28.01.2015 Views

Frontier Tanzania Environmental Research REPORT 100

Frontier Tanzania Environmental Research REPORT 100

Frontier Tanzania Environmental Research REPORT 100

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Frontier Tanzania Environmental Research

REPORT 100

ELIMU YA MAZINGIRA YA BAHARI

MUONGOZO WA MWALIMU

Frontier Tanzania

February 2004

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

ii

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Frontier-Tanzania Marine Research Programme

REPORT 100

Elimu ya mazingira ya bahari ya

kitropiki

Muongozo wa mwalimu

Mumby, R., Fanning, E. Muruke, M. and St John, F. (eds)

Kingereza Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mazingira Kiswahili

Na Ushirika

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari

Jumuiya ya Kuhifadhi Mazingira

50-52 Rivingston Street

London UK

EC2A 3QP

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

S. L. P. 35064

Dar es Salaam

Tanzania

Pemba 2004

iii

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Suggested Technical Report citation:

Frontier Tanzania (2004). Marine environmental education: A Teacher’s Guide (Kiswahili). Frontier

Tanzania Environmental Research Report 100. The Society for Environmental Exploration, London,

UK, The University of Dar es Salaam, The Institute of Marine Science, Zanzibar, DfID Small Grants

Scheme and the Ministry of Agriculture, Natural Resources, Environment and Co-operatives, Zanzibar.

The Frontier-Tanzania Environmental Research Report Series is published by:

The Society for Environmental Exploration

50-52 Rivington Street

London, EC2A 3QP

United Kingdom

Tel: +44 (0)20 7613 3061

Fax: +44 (0)20 7613 2992

Email: research@frontier.ac.uk

Web Page: www.frontier.ac.uk

ISSN 1479-1161 (Print)

ISSN 1748-3670 (Online)

ISSN 1748-5124 (CD-ROM)

iv

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

© Frontier Tanzania 2004, 2005

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mazingira na Ushirika (MANREC)

Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mazingira na Ushirika ni sehemu ya Serikali ya

Mapinduzi ya Zanzibar. Idara ya Mazao ya Biashara, Matunda na misitu (DCCFF) ni

sehemu ya wizara na inawajibika na muongozo wa uanzishaji wa sera ya misitu na

maeneo tengefu, ikiwa ni pamoja na eneo tengefu la bahari la kisiwa cha Misali

(MIMCA) visiwani Zanzibar.

Frontier Tanzania (FT)

Frontier Tanzania ni uhusiano kati ya shirika la kuchunguza mazingira na Chuo Kikuu

cha Dar es Salaam. Shughuli za utafiti katika shirika hili zimeendelea tangu Julai 1989

na zimehusisha watafiti toka Tanzania na nchi za nje. Utafiti unafanywa kwenye aina

tofauti za mazingira yenye baolojia maalum na hadhi za uhifadhi. Maeneo

yanayochunguzwa hujumuisha misitu, savana za kitropiki, uvuvi, miamba ya

matumbawe, mikoko na nyasi za baharini.

Frontier Tanzania Marine Research Programme (FT MRP)

Huu ni mradi uliofanya utafiti wa kibahari, kisiwa cha Mafia (1989-1994), Songo

Songo (1994-1995), na Mtwara (1996-2000). Mradi ulihamia Pemba ambayo ni

sehemu ya Zanzibar mwaka 2001 ukilenga kisiwa cha Misali. Frontier Tanzania

inafanya kazi kwa kushirikiana na MANREC na Taasisi ya utafitu wa sayansi za bahari

(IMS) katika utekelezaji wa shughuli zake.

Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam (UDSM)

Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kilianzishwa Julai 1970 kama kitiuo cha mafunzo na

utafiti katika sayansi za aina mbalimbali. Chuo kinatafiti mimea na wanyama wa

Tanzania na kinafanya utafiti wa uimarishaji wa mazingira na matumizi endelevu ya

maliasili za nchi.

Shirika la kuchunguza mazingira (SEE)

Shirika hili lilianzishwa mwaka 1989 na linafanya kazi isiyo ya kibiashara.

Madhumuni ya Shirika hili ni kukuza, kuendeleza utafiti juu ya mazingira na

kutekeleza miradi kwa vitendo itakayosaidia kuhifadhi mazingira na maliasili zake.

Miradi iliyoanzishwa na kusimamiwa na Shirika hili hushirikisha pia wawakilishi wa

kitaifa wa utafiti katika nchi husika.

v

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

KWA MAWASILIANO ZAIDI

Ministry of Agriculture Natural Resources

Environment & Co-operatives

P.O. Box 159, Zanzibar, Tanzania

Tel: +255 24 223 2840

Fax: +255 24 223 0290

Frontier-Tanzania: Head Quarters

PO Box 9473, Dar es Salaam

Tel: +255 22 2780 063

Email: frontier@africaonline.com

Department for Commercial Crops Fruits & Forestry

PO Box 3526, Zazibar, Tanzania

Tel: +255 24 223 8628

Fax: +255 24 223 6089

Email: dccff@zanlink.com

Dept. of Zoology & Marine Biology

University of Dar es Salaam

P.O. Box 35064, Dar es Salaam, Tanzania

Tel: +255 22 2410462

E-mail: zoology@udsm.ac.tz

The Institute for Marine Sciences

University of Dar es Salaam

P.O. Box 668, Zanzibar, Tanzania

Tel: +255 24 223 0741 / 2128 / 3472

Fax: +255 24 223 3050

Society for Environmental Exploration

50-52 Rivington Street

London, EC2A 3QP. U.K.

Tel: +44 (0)20 7613 3061

Fax: +44 (0)20 7613 2992

E-mail: research@frontier.ac.uk

Internet: www.frontier.ac.uk

vi

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Yaliyomo

Utangulizi Kuhusu Elimu ya Mazingira na Muongozo Huu..............................ix

Kwa nini tunataka Kuhifadhi Mazingira ya Bahari..........................................ix

Maendeleo Endelevu..............................................................................................x

Madhumuni ya FT MRP.......................................................................................xi

Mpango wa Utafiti wa Bahari ..............................................................................xi

Historia Ya FT MRP........................................................................................... xii

SEHEMU YA KWANZA .......................................................................................1

1. Utangulizi Kuhusu elimu ya mazingira ya bahari .........................................2

2. Mikoko (Mikandaa) .........................................................................................3

3. Eneo la maji kupwa na kujaa..........................................................................6

4. Nyasi za Baharini ............................................................................................8

5. Miamba ya Matumbawe.................................................................................10

6. Uhusiano wa Mifumo ya Maisha ya Viumbe Hai Baharini........................13

7. Mambo Unayopaswa na Usiyopaswa Kufanya Baharini ............................15

8. Tishio Linaloyakabili Mazingira ya Bahari .................................................17

SEHEMU YA PILI...............................................................................................19

Shughuli zinazofanyika wakati wa ufundishaji..................................................19

1. Masanamu ya kuchorwa................................................................................20

2. Kusanifu matangazo (mabango)...................................................................21

3. Chemsha bongo ya elimu ya mazingira........................................................22

4. Mchezo wa taa za barabarani........................................................................25

5. Kusema hapana kwa takataka ......................................................................27

6. Mfumo wa ushirikiano wa chakula – 1 ........................................................29

7. Mfumo / mtandao wa chakula (Uhusiano wa viumbe) 2.............................31

8. Matembezi ya nyika hai .................................................................................34

Marejeo .................................................................................................................36

SHUKRANI:

FT MRP inapenda kulishukuru shirika la kuchunguza mazingira (SEE) kwa kufadhili

shughuli mbalimbali za Elimu ya Mazingira, wanafunzi na walimu walioshiriki

katika shughuli hizo, kutoka skuli za Kangani, Fidel Castro na Mizingani, Wizara ya

Elimu Afisi za Pemba hasa Mr Hussein (Afisa Kiongozi) kwa kutoa kibali cha

kuendesha shughuli hizo. FT MRP pia inawashukuru Mr Ambakisye Simtoe kwa

kuandaa shughuli za uelimishaji na kutafsiri muongozo huu, na Chuo Kikuu cha Dares-salaam

kwa kusaidia shughuli za FT MRP za utafiti na watafiti wasaidizi wa kati

ya mwaka 2001 na 2003.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100

vii

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

ACKNOWLEDGEMENTS

This report is the culmination of the advice, co-operation, hard work and expertise of many

people. In particular acknowledgments are due to the following:

SOCIETY FOR ENVIRONMENTAL EXPLORATION

Managing Director: Ms. Eibleis Fanning

Programme Manager (Operations): Mr. Matthew Willson

Programme Manager (Research): Ms. Nicola Beharrell

Project Administration:

Mr. Mike Lamb

UDSM

FT Co-ordinators:

Dr. M. Muruke & Prof. K. M. Howell.

FRONTIER-TANZANIA

Project Co-ordinator: Ms. Carol Daniels

Research Co-ordinator:

Mr. Angus McVean

Assistant Research Co-ordinators: Mr. Edward Mayhew, Ms. Ruth Mumby, Mr. Adam

Pharoah

Environmental Education Officer: Mr. Ambakisye Simtoe

Dive Officer:

Mr. Paulo Pizzolla

Logistics Managers:

Mr. Luke Gordon

Boat Crew:

Mr. Mussa Abdalah, Mr. Khashim Abdallah, Mr,

Mzee Salum Seifu

Security:

Mr. Juma Mbaya Juma, Mr. Ali Osman Khamis, Mr.

Sibouri Makame Kombo

Cook:

Mr. Ramadhani Juma Songoro

Research Assistants:

Ms. Alice Addison, Mr. Andrew Ashton, Ms.

Katherine Barber, Mr. Matthew Bennett, Mr.

Michael Brown, Ms. Hilary Cartwright-Taylor, Mr.

Alasdair Cockburn, Ms. Charlotte Cranfield, Mr.

Sharif Mohammed Faki, Mr. Christopher Faunce-

Brown, Ms. Anna Franheim, Mr. Conrad Freese, Mr.

Peter Nestory Gabagambi, Mr. Angus Galloway, Ms.

Lydia Gaspare, Mr. Christopher Goatley, Ms.

Eleanor Harrison, Ms. Jacqui Height, Mr. David

Henderson, Ms. Frances, Ms. Lorraine Howe, Illsley,

Ms. Louise Jary, Mr. Ben Jones, Mr. Ali Kitwana,

Ms. Emilia Lascelles, Ms. Andrea Leedale, Ms.

Helen Lofthouse, Mr. Edward Lousley, Mr. Chris

Lovett, Ms. Christine McIntyre, Mr. Jacob Miller,

Mr. Zahor Mohammed, Ms. Lauren Morgan, Mr.

James Moss, Mr. Mathias Msafiri, Mr. Kevin

Murphy, Ms. Olivia Palin, Mr. Adam Partington, Mr.

Rashid Juma Rashid, Mr. David Roadknight, Mr.

Andy Roddis, Mr. Peter Shunula, Mr. Julian Skeels,

Ms. Rachael Smith, Ms. Eike Stubner, Ms. Elinor

Thomas, Ms. Betty Vestberg, Ms. Rhiannon

Williams,

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100

viii

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Local Staff

Utangulizi Kuhusu Elimu ya

Mazingira na Muongozo Huu

Kwa miongo kadhaa elimu ya mazingira imekuwa ikifundishwa duniani kote kwa

msisitizo mkubwa. Si muhimu kuwa imekuwa rasmi au la, lakini elimu ya mazingira

imekuwa ikifundishwa kwa njia zote rasmi na zisizo rasmi kwa watu wa rika na

mifumo tofauti. Elimu ya mazingira inapaswa kutoa msingi wa mabadiliko wa muda

mrefu ambao unaweza kutumika katika maisha ya kila siku kwa kujiendeleza kiujuzi,

matokeo ya kazi za vitendo na uwajibikaji binafsi.

Katika kukabiliana na hali halisi na kwa njia sahihi, ni muhimu kwa muelimishaji

kuielewa jamii husika na yanayoizunguka. Ni lazima ikumbukwe kuwa maarifa na

mawazo kutoka katika jamii na tamaduni tofauti huwa havishabihiani pamoja. Hivyo

mwelimishaji lazima awe na uwezo wa kubadilika na mwenye kupenda kujifunza ili

kuwa na ujuzi unaohitajika kwa jamii husika. Waelimishaji wa mazingira lazima

wahakikishe kuwa elimu inatolewa kwa njia sahihi ili kuongeza uwezo endelevu

katika hifadhi ya mazingira.

Mwongozo huu umeandaliwa kwa ajili ya waalimu na waelimishaji wengine wa

elimu ya mazingira. Sehemu ya kwanza inatoa utangulizi wa mazingira ya bahari

kufuatana na mgawanyiko wa mfumo wa maisha ya viumbe hai baharini; kwenye

mikoko, maeneo ya maji kupwa na maji kujaa, nyasi za baharini na miamba ya

matumbawe

Sehemu ya pili ya mwongozo huu ina shughuli mbalimbali zinazoweza kufanyika

wakati wa uelimishaji ili kusisitiza elimu ya mazingira kwa vitendo. Shughuli hizi si

halisi lakini zinatoa mwongozo juu ya mwelekeo halisi wa mazingira ya bahari na

shughuli za hifadhi. Ukitumika pamoja na vifaa vingine utakuwa msaada mkubwa

kama kifundishio msaada. Izingatiwe kuwa baadhi ya maeneo ya mwongozo huu

hayana tafsiri ya moja kwa moja ili kukidhi mahitaji ya jamii husika.

Kwa nini tunataka Kuhifadhi

Mazingira ya Bahari

• Bahari inatoa rasilimali zitumikazo na watu waishio pwani.

• Mazingira yanayozunguka bahari kama vile mikoko na nyasi za baharini

zinahitajika kuhifadhiwa, kama kimojawapo kitaharibiwa kitaathiri kingine.

• Kuongezeka kwa idadi ya watu, kunamaanisha kuongezeka kwa msukumo

kwenye mazingira ya bahari, matokeo hayo yanahitajika kuwa endelevu ili kuwa

na uhakika wa rasilimali za baadaye.

• Mazingira mazuri ya bahari hutoa uhakika wa kuwepo kwa rasilimali za kutosha

kwa jamii za pwani.

• Mazingira mazuri ya bahari huwa kivutio kikubwa cha utalii na hivyo kukuza pato

la Taifa.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100

ix

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Maendeleo Endelevu

Maendeleo endelevu ni hali ya mabadiliko ambayo huhusisha matumizi ya rasilimali,

mielekeo ya uwekezaji, mzunguko wa maendeleo ya teknolojia, na mabadiliko ya

kitaasisi yenye utulivu na mwelekeo wa kumsaidia binadamu kupata mahitaji yake

kwa sasa na baadaye (Taarifa ya WCED, 1987).

Hii haimaanishi kuwa bahari na ardhi visitumike kwa chakula na nishati, lakini ni

kusema kwamba rasilimali hizi zitumike kwa sasa na kuwepo pia rasilimali za

kutosha kwa vizazi vijavyo kwa viwango vilevile au vikubwa zaidi kuliko vya sasa.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100

x

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Madhumuni ya FT MRP

Mpango wa Utafiti wa Bahari

Utafiti wa makazi na rasilimali za bahari hufanywa ili kutoa taarifa (Takwimu)

muhimu kwa mwongozo wa matumizi ya rasilimali hizo kupitia uchoraji wa ramani

zinaonyesha kiasi cha rasilimali na mgawanyiko wake kwenye maji yenye kina chini

ya meta 30 na mifumo ya kimaisha ya viumbe hai iliyoko kwenye eneo la maji kupwa

na maji kujaa. Takwimu hizi za msingi hutoa nafasi kwa utafiti yakinifu kufanyika.

Hali za kibaologia, samaki waishio kwenye miamba ya matumbawe, idadi ya

matumbawe na idadi ya wanyama wasio na uti wa mgongo vitafanyiwa utafiti kwa

kutumia kielelezo cha hali ya juu kilichobuniwa na kufanyiwa marekebisho kwa

miaka 12 ya kuwepo kwa FT MRP.

Takwimu zinazokusanywa zitafanya kazi muhimu ya msingi katika kusimamia azma

ya kuruhusu na kufanikisha madhumuni ya uongozi na utaratibu wa muda mrefu.

Utafiti hufanywa na wafanyakazi wa FT MRP, watafiti wasaidizi toka mataifa

mbalimbali na washirikishwaji toka taasisi mbalimbali kama vile Taasisi ya Sayansi

za Bahari (IMS), Idara ya Mazao ya Biashara, Matunda na Misitu (DCCFF) na Idara

ya Uvuvi na Rasilimali za Bahari (DFMR). Watafiti wote hufundishwa na

kusimamiwa na wanabiologia ya bahari waliobobea .

Vyanzo vya fedha vinapokuwa vizuri na vya uhakika, Vifaa vya kujifunzia hutolewa

bure kwa washiriki kutoka Tanzania, wakati wanafunzi toka ng’ambo hujigharimia

vitu vifuatavyo;

• Cheti cha uzamiaji

• Mafunzo ya utafiti wa bahari

• Cheti cha BTEC ambacho ni sawa na cheti cha Darasa la 14 la uingereza

Kuongeza ufahamu juu ya mazingira ya bahari

• Mafunzo na majadiliano na wadau wa rasimali za bahari

• Kuandaa na kugharimia siku za elimu ya mazingira kwa skuli za Pemba hasa zile

zilizo kandokando ya bahari.

FT MRP haikusudii kuzuia uvuvi Pemba. FT MRP inalengo la kufanya kazi na

wavuvi waliopo, na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha kuwa shughuli za

uvuvi sasa na kwa vizazi vijavyo zinaendelea kuwa endelevu na samaki wa

kutosha wanakuwepo.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100

xi

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Historia Ya FT MRP

Kisiwa cha Mafia 1989 – 1994

Kisiwa cha Mafia kilitunukiwa kuwa eneo tengefu la Kibahari mwaka 1995 ikiwa ni

matokeo ya kazi ya FT MRP iliyofanyika kati ya mwaka 1989 hadi 1994. Kwa sasa

hifadhi hii inasimamiwa na Idara ya Hifadhi za Taifa la Tanzania kwa kushirikiana na

WWF.

Kisiwa cha Songo Songo 1994 – 1996

Baada ya Utafiti Kisiwani Mafia kukamilika huku kukiwa na mafanikio makubwa,

mradi wa FT MRP ulihamishiwa kisiwa kidogo cha Songosongo. Kisiwa hiki kina

aina tofauti za matumbawe ambazo zilichunguzwa na kufanyiwa utafiti wa kina kisha

ramani zikachorwa kuonyesha mpangilio wa rasilimali hizo, kazi iliyofanyika kwa

muda wa miaka miwili. Vilevile kazi ya utafiti wa uvuvi iliyofanyika hapa ilikuwa ya

muhimu zaidi kutokana na wavuvi wengi kukitumia kisiwa hiki kwa mapunziko

mafupi kabla ya kupeleka samaki wao bara.

Kilwa Kivinje 1997

Ulikuwa ni mpango wa muda mfupi uliolenga maeneo ya maingilio ya mto Rufiji

baharini. Taarifa juu ya aina mbalimbali za mikoko zilitumika kutengeneza ramani na

matumizi yake yalichunguzwa kwa kina zaidi. Bahati mbaya eneo hilo lilikutwa likiwa

limeathirika na mradi mkubwa wa ufugaji wa kamba. Madhara zaidi ya mradi huu

yaelekea kusababishwa na kugeuzwa kwa hekta 20,000 za mikoko kuwa mabwawa ya

kufugia kamba.

Rasi za Mnazi, Mikindani na Mtwara 1997 – 2000

Baada ya kutengeneza ramani ya ukanda wa kati wa Pwani ya Tanzania, FT MRP

ilihamishia shughuli zake pwani ya kusini karibu ya mpaka wa Msumbiji. Mradi

ulianza shughuli zake za utafiti Rasi ya Mnazi baada ya kushauriwa na Shirika la

Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ambapo ilipendekezwa kuanzishwa kwa eneo

tengefu la kibahari. Baada ya hapo mradi ulihamia Rasi ya Mtwara mwaka 1998 na

kufanya utafiti eneo lote la ukanda wa Pwani ya Kusini kuzunguka Wilaya ya Mtwara

Mikindani.

Wakati huo takwimu na taarifa juu ya uharibifu wa matumbawe uliosababishwa na

mvua za El-Nino kusini mwa Tanzania. Kwa ujumla zilionyesha uharibifu mkubwa wa

matumbawe na hasa katika pwani ya kusini mwa Tanzania. Kwa hiyo miradi zaidi

ilianzishwa ili kurekebisha / kuondoa uharibifu na kuangalia utengamavu wa

matumbawe. Miradi hii ilikamilika mwishoni mwa mwaka 2000.

Kisiwa Cha Pemba 2001 – 2003

FT MRP ilihamishia shughuli zake kisiwani Pemba mwezi wa pili mwaka 2001.

Kisiwa cha Pemba kiko kaskazini mwa kisiwa cha Unguja na ni kimojawapo kati ya

visiwa vikubwa viwili vinavyounda Zanzibar na kinatambulika Kimataifa kwa kuwa

na rasilimali nyingi za bahari. Kwa pamoja Unguja na Pemba zina maeneo mengi

yenye viumbe hai wa aina tofauti na wenye umuhimu mkubwa kimataifa (UNEP

1989).

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100

xii

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Idadi na aina tofauti ya matumbawe iliyoripotiwa mwaka 1990 visiwani Zanizibar ni

mara mbili zaidi ya ile iliyoripotiwa hapo mwanzo.

Kwa pwani yote ya Africa mashariki na kati pwani ya Pemba ina mikoko mingi (Jean

Veron, Pers comm.) ambayo ni moja ya maeneo makubwa ya uvuvi na hivyo kuwa

chanzo kikubwa cha protini kwa wakazi wake. Mikoko ya Pemba kama ilivyo mingine

yote ya Tanzania inahifadhiwa chini ya mpango maalumu wa hifadhi ili kupunguza

madhara yanayosababishwa na binadamu.

Mipango ya mwanzo ya FT MRP ililenga kwenye mpango wa hifadhi ya maeneo ya

kisiwa cha Misali (MICA) ikiwa ni mipango ya miaka mitutu. FT MRP inafanya kazi

kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mazingira na Ushirika Zanizibar

(MANREC), Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS), Shirika la Kuhifadhi Mazingira ya

Kisiwa cha Misali, (MICA), CARE – Tanzania na wadau asilia.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100

xiii

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

SEHEMU YA KWANZA

1. Utangulizi Kuhusu elimu ya mazingira ya bahari

2. Mikoko (Mikandaa)

3. Eneo la maji kupwa na kujaa

4. Nyasi za baharini

5. Miamba ya Matumbawe

6. Uhusiano wa Mifumo ya Maisha ya Viumbe Hai

Baharini

7. Mambo Unayopaswa na Usiyopaswa Kufanya

Baharini

8. Tishio Linaloyakabili Mazingira ya Bahari

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 1

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

1. Utangulizi Kuhusu elimu ya

mazingira ya bahari

Kihistoria, wakazi wa pwani wameyatumia mazingira ya bahari kujipatia chakula,

vifaa vya ujenzi sehemu za kutabaruku na njia za usafirishaji. Kuongezeka kwa idadi

ya watu, na kukua kwa sayansi na teknologia, kumesababisha ongezeko kubwa la

matumizi ya bahari na mali asili zake na, upande mwingine kumekuwa na ongzeko la

uharibifu wa mazingira na kupungua kwa rasilimali. Baadhi ya viumbe vimepotea na

baadhi viko hatarini kupotea kama vile nyangumi na pomboo. Kwa hiyo hatua za

haraka zinahitajika kuchukuliwa ambazo zitapelekea kuwekwa kwa taratibu na

mwongozo madhubuti wa matumizi ya rasilimali za bahari upande mmoja, na

kuhifadhi mazingira upande mwingine. Hivyo Elimu ya kutosha juu ya mazingira ya

bahari na rasilimali zake inahitajika.

Kabla ya menejimenti ya mazingira kufanyika ni muhimu kuelewa yaliyomo ndani ya

mazingira ya bahari. Sura zifuatazo zinaelezea kwa ufupi yaliyomo kwenye mazingira

ya bahari. Mazingira ya bahari ya kitropiki yanapatikana kati ya nyuzi 25 za latitudi

pande zote mbili za ikweta. Ndani ya ukanda huu mdogo wa mazingira ya bahari

duniani kote huwa katika mpangilio ufuatao toka nchi kavu kwenda baharini.

• Misitu ya mikoko / mikandaa

• Eneo la maji kupwa na kujaa

• Nyasi za baharini

• Miamba ya matumbawe

Kila eneo lina uhusiano na jingine, mara nyingi hutegemeana ili viumbe hai viishi.

Kutegemeana huko kumejadiliwa kwenye sehemu ya kwanza ya mwongozo huu,

ambayo hutoa maelezo ya kila eneo kwa ufupi.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 2

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

2. Mikoko (Mikandaa)

2.1 Utangulizi

Miti na vichaka vya mikoko hupatikana kati ya sehemu ya juu kabisa maji yanapojaa

na sehemu ya chini kabisa maji yanapokupwa. Ni mimea ambayo hustawi vizuri

kutokana na tabia maalum zinazoiwezesha kunawiri kwenye eneo hili, sifa hizo ni

pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kuvumiliwa kiwango kikubwa cha

chumvichumvi ndani ya maji, kuwa na mizizi yenye sifa maalum ya kutoa chumvi

ijulikanayo kama `pneumatophores` ambayo imejitokeza nje ya udongo hivyo

kuruhusu uvutaji hewa rahisi kwenye tope lisilo na hewa (anoxic). Mpangilio wa aina

za mikoko hutegemea uwezo wake kuvumilia chumvi chumvi ndani ya maji, aina ya

udongo ilipomea na hali ya hewa.

Mikoko hutumika kama chanzo cha nishati, miti ya kujengea na pia maeneo ya kuvua

Samaki na shughuli zingine. Mikoko pia hutumika kama mazalio ya wanyama wa

baharini, vifyonza virutubisho na kwenye mzunguko wa virutubisho hivyo, na pia

huzuia mmomonyoko wa udongo pwani. (Semesi na Howell 1989).

Mikoko ilipewa hadhi ya kulindwa Tanzania mwaka 1930, lakini kumekuwa na

kutoelewana kati ya wanavijiji ambao wangependa kutumia maliasili zao na

wanaohusika na kuzihifadhi. Imetokea mara nyingi kuwa wanakijiji hawakuruhusiwa

kutumia mikoko wakati makampuni ya kibiashara yaliruhusiwa kufyeka mikoko kwa

ajili ya kilimo cha mpunga, maeneo ya kutengeneza chumvi au maeneo ya kufugia

samaki (Semesi na Howell 1989). Sheria zaidi zilizopitishwa Zanzibar mwaka 1968

na Tanzania kwa ujumla mwaka 1991, kuzuia kukata mikoko kwa matumizi ya

kibinadamu (Semesi 1998). Sheria hizi zilimaanisha kushabirisha matumizi ya kila

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 3

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

siku na mwongozo endelevu wa mfumo wa maisha ya viumbe hai (Semesi na Howell

1989).

2.2 Mikoko (mikandaa) ya Tanzania

Ukanda wa Pwani wa Tanzania una urefu wa Kilometer 800 na kati ya hizo km 600

zina matumbawe, majani ya bahari na mikoko.

• Moja kati ya maeneo yenye mikoko mingi kabisa Africa Mashariki ni eneo la mto

Rufiji unapoingia baharini lenye ukubwa wa jumla ya Kilometa za mraba 1000

2.3 Mikoko ni nini

• Mimea (miti / vichaka) inayovumilia mazingira ya chumvi inayopatikana eneo la

bahari linalokupwa na kujaa maji

• Mikoko hustawi kati ya eneo la kati na lile la chini kabisa maji yanapojaa na

kupwa na mpangilio wa aina zake hutegemea muda wa maji kujaa

• Mikoko ina sifa maalum zinazoiwezesha kuvumilia muongezeko na mabadiliko

ya chumvichumvi ndani ya maji na hali ya kukosa hewa kwenye udongo

• Kuna aina 60 za mikoko zinazostawi duniani kote, Tanzania inazo 10 kati ya hizo

2.4 Hifadhi ya mikoko

• Ni vigumu sana kulinda maeneo yote ya mikoko kwa kuwa mikoko imesambaa

sehemu kubwa ya pwani ya Tanzania

• Elimu ya umuhimu wa mikoko na ushirikishwaji wananchi vinategemewa

kusaidia utunzaji na matumizi mazuri ya mikoko ili iendelee kuwepo

2.5 Tabia / Sifa maalum za mikoko

Aina zote za mikoko zina tabia / sifa maalum zilizofanana zinazoiwezesha kuwepo

maeneo ilipo.

• `Pneumatophores’ (vikua) hii ni mizizi inayojitokeza nje ya udongo, hutokea sana

kwenye maeneo yenye maji yaliyosimama

• Viotea, hizi ni mbegu nene zenye uzito wa kutosha ambazo humea zingali kwenye

mti mama hivyo huendelea kukua kwa haraka sana zinapoanguka kwenye tope

• Ina uwezo wa kuvumilia kiasi kikubwa cha chumvi chumvi ndani ya maji, lakini

kiwango kikubwa zaidi cha chumvichumvi hizo huweza kuiua mikoko

• Ina uwezo wa kuzuia chumvichumvi kuingia kwenye mfumo wa mikoko

• Majani yake yana ute wa nta juu yake na stomata zilizotumbukia ndani kupunguza

upotevu wa maji baridi

2.6 Kwa nini mikoko ni muhimu

Mikoko huchuja takataka zilizo chini ya ardhi na kufyonza virutubisho kwa kutumia

mizizi hivyo husaidia mzunguko wa virutubisho ambavyo huhitajika na viumbe

vengine.

• Huchuja matamahuruku na takataka kutoka nchi kavu hivyo huzilinda nyasi za

baharini na matumbawe

• Mizizi ya mikoko hufyonza maji baridi hivyo kupunguza kiwango cha maji hayo

kinachoyafikia matumbawe ambacho kikizidi huweza kuyaharibu

• Hupunguza mwendo kasi wa maji na hivyo kuruhusu lava na kamba kuishi salama

• Pia ni makazi salama kwa viumbe mbalimbali

• Chanzo cha chakula kwa binadamu – wanawake huvua samaki kwenye maeneo

haya kwa matumizi ya nyumbani

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 4

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

• Chanzo cha nishati – hasa kwa jamii za pwani

• Hutumika kujengea zio, nyumba, mitumbwi na madema n.k

• Madawa asilia – Madawa ya kutibu magonjwa mbalimbali kama vile magonjwa

ya tumbo na mikwaruzo

• Ni kivutio kikubwa kwa watalii, kwa mfano misitu ya Jozani Unguja

2.7 Ukataji / Uharibuifu wa mikoko

• Ukataji wa mikoko kibiashara na matumizi ya kawaida sio endelevu na hasa

inapokatwa bila uangalizi wowote

• Mikoko hukatwa ili kuchoma mkaa na pia kupata maeneo ya uzalishaji wa chumvi

• Upasuaji wa Mbao

• Kilimo na ufugaji wa samaki

• Umwagaji wa bidhaa za petroli na mabaki mengine

• Matumizi ya kawaida (Uvuvi na nishati) husababisha madhara kidogo kuliko

matumizi ya kibiashara

• Madhara asilia kama vile milipuko ya Volkano na tufani huharibu mikoko pia.

Athari zitokanazo na haya huwa ni kubwa mno hasa kama zitaambatana na

uharibifu unaosababishwa na binadamu

2.8 Matokeo ya kuharibu Mikoko

• Kupungua kwa viumbe hai

• Kuongezeka kwa mmomonyoko wa Pwani, miji iliyo karibu na pwani na mahoteli

ya kitalii vyaweza kuathirika

• Kuongezeka kwa matamahuruku kwenye matumbawe hupunguza uzalishaji na

utalii

• Chakula na nishati vitapungua na hivyo wanawake kulazimika kusafiri mbali

kupata vitu hivyo

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 5

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

3. Eneo la maji kupwa na kujaa

3.1 Utangulizi

Eneo la maji kupwa na kujaa ni ukanda mwembamba, ni eneo ambalo hali ya ardhi

yake hubadilika sana kuliko jingine lolote lile baharini, hivyo ni mazingira yenye

taabu nyingi kwa viumbe wanaoishi hapo. Aidha mwendeleo wa kujaa na kupwa kwa

maji umekuwa ukiviathiri viumbe hai ambao huhitaji uzoefu mkubwa wa mazingira

haya ili viweze kuvumilia mabadiliko makubwa ya joto, chumvichumvi na mawimbi.

Ingawa ni asilimia ndogo sana ya bahari yenye maji kupwa na kujaa duniani kote,

eneo hili limekuwa na umuhimu mkubwa kutokana na kuwa na aina mbalimbali za

viumbe hai. Pia kwa vile hufikika kwa urahisi na lina maliasili nyingi, sehemu nyingi

huambatana na uvunaji mkubwa wa maliasili hizo.

3.2 Umuhimu wake Kibaologia

Eneo la maji kupwa na maji kujaa ni muhimu sana kwa kuwa chanzo kikubwa cha

chakula kwa ajili ya jamii za pwani. Ukusanyaji wa makombe na uvuvi wa pweza na

ngisi huzipatia jamii hizo vyanzo muhimu vya protini kama nyongeza kwa ile

wanayoipata kwenye samaki. Maeneo haya pia huweza kuwa na mchanga au miamba.

Mchanga wa Pwani ni kivutio kkikubwa cha watalii hivyo kuongezeka pato kwa taifa.

Kwa mfano kisiwa cha Misali kina eneo hili kubwa ambalo huvutia watalii kulitumia

kama sehemu ya kujifunza mengi na kupumzika (Kutabaruku).

3.3 Uvunaji na uharibifu

Kutokana na urahisi wa kufikika kwa eneo la maji kupwa na kujaa husababisha

urahisi wa uvunaji wa maliasili zilizopo. Hivyo kama uvunaji huo hautazingatia

taratibu za hifadhi na matumizi endelevu idadi ya viumbe hai inaweza kuathirika.

Kwa kawaida mikuki na fimbo hutumika katika uvuvi wa pweza. Aina hii ya uvuvi

yaweza kuwa endelevu ingawa bado kunahitajika takwimu sahihi ili kuepusha

maamuzi yasiyoshabihiana na ukweli halisi. Kama idadi ya watalii itaongezeka juu ya

kiwango kinachohitajika basi kuna uwezekano wa eneo hili kuathiriwa na shughuli

mbalimbali kama vile kutembeatembea, kutupa taka na kuokota kombe, ambazo

zaweza kuathiri mazingira aslilia.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 6

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

3.4 Uhifadhi wake

Uhifadhi ya maeneo haya hufanana ama na yale ya nchi kavu kwa upande moja au na

yale ya bahari kwa upande mwinginehivyo uhifadhi wake huwamgumu, na hata

katika utekelezaji wa mwongozo wa matumizi yake. Mara kwa mara kuna migongano

juu ya idara ipi inahusika na uangalizi wa eneo hili. Pia kwa jinsi eneo hili

linavyoonekana kama tupu hudhaniwa kuwa halina faida kwa viumbe wengi, mawazo

ambayo sio sahihi.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 7

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

4. Nyasi za Baharini

4.1 Utangulizi

Nyasi za baharini ni mimea ya nchi kavu ambayo imeweza kujijengea tabia ya kuishi

baharini mpaka kina cha meta 50. Kuna aina 50 za majani ya baharini duniani kote,

hupatikana zaidi kwenye maji kuanzia Antaktiki hadi Tanzania. Hufanana na nyasi za

kawaida katika muonekano wake.

4.2 Umuhimu wa majani ya baharini

Majani haya huota kwenye maeneo tofauti kuanzia kwenye tope hadi kwenye miamba

laini na yana uwezo wa kufunika meta moja ya mraba ambayo ya vikonyo vya nyasi

4000 (Nybakken 2001). Vikonyo vya majani hayo huwa na mizizi imara ambayo

huzashikilia vizuri hivyo kushinikiza mashapo sawia. Pia hutoa chakula kwa samaki,

ulumba / ufuma na Kobe wa baharini. Mimea mingine ya baharini hujishikisha

kwenye nyasi hizi. Samaki wadogo wadogo wanaokua hupata chakula, maeneo ya

kujificha na makuzio. Hivyo nyasi za baharini ni makazi na maeneo muhimu ya uvuvi

wa viumbe wadogo wadogo kama vile kamba.

4.3 Manufaa / Matumizi / Uharibifu

Hushikiza vizuri matamahuruku, hii huelezea umuhimu wa majani ya bahari kwa

mfumo bora na imara wa maisha ya viumbe hai. Majani haya huweza kuharibiwa kwa

njia nyingi.

Njia asilia

• Tufani kali

• Mabadiliko ya kiasi cha chumvichumvi ndani ya maji kutokana na kuingia kwa

maji baridi

Binadamu

• Maendelezo ya pwani pamoja na uchimbaji mchanga

• Ujenzi wa mahoteli na viwanda huongeza kasi ya maji na hivyo waweza

kusababishaa ongezeko kubwa la matamahuruku

• Uchafuzi kutokana na umwagaji wa mafuta, maji taka na madawa

• Utiaji nanga na uharibifu wa panga-boya

• Uvuvi wa kupita kiasi

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 8

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

4.4 Matokeo / Madhara

Ili kurudi katika hali ya kawaida baada ya kuharibiwa, nyasi za baharini huchukua

muda wa miaka sita hadi mia moja kutegemea na ukubwa wa uharibifu uliotokea.

Kwa hiyo uharibufu wowote huathiri mfumo mzima wa maisha ya viumbe hai

baharini. Bila nyasi hizi mazalio na makuzio ya viumbe hai wengi yatakosekana na

hivyo kupungua kwa idadi ya viumbe hivyo. Nyasi pia huzuia mashapo yasiyafikie

matumbawe, hivyo kuondolewa kwake kutayaathiri matumbawe kwa kiasi kikubwa.

4.5 Hifadhi yake

Ni rahisi kuzihifadhi nyasi za baharini. Kinachohitajika ni kuweka vikwazo kwa

waendeshaji / Wajenzi wa pwani ili kutoa nafasi kwa majani kustawi tena.

Kwa vile nyasi hizi ni makazi ya aina mbalimbali za samaki na maeneo muhimu ya

uvuvi, ni muhimu kuhakikisha kuwa maeneo hayo hayaharibiwi kwa faida ya wakazi

wa pwani. Kama uharibifu ungalifanywa kwa nia ya kuwanufaisha wakazi wa pwani,

basi manufaa hayo yangalikuwa ya muda mfupi tu. Manufaa yaweza kupatikana kwa

maongozi endelevu. Ulinzi asilia unaotolewa na nyasi baharini kwa matumbawe

hauwezi kufanywa na maumbo ya kuundwa na binadamu.

Waendelezaji wa mahoteli wanaweza kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa nyasi

za baharini. Wajenzi hawa huziondoa nyasi kwa vile husadiki kuwa huleta

muonekano mbaya wa eneo la hoteli kwa wageni na kwenye fukwe za mchanga. Ili

kuzihifadhi, hatua madhubuti zinahitajika kuchukuliwa. Wenyeji wanahitaji

kuelimishwa kuwa majani wasioyapenda yasipokuwepo fukwe na matumbawe

ambayo watalii hulipia kuviona vitakuwa hatarini kutoweka.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 9

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

5. Miamba ya Matumbawe

5.1 Utangulizi

Mara nyingi matumbawe huwa katika mkusanyiko ujulikanao kama “Koloni” la

wanyama wenye uhai ambao huitaji mwanga wa jua na chakula kukua. Kila mnyama

mmoja kwenye koloni huwa na uhusiano wa kufaidiana aina ya mwani ambayo

huonekana kwa darubini tu. Uhusiano huu hufanyika kwa matumbawe kutoka madini

ya chokaa ambayo ndio hutengeneza sehemu kubwa ya mfumo wa miamba ya

matumbawe.

Mimea hii midogodogo ndani ya matumbawe huishi kwa kuzaliana kwa kutumia

mfumo wa mwanga wa jua na hewa ya kabondayoksaid toka kwenye matumbawe.

Wakati huo huo matumbawe hupata hewa ya oksijeni na chakula kutoka kwenye

mimea hii. Lakini pia kuna aina ya matumbawe (Yasiyojenga miamba) huweza kukua

bila ya mimea hii, pia hayahitaji mwanga kukua hivyo hupatikana kwenye kina kirefu.

Kwenye matumbawe pia kuna viumbe wanaotengeneza chokaa inayosaidia kujenga

miamba. Viumbe hivi hujumuisha mwani wa kwenye matumbawe, matumbawe laini,

na wanyama wasio na uti wa mgongo kama vile sponji na makombe madogo

5.2 Umuhimu wa matumbawe

Matumbawe ni muhimu kwa kuwa yanahifadhi aina nyingi za viumbe hai na kwamba

ni chanzo muhimu cha chakula kwa mamilioni ya watu kupitia uvuvi wa samaki,

makombe, na viumbe wengine. Pia huzuia mawimbi makubwa hivyo huyalinda

mazingira ya pwani, fukwe na nchi kavu. Ili yaweze kustawi/kukua vizuri

matumbawe yahahitaji mazingira maalum ambayo yamejadiliwa hapa chini.

5.2.1 Joto

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 10

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Kwa ukuaji mzuri, matumbawe huhitaji nyuzi joto kati ya 25-37 0 C kwa sababu hii

matumbawe hupatikana ndani ya ukanda ulioko 25 0 kaskazini na 25 0 kusini ya Ikweta

na kwenye kina kifupi cha maji.

5.2.2 Mwanga wa kutosha

• Mwanga husaidia mimea inayoishi kwenye matumbawe kufanya shughuli zake

vizuri ambazo huongeza kasi ya ukuaji wa matumbawe na kuwepo kwa

virutubisho vya kutosha

• Matumbawe hupungua kwa kasi kadiri kina cha maji kinavyoongezeka hivyo

kwenye kina cha meta 30 – 40 si rahisi kuyakuta

5.2.3 Kutuama kwa mashapo / takataka

• Kiasi kikubwa cha taka na matamahuruku kwenye maji hupunguza kiasi cha

mwanga kinachoyafikia matumbawe na kuathiri uzalishaji wa chakula kwa

kutumia mimea, hivyo kasi ya ukuaji huathirika pia

• Utupaji wa taka huweza kutokea kwenye matumbawe na hili likitokea

husababisha matumbawe kufa

• Matumbawe hutumia nishati kubwa kuondoa uchafu

5.2.4 Chumvi Chumvi

• Mabadiliko kidogo tu ya chumvi ndani ya maji huweza kuathiri matumbawe.

Hunawiri vizuri kwenye kiasi cha juu cha chumvi chumvi ndani ya maji, ukuaji

wake hupungua au kusitishwa kabisa kiwango cha chumvi kinapopungua na

hayaoti kabisa kwenye maji baridi kama vile kwenye maingilio ya mito Amazoni

na Orinoko

5.3 Uvunaji / uharibifu wa matumbawe

• Matumbawe huharibiwa na aina yoyote mbaya ya uvuvi

• Matumbawe huvunwa kwa ajili ya kutumika katika ujenzi, kama vivutio, na

utengenezaji wa chokaa

• Ukusanyaji wa makombe toka kwenye matumbawe

• Ukataji wa mikoko – kwa ajili ya nishati, ujenzi na kwa kilimo na ufugaji

• Uchafuzi kutokana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na binadamu kama vile

kilimo, maji taka, viwanda n.k

• Utalii – uzamiaji, uogeleaji na utiaji nanga

5.4 Hifadhi ya matumbawe

Kwa vile matumbawe huishi na viumbe wengine wengi, ni muhimu kuwa waangalifu

wakati wa kufanya hifadhi. Hii yaweza kufanywa kwa:

• Kusitisha uvunaji wa matumbawe kwa ajili ya ujenzi na mapambo

• Kuacha ukusanyaji wa makombe toka kwenye matumbawe

• Kuzuia utiaji nanga kwenye matumbawe

• Matumizi ya aina salama za uvuvi, kwa mfano kutembea juu ya matumbawe, na

uvuvi wa mabomu na sumu havitakiwi

• Ujenzi wa aina yoyote katika fukwe ni lazima uhakikishe kuwa hauathiri viumbe

vya baharini

Uangalizi wa matumbawe duniani kote unazingatiwa na unaelekea kuwa ni wenye

mafanikio makubwa. Kisiwa cha Mafia nchini Tanzania kimefanywa kuwa eneo

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 11

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

tengefu la kibahari la jumla. Hii inamaanisha kuwa wakazi wa sehemu hiyo

wanaruhusiwa kuvua lakini kwa mpango maalum unaoonyesha idadi na ukubwa wa

samaki wanaopaswa kuvuliwa. Watalii wanaruhusiwa kufanya shughuli zao lakini

mahoteli na vituo vyao vimewekewa mipaka maalum.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 12

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

6. Uhusiano wa Mifumo ya Maisha

ya Viumbe Hai Baharini

6.1 Utangulizi

Kuna uhusiano wa kimaisha / mazingira kati ya mikoko, nyasi za baharini na

matumbawe. Hivyo ni muhimu kila mfumo kupewa kipaumbele katika hifadhi. Nyasi

za baharini na mikoko huchuja uchafu / mashapo hivyo kuhakiki usalama wa

matumbawe. Kwa upande wa pili matumbawe hupunguza kasi za mawimbi

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 13

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

maharibifu hivyo kuzuia uharibifu ambao ungeweza kutokea kwenye mikoko na nyasi

za baharini.

6.2 Mtazamo wa jumla

Mpangilio ufuatao unaonyesha jinsi ambavyo kila eneo la bahari linavyofaidisha

jingine.

6.3 Mikoko

• Huchuja matamahuruku na kufyonza virutubisho, hivyo huzipatia nyasi za

baharini na matumbawe maji safi. Mashapo / uchafu vikizidi huua matumbawe

• Huzuia mmomonyoko wa udongo kwenye fukwe

• Hupunguza kiwango cha maji baridi kinachoyafikia matumbawe hivyo kupunguza

mabadiliko ya chumvi chumvi ambayo huathiri matumbawe

• Makuzio ya samaki wadogowadogo

• Hupunguza kasi ya mawimbi hivyo huwezesha lava kuishi

6.4 Nyasi za baharini na Maeneo ya maji kupwa na maji kujaa

• Makulio ya samaki wadogowadogo

• Hupunguza kasi ya mawimbi hiyo lava huweza kuishi

• Huzuia mmomonyoko wa fukwe

• Ni sehemu ambayo uozo mwingi hupatikana hivyo kuwa chanzo kikubwa cha

chakula kwa viumbe vingi vya baharini

• Huchuja / huzuia taka zisiyafikie matumbawe

6.5 Matumbawe

• Huzuia mawimbi makali kuyafikia majani ya baharini, mikoko na eneo

linalokupwa na kujaa maji

• Hutoa sehemu salama na imara kwa viumbe wa aina tofauti kuishi na kuzaliana

• Aina ya viumbe wengi wanaopatikana kwenye matumbawe, huwezesha kuwa na

mfumo mzuri wa mahusiano kibaologia (mahusiano yenye kufaidiana)

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 14

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

7. Mambo Unayopaswa na

Usiyopaswa Kufanya Baharini

7.1 Utangulizi

Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya maliasili za baharini kwa upande mmoja na

haja ya matumizi endelevu kwa upande mwingine, kuna haja ya kuwa na njia salama

za matumizi ya maliasili hizo. Kwa hiyo kila mdau analazimika kufahamu yampasayo

na yasiompasa kufanya anapokuwa kwenye mazingira ya bahari. Taratibu zifuatazo

zinapaswa kuzingatiwa na wadau wote, kwa nia ya kutunza mazingira na usalama

binafsi, izingatiwe kuwa hizi ni sehemu tu ya taratibu zinazopaswa kuzingatiwa.

7.2 Unapaswa

• Kujua hali ya hewa kabla ya kwenda baharini

• Uwe mwangalifu kwenye matumbawe

• Kutia nanga mchangani

• Kuchukua uchafu nyumbani

• Kuacha matumbawe na vitu vingine kama ulivyovikuta

• Kuipenda bahari na maliasili zake na kuzitunza

7.3 Hupaswi

• Kuogelea kwenye tufani, mawimbi makali au upepo mwingi

• Kwenda kuzamia au kuogelea peke yako

• Kuyasumbua au kuyachukua matumbawe au makombe (hai au Mafu)

• Kugusa au kusimama kwenye matumbawe

• Kutia nanga kwenye matumbawe

• Kusababisha uchafuzi wa bahari

• Kuvuna rasilimali yoyote kupita kiasi

• Kutumia madawa ya aina yoyote baharini

• Uvuvi wa kupita kiasi

• Kuchimba mchanga pwani / ufukweni

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 15

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

• Kukata mikoko hovyo na kuchimba chambo kwenye mikoko

7.4 ACHA!

Kufanya shughuli yoyote inayoharibu mazingira ya bahari!

7.5 ANZA!

Kutumia njia salama kuvuna rasilimali za baharini ili kuhifadhi mazingira yake kwa

ajili ya vizazi vijavyo.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 16

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

8. Tishio Linaloyakabili Mazingira

ya Bahari

8.1 Utangulizi

Maeneo ya bahari muhimu na yanayokabiliwa na tishio la uharibifu mkubwa ni

mwamba wa matumbawe, mikoko, nyasi za baharini na maeneo ya maji kupwa na

kujaa. Maeneo haya yanauhusiano wa kibaologia. Maeneo haya si muhimu tu kwa

viumbe waishio baharini lakini pia ni muhimu kwa binadamu na hasa wakazi waishio

pembezoni mwa bahari ambao uchumi na maisha yao hutegemea rasilimali za bahari.

Hivyo kuna ulazima wa kuhifadhi mazingira ya bahari na maliasili zake.

Tishio linalokabili mazingira ya bahari laweza kugawanywa sehemu mbili, tishio

asilia na tishio linalotokana na binadamu.

8.2 Tisho asilia linalohat arisha mazingira ya bahari

1. Kiti cha Pweza chenye miiba (Acanthaster planci)

Aina hii ya samaki ni hatari sana na hupatikana kwa wingi katika bahari ya pasifiki.

Viumbe hivi chakula chao kikuu ni matumbawe, mara nyingi husababisha eneo

kubwa la mwamba wa matumbane kuathirika na hata wakati mwingine kufa.

2. Magonjwa

Ugonjwa kama vile ‘blackland’ huvamia matumbawe na kuyabadilisha rangi yake na

hata kuyaua kabisa.

3. Matumbawe meupe

Husababishwa na kuongezeka kwa jotoridi la maji ambapo mimea inayoishi na

matumbawe hupoteza rangi na hivyo hushindwa kuzalisha chakula, hali hii hupelekea

matumbawe kufa.

4. Tufani na mawimbi yaendayo kasi

Husababisha matumbawe, majani ya baharini, na mizizi ya mikoko (vikua) kufunikwa

na takataka zinazotuama ambazo huathiri ukuaji, taka hizi zinapoongezeka huweza

kusababisha vifo.

8.3 Tishio linalotokana na binadamu

1. Matumizi ya njia mbaya za uvuvi

Uvuvi si lazima uwe mbaya na tishio kwa usalama wa mazingira ya bahari hasa

unapokuwa katika hatua ya kuwa endelevu. Matatizo yanaweza kusababishwa na

uvuvi wa kupita kiasi na kuvua samaki wachanga ambao ni tegemeo la baadaye. Aina

zifuatazo za uvuvi ni tishio kubwa kwa mazingira ya bahari.

- uvuvi wa kokolo / Juya

- uvuvi wa mabomu / milipuko

- uvuvi wa kigumi / neti za kojani

- uvuvi wa sumu

Njia hizi za uvuvi zinapaswa kuepukwa na kupingwa na kila mtu mwenye mapenzi

mema na rasilimali za bahari na vizazi vya baadae.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 17

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

2. Utupaji taka / uchafuzi

Uchafuzi huathiri viumbe vya bahari na mazingira yao. Takataka nyingi ni sumu

kama vile mafuta, uchafu wa majumbani, takataka na mabaki ya kwenye vyombo vya

usafiri.

3. Utiaji nanga

Huharibu matumbawe, mara nyingi ni kutoka kwenye vyombo vya uvuvi na uzamiaji.

Waweza kuzuia uharibifu kwa kuwa na vifaa vya kutilia nanga vinavyoelea au kuwa

waangalifu wakati wa utiaji nanga.

4. Wazamiaji

Wasipokuwa waangalifu huweza kuharibu na hata kuua viumbe na mazingira ya

baharini hasa kwenye mwamba wa matumbawe. Wazamiaji wanapaswa kuelimishwa

juu ya uzamiaji salama.

5. Biashara ya makome, makunguju, mabaragumu na makombe.

Viumbe hawa wakiwa hai au wafu ni mapambo yanayopendwa. Lakini wokotaji wa

vitu hivi waweza kuharibu mfumo wa usawa baharini, ni kwa sababu viumbe hivi

huoza na kutengeneza miamba au mchanga wa ufukweni. Kama makombe mafu na

matumbawe vitaondoshwa utengenezaji wa mchanga utasitika na kama makombe na

matumbawe hai vitaondolewa viumbe wengine wataathirika pia kwa kukosa ama

chakula au makazi.

6. Ukataji mikoko hovyo

Ukataji hovyo mikoko ni hatari sana kwa vile huharibu mandhari ya fukwe zetu,

mazalio na makulio ya samaki. Mikoko pia huzuia mmonyoko wa ardhi na kuzuia

uchafu kutoka nchi kavu kuyafikia matumbawe. Hivyo tunapaswa kuitunza mikoko

na kuitumia kwa uangalifu.

Hivyo ni jukumu la wadau kutumia rasilimali na mazingira ya bahari kwa

uangalifu mkubwa ili kupunguza na hatimaye kuzuia kabisa tishio

linaloyakabiri mazingira ya bahari.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 18

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

SEHEMU YA PILI

Shughuli zinazofanyika wakati wa

ufundishaji

1. Masanamu ya kuchorwa

2. Kusanifu matangazo (mabango)

3. Chemsha bongo ya elimu ya mazingira

4. Mchezo wa taa za barabarani

5. Kusema hapana kwa takataka

6. Mfumo wa ushirikiano wa chakula – 1

7. Mfumo / mtandao wa chakula (Uhusiano wa

viumbe) 2

8. Matembezi ya nyika hai

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 19

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

1. Masanamu ya kuchorwa

1.1 Utangulizi

Masanamu ya kuchorwa huwa ni mapambo yenye mvuto mkubwa kwa jamii, kama

yakibuniwa vizuri huweza kuwa njia bora ya kufikisha ujumbe kwa jamii husika.

Uhusiano wa maumbo na mazingira halisi ni muhimu sana ili kuleta mvuto na hisia

juu ya ujumbe uliopo hivyo ni muhimu kuyazingatia haya wakati wa usanifu.

1.2 Nini cha kufanya

Sehemu ya kuweka masanamu inapaswa kuchunguzwa kabla ya ubunifu wa mchoro.

Baada ya hilo sanamu inaweza kubuniwa na kuchorwa kwenye kuta za pembeni za

skuli kwenye maeneo yanayoonekana kirahisi au katika kuta za zege vijijini. Kitu cha

kuzingatia ni rangi zinunuliwe mapema na ziwe zinazoelekeana na aina ya mchoro,

eneo unapochorwa na ujumbe uliokusudiwa.

1.3 Vifaa

Rangi za kawaida zinazotumika majumbani pamoja na vipakio, karatasi na kalamu

1.4 Usanifu

Chora mchoro kwenye karatasi ndogo na upake rangi, hii itawezesha tatizo lolote la

mchoro kujulikana na kufuatiliwa mapema. Pia mchoro huo waweza kutumika kama

mfano siku ya uchoraji mkubwa.

1.5 Mawazo ya kisanifu

Mchoro unaweza kuonyesha muonekano wa ndani ya maji, jinsi ya kutunza mazingira

yanayoizuinguka jamii husika, Jambo lolote la kiulimwengu kama vile ukataji miti

hovyo, viumbe vilivyo hatarini kupotea n.k. Mchoro unapaswa uwe na ujumbe wa

kuihimiza jamii husika kuwa na mwelekeo wa kutunza mazingira.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 20

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

2. Kusanifu matangazo (mabango)

2.1 Lengo

Kuwafanya washiriki kufikiria juu ya hali ya mazingira na jinsi wao binafsi

wanavyoweza kuathirika. Kujenga mawazo juu ya mambo / mafunzo ya kila siku,

kutoa mawazo yao katika usanifu kupitia vitabu, usanifu binafsi husaidia kujenga

mawazo juu ya tangazo lililobuniwa. Kama unataka kazi hii iwe ni yenye mafanikio,

hakikisha kuwa kuna mada rasmi itakayotoa ujumbe unaoonekana kwenye tangazo na

washiriki wapewe nafasi ya kuchangia mawazo. Mfano ni matatizo gani yanayokabili

mazingira ya bahari ama ni jinsi gani ukanda wa pwani unaweza kuhifadhiwa /

kutunzwa. Toa nafasi ya majadiliano kwa kila mmoja kushiriki.

2.2 Vifaa

Karatasi

Penseli / kalamu za rangi / rangi

Maelezo ya kufuatisha

2.3 Jinsi ya Kufanya

Ruhusu washiriki kuunda mawazo ya kibunifu kwa kupitia vitabu. Mada

ikishapatikana ubunifu waweza kuanza na baada ya kumaliza jadili na wabunifu

kilichomo ndani ya mabango yao na wanategemea watu watapata tafsiri gani.

2.4 Mawazo muhimu

Ili kufanya mchezo wenye faida weka mada maalum ambayo washiriki watapaswa

kuijadili. Kwa mfano kuna msukumo gani kwenye mazingira na namna gani fukwe

zinaweza kutunzwa. Ruhusu mjadala ili kupata mlolongo wa maelezo. Kisha ruhusu

washiriki kubuni mabango yenye ujumbe unaoendana na yaliyojadiliwa.

2.5 Mawazo ya ziada

Unaweza kuonyesha mchezo wa “coat of arms”. Wagawanye washirki katika

makundi matatu, moja liwe picha zinazoonyesha mazingira yaliyoathirika, jingine

picha zinazoonyesha vitu vilivyo sababisha uharibifu na la mwisho picha

zinazoonyesha jinsi ya kubadilisha uharibifu wa mazingira uliotokea.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 21

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

3. Chemsha bongo ya elimu ya

mazingira

3.1 Utangulizi

Ni vizuri washiriki wakapewa changamoto juu ya uelewa wao. Kuwapa elimu / ujuzi

kutahakikisha kuwa mawazo yanajengeka na kuimarika. Chemsha bongo ya

mazingira yaweza kuhusisha mambo mapya au ya zamani. Kuwapa nafasi washiriki

kwa uhuru zaidi bila hofu itarahisisha kujifunza na kukumbuka. Chemsha bongo

yaweza kufanyika mara nyingi iwezekanavyo ili kukuza ufahamu juu ya mazingira.

3.2 Lengo

Kushirikisha timu zote kwenye mchezo hivyo kwanza unaanzia kwenye kona ya

kwanza ya mbao kisha unaendelea mpaka mwisho. Kila sehemu ya mchezo ni lazima

swali lijibiwe sawia ili kuendelea mbele na ili ujumbe uweze kuzingatiwa.

3.3 Vifaa

• daisi ya koro koro

• ubao mpana

• maswali

• kalamu / rangi

3.4 Jinsi ya kufanya

Utengenezaji wa mchezo

• Tengeneza ubao mdogo wenye vyumba (Mraba) toka mwanzo na hata mwisho

(kama drafti)

• Andika kwenye vyumba hivyo umepotea au rudi nyuma hatua moja, hii

itauchangamsha mchezo

• Wape vikadi kila timu zenye maumbo ya samaki au wanyama

• Andaa maswali yanayoendana na umri wa washiriki

Jinsi ya kucheza

• Gawanya timu katika makundi mawili kisha weka hesabu zote mwanzo

• Chagua timu inayoanza na uliza swali, jibu sahihi litapelekea timu hiyo kurusha

daisi na kusonga mbele kwa nafasi zilizoamuliwa

• Kuelekea kwenye mraba timu inapaswa kusubiri timu nyingine kujibu swali

kwanza

• Kama itatoa jibu sahihi itarusha pia daisi na kusonga mbele nafasi sawia

• Kwa hiyo mchezo utaenda timu ya kwanza na kuendelea mbele na nyuma

• Swali lisipopata jibu sahihi timu hairushi daisi na haisongi mbele, lazima wasubiri

mzunguko wa pili

3.5 Mawazo muhimu

Hakikisha kuwa unazingatia amri za Umekosea na urudi nyuma hatua moja

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 22

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

3.6 Mawazo ya ziada

Maswali yatoke kwenye mada tofauti kama vile, tishio, hatari, rasilimali, na wadau

wa mazingira ya bahari. Vikadi vya maswali na miraba vipake rangi kiasikwamba

mada husika, swali na mraba wake vifanane. Kwa mfano kama kadi ya swali la tishio

linalokabili mazingira ya bahari ina rangi nyekundu, hili ndilo swali inabidi lijibiwe

kama daisi itatua kwenye mraba wa rangi hiyo katika ubao.

3.7 Maswali ya chemsha bongo

S Taja aina moja ya uvuvi mbaya

J Mabomu, Sumu, Kokolo

S

J

S

J

S

J

S

J

S

J

S

J

S

J

S

J

S

J

Taja njia za uvuvi salama

Madema, Ndoana

Kwa nini watu wakitaka kutupa nanga lazima kuwa waangalifu

Nanga inaweza kuharibu matumbawe

Kipi chaweza kuoza haraka – Plastiki au bati

Bati, Plastiki, huchukua miaka mingi sana kuoza na ikichomwa moto

huongeza. Madawa yenye sumu hewani

Kwanini hairuhusiwi kuokota kome ufukweni au kwenye matumbawe

Zinapooza hutengeneza mchanga ambao ni muhimu katika kuweka hali nzuri

ya fukwe, pia kome ni nyumba za baadhi ya viumbe kama vile kaa na pweza

Kwanini hushauriwa kuweka bidhaa zote kwenye mfuko mmoja wa

plastiki, na Kuutumia tena mfuko huo huo

Kupunguza idadi ya mifuko ya plastiki, inamaana kupunguza uchafu kwenye

makazi. Kutumia tena ule wa mwanzo itamaanisha kupunguza zaidi hivyo

mazinira safi

Kama una takataka na huna kwa kuzitupa, je utazitupa baharini

Utatupa chini Au Utaweka mfukoni

Utaziweka mfukoni hadi ukute shimo la taka

Taja vitu vitano visivyotakiwa kuachwa kwenye ufukwe

Plastiki, Vioo, Nyuma na taka kwa ujumla

Mikoko inaisadiaje matumbawe

Kwa kuzuia uchafu unaotoka nchi kavu usiyafikie matumbawe

Kwa nini ni muhimu kwa wanabiologia ya bahari na wataalamu wa uvuvi

Kuzungumza na maofisa wa uvuvi kujua aina na kiasi cha samaki

kinachovuliwa

Kuhakikisha kuwa aina fulani ya samaki haipotei kwa kuvuliwa sana, pia

kujua kiasi Kilichopo na kilichovuliwa kutasaidia kumonita wavuvi

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 23

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

S

J

S

J

S

J

S

J

S

J

S

J

Kwanini hupaswi kununua kombe dukani

Kombe wanaopatikana dukani ni wale waliochukuliwa toka kwenye

Matumbawe wana uhusiano wa kibaolojia na matumbawe na viumb wengine.

Hivyo kupungua kwa kombe kwaweza kuathiri ukuaji wa matumbawe

Taja umuhimu wa majani ya baharini

Huzuia mmomonyoko wa udongo hivyo huyalinda matumbawe, pia

huwaficha samaki wadogowadogo wasiliwe na wakubwa

Weka mpangilio huu wa chakula kwenye mnyororo kiti cha pweza

chenye miiba, Binadamu ,baragumu , pweza na matumbawe

Matumbawe – kiti chwa pweza chenye miiba- baragumu – pweza –binadamu

Kwanini Elimu ya mazingira ni muhimu sana

Elimu ya mazingira hutueleza jinsi tunavyoweza kuyatunza na kuyahifadhi

mazingira yetu hivyo kurefusha maisha pia hufundisha madhara

yatakayotokea tusipotunza mazingira

Je mtu mmoja anaweza kuleta mabadiliko kwenye mazingira

Ndiyo

Taja njia tatu zinazoharibu matumbawe

Utalii

Ukusanyaji Kome

Uzamiaji

Utupaji nanga

Uvuvi- nanga, mabomu, kigumi, sumu na uvuvi wa kutumia neti zenye

matundu madogo sana (kojani nets)

Sababu asilia – tufani na mawimbi makali

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 24

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

4. Mchezo wa taa za barabarani

4.1 Lengo

Kupima kumbukumbu za washiriki juu ya mambo waliojifunza siku za nyuma na siku

ya mazingira. Pia kupima ufahamu wa mshiriki juu ya mazingira na uwezo wa

kufikiria.

4.2 Vifaa

• Mifuniko mitatu ya plastiki ya duara (bluu, kijani, zambarau)

• Karatasi na kalamu

• Karatasi ngumu

• Rangi (Njano, Kijani na Nyekundu)

4.3 Jinsi ya kuandaa michezo

• Tengeneza viboksi vidogo vitatu kwa kila kundi kwa kila kundi kimoja cha kijani,

kimoja chekundu, na cha njano

• Kijani – Salama / endelea

• Nyekundu – hatari / zuia / acha

• Njano – tahadhali / kuwa mwangalifu / tafakari

• Kila kikundi huwa na viboksi vitatu vya aina zote

• Tengeneza uwanja wa michezo ambao huwa na umbo la mraba, katikati huwekwa

mifuniko mitatu ya duara yenye rangi tofauti

• Andaa karatasi yenye maelezo ambayo yanaendana na rangi za viboksi (hatari,

Salama na tahadhari)

• Washiriki waweza kuwa kwenye makundi manne au zaidi

4.4 Jinsi ya kucheza

• Kila kundi hukaa pembe yake umbali sawia toka katikati

• Maelezo husomwa kisha mwamuzi hutoa sekunde kadhaa kwa makundi kuamua

kama ni hatari, tahadhari au salama

• Kisha kwa haraka humpa mshiriki mmojawapo kisanduku husika, mwamuzi

huhesabu moja, mbili, tatu – goo! kwa haraka mshiriki toka kila kundi atakimbia

kuweka kisanduku katikati. Atakayeweka kwenye mfuniko wa bluu kisanduku

sahihi kundi lake litapata alama tatu, kwenye kijani alama mbili na kwenye

zambarau alama moja wa nne atapata sifuri kwa kuchelewa. Alama hutolewa kwa

jibu sahihi tuu

• Kama kuna mgongano wa majibu mwamuzi ataruhusu mjadala kidogo na kutoa

jibu sahihi

• Aina ya maelelezo itategemea rika ya washiriki

• Badili nafasi ya mifuniko ktk kila baada ya swali moja

4.5 Mawazo ya Ziada

Endelea na sentensi zingine na fikiria ambazo zinaendana na rika na kiwango na

uelewa wa washiriki na topiki inayofundishwa, waweza pia kutoa zawadi kwa

washindi, zaweza kuwa vifaa vya shule na vitabu vya mazingira.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 25

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Team A

Team B

Rotate lids regularly

Judge

3 points 2 points

Reader

1 point

Team D

Referee

Team C

4.6 Mfano wa maelezo na majibu yake

1. Kukata mikoko ovyo – Nyekundu

2. Shughuli za uvuvi – Njano

3. Utupaji taka – Njano

4. Kukata miti ovyo – Nyekundu

5. Kutumia mifuko ya plastiki ni kuzuri – Myekundu

6. Kutia Nanga – Njano

7. Uzoaji wa mchanga ufukweni – Nyekundu

8. Umwagaji wa mafuta baharini – Nyekundu

9. Utafiti wa kisayansi – Njano

10. Kufanya kazi na Frontier – Kijani

11. Kuchoma mkaa – Njano

12. Kupandikiza mikoko – Kijani

13. Ujenzi wa vituo vya Utalii – Njano

14. Kuokota kome ufukweni – Nyekundu

15. Uchomaji matumbawe kutengeneza chokaa – Nyekundu

16. Uvuvi wa mabomu – Nyekundu

17. Mbuyu ni aina mojawapo ya mikoko – Nyekundu

18. Majani baharini si muhimu – Nyekundu

19. Tanzania na Uingereza ni marafiki – Kijani

20. Chips mayai ni chakula kizuri – Yeyote

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 26

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

5. Kusema hapana kwa takataka

5.1 Utangulizi

Ingawa kumekuwa na mambo mengi yanayoathiri mazingira lakini ni vigumu kujua

ni lipi kati ya hayo litakuathiri wewe binafsi. Pia katika sehemu nyingi duniani watu

hawana nguvu ya kutatua matatizo hayo kutokana na ukosefu wa fedha au kipato

kidogo. Lakini pamoja na hilo watu ulimwenguni kote hushiriki katika matumizi ya

bidhaa zinazosababisha uchafu kwa kiwango tofauti. Kwa mfano nchi nyingi hutumia

mifuko ya plastiki kubebea mahitaji na hata kuhifadhi bidhaa. Baada ya kutumia

mifuko hairudiwi tena bali hutupwa mbali kama uchafu. Plastiki, makopo, vioo na

vyuma vyaweza kuwa hatari kwa watu na kuweza kuua wanyama kwa

kuwasababishia vidonda au kwa kuvimeza.

Katika nchi nyingi uzoaji wa taka ni kidogo kutokana na njia za usafiri kuwa duni.

Kutokana na wakazi wengi huzichoma takataka na kuzifukia chini.

Hii yaweza kuwa nzuri kwa vile inasaidia kupunguza taka lakini yaweza kuongeza

tatizo watu wasipokuwa makini.

Kama watu watatumia mifuko ya plastiki ile ile kwa kuikataa mipya inapokuwa si

muhimu kuwa nayo, idadi ya plastiki na uchafu kwa ujumla waweza kupungua

kwenye makazi. Na juu ya hili kama wanunuzi wa bidhaa watakuwa waangalifu na

kuwa makini na wenye kiasi kwenye ununuzi wa bidhaa ingeweza kupunguza kasi ya

uongezekaji wa taka kwenye makazi ya watu na wanyama. Kuwafahamisha watu juu

ya nguvu waliyonayo juu ya taka kwa kuwahusisha katika mazoezi rahisi inaweza

kusaidia watu kufikiria juu ya uwajibikaji.

5.2 Lengo

Andaa / buni eneo la mikoko lenye taka, Washiriki wanapaswa kutembea kutoka kiti

kimoja hadi kingine bila ya kugusa ardhi kwa msaada wa daraja la mbao,

wakikusanya taka na kuziweka kwenye pipa. Mchezo huu ni kama kituko lakini watu

wanaweza kuulizwa kwamba wana maoni / hisia gani juu ya taka, kuufanya mchezo

uwe mzuri zaidi. Pia hutakiwa kuelezea uchafu unaharibu mazingira yao kwa kiasi

gani.

Maoni yaweza kutolewa mwishoni mwa mchezo ni kwa jinsi gani mazingira mazuri

yanaweza kufanywa na jinsi gani ya kuwa wawajibikaji.

5.3 Vifaa

• Viti 6-7

• Mbao mbili

• Pipa la taka

• Karatasi

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 27

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

5.4 Jinsi ya kufanya

• Kabla ya hapo tengeneza bango linaloonyesha madhara ya taka zinapokuwepo na

jingine linaloonyesha faida za taka kutokuwepo ili iwasaidie washiriki kuelewa.

Mfano wa madhara ya taka, kuchomwa plastiki huongeza kemikali zenye sumu

hewani, taka ndogo zikimezwa na wanyama huwa hatari na pia taka hazipendezi

kuziona. Faida za kutokuwa na taka ni pamoja na makazi safi ya kuishi, hali safi

ya hewa na maisha salama

• Tafuta eneo zuri la kuweka msitu wa kubuni wa mikoko

• Panga viti vizuri ili kuruhusu washiriki kuweka mbao juu yake na kutembea

upande mmoja hadi mwingine

• Sambaza takataka kwa washiriki kuokota

• Toa muda maalum kwa muokota taka kumaliza eneo lote la mikoko

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 28

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

6. Mfumo wa ushirikiano wa

chakula – 1

6.1 Utangulizi

Viumbe hai wote wanauhusiano wa mzunguko wa nishati. Uhusiano huo hujulikana

kama mfumo / mtandao wa ushirikiano wa chakula. Mimea iko chini / ngazi ya

kwanza ya mfumo huo kama wazalishaji wa msingi. Kwa upande mwingine wanyama

walao mimea wako katikati na juu yao ni wale wanyama walao nyama. Kutokana na

kwamba wala nyama hula wanyama wenzao ambao wengi wao hula mimea, kuna

usawa kati yao ambao huweza kuathiriwa na binadamu. Kwa mfano, idadi ya

baragumu huongezeka haraka kukiwa na hali nzuri ya kimazingira, hivyo samaki

wawalao pia huongezeka, lakini samaki wakiongezeka kupita kiasi hupelekea idadi ya

baragumu kupungua na hivyo samaki wawalao pia huathirika.

Wakazi wa pwani hutegemea samaki kwa mlo kamili na kujipatia kipato. Uvuvi

mdogo mdogo hauna athari kwa mtandao wa chakula. Lakini uvuvi ukiongezeka sana

kupita kiasi cha samaki basi samaki hao wataanza kupungua. Kupungua huko kwa

samaki kunaweza kuathiri viumbe wengine.

6.2 Lengo

• Kujenga uelewa juu ya uhusiano kati ya Viumbe

• Washiriki kuelewa madhara ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja

yanayoweza kusababishwa na binadamu kwenye mazingira baharini

6.3 Jinsi ya kufanya

• Buni mifumo / Mtandao wowote wa chakula (tumia mfumo huo hapo chini)

• Uchore mfumo huo tayari kwa majadiliano

• Tayarisha vipande vya karatasi zenye picha ya vitu vyote / viumbe vilivyoko

kwenye mfumo huo

• Mpe kila mshiriki picha / Mchoro kisha jadili mtandao / mfumo huo wa chakula

na mahusiano kila kiumbe na chenzie

• Washiriki wawe katika duara wakielekeaa upande mmoja na nyuso zao katikati

• Athari zitokanazo na binadanu ziwe nje ya duara

• Washiriki wajivute ndani ya duara na wakaribiane kiasi cha kutegemeana. Hili

huitaji mazoezi

• Mshiriki anayehusisha madhara yatokanayo na binadamu atamvuta mmoja wao

kwa nguvu na kumwondoa kwenye duara, hilo litasababisha duara zima

kuharibika.Hii huonyesha kitu halisi kinachoweza kutokea kwenye mtandao wa

chakula

• Hii ni njia rahisi kwa mshiriki kuona jinsi gani mfumo mzima na mtandao wa

chakula huweza kubomoka kabisa ukiathiriwa na kitu chochote toka nje

• Unaweza kurudiwa mara nyingi ili kutilia mkazo ujumbe uliopo. Kuhitimisha

washiriki wanaweza kujadili kwa mjumuisho juu ya maada husika na

kuzungumzia shughuli zozote wazifanyazo kila siku zenye athari kwenye mfumo

mzima wa mtandao wa chakula

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 29

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 30

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

7. Mfumo/mtandao wa chakula

(Uhusiano wa viumbe) 2

7.1 Lengo

• Kukuza ufahamu juu ya mahusiano ya viumbe hai na mazingira yao

• Kuonyesha / kujifunza athari zitokanazo na binadamu kwenye mazingira haya

7.2 Vifaa

• Kalamu za kawaida na za rangi

• Karatasi aina ya A4

• vijiboksi vidogo (4 kwa kila kiumbe)

• Karatasi aina ya A1 moja au mbili

7.3 Jinsi ya kuandaa

• Buni mfumo / mtandao wa chakula na uchole kwenye karatasi kubwa aina ya A1

bila ya kuonyesha majina ya viumbe husika, ambayo yanaweza kuwakilishwa na

namba

• Chora picha zinazoelekeana na mchoro huo hapo juu kwenye karatasi au viboksi

• Kama washiriki ni wengi wagawe kwenye makundi ya watu 4 au 5

7.4 Jinsi ya kufanya

• Tundika mchoro mkubwa kwenye ubao unakoweza kuonekana na kila mmoja

• Wagawie wanafunzi picha

• Kwa kujadiliana wape nafasi wanafunzi kuamua picha ipi inaelekeana na namba

ipi kwenye mchoro

• Baada ya kukamilisha upangaji wa picha zote kwenye mchoro jadiliana na

wanafunzi madhara ya kuiharibu sehemu mojawapo katika mchoro huo

• Husianisha mjadala na mazingira halisi na jadili shughuli zifanywazo na

binadamu zinazoweza kuathiri mfumo huo

7.5 Kwenye mchoro wa mfano ulioonyeshwa hapo chini namba zinawakilisha

1. Papa – mla nyama

2. Mcheche – mla nyama

3. Ndege wa baharini

4. Pweza – mla nyama

5. Samaki – Kipepeo

6. Samaki – Tembo

7. Baragumu

8. Kiti cha pweza chenye miiba

9. Kamba

10. Matumbawe

11. Ufuma / ulumba

12. Mwani

13. Majani

14. Majani ya baharini

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 31

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

7.6 Mawazo ya ziada

Tumia viboksi kuonyesha mabadiliko ya usawa wa mfumo mzima. Weka viboksi 2

katika kila hatua kwenye mchoro. Kisha waweza punguza kimoja sehemu mojawapo

hii itapelekea kupungua kwa idadi ya viumbe husika na kuongezeka kwa viumbe

walioko chini zaidi ya mfumo huo hivyo yaweza kuathiri mfumo mzima.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 32

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

1

2 3

4

5 6

7 8

9

10 11

12

13

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 33

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

8. Matembezi ya nyika hai

8.1 Utangulizi

Unapofundisha ni muhimu kutumia rasilimali zote zilizopo na zinazofikika.

Kutembea na kuangulia mazingira yaliyopo huleta hamasa zaidi kwa ulimwengu huu

wa kushangaza. Kujifunza toka kwenye mazingira halisi zaidi kuliko kwenye vitabu

humwezesha mwanafunzi yeyote kuielewa hali ilivyo na kukubaliana na mazingira

hayo kwa moyo wa dhati.

Kwa mfano mikoko huweza kuonekana kwa haraka haraka kama mimea isiyo na

faida hivyo hutumika tu hovyo hovyo bila kujali, lakini ukichunguza kwa uangalifu

zaidi utagundua kuna idadi kubwa ya viumbe kama vile ndege, kaa, kamba, kome na

vinginevyoo vilivyojizoesha kuishi kwenye mazingira haya magumu ya mikoko.

Hakikisha wanafunzi wanapata muda na nafasi ya kutosha kujifunza kwenye

mazingira halisi na pia ruhusu maswali.

8.2 Lengo

• Kuelewa jinsi viumbe vinavyoishi katika mazingira yake na binadamu

anavyoweza kuathiri mfumo huo. Kujifunza darasani mara nyingi humaanisha

kuelewa tu bila kukubaliana na hali halisi kwenye mazingira husika

• Kwa kuzungukwa na mazingira asilia yanayotumika kujifunza hurahisisha

ufundishaji na kuwawezesha washiriki kupata ujumbe kirahisi. Kuweza kuona

jinsi mshabihiano laini wa viumbe na mazingira yao ulivyo yaweza kukazia

uelewa unaoendana na uwajibikaji kwa jinsi ambavyo binadamu anaathiri viumbe

hivyo, hivyo kubadili mwelekeo

8.3 Jinsi ya kufanya

• Orodhesha mifumo yote ya kimazingira inavyoweza kutembelewa ambayo

binadamu anaathiri viumbe hai wake, kama vile mikoko, majani ya baharini na

maeneo ya maji kupwa na kujaa

• Chunguza ni lipi linaendena na mada ya siku husika

• Panga ni jambo gani ni muhimu liangaliwe wakati wa kutembelea mahali hapo,

kwa mfano unataka kuona athari ya binadamu kwenye msitu wa karibu au ndege

waishio kwenye mikoko

• Hakikisha kuna muda wa kujiandaa kwa washiriki juu ya maada husika, hii

itarahisisha matembezi hayo

• Chukua kibeseni kipana cha kuangalizia wanyama na mimea midogo midogo na

vifaa vingine muhimu, kutegemea na lililokusudiwa kuelekezwa

Tafadhali hakikisha hakuna kiumbe chochote kitakachoumizwa na mara baada ya

kujifunza kirudishwe kilipokuwa

8.4 Mahitaji muhimu

• Vifaa vya utafiti na maendeleo juu ya mfumo mzima wa mazingira na viumbe hai

unaotegemewa

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 34

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

8.5 Mfano

Kutembelea msitu wa mikoko

Mambo muhimu unayoweza kujifunza / kufundisha

• Aina ya Mikoko iliyopo na mpangilio wake

• Maeneo inapostawi mikoko baharini

• Aina ya udongo ndani ya mikoko

• Idadi ya mikoko kwenye eneo la mraba

• Urefu na umri wa mikoko

• Viumbe wengine waishio ndani ya mikoko

• Aina mbalimbali za mizizi na inavyofanya kazi kuchuja uchafu na matamahuruku

• Athari za binadamu kwenye mikoko

• Kama imeathirika sana, waweza pia kufundisha upandikizaji wake na namna ya

kufanya zoezi hilo kwa vitendo

N.B

kumbuka elimu kwa vitendo hutolewa ili kumwezesha mwanafunzi kuzingatia

zaidi alivyojifunza, hivyo shirikisha zaidi wanafuzi katika vitendo. Kama

mwalimu jiepushe kuhodhi mambo yote darasani.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 35

Elimu ya mazingira ya bahari ya kitropiki: Muongozo wa mwalimu

Marejeo

Collins Concise English Dictionary 2000 (1982) Harpers Collins Publishers, Great

Britain.

Eade, D and Williams, S. (1995) The Oxfam Handbook of Development and Relief

Volume 1. Oxfam (UK and Ireland)

Nybakken, J.W. (2001) Marine Biology: An ecological approach. 5 th Edition. Moss

Landing. Addison Wesley Longman.

Semesi, A.K., and Howell, K. (1989) The Mangroves of the East African Region.

UNEP, Nairobi. 45pp.

Semesi, A.K., Mgaya, Y.D., Muruke, M.H.S., Francis, J., Mtolera, M. and Msuni, G.

(1998) Coastal resources utilization and conservation issues in Bagamoyo, Tanzania.

Ambio Vol 27 No. 8:635-644. Royal Swedish Academy of Sciences. P635-644.

10pp.

Frontier-Tanzania Environmental Research Report 100 36

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!