19.02.2015 Views

i MIAKA 50 YA UHURU MKOA WA KILIMANJARO UJUMBE WA ...

i MIAKA 50 YA UHURU MKOA WA KILIMANJARO UJUMBE WA ...

i MIAKA 50 YA UHURU MKOA WA KILIMANJARO UJUMBE WA ...

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

MIAKA 50 YA UHURU MKOA WA KILIMANJARO

UJUMBE WA MKUU WA MKOA

Mhe. Meja Jenerali (Mst.) Said S. Kalembo

Mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa 21 ya Tanzania Bara, ambao ulioanzishwa

rasmi kwa Tangazo la Serikali Na.450 la mwaka 1963 ukiwa na Wilaya za

Kilimanjaro na Pare. Kabla ya hapo eneo hilo linaloitwa Mkoa wa Kilimanjaro

lilikuwa sehemu ya Jimbo la Kaskazini (Northern Province) lililokuwa linaundwa

pia na wilaya za Arusha na Mbulu; wakati wilaya ya Pare ilikuwa sehemu ya

Jimbo la Tanga (Tanga Province). Wakati nchi yetu inapata Uhuru tarehe

09.12.1961 Mkuu wa Jimbo la Kaskazini (Provisional Commissioner) alikuwa

Mheshimiwa PC Edward Barongo ambaye alitawala hadi 1963, na alipokelewa na

Mheshimiwa Peter Kisumo, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa mantiki hiyo Mkoa umetimiza miaka 38 tangu kuanzishwa kwake ukiwa

umeongozwa na Wakuu wa Mkoa 18 hadi hivi sasa.

Mkoa wa Kilimanjaro una eneo dogo la utawala lenye kilomita za mraba 13,209,

lakini ukiwa na msongamano mkubwa wa watu, vivutio vingi vya utalii mojawapo

ukiwa mlima Kilimanjaro, wasomi wengi, miundombinu mizuri na ya uhakika,

wachapa kazi ambao wanajituma katika kazi za kitaalamu na ujasiriamali, vyote

hivi vikiwa ni vichocheo vikubwa vya maendeleo yake.

i

Napenda kuwapongeza viongozi wakuu wa mkoa huu 18 waliotangulia hadi

kufikia mwaka huu 2011; kwani ndio walioweka misingi bora na imara ya

maendeleo yaliyofikiwa hivi sasa, kama inavyoonyeshwa kwenye mafanikio kwa

kila sekta katika taarifa ya mkoa.

Shukrani za dhati kwa serikali katika jitihada zake za kufikisha huduma na

maendeleo kwa wananchi wa mkoa huu kupitia ngazi mbali mbali za kiutawala

kuanzia ngazi ya Mtaa/Kitongoji, Kijiji, Kata na Halmashauri/Wilaya.

Mkoa wa Kilimanjaro una fursa nyingi za kimaendeleo ambazo zinawezesha

uwekezaji unaotokana mazingira mazuri yaliyopo sasa hivi kama vile:-

(i) Miundombinu ya kuaminika na mawasiliano kama vile mtandao

mzuri wa barabara za lami na changarawe zinazopitika kwa vipindi

vyote vya mwaka;

(ii) Njia za mawasiliano ya Simu, Viwanja vya Ndege kikiwepo kiwanja

cha Kimataifa KIA na viwanja vidogo vya Moshi Mjini na kile cha

Utalii Same na njia ya Reli ya Moshi - Arusha – Dar es Salaam;

(iii) Upatikanaji wa kuridhisha wa huduma za tiba, maji, umeme na

elimu;

(iv) Upatikanaji wa huduma na vivutio vya utalii kama vile Mlima

Kilimanjaro, Hifadhi za Wanyamapori za Kilimanjaro na Mkomazi,

misitu ya asili, mazingira yanayovutia tamaduni za asili na

mapango ya kale;

(v) Uwepo wa vyombo vya kifedha kukidhi haja kama vile benki 13,

SACCOS 217, mifuko ya hifadhi ya jamii na asasi nyingine ndogo

ndogo za fedha kama vile vikoba;

(vi) Ulinzi na usalama wa kuridhisha.

ii

Nina uhakika tukiweza kuimarisha mazingira haya mazuri ya uwekezaji na

kuboresha miundombinu iliyopo sasa, Mkoa unayo nafasi nzuri ya kupiga

hatua kubwa zaidi ya kimaendeleo katika miaka 50 ijayo. Hii ikiwa ni

pamoja na kutumia ardhi ndogo tuliyo nayo kikamilifu kwa kujenga majengo

kwa kwenda juu (vertical expansion) badala ya ujenzi wa kusambaa

(horizontal development);

Mafanikio haya yamepatikana kutokana na ushirikiano na mshikamano kati

ya viongozi mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali, chama, dini na

wananchi wa mkoa wetu wa Kilimanjaro. Tutaendelea kuwategemea kwa

miaka 50 ijayo Inshaalah Mwenyenzi Mungu akitujalia.

“TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE”

Said S. Kalembo

Meja Jenerali (Mst)

Kaimu MKUU WA MKOA

KILIMANJARO

iii

NENO LA SHUKRANI KUTOKA KWA

KATIBU TAWALA MKOA KILIMANJARO

Taarifa hii ya mafanikio ya Miaka 50 (Jubilee) ya Uhuru ya Mkoa wa

Kilimanjaro imetayarishwa/andaliwa na kamati maalum ya wataalam kutoka

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa

Halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro. Licha ya kuandaa taarifa hii, kamati

imejihusisha kikamilifu na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru

wa Tanzania Bara ambapo mkoa wa Kilimanjaro umepangiwa tarehe 21/8 –

24/8/2011. Kazi hii imefanyika katika mazingira ya kujituma na kujitolea

kwa hali ya juu na hivyo sina budi kuwashukuru wote kwa bidii na moyo

wao wa kujituma ambao kwa pamoja umewezesha kukamilika kwa taarifa

hizi na maadhimisho katika mkoa wetu na wilaya zake zote sita.

Napenda kuunga mkono ujumbe wa Mkuu wa Mkoa, katika maadhimisho

haya kwamba japo mkoa wa Kilimanjaro una eneo dogo la ardhi, mkoa una

fursa nyingi za kuwezesha kuinua hali ya uchumi kwa wakazi wake. Fursa

hizo ni pamoja na mlima Kilimanjaro, barabara zinazopitika wakati wote wa

mwaka, hifadhi za wanyama na miundombinu ya kutolea elimu kuanzia

elimu ya awali hadi chuo kikuu. Uwezo wa wakazi wake kielimu pamoja na

miundombinu iliyowekezwa katika eneo hili dogo tangu kupatikana kwa

Uhuru, fursa na rasilimali muhimu sana katika kupiga hatua ya kimaendeleo

kwa kuwekeza zaidi katika ardhi ndogo iliyoko ili iweze kuzalisha zaidi

(intensive agriculture), kuwekeza zaidi katika viwanda kwani hakuna

uwezekano wa kupanua ardhi iliyoko kwa kilimo na mwisho kuwekeza zaidi

katika elimu na kuufanya mkoa kuwa “centre for excelency” katika Elimu.

Yote haya yatawezekana endapo kila mwananchi atatimiza wajibu wake

pale alipo kwa kutumia fursa na rasilimali zilizopo.

iv

Napenda kuzishukuru Taasisi za Dini Mkoani Kilimanjaro na wananchi kwa

ujumla kwa michango mikubwa waliyotoa na wanayoendelea kutoa katika

maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro hususan katika huduma za kijamii.

Mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika miaka hii 50 ya Uhuru wa

Tanzania Bara katika mkoa wetu ziwe ni chachu ya kutafuta maendeleo

zaidi katika miaka 50 ijayo katika mkoa wetu wa Kilimanjaro.

“TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNAZIDI KUSONGA MBELE”

Hassan M. Bendeyeko

KAIMU KATIBU TAWALA WA MKOA

KILIMANJARO

v

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!