10.07.2015 Views

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

watu wataelewa hivyo na ndivyo ilivyosemwa leo asubuhi katika redio na wengine wamechangia hapa ,nimesikia bado wanarudi huko huko dumping kwa maana ya kutupa. Kwa hiyo, ikiwa sisi wenyewehatujaelewa wananchi wataelewa vipi? Naomba liangaliwe, kama kuna jina lingine ambalo litatumikabadala yake ili watu waweze kuelewa vizuri zaidi na kwa maana inayokusudiwa.Mheshimiwa Naibu Spika, kuna vitu ambavyo tunahitaji nchini, kuna vitu ambavyo kweli tunavyokatika viwanda vyetu kama tulivyosema mfano sukari. Sukari sasa hivi tunayo ya kutosha, hivyo tunawezakumlinda, tukakataza kuingiza sukari hapa nchini. Lakini vile vile kutokana na huu utandawazi hakunasababu ya kukataza kuingiza sukari, si unaongeza kodi tu. (Makofi)Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri atakubaliana na mimi kwamba asilimia zaidi ya tisini ya kodihii tunayookota bilioni 120 sasa hivi kwa mwezi inapatikana Dar es Salaam na Dar es Salaam kwa maanaya bidhaa zinazoingizwa bandarini. Kwa hiyo, kwa maana hiyo kwamba vile vitu vinawekwa kodi na ilekodi sasa ndiyo hiyo inayotusaidia sasa hivi, asilimia kama kumi tu ndiyo nchi nzima inalipa, lakiniasilimia zaidi ya tisini inapatikana Dar es Salaam kwa maana ya bandari. Kwa mfano matairi, tairi moja laGeneral Tyre la size 12 ni shilingi 220,000/=, lakini tairi moja la Michelin la size hiyo hiyo ni shilingi500,000/=, lakini mtu anakwenda kununua tairi hiyo ya Michelin ya shilingi laki tano, anaacha tairi laGeneral Tyre la shilingi 220,000/= na hayo mambo tuyaangalie kabla hatujapitisha hii sheria, kwambamadhara yatakuwa vipi, kwa nini huyu mtu tairi ya size 12 ananunua kwa shilingi laki tano anaacha hili laGeneral Tyre linalouzwa kwa shilingi 220,000?Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hayo kama hatuyaangalii tutasema zuia matairi ya nje, kila sikumagari yatapata ajali hapa, kwa matairi hafifu tutakufa Watanzania. Kwa hiyo, ninachosema sheria yakulinda bidhaa ni nzuri sana tuwe macho. Niliona jinsi Sweden au Denmark nchi za Scandinaviawanavyolinda viwanda vyao na vitu vyao lakini walichokifanya ni nini? Yaani huingizi vitu lakini vile vilehuwezi kununua shati Denmark ukaja kuliuza hapa Tanzania, haliuziki bei ni kubwa sana. Huwezikununua chochote kule, lakini wao wananunua, wanafanyaje? Mshahara kima cha chini kule ni shilingimilioni mbili na nusu, kwa hiyo na vitu wakajiongezea bei. Sasa wewe mgeni ukifika pale kichwa kichwana dola zako mia tano hununui kitu pale, kwanza wanakushangaa. (Kicheko)Mheshimiwa Naibu Spika, nina maana gani hapa, nchi inatakiwa iwe katika hali hiyo ya kwambasasa tunapofanya hiki huyu anayetakiwa kufanyiwa tunamfanyaje ili afanane fanane katika misingi hiyokama walivyokuwa wale wa Denmark. Sasa wanaishi vizuri wanakushangaa wewe unayesema kitu hiki nighali. Niliuliza kalamu ya kawaida tu pale Amsterdam nikaambiwa shilingi laki tatu mpaka laki tano kwaexchange rate ya hapa, dola 560. Sasa hapa ukimwambia mtu dukani si atakushangaa atasema labda yadhahabu. Kwa hiyo, nilitaka vitu hivi viangaliwe kwa mapana kabla ya kuweka sheria ambayo labdainaweza kutuumiza, lakini kulinda bidhaa za ndani kama zipo mimi nakubaliana nayo. (Makofi)Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tuangalie bidhaa zinazotoa ruzuku. Nilikuwa nimezungumziamagunia hapa. Kweli niliambiwa magunia ya katani ni magumu na yana nguvu na yanadumu. Wala sinaubishi na hilo ni magumu, yana nguvu na yana dumu lakini hayo magunia huwezi kuweka unga, ulezi aumchele, labda uweke korosho ambazo hazijabanguliwa kwa sababu yana matundu makubwa, unawezakuingiza vidole. Hayapo kama hayo tunayosema sisi ni mabaya. Kwa hiyo, sasa ndiyo maana watuwanakimbilia hayo ya jute, lakini hata hivyo hilo la kwetu la katani ya hapa bei yake sasa ni hatari.Mimi nilimwuliza Mheshimiwa Waziri wa Fedha, akasema kule Bangladesh wana subsidy 50%fine, lakini Bangladesh ni nchi maskini kama Tanzania. Sisi ni nini kinatufanya tusi-subsidy, tutasemahatuna hela, sasa wale wenzetu mbona nao ni maskini? Tuangalie vitu vinavyoweza kusaidiwa kwa namnaya pekee ya ku-subsidy. Kama wanatunyima hao wakubwa kutoa ruzuku basi tuangalie namna ya kufanyahizo incentives tunazosema kwamba umsamehe kodi, automatic unakuwa tayari umekwisha subsidy kwanamna moja au mbili. Lakini kama tutakwenda hivi hivi, kichwa kichwa, tutasema hatuwapi sasa nibiashara wakulima mfanye hivyo, ndugu zangu tutaendelea kuvaa mitumba, tutakuwa Wamachinga,tutakuwa tunafukuzana na Polisi Dar es Salaam, tutashindwa kurudi kulima na nchi itakuwa maskini,maskini kabisa.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!