19.02.2015 Views

Elimu bora bila mafunzo endelevu kwa walimu.pdf - HakiElimu

Elimu bora bila mafunzo endelevu kwa walimu.pdf - HakiElimu

Elimu bora bila mafunzo endelevu kwa walimu.pdf - HakiElimu

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

ELIMU BORA

Bila Mafunzo Endelevu

kwa Walimu Kazini?

Mwandishi wa hadithi:

Richard Mziray

Mchoraji:

Ismael Abdoulkarym.

Wahariri:

Elizabeth Missokia

Robert Mihayo

Wachangiaji: Benedicta Mrema, Edwin Mashasi, Honoratus Swai,

Wambura Wasira, Agnes Mangweha

© HakiElimu 2010

SLP 79401, Dar es Salaam, Tanzania

Simu: (25522) 2151852 au 3

Nukushi: (255 22) 2152449

Barua pepe: info@hakielimu.org

Tovuti: www.hakielimu.org

ISBN: 9987-9331-3-6

Unaruhusiwa kunakili sehemu yoyote ya kijitabu hiki kwa minajili isiyo ya kibiashara. Unachotakiwa

kufanya ni kunukuu chanzo cha sehemu iliyonakiliwa na kutuma nakala mbili HakiElimu.

2

Utangulizi

Ni ukweli uliodhahiri kwamba maendeleo ya jamii yoyote yanahitaji elimu iliyo bora. Elimu hii ni ile

itakayowawezesha wanafunzi kushiriki kikamilifu katika kutatua matatizo na kupambana na changamoto

mbalimbali katika maisha yao ya kila siku. Elimu bora ni zaidi ya uwepo wa vifaa na mazingira mazuri

ya kufundishia.

Elimu bora lazima imwezeshe mwanafunzi kuwa na uwezo katika nyanja mbalimbali ili aweze kufanya

vizuri katika ulimwengu wa maendeleo. Elimu bora ni ile inayompa mwanafunzi ujuzi kutokana na

masomo mbalimbali anayofundishwa sambamba na kumwezesha kuwa mdadisi wa mambo na kuwa

mbunifu. Pia elimu bora humjengea mwanafunzi tabia ya kujiamini na hatimaye kuwa na ujasiri katika

kukabiliana na kutatua changamoto mbalimbali katika maisha.

Walimu ndio watendaji wakuu katika mchakato wa kujifunza na kufundisha. Hii ina maana kwamba

matarajio ya elimu bora ndani ya jamii yanatokana na mafunzo bora ya walimu. Walimu wakiwa na elimu

bora watakuwa na uwezo wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wanaowafundisha. Ili mtu aweze kuwa

mwalimu anahitaji kupata mafunzo ya kutosha na yanayoendana na masomo anayotarajia kufundisha.

Mafunzo ya walimu ni mchakato maalum wa kumwandaa mtu kwenda kufundisha. Mafunzo haya

huendeshwa kwa muda maalum, mazingira maalum, nadharia na vitendo maalumu. Mafunzo haya

ni lazima yamjenge mwalimu mtarajiwa kwenye maeneo matatu muhimu: Kwanza, ni lazima apate

taaluma na maarifa ya kutosha ya somo analofundisha ili aweze kulimudu somo hilo. Pili, ajue mbinu

za kutosha kufundishia na nadharia zinazoambatana na mbinu hizo.Tatu, sharti aifahamu falsafa na dira

ya taifa ya elimu ili awasaidie watoto kuitafsiri falsafa ya nchi na malengo ya elimu

3

Ili kuenda sambamba na mabadiliko ya kimaisha na mitaala yanayotokea kila kukicha katika ulimwengu

wa leo, walimu wanahitaji fursa ya kupata mafunzo kazini ili waweze kufundisha kulingana na mabadiliko

hayo na hatimaye kuwajengea wanafunzi uwezo na mbinu endelevu za kupambana na changamaoto

zinazotokana na mabadiliko hayo. Mafunzo ya walimu kazini ni mafunzo yanayotolewa kwa walimu

wakiwa kazini kwa lengo la kuamsha na kuongeza ujuzi na maarifa kwenye utaalam na taaluma ya

ualimu katika nadharia na vitendo vya kufundishia. Vilevile mafunzo haya yanalenga kuchagiza maadili

na hisia za kufundisha, kuchochea ari ya kufundisha na kusimamia mchakato wa kufundisha.

Kitabu hiki kwa kutumia katuni ambazo ni rahisi kuzisoma, zinazofurahisha na kuburudisha, kinalenga

kuonesha athari zinazotokana na walimu kutopata mafunzo kazini. Athari hizo ni pamoja na kushuka

kwa kiwango cha elimu kutokana na wanafunzi kutokuwa na uelewa wa kutosha katika masomo, na

hatimaye kumaliza elimu ya msingi bila maarifa wala ujuzi wa kuwawezesha kukabiliana na changamoto

mbalimbali za maisha.

Hadithi hii yenye kichwa cha habari “Elimu Bora Bila Mafunzo Endelevu kwa Walimu kazini?” pia

inalenga kuonesha umuhimu wa mafunzo kwa walimu kazini sambamba na kuwahamasisha walimu

kujua haki zao za msingi na kuzitetea ikiwa ni pamoja na haki ya kupata mafunzo kazini. Inamulika

ushiriki wa wananchi katika upatikanaji wa elimu, wajibu wa wazazi kushiriki katika vikao na kutoa

maoni na mapendekezo yao kuhusu maendeleo ya elimu kwa watoto wao na shule kwa ujumla,

ili kufanikisha upatikanaji wa elimu bora nchini. Mhusika mkuu katika hadithi hii ni mtoto “Sadiki”

anayetumika kuonesha harakati za kuleta mabadiliko katika shule yao, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa

ikifanya vibaya kutokana na wanafunzi kuwa na uelewa mdogo katika masomo. Hali hii ilisababishwa

na walimu kutokuwa na mbinu mpya za ufundishaji kutokana na ukosefu wa mafunzo kwa walimu

kazini. Lakini baada ya walimu kuanza kupata mafunzo kazini, ufanisi katika shule ile ulibadilika kwa

kiwango kikubwa.

4

Lete mawazo yako kuhusu kitabu hiki:

Tarehe ya kupokea kitabu hiki ……………………………

Jina…………………………………………………………...............

Anwani ya Posta…………………………………………….........

Namba ya simu……………………………………………………..

Barua pepe……………………………………………………………

Jinsi Mme / Mke

Umri

Kiwango cha Elimu

7 – 14 Elimu ya Msingi

15 – 19 Elimu ya Sekondari

20 – 30 Chuo

31 – 40

Zaidi ya 41

1. Kitabu hiki kina habari muhimu?

Ndiyo Hapana Kiasi

2. Kitabu hiki kina manufaa?

Ndiyo Hapana Kiasi

3. Kitabu hiki kinaeleweka kiurahisi?

Ndiyo Hapana Kiasi

4. Kitabu hiki kinavutia?

Ndiyo Hapana Kiasi

5. Kitabu hiki kimeandikwa vizuri?

Ndiyo Hapana Kiasi

6. Umependa michoro ya kitabu hiki?

Ndiyo Hapana Kiasi

40

Umependa nini kwenye kitabu hiki?

Kitabu hiki kinawezaje kuboreshwa?

Unategemea kutumiaje kitabu hiki?

Mengineyo:

Ukimaliza kujaza fomu hii itume kwa: HakiElimu, Uchapishaji, SLP 79401, Dar es Salaam.

41

Kuhusu kijitabu hiki

Hali ya elimu katika kijiji cha Kisiwani ni mbaya. Kiwango cha ufaulu kwa

wanafunzi wa shule ya Msingi Ilaba kiko chini sana. Shule hii inakabiliwa

na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanafunzi kutokufaulu

kutokana na ukosefu wa walimu wenye taaluma ya kutosha kufundisha

kwa kiwango kinachotakiwa, nyumba bora za walimu, pamoja na ukosefu

wa vitabu vya kutosha. Hali halisi ya elimu katika shule ya msingi Ilaba

inawachukiza sana wazazi wa kijiji cha Kisiwani. Mkutano unaitishwa shuleni

kwa lengo la kujadili sababu za wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika

masomo yao. Wazazi, wanafunzi pamoja na walimu wanahudhuria. Kila

mmoja anatoa maoni yake kuhusu hali halisi ya elimu na kutoa mapendekezo

ambayo yanafanyiwa kazi na hatimaye kwa pamoja wanafanikiwa kuleta

mabadiliko ambayo yanasaidia kuleta elimu bora katika kijiji chao. Shule ya

msingi Ilaba iliyokuwa ikifanya vibaya imebadilika na kuwa moja ya shule

zinazofanya vizuri kwani idadi kubwa ya wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo.

Sadiki akiwa ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ilaba ambaye pia anachukizwa na hali halisi ya maendeleo ya elimu katika shule yao. Ingawa

ni mlemavu wa miguu, anafanya juhudi za makusudi kwa kuwahamasisha na kuwaongoza wenzake katika harakati za kuleta mabadiliko

katika shule yao. Harakati hizi zinazaa matunda yanayorudisha tena matumaini mapya kwa wanafunzi, walimu na wananchi wa Kisiwani

kwa ujumla. Kutokana na mafanikio hayo wazazi, walimu na wanafunzi katika kijiji cha Kisiwani wanadhamiria kushirikiana zaidi katika

kuendeleza harakati za upatikanaji wa elimu bora na kuhakikisha shule yao inaendelea kuwa shule bora na ya kuigwa katika wilaya yao.

HakiElimu inafanya kazi kufikia usawa, ubora, haki za binadamu na demokrasia katika elimu kwa

kuwezesha jamii kubadili shule na mfumo wa sera za elimu,

kuchochea mijadala yenye ubunifu na kuleta mabadiliko,

kufanya utafiti yakinifu, kudadisi, kufanya uchambuzi na utetezi na

kushirikiana na wadau kuendeleza manufaa ya pamoja na haki za jamii.

SLP 79401 • Dar es Salaam • Tanzania

Simu: (255 22) 2151852 au 3 • Faksi: (255 22) 2152449

info@hakielimu.org • www.hakielimu.org

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!