10.07.2015 Views

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI alijibu:-Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omar Juma Omar, Mbunge wa Pandani,kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, kimsingi ZANTEL haijakatazwa kutoa huduma Tanzania Bara. Inaweza nainaruhusiwa kutumia minara ya TTCL na ya Kampuni za simu nyingine za mikononi. Sababu pekee na yamsingi inayosababisha ZANTEL isiweze kutumia mfumo wake kutoa huduma za simu Tanzania Bara niMuda Maalum wa miaka minne uliopewa Kampuni ya Simu ya TTCL kutoa huduma zake hapa nchinihususan kwa huduma za simu za kawaida.Mheshimiwa Spika, napenda kutoa taarifa kuwa muda maalum wa TTCL kutoa huduma peke yakeutakwisha mwezi Februari, 2005 na Serikali imekwishatamka wazi kuwa baada ya muda huo kumalizika,TTCL hawataongezewa muda tena. Kuanzia hapo Kampuni zote ikiwa ni pamoja na ZANTEL zitaruhusiwakutoa huduma hizo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.Tayari ZANTEL na Mamlaka ya Mawasiliano, wameanza majadiliano kuhusu suala hili na taarifatulizonazo ni kuwa majadiliano yanaendelea vizuri.Na. 56Kuangamiza Mazalio ya MbuMHE. DR. CHRISANT M. MZINDAKAYA aliuliza:-Kwa kuwa katika miaka kama 30 hivi ya nyuma mbu hawakuwa wanazaliana kwa kiwangokikubwa kama ilivyo sasa; na kwa kuwa kwenye maeneo ya baridi kama vile Ufipa ya Juu, Mbeya, Iringa,Ruvuma, Arusha na sehemu zenye miinuko mikubwa hapakuwa na mbu na kwamba wakati ule MabwanaAfya walikuwa na zana na dawa za kuua vyanzo vya mazalio ya mbu:-(a)(b)(c)Je, kwa nini maeneo ambayo hayakuwa na mbu sasa yana mbu?Je, isingekuwa vyema kukinga malaria kwa kuweka mipango ya usafi na kuangamizamazalio ya mbu?Je, Serikali inafahamu kuwa ugonjwa wa malaria ndio unaoua watu wengi zaidi kulikomaradhi mengine wakati uwezekano wa kutokomeza ugonjwa huo upo?NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Afya, napenda kujibu swali la Mheshimiwa ChrisantMajiyatanga Mzindakaya, Mbunge wa Kwela, lenye sehemu ya (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-(a) Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kuna baadhi ya maeneo hususan yale ya baridiambayo hayakuwa na mbu hapo zamani na sasa yana mbu wanaoambukiza ugonjwa wa malaria. Hali hiiimejitokeza kutokana na shughuli kadhaa za kibinadamu katika kilimo, ujenzi na uharibifu wa mazingira.Shughuli hizi zimetengeneza mazingira muafaka ya mazalio ya mbu. Aidha, ongezeko la joto Duniani(Global Warming) kutokana na kuongezeka kwa joto na kupungua kwa tabaka la ozone (Ozone Layer),kumetengeneza mazingira mazuri kwa mbu kuweza kuzaliana.(b) Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya bado inazingatia kuwa usafi wa mazingira ni njiakubwa na muhimu katika kupambana na ugonjwa wa malaria pamoja na magonjwa mengineyanayoambukiza. Mikakati ya usafi wa mazingira inafanywa katika ngazi ya Halmashauri ambapowanashughulikia ukusanyaji na utupaji wa taka na usafishaji wa mifereji ya maji ya mvua. Aidha, elimukwa wananchi inatolewa kwa ajili ya kujikinga na malaria ikiwa ni pamoja na kuhimizwa kuweka usafi wamazingira wanamoishi na kufukia madimbwi ya maji.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!