19.02.2015 Views

MAELEZO MAFUPI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO MHE ...

MAELEZO MAFUPI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO MHE ...

MAELEZO MAFUPI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO MHE ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

MAELEZO MAFUPI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO

MHE: MOHAMMED A. BABU KWA MHE: WAZIRI MKUU KWENYE

UZINDUZI WA TOVUTI YA OFISI YA MKUU WA MKOA WA

KILIMANJARO – TAREHE 19 FEBRUARI 2009:

• Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb) - Waziri Mkuu wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

• Mhe. Katibu Tawala wa Mkoa Kilimanjaro,

• Wahe. Wakuu wa Wilaya,

• Mhe. Mstahiki Meya Manispaa ya Moshi,

• Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya,

• Wakurugenzi Watendaji, Halmashauri za Wilaya na

Manispaa,

• Makatibu Tawala wasaidizi Sekretarieti ya Mkoa,

• Wataalam na washauri wa Sekretarieti ya Mkoa,

• Wageni waalikwa,

• Mabibi na Mabwana.

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia

sote kuona mwaka huu wa 2009. Napenda kukukaribisha sana katika

Makao Makuu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kutuzindulia

TOVUTI ya mkoa na kuongea na watumishi.

Mhe. Waziri Mkuu, Mkoa wa Kilimanjaro kwa ushirikiano na Wizara

yako, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa

tumekuwa katika mchakato wa kuweka mfumo wa habari na

mawasiliano (TEKNOHAMA) katika ngazi ya mkoa na halmashauri za

wilaya kwa lengo la kutekeleza azma ya kuwa na serikali mtandao (e-

1

government). Kuimarika kwa matumizi haya ya (TEKNOHAMA)

kutasaidia sana kurahisisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika

shughuli mbalimbali za kila siku ndani ya serikali, mkoa, halmashauri

za wilaya na wadau wengine.

Ili kukuza serikali-mtandao, mkoa umejiwekea malengo yafuatayo ya

utekelezaji;-

i) Utengenezaji na uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano

na vitendea kazi;

ii) Kuboresha na kuhimiza matumizi ya mifumo ya kompyuta

iliyopo pamoja na kutengeneza mifumo mingine kwa ajili ya

kurahisha kazi. Hii inakwenda sambamba na utoaji wa

mafunzo ya kompyuta kwa watumiaji wa mifumo katika ngazi

ya mkoa na halmashauri;

iii) Kufanya mawasiliano kwa kutumia mtandao;

iv) Kutuma na kupokea habari kwa kupitia mtandao.

Mhe. Waziri Mkuu, nafurahi kukujulisha kuwa hivi sasa mkoa

umefanikiwa kuwa na chumba cha darasa kwa ajili ya kutolea mafunzo

mbalimbali ya kompyuta na mifumo tuliyonayo, na tayari Wilaya ya

Moshi imeanza kupata mafunzo hayo. Mafunzo kwa wataalamu wa

sekretarieti ya mkoa na halmashauri zilizobaki yatafanyika baadaye.

Pia mkoa umefanikiwa kuboresha mitandao ya mawasiliano ya sauti

na data katika jengo la Mkuu wa Mkoa na kusimika mifumo mbalimbali

ya kurahisisha utendaji kazi wa ofisi. Gharama ya uanzishaji ni

shs.65,000,000/=.

2

Tovuti ya Mkoa wa Kilimanjaro inapatikana kwa anwani ya

www.kilimanjaro.go.tz. Anuani za tovuti za mikoa mingine ni

katika muundo huo na kwa jina la mkoa husika.

Katika TOVUTI ya mkoa wa Kilimanjaro taarifa mbalimbali za kisiasa,

kiuchumi na kijamii zinazohusu mkoa zitakuwa zinapatikana.

Taarifa hizi zinawezesha wadau ndani na nje ya Tanzania kupata

taarifa za mkoa na halmashauri ambazo ni muhimu sana katika

kupanga na kutoa maamuzi, kuhusiana na mipango ya maendeleo.

Mhe. Waziri Mkuu, uzinduzi wa TOVUTI hii unatupa changamoto ya

kuhakikisha kuwa teknolojia hii inawafikia wananchi wa kawaida .

Changamoto hizo ni pamoja na kutokamilika kwa mfumo wa kujenga

serikali mtandao (e-overment) katika halmashauri zote. Ninatoa wito

kwa kila halmashauri kuharakisha ufungaji, uboreshaji na utumiaji wa

teknolojia hizi kwa lengo la kuharakisha maendeleo kwa mkoa wetu

wa Kilimanjaro.

Mhe. Waziri Mkuu, baada ya maelezo hayo mafupi ya utangulizi, kwa

heshima na taadhima kubwa ninakuomba sasa utuzindulie TOVUTI

yetu ya mkoa yenye anwani www.kilimanjaro.go.tz na kuongea

na watumishi wa Sekretarieti ya mkoa na halmashauri.

KARIBU SANA.

3

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!