08.01.2015 Views

MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - Equator Initiative

MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - Equator Initiative

MULIRU FARMERS CONSERVATION GROUP - Equator Initiative

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Empowered lives.

Resilient nations.

MULIRU FARMERS

CONSERVATION GROUP

Kenya

Miradi ya Equator

Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

MIRADI YA UNDP EQUATOR

Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni mbinu zinazonuiwa kuyakidhi mahitaji yao ya kila siku na ya kimazingira. Kuna kazi

chache ambazo zimechapishwa za kuelezea kinagaubaga hizo mbinu bunifu na vile zilianzishwa,vile ziliathiri wakaaji wa

sehemu mbali mbali na vile zimekuwa zikibadilika pindi wakati unapotita. Wachache wamejitokeza kuelezea wazi wazi juu

ya miradi yao, na hata wale ambao wamefanya hivyo ni wakuu wa vijiji ambao wamefanya kuelezea kufaulu kwao.

Mradi huu wa Equator Katika unadhamiria kujaza hili pengo kama njia moja ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa

kwake. Masimulizi juu ya huu mradi ni baadhi tu ya mingi ambayo imefaulu na kushinda tuzo za Equator baada ya kukaguliwa

na kutathiminiwa katika kitengo cha makundi ya kijamii yanayo hifadhi mazingira na kuinua maisha ya wanafijiji. Miradi hii

inakusudiwa kuwa mifano ya kuiwa na kuwatia shime kuzungumzia ilivyofaulu ili kuhamasisha ulimwengu juu ya uhifadhi

wa mazingira.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi

Wahariri

Mhariri Mkuu :

Muhariri Meneja :

Wahariri Waliochangia :

Joseph Corcoran

Oliver Hughes

Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Erin Lewis, Whitney Wilding

Wahandishi Waliochangia

Edayatu Abieodun Lamptey, Erin Atwell, Toni Blackman, Jonathan Clay, Joseph Corcoran, Larissa Currado, Sarah Gordon, Oliver Hughes,

Wen-Juan Jiang, Sonal Kanabar, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Rachael Lader, Patrick Lee, Erin Lewis, Jona Liebl, Mengning Ma,

Mary McGraw, Gabriele Orlandi, Juliana Quaresma, Peter Schecter, Martin Sommerschuh, Whitney Wilding, Luna Wu

Uchoraji

Oliver Hughes, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Amy Korngiebel, Kimberly Koserowski, Erin Lewis, John Mulqueen, Lorena de la Parra,

Brandon Payne, Mariajosé Satizábal G.

Shukrani

Equator ingependa kuwashukuru wanachama wa Muliru Farmers Conservation Group, haswa mwongozo na mchango wa James Ligare.

Picha ni za Muliru Farmers Conservation Group, ramani ni za CIA World Factbook na Wikipedia. Masimulizi juu ya mradi huu yalitafsiriwa

kwa Kiswahili na Dr. Ken Ramani.

Nukuu Ziada

United Nations Development Programme. 2012. Muliru Farmers Conservation Group, Kenya. Equator Initiative Case Study Series. New York,

NY.

MULIRU FARMERS

CONSERVATION GROUP

Kenya

MAELEZO KUHUSU MRADI HUU

Kikundi cha wakulima wahifadhi wa Muliro ni shirika

la kijamii linalopatikana karibu na msitu wa Kakamega

magharibi mwa Kenya. Kikundi hiki hujipatia riziki kwa kuuza

dawa ya kienyeji inayoitwa Naturab ambayo hutengenezwa

kutokana na mti spesheli.

Shughuli hizi za kikundi zimesaidia katika uhifadhi wa

msitu wa Kakamega. Wengi wa wanachama wa kikundi hiki

ni wanawake ambao huchuma riziki kwa kuuza dawa hii.

Aidha, baadhi ya pesa zinazopatikana kutoka biashara hii

hutumika kulipia utafiti kuhusu msitu huu na uhifadhi wake

kwa kijumla.

MUHTASARI

ULISHINDA TUZO YA EQUATOR: Mwaka 2010

ULIANZISHWA: Mwaka 1997

ENEO: Mkoa wa Magharibi, Kenya

WANAOFAIDI: Kaya 360

MAZINGIRA: Msitu wa Kakamega

YALIYOMO

Historia na Mandhari 4

Majukumu Makuu na Ubunifu 5

Matokeo ya Kimazingira 7

Matokeo ya Kijamii 7

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu 8

Maono 8

Wahisani 8

3

Historia na Mandhari

Msitu wa Kakamega ndio msitu asilia ulionusurika kutokana

na uharibifu wa kibinadamu. Msitu huu wenye miti aina tofauti

hupatikana mkoa wa magharibi. Msitu huu ndio tegemeo la wakaaji

wa eneo hilo. Wenyeji hutegemea msitu huu kwa mbao, kuni, chakula

cha ng’ombe, miti ya ujenzi na miti ya kutengeneza dawa za kienyeji.

Msitu huu ndo chanzo cha maji safi ya eneo hili pamoja na shughuli

zote za kibiashara. Msitu Kakamega (kama ilivyo kawaida kwa msitu

mingine nchini Kenya) huko karibu kuangamizwa na shughuli za

kibinadamu kama vile: ukulima na ujenzi, mbao ,uchomaji makaa na

utengenezaji wa madawa ya kienyeji. Idadi ya watu karibu na msitu

inaendelea kuongezeka huku eneo la kilomita moja kukaliwa na

watu takriban 1200. Hapa, kiwango cha umasikini ni cha juu huku

watu 35,000 wakitegemea msitu huu.

Kikundi hiki kina malengo manne makuu:

i. Kuimarisha ukuzaji wa kibiashara wa Ocimum Kilimandschirium

miongoni mwa wachochole wanoishi mkabala na msitu wa

Kakamega

ii. Kuunda na kutafutia soko bidhaa zinazotokana na mti huu

ndiposa wakulima wa mashinani wajipatie mapato

iii. Kuhamasisha wakulima kuhusu umuhimu wa kuutunza msitu

wa Kakamega

iv. Kuwakusanya majirani wa msitu huu ili kushiriki kikamilifu katika

shughuli za kuhifadhi msitu huu.

Kukuza na kuhifadhi mti wa dawa

Baadhi ya miti inayopatikana katika msitu Kakamega ni Ocimum

Kilimandscharicum. Tangu jadi mti huu umekuwa ukitumiwa na

wenyeji kwa kutibu mafua na kikohozi. Mti huu huwa na mafuta

yenye mnuko spesheli. Matawi yake yamekuwa yakichemshwa na

kutumiwa kutibu magonjwa ya kupumua. Matumizi mengine ni

kama: kufukuza mbu, kutengeneza asali (nyuki), viungo vya vyakula

na kufukuza wadudu wanavamia ghala za mahindi.

Kikundi cha Muliru kiliundwa mnamo mwaka wa 1997 kikiwa na lengo

la kukuza mti wa Ocimum Kilimandscharicum ambao wangeutumia

kama mbinu ya kuhifadhi msitu wa Kakamega na kuwapa kitega

uchumi majirani wa msitu huu. Kikundi hiki kimechanganya elimu ya

zamani na ile ya kisasa yakiteknolojia na sayansi na kupata washika

dau wa kipekee - wakulima wa mashinani, asasi za utafiti na sekta

ya kibinafsi – ili kuongeza ubora wa mti huu wa dawa. Kikundi hiki

hushirikiana sako kwa bako na wakulima wa mashinani kuunda

bidhaa tofauti tofauti kutokana na mti huu ambao huuzwa kwa

kutumia nembo na jina la usajiri la Naturub. Naturub imesajiriwa

kama dawa ya kutibu mafua, kikohozi, maumivu, kuumwa na

wadudu na miteguko mbalimbali.

4

Majukumu Makuu na Ubunifu

Kikundi cha Muliru huwaleta pamoja majirani wa msitu Kakamega

ili kupanda miche ya Ocimum Kilimanscharicum. Ukulima wa mti

huu huwa biashara muhimu kwa wakulima waliotengwa wa eneo

hii. Wakulima hufunzwa namna ya kutayarisha na kuvuna mti huu

nyumbani mwao. Mti huu huvunwa kwa kukatia sehemu karibu na

mizizi na kisha kuchuma matawi yake. Kitambo, utoaji wa mafuta

ulifanyiwa nyumbani, lakini mnamo mwaka wa 2005, Muliru ilijenga

mtambo wa kazi hiyo katikati mwa eneo hilo. Wakulima husaidiwa na

kikundi kukusanya na kusafirisha matawi mitamboni. Hapa matawi

hupimwa na kukaushwa. Matawi haya makavu hutengenezwa

mafuta maalum ambayo huuzwa kwa nembo ya Naturub.

Utengenezaji na uuzaji wa Naturub

Tangu kuzinduliwa mtambo wa utengenezaji wa mti wa Ocimum

tani 770 zimetengenezwa na kilo 700 za mafuta kidawa yametolewa.

Aidha takriban vidonge 400,000 vya Naturub vimeuzwa mijini na

mashinani kote nchini Kenya. Bidhaa hizi za Naturub zimekubaliwa

vyema masokoni ingawa vimepata ushindani mkubwa kutoka

bidhaa za kimataifa. Kipato cha mradi huu ni takribani dolla 70,000

za kimarikani. Hivi sasa wakulilma kama 360 wanakuza mti huu

mashambani mwao. Ukulima wa mti huu umeongezeka kwa

kiwango kikubwa katika eneo hili.

Uongozi

Kikundi hiki kinaingozwa na bodi iliyoundwa na; mwenyekiti na

naibu wa mwenyekiti, katibu na naibu wa katibu, mwekahazina,

katibu mwandalizi na wanakamati wane, ambao uchaguliwa na

vikundi vya wakulima kuhudumu kwa miaka fulani. Bodi ndiyo inayo

usemi wa mwisho katika kikundi hiki cha Muliru. Jukumu kuu la bodi

ni kuhakikisha kuwa maslahi ya wakulima yanazingatiwa na kupata

ujira mwema wa mauzo yao. Kikundi kina nyapala mkuu ambaye

anaendesha shughuli zote za kikundi hiki na kuripoti kwa bodi.

Shirika hili lina vitengo kadha vyenye kushughulikia mambo tofauti

tofauti; mfano, kitengo cha mauzo ambacho huijishughulisha na

kuuza bidhaa za kikundi hiki katika maduka makuu nchini Kenya,

kitengo hiki vile vile ushirikiana na makampuni ya kibinafsi ili

kutangaza bidhaa za shirika hili. Mwisho kikundi huwa na vitengo

vitatu katika ngazi ya mashinani. Mwakilishi wa vikundi vya

wakulima ambaye hutoa maoni ya wakulima wakati wa mikutano.

Ngazi ya pili, huwa na mwendesha mtambo ambaye husaidiwa na

vijana tisa katika kutoa mafuta malighafi. Ngazi ya mwisho ni askari

gongo mkuu ambaye hushirikiana na utawala wa mkoa ili kuchunga

mali yote ya kikundi.

Licha ya kukuza na kuuza bidhaa za Naturub, shirika hili la uhifadhi

wa msitu huandaa warsha za kimasomo kwa wenyeji wa eneo hili

wakiwafunza juu ya umuhimu wa kuyatunza mazingira na raslimali

asilia kama misitu. Shirika hili hutayarisha miche ya miti asili ambayo

hukabidhiwa wakulima ili kuipanda mashambani mwao.

Ubunifu usiosahaulika wa kikundi hili ni ule wa kuanzisha mradi

uliosajiri dawa, kuunda na kisha kuifanya biashara muhimu ya

kunufaisha wakulima wachochole. Licha ya kuhimiza ukulima wa

mti huu, kikundi kilienda hatua moja zaidi kwa kuanzisha mtambo

uliomilikiwa na kuendeshwa na wakulima wenyewe. Isitoshe,

wakulima wamepata ujira wa kudumu na kuinua viwango vya

maisha yao.

5

Fig. 1: Jendwali la Uongozi

Bodi ya Usimamizi

Nyapala Mkuu

Kitengo cha Mafunzo

Kitengo cha Uundaji

Kitengo cha Mauzo

Mwakilishi wa Wakulima

Msimamizi wa Mtambo

Askari gongo Mkuu

Chanzo: Kikundi Cha Wakulima Wahifadhi Cha Muliru

6

Matokeo

MATOKEO YA KIMAZINGIRA

Matokeo makuu ya mradi huu ni matumizi na uhifadhi mwema wa

msitu Kakamega na vilevile kulinda takribani ndege 350 na mimea

380 inayopatikana humo. Aidha, mradi huu umesaidia wenyeji kuwa

na fikra chanya kuhusu uhifadhi wa msitu pamoja na miti - mradi

huu vilevile umechukuliwa kama kielelezo chema cha uhifadhi wa

msitu na, chama cha msitu cha jamii ya Mwileshi.

Chama cha msitu cha jamii ya mwileshi

Chama cha kitaifa kinachosimamia msitu (KWS) kiko mbioni

kuhusisha jamii za mashinani katika uhifadhi wa misitu. Msitu

wa Kakamega ulichaguliwa ili kufanyia majaribio hayo ambapo

ushirikiano kati ya jamii za mashinani pamoja na kikundi cha Muliru

wamepanda miche 10,000 mnamo Septemba 2010 pekee. Vyama

hivi vilivyokusanywa pamoja hufunza jamii kuhusu umuhimu wa

msitu na namna ya kuitunza misitu kwa jumla.

Kubadili mtizamo kuhusu uhifadhi wa misitu

Utafiti uliofanywa na kikundi cha MuIiru ,ukihusisha wakulima wa

Ocimum 360 ulionyesha wazi kuwa wakulima asilimia 85 huhifadhi

msitu. Matokeo kamili ya utafiti huo ni kama ifuatavyo; Asilimia 49 ya

wakulima hao husambaza elimu ya uhifadhi wa misitu kwa wenzao,

asilimia 59 wamepunguza ukusanyaji kuni , chakula cha ng’ombe na

mbao msituni humo, asilimia 37 wamewakataza wanajamii wengine

dhidi ya kutumia msitu vibaya na asilimia 5 ya wakulima wameripoti

visa vya uwindaji haramu kwa utawala wa mkoa. Uvunaji wa Ocimum

hauharibu mazingira, mimea ya Ocimum humea tena baada ya

kukauka na hivyo jamii hupata kipato kisichoisha. Bidhaa za Naturub

huwa na onyo na mawaidha ya kuhimiza uhifadhi wa mazingira.

MATOKEO YA KIJAMII

Kikundi cha Muliru kimetanda miongoni mwa wilaya 5

zinazouzunguka msitu wa Kakamega ,na idadi ya watu ni kama2,500

na wanachama wa kikundi wakiwa ni 360.Wengi wa watu katika

eneo hili wametengwa kiuchumi na wengi ni wachochole walio na

mashamba madogo mno yasiyoweza kuwakimu kimaisha. Kikundi

hiki cha Muliru kimebadili hii hali kwa kuwapa wenyeji fursa ya kazi

na njia ya kujipatia riziki. Takribani watu 8 wa eneo hili wamepata

kazi ya kudumu mitamboni . Isitoshe takribani wakulima 900 wana

kazi ya kulima mmea huu hadi sasa vidonge 400,000 vimeuzwa kote

nchini hususan kwenye maduka makuu kama vile; Uchumi,Turskeys

na Eastmat. Naturub vilevile hupatikana kwenye maduka ya dawa

nchini Kenya. Wakulima hupata marupurupu yao mara tatu kwa

mwaka na wameona kipato chao kikiongezeka kwa asilimia 300

tangu mradi huu kuanzishwa.

Faisa Nynginezo

Kutokana na utafiti wa awali uliofanywa na kikundi hiki cha Muliru,

kulipatikana faida nyinginezo kama; asilimia 31 ya wakulima hutumia

hela walizozipata kutoka kwa mradi huu kuanzisha biashara ndogo

ndogo na hivyo kuongezea kipato chao. Isitoshe , asilimia 83.5

hutumia hela zao ili kununulia familia zao chakula . Asilimia 57 hulipia

watoto karo ,asilimia 26 hujinunulia nguo, asilimia17.65 hutumia

pesa hizo kukarabati nyumba zao. Wenyeji vilevile wamenufaika

na elimu ya kibiashara wanaopewa na mashirika mengine. Mradi

huu vilevile umeinua kiwango cha maisha ya wenyeji. Wakulima

nao ni kati ya washika dau wa shirika hili . Wakulima kwa sasa wana

ufahamu mkuu kuhusu kilimo, uwekaji pesa na kuhusu umuhimu

wa mshikamano wa kijamii.

Mradi huu aidha umehimiza usawa wa kijinsia ambapo jamii ya hapa

imekubali ukweli kuwa uchumaji ni kazi ya mke na mume .Wanawake

pia wanastahili kuchaguliwa kwenye nyadhifa za uongozi

7

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu

JINSI YA KUDUMISHA MRADI HUU

Kikundi cha Muliru kilikua na mpango wa miaka kumi ya matumizi

ya faida inayotokana na mauzo ya Naturub. Mpango wenyewe ulikua

kama ufuatao; asilimia 10 kusaidia katika uhifadhi wa msitu wa

Kakamega, asilimia 10 iingie kwenye mfuko wa maendeleo ya jamii

inayozunguka msitu Kakamega, asilimia 60 kupewa wanachama wa

kikundi cha Muliru, na asilimia 20 kuingia kwenye mfuko wa kusaidia

utafiti. Kikundi kinachokisia kuwa shirika hili litajisimamia kifedha

na kukua zaidi. Naturub ndiyo dawa pekee ya kienyeji kupata usajili

wa kiserikali pamoja na shirika la madaktari linalosimamia dawa

na sumu nchini. Upelelezi wa siri kuhusu Naturub umeonyesha

kuwa dawa hii inazaa takribani shilingi million 100 kwa kila mwaka

mijini. Kikundi cha Muliru kimetegemea mashirika ya nchini na

kimataifa katika kufikia malengo yake. Muliru imewahi kushirikiana

na kampuni kadhaa za matangazo na utangazaji katika kuendeleza

malengo yake. Mashirika mengine ambayo yamefadhili Muliru ni

kama chuo kikuu cha Nairobi, kituo cha dunia cha misitu, shirika la

wanyama pori la Kenya (KWS) na mengineyo. Maono mengine ya

kikundi ni kuongeza usalishaji, kutafuta masoko mengine ya nchini

na kitaifa, kufanya utafiti zaidi kuhusu mmea huu kuwapa mafunzo

zaidi wakulima na kuimarisha na kuhimiza wanawake na vijana

kuunga mkono mradi huu.

MAONO

Budongo nchini Uganda. Kulingana na maoni ya kikundi cha Muliru,

mafunzo yanayobadilishwa miongoni mwa watu wenye rika moja

huzama na kueleweka zaidi

WAHISANI

• Kituo cha kimataifa cha uchunguzi wa Wadudu

• Chuo Kikuu cha Nairobi

• Shirika la Dunia la Misitu

• Taasisi ya Utafiti waMisitu la Kenya [KEFRI]

• Shirika la Wanyama Pori la Kenya [KWS]

• Shirika la[GBDI]

• Wakfu wa Ford

• Wakfu wa Bio Vision

• Wakifu wa Macarthur

• Huduma za kiuduma za Kijerumani [DED]

• PACT-Kenya/USAid

• WHO Multilateral Initiative on Malaria/Research and Training in

Tropical Diseases (TDR)

Kikundi hiki kimebadilisha mawazo ya mradi na wanajamii wa nchi

kama Uganda, Tanzania, Afrika kusini na Nigeria na vilevile jamii

zingine za humu nchini. Zaidi ya watu 830 wametutembelea ndiposa

wapate masomo ya moja kwa moja . Mafunzo yanayopatikana kutoka

kwa mradi huu yamesambazwa kupitia kwa mihadhara ,uigizaji,

utambaji na matembeleano. Isitoshe , mradi huu umeonyeshwa

na kutangazwa na vyombo mbalimbali vya kimataifa kama redio

na televisheni. Kutokana na utangazaji huo, mradi wetu umeigwa

na jamii kadhaa mfano kikundi cha kuifadhi misitu cha mashariki

ya Usambara nchini Tanzania na kikundi kinachohifadhi misitu ya

8

MAREJELEO YA ZIADA

• Muliru Farmers Conservation Group PhotoStory (Vimeo) vimeo.com/15780379

• Video on Muliru Farmers Conservation Group (Vimeo) vimeo.com/43207923

Masimulizi kuhusu miradi mingine, bonyeza hapa:

Equator Initiative

Environment and Energy Group

United Nations Development Programme (UNDP)

304 East 45th Street, 6th Floor

New York, NY 10017

Tel: +1 646 781-4023

www.equatorinitiative.org

Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ndio unaoendesha miradi ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni

kwa kutoa mwito wa mageuzi na kuelekeza mataifa kwa maarifa, na malighafi ili kusaidia watu kujiimarisha kimaisha.

Mradi huu wa Equator huleta pamoja Umoja wa Mataifa , serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanyibiashara na makundi ya

mashinani ili kutambua na kuimaliza maendeleo himili kwa watu na jamii kwa jumla.

©2012 Haki Zote ni za Mradi wa Equator

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!