10.07.2015 Views

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

miradi umeanza kutumika mwaka 1994 kufuatia mapendekezo ya Tume ya Shellukindo. Takwimutulizonazo zinaonyesha kuwa katika kipindi cha 1994/1995 hadi Januari 2003/2004, Serikali ya MapinduziZanzibar imepata, kupitia chanzo hiki, jumla ya shilingi bilioni 61.167 sawa na asilimia 128.4. Mwaka wafedha 2000/2001, zilitolewa shilingi bilioni 12.497, ambayo ni asilimia 6.65 na mwaka 2001/2002zilitolewa shilingi 8.804 bilioni ambayo ni asilimia 5.22. Mpaka kufikia Januari, 2004, Serikali yaMapinduzi Zanzibar ilikwishapokea shilingi bilioni 9.133 au asilimia 88.6 hivyo kubakiwa na shilingi1.165 bilioni au asilimia 11.4 hadi kufikia Juni, 2004.Mheshimiwa Spika, kuanza kazi kwa Tume ya Pamoja ya Fedha inayoon<strong>go</strong>zwa na Mwenyekitiwake, Mheshimiwa William Shellukindo, M<strong>bunge</strong> wa Bumbuli, kutatuweka katika nafasi nzuri zaidi yakuimarisha uhusiano wa kifedha kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.MHE. BAKAR SHAMIS FAKI: Ahsante Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.(a) Kwa kuwa formula ya mgao ya asilimia 4.5 ilianza miaka kumi iliyopita, je, mgao wanyuma utalipwa vipi?(b) Kwa kuwa SMZ inadaiwa na TANESCO fedha nyingi tu. Je, isingekuwa vyema deni hilolikalipwa kutokana na mgao ambao SMZ haikulipwa?WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kama tulivyoeleza kwenye jibu letu la msingi kablaya Tume ya Mheshimiwa Shellukindo kuundwa, kulikuwa hakuna utaratibu huu wa asilimia 4.5. Tume yaMheshimiwa Shellukindo, ndiyo iliyopendekeza hiyo asilimia 4.5 na Serikali zote mbili zikakubali na kwahiyo tukaanza kutekeleza hiyo asilimia 4.5.Lakini hili ni suala la misaada na matumizi ya misaada ndani ya bajeti, kama hakuna namna yaSerikali ya Muungano inavyoweza kutumia asilimia hizi kwenda kulipia umeme kwa Serikali yaMapinduzi Zanzibar, hili ni suala la kibiashara, wao watatafuta njia zao za kulipia umeme isipokuwa kamawakitaka wao kama sehemu yao ya matumizi chini ya hiyo 4.5 wakitaka wao kutumia fedha hizi kulipiaumeme huo ni uamuzi wao Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.MHE. ABDULLATIF HUSSEIN ESMAIL: Ahsante Mheshimiwa Spika, kwa kunipa fursa yakuuliza swali la nyongeza. Adamu alimuoa Hawa, ukiuliza lini, kamuoa nani, utaambiwa mwulize babuyako aliyekuwepo siku hizo.Mheshimiwa Spika, swali langu ni kwamba uendeshwaji wa Muungano nadhani ni cost of theUnion, ninavyoelewa mimi ni kubwa sana. Namwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri, je, nani anayelipiagharama kubwa hiyo?SPIKA: Halitokani na swali la msingi, lakini Mheshimiwa Waziri wa Fedha analo jibu.WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, gharama za kuendesha Serikalihii ya Muungano ni kubwa na ni kweli vile vile kwamba, gharama hizi hazigharamiwi pro rata yaaniukipata huduma hii uilipie ila inalipiwa kiujumla kutokana na bajeti tunayoidhinisha hapa Bungeni. Lakinisuala zima hili linashughulikiwa bado na Tume ya sasa ya Mheshimiwa Shellukindo, kama tulivyosemakwenye jibu letu.Mheshimiwa Shellukindo na Makamishna wenzake, wataliangalia tena suala hili na kupendekezaiwe vipi. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa M<strong>bunge</strong>, asuburi mpaka Tume ya Mheshimiwa Shellukindo,itakapokuja na mapendekezo na Serikali zetu kuamua.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!