vikaweza kuingia katika soko jipya kwa haraka sana, wanatumia mbinu mbalimbali za kujitanua. Kwahiyo, dhamira yao kubwa wao ni kuua viwanda vya nchi ndogo kama zetu zinazoendelea wakatanuaviwanda vyao. Sasa basi, tukisema tunaachilia tu hivi viwanda, kusema kweli bila kuvilinda ni kama mtuambaye umejenga nyumba nzuri ambayo haina ua wa kuikinga na wakati wowote inaweza kupata madharayoyote.Kwa hiyo, tunavilinda viwanda vyetu kutokana na madhara haya na katika mazungumzo yetubaadhi yetu wanafikiria kwamba unapolinda viwanda labda hufanyi lile linalotakiwa. Unapolinda viwandakusema kweli unalinda viwanda vyetu, unalinda uchumi wetu kwa sababu kama nilivyosema zaidi yakuleta ajira, zaidi ya kusaidia sekta nyingine za uchumi kukua, viwanda hivi pia vinawezesha kupata fedhaza kigeni nyingi na manufaa mengine mengi sana ya kiuchumi.Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo haya ni masuala muhimu ambayo inafaa tuyazingatie. Sasahivi tuko katika dunia ya utandawazi kama nilivyosema. Dunia ya utandawazi, bidhaa katika sokozinakwenda kwa ushindani ulio halali na ushindani usio halali. Sisi hapa najaribu kuzuia, ni kuzuiaushindani ambao sio halali na baadhi yetu wamekuwa wakidhani kwamba labda pale tunaposema kwambatunataka bei au Wizara au Serikali inataka bei isiwe ndogo zaidi kuliko ile ya kawaida, ni pale ambapo beiya bidhaa zinazohusika ni kwamba inauzwa kwa bei ya kawaida lakini katika kuingia katika soko fulaniwameteremsha bei ili walete madhara kwa viwanda hivyo na sisi hapa huu Muswada una madhumuni yakuzuia hilo lisitokee.Kusema kweli hili ndilo jambo linalofanyika duniani kote sasa hivi na kwa kuwa Tanzania niwanachama wa World Trade Organization na World Trade Organization ina sheria na kanuni nyingiambazo wanachama wake wanastahili wazifuate ili kuwa na biashara nzuri duniani yenye kuwafaidiawanachama na kuwafaidia wanachama wengine wote, hivyo basi panapokuwa na fursa kama hii ya kuwepona sheria kama hii, inabidi sisi tuchukue fursa ile bila kuzubaa. Inabidi tuchangamkie kwa sababutusipoichangamkia hatutakuwa na uwezo wa kulinda viwanda vyetu, hatutakuwa na uwezo wa kuvutiauwekezaji kwa sababu pasipokuwepo na sheria hii, hata soko la ndani tutashindwa kulilinda, hatawazalishaji wa ndani tutashindwa kuwalinda. Kwa hiyo, itakuwa ni soko la holela tu limeingiliwa bilautaratibu mzuri unaotakiwa katika kufanya biashara za Kimataifa.Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tunaposema hivi, hatusemi kwamba basi tuviachie viwandavyetu, tuvihami bila kufanya shughuli yoyote ambayo inatakiwa ili vifanye kazi zake barabara. Viwandavyetu viko katika dunia yetu ya sasa hivi ambayo ni ya utandawazi ambayo inaendeshwa kwa misingi yabiashara huria, ambayo inaendeshwa kwa misingi ya kushindana. Hivyo basi, ni matumaini yetu kwambaviwanda vyetu havitazorota pale ambapo tutapata habari kwamba Serikali inavilinda viwanda hivyo, itazidikushindana na wengine ili wananchi waweze kupata huduma nzuri, kupata bidhaa zenye hali nzuri nakupata bei halali kwa bidhaa zao wanazozihitaji. Hii hatua inachukuliwa tu kulindwa kwa bidhaa zilezinazofanana na hizo ambazo zinatoka nje.Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kama unavyojua tayari baadhi ya viwanda vyetuvimeshaathirika kwa kiasi fulani kutokana na dumping. Tumezungumza na tunajua Viwanda vya Nguovinaathirika, Viwanda vya Ngozi kwa namna fulani, Mafuta, Magunia yameathirika kwa kiasi fulani; sasahaya ni mambo ambayo si mazuri tuyaache yaendelee. Mimi nashauri Muswada huu tuupitishe ili uwesheria na unapokuwa sheria tuanze kufanya kazi mara moja. Sisi tumeona adha nyingi sana kwa mfanoViwanda vya Magunia, sasa hivi kuna mkonge mwingi tunauchoma badala ya kuwapa wananchi wetu ajirabadala yake tunachoma. Tunapoteza fedha ile, tunaagiza magunia mengine kutoka nje (magunia ya jute),kule wanaolima tunawaachisha kazi. Kwa hiyo, ni kitu kibaya sana. Viwanda vya Nguo navyo vina atharikama hizo.Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nashauri, nawasihi ndugu zangu kwamba tafadhalini sanaMuswada huu tuuchukulie katika hali ya kujua kwamba tunafanya kwa madhumuni ya kulinda viwandavyetu kwa madhumuni ya kuwaendeleza watu wetu. Kwa hiyo, naunga mkono hoja hii asilimia mia mojana nashauri ndugu zangu wote tuunge mkono na tuutakie kheri utekelezaji wake uwe wa makini ili tuwezekuvihami viwanda vyetu na uchumi wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)MHE. BENEDICTO M. MUTUNGIREHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipanafasi ya kuchangia katika Muswada ulipo mbele yetu. Nitaomba radhi kidogo kwa sababu kwa haliilivyokuwa asubuhi, nataka kuwapongeza wenzangu ambao wameshindwa kwa kishindo kuwa katikaBunge la Afrika. Nawapongeza sana. (Makofi)Vile vile napenda kuwapongeza ambao hata mimi hawakunichagua kwa sababu tulikuwa wengi,sasa nisingeweza kujipendelea kwamba kura zote wanipe mimi na pengine labda ni kutokana na udhaifuambao waliona ninao. (Makofi)Mwisho kabisa niwapongeze wale wote ambao walinipa kura zao kwa sababu nilidhani tungepigakichama, basi mimi ningepata kura nne au tano, lakini niliweza kupata kura 25. Kwa hiyo, nawashukurusana hawa ambao walikuwa courageous enough kunichagua. (Makofi)Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuyasema hayo, nadhani sasa nitajirekebisha maana yakewaliniambia kwamba sauti yangu inatisha kweli! Hata Bungeni huwa wananiuliza mbona tunakuonamwembamba halafu sauti ni kubwa sana? Lakini ndio hivyo, ila nitaomba radhi kwamba walewanaodhani kwamba ninakuwa na sauti nitakapokuwa nazungumza kukawa hakuna hoja wawewananiandikia ki-memo kwamba hapo you are out of point ili niweze kujirekebisha, lakini vinginevyoargument ina argument. (Kicheko)Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuyasema hayo, naunga mkono Muswada huu. (Makofi)Mheshimiwa Naibu Spika, jana tumepata Semina nikapata kuelewa kwa undani na kwambawengine tulijaribu kutaka kuchanganya kwamba Muswada huu basi ulikuwa ndio mwarubaini wa ku-covermatatizo yote yanayotokana na aina za dumping wengine ambao tulikuwa hatujawa-aware. Lakinikatika maelezo ambayo yametoka na kwa kuwa hii inahusu viwanda kama alivyosisitiza MheshimiwaWaziri mhusika jana, ningependa tu kutoa tahadhari kwamba viwanda kama viwanda haviwezi kuwepo inisolation na kinachopelekea dumping pengine ni connections za vitu mbalimbali ambavyo nikuanzia hata ile nchi ambayo inataka ku-dump hizo materials zake katika nchi yetu. Maana naelewailizungumzwa jana na pengine kwenye Muswada kwamba nchi za Ulaya na nchi nyingine pamoja nasababu inayowafanya wateremshe bei za bidhaa zao kwa makusudio ya kutaka kwanza watulainishewaweze kupata soko ili hatimaye sasa waweze kupandisha bei. Sababu ya kwanza ni kwamba pamoja namambo mengine wanatoa ruzuku kwa bidhaa ambazo wanazozitumia katika kutengeneza hizo bidhaa zao.Sasa kama hivyo ndivyo, kumbe hoja ya msingi haianzii kwenye kiwanda per se, inaanzia katika mkururona mlolongo mzima wa uzalishaji. Kama ni suala la subsidy libaki linaanzia huko kwingine. Sasatahadhari ambayo nataka kuiweka ili na sisi tuielewe na tuweze kufanya kazi kwa pamoja na wale waliokokwenye Serikali waweze kuona kwamba sekta hizi zinategemeana, maana kama tunazungumza suala laviwanda vya nguo vya Tanzania, wamezungumza Waheshimiwa kuhusu masuala ya umeme, lakiniutazungumza vile vile kuhusu masuala ya pamba. Ubora wake, halafu hivyo viwanda vinavyotengenezahiyo pamba vinawasaidiaje Watanzania wanaolima pamba ili kuweza kuongeza pato lao?Pia ikawekwa kwenye Muswada kwamba anayepaswa kulalamika sasa ni mtu mwingine hatakama sio mwenye kiwanda au mtu ambaye anaona kwamba kwa kufanya hivi, wale wanaofanya dampingyao hapa wanasababisha sisi viwanda vyetu visilipe kodi na mambo mengine. Sasa kama mimi ninalimahalafu naona watu fulani wanaleta zile khanga za India, lakini kwa vitendo vyao hivyo vinasababisha mimipamba yangu isiweze kununulika, sijui nitakuwa na haki ya kunung’unika au sitakuwa na haki yakunung’unika! Lingine niliseme kabla sijaingia ndani kabisa kwenye Muswada wenyewe kipengele kwakipengele, hilo la subsidy mimi ningependa kutoa caution, huenda nikabishiwa kwamba sio kweli, lakinisasa hivi tulipokumbwa na njaa nina uhakika Serikali inataka kuleta Muswada hapa tuongeze bajeti. Hizohela tungesema tuziweke huko tuzitumie tukasie kabla njaa haijaja, tumwagilie na tuwape motishawakulima, nadhani tungegombana kwamba hela haziko. Sasa kama inafika mahali mtu unauguliwa mtotounaambiwa twende tukamtibu unasema mimi siwezi kuuza mbuzi wangu, halafu anakufa wewe unachinjambuzi ili ule kwenye msiba si vizuri. (Kicheko)
- Page 1 and 2: BUNGE LA TANZANIA_______________MAJ
- Page 3: jana tarehe 5 Februari, 2004, suala
- Page 6 and 7: La pili ni kwamba, Mkandarasi huyu
- Page 9 and 10: (a) Je, Serikali ina mpango gani wa
- Page 11 and 12: mambo mengine, umebainisha kwamba S
- Page 13 and 14: La pili, kama itakuwa Chuo Kikuu je
- Page 15 and 16: Na. 54Mikoa isiyo na Viwanda Nchini
- Page 17 and 18: (c) Mheshimiwa Spika, napenda kumha
- Page 19 and 20: kutumia dawa ya kujipaka mwilini, k
- Page 22 and 23: Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mb
- Page 24 and 25: HON. AMBASSADOR GETRUDE I. MONGELLA
- Page 26 and 27: DEPUTY SPEAKER: Honorable Omar Mjak
- Page 28 and 29: DEPUTY SPEAKER: Honorable Kidawa Ha
- Page 30 and 31: DEPUTY SPEAKER: Honorable Dr. Amani
- Page 32 and 33: I think the issue is stipulated cle
- Page 34 and 35: I do feel that the experience and e
- Page 36 and 37: DEPUTY SPEAKER: Don’t...HON. GEOR
- Page 38 and 39: I come to you with considerable exp
- Page 40 and 41: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema h
- Page 42 and 43: Kwa hiyo, sisi hatujawahi kuona suk
- Page 44 and 45: Vile vile Mheshimiwa Dr. Juma Ngaso
- Page 46 and 47: Kundi la Wanawake walikuwa wagombea
- Page 50 and 51: Mheshimiwa Naibu Spika, haya ninayo
- Page 52 and 53: ambayo tunaona yanaweza kuleta atha
- Page 54 and 55: kweli waweze kuchambua ili tusije t
- Page 56 and 57: Nikaona hii labda hii Kiswahili cha
- Page 58 and 59: Naomba nichukue nafasi hii kumponge
- Page 60 and 61: kwa sheria ya Bunge hili kwamba Mak
- Page 62 and 63: General Tyre kinaendelea kufanya ka
- Page 64 and 65: Mheshimiwa Naibu Spika, juzi niliku
- Page 66 and 67: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo na
- Page 68: Sasa kutokana na hayo mimi nafikiri