Kilimo bora cha zao - Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives

Kilimo bora cha zao - Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives Kilimo bora cha zao - Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives

18.02.2015 Views

UTANGULIZI Zao la soya lina protini nyingi yenye ubora wa hali ya juu kuliko iliyoko katika aina nyingine ya mazao ya mimea. Kiasi cha protini katika soya inazidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai na maziwa. Sifa nyingine za zao la soya ni pamoja na kuwa na mafuta yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol), uwezo wa mmea wa soya kuongeza mbolea aina ya nitrojeni kwenye udongo, gharama ndogo za uzalishaji ukilinganisha na mazao mengine, uwingi wa protini unaoweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na kinga kwa magonjwa ya kansa, shinikizo la damu na kuwaongezea nguvu wagonjwa wa UKIMWI na magonjwa mengine. Aidha, uwezo wa soya kustawi katika maeneo yanayostawisha mahindi na maharage unamaanisha kwamba zao hilo linaweza kulimwa sehemu nyingi nchini Tanzania. Sifa hizo zimefanya zao la soya kuwa muhimu katika chakula cha binadamu na mifugo na katika kutengeneza bidhaa mbalimbali za vyakula na madawa. Pamoja na manufaa hayo ya zao la soya, zao hilo halifahamiki kama ilivyo mazao mengine mfano maharage na mahindi. Wakulima wengi hawazijui kanuni za kilimo bora cha soya. Hii inatokana na kutojua umuhimu wa zao hilo na hivyo kutotilia maanani katika kulilima na kulitumia kuboresha afya na kipato hasa katika ngazi ya kaya. Lengo kuu la kijitabu hiki ni kuwafahamisha wakulima, maafisa ugani na wadau wengine faida zinazotokana na uzalishaji na matumizi ya soya. Pia kijitabu hiki kina lengo la kuhamasisha wakulima na kuendeleza uzalishaji na matumizi ya zao hilo lililoingizwa nchini kwa mara ya kwanza mwaka wa 1907. Ni matarajio ya Wizara ya kuwa wakulima na wadau wengine watafaidika kwa kutumia kijitabu hiki kwa ajili ya kuendeleza na kuongeza uzalishaji, tija na matumizi ya soya hapa nchini. iv kijitabu hitimisho.indd 6 5/17/06 11:36:04 PM

SURA YA KWANZA HISTORIA, UMUHIMU NA AINA ZA SOYA Historia ya zao la Soya nchini Tanzania Soya (Glycine max) ni zao la jamii ya mikunde. Zao hilo asili yake ni nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800 iliyopita. Zao la soya liliingizwa nchini Tanzania mwaka wa 1907 katika maeneo ya Amani mkoani Tanga. Kati ya miaka ya 1930 na 1960, kilimo cha soya kilipanuka na kuenea hadi maeneo ya Nachingwea mkoa wa Mtwara, Kilosa mkoa wa Morogoro na Peramiho mkoa wa Ruvuma. Kuenea kwa zao hilo katika maeneo hayo kulitokana na msukumo wa mashirika ya Overseas Food Co-operation – (OFC), State Trading Cooperation (STC), General Agricultural Production for Export – (GAPEX) na National Milling Corporation – (NMC). Mashirika hayo yalisafirisha soya kwenda katika nchi za Japan na Singapore. Kwa kuwa uzalishaji wa zao hilo katika mikoa hiyo ulilenga soko la nje, wananchi hawakufundishwa matumizi yake na kwa sababu hiyo baada ya mashirika hayo kuacha biashara ya zao hilo kilimo cha soya kilififia hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambapo uzalishaji ulianza tena baada ya jamii kuhamasika katika matumizi ya soya hasa katika kutengeneza vyakula vya watoto. 1 kijitabu hitimisho.indd 7 5/17/06 11:36:04 PM

SURA YA KWANZA

HISTORIA, UMUHIMU NA AINA ZA SOYA

Historia ya zao la Soya nchini Tanzania

Soya (Glycine max) ni zao la jamii ya mikunde. Zao hilo asili yake

ni nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800

iliyopita. Zao la soya liliingizwa nchini Tanzania mwaka wa 1907

katika maeneo ya Amani mkoani Tanga. Kati ya miaka ya 1930

na 1960, kilimo cha soya kilipanuka na kuenea hadi maeneo ya

Nachingwea mkoa wa Mtwara, Kilosa mkoa wa Morogoro na

Peramiho mkoa wa Ruvuma. Kuenea kwa zao hilo katika maeneo

hayo kulitokana na msukumo wa mashirika ya Overseas Food

Co-operation – (OFC), State Trading Cooperation (STC), General

Agricultural Production for Export – (GAPEX) na

National Milling

Corporation – (NMC). Mashirika hayo yalisafirisha soya kwenda

katika nchi za Japan na Singapore.

Kwa kuwa uzalishaji wa zao hilo katika mikoa hiyo ulilenga soko

la nje, wananchi hawakufundishwa matumizi yake na kwa sababu

hiyo baada ya mashirika hayo kuacha biashara ya zao hilo kilimo

cha soya kilififia hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni

mwa miaka ya 1990 ambapo uzalishaji ulianza tena baada ya jamii

kuhamasika katika matumizi ya soya hasa katika kutengeneza

vyakula vya watoto.

1

kijitabu hitimisho.indd 7

5/17/06 11:36:04 PM

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!