TAARIFA YA TATHMINI YA HALI YA VIWANDA - Tanzania Dairy ...
TAARIFA YA TATHMINI YA HALI YA VIWANDA - Tanzania Dairy ...
TAARIFA YA TATHMINI YA HALI YA VIWANDA - Tanzania Dairy ...
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
TAARIFA YA TATHMINI YA HALI YA VIWANDA

VYA KUSINDIKA MAZIWA TANZANIA OKTOBA 2006

N.R. Mbwambo, C.M.D. Mutagwaba, M. Tsoxo na A.E. Temba

1. UTANGULIZI

Jukumu la kufanya mapitio lilitolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya

Mifugo. Madhumuni ya mapitio yalikuwa ni kutathmini hali ya viwanda vya

kusindika maziwa ili kuweza kuandaa mikakati ya kuendeleza sekta. Jukumu

lilitakiwa kuhusisha viwanda vyote yaani vinavyofanya kazi kwa sasa na ambavyo

havifanyi kazi. Taarifa ya mapitio ilitakiwa kuainisha matatizo yanayovikabili

viwanda na mapendekezo ya hali ya baadaye.

2. NJIA ZA KUKUSANYA TAKWIMU

(i) Utambuzi wa viwanda:

Kwa sasa hakuna orodha maalum na ya kuaminika inayoorodhesha

viwanda vyote vya maziwa hapa nchini kwa hiyo njia kadhaa zilitumika

nazo ni:

(a) “Proceedings of the 4 th National Dairy Development Conference”,

hususan mada ya, “The contribution of Dairy Industry to the

National Economy, Poverty Alleviation and Household Food

Security in Tanzania” ya Kurwijila, Ryoba na Kyomo, 2002.

(b) Orodha ya Wanachama wa Chama cha Wasindikaji Maziwa

Tanzania (TAMPA) na

(c) “Proceedings of the 6 th National Dairy Development Conference”

hususan mada ya “Value chain analysis and Socio-economic

Assessment of the Dairy Industry in Tanzania iliyowasilishwa kwa

pamoja na SCANAGRI na Business Care Services 2006.

Vyanzo hivi vinaonekana kwa pamoja kutoa orodha ya kuaminika zaidi ya

viwanda vya kusindika maziwa nchini kwa kuanzia.

3. UKUSANYAJI WA TAARIFA ZA AWALI.

Iliandaliwa hojaji fupi na rahisi na kutumwa kwa barua-pepe kwenda kwa

viwanda vilivyoorodheshwa kutumia njia iliyotajwa hapo juu (Kiambatanisho I).

Aidha wenye viwanda/mameneja wa viwanda walihojiwa kwa simu. Njia ya simu

ilisaidia sana kwa sababu viwanda vingi vilichukua muda mrefu kujibu barua

pepe. Kwa viwanda vilivyopo Dar es Salaam mipango ya kuvitembelea

iliandaliwa ambapo mahojiano ya kina ya ana kwa ana yalifanyika.

4. MATOKEO YA AWALI

1
Taarifa ya uwezo wa viwanda na hali halisi ilivyo sasa hivi inapatikana katika

jedwali na.1. Inayonyesha kuwa hadi sasa hivi kuna viwanda 35 vyenye uwezo

wa kusindika zaidi ya lita 1000 kwa siku kwa kila kimoja. Kati ya hivyo ni

viwanda 28 tu ambavyo vinazalisha hadi sasa na vingine 7 ama vimefungwa au

kusimamisha uzalishaji. Kuna baadhi ya viwanda vinatumia hadi zaidi ya 80% ya

uwezo wake na vingine chini ya 16%. Kwa vile kuna viwanda visivyozalisha

kabisa, wastani wa matumizi ya uwezo wa kusindika ni 12% tu.

Uwezo wa jumla wa viwanda vyote ni kusindika, lita 428,500 kwa siku lakini hali

halisi ni kusindika lita 52,330 kwa siku. Hali hii inaonyesha kuwa juhudi kubwa

zinahitajika ili kuwezesha sekta ya viwanda vya maziwa kuwa na uwezo wa

ushindani na kutoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa taifa.

5. MATATIZO YANAYOATHIRI USINDIKAJI WA MAZIWA

Matatizo yanayovikabili viwanda vya maziwa ni mengi na yanahitaji uchunguzi wa

kina katika kila kiwanda ili kutoa ushauri kwa kila kiwanda husika, lakini matatizo

yaliyotajwa na viwanda vyote ni kama yafuatayo:

5.1 Ukosefu wa maziwa ya kutosha.

Ingawa Tanzania inakadiriwa kuzalisha lita 1,400 milioni za maziwa kila mwaka

kiasi cha maziwa yanayopatikana kwa ajili ya kusindika ni kidogo sana. Hali hii

inatokana na maziwa mengi kuzalishwa na wafugaji wa jadi ambayo kiasi

kikubwa kinatumika na wafugaji wenyewe, uzalishaji ni wa msimu na ukusanyaji

ni mgumu. Wafugaji hawa ndio huzalisha 70% ya maziwa yote nchini.

Upungufu wa maziwa ya kusindika ambao huwa zaidi wakati wa kiangazi

unachangiwa na sababu nyingi ambazo ni:

• Gharama kubwa na ugumu wa kukusanya maziwa ya wafugaji

waliosambaa maeneo ya mbali

• Ushindani na wachuuzi wadogo wadogo.

• Faida ndogo kutokana na matumizi kidogo ya uwezo wa viwanda.

• Uzalishaji wa msimu ambapo maziwa mengi hupatikana msimu wa mvua

na kidogo sana wakati wa kiangazi na hivyo kushindwa kutosheleza

2
Jedwali na. 1 Hali halisi ya viwanda vya kusindika Maziwa Mwezi Oktoba, 2006

No. Mkoa Jina la kiwanda Hali ya sasa Uwezo wa

kiwanda

(lts)/siku

Usindikaji

kwa sasa

(lts)/siku

Matumizi

ya uwezo

1 Dar es Salaam Royal Dairy Products Ltd Prod. suspended 90,000 0 0

3 Azam Dairy Operating 3000

4 Tommy Dairy Prod. suspended 15000 0 0

5 Tan Dairies Operating 15000 4000 27

6 Tanga Azania Dairies Ltd (Ex

TDL)

Operating 12,000 6000 50

7 Tanga Fresh Operating 15000 14000 80

8 Morani Operating 5000 1000 30

9 Arusha Ex TDL New Northern

Creamaries

Operating 45000 2500 16

10 International Dairy Products Operating 5000 1200 24

11 Arusha Dairy Company Operating 5000 2000 40

12 Kilimanjaro Nronga Women Operating 5000 2000 40

13 West Kilimamnjaro Operating 1000 300 30

14 Mboreni Women Operating 1000 200 20

15 Marukeni Operating 1000 200 20

16 Ng'uni Women Operating 1000 200 20

17 Kalali Women Operating 1000 280 28

18 Mara/Musoma Ex TDL Musoma Dairy

(Dr. Mazara)

Closed 45000 0

19 Ex TDL Utegi Plant

(Otieno Igogo et.al)

Closed 45000 0

20 Baraki Sisters Operating 3000 2500 80

21 New Mara Milk Operating 8000 4500 33

22 Mwanza Victoria Dairy (Kishimba) Closed 45000 0

23 Lake Side Closed 5000 0

24 Kagera Kagera Milk (KADEFA) Operating 3000 350 12

25 Kyaka Milk Plant Operating 1000 450 45

26 Del Foods Operating 1000 250 25

27 Mini Dairies (several) Operating 1800 1500 83

28 Morogoro SUA Closed 3000 0

29 Shambani Graduates Operating 700 250 36

30 Tabora Ex TDL plant Closed 5000 0

31 Coast Mojata Closed 6000 0

32 Iringa ASAS Dairy Operating 12000 6500 54

33 CEFA Njombe Milk

Factory

Operating 2,000 650 33

34 Mbeya Ex TDL plant Closed/dismantle

d

16000 0

35 Mbeya Maziwa Operating 1000 500 50

JUMLA/

WASTANI

423,500 50,330 27

3
wateja na hivyo wateja wengi kuhamia kwenye maziwa yanayotoka nje ya

nchi.

• Matumizi ya tecnolojia duni kama kutokuwa na uwezo wa kusindika

maziwa kwa teknolojia ya UHT.

5.2. Tatizo la soko.

Matatizo ya soko yanatokana na sababu mbalimbali zikiwemo zifuatazo:

• Sehemu kubwa ya jamii ya kitanzania kutokuwa na utamaduni wa

kutumia maziwa. Matumizi ya maziwa kwa mtanzania kwa mwaka

ni lita 39 tu. Mahitaji ya maziwa yakiongezeka yatavutia usindikaji.

• Ushindani. Maziwa yaliyosindikwa ya Tanzania yanapatikana kwa

msimu na kushindana na yanayotaka nje ya nchi yanayokuwapo

muda wote na yanasindikwa kwa teknolojia ya UHT na hivyo

kutohitaji jokofu kuyahifadhi.

• Uhakika wa kupatikana. Kutokana na uzalishaji wa msimu

upatikanaji wa maziwa ya hapa nchini hauna uhakika hivyo

kupoteza wateja.

• Usafiri – viwanda viko mbali na sehemu yanapopatikana maziwa au

mbali na masoko makubwa na hivyo kuwa na gharama kubwa ya

usafirishaji.

• Kutokana na matatizo ya kutumia teknolojia duni maziwa ya hapa

nchini hayafikii viwango vya ubora wa maziwa yanayoingizwa toka

nchi za nje.

• Kutokana na kutokuwa na vifaa vya kutosha vya usambazaji na

miundombinu duni vijijini ukusanyaji na usambazaji huwa mgumu.

5.3. Kutopatikana na Gharama kubwa ya vifaa vya kukusanyia

maziwa:

Hapa nchini hakuna viwanda vya kutengeneza vifaa vya kukusanyia

maziwa kama makeni, matanki ya kupozea na kadhalika. Vifaa hivi

huagizwa nchi za nje na vikifika bei yake inakuwa kubwa. Hali hii hufanya

wasindikaji kushindwa kukusanya maziwa maeneo ya mbali na kiwanda.

5.4. Ukosefu na gharama kubwa za pembejeo.

Pembejeo zitumikazo kwenye usindikaji kama kimea (starter cultures) na

vifungashio huagizwa toka nchi za nje na hivyo kufanya upatikanaji wake

kuwa mgumu na bei kuwa ghali sana.

4
5.5. Marufuku ya matumizi ya plastiki.

Viwanda vyote vya maziwa hapa nchini hutumia vifungashio vya plastiki

tu. Teknolojia ya kutumia vifungashio vya aina nyingine huhitaji mtaji

mkubwa sana na pia huhitaji kiasi kukubwa cha maziwa. Aidha

vifungashio vya plastiki hupunguza bei ya maziwa kwa mlaji na hivyo

kuongeza matumizi ya maziwa. Ndiyo maana sehemu nyingi duniani sasa

hivi wanahamia kwenye vifungashio vya plastiki hata kwa maziwa ya UHT.

Kwa hiyo kupiga marufuku matumizi ya vifungashio vya plastiki kwenye

maziwa ina maana ya kupiga marufuku usindikaji wa maziwa Tanzania na

kutoa soko la Tanzania kwa maziwa ya nje. Aidha hali hii itafanya

wafugaji wetu kukosa soko la uhakika wa maziwa yao na pia kuongeza

matumizi ya maziwa yasiosindikwa ambayo siyo salama.

5.6. Gharama kubwa za uwekezaji.

Viwanda vya kusindika maziwa huhitaji mashine za gharama kubwa.

Aidha msindikaji huhitaji mtaji mkubwa wa kuendeshea shughuli (working

capital) ili aweze kuwalipa wafugaji hata kabla hajauza maziwa yake. Hii

huhitaji mwekezaji apate mikopo wa riba ndogo na wa muda mrefu

ambayo hapa nchini haipatikani.

5.7. Matumizi ya teknolojia duni.

Mahitaji ya mtaji mkubwa huwalazimisha wasindikaji hapa nchini kutumia

teknolojia duni na hivyo kutoweza kutengeneza baadhi ya bidhaa kama

UHT na kutoa bidhaa hafifu.

5.8. Matatizo ya kimfumo na sera

Katika kundi hili kuna matatizo kama urasimu katika vyombo vya kudhibiti

ubora kama TBS, kuwa na vyombi vingi vya uthibiti, wadau

kutoshirikishwa katika maandalizi ya sera, migogoro kati ya wafugaji na

wasindikaji na vyama vya wadau visivyo imara.

5.9. Matitizo mengineyo:

Haya ni kama kipato kidogo cha wananchi, wawekezaji kuwa na miradi

mingi kwa pamoja, sekta ya maziwa kutokuwa na mvuto kwa wawekezaji,

ukosefu wa vyombo vya mikopo ya muda mrefu na riba ndogo na

kutokuwa na maeneo maalum yenye miundombinu ya kutosha ya kujenga

viwanda.

6. MAPENDEKEZO YA NJIA ZA KUTATUA MATATIZO

6.1. Kuongeza upatikanaji wa maziwa:

Inapendekezwa kuongeza uzalishaji wa kila ng’ombe kwa kuboresha

nasaba za ng’ombe wa maziwa, kuboresha mbinu za ulishaji, kuzuia na

kutibu magonjwa na kuboresha matunzo kwa ujumla. Aidha kuna haja ya

kuwekeza katika mashamba ya kati na makubwa ili kuongeza wingi wa

maziwa kwenye eneo moja. Hii itahitaji serikali kushirikiana na wadau

5
kuongeza upatikanaji wa ng’ombe bora wa maziwa, kufufua miradi ya

kopa ng’ombe lipa ng’ombe, kuhamasisha uwekezaji katika mashamba

makubwa, kuboresha miundombinu na upatikanaji wa mikopo nafuu na ya

muda mrefu. Serikali pia ishirikiane na wadau kuimarisha vikundi vya

wafugaji ili viwe na nguvu za kuweza kumiliki viwanda kama ilivyo kwa

TDCU huko Tanga.

6.2. Kupanua soko la ndani kwa:

• Kuhamasiha jamii kutumia maziwa na hasa kulenga watoto na

vijana kwa mipango ya maziwa mshuleni.

• Kuwajengea wasindikaji uwezo wa kushindana kwa kuwawezesha

kupata vifaa na teknolojia bora ili waweze kuzalisha bidhaa bora.

Aidha serikali itatakiwa kulinda soko la ndani dhidi ya bidhaa

zinazotelekezwa (damping).

• Uhakika wa upatikanaji wa maziwa. Uhakika wa kupatikana

maziwa ya kusindika kwa kipindi chote cha mwaka kutawezesha

viwanda kuwatosheleza wateja muda wote na hivyo hawatahamia

kwenye maziwa kutoka nje.

• Kuboresha miundombinu kama barabara, umeme na upatikanaja

wa vifaa na nyenzo za kukusanyia maziwa hata maeneo ya mbali

6.3. Serikali kwa kushirikiana na wadu iwezeshe upatikanaji wa mashine, vifaa

na mitambo kwa bei nafuu kwa kupunguzwa kodi, na kuagiza kwa wingi.

Hii itawezesha viwanda kupata teknolojia ya kisasa.

6.4. Pembejeo za gharama nafuu. Inapendekezwa serikali iondoe kodi

zote kwenye pembejeo za usindikaji kama kimea (starter cultures)

vifungashio n.k. Aidha kupitia TIC serikali ihamasishe uwekezaji kwenye

viwanda vya mitambo na pembejeo za usindikaji hapa nchini.

6.5. Kuondoa marufuku kwenye vifungushio vya plastiki. Vifungashio

vya plastiki ndiyo pekee vinatumika hapa nchini kufungashia maziwa.

Vifungashio mbadala vinahitaji uwekezaji mkubwa kwenye mitambo mipya

na viwanda havina mtaji huo sasa. Aidha vifungshio mbadala ni ghali na

hivyo vitapandisha bei ya maziwa kwa mlaji. Kama marufuku hii

haitaondolewa usindikaji hapa nchini utakuwa umefungwa.

6.6. Mitaji na gharama za uendeshaji. Kunahitajia kuwa na chombo cha

mikopo ya uwekezaji kwenye sekta ya maziwa (Dairy Development Fund)

kitakachotoa mikopo nafuu na ya muda mrefu (kama nchini India) aidha

uanzishaji wa SACCOS unaweza kusaidia katika mikopo midogo midogo.

Mazingira ya uwekezaji katika viwanda vya kutengeneza mitambo ya

usindikaji na vifungshio hapa nchini yaboreshwe ili kuwavutia wawekezaji

6
kwenye viwanda hivi. Aidha bidhaa za maziwa ziondolewe kodi ya VAT

(Zero rating) kwa kipindi maalum kuwawezesha wasindikaji kujijengea

uwezo wa ushindani kwenye soko la Afrika Mashariki.

6.7. Kuboresha teknolojia ya usindikaji sambamba na kuongeza upatikanaji wa

maziwa kuna haja na mafunzo kwa wafugaji na wa wasindikaji ili kuzalisha

maziwa bora na kusindika bidhaa za aina mbalimbali na zenye ubora

uaotakiwa.

6.8. Kuboresha upatikanaji wa Taarifa na Takwimu.

Kuna haja ya Serikali na Wadau kuanzisha mfumo wa kukusanya,

kuchakata na kusambaza taarifa kuanzia vijijini kutumia maafisa ugani

hadi Wizarani ili ziweze kuwa sahihi na kupatikana kwa haraka.

6.9. Utatuzi wa maswala ya kisera.

• Kuwepo uwajibikaji kwenye vyombo vya udhibiti na vyombo hivi

madhumni yake, yawe ni kuwezesha na siyo kukwamisha.

Inapendekezwa kuwa shughuli zote za udhibiti wa sekta ya maziwa

zifanywe na Bodi ya Maziwa tofauti na sasa ambapo vyombo vingi

hufanya hivyo;

• Serikali iondoe kodi zote zenye kero kama ushuru unaotozwa na kila

wilaya au zitozwe mara moja tu.

• Wadau washirikishwe katika utayarishaji wa sera zinazohusu sekta ya

maziwa.

• Serkali itafute njia ya kuimarisha vyama vya kitaifa vya wadau (TAMPA,

TAMPRODA) ili viwe kweli vya kitaifa na vyenye uwezo wa kushirkiana na

Serikali kundeleza sekta.

• Bodi ya Maziwa iliyoanzishwa kisheria iwezeshwe kufunya shughuli zake

kwa kupewa rasilimali zinazotakiwa tofauti na sasa ambapo Bodi ipo kwa

jina tu.

• Uwepo mpango wa wafugaji wadogo kuzunguka mashamba makubwa

(outgrowers scheme) ili nao wapate teknolojia toka kwenye mashamba

makubwa.

• Wahitimu vyuo vya mifugo na vyuo vikuu na wataamu wastaafu

wawezeshwe kuwekeza kwenye sektka ya maziwa.

• Serikali iwezeshe utafiti kufanyika katika sekta ya maziwa kuanzia kwenye

uzalishaji hadi kwa mlaji.

7
6.10 Utatuzi wa Matatizo mengineyo

7. HITIMISHO

• Miundumbinu iboreshwe ili kuwezesha maziwa kukusanywa toka maeneo

ya mbali.

• Bodi na vyama vya wadau wawezeshwe ili kutoa ushauri unaofaa ili

wawekezaji waweze kushauriwa vizuri na pia kusimamia na kuondoa

wawekezaji wasio na nia nzuri.

Taarifa inaonyesha kuwa sekta ya usindikaji maziwa hapa nchini bado ni ndogo

sana kulinganisha na nchi majirani. Ili sekta hii iweze kuhimili ushindani kutoka

nje na kuweza kutoa mchango wake kwenye uchumi wa taifa juhudi kubwa

hazina budi kufanyika na wadau wote pamoja na serikali. Matatizo yaliyotajwa ni

kweli yapo na matokeo yake ni dhahiri katika viwanda vilivyosimamisha usindikaji

na pia matumizi madogo ya uwezo wa viwanda vinavyoendelea kusindika.

Matatizo haya ndiyo makubwa na yakitatuliwa yatawezesha sekta kukua kwa

haraka na kutoa ushindani wa kutosha.

Inapendekezwa kuwa njia zilizopendekezwa na wadau kutatua matatizo haya

zijumuishwe kwenye mipango ya Bodi ya Maziwa na kwenye programu za

utekelezaji wa sera ya maendeleo ya mifugo. Vyama vya Kitaifa vya wadau

ambao ndiyo watekelezaji wakuu vipewe uwezo na vihusishwe kama wabia

katika ngazi zote za utekelezaji. Aidha inapendekezwa kuwa, kwa vile

haikuwezekana kufanya uchambuzi wa kina kwa kila kiwanda, uchambuzi huu

uendelezwe hadi ngazi ya kila kiwanda na kila eneo ili kubaini na kuainisha

matatizo ya kila kiwanda na hata kutoa ushauri kwa kila kiwanda na kutoa taarifa

ya kina zaidi.

8. MAREJEO

1. K.R. Lusato, R. Ryoba na M.L. Kyomo, 2002. The contribution of Dairy

Industry to the National Economy, Poverty Alleviation and Household Food

Security in Tanzania. In. Proceedings of the 4 th National Dairy Development

Conference. 5 th – 6 th June 2002. AICC. Arusha Tanzania.

2. UNDP/GSB – Value Chain Analysis and Socio economic Assessment of the

Dairy Industry in Tanzania. Report presented by SCANAGRI and Business Care

Services. In. Proceedings of the 6 th National Dairy Development Conference, 2 nd

June 2006 Morogoro, Tanzania.

Kiambatanisho na. 1

DODOSO/QUESTIONNAIRE:

INVENTORY REPORT ON MILK PROCESSING IN TANZANIA/

8
TAARIFA YA TATHMINI YA MAENDELEO YA USINDIKAJI MAZIWA TANZANIA

SECTION A/SEHEMU A: Company business profile/ Maelezo ya kiwanda.

Fill the following table/

Jaza jedwali lifuatalo

Name/ x Designation/ x

Jina:

Cheo:

Company name/ x Year of establishment /

Jina la Kampuni

Mwaka ulioanza

Installed processing

capacity (lts/day)/

Uwezo wa kiwanda

kusindika (lita/siku)

Products processed in

your factory/

Aina ya bidhaa

zinazosindikwa

kiwandani kwako

Employment (number

of employees/

Ajira (idadi ya

wafanyakazi)

x Actual (running)

processing capacity

(lts/day)/Uwezo

halisi wa kiwanda

kusindika (lita/siku)

Maximum/

Kiasi cha juu

Minimum/

Kiasi cha chini

Type/Aina Amount (per year/

Kiasi (kwa mwaka)

x x

x x

x x

x x

x x

x x

Etc/n.k. Etc/n.k.

Skilled labourers

/Wataalam

Unskilled labourers

/Vibarua

SECTION B/SEHEMU B: Problems/Matatizo

What are the major problems facing your factory/business?

Kiwanda/biashara yako/yenu inakumbana na matatizo gani?

x

x

x

x

x

9

SECTION C/SEHEMU C: Solutions/Suluhisho

What should be done to solve problems faced by your factory/business?

Nini kifanyike kutatua matatizo yanayokabili kiwanda/biashara yako/yenu?

SECTION D/SEHEMU D: Opinion/Maoni

What are your opinions on how milk processing business can develop?/

Toa maoni yako kwa vipi vinwanda/bishara ya usindikaji maziwa iweze kuendelea?

10