Kundi la Wanawake walikuwa wagombea wawili, Mheshimiwa Dr. Aisha Kigoda, amepata kura65 na Mheshimiwa Balozi Getrude Mongella, amepata kura 169, idadi ya wapiga kura ilikuwa ni 234 nahakuna kura iliyoharibika. (Makofi)Kundi la Tanzania Zanzibar walikuwa wagombea 6 idadi ya kura kwa kila mgombea ni kamaifuatavyo, Mheshimiwa Dr. Haji Mwita Haji alipata kura 1, Mheshimiwa Dr. Suleiman Juma Omar,amepata kura 7, Mheshimiwa Omar Mjaka Ali, amepata kura 8, Mheshimiwa Balozi Ahmed Hassan Diria,amepata kura 35, Mheshimiwa Kidawa Hamid Saleh amepata kura 39, Mheshimiwa Remidius Kissassi,amepata kura 143. Wapiga kura ni wale wale 234 na kura moja iliharibika. (Makofi)Kundi la Tanzania Bara, waliopiga kura walikuwa 238, hakuna hata moja iliyoharibika. Matokeokwa kila mgombea ni kama ifuatavyo, Mheshimiwa George Mlawa, amepata kura 17, Mheshimiwa Dr.Hassy Kitine, amepata kura 31, Mheshimiwa William Kusila, amepata kura 31, Mheshimiwa KilontsiMporogomyi, amepata kura 50, Mheshimiwa Dr. Milton Mahanga, amepata kura 82, Mheshimiwa Dr.William Shija amepata kura 120 na Mheshimiwa Athumani Janguo, amepata kura 142. (Makofi)Kundi la Kambi ya Upinzani, idadi ya wapiga kura walikuwa 236, kura iliyoharibika hakuna hatamoja. Matokeo kwa kila mgombea ni kama ifuatavyo, Mheshimiwa Benedicto Mutungirehi, amepata kura26, Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed amepata kura 29 na Mheshimiwa Dr. Amani Waridi Kabourou,amepata kura 181. (Makofi)Sasa hiyo ni hatua ya kwanza kila mgombea amepata kura ngapi. Katika hatua kutangazawaliochaguliwa naanza tena. Kundi la Wanawake Mheshimiwa Getrude Mongella aliyepata kura 169 ndiyeamechaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika, namtangaza rasmi kwamba amechaguliwa kuwaMbunge wa Bunge la Afrika. (Makofi)Kundi la wagombea wa Tanzania Zanzibar aliyeongoza kwa kura na alitakiwa mmoja niMheshimiwa Remidius Kissassi mwenye kura 143. Namtangaza Mheshimiwa Remidius Kissassi kuwaamechaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament). (Makofi)Kundi la Tanzania Bara walitakiwa wawili sasa nawatangaza wawili wafuatao, kwamba ndiyowaliochaguliwa kuwa Wabunge wa Bunge la Afrika. Mheshimiwa Athumani Janguo mwenye kura 142 naMheshimiwa Dr. William Shija mwenye kura 120. Nawatangaza rasmi wawili hao kwambawamechaguliwa kuwa Wabunge wa Bunge la Afrika.Kundi la Vyama vya Upinzani kulikuwa na nafasi moja, namtangaza Mheshimiwa Dr. AmaniKabourou mwenye kura 181 kwamba ndiye aliyechaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika. (Makofi)Mwisho wa matangazo ya matokeo ya upigaji kura. Sasa nasitisha shughuli za Bunge hadi saa11.00 jioni. (Makofi)(Saa 07.00 mchana Bunge lilifungwa mpaka saa 11.00 jioni)(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)Hapa Naibu Spika (Mhe. Juma J. Akukweti) Alikalia KitiNAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita mchangiaji wa kwanza naombanichukue nafasi hii kuwapongeza sana wale ambao wamechaguliwa kuwa Wabunge wetu katika Bunge laAfrika. Mimi kwa sababu nilikuwa hapa nikishuhudia ile kasheshe. Naomba sana niwapongeze walewote walioshinda. (Makofi)Baada ya maelezo hayo, sasa namwita mchangiaji wa kwanza mchana huu, Mheshimiwa MbarukKassim Mwandoro, halafu atafuatiwa na Mheshimiwa Benedicto Mutungirehi.
MHE. MBARUK KASSIM MWANDORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.Nakushukuru kwa kunipa fursa hii na mimi kuchangia Muswada huu wa Anti-Damping na CountervailingMeasures.Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote ningependa kuchukua fursa hii kukupa pongezi wewepamoja na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kufika salama katika mwaka 2004 na ninawatakia kila lakheri, mafanikio na maendeleo mema. (Makofi)Vile vile ningependa kuwapongeza ndugu zetu ambao wameshindania na wale waliobahatikakuchaguliwa kuwa Wabunge wa Pan African Parliament. Nawapongeza sana. (Makofi)Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa vile vile kuchukua fursa hii kumpongeza sanaMheshimiwa Waziri kwa kuweza kuleta Muswada huu mzuri na muhimu kwa wakati. Ningependakumpongeza Waziri Ngasongwa, Naibu Waziri wake, Katibu Mkuu na Wataalam wote wa Wizarani waOfisi ya Mwanasheria Mkuu na wengine wote ambao kwa kusema kweli wamejitahidi sana kuuletaMuswada huu unavyotakikana.Mheshimiwa Naibu Spika, Muswada huu ni wa muhimu sana na kusema kweli umeletwa kwawakati muafaka. Ni muhimu kwa sababu unalinda sio tu viwanda, lakini unasaidia vile vile kuhamasishauchumi wetu kwa ujumla. Kabla sijaenda mbali, ningependa kuchukua fursa hii kusema kwamba naungamkono hoja hii kwa asilimia mia moja. (Makofi)Viwanda kama inavyosema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000 ndiyo Sekta kiongozi nandiyo inayotarajiwa kuupeleka uchumi wetu katika hali ya modernization na kwamba ifikapo mwaka 2025nchi yetu iwe na viwanda vya kati na uchumi ulioendelea na itakayofanya kazi hiyo kubwa sana niviwanda. Viwanda ni sekta kiongozi kwa sababu kilimo, mifugo, maliasili, madini vyote kwa sehemukubwa vinategemea sana viwanda viendelezwe. Kwanza mahitaji yake ya kuzalisha yanapita kiwandani,lakini mazao yake yanapata thamani zaidi wakati yanapokwenda kiwandani ili yaweze kupata thamanizaidi na kuongeza fedha za kigeni zaidi kwetu na kuleta ajira kwa wananchi, kuongeza kodi na mambokama hayo. Kwa hiyo, Sekta ya Viwanda ni sekta muhimu sana na ndio maana Serikali yetu ya Chama chaMapinduzi imefanya jitihada kubwa sana kuitengenezea mazingira mazuri na kuweza kuipatia mahitajiyake mbalimbali na miundo mbinu.Sasa hivi sekta nyingine za kilimo, madini zinafaidi sana kutokana na kuwepo viwanda naviwanda viendelee kuwepo. Hivi karibuni tulipata fursa ya kutembelea viwanda mbalimbali, tumeona jinsigani sasa hivi kwa mfano viwanda vya mbegu vimetanuka sana, vimeendelea sana, vinatusaidia sanakuboresha sio tu chakula chetu tunachopata na mazao yetu viwandani, lakini yanawawezesha vile vilewakulima kujipanua na kuendelea zaidi kilimo hapa nchini. Kuna viwanda vingi sana ambavyo sasa hivivinasindika mali zetu za humu nchini. Hii ni muhimu sana kwa uchumi mzima na kwa hiyo hivi viwandavilivyopo na hivi ambavyo tunajaribu kuviweka chini ya utaratibu wa EPZ ni muhimu sana kwa kuboreshana kuendeleza uchumi wetu.Hivi viwanda ni muhimu basi vilindwe kwa sababu viwanda mfano wake ni kama vile kichwa chatreni katika behewa. Kichwa cha treni kikienda kasi na mabehewa mengine yatakwenda kasi. Sekta yaViwanda inapoendelea ndio sekta nyingine vile vile zinapata fursa ya kutanuka na kuendelezwa vizurizaidi.Sasa katika dunia hii ya utandawazi, ni muhimu sana kuchukua hatua thabiti kuweza kuvilindaviwanda. Pamoja na kuchukua jitihada ya kuboresha viwanda hivi na kuvifanya viwe vingi lakini kunaumuhimu wa kuvilinda kutokana na vitimbi vya wakubwa mbalimbali hasa haya Makampuni ya Kimataifayanayoitwa Transnational. Haya Makampuni yana mbinu na hila mbalimbali za kudidimiza Makampunikama haya yetu kwa sababu viwanda kama ni vidogo ambavyo vinajitokeza katika nchi changa watawezakuviua viwanda hivi ili wao waweze kujitanua. Moja ya mbinu kubwa wanayotumia hawa wenzetu nimbinu ya kuteremsha bei ama kwa kupata fidia ya ushuru ama kupata ruzuku ya namna nyingine yoyote aumipango mingine yoyote ambayo wanaweza kuteremsha bei kwa kuanzia na hatimaye viwanda hivi
- Page 1 and 2: BUNGE LA TANZANIA_______________MAJ
- Page 3: jana tarehe 5 Februari, 2004, suala
- Page 6 and 7: La pili ni kwamba, Mkandarasi huyu
- Page 9 and 10: (a) Je, Serikali ina mpango gani wa
- Page 11 and 12: mambo mengine, umebainisha kwamba S
- Page 13 and 14: La pili, kama itakuwa Chuo Kikuu je
- Page 15 and 16: Na. 54Mikoa isiyo na Viwanda Nchini
- Page 17 and 18: (c) Mheshimiwa Spika, napenda kumha
- Page 19 and 20: kutumia dawa ya kujipaka mwilini, k
- Page 22 and 23: Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mb
- Page 24 and 25: HON. AMBASSADOR GETRUDE I. MONGELLA
- Page 26 and 27: DEPUTY SPEAKER: Honorable Omar Mjak
- Page 28 and 29: DEPUTY SPEAKER: Honorable Kidawa Ha
- Page 30 and 31: DEPUTY SPEAKER: Honorable Dr. Amani
- Page 32 and 33: I think the issue is stipulated cle
- Page 34 and 35: I do feel that the experience and e
- Page 36 and 37: DEPUTY SPEAKER: Don’t...HON. GEOR
- Page 38 and 39: I come to you with considerable exp
- Page 40 and 41: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema h
- Page 42 and 43: Kwa hiyo, sisi hatujawahi kuona suk
- Page 44 and 45: Vile vile Mheshimiwa Dr. Juma Ngaso
- Page 48 and 49: vikaweza kuingia katika soko jipya
- Page 50 and 51: Mheshimiwa Naibu Spika, haya ninayo
- Page 52 and 53: ambayo tunaona yanaweza kuleta atha
- Page 54 and 55: kweli waweze kuchambua ili tusije t
- Page 56 and 57: Nikaona hii labda hii Kiswahili cha
- Page 58 and 59: Naomba nichukue nafasi hii kumponge
- Page 60 and 61: kwa sheria ya Bunge hili kwamba Mak
- Page 62 and 63: General Tyre kinaendelea kufanya ka
- Page 64 and 65: Mheshimiwa Naibu Spika, juzi niliku
- Page 66 and 67: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo na
- Page 68: Sasa kutokana na hayo mimi nafikiri