Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hassan Chande Kigwalilo, Mbunge waLiwale, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-(a) Mheshimiwa Spika, ni kweli Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinafikiriwakupandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu. Hata hivyo, hatua hiyo inaweza kufikiwa tu pale ambapomasharti husika yametimizwa. Hadi sasa Chuo kimekwisha tekeleza taratibu zote ikiwa ni pamoja nakufanya majadiliano na wadau wote kama vile Baraza la Elimu ya Juu na Ithibati (Higher EducationAccreditation Council - HEAC), Vyuo Vikuu na Wizara mbali mbali.Mheshimiwa Spika, kwa kuwa vipo vyuo vingi hapa nchini ambavyo vina ari ya kupandishwahadhi kuwa Vyuo Vikuu, Serikali imeonelea kuwa, ipo haja ya kuipa nafasi Wizara ya Sayansi, Teknolojiana Elimu ya Juu, kutafakari kwa kina na hatimaye kuweka utaratibu mzuri wa kuvipandisha hadhi vyuohivyo.(b) Mheshimiwa Spika, Wizara yangu na Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu,imekamilisha uchambuzi wa kina kuhusu namna bora ya kubadilisha IFM kuwa Chuo Kikuu. Uchambuzihuo na mapendekezo yetu bado yanapitia ngazi za juu Serikalini kwa lengo la kufikia uamuzi wa mwisho.Naomba Mheshimiwa Mbunge, avute subira kwani suala la kuanza Chuo Kikuu linahitaji kufikiriwa kwamakini sana na wadau wote nje na ndani ya Serikali.MHE. HASSAN C. KIGWALILO: Nashukuru kwa majibu mazuri niliyoyapata. Pamoja namajibu hayo mazuri ningetaka kujua Serikali inachukua hatua gani za dhati ili kuboresha hudumambalimbali za Vyuo Vikuu hivyo vinavyofunguliwa ili kuwafanya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyowaweze kupata huduma wanayohitaji kikamilifu kwa kuwa hivi sasa kuna upungufu wa mambo mengi tu,TELEX hazitoshi, vyoo havitoshi, meza wala madeski hayatoshi na sehemu zingine zingine, wanazozihitajikwa mafunzo hayo?SPIKA: Hiyo inahusu Wizara nyingine.WAZIRI WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ELIMU YA JUU: Okay, ingawa halihusianisana na Chuo cha Usimamizi wa Fedha, lina ujumla hadi linalenga Wizara yangu, ni kwamba kabla Chuohakijakubalika kuwa Chuo Kikuu, masharti muhimu yamewekwa na Baraza la Ithibati na lazimayatekelezwe ndiyo Chuo kiwe Chuo Kikuu. Kuna hatua tano ambazo zinachukuliwa kabla chuohakijapewa full accreditation.Nadhani Mheshimiwa Mbunge anazungumzia vyuo ambavyo vimo katika hatua mbalimbali kablaya full accreditation na zinakubalika kabisa kuwa ni Chuo Kikuu kikamilifu na ndiyo maana tukirudikwenye swali la msingi la Chuo cha IFM kuna masharti fulani fulani ambayo bado tunakazia yatekelezwendiyo kikubalike katika ubora wa Chuo Kikuu, Serikali inachukua hatua ya kuwa wakali. Hatuchukui kilaChuo Kikuu kinachoomba kuwa Chuo Kikuu kiwe Chuo Kikuu mpaka wametimiza masharti yote, mfanoWalimu. Kwa sababu upande wa masomo ya sayansi, uwiano wa wanafunzi usiwe chini ya moja kwasaba, kwa masomo ambayo ni ya sanaa isiwe chini ya moja kwa kumi. (Makofi)Kwa hiyo, tunachukua hatua. Ahsante.MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii yakuuliza swali la nyongeza. Katika Tanzania tumekuwa na vyuo fulani ambavyo vinafundisha watu wangazi fulani ili waende kutumikia nchi yao au wajiajiri wenyewe. Kwa mfano, sasa hivi tuna vyuo vyaVETA nchi nzima ambavyo kazi yake ni ku-train vijana waweze kwenda kujiajiri wenyewe.Hivi majuzi tumesoma katika vyombo vya habari kwamba, VETA nayo inataka kuwa Chuo Kikuu.Kwanza nina maswali. La kwanza je, Serikali inakubali kwamba kweli VETA inakuwa Chuo Kikuu?(Kicheko/Makofi)
La pili, kama itakuwa Chuo Kikuu je, Serikali ina mpango gani wa ku-train vijana wetu haowaliokuwa wanakuwa trained na VETA wa ngazi za chini maadam sasa kitakuwa Chuo Kikuu?(Kicheko/Makofi)WAZIRI WA KAZI, MAENDELEO YA VIJANA NA MICHEZO: Mheshimiwa Spika,naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wote kwamba, VETA hakunawazo la kuibadili VETA kuwa Chuo Kikuu, wala hatujafikiria kabisa, VETA itaendelea na wajibu wake uleule katika jamii wa kuzalisha mafundi stadi. (Makofi)MHE. BAKARI SHAMIS FAKI aliuliza:-Na. 53Msaada wa Serikali ya MuunganoKwa kuwa Serikali ya Muungano wa Tanzania inapata misaada mbalimbali, ikiwemo fedha,vyakula, dawa na kadhalika; na kwa kuwa misaada hiyo iko ya aina mbili, yaani ile ambayo inalengamiradi maalum na ile ambayo haikulenga miradi maalum na hugawiwa baina ya Serikali ya Muungano waTanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo Zanzibar hupata asilimia 4.5%:-(a) Je, ni vigezo gani vinavyozingatiwa katika kuelewa aina hizo mbili katika kugawamisaada hiyo kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar?(b) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imepata kiasi gani kama mgao wake tokeakuasisiwa Muungano wetu?(c) Ni utaratibu gani unaotumika katika kupata misaada ya miradi maalum?NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. DR. FESTUS B. LIMBU) alijibu:-Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bakari Shamis Faki, Mbunge wa Ole,lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kushuhudiaongezeko la misaada kutoka kwa nchi wahisani na mashirika mbalimbali ya Kimataifa kutokana na juhudikubwa zilizokuwa zinafanywa na Serikali za awamu zote katika jitihada zake za kukuza uchumi nakuwaondolea wananchi umaskini. Kuna aina mbili za misaada hiyo:-Aina ya kwanza, ni misaada kwa ajili ya miradi ya maendeleo au Project Grants, ambayohutolewa na wahisani kwa lengo la kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii. Miradi hiyohuwa tayari imekwisha ainishwa. Misaada hii hutolewa na wahisani kwa walengwa kwa mujibu wamakubaliano yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili. Aidha, misaada hiyo yaweza kupitia katika utaratibuwa kawaida wa kifedha wa Serikali au kwenda moja kwa moja kwenye miradi husika ambapo Serikalihuwajibika kupata taarifa za misaada hiyo.Aina ya pili, ni misaada kwa ajili ya mipango maalum ya maendeleo au Programme Grants,pamoja na ile ya kibajeti ambayo hutolewa na wahisani kwa Serikali ili kuongeza uwezo wa Serikali wakugharamia mipango yake mbalimbali ya kimaendeleo. Misaada hii huingizwa moja kwa moja kwenyeMfuko Mkuu wa Serikali. Fedha hizi zinalenga zaidi katika kukamilisha miradi au kuanza miradi mipya.Ni kutokana na misaada ya aina hii, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikipata mgao wa asilimia 4.5.Mheshimiwa Spika, vigezo vinavyotumika kutambua aina hizi za misaada ni maudhui ya misaadayenyewe kama inavyokubalika wakati wa majadiliano baina ya Serikali na wahisani.Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 1964, Serikali ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikitoaruzuku ya fedha (OC), ili kuziba pengo linalojitokeza katika Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,kugharamia shughuli mbalimbali za maendeleo. Utaratibu wa mgao wa asilimia 4.5 ya misaada isiyo ya
- Page 1 and 2: BUNGE LA TANZANIA_______________MAJ
- Page 3: jana tarehe 5 Februari, 2004, suala
- Page 6 and 7: La pili ni kwamba, Mkandarasi huyu
- Page 9 and 10: (a) Je, Serikali ina mpango gani wa
- Page 11: mambo mengine, umebainisha kwamba S
- Page 15 and 16: Na. 54Mikoa isiyo na Viwanda Nchini
- Page 17 and 18: (c) Mheshimiwa Spika, napenda kumha
- Page 19 and 20: kutumia dawa ya kujipaka mwilini, k
- Page 22 and 23: Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mb
- Page 24 and 25: HON. AMBASSADOR GETRUDE I. MONGELLA
- Page 26 and 27: DEPUTY SPEAKER: Honorable Omar Mjak
- Page 28 and 29: DEPUTY SPEAKER: Honorable Kidawa Ha
- Page 30 and 31: DEPUTY SPEAKER: Honorable Dr. Amani
- Page 32 and 33: I think the issue is stipulated cle
- Page 34 and 35: I do feel that the experience and e
- Page 36 and 37: DEPUTY SPEAKER: Don’t...HON. GEOR
- Page 38 and 39: I come to you with considerable exp
- Page 40 and 41: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema h
- Page 42 and 43: Kwa hiyo, sisi hatujawahi kuona suk
- Page 44 and 45: Vile vile Mheshimiwa Dr. Juma Ngaso
- Page 46 and 47: Kundi la Wanawake walikuwa wagombea
- Page 48 and 49: vikaweza kuingia katika soko jipya
- Page 50 and 51: Mheshimiwa Naibu Spika, haya ninayo
- Page 52 and 53: ambayo tunaona yanaweza kuleta atha
- Page 54 and 55: kweli waweze kuchambua ili tusije t
- Page 56 and 57: Nikaona hii labda hii Kiswahili cha
- Page 58 and 59: Naomba nichukue nafasi hii kumponge
- Page 60 and 61: kwa sheria ya Bunge hili kwamba Mak
- Page 62 and 63:
General Tyre kinaendelea kufanya ka
- Page 64 and 65:
Mheshimiwa Naibu Spika, juzi niliku
- Page 66 and 67:
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo na
- Page 68:
Sasa kutokana na hayo mimi nafikiri