11.07.2015 Views

Jarida la Kilimo, Oktoba

Jarida la Kilimo, Oktoba

Jarida la Kilimo, Oktoba

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Toleo la NaneISSN: 1821- 8113 Oktoba - Disemba, 2011Mhe. Ramadhan A. Shaaban Kaimu Waziri wa Kilimo na Maliasili akikabidhi vyeti kwa wahitimuwa mafunzo ya cheti cha kilimo katika mahafali ya 10 yaliyofanyika tarehe 31/12/2011 Chuo chaKilimo Kizimbani, Wilaya ya Magharibi Unguja.YaliyomoMaoni ya Mhariri/Picha ya Jalada............................................................................Uk.2Matayarisho ya Upandaji Miche ya Mikarafuu......................................................Uk.3Umuhimu wa Chanjo kwa Mifugo......................................................................Uk.4Popo wa Pemba.........................................................................................................Uk.5Programu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini ...........Uk.6 - 7Matukio katika Picha.............................................................................................Uk.8 - 9Mahafali ya 10 ya Chuo cha Kilimo Kizimbani..................................................Uk.10Mchango wa TASAF katika Usarifu wa Mazao.......................................................Uk.11Usarifu wa Mazao ya Kilimo............................................................................Uk.12-13Umwagiliaji Maji ndani ya Greenhouse................................................................Uk.14Mafanikio katika Bonde la Kianga Mwembe Msala.........................................Uk. 15-16

Oktoba - Disemba, 2011WAHARIRI/MAONI/PICHA YA JARIDABodi ya WahaririWashauriAffan O. MaalimJuma Ali JumaDk. Bakar S. AsseidMhariri MkuuDk. Juma M. AkilMsanifu na MhaririMtendajiHashim H. ChandeWahariri WasaidiziMakame M. AbdulrahmanNassor S. MkarafuuNassor S. MohammedMpiga chapaFatma A. JumaMpiga pichaKhamis A. BakariANUWANIWizara ya Kilimo,Maliasili - ZanzibarS.L.P. 159Simu: +255 24 2230986Fax: +255 24 2234650E-mail: kilimo@zanlink.comTovuti: kilimoznz.or.tzMAONI YA MHARIRINdugu Wakulima, kuja kwa programu ya masoko, uongezaji thamani na hudumaza kifedha vijijini [MIVARF] kutaongeza fursa nyingi za utoaji wa ajira vijijini.Makamo wa pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Iddi aliyasema hayo huko Bwawanitarehe 29-11-2011 wakati alipokua akizindua programu hii yenye lengo lakusukuma mbele maendeleo ya wakulima, wafugaji na wavuvi hasa waliokovijijini ambao hukabiliwa na hali ngumu ya maisha.Ndugu Wakulima, hii ni moja kati ya hatua za Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano nawashirika wa maendeleo kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili katika jitihadazake za kuleta mapinduzi ya kilimo ambapo utekelezaji wa programu hii ndioutakaoongeza uzalishaji pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa nakuongeza kipato kitakachosaidia kuleta maendeleo ya nchi yetu.Ndugu Wakulima, Sekta ya kilimo husaidia upatikanaji wa ajira kwa asilimia70 kwa wananchi wake na kuchangia asilimia 50 ya chakula ambachotunakizalisha. Sekta hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa nchi inajitoshelezakwa chakula na kuweza kumkomboa mwananchi kuondokana na umasikini.Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikichukua juhudi kwa mashirikianona watendaji wa Sekta ya Kilimo kuandaa miradi mbali mbali na kuwafi kishiawananchi walioko vijijini.Ndugu Wakulima, programu ya MIVARF imekusudia kuinua kipato chawakulima, wafugaji na wavuvi wa vijijini pamoja na kuwasaidia kuondokana nauzalishaji duni, ukosefu wa masoko na usafi rishaji wa bidhaa zikiwa ni miongonimwa changamoto zinazowakabili walengwa hao, hivyo ujaji wa MIVARF utaletamafanikio kama yalivyopatikana kupitia programu zilizotangulia za PADEP naASSP/ASDP-L na wananchi walivyoweza kunufaika.Ndugu Wakulima, wakati wa uzinduzi wa mradi huu akitoa nasaha zake Mhe.Balozi Seif amefahamisha kuwa programu hii ya MIVARF ni muendelezo wamafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Programu mbili zilizotanguliakati ya hizo ni pamoja na Pogramu ya Uendeshaji wa Mifumo ya Masoko yaMazao ya Kilimo na Huduma za Kifedha Vijijini ambapo Programu hizo mbilizilitekelezwa katika baadhi ya Mikoa ya Tanzania Bara kwa kipindi cha 2002-2010 na walengwa wa programu hizo waliweza kunufaika kwa ujenzi wa masokopamoja na ukarabati wa maghala na barabara pamoja na kumuongezeamkulima kipato chake.Ndugu Wakulima, Programu ya MIVARF ina uwezo mkubwa wa kuleta mafanikiona kumkomboa mkulima na mfugaji kutokana na hali duni ya maisha. Aidha,Balozi Seif alisema ujaji wa Programu hiyo uende sambamba na kuwawezeshawananchi kukabiliana na ushindani wa soko katika ulimwengu huu wautandawazi na kuzijengea uwezo asasi za wakulima pia kupanua wigo kwawazalishaji na wasiokua wazalishaji pamoja na kuwapa fursa ya kuamua hatmaya maisha yao.Ndugu Wakulima, kuwepo kwa programu ya MIVARF ni moja ya hatua muhimuya kuweza kujiletea maendeleo katika nchi yetu kama malengo yatawezakufi kiwa na hapana budi jitihada za makusudi zichukuliwe ili kufi kia malengoyaliyowekwa katika utekelezaji wa Programu hiyo. Aidha, ni matarajio ya Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili iwapo walengwawote watatimiza wajibu wao na kusimamia ipasavyo malengo ya programuhii uzalishaji utaongezeka, kipato, uhakika wa chakula vijijini na hatimaekupunguza umasikini.PICHA YA JALADAKatika picha anaonekana Kaimu Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe.Ramadhan Abdalla Shaaban akikabidhi vyeti kwa wahitimu wamafunzo ya kilimo katika mahafali ya 10 yaliyofanyika tarehe 31/12/2011 Chuo cha Kilimo Kizimbani, Wilaya ya Magharibi Unguja. Akiwapamoja na viongozi wengine wa Wizara ya Kilimo na Wizara nyengineza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.2

MICHE YA MIKARAFUU Oktoba - Diseemba, 2011MATAYARISHO YA UPANDAJI WA MICHE YAMIKARAFU KWA MSIMU WA MASIKA 2012Na Rashid KhamisZao la karafuu ni muhimukwa uchumi wa Zanzibarna linachangia katika pato lawakulima na Taifa kwa ujumla.Katika msimu wa karafuu zamwaka uliopita 2011 kiasi chaShilingi bilioni 63 zililipwa kwawakulima baada ya kuuza tani4,214 za karafuu kwa Shirikala Taifa la Biashara la Zanzibar(ZSTC), ambapo fedha hizozilizopatikana zinawasaidiawakulima na wananchi wote.Historia ya Zanzibar inaonyeshakwamba takriban karne mbilizimepita tangu Zanzibarilipoanza kuotesha mikarafuu.Tokea wakati huo kushamiri kwazao hilo kunatokana na juhudizinazochukuliwa za kutayarishamiche, kupanda na kuhudumiamashamba hayo.Wizara ya Kilimo na Maliasilikupitia Idara ya Misitu naMaliasili zisizorejesheka tayariinaendelea na uzalishaji wamiche ya mikarafuu ambapokwa mwaka 2011/12 imepangakuzalisha kiasi cha miche lakitano (500,000) na inatarajiwakutolewa bure kwa wakulimakatika msimu huu wa masika.Hivyo wakulima mnaombwakufanya matayarisho yamashamba yenu mapema.Utayarishaji na upandaji wamiche ya mikarafuu unaanzakwa kuchagua eneo lenye ardhinzuri kwa ustawi wa mikarafuu.Kwa Unguja ardhi nzuri ni zenyeudongo wa kinongo ambazozinapatikana Wilaya za KaskaziniA na B pamoja na Wilaya zaBaadhi ya miche ya mikarafuu iliyozalishwa katika vitalu vya serikali ikisubiri kugaiwakwa wananchi ili kupandwa katika mashamba yao msimu wa masika 2012Magharibi na Kati. Sehemukubwa ya ardhi ya Pemba inaudongo wa aina ya Bopwe naUtasi, ambazo ni ardhi nzuri kwauoteshaji mikarafuu.Wakulima wanashauriwawasipande mikarafuu kwenyemabonde yanayotuama maji,maeneo ya uwandani nayenye kina kidogo cha udongokwani husababisha kufakwa mikarafuu. Vilevile, juakali wakati wa kiangazi kwabaadhi ya maeneo yanayopatamvua chache husababishakukauka kwa unyevu ardhinina kusababisha kufa kwamikarafuu kwa vile miti hiiinahitaji mvua nyingi zipatazowastani wa milimita 2,000 hadi3,000 kwa mwaka.Mikarafuu inatakiwa ipandwekwenye mistari iliyonyookakwa masafa ya mita 8 hadi 10wastani wa hatua za mtu mzima9 hadi 11, ni muhimu kupandakwa masafa yanayopendekezwaili mikarafuu iweze kustawivizuri na kuweza kutoa mavunomengi. Mavuno yatapunguaikiwa mikarafuu itapandwakaribu au mbali sana kutokamche mmoja hadi mwengine.Upandaji unashauriwa ufanyikepale ambapo mvua za masikazimeshamiri.Mashimo ya kupandayatayarishwe kabla ya kuchukuamiche ya mikarafuu kutokakwenye vitalu. Mche wamkarafuu unahitaji shimo lasentimita 45 kwa sehemu zoteyaani upana na urefu. Wakatiwa kuchimba shimo tenganishaudongo wa tabaka ya juu na yachini, kwa kawaida udongo watabaka la juu una virutubishovingi zaidi kuliko ule wa chini,hivyo ni vyema kutangulizatabaka la juu wakati wa kupanda.Mashimo yaliyotayarishwavizuri kwa ajili ya upandaji wamikarafuu yanasaidia michekuishi na kukua vizuri.3

Oktoba - Disemba, 2011CHANJO KWA MIFUGOUMUHIMU WA CHANJO KWA MIFUGONa Nassor S. MohammedMifugo ni rasilimali ambayo huwapafaida kubwa wafugaji na wananchiwa Zanzibar. Ili mifugo itoe mazaoyenye tija inahitaji kupatiwa hudumabora za malisho, maji, kinga na tibaza maradhi. Maradhi ni moja kati yamatatatizo yanayozorotesha sekta yaufugaji na kupunguza uzalishaji. Katikakukabiliana na changamoto hiyo hatuaza kuyadhibiti maradhi zinachukuliwaduniani kote ili kuimarisha ufugaji nakupata tija.ChanjoChanjo ni mchanganyiko maalum wenyevijidudu ambavyo vimepunguzwanguvu ili visilete madhara kwawanyama au watu waliochanjwa. Hiini njia mojawapo inayotumika katikakudhibiti maradhi dunianiAsili ya chanjo ilitokana na ugunduziwa mwanasayansi wa UingerezaBw. Edward Jenner katika karneya 18 ambapo aligundua kwambawahudumu wa ng’ombe hawakupataugonjwa aina ya ndui (small pox)kutokana na kuwa na vijidudu vyaugonjwa wa ndui za ng’ombe (cowpox) hali ya kuwa maeneo menginewasiokuwa wahudumu wa ng’ombewaligundulika kuwa na ugonjwa huo.Chanjo husababisha mwili wamnyama au binadamu kuandaa askari(vikinga mwili ni antibody) ambaohukaa mwilini kwa muda maalumna huukinga mwili kukabiliana navijidudu vya maradhi. Aidha, chanjoikipungua nguvu inahitajika wanyamawachanjwe tena kwa muda maalumuliopendekezwa kutokana na aina yachanjo au mnyama.Aina za chanjoMiongoni mwa chanjo maarufuzinazotumika kwa mifugo ni; HitcherB1, LaSota, S19/ Rev- 1 strain,Blanthrax, Rabisin, Tetanus Toxoid,Newcastle Disease vaccine EDS – 76 +ND + IBD, Fowl pox, Clon CL/76 strain,Canine distemper, Marek’s diseasevaccine, Foot and Mouth Disease,Gumboro, Mahepe/Mdondo/Kideri,Ndui, Pepopunda, Kimeta, Chambavu,Ugonjwa wa kutupa mimba kwang’ombe, Ugonjwa wa mapafu wang’ombe na mbuzi, Ugonjwa wa bondela ufa, Ugonjwa wa ngozi (Lumpyskin, Streptothricosis, Warts, Mange)Ugonjwa wa miguu na midomo,Maradhi yanayochanjwa na mudaunaopendekezwa.Chanjo ya Gumboro kwa kukuMiongoni mwa chanjo maarufu zinazotumika kuchanja/kuzuia maradhi ya mifugo kamaFoot and Mouth Disease, Gumboro, Mahepe/Mdondo/Kideri, Pepopunda, Kimeta naChambavu.wachanga mara moja katika uhaiwake;Chanjo ya Mahepe/Mdondo/Kiderikwa kuku mara mbili katika uhai wake;Chanjo ya Ndui kwa kuku na ng’ombemara moja;Chanjo ya ugonjwa wa kutupa mimbakwa ng’ombe mara moja kwa mwaka;Chanjo ya ugonjwa wa Kimeta kwang’ombe kila mwaka;Chanjo ya ugonjwa wa Chambavu kwang’ombe kila mwaka;Chanjo ya ugonjwa wa pepopunda(Tetenasi ) kwa ng’ombe kila mwaka;Chanjo ya ugonjwa wa ngozi kwang’ombe, mbuzi na kondoo kilamwaka;Chanjo ya ugonjwa wa miguu namidomo kwa ng’ombe kila mwaka;Chanjo ya ugonjwa wa homa ya mapafukwa ng’ombe na mbuzi kila mwaka;Chanjo ya Kichaa cha mbwa kwa mbwakila mwaka;Chanjo ya ugonjwa wa matumbohasa kwa mbwa wadogo pia unawezakuchanja kwa wakubwa kila mwaka;Chanjo ya Ugonjwa wa sotoka kwang’ombe kila mwaka;Chanjo ya ugonjwa wa bonde la Ufakwa ng’ombe;Chanjo ya ugonjwa wa Farasi kwafarasi kila mwaka.Wanyama wanaochanjwaWanyama hao ni pamoja na ng’ombe,mbuzi kondoo, nyati, ngamia, mbwa,paka, farasi na jamii ya ndegewakiwemo kuku wa aina zote wa mayainyama na wa kienyeji.4Faida za Chanjo• Chanjo hudhibiti magonjwayanayosababishwa na vimelea vyaaina ya virusi, bektiria, rikesia naprotozoa;• Chanjo huongeza uwezo wamnyama kujikinga na maradhi;• Chanjo hulinda afya ya mifugobaada ya lishe bora na;• Chanjo hudhibiti magonjwayasiyoweza kutibika.Njia na sehemu za kuchanja• Kupitia mdomoni kwa magonjwaya mahepe/mdondo/kideri,Gumboro kwa kuku;• Kwenye bawa kwa ugonjwa wandui kwa kuku;• Chini ya ngozi kwa magonjwakama ya ngozi.Mambo ya kuzingatia katikauchanjajiChanjo zihifadhiwe kwenye haliya ubaridi na zisiwekwe kwenyejoto au mwanga wa jua, wanyamawanaochanjwa ni lazima wawe naafya nzuri na hawajaambukizwamagonjwa yaliyokusudiwa kuchanjwa.Inashauriwa chanjo zifanywe nawataalamu wa mifugo au wafugajiwaliopewa mafunzo ya kuchanja.Chanjo zinaweza kuleta madharaikiwa zitatumiwa wakati muda wakewa matumizi umekwisha (expired).Aidha, chanjo zenye vijidudu vilivyohaizinaweza kuambukiza maradhi kwawanyama waliochanjwa.‘KINGA NI BORA KULIKO TIBA’ .

POPO WA PEMBA Oktoba - Disemba, 2011POPO WA PEMBANa Hashim H. ChandePopo ni viumbe wa ajabu, ambaowatu wanaendelea kubishanakwamba ni ndege au mnyama,lakini pamoja na hayo viumbe hawawanachangia katika utunzaji wamazingira na inakadiriwa kwambakiasi cha asilimia 40 ya miti yamatunda inayoota misituni katikakisiwa cha Pemba husambazwana popo hao.Jumuiya inayohifadhi mazingira kisiwaniPemba “KIDIKE” iliyopo Ole, Wilaya yaWete, Pemba iliyoanzishwa mwaka1992 ni jumuiya ambayo inaendelezakazi ya kuwahifadhi viumbe haoambao ni adimu zaidi duniani na nimiongoni mwa viumbe ambao wakohatarini kutoweka. Kufuatia utafi tiuliofanyika mwaka huo ambaouligundua kuwa kiasi cha popo waPemba 101 tu ndio waliohamia katikamsitu huo mdogo wa Ole Kidike.Hivyo, hatua za kulifanya eneo hilokuwa tengefu zilichukuliwa sambambana kuweka ulinzi na kuwaelimishawanajamii umuhimu wa kuwepo nakuwatunza popo wa Pemba.Katika kuunga mkono juhudi zawananchi hao za uhifadhi wamazingira ikiwemo upandaji wa mitina uhifadhi wa popo wa Pemba ,Mradi wa Usimamizi wa Mazingiraya Bahari na Ukanda wa Pwani(MACEMP) uliwasaidia kutengenezakidungu maalum kwa ajili ya wageniwanaokwenda kuangalia popo hao,ushajiishaji wa uhifadhi wa popowa Pemba kwa kupitia vyombo vyahabari kama vile redio, magazeti natelevisheni, kuwapatia wananchielimu ya mazingira pamoja na uwekajiwa mabango maalum ya utoaji wataarifa zinazotambulisha kuwepo kwasehemu ya uhifadhi, utambulisho wamiti adimu na sehemu za historia zauhifadhi huo.Popo wa Pemba wakiwa katika maeneo yao ya msitu wa Hifadhi Ole Kidikekatika msitu huo kuangalia popo waPemba na uhifadhi wa mazingirapia yanatumika kusaidia maendeleoya jamii.Kuwepo kwa popo hao katika eneohilo kunachangia kwa kiasi kikubwauingiaji wa wageni kutoka nje ya nchikwa ajili ya utalii pamoja na kazi zautafi ti. Mbali na kazi za utafi ti na utaliiinaaminika kwamba asilimia kubwa yapopo wa Pemba wanasaidia harakatiza usambazaji wa mbegu za miti hasaya matunda kama vile miembe namibungo hudondoshwa na popo hao.Popo wa Pemba wanakawaida yakula matunda na kutembea na kokwaza matunda hayo wanapozidondoshandio miti hiyo huota. Kwa kawaidaPopo hao wana uwezo wa kusafi riumbali wa kilomita 15 hadi 20 wakatiwa usiku kutafuta chakula, hivyoinawezekana kabisa kwa popo waKIDIKE akafuata chakula katika msituwa Ngezi na akaangusha mbeguza miti ya matunda katika eneo laLimbani, Wete wakati wa kurudi.popo hao kunaongeza kasi ya uotajiwa miti katika sehemu mbalimbali.Licha ya ongezeko kubwa la popohao katika msitu wa Kidike piaimegundulika kwamba kuna baadhiya maeneo kama vile Wete Bandarini,Msitu wa Ngezi, Kichunjuu Mkoani naMicheweni popo hawa wanapatikanahivyo, ipo haja ya kuzishajiishajamii zinazoishi katika maeneo hayokuanzisha jumuiya za uhifadhi wa popowa Pemba ili kuwalinda popo hao,kwa faida ya jamii husika na serikalikwa lengo la kutunza mazingira nakuongeza pato.Kupatiwa ufadhili huo umeweza piakusaidia harakati za kijamii pembezonimwa hifadhi hiyo kwa kuwawezeshawanajamii kujikusanya pamoja nakuanzisha miradi midogo midogo yakazi za mikono kama vile kutengenezamatenga kwa kutumia muwaa, vyunguna mikoba bidhaa ambazo huwauziawatalii wanaofi ka katika hifadhi hiyona kujiongezea kipato. Aidha, mapatoyanayopatikana kwa kuingia wageniMiti ambayo popo wa Pembawanapendelea kulala ni migulele,misufi , mikungu, milangilangi pamojana miembe ambayo kawaida huwamirefu sana. Hadi kufi kia mwaka2010 inakadiriwa msitu wa Kidikeulikua na popo wasiopungua 7,700 haliinayotokana na mafanikio makubwaya Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingiraya KIDIKE kwa kuwatunza nakuwaendeleza kwani kuongezeka kwa5Popo wa Pemba anavyonekanaakiwa na tunda mdomoni

Matukio kaOktoba - Disemba, 2011MATUKIO KAKaimu Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe. Machano Othman Said wa kwanza kulia, KatibuMkuu wa Wizara hiyo akiwa kushoto na Mwakilishi Mkaazi wa Tanzania wa Shirika laChakula Duniani (WFP) Bwana Richard Ragan wakiwa katika makabidhiano ya kompyutakwa ajili ya kuimarisha kitengo cha utoaji wa taarifa za tahadhari ya mapema cha Idara yaUhakika wa Chakula na lishe.Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya ZanzibaProgramu ya Masoko, Uongezaji thamaniuzinduzi wa Programu hiyo tarehe 30/11/201Hoteli ya Bwawani, Zanzibar.Bwana Khamis Uledi Sheha wa Shehia ya Pujini,Chake Chake - Pemba aliyesimamaakiwaelezea wanashehia umuhimu wa kuanzishwa kwa Kamati za shehia za Uhakika waChakula na Lishe wakati wa uteuzi wa wanajamii 30 uliofanyika katika shehia hiiyo ambaowataisaidia kamati hiyo katika kuibua mradi na utekelezaji wake. tarehe 8/12/20118Wahitimu wa cheti cha kilimo, mkupuo wa tiskupokea vyeti vyao iliyofanyika tarehe 30/12/20

TIKA PICHA Oktoba - Disemba, 2011tika Pichar wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusuna Huduma za Kifedha vijijini wakati wa1 katika ukumbi wa mkutano wa Salama,Mhe. Mwanajuma Majid, Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake akifunguwa mafunzo ya utayarishajiwa mpango kazi wa kamati za Uhakika wa Chakula na Lishe za shehia ya Pujini na Mbuzini,tarehe 4/12/2011 katika Ukumbi wa mkutano wa Uwanja wa Gombani, Pemba, kulia kwake niNdugu. Mzee Rajab mtaalamu wa Lishe wa Idara ya Uhakika wa Chakula na Lishe na kushotokwake ni Ndugu Ali Haji, Mratibu wa FAO- Zanzibar.a na wa kumi wakiwa katika mahafali ya11 katika chuo cha Kilimo, Kizimbani.Ndugu Mberek Rashid Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo akitoa maelezo kuhusu mipango yamaendeleo ya kilimo kwa Mgeni rasmi mama Asha Seif wakati wa maonyesho ya wajasiriamaliyaliyofanyika Tunguu, Wilaya ya Kusini Unguja9

Oktoba - Disemba, 2011MAGHAFALI YA CHUOMAHAFALI YA 1O YA CHUOCHA KILIMO KIZIMBANINa Sabiha KessiChuo cha Kilimo Kizimbanikilicho chini ya Wizara yaKilimo na Maliasili hivi karibunikiliadhimisha mahafali ya kumi kwawanafunzi waliomaliza mafunzoyao ya Astashahada ya Kilimo naMifugo yanayotolewa kwa muda wamiaka miwili.Jumla ya wanafunzi 132wamemaliza mafunzo yao nakutunukiwa vyeti. Mahafali hayoyalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Kaimu Waziri waKilimo na Maliasili, Naibu Waziriwa Afya, Katibu Mkuu wa Wizaraya Kilimo na Maliasili, KatibuMkuu Wizara ya Afya, Katibu MkuuWizara ya Mifugo, Naibu KatibuMkuu Wizara ya Kilimo na Maliasilipamoja na wafanyakazi wa Wizaraya Kilimo na Maliasili.Mgeni Rasmi katika mahafali hayoalikuwa Kaimu Waziri wa Kilimo naMaliasili Mheshimiwa RamadhanAbdalla Shaaban ambae alianzakwa kusema kuwa mwaka wafedha ujao Serikali itaendelea najuhudi zake za kukisaidia Chuocha Kilimo Kizimbani ili kuwezakuimarisha miundombinu pamojana vifaa vya kufundishia.Mhe. Shaaban aliyasema hayowakati alipokua akiwatunuku vyetiwahitimu waliomaliza mafunzoyao ya kilimo na mifugo katikamahafali yaliyofanyika Chuonihapo Kizimbani nje kidogo ya mjiwa Zanzibar.Amesema kuwa tokea MapinduziMatukufu ya Zanzibar ya Januari1964, Serikali ya MapinduziZanzibar imekua ikitoa fursa kubwakwa wakulima kujiendeleza. Katikamsimu huu Serikali kupitia Wizaraya Kilimo na Maliasili imeongezafursa hizo kwa wakulima wadogowadogo kupitia vikundi vya ushirikakwa kuwapatia huduma bora zakilimo, zana za kisasa, kamamatrekta, mbegu bora, mbolea nadawa za kuulia wadudu waharibifuMwenyekiti wa Bodi ya Chuo ya Chuo cha Kilimo, Kizimbani Ndugu. MakameSalum, akipeana mkono na mhitimu baada ya kukabidhiwa cheti chake namgeni rasmi Mhe. Ramadhani A. Shaaban.na magugu kwa bei nafuu.Mhe. Shaaban amesisitiza kuwaSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibarimeanzisha mpango maalumwa mageuzi ya kilimo ambaoumeelekeza kutoa huduma zakilimo na ushauri kwa wakulima iliwaweze kuongeza uzalishaji kwakiwango cha biashara badala yakujikimu.Aidha, amewataka wahitimuhao kuyatumia vizuri mafunzowaliyoyapata kwa kuweza kujiajiriwao wenyewe binafsi badala yakusubiri ajira kutoka Serikalini.Nae Mkurugenzi wa Chuo cha KilimoKizimbani Ndugu MohammedKhamis Rashid amesema kuwaChuo hicho kimeweza kupiga hatuambalimbali zikiwemo upatikanajiwa nyenzo za kutendea kazipamoja na kupata usajili katikabaraza la vyuo Tanzania.Mkurugenzi huyo, amefahamishakuwa pamoja na mafanikioyaliyopatikana chuo hichokinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo upungufu wa vifaa10vya kusomeshea, miundombinupamoja na maabara mamboambayo hurudisha nyuma jitihadaza walimu wakati wa kufundishia.Utoaji wa vyeti kwa wahitimuulifuatiwa na zawadi kwa wanafunzibora na wafanyakazi waliomalizamuda wao wa utumishi chuoni.Wanafunzi bora waliotunukiwazawadi ni Thabit Ali na Ramlat AliHaji.Akiendelea na nasaha zake kwawahitimu na waliohudhuria, Mhe.Shaaban amefahamisha kuwaSerikali ya Umoja wa Kitaifainayoongozwa na CCM inaendeleakutekeleza ilani ya uchaguzi yamwaka 2010-2015 ambapo mojakati ya maelekezo muhimu yaliyomondani ya ilani hiyo ni kukiimarishaChuo ili kiweze kutoa mchangomkubwa katika kuendeleza sektaya kilimo hapa nchini kwani Chuohicho hutoa wataalamu ambaohuwa mstari wa mbele katikakutoa ushauri wa kitaalamu kwawakulima na wafugaji.

TASAF NA USARIFU WA MAZAO Oktoba - Disemba, 2011MCHANGO WA TASAF KATIKAUSARIFU WA MAZAO, MANGAPWANINa Shabaan AbdulmalikMradi wa kusarifu matundana kusindika katikamikebe Shehia ya Mangapwanini mradi wa kundi maalumu lavijana wasio na ajira ambaoumeanzishwa mwaka 2002na kikundi cha kina mamakinachocheza upatu.Mradi huu una wanachamawanane wote wakiwa wanawake.Kina mama hawa walianzakutengeneza achari ya embembichi na mbirimbi kwa njiaza kienyeji bila mafanikio kwakuwa achari hizo zilikuwa hazinaubora na ziliishia kuharibikaBaada ya kupata mafunzokutoka kwa mtaalamu wa usarifuwa matunda wa Wizara ya Kilimona Maliasili, hivi sasa wamepatataaluma ya kutosha juu yakusarifu na kuhifadhi matundaya aina mbalimbali yakiwemomananasi, machungwa, embe,ndimu, mbirimbi, tungule nandizi na inategemea upatikanajiwa matunda katika misimu.Kikundi hicho kwa hivi sasakinaendelea na kazi za usarifuwa matunda, kuyasindikana kuyauza. Miongoni mwamatunda yanayosarifi wa nipamoja na Tungule, Nanasi naChungwa kwa kuyatengenezaJamu, Ndimu na Embehutengeneza achari.Vilevile Tungule hutengenezewachatne, wanatengeneza sosiinayotokana na pilipili naachari ya mbirimbi ya kuanikaViongozi wa Kikundi usarifu wa mazao cha Mangapwani: wakiwa nabidhaa walizozisarifu kutokana na matunda.na kupika mapishi yote hayayanachanganywa na viungomaalumu ambavyo ni virutubishomwilini na vina ladha nzuri.Kina mama hawa kwa kawaidahawatumii kemikali yoyotekatika kusarifu matunda yao.Kikundi hiki cha Mangapwanikimepatiwa jumla ya shilingimilioni 11.9 kutoka Mfuko waMaendeleo ya Jamii TASAF.Aidha, mchango wa nguvu zawanakikundi hiki umepelekeakuongeza nguvu na sasawameweza kujenga Ofi si yao,kununua vifaa vya mapishi nawamepata mafunzo, maalumuambapo hayo yote yamewezakuwaletea mafanikio katikautekelezaji wa kazi zao za kilasiku.Mafanikio mengine waliyoyapata11wanakikundi hawa kupitia TASAFni pamoja na kujitangaza katikamaonesho mbalimbali yakiwemoya nane nane pia wamewezakujifunza mbinu mpya za kazizao na kuongeza kiwango chaushindani kilichopo katikabiashara yao kwa kulingana namahitaji ya soko.Kazi hii ya usarifu wa mazaoimewapatia ajira viongozi nawananchi, hasa baada yakupata vifaa ambavyo kwa sasavinawawezesha kufanya kaziya kutosha ya kulitafuta sokona kuandaa bidhaa kwa ajili yasoko hilo. Hata hivyo, kikundibado kinaendelea kutafutataaluma zaidi ya kusarifu nakuhifadhi matunda ili yawezekutumika kwa muda mrefu nayawe na ubora.

Oktoba - Disemba, 2011USARIFU WA MAZAO YA KILIMOUSARIFU WA MAZAO YA KILIMONa Mussa H. MakameKwa muda mrefu wakulimawa visiwa vya Unguja naPemba wamekuwa na kilio chakukosa soko la uhakika kwamazao yao. Hii ni kwa sababumazao hayo ni ya msimu napia yanakomaa katika kipindikimoja; pia wakulima wengiwanakosa taaluma na nyenzoza kuyahifadhia mazao yao kwamatumizi ya baadae.Taarifa za utafi ti zinaoneshakuwa takriban asilimia 40ya muhogo unaolimwa hapaZanzibar unaharibika auunapotea baada ya kuvunwa.Hali hii pia inawezekana kuwepokwa mazao mengine ambayohayajafanyiwa utafi ti.Hali hii husababisha hasarakwa wakulima pamoja nakukata tamaa kwa vile wanahisikuwa wamepoteza nguvu zaobila ya mafanikio. Tatizo hiliJengo la usarifu wa mazao linaloendelea kujengwa katika kituo cha KilimoKizimbani kwa ajili ya kuwasaida wakulima pamoja na wajasiriamali kupatamafunzo ya usarifu wa mazao ya kilimo.kwa kiasi kikubwa linatokanana kuanguka kwa bei ya mazaohayo hasa wakati wa msimuwa mazao husika mfano zao laEmbe , Machungwa na mazaomengineyo.Mpango wa Taifa wa KukuzaUchumi na Kupunguza Umasikiniumezingatia uwepo wa tatizohili kwa kusema kuwa mfumombaya wa soko la bidhaa zakilimo na upotevu wa kuharibikakwa mazao baada ya kuvunwani miongoni mwa mamboyanayokwamisha maendeleo yaSekta ya Kilimo hapa Zanzibar.Vile vile Sera ya Kilimo yaMwaka 2002 inatilia mkazosuala la uekezaji katika usarifuwa mazao na kuongeza thamanimazao ya Kilimo ili kuwa naukuaji endelevu wa kiuchumi nakupunguza umasikini.Baadhi ya bidhaa zilizosarifi wa na wakulima wa Zanzibar kutokanana mafunzo ya usarifu wa mazao ili kuyaongezea thamani.12Uekezaji katika usarifu wamazao unaweza kuwa ni chanzomuhimu cha kiuchumi na ajirakwa vijana na wanawake pamojana watu wengine ambao kwa njiamoja ama nyengine wamekosaajira katika sekta rasmi; hasakwa vile kilimo pamoja na sektanyengine hazijaweza kutoa ajira

USARIFU WA MAZAO YA KILIMO Oktoba - Disemba, 2011za kutosha kwa wananchi waZanzibar. Hata hivyo watu wengiwana mtazamo mbaya dhidi yabidhaa za kilimo zilizosarifi wana wazalishaji wadogo wadogohapa Zanzibar. Bidhaa hizozinaonekana kuwa ni za kiwangoduni ikilinganishwa na zilezinazotoka nje ya nchi au hataTanzania Bara.Kwa kuzingatia uzito wa tatizohili, Wizara ya Kilimo na Maliasiliya Zanzibar kwa kushirikianana Shirika la Mashirikiano yaKimataifa la Korea (KOICA), ipokatika matayarisho ya Mradi wausarifu wa mazao ya kilimo hapaVisiwani Unguja na Pemba kwanjia ya kisasa.Mradi huo una lengo lakupunguza upotevu wa mazaoya kilimo baada ya kuvunwa,kuongeza chakula na lishe,kukifanya chakula kuwa salamakwa walaji, chakula kukaa kwamuda mrefu bila ya kuharibikasambamba na kupunguzaumasikini wa kipato kwawakulima.Vile vile Mradi huo umelengakuwajengea uwezo wakulima juuya usarifu wa mazao ya kilimona Ujasiriamali pamoja na kutoahuduma za udhibiti wa uborakwa bidhaa zinazozalishwakwa lengo la kuongeza ajira nakipato kwa wazalishaji.cha Kilimo, Kizimbani Wilayaya Magharibi Unguja ambapokimewekwa Jiwe la msingitarehe 7/01/2011 na Makamuwa Pili wa Rais wa ZanzibarMhe. Balozi Seif Ali Idd. katikasherehe za kuadhimisha miaka47 ya Mapinduzi matukufu yaZanzibar ya tarehe 12/01/1964.Kwa sasa mradi wa Usarifu waMazao ya Kilimo unaendeleana utafi ti juu ya hali ya usarifuwa mazao ya kilimo ilivyohapa Zanzibar. Utafi ti huupamoja na mambo mengineutawatambua wajasiriamaliwanaojishughulisha na usarifuwa mazao ya kilimo mahaliwalipo, bidhaa wanazozalisha,uwezo wao wa kuzalisha, vifaana njia wanazotumia kusarifumazao hayo.Pia kuzijua tasisizinazowaendeleza wajasiriamalihao, upatikanaji wa mafunzo naaina ya mafunzo pamoja na kujuahali ya usajili kwa wazalishajihao sambamba na kufahamumatatizo yanayokwamishaukuaji wa biashara zao baadaya kuzalisha ili kutafuta njiamuafaka. Matokeo ya utafi ti huoyatatoa mwanga juu ya namnaya kuwaendeleza wajasiriamalikatika usarifu wa mazao.Matokeo haya yanatarajiwakutolewa mara tu baada yakukamilika kwa utafi ti.Bila shaka utekelezaji wa Mradiusarifu wa mazao ya kilimoutaleta faraja kubwa kwaWakulima na Wajasiriamaliwanaosarifu mazao ya kilimo,sambamba na kuwapunguziaukali wa maisha wakazi wamijini na vijijini kwa kupata fursaya kujiajiri wenyewe. Hata hivyowananchi wenyewe wanapaswakuwa tayari kutumia fursa nahuduma zitakazotolewa katikaKituo cha Usarifu wa Mazao yaKilimo huko Kizimbani.Aidha, hatua inayoendelea hivisasa ni ujenzi wa Kituo chamafunzo ya usarifu wa mazaoya kilimo kwa wakulima pamojana wajasiriamali katika visiwavya Unguja na Pemba. Kituohicho kipo katika eneo la ChuoNdizi zilizoharibika sokoni kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya usarifuwa mazao.13

Oktoba - Disemba, 2011UMWAALIAJI MAJIUMWAGILIAJI MAJI NDANI YA GREENHOUSENa Amour U. VuaiMicro-irrigation huu ni mfumowa umwagiliaji maji wamazao unaofanyika ndani ya eneomaalumu lililojengwa kwa kutumiavifaa vya plastiki au vioo (greenhouse). Mazao yanayozalishwakupitia mfumo huu ni Maua,mboga mboga kama vile Tungule,Pilipili mboga, Matango na mazaomengine. Umwagiliaji huu ni wakisasa na hufanyika zaidi katikanchi zilizoendelea, hata hivyohivi sasa umeanza kueleweka nakutumika katika baadhi ya maeneoya wakulima wa Zanzibar.Awali ukulima huu ulikuwaukifanyika kwenye maeneo ya utaliikwa upandaji wa maua Kiwengwa.Kwa vile visiwa vya Zanzibar vinauchache wa ardhi kama ilivyokwenye visiwa vyengine duniani,kilimo hiki kinahitajika sana, kwaniwakulima wanaweza kutumia eneodogo kwa kuzalisha mazao mengina bora.Faida zinazopatikana kwaumwagiliaji maji ndani ya greenhouse:• Kupata mavuno makubwa nayenye ubora;Greenhouse inayotumiwa na ndugu Othman Omar Juma mkulima waMasingini, Wilaya ya Magharibi Unguja katika kuimarisha kilimo chambogamboga cha umwagiliaji maji.• Maradhi na wadudu waharibifuni rahisi kudhibitiwa;• Matumizi madogo ya kemikali;• Hauhitaji wafanyakazi wengikatika kuhudumia;• Huleta ufanisi mkubwa katikautumiaji maji;• Unaweza kuchanganya maji nambolea;• Hupunguza ukuwaji wa maguguna;• Unatumia njia ya kilimo chakisasa.Hasara za umwagiliaji majindani ya greenhouse.• Gharama za kuanzia ni kubwa;• Unahitaji utaalamu ilikuendesha mfumo huu;• Mkusanyiko wa chumvi kwenyesehemu zinazoroa majihupelekea kufa kwa mimea.Aina za greenhouse1. Greenhouse za nyumbani(home greenhouse)2. Greenhouse za kusimama (freestand structure)Greenhouse za nyumbaniAina hizi za greenhouse maranyingi huwa maeneo ya nyumbani,pia zinaweza kushikana na ukutawa nyumba kwa upande mmojana upande mwengine kubakiapaa (top sheet) kuelekea upandewa chini, ambalo ni maalumukwa kupunguza mionzi ya jua namatone ya mvua.Mitungule iliyopandwa ndani ya greenhouse ya mkulima wa mboga mbogawa Masingini.14Ukubwa wa greenhouseunategemea na upatikanaji wavifaa kutoka katika kiwanda husikalakini kiwango cha kawaida ni mita

BONDE LA MWEMBE MSALA, KIANGA Oktoba - Disemba, 2011MAFANIKIO YA UMWAGILIAJI MAJI WABONDE LA KIANGA MWEMBE MSALANa Shaaban A. MalikMradi wa Kilimo chaUmwagiliaji maji Shehiaya Kianga – Mwembe msala nimradi wa kusaidia wanajamiiwenye uwezo wa kufanya kazilakini hali zao za maisha niza kipato cha chini. Mradihuu uliopo Shehia ya Kiangaunawashirikisha wanajamiiwapatao 100 wakiwemowanawake asilimia 70. Uzinduziwa mradi huu ulifanyika rasmimwezi wa Agosti 2011 nakuanza utekelezaji mwezi huohuo 2011.Bonde la Kilimo KiangaMwembe Msala ni kwa ajiliya Kilimo cha Mpunga naMbogamboga kwa kumwagiliamaji kutoka katika chemchemza asili zilizopo eneo hilo,pamoja na kuwepo kwa vyanzohivyo vya maji wananchi waeneo hilo walikuwa wakilimakwa tabu, mara mojakwa mwaka kutokana nakutokuwepo kwa miundombinuya kusafi risha na kusambazamaji katika mashamba yao.Hivi sasa Bonde la KiangaMwembe Msala lina jumlaya mita 450 za Mtaro wasaruji na milango ya kudhibitimaji ambayo yanasafi rishwakutoka katika vianzio mpakakwenye mashamba kwa mudamfupi. Wakulima wa eneo hilisasa wanalima Mpunga nambogamboga mara tatu kwaWakulima wa bonde la Kianga Mwembe msala wakiwa katika ujenziwa mtaro wa kumwagilia maji.mwaka ambapo wana uhakikawa kupata chakula chao. Piamaeneo yote yaliyozungukabonde na vianzio vyamaji yamepandwa miti nayanalindwa kwa uhifadhi wamazingira. Wananchi wa eneohilo kupitia programu ya TASAFwamepatiwa elimu ya kuhifadhifedha, usimamizi wa miradi namaarifa ya kuhifadhi mazingirana vyanzo vya maji.Kazi kubwa iliyofanywa namradi huu ni kuimarishamiundombinu ya umwagiliajiikiwemo uhifadhi wachemchem za maji na ujenziwa mitaro ya saruji kwa ajili yakumwagilia maji mashambaya mpunga na mbogambogayapatayo ekari 60.TASAF imetoa mafunzo ya15usimamizi wa fedha na miradikwa walengwa wa mradihuu pamoja na kuwapatiafedha za matumizi baada yakumaliza kiasi fulani cha kaziili kujikimu kimaisha. Jumla yashilingi milioni 16. 6 zilitumikakuwalipa walengwa hao ikiwani asilimia 50 ya gharama zamradi huo.Mafanikio ya Mradi waUmwagiliaji Kianga MwembeMsala yametokana na msaadawa shilingi milioni 33.3 kutokaTASAF na wananchi walipataposho dogo la kusaidia maishayao, kiasi chengine cha fedhawakaweza kununua vifaa nakutekeleza kazi walizojipangiakwa wakati. Mategemeomakubwa waliyokuwa nayoya kujitegemea kwa chakulana fedha yaliwapa ari ya

Toleo la NaneOktoba - Disemba, 2011utekelezaji wa mradi wao.Mafanikio mengine ya mkulimammoja mmoja yanasimuliwana Mzee Mussa MalechaMafula ni mzee wa makamoambae ni mkulima wa matangokatika eneo la Kianga mwembemsala, anasema katika eneolake dogo anavuna vipolo 10hadi 13 kwa siku na mavuno nikila baada ya siku moja, bei yakipolo cha matango wakati wamsimu mzuri shilingi 30,000,maana yake ni kuwa kilabaada ya siku moja mzee huyuanafanya mauzo ya shilingi300,000.Aidha, wakulima wa eneo hiliwameanza kuiga na kujifunzamaarifa ya ukulima wambogamboga kutoka kwa mzeehuyo pamoja na usimamizi waAfi sa wa elimu kwa wakulimawa eneo hilo, kwani hapo kablaeneo hilo lilikuwa likiachwabila kulimwa baada ya mavunoya mpunga, sasa wakulimawengi wamejifunza na kwasababu ya miundombinuiliopo eneo kubwa linalimwambogamboga.Mzee Malecha sasa anauhakika wa chakula chake,akiba na mahitaji muhimu yamaisha yake pia amewezaWakulima wakifarijika kutokana na miundombinu bora yaumwagiliaji maji katika bonde la Kianga Muembe msala.kuajiri watu wengine katikashamba lake.Hapana shaka kama utafi kakatika eneo la Kianga mwembeMsala utaona mabadilikomakubwa kutokana na kuwepokwa mradi wa wananchiuliosaidiwa na TASAF,kuwepo kwa miundombinu yakumwagilia kumesababishamaji kuenea katika mashambakwa ufanisi. Aidha, wakulimawamejifunza matumizi yambegu bora na mbolea,mpango wa kilimo cha kisasa,usimamizi na matengenezoya mfumo wa kumwagilia.Wakulima wa Mwembe msalapia wameanzisha Jumuiya yawatumiaji wa maji ambayoina dhamana ya uendeshaji,matengenezo na usimamizi.Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar kupitia Wizara yaKilimo na Maliasili imewekawataalamu wa kilimo chakumwagilia kusaidia sehemuhiyo.Uongozi wa bonde la Kiangamwembe msala umesema:ni muhimu kuhakikishavyanzo vya maji vinalindwana kuhifadhiwa kwa matumiziendelevu. Kwahiyo watajitahidikuendelea kutafuta utaalamuwa uzalishaji pamoja namasoko kwa bidhaa zao.GAZETI HILI HUTOLEWA KILA BAADA YA MIEZI MITATU NAWIZARA YA KILIMO NA MALIASILI - ZANZIBARP. O. Box 159 Zanzibar, Simu: +255 24 2230986, Fax: +255 24 2234650Barua pepe: kilimo@zanlink.com, Tovuti: www.kilimoznz.or.tz

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!