Kilimo bora cha zao - Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives

Kilimo bora cha zao - Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives Kilimo bora cha zao - Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives

18.02.2015 Views

Mchoro Na. 2a: Shamba la soya - Sesa. Mchoro Na. 2b: Shamba la soya - Matuta ya kukinga mteremko. 10 kijitabu hitimisho.indd 16 5/17/06 11:36:23 PM

eneo analotaka kulima soya hususani mahitaji ya mvua. Kwa sababu hiyo ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri toka kwa mtaalam aliyekaribu naye kabla ya kuamua kulima soya. Aidha, mkulima anashauriwa kununua na kutumia mbegu kutoka katika sehemu ambazo chanzo cha mbegu hizo kinaeleweka. Mfano wa sehemu hizo ni pamoja na maduka ya pembejeo, wakala wa mbegu, mashamba ya mbegu na vituo vya utafiti. Hii ni kwa sababu mbegu ya soya hupoteza nguvu ya uotaji katika msimu mmoja hasa katika sehemu za joto. Kwa hiyo mkulima anatakiwa kuhakikisha kuwa anapanda mbegu itakayoota. Kama mkulima hana uhakika na chanzo cha mbegu au ana wasiwasi wa kuota kwa mbegu alizonazo anaweza kufanya majaribo ya uotaji (germination test) kabla ya kupanda. Njia rahisi ni kuzilowesha mbegu kwa maji na kisha kuziweka kwenye kitambaa mahali penye joto la kutosha. Mbegu ziloweshwe na maji kila siku mpaka zitakapoota. Hesabu mbegu zilizoota na iwapo mbegu zilizoota ni chini ya 75 kati ya mbegu 100 yaani asilimia 75, mkulima anashauriwa kutopanda mbegu hizo. Wakati wa kupanda Upandaji wa soya unategemea na aina na mahali husika. Kwa aina za soya zinazokomaa mapema, soya ikipandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua katika maeneo yanayopata mvua kwa kipindi kirefu itakomaa wakati mvua bado zinaendelea kunyesha na hivyo kufanya uvunaji na ukaushaji kuwa mgumu na kuhitaji nguvu kazi na muda wa ziada la sivyo mbegu zitaoza au kuanza kuota na kupoteza ubora wake. Kwa hiyo ni budi kujua mwenendo wa mvua mahali husika ili kupanda kwa wakati na aina ya soya kulingana na mahali hapo. Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa soya inakomaa wakati hakuna mvua ili kurahisisha uvunaji 11 kijitabu hitimisho.indd 17 5/17/06 11:36:23 PM

Mchoro Na. 2a: Shamba la soya - Sesa.<br />

Mchoro Na. 2b: Shamba la soya - Matuta ya kukinga mteremko.<br />

10<br />

kijitabu hitimisho.indd 16<br />

5/17/06 11:36:23 PM

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!