10.07.2015 Views

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo, sasa naomba niingilie suala la Muswada. Ninaungamkono kwamba Muswada huu uwepo, lakini napenda nitahadharishe kwamba huu Muswada wa Anti-Dumping kama usipochukuliwa vizuri unaweza ukaturudisha huko nyuma wakati ambapo vitu vingivilikuwa vinakosekana. Ninaelewa kabisa kwamba Anti-Dumping maana yake wakati mwingineinawezekana isieleweke vizuri.Mheshimiwa Spika, hata ukienda nchi zilizoendelea utakuta kwamba kuna bidhaa ambazozinatengenezwa kwa ajili ya watu ambao hawana uwezo mkubwa. Kwa mfano, China, ukienda hukoutakuta kabisa kwamba kuna bidhaa za kila aina, mwenye uwezo mkubwa anapata kununua vitu vyenyethamani kubwa sana na mwenye uwezo mdo<strong>go</strong> na yeye anapewa nafasi hiyo.Kwa mfano, katika suala la nguo nimeona kabisa Mjini Beijing kuna nguo nyingine suit unawezakununua hata kwa shilingi milioni moja. Hata kwa mfano gauni la first class silk linauzwa kwa bei kubwasana. Kwa hiyo, katika suala la hii Anti-Dumping nashauri kwamba tujaribu kuona uwezekano ili tusijetukarudi kule tulikotoka.Mheshimiwa Spika, wakati fulani tulipokuwa na upungufu wa vitendea kazi nakumbuka wengiwalitaka hata kuoza midomo kwa sababu Colgate yenyewe ilikuwa haionekani. Kwa hiyo, nafikirikwamba hii sheria isipotekelezwa vizuri inaweza ikasababisha upungufu wa bidhaa katika soko. Kwa hiyo,nashauri kwamba katika kutekeleza hili tusirudishwe kule tulikotoka.Mheshimiwa Spika, napenda niseme kwamba sheria hii ni nzuri, lakini vile vile naomba Wizaranyingine zinazohusika hasa Wizara ya Kilimo na Chakula na yenyewe ilete hapa sheria ya Anti-Dumpingkatika agricultural products (chakula). Pamoja na kwamba hapa Tanzania tulikuwa na utaratibu mzuri wakilimo, kilimo hicho kilikuwa kinasaidia katika raw materials kwenye viwanda vyetu, lakini baada yakubinafsisha viwanda vingi, kumekuwepo na matatizo kwamba bidhaa nyingi za kilimo zinatoka nje yanchi.Mheshimiwa Spika, nichukulie mfano wa Kampuni ya Bia. Kampuni hiyo zamani walikuwawanatumia barley ambayo inazalishwa hapa, lakini sasa hivi mashamba yetu ya barley yote sasa hiviyamekufa, umaskini unakithiri na mzunguko wa fedha umekuwa ni mbaya sana kwa watu wa kawaida.Mheshimiwa Spika, vile vile, nafikiri kwamba sheria kama hii ya kuzuia ipatikane, kwamba kamakuna mtu anataka kuwa na kiwanda hapa atumie raw materials za hapa ili kusudi wananchi wetu vile vilewaweze kufaidika. Suala hili lisipoangaliwa linaweza likaleta athari sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, zamani tulikuwa na viwanda vilivyokuwa vinasaga unga, lakini na wenyewesasa hivi utakuta wanaleta ngano kutoka nje na wakati mwingine ni second grade ngano. Pia nashaurikwamba, suala hili na lenyewe lifikiriwe ni namna gani hii Anti-Dumping kwenye upande wa kilimoinaweza kuwa controlled ili kusaidia mzunguko wa fedha kwa watu wetu.Mheshimiwa Spika, ninaelewa sasa hivi Serikali inapata mapato makubwa sana, lakini ukiendakwa Wananchi utakuta kabisa kwamba mzunguko wa fedha umekuwa mbaya sana na hasa umechangiwana ukame ambao tunao kwa muda mrefu. Kwetu Shinyanga tuna ukame sasa hivi ni takriban miaka mitatuna ukitazama Mkoa wa Shinyanga ni Mkoa wa kilimo na kilimo kinaposhindikana Wananchi wanakuwamaskini sana.Mheshimiwa Spika, kwa kutumia nafasi hii napenda kuihamasisha Serikali kwamba miradi yaumwagiliaji na uvunaji maji iletwe mapema ili kuweza kuhakikisha kwamba tunajiweka sawa katika sualahili la Anti-Dumping.Naomba niishie hapo, ninashukuru sana na ninaamini kabisa kwamba ushauri wangu Serikaliitauchukua na kwamba sheria ya Anti- Dumping katika suala la bidhaa za kilimo na yenyewe iletwe hapamapema ili tujaribu kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanapata soko lauhakika la mazao yao hasa mazao ya kilimo.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!