? Serikali lazimaichukue hatua. (Kicheko)Mheshimiwa Spika, kuna tatizo kubwa la wafugajikatika Wilaya ya Kilosa, mpaka leo ng’ombewameuawa Parakuyo…(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)SPIKA: Pole, muda umeisha. Sasa nitamwitaMheshimiwa Joyce Mukya, Mheshimiwa David Mallole,Mheshimiwa Profesa Kapuya na Mheshimiwa MhongaRuhwanya wajiandae.MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Spika,ninakushukuru kwa nafasi hii na pia nashukuruMwenyezi Mungu kwa kunipa pumzi na uhai mpakasasa hivi. Katika bajeti hii ya Waziri Mkuu, mimi nitajikitakatika sehemu tatu; huduma za jamii ambaponitaongelea huduma ya afya katika Wilaya yaNgorongoro, Mkoani Arusha, watumishi Wilaya yaLongido, Mkoani Arusha na msongamano wa magarikatika Mkoa wa Arusha, Wilaya ya Arusha Mjini.Mheshimiwa Spika, naomba nianze namsongamano wa magari katika Mkoa wa Arusha,Wilaya ya Arusha Mjini. Kwa wale ambao mmeshafikaArusha Mjini siku za hivi karibuni, mtakubaliana na mimi136

kabisa kuwa msongamano wa magari umekuwa nimkubwa sana na ni kero kubwa kwa wafanyakazi.Mikutano mingi ya Kitaifa inafanyika katika Mkoa ule,Arusha Mjini inajulikana kama kitovu cha utalii katikanchi hii ya Tanzania, watalii wamekuwa wakipata shidasana lakini sasa ninaiomba Serikali ichukue uamuzi wabusara kuweza kusimamia biashara nzima ya utalii kwasababu tusipofanya hivyo, tunapoteza fedha za kigenikatika biashara hii.SPIKA: Wanaomba uongee taratibu,wanashindwa kukuelewa, punguza speed.MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Spika,ninashukuru. Naomba kuingia katika huduma za jamiikuhusiana na suala zima la afya katika Wilaya yaNgorongoro, sehemu ya Loliondo. Kumekuwa na shidakubwa ya huduma ya afya katika Wilaya ya Loliondo,wananchi wanapata shida sana, kuna Kituo cha Afyakatika eneo la Loliondo ambacho ni cha zamani sanalakini kuna Hospitali ya Wilaya ambayo inamilikiwa naKanisa Katoliki, Parokia ya Arusha Mjini ambayoinapata ruzuku kutoka Serikalini kama wahudumu,vifaa vya matibabu, dawa kupitia Halmashauri yaWilaya ya Ngorongoro, wananchi wengi hutumiahospitali hiyo. Lakini kutoka katika hospitali hiyo, kunaKituo kingine cha Afya katika sehemu inayoitwaSakala. Kituo hicho kimejengwa katika miaka ya 2000,ni kikubwa sana lakini kutoka hapo kuelekea katika kijijikinachoitwa Nani, katika Kata ya Unguselusambuhakuna Kituo cha Afya kabisa, wananchi wanapatashida sana kutokea katika Kituo cha Nani ambacho nikijiji kuelekea katika Hospitali ya Wilaya ya Loliondo137

hasa wanawake wajawazito kama unavyoelewawanawake wajawazito wanatakiwa kwenda kliniki kilamwezi. Wanawake hawa hawaendi klinikiwanajifungua kwa kutumia Wakunga wa Jadi.Wajawazito hawa wanapata shida sana kwa sababuKituo cha Afya kiko mbali. Katika kijiji cha Nani mwakajana walikufa watoto kumi kutokana na ugonjwa waSurua. Watoto hawa wamekufa kwa kuwa hawapatichanjo wakati wamezaliwa kwa kuwa mama zaowanajifungua kupitia Wakunga wa Jadi. Hili ni tatizokubwa katika Wilaya ya Ngorongoro na wakazi wapale wamelalamika sana kwa sababu ni tatizo lipo kwamuda mrefu.Mheshimiwa Spika, Serikali imejenga Kituo chaAfya katika eneo la Sakala wakati ni kilomita tano tukutokea katika Hospitali ya Wilaya ya Loliondo ambayoinamilikiwa na Kanisa Katoliki. Kwa nini Serikalihaikujenga Hospitali hiyo katika kijiji cha Nani, katikaKata ya Unguselusambu ambayo ingesaidia wananchikutoka umbali wa kilomita sabini kuelekea katikahospitali hii ya Wilaya ya Loliondo, tatizo hili ni kubwasana kwa wananchi wa Loliondo.Mheshimiwa Spika, kitu kingine ni uhaba waWatumishi katika Wilaya za pembezoni, naongeleaWilaya ya Longido. Wilaya ya Longido imepataWahasibu mwaka jana mwezi Septemba na mweziOktoba, watumishi hao wamekaa chini ya miezi sitakatika kituo kile cha kazi na wameondoka katikamazingira ya kutatanisha. Mtumishi mmoja ambayeanaitwa somebody Mkonyi alitoroka na mpaka leohakuna taarifa kuwa ameelekea sehemu gani na138

mtumishi mwingine sikumbuki jina lake vizuri nawezanikaleta taarifa kwenye Meza yako, aliomba kuhamiaMkoa wa Tanga kupitia Katibu Tawala Mkoa wa Arushalakini baada ya Mkuu wa Mkoa kuelekea katikaHalmashauri ya Longido alipewa malalamiko haya nawakazi wa Halmashauri ya Longido na akamwombaRAS ambaye ni Mama Itanisa ampe maelezo kamili.Mama Itanisa akamwambia kuwa maelezo kamili nikuwa yeye hajatoa uhamisho wowote kwa mtumishihuyo lakini mtumishi huyu alimwomba ruhusa kuelekeaMkoa wa Tanga na yeye akakataa lakini mtumishi huyuakapitia wafanyakazi wake wengine kwa njia yamlango wa nyuma na akapata ruhusa hii na mtuambaye amempa ruhusa hii anaitwa somebody Nkyaambaye ndiye ali- sign barua hii.Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziriatakapokuja kujibu hoja hizi atuambie Mheshimiwahuyu Nkya amechukuliwa hatua gani mpaka sasa hivikwa sababu tukio hili ni la muda mrefu kidogo.Atuambie watumishi hawa kama bado wanapokeamishahara yao mpaka sasa na atuambie watumishihawa wako wapi. Kwa sababu walipangiwa kazi katikaHalmashauri ya Longido na Halmashauri ya Longidohaina watumishi wa kutosha, Wahasibu, kwa sababuwatumishi hawa wanakwepa kukaa vijijini na wakatiwatu wengine wanakaa vijijini kwani wao ni akina nanina kwa nini wasikae vijijini. Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali amekuwa akitoa taarifa kila mwaka kuwamabilioni ya pesa yanatumika kuwalipa watumishihewa, watumishi ambao hawakai katika maeneo yaoya kazi, watumishi waliofariki, watumishi hawawamekuwa wakichukua mishahara hii aidha139

wanachukua au hawachukui lakini mishahara hiiinaenda wapi? Naomba Mheshimiwa Waziri Mkuuatakapokuwa anajibu hoja hizi aweze kusema suala hililimefikia wapi mpaka sasa hivi, ninashukuru. (Makofi)SPIKA: Hata mimi nilipokuwa ninaanza, nilikuwanina speed ya kuongea. Sasa nimwite Mheshimiwa Dkt.David Mallole atafuatiwa na Mheshimiwa ProfessorKapuya na pia atafuatiwa na Mheshimiwa MhongaRuhwanya.MHE. DKT. DAVID M. MALOLE: Mheshimiwa Spika,ninashukuru sana kwa kunipatia nafasi hii ili na miminiweze kuchangia katika hoja ya Mheshimiwa WaziriMkuu.Mheshimiwa Spika, suala la kwanza kabisa,naomba nizungumzie kuhusu kilimo cha zabibu.Tunashukuru sana kwamba mazao mengi yametiliwaumuhimu kama vile pamba, kahawa, chai na menginemengi lakini kwa bahati mbaya, zao la zabibuhalikuweza kuzungumziwa vya kutosha katika hoja yaMheshimiwa Waziri Mkuu. Mimi napenda nitumie nafasihii kumwomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu ajaribukuliangalia suala hilo kwa karibu kwamba wananchiwetu siku za nyuma walijitahidi sana kulima zabibu nawalipata moyo wa kuendelea kulima zabibu baada yakuwa na kiwanda cha DOWICO ambacho bahatimbaya baada ya muda kilifungwa. Kipindi kile wakatikiwanda cha DOWICO kipo, maisha ya wananchi waDodoma yalibadilika sana. Kwanza watu walipata ajiralakini katika kuuza zile zabibu, watu walijikwamua naumaskini kwa kiwango kikubwa sana. Baada ya kile140

kiwanda kufungwa, kilimo cha zabibu kikashuka.Tunashukuru kwa sasa hivi kwa kuwa kuna kiwandacha CETAWICO kule Hombolo. Tunamshukuru BwanaKato pia na yeye ameanzisha kiwanda cha kununuazabibu lakini pia tunashukuru hata viwanda vilivyokokule Bihawana pamoja na Miyuji.Mheshimiwa Spika, viwanda hivi ni vidogovidogo,watu wamehamasika kulima sana zabibu lakini mwishowa yote zabibu yao yote inakuwa haiwezi kununuliwa.Watu wanayumba hapa Mjini Dodoma kuuza zabibuzao kidogokidogo lakini hatimaye hawawezi kunufaikahata kidogo na sielewi zile ambazo wanashindwakuuza wanazipeleka wapi. Tunaomba sana katikabajeti yako ujaribu kuliangalia hili kwa karibu, suala lakilimo cha zabibu na aidha kufufua kiwanda chaDOWICO na pengine labda kuanzisha viwanda vinginevidogovidogo hasa kwenye maeneo ambako zabibuzinalimwa sana kama vile Mbabala, Mpunguzi,Makutopora na maeneo mengine mengi katika mji waDodoma. Hali hii itasaidia kupunguza tatizo la ajiralakini pia watu wetu watauza zabibu zao nawanaweza kupata nafasi kubwa sana ya kuwezakujikwamua kiuchumi.Mheshimiwa Spika, la pili, naomba nizungumziehabari ya matrekta. Tunashukuru sana MheshimiwaWaziri kwa kupunguza bei ya matrekta kutoka shilingimilioni ishirini na tano mpaka shilingi milioni kumi na sitakwa yale yenye horsepower hamsini na kutoka kwenyeshilingi milioni arobaini na tano kwenda kwenye shilingimilioni thelathini na nane point nane kwa yale yenyehorsepower sabini. Hata hivyo, bei ya matrekta haya141

ado ni kubwa sana. Ni vigumu sana kuweza kupatawananchi ambao wanaweza kununua matrekta hayakwa bei hiyo.Mheshimiwa Spika, mimi binafsi ninazo Kata 37 navijiji visivyopungua pia 39, katika Vijiji vile 39 hata kamatungesema tufanye uchambuzi sijui tutapata watuwangapi watakaokuwa na uwezo wa kununua hatalile trekta lenye horsepower hamsini, labda katika vijijivyote 39 wanaweza wakapatikana watu wawili auwatatu. Matrekta yatabaki, halafu hata mapinduzi yakilimo tunayoyazungumzia itakuwa ni vigumu sanakuyafikia. Naiomba sana Ofisi ya Waziri Mkuu na WaziriMkuu yupo hapa anatusikiliza, ajaribu kuangalia jinsimatrekta haya yatakavyoweza kupelekwa kwawananchi ili waweze kuyatumia na kuleta mapinduziya kilimo katika nchi yetu.Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Dodomatunalima sana uwele, kampuni ya Tanzania Breweriesinahitaji sana mtama. Nashauri kwa upande waDodoma, matrekta hayo yangepelekwa kila kijiji yalimehalafu baada ya kutoka hapo wananchiwatakapokuwa wamevuna chakula chao, kila ekarimoja mtu achangie debe moja, kama ana ekari mbili,madebe mawili na kama ni ekari tano madebematano kutegemeana na ukubwa wa shamba lake.Ninaimani kabisa kwamba mtama huo Serikaliitawauzia kampuni ya Tanzania Breweries, mtapatapesa na baada ya misimu miwili, mitatu, ninaimanikabisa kwamba deni lenu lote la shilingi milioni kumi nasita litakuwa limekwishalipwa. Hiyo itasaidia sana kuletamapinduzi ya kilimo katika maeneo yetu.142

Mheshimiwa Spika, suala la tatu nakwendakwenye mabwawa. Dodoma ni eneo kame, hii hatunahaja ya kuijadili sana. Mwaka jana kwa mfanoDodoma imepata mvua kwa muda wa siku 14 tu.Tunaomba sana na kwa sababu mji unakua, VyuoVikuu vingi, UDOM, Chuo Kikuu cha St. Johns hataChuo cha Madini, Chuo cha Mipango tayariwameshaanza kutoa Digrii na Chuo cha CBE na ziposhule nyingi sana za Sekondari za mabweni ambazozinahitaji mbogamboga. Tunayo mabwawa 20 kwenyeJimbo la Dodoma Mjini, kama yote yaleyangechimbuliwa vizuri, baadaye mvua zinapokujazikajaza maji, itaimarisha kilimo cha mbogambogakama nyanya, mchicha, kabichi na mbogambogazingine ambazo hatimaye zinaweza zikauzwa katikavyuo vyetu mbalimbali na Mji wa Dodoma ambaounaendelea kukua kwa kasi. Nashukuru kwambamlishatenga pesa kipindi kilichopita katika mabwawafulani kama vile Vikonje, ambako mlipeleka kamashilingi milioni 400 lakini bado kuna milioni 200, mpakadakika hii bwawa lile halijaanza kutengenezwa.Mabwawa ya Makutupora, tumeambiwa kwambatayari yataanza kutengenezwa, Mbalawala namaeneo mengine lakini mpaka dakika hii kazi hiyohaijaanza. Naomba mabwawa haya 21, hebumyafanyie kazi kutokana na hali ya ukame wa mji wetuwa Dodoma na moja kwa moja hata maeneo yaleambayo mliyokuwa mmeahidi kwamba mtapelekapesa muanze kupeleka. Baada ya hapa, mimi nilikuwanatarajia nianze ziara nyingine mpya, nitakapokuwanimefika kwenye mabwawa hayo sijui nitajibu niniwakati niliwaambia kwamba hayo mabwawa143

yanapanuliwa lakini mpaka leo hakuna kazi yoyoteambayo tayari imeshaanza.Mheshimiwa Spika, nizungumzie kwa kifupi piakuhusu suala la maji vijijini. Naishukuru sana Serikaliinajitahidi sana kupeleka miradi ya maji lakini labdatuweke utaratibu wa kufuatilia kama miradi hiyo yamaji inafanya kazi. Mimi ninazo Kata 37 kwenye Kata 37miradi ya maji ilishapelekwa kwenye Kata zipatazo 35lakini mpaka dakika hii maji yanapatikana kamakwenye Kata 18, zilizobaki mitambo ilishakufa nahaifanyi kazi. Ni sawasawa na kusema kwamba robotatu ya Jimbo la Dodoma halina maji safi na salama yakunywa. Naomba utaratibu huo ufuatiliwe ama piafedha za bajeti ya maji ziongezwe ili kusudi mitamboyote iliyoharibika iweze kukarabitiwa na watu wawezekuendelea kupata maji ya kunywa safi na salama.(Makofi)Mheshimiwa Spika, tatizo lingine liko kwenye Benkiya Dunia, tunawashukuru kwamba wao wanatupatiamsaada sana wa maji, lakini masharti yaliyopo yakwamba wanatakiwa wananchi kuchangia asilimia 2.5,inaonekana kiasi hiki ni kidogo kusema asilimia 2.5,lakini pesa wanazotoa ni mamilioni na mabilioni yapesa, wananchi wanashindwa kutoa hiyo asilimia 2.5.Hivi kwa nini maji yasingeweza kupelekwa kule, watuwakapewa na baada ya hapo maji yatakapokuwayamefika, kila anayekwenda kuchota ndoo ya majiakachajiwa pesa kidogo ili mwisho wa yote ile asilimia2.5 itapatikana na moja kwa moja itapelekwakunakotakiwa.144

Mheshimiwa Spika, nitakuwa sijamaliza hotubayangu kama wananchi wa Dodoma hawatasikianikiongelea kuhusu CDA. Naomba sasa nizungumziekidogo kuhusu barabara pamoja na masuala ya CDA.Nashukuru barabara zimeanza kukwanguliwa, naombabarabara hizi zitengenezwe katika kiwangokinachotakiwa na ziweze ku-cover mji wote waDodoma, zisifanywe kiubaguzi. Maeneo mengi katikaMji wa Dodoma bado barabara hizi hazijafika,naomba zifike kote kwa sababu mabilioni ya pesayaliyotengwa ni mengi mno.Mheshimiwa Spika, lakini naomba hata zilebarabara za lami kwa mfano Area C, Area D, maeneoyote ya kuelekea Soko la Majengo na maeneomengine, tusiweke virakaviraka katika Mji Mkuu waSerikali. Lami yote iliyochakaa ifumuliwe kabisa na lamimpya iwekwe ili Mji wa Dodoma upate kupendeza.Mheshimiwa Spika, nimalizie habari ya CDA.Mwaka jana nilichangia kuhusu mahusiano na CDA,nataka niwahakikishie wananchi wangu kwambaSerikali imesikiliza suala hili. Sasa hivi Mkuu wa Wilayana Mkuu wa Mkoa wameshatambua kabisa upungufumwingi uliopo CDA, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya WaziriMkuu, Mheshimiwa Lukuvi amefanya kazi kubwa sanakuisahihisha CDA na sasa hivi ina mwelekeo mzuri.Wananchi wa Dodoma mtagawiwa viwanja vyotevilivyopo hapa ambavyo vilikuwa vimefungiwa tokamwaka 2008, sasa vitagawiwa na ninyi mtapewa. Kwahiyo, nataka niseme watu wa Nzunguni na maeneomengine yote yaliyopo hapa ambayo mlikuwammeweka msimamo kabisa kwamba hamtaki145

kuonewa, sasa acheni waje wapime, mtapewaviwanja kama kawaida na hakuna atakayenyimwa nawale wengine wote wananchi mliopo hapa mliokuwamnaomba viwanja pamoja na Misikiti na Makanisambalimbali pamoja na Waheshimiwa Mawaziri naWabunge mliopita kwangu ambao mpaka dakika hiiviwanja vilikuwa bado vimekaliwa, sasa mtagawiwa nawote mtapewa. Nataka niseme kwamba MheshimiwaLukuvi amesisitiza kabisa kwamba kuwe na utaratibumzuri ikiwezekana hata litumike boksi kubwa la kuwekamle ndani na watu waje wapate kwa kura ili mtuasinyimwe. Nashukuru sana katika hili na naungamkono hoja ya Waziri Mkuu, ananipenda nanitazunguka naye hapa Dodoma Mjini muweze kuonakwamba tupo pamoja. (Kicheko/Makofi)SPIKA: Asije akawadanganya, mnagawiwa bure?Hamna bure siku hizi. Haya tunaendelea na ProfesaKapuya atafuatiwa na Mheshimiwa MhongaRuhwanya na Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmedajiandae.MHE. PROF. JUMA A. KAPUYA: Mheshimiwa Spika,nianze na shukrani. Kwanza namshukuru MwenyeziMungu kunijalia kuwepo hapa leo kuweza kusimamana kuzungumza mbele ya Bunge hili. Pili nakushukuruSpika kwa kunipa nafasi. Tatu, nawashukuru sanawananchi wa Urambo Magharibi kwa kuniwezeshakuwa hapa baada ya kunichagua mwaka 2010,nashukuru vile vile kwa Wilaya ya Kaliua kuzaliwa.Mheshimiwa Spika, kuzaliwa kwa Wilaya ya Kaliuakumenifundisha mambo mengi sana. Jambo la kwanza146

ni kwamba kumbe ndiyo maana wahenga walisemamkulima ni mmoja lakini akiivisha walaji ni wengi, leokuna mtu alisimama hapa akazungumza habari zaKaliua. Nashukuru kuzaliwa kwa Kaliua, lakini kamakulikuwa na wapingaji yeye alikuwa ni mmojawapokatika watu waliokuwa wakipinga sana kuzaliwa kwaWilaya ya Kaliua, leo anashukuru na mimi nashukurusana. (Makofi)Mhehsimiwa Spika, namshukuru sana Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu yeyekwa kweli ndiye alipanga kipaumbele. NimshukuruWaziri Mkuu alihangaika sana kuhakikisha kwambaWilaya ya Kaliua inazaliwa. Nawashukuru Mawaziriwote wa TAMISEMI waliopitia katika Wizara ile nanikiwataja kwa majina ni Mheshimiwa Kombani,Mheshimiwa Mkuchika, Mheshimiwa Mwanri wote walewanajua jinsi ambavyo walikuwa wakinisaidiakuhakikisha kwamba Wilaya ya Kaliua inazaliwa.Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mkuu wetuwa Mkoa wa zamani, Mheshimiwa Mwinyimsa kupitiaRCC zilivyokuwa ngumu lakini alihakikisha kwambaajenda inakwenda mbele. Nawashukuru sanawananchi wa Urambo Magharibi kwa jinsitulivyoshikamana, nawashukuru wananchi wa UramboMashariki kwa jinsi walivyokuwa tayari kuizaa Wilaya yaKaliua.Mheshimiwa Spika, baada ya shukrani hizo,naomba sasa nijikite katika habari za Wilaya hii mpya.Waziri Mkuu, Wilaya inayozaliwa ni sawasawa na mtotomdogo aliyezaliwa. Mtoto mdogo anapozaliwa katika147

familia, familia ile huwa inahakikisha kwamba mtotowao anapewa chakula ili aweze kukua bilakwashakoo. Naomba Waziri Mkuu Wilaya hii mpya sasaya Kaliua rasilimali ziwekezwe huko ili kuhakikishakwamba kweli inaanza vizuri.Mheshimiwa Spika, nataka nikuhakikishie kwambakama tukianza vizuri, sisi suala la njaa katika Wilaya ilempya ya Kaliua halitakuwepo. Tumeshapoteza miakamiwli katika kusubiri uundwaji wa Serikali ya Wilaya,sasa tunaomba Halmashauri isichelewe kuanza kwasababu kama mnavyojua mtekelezaji mkuu wa Ilaniambayo ndiyo Ilani ya CCM ni Halmashauri. Tunaombaututajie Halmashauri yetu mapema na Mkurugenzialetwe mapema pale kuhakikisha kwamba kazizinaanza vizuri.Mheshimiwa Spika, Wilaya hii ni kubwa, ina kilomitaza mraba 16,000. Kwa hiyo, wananchi wake wanahitajikufika katika Makao Makuu ya Wilaya na ili wafiketunahitaji barabara, hasa barabara ya kuelekea Ugalaambako tunapakana na Waziri Mkuu, kule hakunabarabara kabisa, masika wanakuwa kamawamefungiwa kabisa. Vilevile Waziri Mkuu barabaranyingine inaelekea kaskazini ambayo ndiyo inakwendaUyoa, Makasi, Kashishi mpaka kufika Kahama kule. Hizibarabara zikitengenezwa, zitafungua uchumi wawananchi hawa. Madhumuni ya kupata Wilaya mpyani kuhakikisha kwamba tunasogeza huduma kwawananchi, hatusogezi huduma kama barabara hizihazijatengenezwa.148

Mheshimiwa Spika, baada ya kutangazwa kuwatumekuwa Wilaya ilikuja Tume ya watalaam kutokaREA, wamefanya survey kubwa sana, wametuahidikwamba tutapata umeme, lakini hizi zimebaki kuwa niahadi kama ripoti tu. Naomba Waziri Mkuu utekelezajisasa uharakishwe sana. Kuna umeme tunaoupata waphase moja unatokea Urambo mpaka Kaliua, lakiniutashangaa unapita katika vijiji vya Isanjandungu, Kijijicha Isimbi unapita wima tu, sasa wananchiwanashangaa hivi sisi tumepita hapa kama barabaratu? Kwa heshima, naomba vijiji hivi sasa katika umemeule ambao upo, kazi hii ianze ya kutupatia umemelakini vipo vijiji vingine ambavyo nitamkabidhi Waziri waNishati ili aweze kutusaidia.Mheshimiwa Spika, katika suala la uwezeshajiwananchi, nikisoma kitabu hiki cha hotuba yako WaziriMkuu umezungumzia kwamba mifuko ya uwezeshajiwananchi ambayo inaongozwa na Baraza la Uchumila Taifa ndiyo ambayo kama mhimili mkuu naviunganishi ni SACCOS. Kuna microfinance Institutionmoja inaitwa SCULT, wananchi wa Kanoge walichangakupitia SACCOS yao shilingi milioni 27, mwaka wa tatuhuu hawajapata chochote. Nimezungumza na mtu waSCULT ananijibu majibu ya ovyoovyo tu, bahati nzurinilishazungumza na Mheshimiwa Nagu amenihakikishiakwamba atamwita hapa aje kuhakikisha kwambatunafikia solution. Mambo kama haya yanawavunjamoyo wananchi.Mheshimiwa Spika, TASAF, kipo Kijiji kinaitwaKazanaupate katika Kata ya Igadala…149

MBUNGE FULANI: Kinaitwaje?MHE. PROF. JUMA A. KAPUYA: KinaitwaKazanaupate, tulibuni mradi mwaka 2006/2007 waujenzi wa shule kwa jumla ya shilingi milioni 34, Serikaliichangie shilingi milioni 29 sisi wananchi tuchangieshilingi milioni sita (6). Wananchi walifyatua tofali, tukotayari kuchota, mpaka leo hatujapata hata senti mojakutoka TASAF, ukiuliza unaambiwa ilikuwa TASAF I,TASAF I imekwisha sasa tunahitaji TASAF II na TASAF IInayo inakwisha tunaingia TASAF III. Waziri Mkuunaomba hawa wananchi wasipuuzwe kwa sababuitakuwa kazi ngumu sana kwenda kuwashawishi tenakuchangia katika mambo ya maendeleo.Mheshimiwa Spika, kuhusu kilimo, kilimo ndiyo utiwa mgongo, sehemu zingine mnasema asilimiathemanini kwa Kaliua ni asilimia 99 shughuli zetu zotezinajikita pale na kilimo chetu kikubwa sisi ni tumbaku.Tunalo tatizo na wawekezaji hawa wa tumbaku.Wamechukua nafasi wakawa wanatupangia hata ninani alime na nani asilime. Kila mwaka vijanawanamaliza darasa la saba na wanamaliza form fourwanapotaka kulima, wanakatazwa mpaka Mzunguakubali, sasa unashangaa tutawezaje kuingia maishabora kwa kila Mtanzania? Mwaka juzi tulizalishatumbaku nyingi sana, wakakataa kuinunua, wakasemani nyingi mno, mlipowabana wakasema tutanunuayote lakini wakateremsha bei ili kwa fedha zilezilewaweze kununua tumbaku ileile. Hii kwetu haitusaidiikabisa. Naomba tusaidiwe kwa Serikali kuingia katikamazungumzo na nchi nyingine kama Uturuki, China na150

kadhalika ili kuhakikisha kwamba wanunuzi watumbaku wanaongezeka.Mheshimiwa Spika, zao lingine tunalolima sisi nimahindi, inawezekana hatupo katika the big four lakininataka nikuhakikishie kwa mvua tulizonazo sisi tunalimamahindi ya kutosha na ukizingatia na kanuni za kilimokwanza tumeweza kuzalisha mahindi mengi sana.Lakini sasa ikaja sera ya kukataza kuuza mahindi hayanje ya Wilaya, ilituathiri sana. Kwa hiyo, naomba WaziriMkuu, sera hii ya kusema kwamba mahindi yazuiliwekuuzwa kwa sababu sisi kweli wapo wanaolimatumbaku na wapo wanaolima mahindi kama zao labiashara, mnapowakataza inaleta balaa,wanashindwa kusomesha watoto wao, wanashindwakupelekwa wagonjwa wao hospitali. Naomba sanaWaziri Mkuu hili lizingatiwe.Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la maji,limezungumzwa sana suala la World Bank hapa, sisituna vijiji vitatu pale Kaliua Mashariki, Kaliua Magharibina Ushokora. Tulipata mradi wa World Bank lakinitumechimba visima 12, vitatu ndiyo vyenye maji. Sasamkataba tunaowekewa tunaambiwa kwamba atakujakuchimba visima 12, alipochimba 12 vitatu vina majitisa havina maji akasema, mimi tayari, sasa tofauti nidefinition. Kwa mwananchi wa kawaida kisima ni kilechenye maji, yeye anasema nimeshakuchimbiamashimo yako kumi na mbili shauri yako, sasa inakuwamatatizo makubwa. Itatupatia matatizo makubwa sisikuwachangisha tena milioni tano katika miradi mingineambayo mtakuja kutuletea. Waziri Mkuu, tusaidie ilitufikie solution hapo.151

Mheshimiwa Spika, kuhusu hifadhi, suala la hifadhisisi ni tatizo kubwa sana. Kuna baadhi ya wanasiasawanatumia hili kama mtaji wa kupatia kura.Wanawashawishi wananchi, wanakuja kuhamia mahalipale na wanaingia katika hifadhi, ukienda utakutakatika hifadhi zetu zote asilimia 99 ni kabila moja,asilimia 99 kazi ni moja, asilimia 99 wote Chama kimoja,unashangaa, Waziri Mkuu tusiruhusu mambo ya namnahii. (Makofi)Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, katika bajetimama ambayo Waziri wa Fedha alipitisha, tutaajiriwafanyakazi wapya 71,000, naomba asilimia kubwaiwe wafanyakazi wa Wizara ya Afya maana tunamatatizo katika zahanati zetu. Tuna sera ya kuanzishavituo vya Afya, watatushangaa wananchi hawatunaanza kujenga vituo vya afya kabla zahanatihazijajaa watumishi. Nakushukuru sana, ahsante sana,naunga mkono hoja. (Makofi)SPIKA: Ahsante sana. Sasa nimwite MheshimiwaMhonga Ruhwanya, Mheshimiwa Rukia Ahmed naMheshimiwa Moza Abedi wajiandae.MHE. MHONGA S. RUHWANYA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi angalauniweze kuchangia kidogo katika hotuba ya Bajeti yaWaziri Mkuu. Kwanza kabisa, namshukuru MwenyeziMungu kwa kunipa afya nimeweza kusimama hapa iliniweze na mimi kutoa mchango wangu.152

Mheshimiwa Spika, nitaanza na usafiri wa reli.Kama unavyofahamu, Kigoma tuna matatizo sana yausafiri, kuanzia usafiri wa anga, barabara zenyewendiyo hivyo hatuna. Kwa hiyo, tunategemea reli kwakiasi kikubwa na ndiyo usafiri rahisi ambao Watanzaniawengi wanaweza kuutumia hasa wa kutoka kwetuKigoma.Mheshimiwa Spika, nitaanza na treni yenyewe,mabehewa kwa kweli yanasikitisha, yamechakaa mno,vyoo vyenyewe ni vichafu, hakuna vioo kwenyemadirisha, watu wanasafiri mchana vumbi lao, usikubaridi yao, kwa kweli ni usafiri ambao hauna staha. Vitivimechakaa, hakuna hata sponchi, mende, kunguni,kwa kweli ni usafiri wa ajabu sana. Napenda kujua hivitunahitaji mtaji kiasi gani kuweka tu sponchi kwenyevile viti, kusafisha yale mabehewa, kwa kufanya hatafumigation, inasikitisha mno kwa kweli. Usiendeukapanda ile treni hasa second class ambayo nikukaa, utajionea maajabu. Naomba sana kama Wazirianayehusika hajaliona hili akaangalie tena.Nimeshawahi kumwona mara nyingi kwenye treni lakinisijaona akilisemea hili. Uchafu, kwa kweli mabehewa nimachafu mno. (Makofi)Mheshimiwa Spika, suala lingine ni tiketi,upatikanaji wa tiketi ni mgumu, nashindwa kuelewa.Naomba Waziri Mkuu kama Waziri wa sekta, nalo hilihajaliona, ulisemee wewe. Kwa mfano Kigoma watuwanatakiwa kukata tiketi siku hiyohiyo ya safari. Sasawanatoka Kibondo, wanatoka Kasulu na maeneomengine ya Mkoa kwa mfano treni ni siku ya Alhamisna siku ya Jumapili, wanalala pale, kama mtu anataka153

kusafiri Alhamis, anaondoka kwake siku ya Jumatano,anakuja kulala stesheni ili alfajiri awahi kupata tiketi,matokeo yake sasa bei inakuwa ya kuruka, tiketi nishilingi elfu kumi na tisa, mtu kama ana uwezo wakutoa pesa kidogo ili asipange foleni, anawatumiawalewale wafanyakazi wa pale stesheni, wanalipatiketi mpaka shilingi 35,000, mimi sidhani hapo kamatunamsaidia Mtanzania, tunazidi kumrudisha nyuma.(Makofi)Mheshimiwa Spika, napenda kujua huyo aliyetoahilo agizo ni nani kwani ni Quran au Biblia haiwezikubadilishwa? Ninaomba utaratibu wa zamaniurejeshwe. Tulikuwa tunakata tiketi kama unajuautasafiri wiki ijayo, mwisho wa mwezi umepata helayako unaenda kukata tiketi tarehe fulani nitasafiri, sikuikifika unakwenda unasafiri kwa staha lakini sasa hiviwatoto, akina mama wazee, wagonjwa wanalala palestesheni kuhakikisha kwamba labda kesho yakewatapata tiketi na ikitokea kama Jumatanohawakupata, kwa hiyo, maana yake Alhamis hatasafiri,wakati mwingine hawezi kurudi kwake Kibondo auKasulu au maeneo mengine analala pale tena mpakasiku ya Jumamosi ili Jumapili aamkie pale awezekupata tiketi, sasa mazingira ya stesheni pia yanakuwamabaya, machafu. Kwa kweli tunaomba tubadilishiweutaratibu, huu hautufai hata kidogo na sisi ni watuwastaarabu tunahitaji ustaarabu.Mheshimiwa Spika, nitaongelea vilevile suala lamaji, inasikitisha tunalo Ziwa Tanganyika lakini tunapatamaji mara moja kwa wiki. Kama iliwezekana zamaniwatu walipata maji kila siku, inakuwaje sasa hivi154

tushindwe? Nakumbuka Bunge la Tisa niliwahikuongelea suala hili, nikajibiwa kwamba matatizo ni yaumeme, kwa hiyo pampu haiwezi kusukuma maji nawananchi wakaweza kupata na ndiyo maana watuwalikuwa wanapata maji mara moja moja, lakini sasahivi umeme upo, hata kama ni wa mgawo lakiniangalau upo siyo kama zamani. Naomba kujuasababu ya msingi hasa ni nini?Mheshimiwa Spika, majibu mengine ambayoyalikuwa yakitolewa ni kwamba mabomba ni chakavu,miundombinu ya mabomba inabadilishwa, kwa hiyosasa hivi watu wataanza kupata maji safi na salama,lakini mpaka leo maji bado hayatoki, ukienda Gungu,ukienda Kisangani, ukienda Ujiji, na maeneo yote kwakweli yanasikitisha maji hayapatikani. Vijana wenyenguvu ndiyo wamejiajiri sasa wanaenda ziwaniwanachota maji, wanawauzia watu, inategemea naumbali, dumu shilingi mia tano mpaka wakati mwingine1500. Mimi naona hii siyo sawa kwa kweli. Maishayenyewe magumu, mfumuko wa bei na kule kwetukulivyo mbali mpaka kitu kifike, sementi tunanunuampaka shilingi 25,000 mafuta ya petroli tunanunuampaka shilingi 2600, 2700 na kuendelea, kwa hiyomaisha yetu yanazidi kuwa magumu, naombamturahisishie kwa kweli. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kujua ni linitutapata maji safi na salama, kwa vile hili ni tatizokubwa kwetu. Napenda tu niwaambie Serikali yaChama cha Mapinduzi, kama mtaendelea kuachakero nyingi ziendelee kututawala wananchi wa Mkoawa Kigoma, kama kuvamiwa, tunakamatwa kama siyo155

aia na mengine mengi, inawezekana hata hayoMajimbo matatu yaliyobakia msiyapate tena, yoteyaingie upinzani kwa sababu tumechoka, tuna ahadinyingi lakini hazitekelezwi. (Makofi)Mheshiimiwa Spika, niende tena kwa upandemwingine wa afya, tuna matatizo sana ya watumishi.Najua hili ni tatizo lipo nchi nzima lakini siwezi kuachakulisemea kwa kweli tuna matatizo. Nikitolea mfano tutunaye Daktari Bingwa mmoja wa watoto Mkoa mzimana anatumika kwa Wilaya zote ambazo tunazo zaKasulu, Manyovu, Kibondo, Kigoma Manispaa namaeneo mengine, tunamtegemea huyo DaktariBingwa mmoja wa watoto na bingwa mmoja wawanawake. Nikichukulia mfano mmoja mdogo waWilaya ya Uvinza na Wilaya ya Kigoma, kuna mahitajiya watumishi wa afya 559, tunao 255 peke yake. Kwahiyo, upungufu hapa ni kama 307. Katika hao ClinicalOfficers wanaohitajika ni 112 na Nurse Midwife ni 113.Kwa hiyo, tunaomba sana utaratibu wa kupangawatumishi ukifika, mtuangalie kwa jicho la huruma.Mlimsikia hata Mheshimiwa Buyogera hapa alielezeaKasulu hali ilivyo, tunahitaji sana watumishi katika ngazihiyo ya afya. (Makofi)Mheshimiwa Spika, vilevile Hospitali ya Mkoaimeelemewa mno kwa sababu Hospitali kwa mfanoWilaya ya Kigoma na Uvinza ambayo tulikuwatunaitegemea haijakamilika. Kwa hiyo, maana yakewagonjwa wa maeneo yote hayo wanatakiwawaende wakatibiwa katika Hospitali ya Mkoa ambayokwa kweli hali yake nayo ni duni kwa sababuimeelemewa. (Makofi)156

Mheshimiwa Spika, nikienda upande mwingine waelimu. Nikiangalia tu shule za msingi bado mazingirayake ni magumu mno, watoto wanajifunzia chini,madarasa mengine wengine wanasoma chini ya miti,hali siyo nzuri kwa kifupi. Matokeo yake ndio maanawanafunzi wanakuja kumaliza darasa la saba hawajuikusoma wala kuandika. Ni kwamba mazingirayenyewe ni mabaya. Wanafundishwa Tehama kwakuchorewachorewa computer kwenye ubao,wataionaje wakati maeneo mengine kwanza hataumeme hakuna? Mimi naomba tufundishwe vituvinavyoendana na mazingira yetu vilevile. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini tunao upungufu mkubwapia Walimu, mbali na hayo madawati, vitabu, sijui navitu vingine, tuna upungufu mkubwa sana wa Walimu.Nimechukua tu kesi study ya Wilaya ya Kigomaambayo ni Uvinza na Kigoma yenyewe, tuna upungufuwa Walimu wa shule za msingi kama 600. Kwa kwelimkipanga Walimu mkumbuke Mkoa wetu. Mazingirayetu ni mazuri, naamini wanaweza tu wakaja. Vilevilena Serikali iangalie uwezekano wa kuboreshamazingira ya kufundishia Walimu, iongeze hizo posho ilikuhakikisha kwamba Walimu wanaokwenda kwenyemazingira magumu waweze kuona wako sawasawana Walimu wengine ambao wanafundisha mjini.(Makofi)Mheshimiwa Spika, naenda katika kilimo chamchikichi. Ukurasa wa 18 na 19 wa Hotuba hii ya Bajeti,nimeona Waziri Mkuu ameongelea mazao menginekama korosho, kahawa, pamba, sijui kwa nini mchikichihajaona kama ni zao muhimu. Nakumbuka miaka ya157

1960 katika kusomasoma, niligundua kwamba watu waMalaysia walikuja hapa Tanzania kujifunza juu ya zaohili, sasa hivi zao hili ni zao kuu kwao na wanalilimakatika mtindo wa kisasa. Sasa nashindwa kuelewa kwasababu mafuta haya ni mazuri sana kiafya, yanavitamini nyingi, hayana cholesterol, kwa nini zao hililisiboreshwe tukaanzia labda na wale wakulimawadogowadogo wakawezeshwa kufanya kilimo chakisasa?Mheshimiwa Spika, vilevile kuna Gereza mojalinaitwa Kwitanga wanalima sana mchikichi,wanazalisha kwa kiasi kikubwa sana. Mimi naombaSerikali basi ianzie hapo kuwa-support pamoja nakwamba nguvu kazi inayotumika pale ni ya wafungwalakini pia kile ni Chuo cha Mafunzo siyo lazima kwambanguvu zao ziendelee kutumika tu siku zote. Tunawezatukawapelekea mafunzo, wakaweza kulima kilimo chamawese cha kisasa. Vilevile Serikali ikaangaliauwezekano wa kuwakopesha matrekta ambayoyamewekwa pale, ya Mwenge na mengineyamewekwa pale kinachoitwa Kilimo Kwanza, wawezekukopeshwa ili waweze kuzalisha zaidi. Mimi nafikiri nimuhimu sana kuongeza uzalishaji wa mafuta nchinikwa sababu tuna mahitaji makubwa.Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi.(Makofi)MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niwezekuchangia hoja hii katika Bunge lako Tukufu. Kabla yakuchangia, naomba niseme kitu kidogo, katika Kitabu158

cha Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, ukurasa wa33 alisema kuwa CCM na Washirika wakewanakishutumu Chama kimoja ambacho ni makinikwa kusema kuwa chama hicho ni cha Kidini, Ukabilana Ukanda. Lakini napenda niseme kwamba Washirikawa CCM, nadhani kwa muono wangu mimininavyoona ni Mawaziri, Manaibu Waziri pamoja naManaibu Waziri Kivuli. Nadhani hawa ndio Washirika waCCM. Au tukiacha hilo kwa muono wangu basiWashirika wa CCM ni sote tuliomo katika mjengo huukwa sababu tunafanya mambo kwa pamoja kwamaslahi ya nchi yetu na kwa maslahi ya vizazi vyetu.(Makofi)Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo,naomba sasa niende kwenye hoja. Nataka nielezee nikitu gani kinachowafanya Watanzania wakose imanina Serikali hii sikivu. Wakati tunapokuja hapa katikaBunge la Bajeti, Watanzania wote wanakuwa katikavyombo vya habari kusikiliza ni nini Serikali inawaambiana ambacho Serikali inategemea kuwafanyia.Watanzania hawa hujenga matumaini kwa lile ambalowanalisikia katika vyombo vya habari. Katika kipindicha Bajeti cha mwaka 2011/2012, Serikali wakati wakuwasilisha bajeti yake walisema wataongeza uzalishajikatika sekta ya kilimo. Watanzania walijengamatumaini na wakaona kwamba hili litawafanyawaondokane na hali ngumu ya maisha waliyonayo.Katika kipindi chote kile cha mwaka 2011/2012 nadhanihakuna kilichoongezeka isipokuwa hali ya maishainazidi kuwa ngumu kwa Watanzania wote.159

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha bajetihichohicho cha mwaka 2011/2012, Serikali iliahidi kuwaitaweza kushughulikia suala la wafanyakazi hewa.Wananchi wote walijenga matumaini, Watanzaniawakasema sasa Serikali imeamua na watashughulikiasuala hili la wafanyakazi hewa na fedha ambazo ni zaSerikali zinazovuja zikienda katika mikono ya walaji haozitapatikana na zitakwenda kuendeleza shughuli yamaendeleo katika nchi yetu. Matokeo yakehatukuweza kulisikia suala hili, Mheshimiwa Waziri waFedha juzi alizungumza katika bajeti yake hatukumsikiahata kulitaja. Katika kitabu cha Mheshimiwa WaziriMkuu sikuona hata sehemu iliyozungumzia suala hili lakushughulikia wafanyakazi hewa. Kwa kweli katika halihii ikiwa Serikali itaendelea kuwa na mtindo wakuzungumza mambo halafu matokeo yake katikautekelezaji haupo, hili linawafanya Watanzania wakoseimani na Serikali hii sikivu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, katika kipindi hichohicho chaBajeti cha mwaka 2011/2012, Serikali ilisema kuwaitafufua umeme Nyakato - Mwanza wa MW 60,hatukuona umeme uliofufuliwa wala uliozikwa.(Makofi/Kicheko)Mheshimiwa Spika, napenda niishauri Serikali paleinaposema mambo iwe na uhakika wa kuyatekeleza.Sisi tunajua kama Bajeti yetu tunayokwenda nayo nibajeti tegemezi. Pia tunajua kama bajeti yetu ni bajetiya mali kauli. Bajeti tunaitaja kwa maneno lakinimatokeo yake fedha tunakuwa hatuna. Basi miminaishauri Serikali pale inapokuwa tumeshindwakuyatekeleza yale ambayo Bunge hili liliambiwa, Serikali160

irudi tena iliambie hili Bunge kwamba tulizungumza hilina hili lakini halikutekelezeka, tusubiri kipindikinachokuja mambo haya yatatekelezwa, wananchiwatajenga imani na hii Serikali tuliyonayo lakinitukienda katika hali hii ya kuwa na maneno mengilakini vitendo ni vifupi, wananchi wanakosa imani naSerikali hii sikivu.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,naomba nijielekeze kwenye mfumuko wa bei.TAARIFAMHE. FELIX F. MKOSAMALI: Mheshimiwa Spika,nilikuwa nataka nimpe taarifa tu kwamba sisi hatukokwenye Serikali kwa sababu amesema kwamba sisiwote humu ndani ni Washirika wa CCM, sasa nimeonanimpe taarifa kwamba sisi hatuko kwenye Serikali nakwa mujibu wa Kanuni zetu kuna Kambi ya Upinzanikwa hiyo sisi siyo CCM hata kidogo. (Makofi)SPIKA: Haya Mheshimiwa Rukia umekubali taarifahiyo?MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Spika,kwanza siitaki taarifa yake hata kuinusa kwa sababu sisisote tunashiriki katika Kamati za Bunge na tunafanyakazi kwa kuisaidia Serikali. (Makofi)Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,naomba niendelee na kuzungumzia mfumko wa bei.Mfumuko wa bei umekuwa ni mkubwa sana, hali hii161

imekuwa ni ngumu sana, Watanzania wanalia,Watanzania wanaishi katika mazingira magumu,maisha yamekuwa magumu, yanazidi kuongezeka sikuhadi siku. Tukiangalia Julai mwaka 2011, mfumukoulikuwa kwenye asilimia 13 hadi kufikia Septemba, 2011tayari ulishafikia asilimia 16.8, hadi kufikia Desemba,2011 mfumuko wa bei ulishafikia asilimia 19.8. Hii ni haliya kutisha, ni hali kukaa Wabunge tukajiuliza ninitufanye kuisaidia Serikali ili wananchi waondokane naugumu huu wa maisha. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hivi sasa Tanzania mtu anawatoto sita (6) ndani ya nyumba, ananunua mchelekilo ni shilingi 2000 mpaka 2600, hivi jamani tunaishi vipi?Tusione sisi tuliomo humu ndani tuna viyoyozi, tunajisikialakini wenzetu wanalala na njaa. Imefika mahaliwanaume wanakimbia nyumba zao kutokana ugumuwa maisha, tunaoteseka ni sisi wanawake na watoto.Baba akikimbia nyumba mwanamke anabaki nawatoto hajui afanye nini, anachanganyikiwa. Tunazidikuongeza idadi ya wajane na watoto wa mitaani.Naiomba Serikali ilione hili ni janga la kitaifa na kwakweli tufanye iwavyo lakini maisha yashuke, wananchiwanalia kwa dhiki. (Makofi)Mheshimiwa Spika, haya yote yanatokana namatumizi mabaya ya Serikali. Mapato ya ndani yaSerikali ni shilingi trilioni 8.7 hayakidhi hata matumizi yakawaida. Matumizi ya kawaida yanakuwayanaongezeka kutokana na Serikali kuongeza matumiziya kiutawala kuliko ya maendeleo, hili halitakimwenge, sote tunaliona. Kuna Mikoa chungu nzimailiyoongezwa na Wilaya, yote hii inataka matumizi na162

matumizi yaliyopo ni kuwa tunabana matumizi yamaendeleo, tunatumia fedha hizi kwa matumizi yakiutawala. Naishauri Serikali ipunguze matumizi yakiutawala na fedha ziende kwenye matumizi yamaendeleo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, la kama tungekubaliana hapakuongeza katika sekta ya kilimo, tukaipa kipaumbelebadala ya asilimia 2.92 iliyopangiwa ikapangiwaasilimia angalau 10 tukaweza kufanya uzalishaji…(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. (Makofi)MHE. MOZA A. SAIDY: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili nami niwezekuchangia Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.Kwanza kabisa, ningetoa angalizo kabla ya yotekwamba sisi tumekuja hapa kwa dhamana yawananchi na tunahitaji kuwawakilisha wananchi iliwajue kwamba ni nini kilichopo, kinachotakiwakifanyike katika maeneo yetu. Hatukuja hapa kwa ajiliya malumbano kuona kila mara au Bunge likawalinaitwa kama huko mitaani wanavyoliita Bunge laMiongozo. Kwa hiyo, naomba tuwe na fikra za dhanakwamba tumetumwa kuja kuwawakilisha wananchi.(Makofi)Mheshimiwa Spika, mimi nielekee katika suala lamaji, maji imekuwa kila anayesimama hapa163

anazungumzia suala la maji, atakayeinukaanazungumzia suala la umeme, hili limekuwa kamajanga la kitaifa katika nchi yetu ya Tanzania. Tunaowatalaam wazuri kabisa ambao wamefundishwa naSerikali hii. Wakafundishwa mpaka wenginewamekuwa Maprofesa wa kilimo ambao hawana hatashughuli zozote, inawezekana kabisa wataalam hawawakatumiwa vizuri, wakatutengenezea mabwawaambayo yatajaa maji yakaweza kutupa umeme napia yanaweza yakasaidia wananchi na hali kadhalikayakatumika katika umwagiliaji. Nafikiri watalaam haotunao na tumewafundisha sisi wenyewe katika Serikalihii. (Makofi)Mheshimiwa Spika, napenda nizungumzie suala laelimu. Suala la elimu, kwa kuwa TAMISEMI imezidiwa namzigo mkubwa au ina mambo mengi na kwa kuwaWizara hii ya TAMISEMI iko chini yako Mheshimiwa WaziriMkuu, kwa kweli katika suala la elimu imezidiwa. Je,sasa hivi inawezekana Wizara hii kwa kuwa naHalmashauri zetu zinashindwa kuisimamia vizuri sekta yaelimu ingefaa kabisa itolewe katika Halmashauri ipewekitengo maalum ili iweze kusimamia vizuri elimu, suala laelimu lazima liboreshwe. Hakuna nyumba za Walimu,Mwalimu huwezi kumtoa hapa ukampeleka kijijini kwamfano kule kwangu umpeleke Changaa, umpelekehuko Hondomailo hakuna maji, umpeleke kilomita 10kutoka Kondoa Mjini mpaka Tumbelo, hakuna maji,hakuna umeme na kumefumuka na madini pia, katikahali kama hiyo uchumi kama huo unajitokeza lakinitunashindwa kuuboresha sisi wenyewe katika Serikali hiiambayo si sikivu jamani naomba tuangalie palipo namatumaini tupeleke nia. (Makofi)164

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo sasa nijekatika suala moja ambalo limejitokeza hapa juzi.Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuwa Serikali imeundachombo cha usalama ili chombo hiki cha usalamakiweze kulinda mipaka yetu, mali zetu pamoja na raialakini kitu cha kusikitisha sana ambacho nimekionakilichojitokeza hapa juzi, kweli hivi kweli lori likatokahuko lilikotoka mpaka likafika katikati ya Mji ambaouna dhana ya kuwa Mji Mkuu wa Tanzania,limesheheni watu mpaka watu wale wamekufa mpakawengine wameharibikia wamekuja kuwashusha katikaMji huu wa Dodoma! Hivi kweli lori hilo lingebeba silahana sisi Serikali ilikuwepo hapa, hivi kweli sisitungekuwepo sasa hivi? Suala hili kwa kweli limeletamasikitiko makubwa na inaonyesha ni rushwa imejaamoja kwa moja, rushwa kubwa ambayo imeeneakatika mageti yetu yote.Mheshimiwa Spika, sasa hivi mkulima akilimashamba lake, akitoa mazao yake kule kijijinikuyapeleka mjini, akifika tu njiani anakutana na geti,lazima afunguliwe, aangaliwe ana magunia mangapi,ahesabiwe atoe hela. Leo hii lori limebeba watu kamawale na watu wale hawawezi kuja hivihivi bila kuwa namkalimani, lazima Watanzania na wenyewe wanashirikihumu. Je, Serikali inaliangaliaje suala hili, mbona nihatari kubwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nije kwenye suala la uwekezaji.Tanzania kweli imejikita katika suala kubwa lauwekezaji. Suala la uwekezaji kwa kweli tunawekezandio kama hawa watu wengine wanaingia katika nchi165

yetu bila sisi wenyewe kujijua kwa ajili ya huruma zetu.Suala la uwekezaji utakuta kwamba mwananchikajivunia mwenyewe, kafyeka shamba lake, kaliandaavizuri limependeza au Kijiji, tayari imekuwa mwekezajipale anakwenda yeye mwekezaji. Hebu tuangaliekwanza migogoro mingi ya ardhi inatokana na kilekilichokuwa kizuri kinatamaniwa na kinaunganishwa nawatu kutoka ngazi za chini kama chain kuja juu kwakuwapa wawekezaji. Tujiangalie kwanza sisi wenyewetumetosheka na ardhi. Kama sisi tumetosheka na ardhina tunayo ya kuwapa Wareno twende tuwarudishe.Tumewaondoa Wajerumani tuwarudishe,tumewaondoa Waarabu tuwalete ili wazidi kujakututawala zaidi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sasa hivi inabidi Serikali kuwamakini zaidi kuangalia na kuratibu hata katika sensazetu watu wanavyopita nyumba hadi nyumbakuangalia nani yupo na nani kaja hapa na kwa nini nani kabila gani. Ipo haja ya kufanya hivyo kutoka nawasiwasi uliopo, maadui wataingia mpaka hapandani. Mpaka hivi sasa tumeuona na tumeshuhudiakwa macho, hii ndiyo Serikali sikivu ya Chama chaMapinduzi ilipotufikisha hapa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, mwisho, nina masikitikomakubwa kuhusiana na migomo ya Madaktari lakinikwa angalizo zaidi, hukumu hii wanayo wananchiwenyewe na wananchi kwa kweli ndiyo wanaopataadha kubwa na wanaona matatizo yanayowakuta.Naomba Serikali yetu ichukue njia zingine za harakakwa ajili ya kuweza kuokoa maisha ya wanadamu.Wanadamu wale ndiyo ambao wanatusaidia sisi. Sisi166

wenyewe pia tukiumwa hapa sasa hivi lazimatukamuone Daktari, kama inafikia hatua hiyo, kwakweli hali inakuwa ngumu.Mheshimiwa Spika, nimalizie na kwamba katikaMkoa wetu wa Dodoma, tulioko hapa, tumeshajengawodi moja ya akina mama, hospitali tunayo hapa nahospitali hii ya Mkoa haina zana za kisasa hata moja, nihospitali hii majeruhi wakitokea hapa lazimawapelekwe Muhimbili. Kwa nini zana za kisasazisiwekwe zote hapa ikawa ni hospitali kama ya rufaa,watu wanaotoka Mwanza basi wakaishia hapa,wasiwe wanapitiliza tena moja kwa moja mpakaMuhimbili. Wametoka Kanda zote huko za Kati waishiehapa hapa Dodoma na huko Mbeya hali kadhalikaikatengenezwa hivyo. Mbona fedha nyingi zipo? Fedhaambazo zinapatikana sasa hivi ni nyingi na madinitunayo, uchumi mkubwa tunao nchi yetu.Mheshimiwa Spika, mwisho niongezee tu kwambakatika Wilaya yangu ya Kondoa kumefumka madini namadini yale kwa kweli wachimbaji wadogowadogowameyavumbua na ni moja ya sura ya nchi katikaTanzania.Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Kondoa pia inamapango. Mapango yale pia yameanza kupaukakatika ile michoro. Naomba katika Idara ya Mambo yaKale iongezewe fedha ili ikaboreshe zaidi mapangoyale na kuwavutia watalii kama ilivyokuwa zamani nakuwaingizia pato la Kitaifa. (Makofi)167

Mheshimiwa Spika, sitaunga mkono hoja mpakahaya yote yatekelezwe na yafanyike kwa ufanisi zaidi ilituweze kulijenga Taifa letu upya na wananchi wawena imani na sisi kama jinsi ilivyo, ahsante. (Makofi)MHE. HAROUB MUHAMMED SHAMIS: MheshimiwaSpika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii yakuchangia katika hotuba hii ya Mheshimiwa WaziriMkuu. Awali ya yote, nimshukuru Mwenyezi MunguSubhuhana Wataalah kwa kunipa afya ya kusimamambele ya Bunge lako hili Tukufu.Mheshimiwa Spika, naomba ruksa yako kidogonikariri ubeti wa shahiri moja unaosema, ni haki sawakwa watu wote kuendeleza itikadi yetu. Utajirishweitikadi yetu, tukatae kuonewa. Siasa itumikie uchumi namwiko huo uchumi kutumikia siasa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ubeti huu ni wimbo wa Taifawa Chama cha Wananchi CUF. Naiomba Serikaliichukue hapo siasa itumikie uchumi na iwe mwikouchumi kutumikia siasa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hapo ndipo tulipojikwa natukishajua tumejikwa wapi, ni rahisi kutatua. Tusiangaliekule tulipoanguka. Tulipojikwa ni kwamba siasainatumikia uchumi.Mheshimiwa Spika, nchi hii ina utajiri wa ainanyingi. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu natulifanya ziara katika Mikoa ya Kusini na Nyanda za Juunikajionea kwa macho. Nilikuwa najua kijeografia, lakininimeona kwa macho yangu na wasema seeing is168

elieving. Nchi hii ina rasilimali kubwa, lakini tatizo nikwamba uchumi unatumikia siasa. Kwa hiyo,tubadilishe hapo ili tuweze kujenga maisha ya watu.Tukibadilisha ikawa siasa inatumikia uchumi, tutawezakuboresha kilimo cha wananchi wetu. Hivi sasa asilimia75 ya Watanzania ambao ni wakulima wana halingumu sana za maisha kutokana na kwamba siasainatumikia uchumi. Wananchi hawa asilimia 75hawana nyenzo za kuendeleza kilimo, Serikali imetengabajeti ndogo kwa ajili ya kilimo ambayo ni 192 bilioni.Kwa kweli hii ni pesa kidogo sana. Wakulima hawahasa wadogowadogo wakiwezeshwa, ndiyotutakapoweza kujenga uchumi imara ambao ndiyotutakuwa tumepunguza umaskini, maradhi nautapiamlo.Mheshimiwa Spika, watoto asilimia 42 walio chiniya miaka mitano (5) wana utapiamlo, maradhi yakwashakoo, hii yote inasababishwa na ukosefu wachakula bora. Hii ni idadi kubwa ya watoto ambaondiyo Taifa letu la kesho tunalolitegemea kuongozanchi hii. Tuimarishe uchumi kwa kuimarisha kilimoambacho ndicho tulikuwa tunaambiwa katika sloganya nchi hii kwamba ndiyo uti wa mgongo wa Taifa hili.Kwa hiyo, ili iwe utii wa mgongo kweli, tuwasaidiewakulima wadogowadogo kuwapa nyenzo za kilimo,mbolea na pia kuwajengea miundombinuitakayowawezesha kufikia masoko, barabara, reli,bandari na pia Serikali isimame mbele kuwatafutiamasoko wakulima ili mazao yao yaweze kuuzwa nakupata maisha yaliyo bora. (Makofi)169

Mheshimiwa Spika, hivi sasa kuna neemaimepatikana ya gesi ambayo tunaambiwainachimbwa huko Mikoa ya Kusini na gesi hii ni utajirimkubwa kwa kweli, tukiutumia vizuri utatunufaishakatika nchi yetu. Naiomba Serikali ichukue ushauriwangu wa siasa kutumikia uchumi, mapato ya gesi hiiyajenge miundombinu ya nchi ya kiuchumi ikiwemokuimarisha barabara, kujenga reli za kisasa, kujengabandari na mambo mengine ya viwandavitakavyoweza kuimarisha mazao ya kilimo ilikuiongezea thamani na wakulima wakapata maishayaliyo bora. Hivi sasa Watanzania wanatumia asilimia50 ya mapato yao kwa ajili ya chakula kutokana namaisha kuwa magumu, bidhaa zimepanda sana napato la Mtanzania ni dogo, ni kutokana na mfumukowa bei ulivyo ni kwamba hii asilimia 50 itaongezeka,itafika mpaka asilimia 65 au 67 ya mapato ya Tanzaniakwenye chakula. Kwa hapa, utaona hatuwezikuendelea au kuwainua watu wetu kiuchumi kwasababu itakuwa ni watu wanaochumia tumbo tu,hawawezi kupata afya nzuri, nyumba nzuri, elimu nzurihata nguo za kuvaa watakuwa wanaishia kuvaamitumba tu ambayo inasababisha maradhi mengi yangozi, wataalamu wengi wamethibitisha hilo. NaishauriSerikali ya CCM ishirikiane na wataalam walioko katikachama cha CUF wa kiuchumi kuweza kuboreshauchumi wa nchi hii na wachukue wasia niliowapa wasiasa kutumikia uchumi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, twende kidogo katika jambolingine la elimu. Hali ya elimu inatisha, wanafunziwanaofaulu hawajui kusoma na kuandika, tatizo sijui ninini labda leo hapa Serikali itueleze kwa ruksa yako170

kwa nini, kuna tatizo gani Baraza la Mitihani?Wanafunzi wanafaulu hawajui kuandika, wenye uwezowa kufaulu wanafutiwa matokeo, hili ni tatizo. Kwahiyo, naiomba Serikali itueleze tatizo hili litakwisha lini nakumuondosha mtumishi mmoja wa Baraza la Mitihani sidawa kwamba ndiyo umetibu tatizo. Nashauri Barazala Mitihani lifumuliwe, wapangwe wataalamu upyawatakaoweza kuisaidia nchi hii kwenda mbele kielimu.Bila ya elimu na miundombinu iliyo madhubuti nainfrastructure za kiuchumi, hatuwezi kupiga hatua,tutakuwa ni taifa siku zote la kuomba na tunaelekeasasa hivi kuwa Taifa la kusaidia. Tuna mwelekeomkubwa wa kuwa donor country, lakini tukilegea,tukaendeleza mtindo wetu wa uchumi kutumikia siasa,tutakuwa beggar country ila yaumul kiama. NaiombaSerikali ya CCM, naishauri Serikali ya CCM ichukuenasaha ninazowapa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, jambo lingine nataka kulielezahapa ni kuhusu utawala bora. Utawala bora ni jambola muhimu ili kila mtu aweze kupata haki yake.Kumnyima mtu haki yake ni kurudisha nyumamaendeleo ya Taifa. Watu wanakuwa waogakujiendeleza kiuchumi kwa sababu utawala boraunawazuia. Kila mtu akijitahidi kufanya kazi, vipingamizivya utawala bora vinamzuia. Kwa hiyo, utawala borani muhimu kuuimarisha kwa masilahi ya Taifa letu. Mimipamoja na kwamba nipo katika Chama cha Upinzani,Chama cha CUF, lakini ni Mtanzania na nina imani kwaTanzania na najivunia kuwa Mtanzania. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mambo mazuritunayowaeleza, tunawaomba au tunawataka171

myachukue, myafanyie kazi na yale ambayo mnaonahayahitaji kufanyiwa kazi, mtuambie, tushauriane. Nchihii ni nchi nzuri ambayo inatizamwa na wengi kwa jichola ubaya. Tusije tukatumbukia katika shimo la kwambatuko katika kutafuta mali, baada ya kupata mali hiyo,tukasema tugombane kwa kugawana mali hiyo, thentukaiacha mali hiyo bila kuitumia. Iko hadithi mojainasema “The good, the bad and the ugly.”Mheshimiwa Spika, nashauri rasilimali tulizonaotuzifanyie kazi vizuri. Nchi iko katika tense, hali hatari.Tatizo ni kwamba vijana hawana ajira ambao ni zaidiya asilimia 70 ambao wanaishi vijijini na ajira ni kilimo.Kwa hiyo, Serikali iongeze zaidi kwenye kilimo ili ajira zavijana zipatikane, wapate kazi na nchi ipate kusongambele.Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ahsante sana.(Makofi)SPIKA: Amenikumbusha Mheshimiwa Mozakwamba tunaitwa Bunge la Miongozo, sasa kutakuwana Waheshimiwa Miongozo humu humu ndani maanawanajulika Waheshimiwa Miongozo.Ahsante, sasa tuendelee na MheshimiwaAnnaMaryStella Mallac, atafuatiwa na MheshimiwaLolesia Bukwimba na Mheshimiwa Abbas ZuberiMtemvu ajiandae.MHE. ANNAMARYSTELLA J. MALLAC: MheshimiwaSpika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ili na miminiweze kuchangia katika hotuba ya Waziri Mkuu.172

Nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii iliyo adimukatika Bunge letu.Mheshimiwa Spika, pili, napenda kuchukua nafasihii nimshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehemaaliyeniwezesha kunipatia afya na nguvu ya kusimamambele ya Bunge lako Tukufu ili niweze kuwawakilishawananchi wa Tanzania ambao bado wanaendeleakutaabika na kuteseka kwa kukosa huduma bora zakimsingi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sitakuwa nimewatendea hakiwananchi wangu wa Mkoa wa Katavi na Rukwa kwakuunga mkono bejeti hii. Nianzie na suala la elimu.Naongeza mbele ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwaupande wa elimu kwa Mikoa yetu Rukwa na Katavi,kwa kweli ni masikitiko makubwa, bado tuko nyumasana. Napenda sana Serikalli itoe kipaumbele kwaelimu ya msingi, kwa sababu elimu ya msingi ndiyongazi ya mwanzo hata kama mwananchi anajenganyumba, kwanza anazingatia kuimarisha msingi ili kuwana nyumba bora. Kwa hiyo, kabla hatujafika ngazi yasekondari na elimu ya juu, kwanza tuimarishe msingi.Mimi ni mwepesi sana kama kawaida yangu huwanikitoka Bungeni sikai mjini, huwa nazunguka kwanzaVijijini kuangalia Watanzania wenzetu wanaishi katikamazingira yapi, kwa kweli inasikitisha sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nitolee mfano Tarafa yaMpimbwe, shule ya Kata ya Majimoto, nilizungukia kulenilitamani kulia na ilibidi nipige picha na wanafunzi naWalimu kwa kumbukumbu. Shule wanazosoma, ni borashule, bora elimu lakini sio elimu bora. (Makofi)173

Mheshimiwa Spika, wanafunzi hawana madawati,wanakaa chini kwenye vumbi, ile vumbi afadhali kamaingekuwa ni sakafu, wamewekewa simenti lakini nikwenye vumbi. Hatujui usalama wa afya za watotowetu ndani ya sketi na kaptula zao, jamani inasikitishasana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, Tanzania tunakokwendabadala ya kusonga mbele, tunazidi kurudi nyuma.Nawapa pole sana wazazi kwa kuwasomesha watoto,Watanzania wenzangu mnaonisikia, poleni sana wazaziwenzangu. Huduma ya maji wanafunzi hawana, mtotoili afaulu vizuri anatakiwa ale chakula, anywe maji safina salama ili akili ichaji, ifanye kazi, aweze kufuatiliamasomo anayofundishwa lakini shule zetu za msingikule hazina kisima hata kimoja. Mtoto tangu alivyotokanyumbani kwa wazazi wake mpaka anatoka shulehajapata maji. Watoto wanahaha kwenye majumbaya Walimu kutafuta maji, lakini na Walimu nao ndiyomkumbo mmoja wanahangaika kutafuta maji. Kwahiyo, mtoto anasoma katika mazingira magumu,midomo imemkauka, maji hana. Nilijaribu kuongea naWalimu wanasema sasa hatuna jinsi ya kufanya.Nilienda kukagua vyoo vyao, kwa vyoo wamejitahidi,vyoo ni vizuri, lakini kwa kuwa hawana visima vya majiwale watoto wanatumia karatasi au majani, jamani!Miaka hamsini ya uhuru? Tumefanikiwa, tunasongambele, sijui kweli? Tunasonga mbele hivi kweli? Mimikwa kweli nashindwa kuelewa, naomba mnisamehesana, lakini naongea ukweli kwa sababu nimezungukana nimejionea kwa macho. Walimu hawana nyumbaza kuishi, Walimu wanasikitisha, baba anapotoka na174

kikoi chake kwenda kuoga huyo inabidi mamaamfuate na kitenge kwenda kuziba ule uwa wamajani, ndiyo baba aoge, atoke. Anaoga huku jualinammulika, ndege wanamchungulia, jamani!(Makofi/Kicheko)Mheshimiwa Spika, kwa kweli tunakokwenda nikugumu sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu boresha Mkoawetu Baba na nina imani unaweza kwa sababu suraya Mji, nikiona pale Mjini, kweli sura imegeuka, Mjiunaleta raha kiasi kwamba tukiendelea namna hiyobado uko madarakani, tutakuwa ulaya. (Kicheko)Mheshimiwa Spika, Shule ya Mwese, hiyo ni Tarafanyingine, sasa hapo nimetoka kwenye Jimbo la WaziriMkuu, naenda Tarafa ya Mwese, shule la Mweseambayo mimi nilisoma wakati baba yangu akiwaMwalimu Mkuu pale. Nimesoma miaka ya sabini nalakini shule ile nilivyoitembelea, nimeikuta kamanilivyoiacha. Nikaingia na nyumba tuliyokuwa tunaishi,kama nilivyoiacha nikiwa shule ya msingi haijafanyiwamatengenezo wala ukarabati wowote. Watotowanakaa chini, simenti zote zilishachimbuka, kutazimepasuka hovyo kiasi kwamba ni hatari kwa maishaya watoto wetu. Jamani tunakokwenda ni wapi? Miminashindwa kuelewa, sijui hili jibu atanijibu nani? Vyoovimefurika, vimetapika, madawati hamna, Walimuwenyewe wanakalia kwenye madawati eti ndiyo vitivya Walimu ofisini, jamani! Kwa kweli hiki ni kitendo chaaibu. Mishahara yao haifiki kwa wakati, hawana usafiriwa kutosha wanapofuata mishahara yao Mjiniambapo ni maili 70, wanahangaika kudandia mabasi175

kama ni masika barabara zetu zenyewe miundombinumibovu, kwa kweli ni shida tupu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba kwa kweli, Wizarazitakapoanza kutenga pesa, mimi naona tatizo likokwenye ukaguzi. Naomba Wakaguzi wa elimu wapewekipaumbele sana kwa sababu hawa Wakaguzi waelimu wangepewa kipaumbele, wakapewa magari yakusafiria, wangezikagua zile shule zetu nazikaboreshwa. Nikiangalia Wakaguzi wana nia yakufanya kazi, lakini unakuta wanategemea gari mojawanyang’anyane na Mkurugenzi na Mkurugenziakijifanya ni Mungu mtu akipandisha mabegi juu basiyule Mkaguzi hawezi kupata nafasi ya kwendakukagua shule. Naomba kwa kweli Wakaguzi wa elimuwapewe kipaumbele, wakague shule zetu, watoetaarifa na mara moja shule zile zipewe kipaumbelekufanyiwa ukarabati, watoto wetu wapate madawatiwasipate magonjwa ya minyoo kwa kupitia sehemu zasiri wanavyokaa kwenye vumbi. Jamani! Inasikitishakweli. Walimu wetu mimi nikiwatembelea naona hataaibu kuwaangalia usoni. Nilitamani kulia walivyokuwawakinilalamikia lakini sina jinsi, nitawasaidia nini? NdiyoSerikali yetu hiyo ya Chama cha Mapinduzi, miakahamsini ya uhuru, tumefanikiwa, tumesonga mbele natutazidi kusonga mbele. Ahsanteni sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nakuja kwenye suala la maji.Maji ni kilio kitupu hasa vijijini. Japokuwa na mjini kunashida sana, tunategemea tanki lenye ujazo wa 100,000yale maji hayatoshi kusambaza mji mzima. Watu wakolaki, hebu ngoja, maana niende na takwimu.176

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Mpanda wako680,000 lakini lile tanki lenye ujazo wa lita 100,linatosheleza kwa watu 41,000 tu...(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)MHE. ANNAMARYSTELLA J. MALLAC:wote wanahaha juani kutafuta maji...WengineSPIKA: Ahsante, hiyo ni kengele ya pili.MHE. ANNAMARYSTELLA J. MALLAC: MheshimiwaSpika, kengele ya pili! Lakini naomba Serikali jamaniiwajali walimu, ituletee maji vijijini. Ahsanteni sana.(Makofi)MHE. LOLESIA J. M. BUKWIMBA: Mheshimiwa Spika,nichukue nafasi hii kukushukuru sana kwa kunipa nafasiya kuchangia jioni ya leo. Lakini pia nichukue nafasi hiikuishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kazi nzuri yakuwasilisha bajeti hii. Kwa sababu, ndani ya bajeti kwakweli, kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Busanda,niseme, umetupendelea sana kwa sababu,imezungumzia kuanzishwa kwa kituo chakuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini,Rwamgasa, lakini vile vile umetupa Mamlaka ya MjiMdogo wa Geita. Hii yote nina uhakika kabisakwamba, unasogeza huduma kwa wananchi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa suala la nishati na madini,nikianzia na nishati, kwa niaba ya wananchi wa Jimbola Busanda, nichukue nafasi hii kuishukuru Serikali kwa177

jinsi ambavyo imetuhudumia wananchi wa Busanda.Sasa hivi nguzo zimewekwa na nyaya katika Kata yaBukoli, Rwamgasa, Nyarugusu na mpaka Katoro sasawanaweka nguzo. Lakini vile vile katika Tarafa yaButundwe, wameweka katika Kijiji cha Bukondo,Chikobe, Chigunga, kwa kweli, sisi wenyewetunajivunia Serikali yetu. Nina uhakika kwamba,wananchi watanufaika na umeme huu. Lakini niombetu kwamba, Serikali inieleze, ni lini utawaka umeme huuili na wananchi wasikie, waanze kujiandaa kwa ajili yauwekezaji. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa habari ya madini. Kwasababu, kinaanzishwa Kituo cha Uwekezaji chakuwasaidia wachimbaji wadogo pale Rwamgasa,niiombe sasa Serikali, iwawezeshe wachimbaji hawakwa kuwapa maeneo ya uchimbaji. Katika Sera yaMadini ya mwaka 2010, imezungumza wazi kabisakwamba, Serikali itawapa maeneo ya kuchimbawachimbaji wadogo na kuwawezesha pia. Naonatayari Serikali imeshaanza hatua kwa kuanzishamaeneo kwa ajili ya kuwawezesha, lakini niombe sasakwa ajili ya wananchi wa Nyarugusu, badohawajapata maeneo ya kuchimba.Mheshimiwa Spika, vile vile na pale Nyaruyeye,mwaka huu tunashukuru kwamba, kulitokea brush,gold brush na wananchi wanachimba kidogo kidogo.Lakini niombe sasa wananchi wa pale Nyaruyeyewapate maeneo ya kuchimba kwa sababuwanapowezeshwa nina uhakika kabisa kwamba,tutaweza kufikia malengo ya milenia kwa sababu,Jimbo la Busanda, tunategemea madini na Geita kwa178

ujumla inaongeza kipato kupitia madini. Kwa hiyo,niiombe kabisa Serikali, iwape maeneo ya uchimbaji ilikuwawezesha wananchi hawa kufaidika na rasilimalituliyonayo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa upande wa elimu. Ninayochangamoto kubwa katika shule za sekondari 16 katikaJimbo la Busanda. Hizi sekondari kwa kweli zinaupungufu wa nyumba za walimu. Walimuwanahangaika sana. Niiombe Serikali kwa sababusuala la umeme sasa inalishughulikia, niombe pia hatanyumba za walimu wa Sekondari iweze kuzishughulikia.(Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini vile vile mazingira siomazuri sana kwa watoto wetu, hasa wa kike ambaomara nyingi wanapata mimba kwa kwenda shule zambali. Kwa hiyo, niombe pia Serikali iangalieuwezekano wa kuanzisha hostel kwa watoto wetu iliwaweze kufanya vizuri katika masomo yao. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, pia hatunaChuo cha VETA katika Wilaya na Mkoa wa Geita. Kwahiyo, Serikali pia ianzishe VETA; hatuna chuo kabisajapokuwa tuna shule nyingi za Sekondari, lakini Serikalikwa kweli, ituwezeshe basi na sisi tuwe na Chuo chaVETA ili watoto wetu wanaomaliza kidato cha IV,wapate nafasi ya kuweza kupata ujuzi. Hivi tunapataumeme sasa, wawe na ujuzi wa kuweza kufanya kazizao vizuri kwa sababu watakuwa na ujuzi kabisa.(Makofi)179

Mheshimiwa Spika, niseme kwamba, pia katikaupande wa elimu ya shule za msingi, tunao WaratibuElimu. Waratibu hawa wanahitaji usafiri, wapewepikipiki pamoja na posho za kuwawezesha, ili wawezekufanya kazi zao vizuri. Unakuta Mratibu wa Elimu,anahudumia shule za msingi nne au tano, hana usafiri.Kwa hiyo, niombe sasa Serikali iangalie hata namna yakuwakopesha ili waweze kufanya kazi zao vizuri naelimu ya shule za msingi iweze kuboreshwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, vile vile katika Jimbo laBusanda na Geita kwa ujumla, tunategemea kilimo.Kwa vile, Jimbo limegusa katika Ziwa Viktoria, nilikuwanaomba kwamba, tuanzishiwe basi skimu zaumwagiliaji hasa katika Vijiji vya Bukondo pamoja nakule Kasamwa, kwa kweli, wanajishughulisha nashughuli za kilimo. Kwa hiyo, tukianzishiwa skimu zaumwagiliaji, nina uhakika kabisa kwamba, suala la njaalitakuwa ni historia. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini vile vile kwa upande wakilimo. Tunashukuru kwa ajili ya ruzuku ambazozinatolewa kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo. Pianiombe kwa upande wa mifugo, Serikali iangalienamna ya kuwasaidia wafugaji. Kwa sababu, wakowafugaji ambao wanahangaika sana hasa hasa kwachanjo ambazo wanalipia hela nyingi sana. NinaombaSerikali iangalie namna ya kuboresha suala la chanjo.(Makofi)Mheshimiwa Spika, vile vile kwa upande wa afya.Waziri Mkuu, aliniahidi gari la wagonjwa, Kituo cha AfyaChikobe. Naomba sasa Serikali, ilete gari hili, ili180

wananchi waweze kufurahia huduma na Tarafa nzimaya Butundwe waweze kutumia gari hili la wagonjwa.Kwa sababu, Kituo hiki kiko mbali na wananchi wakombali, takribani kilometa 50 kutoka katika Hospitali yaWilaya ya Geita, kwa hiyo, wanahitaji gari ili wawezekupata huduma, hasa hasa akinamama wajawazitoambao wanahitaji huduma ili tuweze kupunguza vifovya akina mama ambao ni wajawazito. (Makofi)Mheshimiwa Spika, labda tu nisahihishe kidogokwamba, tunashukuru kwa Halmashauri ya Mji Mdogowa Geita. Pia suala la ulinzi na usalama kidogolimekuwa ni tete katika Jimbo la Busanda, hasa hasakatika Vijiji vya Katoro, mara nyingi kunatokea matukioya ujambazi. Lakini vile vile Kasamwa na Bukondo,kumetokea matukio ya ujambazi. Kwa hiyo, nitumienafasi hii kuiomba Serikali iangalie uwezekano wakuweka ulinzi katika maeneo hayo ili wananchiwaweze kuishi kwa amani na furaha na kuendelea nashughuli zao za kawaida. (Makofi)Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba, Mji waKatoro ni mahali ambapo ni mji mkubwa ambao unashughuli nyingi sana za kiuchumi. Kwa hiyo, unahitajikaulinzi wa kutosha ili wananchi waweze kufanya kazi zaovizuri. Hata ikiwezekana Serikali iangalie namna yauwezekano wa kutengeneza hiyo centre ya kibiasharakwa sehemu za Kanda ya Ziwa kwa sababu, kwa kweli,ni sehemu ambapo kuna biashara nzuri sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, niombetu kwamba, kwa sababu Serikali inaendelea kufanyamambo mazuri hasa katika Jimbo langu, hasa kwa181

kero mbalimbali ambazo zimekuwepo kwa mudamrefu, imeendelea kuzishughulikia na sasa nina imanikabisa kwamba, itaendelea kushughulikia sualaambalo nimelizungumzia, upungufu wa nyumba zawalimu na pia itaendelea kuweka hizo skimu zaumwagiliaji kwa ajili ya wananchi wangu. Lakini vile vileitaleta gari la wagonjwa Chikobe. Lakini sambamba nahilo, itahakikisha ulinzi na usalama katika Jimbo laBusanda kwa ujumla na Geita yote. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache niombekwamba, kwa pale Katoro Serikali iwekeze kwasababu, ni centre kubwa ambayo, nina imani kabisatukiwekeza nina uhakika tutafanikiwa. Kwa vile naumeme unakuja sasa, niiombe Serikali iwekeze, lakinipia hata wananchi wawekeze. Wawekeze mashine zakusaga, za kukoboa mpunga pamoja na shughulimbalimbali ili kuweza kutengeneza ajira kwa ajili yavijana wetu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru sanakwa nafasi hii, nikiamini kwamba, wananchi waBusanda wanaendelea kunipa ushirikiano mkubwa.Pia nawashukuru sana kwa ushirikiano ambaowanaendelea kunipa mpaka sasa na niseme kwamba,nitaendelea kufuatilia kero moja hadi nyingine kwakadri ambavyo itakavyokuwa na Serikali inaendeleakunisikiliza na naamini itaweza kushughulikia kero mojahadi nyingine. (Makofi)Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru sanakwa muda huu ambao umenipa. Naunga mkono hoja182

ya Waziri Mkuu, nikiamini kwamba, kwa kupitisha bajetihii, mambo yatakwenda vizuri zaidi. (Makofi)MHE. ABBAS Z. MTEMVU: Mheshimiwa Spika,kwanza nikushukuru kwa kunipa nafasi hii, lakininaomba niseme taratibu sana kwa sababu, kichwachangu, naona kama hakiko sawasawa.Mheshimiwa Spika, lipo jambo nisipolisemanitakuwa sikutenda haki. Tarehe 18 Aprili, saa 12.00asubuhi, nilipata ajali mbaya sana pale Milima yaGairo. Namshukuru sana Naibu Spika, saa 3.00 alitoataarifa, nikapata simu kutoka sehemu mbalimbali. Pianiwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge watatu,madada zangu ma-Sharif wanaitwa, hawawanajielewa, kwa sababu, wengine walikuwa nyumayangu, wengine walikuwa mbele. Nilipopinduka maratatu, nikaingia kwenye mtaro chini juu na nina uhakikazingezidi dakika 30 kwa sababu, hali ya hewa kule chiniilikuwa mbaya, ningeweza kupoteza maisha. Lakiniwalikuja, wakaita watu, wakaniokoa. Nawashukurusana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, pia nimshukuru sana RC waMorogoro, kaka yangu Joel Bendera na RAS waMorogoro, kwa jitihada zao na Madaktari waMorogoro na RAS wa Dar-es-Salaam kwa mapenzimakubwa. Vile vile niwashukuru Dokta Mareale waMuhimbili na Dokta Mlawa, kwa mapenzi makubwasana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, niwashukuru sana sanawananchi wa Temeke, walikuwa wamejazana183

nyumbani; nilikimbia Hospitali, ikabidi nije nyumbani.Nawashukuru sana kwa mapenzi na dua zao, piawananchi wote wa Dar-es-Salaam, Wabungewenzangu wote wa Dar-es-Salaam, mke wangu nawatoto wangu na hasa Tamia wa miaka nane alikuwaakinitazama na kuniita baba. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sidhani leo kama nina manenomengi. Kwanza niseme mapema kwamba, siiungimkono bajeti hii na sababu za msingi, ninazo.Mheshimiwa Spika, tarehe 16/8/2011 tukiwa hapahapa ndani, Kitabu cha Hansard ninacho hapa, Dares-Salaamtuliongea matatizo yetu yote kwa ujumla,lakini ikatoka kauli hapa ndani kwamba, Wabunge waDar-es-Salaam, matatizo yenu tutakwendakuzungumza kwa pamoja; kauli hiyo aliitoa Waziri Mkuu.Sisi tukaiamini kauli ya Waziri Mkuu wetu, lakinichakusikitisha tumefuatilia, tumesema, hatukupatanafasi ya kuzungumza naye. Sasa tunajaribukujiangalia kweli, iko haja ya sisi kuendelea kuwaWabunge wa Dar-es-Salaam? (Makofi)Mheshimiwa Spika, kama 85% ya mapato ya nchihii yanatoka Dar-es-Salaam, lakini Wabunge wa Dar-es-Salaam hatupewi uzito, tunadharauliwa. Inasikitishasana. Tuna masuala ya msingi pale Kurasini, wananchiwale wanapata shida toka 2005. Tunataka kupanuaBandari, tumechukua eneo lao, lakini kuwalipa fidiatunashindwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, niseme ukweli, pale wanunuziwapo wengi wanapalilia Kurasini. Isipotoka kauli hapa184

ya kwenda kuwalipa wananchi wale, nikirudi nitatafutawanunuzi, tunauza yale maeneo. Liwalo na liwe kwasababu, zile ni nyumba zao na haki ni zao. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kaongea Ndugulile, KigamboniNew City, watu wanateseka. Wakati tunaomba ridhaakwa wananchi, tulisema tutasimamia maisha bora nakila kinachomhusu mwananchi. Sasa matokeo yakeyamekuwa sivyo.Mheshimiwa Spika, lakini wewe ni shahidi na nyoteni mashahidi, pamoja na kwamba tunapoongelea Dares-Salaamhapa, wengi hatukubali kuunga mkono,lakini wengi wetu tunaishi Dar-es-Salaam. Hali ya Dares-Salaamya msongamano inatisha. Sisi Wabungetuliopita, tulikuwa na mpango wa fly over na JAICAalifanya feasibility study, kila kitu kilifanyika. WenzetuKenya, walikuja nyuma, sasa hivi wana fly over. Lakinisisi sijui ni dharau, sijui ule mji unaonekana chuma ulete,hata haifahamiki. Hadi leo Dar-es-Salaam inasikitisha,hatujui sababu yake ni nini? Msongamano kupita kiasi.Inawezekana mliuona zamani msongamano, lakinisasa hivi kwa kuwa mnapelekwa na mapikipiki namagari, hamuuoni msongamano. Lakini hali inatisha.(Makofi)Mheshimiwa Spika, yako mambo ya NationalHousing. Nampongeza sana DG wa National Housingni rafiki yangu, timu yake inafanya kazi nzuri,naipongeza sana. Lakini yako mambo tuliongea ndaniya Bunge hili kuhusu nyumba za National Housing, zileza maghorofa ziuzwe kama apartment. Rais, akiwaIringa nakumbuka na mimi nikiwa Mbunge, ilikubalika.185

Lakini cha kusikitisha na cha aibu, leo National Housing,nyumba zile zile, ukienda Mchikichini, ukiendaChang’ombe, ukienda Ubungo, National Housingwamekwenda wamejenga mbele ya nyumba zile zazamani katika maeneo yale ambayo yalikuwa openspace ya kupitisha fire. Halafu wana tangazo lao mojawanaonesha mtu anakimbiza kuku eti, kuna mabandaya kuku, kuonesha kwamba, wao sasa ndio wamezuia.(Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini nyumba hiziwanazojenga watu wameshanunua, lakini zile ambazotulikubaliana, iko hapa Naibu Waziri akizungumza nayeye. Naibu Waziri, alizungumza hapa kwamba,atakutana na Wabunge wa Dar-es-Salaam,kuzungumzia namna ya kuuza nyumba zile. Lakini liletuliloazimia kwenye Bunge hili, halikuwa kwa Wabungewa Dar-es-Salaam tu, zilikuwa nyumba zote za NationalHousing za nchi nzima; wauziwe watu wanaokaa katikanyumba zile, lakini mpaka leo halijafanyika. Natumainikatika Bunge hili, tutaambiwa utekelezaji wa suala hilo.(Makofi)Mheshimiwa Spika, Temeke kwenye Manispaayangu kulikuwa na ubadhirifu. Namshukuru Waziri,dada yangu mama Ghasia, akatengeneza Tume.Tume ile ikafanya kazi nzuri, imeleta taarifa. Walewabadhirifu mpaka leo bado wako pale ofisini. Sasamimi niwaulize, hivi tukishafanya hiyo kazi kinafuatianini? Au mnatutaka Wabunge, tufanye kazi hiyo sasa?Kwa sababu, majina tunayo, mkituruhusu, nikimalizaBunge, nitakwenda mmoja mmoja namtoa Ofisini,wala sishindwi. Kwa sababu, hayo ni majukumu yenu,186

kama hamfanyi ninyi mnatuachia sisi, sisi tutafanya.(Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini liko jambo lingine ambalosijui ni kwa nini lilifanyika? Jiji la Dar-es-Salaam lilifutwa2010 na sisi tukiwa Wabunge, bila kushirikishwa. Kwahiyo, tumefanya uchaguzi ule wa Meya, ni batili.Mikataba tuliyoingia ni batili. Nasikia Jiji limerudishwa2012. Sasa mimi nauliza, lilifutwa kwa nini? Kwa ninimsituulize? Sisi ndio Wabunge, sisi ndio wawakilishi wawatu wa Dar-es-Salaam, mngetuuliza, mmefuta, sawa,mngetuuliza sisi tungesema sawa, acheni Manispaatatu, lakini mmelirejesha; sasa mtujibu hapa, wakatimmefuta mpaka mmerejesha, ile Mikataba na mamboyote yaliyofanyika, tunahesabu yakoje? Yako sahihi auhayako sahihi? Ni lazima twende kwa utaratibu wakueleweka. (Makofi)Mheshimiwa Spika, utaratibu wa Ring Road.Tulianza utaratibu mzuri pale Dar-es-Salaam,nakumbuka. Waziri Kawambwa, akiwa Waziri waMiundombinu, tulikutana naye hapa, tukiomba bilionitisa, tukapewa bilioni 20 tukaweka mpango mzurikabisa wa kuondoa msongamano, wakati ule RCakiwa Mzee Kandoro, TANROAD manager akiwaNyakabazi ambaye sasa hivi kahamishiwa Mbeya.Tulikuwa tunakwenda vizuri, sisi tunaomba tuendeleena utaratibu wetu ule, hatupendi utaratibu wa mtukupanda juu ya jukwaa akatuambia anatupadaladala 25 kama hisani, tungependa twende nautaratibu ule ule ambao tulikuwa tunakwenda nao.Yule meneja wa TANROAD mtu mzuri sana, mkeweyuko hapa Mbunge, lakini tumeshangaa kaondolewa187

kapelekwa Mbeya wakati alikuwa anatufanyia kazinzuri ya kuondoa msongamano Dar es Salaam.Mheshimiwa Spika, nakushukuru, lakini siungimkono mpaka nipate majibu haya. (Makofi)MHE. KISYERI W. CHAMBIRI: Mheshimiwa Spika,nianze kwa kukushukuru kwa kunipa nafasi ili niwezekuchangia katika hoja hii ya Waziri Mkuu na nashukurukabisa kwamba, hoja hii leo nimeipata wakatimwafaka.Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati tukiwa hapaBungeni, Wapinzani wetu wa Viti Maalum wako hukoBabati na wanatangaza kwamba mnaelewa Mbungewenu hayupo ndani ya Bunge wala haonekanipopote. Sasa kwa kuniruhusu nichangie, naamini sasawananchi wa Babati wananiona nawakilisha tenanawawakilisha vizuri kabisa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, awali ya yote nianze kusemakwamba naunga mkono hoja. Bunge hili la mwishonilikuwa natoka Arusha na basi la Mtei, tulipofika paleMinjingu kuna kijana wa miaka kama 23 wakati ulendiyo tunafanya sherehe zile za miaka 50 akasemakwamba CCM miaka 50 haijafanya chochote,nikamuuliza kijana yule wewe una umri ganiakaniambia nina miaka 23, nikanyamaza. Baada yadakika 45 tukawa tuko Babati Mjini, kabla ya ilebarabara ya lami haijatengenezwa tulikuwatunatembea masaa manne kutoka Minjingu mpakaBabati Mjini. (Makofi)188

Sasa nikauliza yule kijana kwamba bado unafikiriCCM haijafanya chochote, yaani imeongeza maishayako kwa masaa matatu. Sasa matatizo makubwatuliyonayo ndani ya Kambi yetu ya Upinzani nafikiri niumri mdogo. (Makofi)Wawakilishi wanaochaguliwa kuja ndani ya Bungehili wana miaka 20, 25 mkubwa sana 30, hawaelewinchi yetu hii huko nyuma ilikuwa namna gani.Wangeelewa nchi yetu hii ilikuwa namna gani hizi kauliza kusema kwamba hakuna kilichofanywawangezizima kabisa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, iko hadithi moja, Mzee mmojaalikosana na mke wake, kwa hiyo akaamua amfukuze.Wakaenda kwenye kesi akashinda, lakini mzee mmojawa hekima akamwuliza yule kijana kwamba miakayote 20 uliyokaa na mke wako hajakutendea jambohata moja jema, yule kijana akafikiri sana mwishoweakasema mama huyu kwa kulima ni hodari sana.(Makofi/Kicheko)Mheshimiwa Spika, kwa hiyo yule mzee wa hekimaakamwambia sababu mama huyu ni hodari sana kwakulima, basi kwa jambo hilo moja zuri mchukuemwendelee kuishi naye. Sasa hawa siku zotewanapinga tu kweli miaka 50 hakuna hata moja zuriambalo CCM wameona imefanya ? (Makofi)Mheshimiwa Spika, niipongeze Serikali sana…MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, taarifa.189

SPIKA: Naomba tumuachie mtu afanye kazianasema mambo yake, taarifa inatoka wapi.Mheshimiwa Chambiri, naomba uendelee kuchangia.MHE. KISYERI W. CHAMBIRI: Mheshimiwa Spika,niipongeze Serikali sana sababu Mji wa Babati nimakutano ya barabara na sasa barabara zetu karibuzote zina lami, Minjingu-Singida saa hizi tuna lamimpaka Bonga na naelewa inaendelea itafikaDodoma. Lakini kizuri zaidi wameanza kutujengeabarabara kwa Awamu kwenda Galapo, wanatuwekealami, nawapongeza sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sasa nimkumbusheMheshimiwa Waziri Mkuu kwamba wakati Rais alipokujakatika kampeni pale Babati Mjini alituahidi kwambaatatupa kilomita mbili za barabara ya lami. Sasainakwisha miaka miwili hata harufu yake hatujasikia.Nataka sasa katika Bunge hili nielezwe kwamba hiibarabara ya lami ambayo tuliahidiwa itajengwa lini ?Maana muda unakwenda haraka isije kwisha miakamitano hii barabara haijajengwa. Nataka atuelezekwamba hii barabara itajengwa lini.Mheshimiwa Spika, jambo lingine nataka ielewekekabisa kwamba kabla hii mikoa mitatu haijatangazwasisi ndiyo tulikuwa mkoa kitinda mimba, Mji wetu ulitokakuwa Kijiji na kuwa Mji Mkuu wa Mkoa na Halmashauribila kupitia zile taratibu za kawaida za kukua Mji. Kwahiyo, hatuna miundombinu kabisa ndani ya mji wetu.Tutaleta maombi toka Babati kwamba tupate fedha zaziada kuweza kuboresha miundombinu yetu ndani yamji.190

Mheshimiwa Spika, sasa niingie kwenye ardhi.Kampuni ya Tanzania Breweries ilikuwa na shambaambalo ni zaidi ya heka 3,000 katika maeneo ya Kataya Babati Mjini, katika Kijiji cha Singu, wakati huo hiikampuni ilikuwa ni ya Serikali. Kwa hiyo, ile ardhi ilikuwayetu sababu shirika lilikuwa Shirika la Umma. Ile ardhi ilihao Breweries wapewe ilitoka kwa wananchi. SasaBreweries limekuwa shirika binafsi, naamini kwambahisa nyingi si za Watanzania, lakini hawa Breweries japosi shirika tena la Serikali wamechukua ile ardhiwamemuuzia mtu bila sisi wenye ardhi kupewa nafasiya kwanza ya kununua au kuulizwa kwamba tutaihitajiile ardhi.Mheshimiwa Spika, sasa ombi langu ni kwamba,sababu hiyo ardhi ina eneo kubwa ndani ya mji wetuna tunapanga mji wetu. Sasa tuwakilishe ombimaalum na tunawakilisha ombi maalum kwa ofisi yaWaziri Mkuu kusudi hiyo hati miliki ifutwe, tuwezekutumia hilo shamba kwa kupanga mji wetu na kwamatumizi ya wananchi katika Kijiji cha Sigino na katikaKata ya Singu.Mheshimiwa Spika, niendelee kuwapongezawananchi wa Babati Mjini katika hotuba ya Upinzani,Kiongozi wa Kambi ya Upinzani alisema kwamba,kumeanza kujitokeza ukabila, lakini nawapongezawananchi wa Babati Mjini sababu hilo tatizo hawana.(Makofi)Mheshimiwa Spika, wa vijijini hawana na wa mjinipia hawana, inaonekana hayo matatizo yako katika191

maeneo mengine, lakini wamefanya kazi nzuriwametuchagua sisi Wabunge, nawashukuru sana wamjini nawahakikishia kabisa kwamba, nitawatumikiakwa moyo mmoja kama ninavyowatumikia.Nitawafanyia kazi nzuri na nitatumia uwezo wanguwote kuendelea kuwatumikia kwa manufaa ya BabatiMjini, kwa manufaa ya nchi yetu na kwa manufaa yaChama chetu cha Mapinduzi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, niendelee kukushukuru sanakwamba siku ya leo umenipa nafasi ya kuchangiawakati muafaka, nimeondoa mzizi wa fitina kwa yulealiyekuwa ananitangaza kwamba siko huko na sasawamenisikia nimewaongelea, nawatetea na tupopamoja, ahsante sana. (Makofi)MBUNGE FULANI: Kuhusu utaratibu.SPIKA: Kanuni gani? Nyie ndiyo mnafanya hivyokila siku, ninyi wawili ndiyo akina Mr. Utaratibu. (Makofi)Utaratibu kifungu gani cha utaratibu.MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika,nasimama kuomba Mwongozo wako kwa mujibu wakanuni 64(g), naomba ninukuu kwa ridhaa yako: “Bilaya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katibayanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo namajadiliano katika Bunge, Mbunge, fasili ya (g)hatatumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha watuwengine.” Mwisho wa kunukuu.192

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge ambayeamemaliza kuchangia ametudhalilisha Wabungevijana wote wa Kambi ya Upinzani ambao tuko ndani,lakini siyo Wabunge tu kwamba wa Upinzani vijana ilani pamoja na Wabunge vijana wa Chama chaMapinduzi, kwamba hatujui kufikiri sawasawa nakwamba hatujui lolote ndiyo maana tunachangiachangia tu hovyo hovyo. Maneno haya ni yaudhalilishaji namwomba kwa busara MheshimiwaMbunge ayaondoe maneno haya ya kuzungumziakwamba Wabunge vijana hatujui lolote na namtakaakumbuke tunaweza kuwa tunafanya mambo mengitu kuliko wazee wa umri wao mkubwa japokuwakwamba umri wetu ni mdogo.SPIKA: Sikiliza Mheshimiwa, utaratibu sasa ni upiuliovunjwa. Maana yake kuhusu utaratibu maana yakelazima useme utaratibu upi uliovunjwa, maanaunanihutubia sasa, sijui sasa hata utaratibu ni upi?MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika,nimeomba Mwongozo wako, nimesimama kuombaMwongozo…SPIKA: Umesema kuhusu utaratibu.MHE. MOSES J. MACHALI: Hapana, nilisemaMwongozo Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie. Kwahiyo, humu ndani tumekuja wote ni kwa mujibu waKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa umriwetu. (Makofi)193

Mheshimiwa Spika, kwa sababu umri wa kuwaMbunge ni umri wa kuanzia miaka 21 kwa mujibu waKatiba. Sasa Mbunge anapozungumza kitu ambachoanajua fika tuko hapa kwa mujibu wa sheria nikutudhalilisha na inawezekana tutaanza kuhoji pengineuelewa wake na hawatendei haki kwa kweli wananchiwake waliomchagua. Kwa hiyo, tunamwomba afutekauli yake kwa sababu maneno aliyoyatumia siyomazuri, tuko vijana wengi humu ndani wa Upinzani nawasiokuwa Wapinzani. Lakini pia vilevile hata vijanawengine ambao wako mtaani amewadhalilisha sana…SPIKA: Punguza Mwongozo usihutubie watu, youcan take ten minutes kwa ajili ya mwongozo tu.Maneno uliyo-quote itabidi niyaone kwanza kwenyehansard kama ni sahihi. Nitaona kwenye hansard yakwako na kwenye hansard ya Chambiri nitayaona.Tunaendelea Mheshimiwa Batenga, nilikuita, hayupo!Anayefuata Mheshimiwa Yahya Kassim Issa naMheshimiwa Philipa Mturano ajiandae.MHE. YAHAYA KASSIM ISSA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwanza nasemanaunga mkono hoja hii. Sababu ya kuunga mkonohoja hii ninayo; kwa sababu walioleta hoja hii niwanadamu na hakuna mwanadamu aliyekamilika.Nakuja hapa ina maana kwamba, la mmoja haliwezikukamilika kwa hiyo tuchanganye mawazo. Ndiyomaana nasema naunga mkono hoja mia juu ya mia.(Makofi)194

Mheshimiwa Spika, nitachangia mambo matatu,Muungano, Vituo vya Polisi Idunga, Chakwa na kuhususheria dhidi ya wapiganaji wetu Polisi.Mheshimiwa Spika, kwanza tutarudi nyuma,napenda kunukuu baadhi ya hotuba ya Waziri Mkuuya 2008, maelezo yake yanasema kwamba: “Kuratibumgawanyo wa mapato na pande zote mbili zaMuungano. Kufanya utafiti wa mambo ya Muunganona ya siyo ya Muungano kwa lengo la kudumishaMuungano. Pia akasema ili kufuatilia utekelezaji wamakubaliano hayo kwa karibu zaidi vikao vya pamojavitafanyika kila baada ya miezi miwili chini ya Uenyekitiwa Makamu wa Rais.” Mwisho wa kunukuu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hali kadhalika 2011/2012,anasema kwamba: “Serikali itaendelea kuratibu vikaovya Kamati ya pamoja na Serikali ya Muungano waTanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarkushughulikia masuala ya Muungano.” Mwisho wakunukuu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, katika kitabu chetu hiki chamwaka huu, juu ya hayo yote aliyozungumza lakinianasema kwamba katika hoja 13 zimewezakurekebishwa mbili. Nachukulia kama asilimia 15 naasilimia 15 natumai hata mtoto akiwa darasa lakwanza, huwezi kumpeleka la pili, kwa uzoefu nilionao.Kwa hiyo, inaonesha wazi kwamba utendaji kwa kwelihaukidhi na kama vikao vinafanyika kila mara haviletitija inadhihirisha wazi kwamba mafanikio hayawezikupatikana. Katika mambo mawili hayainishi kwambayameleta uzito hususan kwa Zanzibar. Matatizo ya195

Zanzibar yanaeleweka na yale yaliyokuwa muhimukabisa hatuwezi kusema Constituency DevelopmentCatalyst Fund kwamba ni tatizo ambalo tumeliondoahaiingii akilini.Mheshimiwa Spika, tunaelewa wazi kwamba kunamambo ambayo hayo yanatuathiri kamatunavyosema yanayohusu mapato. Hivi juzi katikaKamati, ziko fedha kama bilioni 155 lakini kwa ile hasaraya 4.5 Zanzibar walipata asilimia nane, eight billions,hali hii tusitegemee kwamba Wazanzibar watawezakuleta maendeleo au kupata maendeleo na hayandiyo mambo ambayo yanaleta matatizo katikaMuungano.Mheshimiwa Spika, tunajua wananchi wetuwanapata matatizo katika kodi, unaondoa jambolako au biashara yako kutoka Zanzibar ukifika bandarinipana matatizo na siku zote mnasema kwambatunarekebisha, matatizo tutayaondoa lakini nasematusiwe wasanii. Tusiwe wasanii juu ya mambo mazitokama haya, lazima tuwe wakweli, tunasema kwamba,tumeweka viongozi ili watekeleze majukumu yawananchi ndiyo maana yake, lakini nadhihirisha wazikwamba suala hili limepuuzwa. Niko katika Bunge hilikwa miaka 17, suala hili linapigiwa kelele mpaka leohakuna kinachokwenda. Hili ni tatizo kubwa sana,ambalo halileti maana hata kidogo. Kwa hiyo,tunaomba hizi ghasia zimalizike na nasema Serikali kwaupande mwingine inachangia. (Makofi)Mheshimiwa Spika, Serikali kwa upande mwingineinachangia matatizo ya wananchi, hakuna Mzanzibar196

aliyekuwa hataki Muungano, hakuna na anayesemakwamba labda Mzanzibar hataki Muungano, ndiyowale walioondoka Zanzibar 1964 labda wakaendaDubai. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sasa labda wanatafuta njia yakurejea, njia ipi wapite, mkono upi watumie ili wawezekurejea, lakini hakuna mzawa wa Zanzibar hasa halisiaweze kusema kwamba hataki Muungano si kweli.(Makofi)Kwa hivyo ombi letu, yafanyike marekebishokatika matatizo ambayo yanawakabili wananchi,maana mimi hapa nasema kwa ajili ya Zanzibar,wenzetu sijakusikieni nyie mkatoa sauti ya aina yoyotekama nilikuwa na kijana mmoja wakati ule Waziri Mkuu,unamwambia hivi anaigiliza vizuri kabisa lakinihatekelezi hata moja. Kwa hivyo, inaonyesha ndiyopicha hii mnayotupa wenzetu kimyaa! (Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini huwezi kupata ufumbuziyou don’t know where is our reluctance, naendelea.Mheshimiwa Spika, nakuja kuhusu Vituo vya Polisi.Katika Jimbo langu nina vituo viwili Chakwa na Dungamitini. Kituo cha Dunga Mitini wakati wowote kinawezakuanguka na kuua. Kituo ni kibovu sana na suala hilinapiga kelele kila mara lakini hakuna hatuazinazochukuliwa. Aliwahi kuja Naibu Waziri wakati uleMheshimiwa Kagasheki alikuja na tukamtembezasehemu zote na akaona hali halisi ilivyo, lakini mpakaleo hakuna lililofanyika. Hii ni hatari! Kituo hiki kwa kwelihakina sifa yoyote; kwanza hakina dari, seli hakuna,197

kuta zote zimekatika. Kwa ufupi yule Mama ambaye niMkuu wa Kituo, Inspekta Mtumwa namshukuru sanakwani anajitahidi sana kwa sababu hata baadhi yavifaa anajitahidi kutafuta kwa mbinu zake lakini Serikalihaichukui hatua yoyote. Hili ni suala baya.Mheshimiwa Spika, pia ina maana watafute gariza doria kwa njia ambayo haistahiki, ni magari yakawaida tu ambayo si jambo la busara kabisa. Mudamrefu nalizungumzia suala hili kwamba, vituo hivivipatiwe gari zao, gari ya OCD haisaidii kitu kwani OCDwakati mwingine ana matatizo yake, kuna mambomengine anataka kufuatilia na huku limetokea lingine.Kwa hiyo, naomba wahusika mtusaidie ili tuwezekufanikisha masuala haya. Kituo cha Chwaka kikokiamboni kabisa yaani kijijini kabisa, kimezingirwa nakijiji, Kituo cha Polisi hakiwezi kuwa katikati ya kijiji,haimkiniki. Nyumba kwa kweli hakuna, wanalala katikamazingira magumu kabisa, huamini kwamba hapakalala binadamu na watoto wake, mambo menginehayastahiki kuyasema.Mheshimiwa Spika, dakika zangu nafikiri walizilawakati ule.SPIKA: Haya, ahsante. Haiwezekani! MheshimiwaPhilipa Mturano.MHE. PHILIPA G. MTURANO: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kutoamchango wangu siku ya leo.198

Mheshimiwa Spika, kabla sijafika kwenye madayenyewe kwanza napenda niwapongeze Mawaziriwote waliochaguliwa, lakini kwa dhati kabisaniwapongeze Mawaziri wanawake kwa kazi nzuriambayo wameifanya kwamba hakuna hata mmojaaliyeondolewa, wameendelea kwenye nafasi zaokama kawaida na hata walipobadilishwa lakiniwamebaki kwenye Baraza. Wale ambaohawakuendelea basi karibu kundini.Mheshimiwa Spika, kwanza nishukuru kwa Serikalikuamua kurudisha JKT, lakini naomba hii JKT isielekezwetu kwa vijana kwa sababu hata watu wenginewanahitaji kuwa wazalendo, wanahitaji kuwa nanidhamu katika kazi na katika maeneo mbalimbali.Napendekeza mtindo uliokuwepo zamani kwambamtu hawezi kupata ajira mpaka awe na cheti cha JKT,hatukuweza kuajiriwa sisi mpaka tulipokuwa na vyetivya JKT. Watu wazima waliokuwa maofisiniwaliondolewa maofisini wakapelekwa Jeshi la KujengaTaifa, tumehenya mwaka mzima. Kwa hiyo, kama kunamfanyakazi yeyote ambaye atakuwa hajapitia JKThaijalishi umri wake na yeye apite JKT ili ajifunzeuzalendo wa nchi hii. (Makofi)Mheshimiwa Spika, tumesikia kwamba kuna fedhaya rada imekuja na itatawanywa katika mikoa minne ilikununua madawati. Naomba pesa hii ipelekwe katikamikoa yote ili tugawane kidogo kidogo kwa sababupesa hii imetokana na kodi za Watanzania wote. Kwakuwa, katika mikoa yote karibu Halmashauri zote zinaupungufu wa madawati, basi tugawane kidogo kidogokasungura haka ili wote tufaidi hii pesa ya Rada. Lakini199

pia tuambiwe wahusika wamechukuliwa hatua ganikama vile wengine wanavyochukuliwa hatua na waotuambiwe wamechukuliwa hatua gani.Mheshimiwa Spika, nikija kwenye suala la Walimuwamekuwa wakitishia kufanya mgomo hivi karibunikwa ajili ya kudai stahiki zao. Katika hotuba ya Bajeti yamwaka 2012/2013, ukurasa wa 14 aya ya nne Serikaliimesema kwamba, Wizara ya Fedha ilitoa shilingi bilioni44 kama malipo ya Walimu. Lakini kwenye randama yahotuba ya Waziri Mkuu wanasema kwamba ni bilioni19.2, tunapenda kufahamu ni ipi iliyo sahihi? Piaingesaidia kama tungefahamu hao Walimu waliolipwani akina nani kwa idadi yao na kwa majina ili wawezekujitambua, isije ikawa unatokea ujanja ujanja kwasababu kuna baadhi ya watu ambao wanatakakujinufaisha na hilo.Mheshimiwa Spika, nikizungumzia suala lamsongamano wa Mahabusu Magereza. Hili limekuwani tatizo kubwa hasa kwa Magereza yaliyopo Mkoa waDar es Salaam. Hili nimeliona katika Magereza ya Kekona Segerea. Msongamano ni mkubwa sana na kamailivyoelezwa jana na Mbunge mwenzangualiyechangia, chumba kidogo kinalazimika kuwa nawatu wengi tena wanachanganywa. Yanayotokeahapo ni mengi sana na sina haja ya kuyaeleza kwaniyanaeleweka lakini itambulike kwamba hao watumwisho wa siku baada ya kifungo wanarudi katikajamii. Kuna watu wanakuwa wameathirika kisaikolojiana wengine pengine wamepata magonjwa,wanaporudi kwenye jamii wanakuja tena kuletamatatizo mengine.200

Mheshimiwa Spika, ningependa hili nalolishughulikiwe, waangaliwe wale wenye makosamadogo madogo wapatiwe adhabu nyingine na silazima kuwepo Mahabusu. Kwa sababu haiwezekanimtu amekwapua simu au ameiba kuku, though ni kosalakini akakaa huko miaka miwili au mitatu wakatiupelelezi unaendelea. Napenda hili lishughulikiwe.Mheshimiwa Spika, lakini pia naomba nizungumziesuala la wizi au uharibifu wa miundombinu katika Mkoawa Dar es Salaam. Juzi nimelizungumza kwa kuulizaswali kwa Waziri, akanijibu lakini dukuduku languhalijakwisha, hili nataka Waziri Mkuu alisikie. Watu waDAWASCO na DAWASA wamejitahidi sana kuwekamifuniko ya kuzuia mashimo ya maji taka, lakinikumetokea wajanja wachache wanachukua ilemifuniko wanapeleka wanakojua wenyewe. Mashimoyaliyopo Dar es Salaam yanatisha na viongozi waliowengi wanaishi Dar es Salaam na siyo kwamba waliowengi bali ni karibu wote tunaishi Dar es Salaam.Maeneo ya Posta na hata Upanga Kambi ya Jeshimifuniko imeng’olewa, ukipita na gari unawezaukatumbukia shimoni kama ni usiku na wakatimwingine hata mchana unatumbukia, utawezakuvunja mguu au kupinduka.Mheshimiwa Spika, tunataka kujua, kwanza hiimifuniko ni mizito sana, huyu mtu anawezajekuinyanyua yeye peke yake? Tunaomba uchunguziufanyike, kwani hapa kuna kitu kwenye vyumachakavu, ule mfuniko ni mzito sana, mtu mmoja hawezikuunyanua. Tunaomba uchunguzi ufanyike.201

Mheshimiwa Spika, nikija upande wa elimu,kwanza na-declare interest, mimi nilikuwa Mwalimu nani Mwalimu mpaka sasa, nasikitika sana kuonakwamba kuna wanafunzi ambao wamekwendasekondari wasiofahamu kusoma wala kuandika.Nashangaa hii selection ilikuwa ni ya aina gani. Lakiniushauri wangu ni kwamba, naomba kama siyo lazimahakuna haja ya second selection, ni afadhali tupelekewanafunzi wachache wenye uwezo kuliko tunapelekawanafunzi wengi ambao hawana uwezo eti tu ili mraditujaze shule zetu au tupate sifa kwamba tumefaulishawanafunzi wengi.Mheshimiwa Spika, lakini pia nataka nizungumziekidogo kuhusu ulinzi na usalama. Katika Mkoa waKigoma mimi pia ni mwenyeji wa Kigoma na Wilaya yaKibondo, mimi ni Muha. Mwezi uliopita nimenusurikakutekwa nikiwa kwenye gari langu, baada ya kupitandani ya robo saa Land Cruiser ilikuwa inafuata watuwalitekwa barabara ya Kibondo; kutoka Kibondounakuja Dar es Salaam au Nyakanazi, Land Cruiserilitekwa.Mheshimiwa Spika, niliwahi kuongea na Mkuu waMkoa wa Kigoma kwenye Bunge la Bajeti MheshimiwaSimbakalia kwamba labda sijui itumike mbinu gani aulabda tuombe Jeshi la Wananchi lifanye doria pale.Lakini tunaomba doria izidishwe kwani mimi binafsinaona Polisi wamezidiwa, pale vitendo vya utekajivimekithiri sana kwani pori lile ni kubwa nainawezekana kuna hawa wenzetu kutoka nchi jiranindiyo wanaojipenyeza yaani Burundi na Rwanda na202

inaeleweka. Kwa hiyo, tunaomba Serikali ilifanyie kazi.(Makofi)Mheshimiwa Spika, lingine kabla sijasahau ni sualala wauguzi. Tunatambua kazi yao ilivyo ngumu hasaManesi ambao wanatusaidia akinamama kujifungua.Tunatambua kazi yao ni ngumu na tunaomba maslahiyao yaendelee kuboreshwa siku hadi siku. Lakini,masuala ambayo baadhi ya Manesi wanayafanya siyomazuri na hayawezi kuvumilika hata kidogo.Wamekuwa na lugha ambazo si nzuri kwa akina mamawanapokuwa wanakwenda kujifungua na vitendovyao vinakuwa si vizuri. Kati ya tarehe 18 mpaka 22mwezi Mei katika Hospitali ya Amana Manesiwalisababisha...(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)SPIKA: Ahsante sana nashukuru. MheshimiwaSalum Barwany atafuatiwa na Mheshimiwa Josephinena mwisho atamalizia Mheshimiwa Ngonyani.MHE. SALUM K. BARWANY: Mheshimiwa Spika,ahsante. Kwanza nichukue nafasi hii kwa niaba yaVyama vya Watu wenye Albinism katika Taifa hilikukupongeza wewe na kutoa shukrani zetu za dhatikabisa kwa kukubali kwako kuwa mgeni rasmi kwamaadhimisho ya sita ya siku ya walemavu wa ngoziTanzania. Kukubali kwako kumetufariji sana na piazilikuwa taarifa za ghafla kwako lakini nasema ulijali napia ulitufikia kwa wakati muafaka. (Makofi)203

Mheshimiwa Spika, mtu mzima akitoa machozimbele ya watu inafaa watu wakakaa wakazingatia.Leo asubuhi Mheshimiwa Al-Shaymaa Kwegir chozi lakeambalo alilitoa katika jumba la Bunge la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ni kudhihirisha dhahiri kabisakwamba Maalbino katika Taifam, hili wameshapotezamatumaini ya kuishi kwa amani ndani ya Taifa lao.Mheshimiwa Spika, niseme kwamba, jukumu laBunge ni kuisimamia Serikali na mauaji badoyanaendelea kufanyika katika nchi hii. Hivyo ni jukumula Bunge sasa kama msimamizi mkuu wa Serikali baadaya Serikali kushindwa kudhibiti mauaji kutoa tamko auBunge lipate maelezo ya kutosha kutoka kwa Serikalikwa nini mpaka leo mauaji ya Albino yanaendeleakuwaathiri katika Taifa letu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa kipindi kirefu sasa katikaBunge la Jamhuri ya Muungano, Mikoa ya Kusiniinatajwa sana tofauti na awali, kila Mbunge anatoashukrani zake kwamba Taifa limepata uchumi imara,Taifa sasa litaneemeka kwa sababu tayari kusiniimepatikana gesi, gesi ambayo inasemekanakutakuwa na utajiri mkubwa katika Taifa hili. Lakiniwenzangu wanatafunatafuta maneno hawasemi wazi,hebu niwaambie Wabunge wenzangu kwambawananchi wa Mikoa ya Kusini hawapo tayari kuionagesi yao inatoka Kusini kuja huku bila wao kufahamuwana maslahi gani ndani ya gesi hiyo. Hizi ndiyosalamu za wananchi wa Kusini.Mheshimiwa Spika, tumeona rasilimali na uchumiwa Taifa hili ambao umefika katika mikono isiyo204

salama, Serikali hii imeshindwa kuwanufaisha wenyewekatika maeneo husika. Hili siyo mzaha tena kwanitumeathirika sana kiuchumi katika Taifa hili hususankatika Mikoa ya Kusini. Kupatikana kwa gesi hiitumeona ni ukombozi kwetu, lakini tayari tunaona daliliza wazi kabisa ambazo zimejitokeza kwamba yalematarajio ya wananchi wa Kusini juu ya gesi hiihayaonekani kwa karibu. Tumeona katika vyombo vyahabari juzi yanazungumzwa hapa kwamba mamilioniya shilingi yamekamatwa katika mabenki ya Uswisiyakinasibishwa na upatikanaji wa gesi hiyo. Sasa huondiyo mwanzo tu.Mheshimiwa Spika, lakini niseme tu kwamba, tayarikatika dunia nzima machafuko na migogoroinayotokana na kutokuwa na mgawanyo katika nchihizi. Naamini kabisa kwamba matokeo mabayayatakayotokea katika nchi hizi ni kule kutokuwa namgawanyo rasmi wa rasilimali katika nchi hii. Mikoa yaKusini tumeshiriki katika utumwa wa nchi hii miakamingi, ni mikoa ambayo tayari inatoa mchango katikaTaifa hili kwa zao la korosho ambalo ni zao la tatukatika utoaji wa mchango mkubwa katika Taifa hili,lakini baada ya miaka 50 ya uhuru hatuoni mafanikioambayo yalipatikana kupitia zao la korosho.Mheshimiwa Spika, ukanda wa Mtwara na Masasikupitia Tandahimba na Newala ni ukanda ambaounatoa korosho za kutosha lakini nenda kawaangaliewananchi wa Tandahimba wanavyoishi katikamashaka na umaskini uliokithiri. Huwezi kukubalikwamba Mkoa wa Mtwara ambao unatoa zao lakorosho kwa kiasi kikubwa hawana barabara ya lami,205

hawana maji ya uhakika, hawana hospitali ya uhakikakatika maeneo wala hawana maji ya uhakika.Tunaamini kabisa kwamba mapato yatakayotokanana gesi hayatakuwa na tofauti kabisa na rasilimali yakorosho ambayo tumeipata katika Mikoa ya Kusini.Wenzangu wanatafuna maneno, lakini nimeagizwakabla sijaja katika Bunge hili, nimepita katika Wilayazote wameniagiza kwamba Serikali ni lazima itafutejawabu la msingi kabisa la kuwaambia wananchi wakusini kwamba, kwanza hata kaabla sera ya gesihaijatengenezwa, Serikali imeshaanza kuwekamikataba ya kinyemela, tunataka mikataba hiyo ijeBungeni na tuione ili tuweze kujiridhisha kamamikataba hiyo itakuwa na maslahi kwetu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nirudi kwenye Jimbo langu laLindi Mjini. Tarehe 1 Julai, 2010, Serikali ilitangaza rasmikwamba Jimbo la Lindi Mjini ni Manispaa likiwa na Kata13, lakini baada ya kutangazwa rasmi kuwa Manispaatukawa na Kata 18 yaani ongezeko la Kata tano.Kuonesha udhaifu wa Serikali katika maeneo yetutuliendelea kupata ruzuku ya Kata 13 zile zile hatakama kuna zaidi ya Kata tano ziliongezeka.Mheshimiwa Spika, ndani ya bajeti mbili, badotunapata ruzuku ya Kata 13 wakati huo huo Lindi niManispaa ambayo tayari tuliambiwa kwambakupatikana kwa Manispaa kutakuwa na maendeleomakubwa, lakini tunaona cealing ile ile ambayoilipatikana ndani ya Kata 13, bado inaendelea kuwakatika Kata 18 ambazo tayari nyingine zimetolewakatika Halmashauri ya Wilaya bila ruzuku yakekuongezwa katika Manispaa ya Lindi. Hili linatukatisha206

tamaa kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzihaiko tayari kuona kwamba inanufaisha maeneoambayo tayari walitangaza katika ilani yao kwambaitatumia nguvu kubwa kuhakikisha kwamba maeneoambayo yapo nyuma kiuchumi yanapewakipaumbele. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hayo ndiyo yanatupa mashakandani ya Serikali hii, tuna mambo mengi ya msingiambayo tulitarajia kwamba baada ya kupatikana kwaManispaa ya Lindi tayari wananchi wa Lindiwataboreshewa maisha yao, lakini bado hali ni tetempaka leo.Mheshimiwa Spika, tuna hospitali ya Sokoine yaLindi ambayo ipo kabla ya Uhuru, naamini kwambandani ya uhuru huu tusingepata hospitali ile ambayoilikuwa na majengo mazuri, lakini leo tunashuhudia jinsigani hospitali ile ilivyodorora katika kutoa hudumazake. Hospitali ambayo tunaambiwa leo ni hospitali yarufaa haina Daktari Bingwa hata mmoja, haina x-ray,haina Madaktari, haina watu ambao tayari tunaaminikwamba wanaweza kuwatumikia wananchi katikakuwapatia tiba. Hayo ndiyo matatizo ambayotunakumbana nayo na kuwafanya wananchi wa Lindikutokuwa na imani na Serikali yao.Mheshimiwa Spika, stakabadhi ghalani. Inasikitishatunapokaa hapa tunaona ni watu gani ambaowanaona kwamba, stakabadhi ghalani imewaleteamaslahi wananchi, ni viongozi wa Serikali tu, lakinisijamsikia mwananchi anasema kwamba stakabadhighalani inamletea manufaa, ni watu ambao bado207

hawajaona manufaa ya stakabadhi ghalani. Wakulimawa korosho ni wakulima wa daraja la chini. Amepatakiasi kikubwa ni gunia tatu au nne au tano,anakoipesha zaidi ya miezi sita hajalipwa, anatakakutoa huduma kwa kupeleka watoto shuleni, anatakakuandaa mashamba yake, lakini ndani ya miezi sitamkulima huyu hajalipwa. Hivyo, inafikia mahalikwamba, mtu ambaye unamsikia kwamba stakabadhighalani imewasaidia wakulima ni mtu ambaye hanamkorosho na wala hategemei mapato kupitiamkorosho.Mheshimiwa Spika, hivyo, nasema kwamba waleambao wanasema stakabadhi ghalani imewasaidiawakulima, nasema stakabadhi ghalani haijawasaidiawakulima. Wakulima wa Tandahimba, Newala,Nachingwea na Liwale wananisikia hapa na naaminikabisa wanaunga mkono kauli yangu. Tusiitestakabadhi ghalani ili tuweze kuleta manufaa kwawakulima wetu, tuseme malipo ghalani, malipo yaweghalani na siyo stakabadhi ghalani.Mheshimiwa Spika, mwisho, nizungumzieHalmashauri zetu. Hivi sasa tayari kuna ukiritimba wamabenki ambayo yanafanya kazi pamoja naHalmashauri, Halmashauri tayari wana uhusiano wakaribu kabisa na NMB ambayo tunaamini kabisa kunaubadhirifu mkubwa wa fedha za wananchi. Pia kunaHalmashauri ambazo tayari hazina Uhuru, wanaamuakwenda katika Benki yoyote ambayo wanawezakuweka fedha zao na kuzifanyia kazi.208

Lakini kutokana na ukiritimba wa Serikaliwanalazimishwa kwamba fedha zile wazipeleke NMB.Kuna mabenki ambayo tayari yana uwezo wa kutoariba ambazo zingesaidia kuongeza mapato ya ndaniya Halmashauri zetu. Naishauri Serikali ushauri wa burekabisa kwamba, Halmashauri wapewe uhuru wanamna gani wanaweza kuweka fedha zao katikabenki ambazo zinaweza kutoa riba na kuwaleteamaendeleo wananchi wetu.Mheshimiwa Spika, nasema siungi mkono hoja.(Makofi)SPIKA: Ahsante sana. Nilipokwenda kwenyesherehe ya siku ya albino wana maelezo mazuri sana.Tunawaona wenzetu lakini hatuwafahamu. Kwa hiyotulikubaliana kwamba tukipata muda watakuja kutoasemina ili tuwaelewe wenzetu walivyo.MHE. STEVEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kuniona na kwa kuwa ni marayangu ya kwanza kuchangia, kwanza naombaniwashukuru wapiga kura wangu wa Korogwe Vijijinikwa kuniombea kwa muda mrefu nikiwa mgonjwa nahadi leo nimerudi tena Bungeni nikiwa na nguvu nyingi.Mungu awabariki sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, vilevile nisiache kumpa poleMwenyekiti wangu wa Halmashauri ya Korogwe Mjiniambaye alipata ajali mbaya sana juzi na Mwenyekitiwa Halmashauri ya Korogwe Vijijini pamoja na Meyawa Mji wa Tanga. Sasa hivi ninavyozungumza wakoMoshi wamelazwa katika Wodi ya mifupa na sijui kama209

wanatibiwa ukizingatia kwamba Madaktariwamegoma. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nimshukuru Mheshimiwa Raiskwa kazi kubwa na nzuri sana aliyoifanya ya kuwateuaWakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wapya, hasaMkuu wangu wa Mkoa wa Tanga ambaye amenifanyasiku hizi hamnioni nikisimama na kulalamika kuhusumambo ya mkonge. Mkuu wa Mkoa alituita tukajadili,tukashauriana na sasa mkonge kule tunauona unathamani kubwa sana. Mungu ambariki kwani sikutarajiakwamba haya yangefanyika, lakini vile vile amefanyakazi nzuri sana.Mheshimiwa Spika, vilevile nisiache kumshukuruMwenyekiti wangu wa Kamati ya Bunge ya Huduma zaJamii, mama Sitta. Wakati nikiwa mgonjwa kila sikualikuwa anakuja hospitali kunipa matumaini kwambanitapona. Mungu ambariki sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nirudi kwenye Kilimo Kwanza.Narudi kwenye Kilimo Kwanza kwa sababu katika eneoletu la Mkoa wa Tanga tumezungukwa sana namashamba ya Mkonge ambayo hayaendelezwi.Ukizingatia kwenye Jimbo langu la Korogwe Vijijini ninamashamba 15 ya mkonge na matatu (3) ya chai. Kwa ,hiyo, jumla nina mashamba 18. Sasa kati ya hayo kunamashamba ambayo hayaendelezwi. NamwombaMheshimiwa Waziri Mkuu zile hati ambazo ziko mezaniambazo zinatakiwa kufutwa, ifanywe haraka zifutwemara moja ili tuendeleze huo mradi wa Kilimo Kwanza.(Makofi)210

Mheshimiwa Spika, kwa sababu unapomwambiamkulima kuhusiana na mradi wa Kilimo Kwanza nilazima awe na maeneo ya kutosha ya kulima nakujipatia riziki yake kwa kupanda mazao ya biasharana chakula. Sasa naomba haya, kwa sababutuliambiwa hati ziko mezani kwa Mheshimiwa Rais nasisi watu wake na wanavijiji huko wanalia, basi,aangalie sana haya mashamba ambayohayaendelezwi, hati zifutwe ili wananchi wetuwaendeleze kilimo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, vilevile katika Jimbo langukuna huu utaratibu uliokuja wa mamilioni ya JK.Wananchi wangu wa Jimbo la Korogwe Vijijini hayowanayasikia tu kwenye redio. Hawajawahi kuona hatamara moja na wala hawajui zinakwenda wapi. Kwahiyo, kama kweli huo mradi upo basi ufutwe naitafutwe namna ambayo wale vijana, akinamama,wazee walioko vijijini kabisa ambao wanawezakuendeleza miradi hii wajue ni wapi wanakwendakuzichukua na watazirudisha namna gani, kuliko huumradi kuingia kwenye miji tu na wanapewa wale watuwenye fedha, wale maskini kabisa hasa wa KorogweVijijini hawana msaada wa aina yoyote ambaowanaupata. (Makofi)Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo natakanilisemee ni maji. Maji imekuwa ni kero kubwa sana,ingawa namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu janakabla sijakuja kuchangia amenieleza hali halisi nanimefurahishwa sana kuona kwamba Mkoa wangu waTanga na yale mambo madogo madogo ambayonilikuwa nayataka yote ameyapa kipaumbele. Kwa211

hiyo, naunga mkono hoja mia kwa mia kweli kweli.(Makofi)Mheshimiwa Spika, kuna kitu ambacho kinanikerasana, hili suala la dharura ambalo limejitokeza jana,suala la Ulimboka ambalo limefanya hata mimimwenyewe nimeshangaa Madaktari. Madaktariwamegoma kwa misingi kwamba hawatamhudumiamtu yeyote kwa sababu hawakuelewana na Serikali.Kitendo hiki ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwasababu wanachokifanya siyo kutukomoa sisi,wanawakomoa watu wadogo walioko kwenye...SPIKA: Mheshimiwa Ngonyani!MHE. STEVEN H. NGONYANI: Naam.SPIKA: Hili suala liko Mahakamani. Tulishakubalianaasubuhi kwamba hatutaliongelea. Naomba tafadhali,hili suala liko Mahakamani.MHE. STEVEN H. NGONYANI: Basi na yeyewasimtibu.SPIKA: Aaah, hapana huwezi kuzungumza!MHE. STEVEN H. NGONYANI: WasimtibuMheshimiwa Spika. (Kicheko/Makofi)SPIKA: Mheshimiwa Ngonyani, kwanza unatakiwaukae nikisimama.MHE. STEVEN H. NGONYANI: Sawa Mheshimiwa.212

SPIKA: Kwa hiyo, endelea na mjadala mwingine,hilo liache. Lakini siku nyingine nikisimama weweunakaa. Haya sasa endelea. (Makofi/Kicheko)MHE. STEVEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,samahani sana. Unajua ukiugua unachanganyikiwakidogo ndani ya akili. Unajua licha ya kuugua pianilitangaziwa kifo kwamba nimefariki. Sasa labda hiyoinanifanya pia nakuwa na stress. Kwa hiyo, pole sana.SPIKA: Ndiyo maana nimekupa nafasiuzungumze...MHE. STEVEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Kuna suala la maji kutoka Mkoa waKilimanjaro kuja Mkoa wa Tanga hususan katika Wilayaza Same, Hedaru, Mombo hadi kufika Korogwe. Huumradi naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu tuuangalie nakama upo naomba utekelezwe haraka kwaniWananchi wa Korogwe wanapata sana shida ya majina hasa ukizingatia kwamba tumepitiwa na mradi wamajisafi pale, lakini hatuwezi kuyapata. Naomba sanahili suala liangaliwe kwa hali na mali kwa sababu nikero kubwa inayowasumbua wakazi wa KorogweVijijini. (Makofi)Mheshimiwa Spika, suala la elimu umeshaniambiana mimi nakuunga mkono na sitataka kuchangia sanakwa sababu niliyokuwa nataka kuyachangia, janaumeniambia ana kwa ana kwamba umenisaidia.Nikiwa hospitali umekuja kuniona, nilichokuwa natakani kukupongeza kwa kutuletea Mkuu wa Mkoa na213

Mkuu wa Wilaya ambaye anatupa matumainikwamba, safari hii Mkoa wa Tanga tutapanda bei kwaajili ya zao la mkonge. Naomba wakulima wa mkongewasipangiwe mtu wa kununua mkonge. Popotewatakapoona kuna bei ambayo wanaridhika nayowaende wakauze tu huko badala ya wao kuwawanaambiwa kwa sababu ni wakulima wadogowashikwe na wanaposhikwa wanakuwa hawana faidana mkonge. Huu mkonge ni sera ambayo tulishasemakwamba safari hii ni mwaka wa kupanda mkonge.(Makofi)Mheshimiwa Spika, suala lingine ni kuhusu hiimikataba ya mashamba ya mkonge. Mashamba yamkonge mikataba yake inapokuwa inapitiwa basiwatafutwe watu ambao wataipitia na isitokee tuwachache waamue kwamba, mikataba ifanyike. Hililimejitokeza na inakuwa kero kubwa sana kwetu.(Makofi)Mheshimiwa Spika, suala la pili, nimeona pale HaleTANESCO kwamba panajengwa. Korogwe nakopajengwe na uzuri ni kwamba Mkoa wa Tanga sasahivi umeme unakatikakatika sana. Nashangaa mikoamingine ambayo haina vituo hivyo vya umeme,umeme haukatiki. Kwa nini Mkoa wa Tanga umemeunakatika wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu umeshanipamatumaini kabisa kwamba kila kitu kitaendelea vizuri?Naomba huyu bwana ambaye ametupa matumainikwamba atashughulikia masuala ya TANESCOaangalie kilipo kiini cha umeme, lakini hakuna umeme.Wananchi wanapata shida, hawana maabara,hospitali hakuna dawa, Madaktari ni wachache katika214

Kata na Vijiji vyetu. Haya ndiyo baadhi ya mamboambayo tunayaomba sana kwa Mheshimiwa WaziriMkuu, katika mjadala wake wowote na haya ayawekendani kabisa mia kwa mia ili na sisi tukizunguka Mkoawa Tanga tuonekane.Mheshimiwa Spika, safari hii sitachangia sana,nangoja hizo Wizara nyingine. Namuunga mkono miakwa mia Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kabisa napendakuipongeza Serikali kwa kuja na bajeti ambayotunaamini ikifuatwa vizuri na kama walivyoahidikwamba katika sehemu mbalimbali watajaribu kubanamatumizi na kufuata utaratibu wa matumizi ya fedha,tunaamini tutasonga mbele na tutaweza kupatamaendeleo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napendakuchangia katika suala la kuongeza posho yaMadiwani. Ni ahadi ya siku nyingi naipongeza Serikalikwa kufanya hivyo. Lakini pia naomba waangalienamna ya kuangalia pia viongozi wengine ambao nimuhimu; Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongojipamoja na Mabaraza ya Ardhi. Naamini kwambatukijipanga vizuri tutaweza. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini pia napendakuikumbusha Serikali kuhusiana na suala la kodi katikavipuri vya Matrekta. Tulikwishapitisha mwaka janakatika bajeti kwamba iondolewe lakini hadi leo hiihaijatekelezwa. Lakini pia tunaomba Serikali iangalie215

namna ya kuondoa kodi katika matairi ya trekta, trelaza trekta na pia katika vipuri vya vyombo vyaumwagiliaji. Serikali pia iangalie namna ya kuboreshamfumo mzima wa kufikisha pembejeo nchi nzima iliwakulima waweze kupata pembejeo kwa mudamuafaka na suala la kuchakachua lisiwepo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, pia naipongeza Serikali kwasuala la matrekta kupitia SUMA JKT. Serikali imekubalikuondoa ule uchangiaji wa asilimia 50 wakati unatakakununua trekta na kuipunguza kuwa asilimia 30 na ulemuda wa kulipa lile deni badala ya miaka miwilikuongeza kuwa miaka minne(4). Nawapongeza kwahilo na naamini wakulima wengi zaidi sasa watanufaikakutokana na hayo matrekta. Tunaomba Serikaliiangalie katika maeneo ambayo hayo matrekta badohayajafikishwa, basi utaratibu ufanywe ili yaweze kufikakatika maeneo yote na haya matrekta yafanye kazi ilikuleta tija. (Makofi)Mheshimiwa Spika, katika suala la Jimbo la BabatiVijijini, kuna migogoro ya ardhi. Tunaomba Serikaliiangalie namna ya kutatua hii migogoro ambayo ni yamuda mrefu na ambapo wananchi wengiwameshapoteza maisha na wengine kupoteza malizao na wengi sasa hivi wanakaa bila kujua hatima yaokwamba watafanyaje. Serikali ilikwishaunda Tume,tunaomba hiyo Tume itoe taarifa yake vizuri ili hilo tatizola ardhi litatuliwe hasa katika Bonde la Kiru, pia katikakijiji cha Mwada na wananchi ambao wanazungukaeneo la Tarangire katika vijiji ambavyo ni jirani naTarangire kule Mamire, Gidajabong, Ayamango naGedamari. Wananchi wa maeneo haya wanaishi kwa216

mateso. Wapatiwe eneo mbadala nawamekwishakubali kuondoka, lakini wapatiwe maeneombadala ili wao pia waweze kuishi kwa amani kamaWatanzania wengine.Mheshimiwa Spika, pia tulikuwa tunaomba ahadizile za Serikali zitimizwe; daraja la Mto Magara Serikaliiliahidi kulijenga na ilishatenga fedha lakini hatuoni dalilizozote hadi leo hii kuhusiana na kujengwa kwa darajahilo.Mheshimiwa Spika, pia suala la umeme, tunaitakaSerikali iongeze fedha zaidi katika Mfuko wa UmemeVijijini (REA) ili umeme uende kwa kasi zaidi vijijini ilikukuza maendeleo. Tunaomba mfuko huo uboreshwezaidi. Tulikuwa tunashauri TANESCO ikubali katikamaeneo ambapo nyaya za umeme zinapita juu katikabaadhi ya maeneo ni ule uunganishwaji tu nagharama ndogo, ikubali kukopeshwa na wananchiambao wanaweza kukopa kutoka SACCOS auVICOBA ili wafungiwe umeme. Halafu baadaye hiyofedha irejeshwe kwa kukatwa katika ankara ya bill iliwananchi wale waweze kurudisha hizo fedha katikaSACCOS na VICOBA mahali ambapo watakopa. Lakinipia tunaomba katika maeneo ambayo umeme nimuhimu sana na tunaweza kuongeza uzalishaji kwasehemu kubwa umeme katika Kata ya Riroda, Magara,Mamire, Endakiso, Dabili na Maidunga, ufanyiwenamna uende haraka zaidi.Mheshimiwa Spika, lakini pia tulikuwa tunaombaSerikali iangalie suala la VICOBA. Tunaipongeza kwakuanzisha SACCOS na VICOBA, ndiyo mkombozi wa217

wananchi, lakini VICOBA haiko kisheria. Tunaombasheria hiyo itungwe haraka iletwe hapa ili VICOBAviweze kutambuliwa kisheria na rasmi ili hizo fedhaambazo zinakaa tu vijijini ziweze kuwekezwa katikataasisi za benki na VICOBA, hivyo viweze kukopakutoka benki na waweze kusaidia hao wananchi.Tunaomba hicho kitu kifanywe kwa haraka kutokanana umuhimu wake.Mheshimiwa Spika, katika sehemu mbalimbalindani ya Wilaya yetu kuna matatizo makubwa ya afya.Tulikuwa tunaomba Serikali iendelee kuboreshahuduma ya afya kwa kuongeza huduma katikahospitali ya Dareda na kuiingiza hospitali ya Bashnetikatika mfumo wa kupata ruzuku kutoka Serikalini kwasababu inahudumia zaidi ya eneo la Babati nainahudumia pia Wilaya za jirani. Pia tulikuwa tunaombaile ahadi ya kupatiwa gari la wagonjwa itimizwe ililiweze kuhudumia wananchi ambao wako vijijini.Mheshimiwa Spika, muhimu kuliko yote Serikaliiangalie namna ya kuboresha kilimo kwa sababu ndiyomkombozi wa Watanazania walio wengi. Tulikuwatunaomba fedha nyingi zaidi zitakazowekezwa katikaMfuko wa Pembejeo na TIB zipelekwe vijijini badala yakukopeshwa watu wachache wenye uwezo. Haowenyewe wanaweza kukopa hata katika taasisizingine, lakini hasa hizi SACCOS na VICOBA na vyamavya msingi ndivyo vikopeshwe fedha zaidi ili viwezekukuza kilimo katika maeneo mbalimbali. (Makofi)Mheshimiwa Spika, pia tulikuwa tunaomba Serikaliiangalie suala nililosema la uanzishwaji wa mabonde218

mapya. Ni muhimu sana, lakini pia yale mabonde yazamani yaliyopo ndiyo yangeendelea kuboreshwakwanza hasa katika maeneo mfano ya Babatiambapo tunazalisha karibu asilimia 80 ya mbeguambayo inazalishwa Kanda ya Kaskazini. Maeneohaya yangeboreshwa ili badala ya kutegemea mbegukutoka nje ya nchi tungeweza kuzalisha mbegu ndaniya nchi yetu hapa hapa. Mbegu ambayo itakuwa yaKitanzania, badala ya kutoa ruzuku sasa hivi kwendanje ya nchi kutokana na mbegu kuagizwa nje. Ruzukuhiyo itaendelea kubaki ndani ya nchi.Mheshimiwa Spika, katika sekta ya kilimo naufugaji, Serikali ingeangalia uwezekano wa kuwa nampango maalum wa kusaidia wafugaji kwa kujengamabwawa na majosho katika maeneo ambayowafugaji wanatoka. Migogoro ya ardhi na uhasamakati ya wafugaji na wakulima itaondoka kama walewafugaji wataweza kuondokana na ufugaji ule wakuchunga na kuwa wafugaji bora. Katika maeneo yaMkoa wa Manyara ambapo wafugaji wengiwanatoka, tungeomba Mabwawa yachimbwe katikamaeneo mbalimbali. Pia katika Mkoa wa Manyarakuna masuala mbalimbali ya kuboresha kwa mfano,hospitali ile ya Hanang pale Katesh ingeendeleakuboreshewa huduma na pia mabwawa mengineyangechimbwa katika maeneo ya Hanang ambayosehemu kubwa ni ya ufugaji.Mheshimiwa Spika, kuna lugha ambazozinatolewa hapa, tulikuwa tunaomba tuweze kupatatakwimu sahihi. Kwa mfano, jana kuna mchangiajimmoja alisema kuna wafanyakazi karibu laki nne219

(400,000) katika mashamba ya NAFCO. Sasanilishindwa kuelewa kwa sababu naamini katika Serikaliyenyewe wafanyakazi hawafiki hao laki nne. Sasakama mashamba ya NAFCO wana watu laki nne,walikuwa wanaishi wapi, wanafanya kazi gani kwasababu Hanang yenyewe haina watu laki nne? Kwahiyo, tunaomba maneno mengine ambayoyanasemwa tusiwe tunayasema kwa ajili yakufurahisha watu, bali tuseme kwa kutoa takwimuambazo ni sahihi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nampongeza Kiongozi waKambi ya Upinzani aliposema suala la vyamambalimbali kuingia katika malumbano hasa katikaubaguzi wa rangi, dini, ukabila na aliitaja Babati.Nashukuru kwamba alitambua baadhi ya viongozikatika eneo langu wanavyofanya ubaguzi dhidi yangukutokana na rangi yangu, ukabila au dini yangu.Namshukuru yeye kukemea suala hilo na kwamba liisheili Watanzania tuweze kuishi kama Watanzania wote.Nampongeza kwa hilo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, tulikuwa tunaiomba Serikaliiangalie namna ya kuboresha Procurement Act. Leo hiizile Kanuni bado hazijaja huko katika Halmashauri zetu.Hizo kanuni ziletwe mapema kwani nia na lengo lakuibadilisha hiyo Procurement Act na kuiboreshailikuwa ni kuhakikisha fedha zinatumika vizuri zaidi iliWatanzania waweze kupata maendeleo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lingine muhimu lilikuwa ni sualala PPP. Ningeomba Serikali kwanza kabisa kabla yakutoa haya maneno kwa wananchi ingekaa, Wizara220

zote zipate elimu kuhusiana na suala la PPP. Waowakiishaelewa ndiyo waje kwetu watufundishe ili sualala PPP liweze kuleta maendeleo. Naishukuru Serikali nanawapongeza kwa jitihada zote hizi. Tutaendeleakuchangia katika maeneo mengine. Ahsante. (Makofi)SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nadhani tumefikiaukomo wa wakati wetu. Dakika tano haziwezi kuruhusuwatu wengine kujadili. Kwa hiyo, kwanza kabisanaomba kesho Waheshimiwa Wabunge muweze kujana vitabu Volume III ambayo inahusu PublicExpenditure Supply Votes (Regional). Halafu mje naVolume IV ambayo inahusu Public ExpenditureEstimates Development Votes. Kwa hiyo, hivi vitabumkiishaleta vinabakia hapa mpaka tutakapomalizakazi yetu mwezi wa Nane. Sipendi watu mnakaa hapamnasema “Ndiyo” au “Siyo” kumbe hawasomichochote. Mje navyo na vitabaki humu ndani kwamiezi yote tutakayokuwa hapa ndani.Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, niwashukurusana kwa kazi nzuri mliyofanya leo na mjiandae kwaajili ya kesho kwani tutafanya kazi nzito zaidi ya kuingiakwenye vitabu. Kuna zile wanaita randama, zile nidetails zaidi kuhusu vitabu hivyo. Ni vizuri mkazipitia hizorandama kwani zinajibu mambo yenu mengi sana.Kwa hiyo, tunapowasilisha randama siku mojakabla ya Waziri kusoma lengo letu ni kwamba muwezekuzisoma na kuingia kwa undani zaidi. Hivi vitabuhavisemi kwa undani zaidi, lakini randama zinakwendavote by vote. Kwa hiyo, naamini hizo randama mnazokwa sababu ziliwasilishwa hapa mezani na hivi vitabu221

mnavyo kwa sababu mlipewa. Naomba vihamie humundani kwa sababu ya kazi tutakayokuwa tunaianza.Basi niwatakie jioni njema na hivyo naahirisha kikaocha Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi.(Saa 1.42 Usiku Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaIjumaa,Tarehe 29 Juni, 2012 Saa Tatu Asubuhi)222

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!