Haliuzwi - Femina HIP

Haliuzwi - Femina HIP Haliuzwi - Femina HIP

feminahip.or.tz
from feminahip.or.tz More from this publisher
21.06.2013 Views

26 Si Mchezo! machi-aprili 2012 Ama kweli majuto ni mjukuu! Kijumbe ndo keshatoroka na fedha za mchezo, ameacha vumbi tu! Upatu ni mzuri. Tatizo wengi wetu tunaucheza kienyeji mno!

UKWELI WA MAMBO Yanawakuta wengi! Stori ya Mama Semeni na wenzake haichekeshi bali inasikitisha! Inawezekana hata wewe ama unacheza upatu au una mpango wa kucheza. Inawezekana umeapa kutokucheza tena upatu kwani yaliwahi kukukuta yaliyomkuta Mama Havinitishi na wenzake! Pole! Sio mchezo mbaya Upatu au ‘mchezo’ kama wengi wanavyouita, si jambo baya. Wengi ‘wametoka’ kwa staili hii. Utaukuta mitaani, maofisini, kwa watu ambao ama wako katika ‘kijiwe’ kimoja au wanafanya biashara zinazofanana. Kwa kifupi ni jambo zuri. Ndiyo, kwani si kila mmoja ana uwezo wa kudunduliza vijisenti peke yake hadi mfuko utune. Zaidi ya kuwasaidia watu kuinua mitaji na kujikwamua kimaisha, ‘mchezo’ huu unawasaidia watu kuishi kijamaa, yaani kufahamiana na kusaidiana katika matatizo mbalimbali ya kijamii, wengine wanasema ‘kufa na kuzikana’. Tatizo nini? Tumeshuhudia ngumi zikilika mitaani, watu wakiporomosheana matusi, wengine wakibubujikwa machozi baada ya ‘kuingia chaka’, ukiuliza kulikoni unaambiwa kijumbe ‘kasepa’ na fedha za wanakikundi! Yote haya yanatokea kwa sababu tunaucheza ‘mchezo’ huu kienyeji mno, kama tunavyoona katika stori ya Mama Semeni na wenzake. Walipaswa wakutane, wafanye makubaliano ya kucheza ‘mchezo’, kuwe na orodha ya wanachama iliyoandikwa na zamu za ‘kupokea’, wafanye uchaguzi wa ‘kijumbe’ wajipangie masharti na kuwe na daftari la kusaini mwanachama anapowasilisha mchango na anapopokea. J Kumbuka Ni vizuri muwe ni kikundi cha watu mnaofahamiana vizuri kwa makazi, kipato na tabia, ili kuepusha mambo kwenda mrama. machi-aprili 2012 Si Mchezo! 27

UKWELI WA MAMBO

Yanawakuta wengi!

Stori ya Mama Semeni

na wenzake haichekeshi

bali inasikitisha!

Inawezekana hata wewe ama

unacheza upatu au una mpango

wa kucheza. Inawezekana

umeapa kutokucheza tena

upatu kwani yaliwahi kukukuta

yaliyomkuta Mama Havinitishi

na wenzake! Pole!

Sio mchezo mbaya

Upatu au ‘mchezo’ kama

wengi wanavyouita,

si jambo baya. Wengi

‘wametoka’ kwa staili hii.

Utaukuta mitaani, maofisini,

kwa watu ambao ama

wako katika ‘kijiwe’ kimoja

au wanafanya biashara

zinazofanana. Kwa kifupi ni

jambo zuri. Ndiyo, kwani si

kila mmoja ana uwezo wa

kudunduliza vijisenti peke

yake hadi mfuko utune.

Zaidi ya kuwasaidia

watu kuinua mitaji na

kujikwamua kimaisha,

‘mchezo’ huu unawasaidia

watu kuishi kijamaa,

yaani kufahamiana na

kusaidiana katika matatizo

mbalimbali ya kijamii,

wengine wanasema ‘kufa na

kuzikana’.

Tatizo nini?

Tumeshuhudia ngumi zikilika mitaani, watu

wakiporomosheana matusi, wengine wakibubujikwa

machozi baada ya ‘kuingia chaka’, ukiuliza kulikoni

unaambiwa kijumbe ‘kasepa’ na fedha za wanakikundi!

Yote haya yanatokea kwa sababu tunaucheza ‘mchezo’

huu kienyeji mno, kama tunavyoona katika stori ya Mama

Semeni na wenzake.

Walipaswa wakutane, wafanye makubaliano ya kucheza

‘mchezo’, kuwe na orodha ya wanachama iliyoandikwa

na zamu za ‘kupokea’,

wafanye uchaguzi wa

‘kijumbe’ wajipangie

masharti na kuwe

na daftari la kusaini

mwanachama

anapowasilisha mchango

na anapopokea.

J Kumbuka

Ni vizuri muwe ni kikundi

cha watu mnaofahamiana

vizuri kwa makazi, kipato

na tabia, ili kuepusha

mambo kwenda mrama.

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

27

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!