18.02.2015 Views

Jinsi ya kudhibiti mbu katika mikorosho

Jinsi ya kudhibiti mbu katika mikorosho

Jinsi ya kudhibiti mbu katika mikorosho

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

1 2

3

JINSI YA KUDHIBITI MBU KATIKA

MIKOROSHO

1.0 Utangulizi.

Kuna aina mbili za mbu wa korosho ambao

huleta uharibifu mkubwa sana katika zao la

korosho, hasa katika kanda ya kusini:

♦ Mbu wa mikorosho (Helopeltis spp)

♦ Mbu wa minazi (Pseudotheraptus wayii)

1.1 Mbu wa Mikorosho (Helopeltis spp)

Helopeltis ni wadudu jamii ya mbu wenye

uwezo wa kuruka toka mkorosho hadi

mwingine. Wadudu hawa wenye urefu wa

milimita 5 - 10, wana mchanganyiko wa rangi

ya njano, nyukundu na sehemu ya weusi

kwenye mabawa (Picha 1). Wadudu hawa

huchangamka na kurukaruka nyakati za

mchana, lakini asubuhi huwa watulivu

kutokana na hali ya ubaridi.

1.2. Mbu wa Minazi (Pseudotheraptus wayii)

Mbu wa minazi wanafanana na wadudu

waitwao kangambili ambao ni maarufu sana

kwenye pamba na sufi. Wadudu hawa wana

mchanganyiko wa rangi ya udongo na

nyekundu na wana urefu wa milimita 14 - 15.

Wadudu hawa wakiguswa hutoa harufu kali

kama njia ya kujihami. Wanafahamika vizuri

kwa majina ya kilugha kama vile “Nanoli”

(Kimakonde); “Nandoli” (kimwera, kiyao).

2.0. Mashambulizi

Aina hizi za mbu hushambulia maeneo

machanga hasa majani, machipukizi, maua na

tegu pia. Mbu hawa hutoboa eneo la

mashambulizi kwa kutumia mwiba wa kwenye

midomo yao na kwa kufanya hivyo, mate yao

yenye sumu huingia ndani ya mmea. Mate

yenye sumu huleteleza makovu meusi katika

maeneo ya mashambulizi. Majani

yaliyoshambuliwa huweza kukunjamana,

hatimaye kukauka. Machipukizi na maua

yanaweza kudumaa yasiendelee na ukuaji,

huku yakibaki na makovu meusi.

Penye mashambulizi makali ya mbu wa

mikorosho, machipukizi kukauka pamoja na

majani na kusababisha ugonjwa uitwao

“debeki”. Ukaukaji huanza nchani na

kuteremkia chini ya chipukizi. Mashada ya

maua yaliyoshambuliwa hushindwa kuzaa

kabisa. Miti iliyoshambuliwa sana huonekana

kama imebabuka na moto.

Mbu wa minazi hushambulia pia tegu na

mabibo machanga na kuacha makovu meusi

yenye kuzama ndani kwenye ganda. Tegu

zilizoshambuliwa zikiwa changa sana,

hubadilika rangi na kuwa nyeusi, husinyaa,

kisha hupukutika chini. Pia baadhi ya korosho

hizo huambatana na makovu.

3.0. Jinsi ya Kuthibiti Mbu waharibifu.

Mbu hawa wa aina zote mbili, pamoja na

wadudu wa aina nyingine nyingi, wanaweza

kuthibitiwa kwa njia mbili:

3.1 Kutumia madawa

Aina mbalimbali za madawa zimefanyiwa

utafiti wa kina na kuonekana kwamba dawa

aina ya KARATE ni bora kwa kuangamiza

wadudu wa aina nyingi. Dawa hii hupuliziwa

kutumia mashine za moto (Mist blower) au za

kawaida (Knapsack sprayer) kutegemeana na

ukubwa wa mkorosho. Kiwango

kilichopendekezwa ni kuchanganya mililita 3 -

5 za dawa kwa lita moja ya maji kwa mti

mkubwa. Upuliziaji unaanza mara baada ya

kuonekana mashambulizi na kurudia

inapobidi. Matunda yaliyopuliziwa dawa

yasitumike mpaka baada ya siku 21 (wiki 3).

3.2 Kutumia uthibiti wa kibaolojia

(Biological control).

Pamoja na uwezo mkubwa wa kuthibiti na

kuangamiza wadudu kwa kutumia madawa,

lakini madawa ni ya gharama mno na yana

madhara sana katika mazingara yetu, ikiwa ni

pamoja na kuua wadudu wenye manufaa kwa

mazao yetu. Kwa ajili hiyo jitihada za kiutafiti

zinafanyika ili kumsaidia mkulima kupunguza

uwezekano wa kutumia madawa katika mazao.

Utafiti wa kina umefanyika kuchunguza kama

kuna wadudu aina nyingine ambao wanaweza

kutumika kuangamiza wadudu waharibifu wa

mikorosho. Hatimaye imeonekana kwamba

wadudu aina ya Majimoto (Oecophylla

longinoda) wanao uwezo mkubwa wa

kuangamiza aina zote za mbu waharibifu wa

mikorosho. Katika uchunguzi wetu, majimoto

4 5

wameonekana mara nyingi tu wakikamata aina

hizi za mbu wa mikorosho na kuwakokota hadi

kwenye viota vyao kwa ajili ya kufanya

chakula. Baadhi ya viota vilivyowahi

kufunguliwa, vimekutwa na mabaki ya sehemu

ya mbalimbali za mbu hawa, kama vile

mabawa, miguu, midomo nk.,

Matokeo ya majaribio yetu yameonyesha wazi

kwamba mikorosho yenye majimoto wengi

haishambuliwi na mbu wa mikorosho.

Majimoto wakitanda kwenye machipukizi,

maua au tegu hufanya ulinzi mzuri sana dhidi

ya mashambulizi ya mbu waharibifu. Kwa ajili

hiyo majimoto hujulikana kama rafiki wa

mkulima.

NB: Pata nakala yako ya maelekezo (Na. 3)

juu ya “Majimoto rafiki wa mkulima”

A

B

C

D

UTAFITI NA MAENDELEO

KANDA YA KUSINI

JINSI YA

KUDHIBITI MBU KATIKA

MIKOROSHO

Picha A: Mbu wa Mikorosho (Helopeltis spp)

Picha B: Mashambulizi ya mbu wa Mikorosho

Picha C: Mbu wa Minazi (P. wayii )

Picha D: Mashambulizi ya mbu wa Minazi

Imetolewa na

KITUO CHA UTAFITI,

NALIENDELE,

S. L. P. 509,

MTWARA

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!