La pili ni kwamba, Mkandarasi huyu amechukua kokoto na mawe, kazi ambayo imefanywa naakina mama na wananchi wanaolima barabara wote hawajalipwa mpaka leo. Sasa Mheshimiwa Wazirihaoni kwamba ipo haja ya kwenda kuona kazi hiyo? Lakini vile vile anaweza kulithibitishia Bunge hilikwamba atawaagiza wataalam wake katika kipindi cha wiki mbili aende akalipe madeni ya akina mamakule Mahenge? (Makofi/Kicheko)WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, napendakumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia kwa karibu sana masuala mengi ya maendeleo katikaJimbo lake. Lakini niseme kwamba, tathmini haitachukua muda mrefu kwa sababu kazi imeshaanza nainabidi iendelee. Lakini tutazingatia mawazo aliyoyatoa Mheshimiwa Mbunge, ambaye yuko katika eneohilo na mimi binafsi nitawaagiza watu wangu wafike huko na kuona kazi inavyoendelea. (Makofi)Na.48Walimu Wanaofundisha VijijiniMHE. VENANCE M. MWAMOTO aliuliza:-Kwa kuwa walimu wanaofundisha Vijijini wanaishi katika mazingira magumu sana na taabu nakwa kuwa wengi wanaopangiwa huko huacha kazi, je, Serikali haioni ni vizuri mishahara ya walimu waVijijini ikaongezwa kama motisha na kuwa kivutio kizuri?WAZIRI WA ELIMU NA UTAMADUNI alijibu:-Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Venance Methusalah Mwamoto,Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, kuna baadhi ya walimuwanaoishi katika mazingira magumu hususan wale wanaofundisha katika Shule za Vijiji vya mbali,visivyofikika kwa urahisi. Lakini Wizara yangu haina takwimu zinazoonesha kuwa kuna walimuwalioacha kazi kutokana na mazingira hayo magumu ingawa inafahamika wako ambao hukwepa kuripotiwakipangwa huko.Aidha, Wizara yangu inafuatilia kwa karibu matatizo yote ya walimu yakiwemo ya mazingiramagumu kama vile ya uhaba wa nyumba za kuishi, shida ya maji na ugumu wa njia za usafiri namawasiliano. Suluhisho la kudumu ni upatikanaji wa huduma hizo muhimu na za jamii utakaomwezeshamwalimu kufundisha katika mazingira mazuri. Kwa kutambua hilo, Serikali kwa kupitia Mpango waMaendeleo ya Elimu ya Msingi (2002 - 2006), inatoa Ruzuku ya Maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa ainazote za majengo ya shule pamoja na nyumba za walimu.Katika mwaka wa kwanza na wa pili wa MMEM yamejengwa madarasa 31,825, nyumba zawalimu 7,530 na matangi ya maji katika baadhi ya shule kuliko na shida kubwa ya maji. Aidha, Wilaya 51zilizokuwa katika programu ya DBSPE zilipatiwa baiskeli zipatazo 6,234 ili kuwarahisishia walimu usafirikwenda kujiendeleza katika Vituo vya Walimu yaani Teachers Resources Centres.Mheshimiwa Spika, huo ni ushahidi wa hatua zinazochukuliwa na Serikali kupunguza adha yamaisha kwa walimu. Kwa hiyo, Serikali haina mpango wa kuongeza mishahara ya walimu wanaofundishakatika shule za Vijiji vya mbali kwa sababu katika Vijiji hivyo wako pia watumishi wengine wa Serikalipamoja na wananchi tunaowatumikia wanaokabiliwa na uduni wa maisha kama walimu. Kwa hiyo, haliitakaporuhusu, Serikali itaongeza mishahara kwa watumishi wote nchini wakiwemo walimu kamailivyofanya kuanzia Julai, 2003.MHE. ATHUMANI S. M. JANGUO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi yakuuliza swali la nyongeza. Ningependa kumwuliza Mheshimiwa Waziri, kwa kutambua uchache wawalimu na kwa kuwa walimu wa Vijijini wako katika mazingira ambayo yamesemwa na mwuliza swali la
msingi, je, Mheshimiwa Waziri haoni kwamba kama si kuwalipa mishahara basi wapewe posho maalumambayo itakuwa kivutio cha kwenda kule Vijijini? (Makofi)WAZIRI WA ELIMU NA UTAMADUNI: Mheshimiwa Spika, kuhusu kutambua uchache wawalimu, hili linafahamika katika Serikali na pia ndani ya Bunge hili, ndio maana katika Mpango waMMEM imepangwa kufundisha na kuajiri walimu wapya 45,000 na tayari katika miaka miwili ya mwanzoya MMEM tumeajiri walimu 25,000 wakiwemo wale 15,000 waliokuwa wana vyeti mwaka 2000wakisubiri ajira. Kwa hiyo, kero ya kusubiri ajira tumeimaliza kabisa.Pia mwaka 2003 walimu wapya waliotoka katika Vyuo ni 15,000 ambao tena wamepangiwakatika Wilaya mbalimbali kwenda kupunguza uhaba huo. Kwa hiyo, uhaba wa walimu uliopotunaushughulikia kwa kufundisha na kuajiri walimu wapya. Tatizo nililolisema pale mwanzo, hataukiweka posho maalum kwa walimu katika maeneo magumu, bado itabidi kama Serikali tujibu watumishiwengine wa Serikali walio katika maeneo hayo hayo na wanafanya kazi. Waingereza wanasema: "What isgood for the goods is good for the gender". Unachoona kizuri kwa mmoja na kwa mwingine ndani yaSerikali itabidi kiwe kizuri hivyo hivyo kwa sababu wanafanya kazi katika mazingira yanayofanana.(Makofi)Na.49Barabara ya Mlali - Makutupa - Mang’wetaMHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:-Kwa kuwa barabara ya kutoka Mpwapwa hadi Mlali kupitia Vijiji vya Lupeta, Makutupa, Mbori,Mang’weta, chamkoroma Suguta hadi Mlali ni mbaya sana; na kwa kuwa Serikali imefanya kazi nzuri yakutengeneza barabara ya Lupeta hadi Makutupa yenye urefu wa Kilometa 7.5 na pia kutengeneza barabaraya Chamkoroma hadi Mang’weta Kilometa tano:-(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza eneo la barabara lililobaki kuanziaMakutupa hadi Mang’weta yenye urefu wa Kilometa 15 ili kuunganisha barabara hiyo muhimu kiuchumi?(b) Je, Serikali itakubaliana nami kwamba iwapo barabara ya Makutupa - Mang’weta kupitiaMbori itatengenzwa, eneo kubwa la barabara ya kutoka Mpwapwa hadi Mlali itakuwa imefanyiwamatengenezo na kupitika bila matatizo yoyote?NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa George Lubeleje, Mbunge waMpwapwa, napenda kutoa maelezo mafupi kama ifuatavyo:-Barabara ya Ng’ambi kwenda Mpwapwa - Mlali hadi Pandambili inayopita kwenye Vijiji vyaLupeta, Makutupa, Mboli, Mang’weta, Chamkoroma na Suguta inahudumiwa na Wizara ya Ujenzi kupitiaWakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dodoma. Barabara hii ina jumla ya urefu wa Kilometa 105.Katika mwaka wa fedha 2002/2003, sehemu ya barabara hii ya Lupeta hadi Makutupa jumla yaKilometa 7.5 zilifanyiwa matengenezo ya dharura na kati ya Chamkoroma hadi Suguta jumla ya Kilometa6.9 zilifanyiwa matengenezo ya sehemu korofi hivyo kubakiza kipande cha urefu wa Kilometa 48.6kuanzia Makutupa hadi Mang’weta na Chamkoroma hadi Suguta na Mlali hadi Pandambili kilometa 19.4,hizi hazipo katika hali nzuri.Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo mafupi, napenda sasa kujibu swali la MheshimiwaGeorge Lubeleje, Mbunge wa Mpwapwa, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-(a) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kufanya matengenezo sehemu hiiya barabara inayojumuisha eneo kati ya Makutupa hadi Mang’weta pamoja na kuendelea kufanyia
- Page 1 and 2: BUNGE LA TANZANIA_______________MAJ
- Page 3: jana tarehe 5 Februari, 2004, suala
- Page 9 and 10: (a) Je, Serikali ina mpango gani wa
- Page 11 and 12: mambo mengine, umebainisha kwamba S
- Page 13 and 14: La pili, kama itakuwa Chuo Kikuu je
- Page 15 and 16: Na. 54Mikoa isiyo na Viwanda Nchini
- Page 17 and 18: (c) Mheshimiwa Spika, napenda kumha
- Page 19 and 20: kutumia dawa ya kujipaka mwilini, k
- Page 22 and 23: Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mb
- Page 24 and 25: HON. AMBASSADOR GETRUDE I. MONGELLA
- Page 26 and 27: DEPUTY SPEAKER: Honorable Omar Mjak
- Page 28 and 29: DEPUTY SPEAKER: Honorable Kidawa Ha
- Page 30 and 31: DEPUTY SPEAKER: Honorable Dr. Amani
- Page 32 and 33: I think the issue is stipulated cle
- Page 34 and 35: I do feel that the experience and e
- Page 36 and 37: DEPUTY SPEAKER: Don’t...HON. GEOR
- Page 38 and 39: I come to you with considerable exp
- Page 40 and 41: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema h
- Page 42 and 43: Kwa hiyo, sisi hatujawahi kuona suk
- Page 44 and 45: Vile vile Mheshimiwa Dr. Juma Ngaso
- Page 46 and 47: Kundi la Wanawake walikuwa wagombea
- Page 48 and 49: vikaweza kuingia katika soko jipya
- Page 50 and 51: Mheshimiwa Naibu Spika, haya ninayo
- Page 52 and 53: ambayo tunaona yanaweza kuleta atha
- Page 54 and 55: kweli waweze kuchambua ili tusije t
- Page 56 and 57:
Nikaona hii labda hii Kiswahili cha
- Page 58 and 59:
Naomba nichukue nafasi hii kumponge
- Page 60 and 61:
kwa sheria ya Bunge hili kwamba Mak
- Page 62 and 63:
General Tyre kinaendelea kufanya ka
- Page 64 and 65:
Mheshimiwa Naibu Spika, juzi niliku
- Page 66 and 67:
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo na
- Page 68:
Sasa kutokana na hayo mimi nafikiri