Haliuzwi - Femina HIP

Haliuzwi - Femina HIP Haliuzwi - Femina HIP

feminahip.or.tz
from feminahip.or.tz More from this publisher
21.06.2013 Views

Mila katika kupambana na VVU Unyago ni sehemu ya utamaduni wa watu wa Pwani ya Tanzania kumfundisha mtoto wa kike anapovunja ungo mambo muhimu yanayohusu afya ya uzazi, usafi na majukumu mengine yanayomhusu. Utamaduni huu umesaidia kwa kiasi kikubwa kuweka njia kwa watu wazima (manyakanga) kuwaandaa wasichana kwa maisha ya utu uzima. Mwisho wa mafunzo ya unyago wasichana ambao huitwa wali hutolewa nje kwa sherehe maalum ya kuhitimu ijulikanayo kama “kunema”. Hatua zimechukuliwa… Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya PAYODE (Partnership for Youth Development) katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha iliendesha mafunzo shirikishi kwa manyakanga kuhusu afya ya uzazi na kujikinga na maambukizi ya VVU. Mafunzo haya yalisaidia kuboresha uelewa wa manyakanga na kuwajengea stadi za kuingiza elimu hii ndani ya mafunzo ya unyago. Jumla ya manyakanga 40 wamepata mafunzo kupitia PAYODE tangu mwaka 2008. 30 Si Mchezo! machi-aprili 2012 Watu wanasemaje? ZINDUKA Mtazamo uko hivi… Wasichana na wanawake wapo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya VVU ikilinganishwa na wavulana na wanaume wa umri sawa na wao. Hata hivyo njia rahisi ya kuwafikia vijana hasa wasichana kwa shughuli za uelimishaji kuhusu ujana na makuzi bado ni changamoto kutokana na mila na desturi ya Mtanzania. Ushuhuda unaonyesha kuwa elimu ya unyago inayotolewa na manyakanga hawa waliopatiwa mafunzo imesaidia kupunguza tatizo la wasichana kuachishwa shule kwasababu ya ujauzito katika maeneo ya mradi. Jamii na serikali imefurahishwa na hatua ya PAYODE kutumia utamaduni wa watu wa Pwani kama njia chanya ya kufikishia wasichana elimu ya afya ya uzazi . “Natamani watoto wangu wangeliyajua haya yote kabla,” anasema mwenyekiti wa manyakanga, Mama Blandina Mbaji.

. USHAURI Swali Nina mpenzi ambaye tumekamilisha taratibu zote za ndoa, lakini kabla ya ndoa akapata ujauzito. Baada ya kuanza huduma za kliniki akaonekana ana maambukizi ya VVU, na mimi nilipopimwa nikawa salama. Je, mpenzi wangu huyu anafaa kuoa ? Ushauri tafadhali. Msomaji Si mchezo! Lindi-Pwani Kama mmepima na ukagundua mwenzio ana VVU usimuache. nendeni kwa mshauri nasaha atawashauri jinsi ya kumkinga mtoto na wewe mwenyewe usipate maambukizi na mtaishi kwa raha. Amosi wa Mkuranga Kama kweli unampenda mwenzi wako, nakushauri endelea kuwa naye kama rafiki yako wa karibu sana. Pia kuwa mshauri wake katika hali aliyonayo maana kuwa na VVU siyo kufa na urafiki au uhusiano usivunjike. Ibrahim Manjale, Mkuranga SWALI LA TOLEO LIJALO Pole kaka yangu, kama kweli hiyo mimba ni yako na unampenda mkeo nakushauri umuoe. Kuwa na VVU siyo mwisho wa mapenzi na hakuzuii kuendeleza mipango yenu. Nendeni kwenye kituo cha huduma na tiba kwa ushauri zaidi. Hamisi Nuru Jimowaco-Mkuranga Kuna binti tumependana na nimependa tabia zake. Yuko tayari kuoana nami lakini naogopa kwasababu nimetembea na dada yake ambaye kwa sasa ameolewa. Ila binti huyo sijafanya naye ngono, anasema mpaka tuoane. Naombeni ushauri wenu. Festo Mgaya, Songea. Nawapongeza kwa kupima. Yeyote anayeishi na VVU ana haki zote za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuoa/kuolewa, kuwa na familia n.k. Maamuzi ya kumuoa au kutokumuoa ni yako na yeye. Katika upimaji VVU kuna uwezekano kwa sasa ukawa salama lakini baada ya muda ukakutwa nawe hauko salama. Nenda katika kituo cha ushauri nasaha watakupa elimu ya kuishi na mke mwenye maambukizi ya VVU bila wewe kupata maambukizi na kupata watoto wasio na maambukizi. Asante Betty Liduke ni rafiki mkubwa wa vijana, hata wewe unaweza kulonga naye. Ni msambazaji mkubwa wa wa Jarida la Si Mchezo! Mkoani Njombe. Ni mshauri nasaha na ni mratibu wa kitengo cha udhibiti Ukimwi katika Kampuni ya TANWAT, Njombe. Mwandikie kupitia Jarida la Si Mchezo! Si Mchezo! S. L. P. 2065 Dar es Salaam au tuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba 0715 568222 na utuambie kama ungependa uchapishwe. machi-aprili 2012 Si Mchezo! 31

Mila katika kupambana na VVU

Unyago ni sehemu ya utamaduni wa watu wa Pwani

ya Tanzania kumfundisha mtoto wa kike anapovunja

ungo mambo muhimu yanayohusu afya ya uzazi, usafi

na majukumu mengine yanayomhusu. Utamaduni huu

umesaidia kwa kiasi kikubwa kuweka njia kwa watu

wazima (manyakanga) kuwaandaa wasichana kwa

maisha ya utu uzima. Mwisho wa mafunzo ya unyago

wasichana ambao huitwa wali hutolewa nje kwa sherehe

maalum ya kuhitimu ijulikanayo kama “kunema”.

Hatua zimechukuliwa…

Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya PAYODE

(Partnership for Youth Development)

katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha

iliendesha mafunzo shirikishi kwa

manyakanga kuhusu afya ya uzazi

na kujikinga na maambukizi ya VVU.

Mafunzo haya yalisaidia kuboresha uelewa

wa manyakanga na kuwajengea stadi

za kuingiza elimu hii ndani ya mafunzo

ya unyago. Jumla ya manyakanga 40

wamepata mafunzo kupitia PAYODE

tangu mwaka 2008.

30 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Watu wanasemaje?

ZINDUKA

Mtazamo uko hivi…

Wasichana na wanawake

wapo katika hatari zaidi ya

kupata maambukizi ya VVU

ikilinganishwa na wavulana

na wanaume wa umri sawa na

wao. Hata hivyo njia rahisi ya

kuwafikia vijana hasa wasichana

kwa shughuli za uelimishaji

kuhusu ujana na makuzi bado ni

changamoto kutokana na mila

na desturi ya Mtanzania.

Ushuhuda unaonyesha kuwa elimu ya unyago

inayotolewa na manyakanga hawa waliopatiwa

mafunzo imesaidia kupunguza tatizo la

wasichana kuachishwa shule kwasababu ya

ujauzito katika maeneo ya mradi. Jamii na

serikali imefurahishwa na hatua ya PAYODE

kutumia utamaduni wa watu wa Pwani kama

njia chanya ya kufikishia wasichana elimu ya afya

ya uzazi . “Natamani watoto wangu wangeliyajua

haya yote kabla,” anasema mwenyekiti wa

manyakanga, Mama Blandina Mbaji.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!