Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
SAUTI YANGU

Si Mchezo!

Femina HIP

SLP 2065,

DSM

Acheni siasa, leteni

maendeleo

Nakereka sana na Baraza la Madiwani

kugombana na Mkurugenzi wa

Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.

Kila siku ni mifarakano isiyokuwa na

tija. Mpaka sasa maendeleo hakuna

na hatupigi hatua yoyote mbele.

Miundombinu ni mibovu, hospitali ya

wilaya hakuna chumba cha kuhifadhia

maiti, vijana hawana ajira na maisha

ni magumu kwa ujumla. Nawaomba

viongozi hawa wakae pamoja na kutatua

tofauti zao, washikamane na kutuletea

maendeleo katika wilaya yetu.

Saidi Juma Aina

Mkuranga

28 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Kama una chochote

unachotaka kusema

tuandikie ili upate

fursa ya kuwaelimisha

wengine

Maoni yaliyotolewa katika ukurasa huu

ni ya wasomaji, si lazima yalingane na

msimamo wa Femina HIP.

Wateja wengine

wa saluni...

Sipendi tabia ya baadhi ya wateja wanaokuja

saluni kupata huduma za urembo wa nywele

na nakshi nyingine. Wengi wanajisahau

kwamba hili ni eneo la biashara na kazi.

Wanajazana na kuanza kupiga umbea, wakati

mwingine nafasi inakosekana kwa wateja

wanaohitaji kupata huduma. Hii ni kero

hapa kwetu na mbaya zaidi wanaume nao

wanashiriki mambo haya. Jamani nendeni

maeneo yenu mkafanye vijiwe vya umbea na

majungu mtuache sisi tufanye kazi.

Marium a.k.a Mama Zai

Kimanzichana-Mkuranga

Acheni kutudharau

Kuna imani kwamba ukifanya

kazi nyumba za kulala wageni

maarufu kama guest house,

baa au ukiwa mhudumu wa

hoteli jamii inakuchukulia

kama mhuni. Hii si sahihi hata

kidogo kwani wanaofanya

kazi hizi wanajiheshimu, kama

yeyote yule anayefanya kazi

katika sekta nyingine. Acheni

kuwashikashika wahudumu.

Jua kwamba wapo kazini na

siyo sehemu ya kuendekeza

mapenzi ya kulazimisha.

Heshimu utu wao.

Judith Macha

Mkuranga-Pwani

Wewe pia unaweza kulonga na vijana

wenzako. Tuandike maoni,

ushauri, vichekesho,maswali

nk, weka anuani yako na tuma

ukiambatanisha na picha yako

kwa Mhariri, Jarida la Si Mchezo!,

S.L.P 2065 Dar es Salaam.

simchezo@feminahip.or.tz

Au tumbukiza katika boksi la Si

Mchezo! kama lipo katika eneo

unaloishi.