Haliuzwi - Femina HIP

Haliuzwi - Femina HIP Haliuzwi - Femina HIP

feminahip.or.tz
from feminahip.or.tz More from this publisher
21.06.2013 Views

Minyoo bwana! Hahahahaaaa! Watu bwana! Bila shaka umewahi kusikia mtu akisema eti binadamu lazima awe na minyoo! Eti minyoo ina kazi ya kulainisha chakula katika tumbo la binadamu! Dokta Lugano Kiswaga wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga anasema huo ni uongo mtupu! “Minyoo iko ya aina nyingi na hakuna aina yoyote ya minyoo yenye faida katika mwili wa binadamu, ila huingia katika mwili wa binadamu au mnyama kwani ndiyo mazingira yanayoiwezesha kuzaliana,” anasema. Mh! Inaingiaje? “Kuna njia nyingi za kuingia ila kubwa ni kupitia chakula kisichosafishwa vizuri, nyingine ni kujipenyeza katika matundu madogomadogo ya ngozi ya mwanadamu,” anasema. “Ukila chochote bila kunawa mikono vizuri kwa sabuni na maji safi, unaweza kuingiza minyoo tumboni. Usipoosha vizuri matunda na mboga za majani zinazoliwa zikiwa mbichi, mfano kabichi, karoti, nyanya nk, unaweza kula minyoo”, anasema. “Minyoo inapopenya katika matundu ya ngozi, inakwenda katika mishipa ya damu, kisha kwenye moyo, halafu kwenye mapafu na hatimaye unaikohoa inaingia katika utumbo. Inapofika humo huweka makazi, ikakua, ikataga mayai, kisha ukayatoa mayai hayo kupitia haja kubwa, yanaanguliwa nje ya tumbo la binadamu na mzunguko hujirudia kama kawaida”, anasema. 22 Si Mchezo! machi-aprili 2012 PASIPO NA DAKTARI Utajuaje kama una minyoo? n Unaweza kuiona katika kinyesi n Kukohoa n Inatoboa utumbo, hivyo unaweza kuona damu kidogo katika kinyesi n Kuwashwa sana usiku sehemu ya haja kubwa (hasa kwa watoto) n Kukonda n Kukosa hamu ya kula n Upungufu wa damu n Ngozi kupauka n Ukuaji hafifu (kudumaa – hasa kwa watoto) Chonde chonde! Ukiona dalili hizi au hata baadhi yake, kamwone mtaalam wa afya kwa vipimo na ushauri kwani linaweza kuwa ni tatizo la minyoo, ambalo linaweza kuleta athari kubwa kwa binadamu, ikiwamo upungufu mkubwa wa damu na hata kifo! Usimeze dawa za minyoo bila ushauri wa daktari. J Kumbuka Zingatia usafi kujiepusha na magonjwa

HUDUMA Walianza kama utani! Siku moja wanawake 30 walikaa kikao ‘wakateta’ jambo. Walichoka kuona jinsi janga la Ukimwi lilivyokuwa likienea kwa kasi katika jamii. Waliunda kikundi chao ‘wakakibatiza’ jina la JIMOWACO, yaani Jipeni Moyo Women and Community Organisation, kikundi ambacho leo hii ni gumzo kubwa Kisarawe na Mkuranga. Hawa, ni wanawake ambao waume zao walikuwa wakifanya kazi katika mgodi wa chokaa huko Kisarawe na hiyo ilikuwa ni mwaka 2003. Walichangishana pesa, wapo walioomba kwa waume zao, wapo waliovunja ‘vibubu’ vyao, ili mradi wazo lao lifanikiwe! Wako mbali! Leo hii JIMOWACO imesimama! Imeajiri wafanyakazi 12 na tayari imefungua tawi wilayani Mkuranga, imeanzisha vikundi 20 vya kuweka na kukopa katika jamii, vikiwa na mchanganyiko wa watu waishio na VVU na wasio navyo. Wanatoa mahitaji ya shule na huduma za afya kwa watoto wapatao 7,093 na wanatoa huduma kwa watu waishio na VVU/Ukimwi wapatao 1,913 (Mkuranga) na 1,200 (Kisarawe)! Ama kweli hata mbuyu ulianza kama mchicha! Mambo sio mteremko! Wana malengo! “Tulipoanza tulikusudia kusadia yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, wajane, na waishio na VVU/Ukimwi”, anasema Flaviana Mlaki, Mratibu wa Watoto-JIMOWACO. Mwananchi akifurahia msaada wa sare za shule kutoka JIMOWACO Pamoja na mafanikio makubwa waliyoyapata, Flaviana anasema vikwazo pia vipo: n Hawana uwezo wa kuwafikia watoto wote wanaohitaji huduma yao kwani ni wengi sana katika jamii. n Unyanyapaa nao bado upo na ni kikwazo kwa watu kujitokeza kwenda kupima VVU. n Licha ya elimu inayotolewa, maambukizi mapya bado yanajitokeza kwa kasi kwani waliokuwa wagonjwa baada ya kupata ahueni wanaendelea kuambukiza wengine. n Baadhi ya watu wanapougua kutokana na Ukimwi wanaamini wamerogwa, hivyo wanakwenda kwa waganga wa kienyeji. Wana ujumbe kwetu! JIMOWACO wanaamini kwamba hata wewe msomaji pamoja na watu waliokuzunguka mnaweza kuanzisha mkakati kama huu katika eneo lenu. Siri ya mafanikio ni subira, kujiamini na kupeana moyo! machi-aprili 2012 Si Mchezo! 23

HUDUMA

Walianza kama utani!

Siku moja wanawake 30 walikaa kikao ‘wakateta’

jambo. Walichoka kuona jinsi janga la Ukimwi lilivyokuwa

likienea kwa kasi katika jamii. Waliunda

kikundi chao ‘wakakibatiza’ jina la JIMOWACO, yaani

Jipeni Moyo Women and Community Organisation,

kikundi ambacho leo hii ni gumzo kubwa Kisarawe na

Mkuranga.

Hawa, ni wanawake ambao waume zao walikuwa wakifanya

kazi katika mgodi wa chokaa huko Kisarawe na hiyo

ilikuwa ni mwaka 2003. Walichangishana pesa, wapo walioomba

kwa waume zao, wapo waliovunja ‘vibubu’ vyao,

ili mradi wazo lao lifanikiwe!

Wako mbali!

Leo hii JIMOWACO imesimama!

Imeajiri wafanyakazi

12 na tayari imefungua

tawi wilayani Mkuranga,

imeanzisha vikundi 20 vya

kuweka na kukopa katika

jamii, vikiwa na mchanganyiko

wa watu waishio na

VVU na wasio navyo. Wanatoa

mahitaji ya shule na

huduma za afya kwa watoto

wapatao 7,093 na wanatoa

huduma kwa watu

waishio na VVU/Ukimwi

wapatao 1,913 (Mkuranga)

na 1,200 (Kisarawe)!

Ama kweli hata mbuyu

ulianza kama mchicha!

Mambo sio mteremko!

Wana malengo!

“Tulipoanza tulikusudia kusadia

yatima na wanaoishi katika

mazingira hatarishi, wajane,

na waishio na VVU/Ukimwi”,

anasema Flaviana Mlaki, Mratibu

wa Watoto-JIMOWACO.

Mwananchi akifurahia msaada wa sare za

shule kutoka JIMOWACO

Pamoja na mafanikio makubwa waliyoyapata, Flaviana

anasema vikwazo pia vipo:

n Hawana uwezo wa kuwafikia watoto wote wanaohitaji

huduma yao kwani ni wengi sana katika jamii.

n Unyanyapaa nao bado upo na ni kikwazo kwa watu kujitokeza

kwenda kupima VVU.

n Licha ya elimu inayotolewa, maambukizi mapya bado

yanajitokeza kwa kasi kwani waliokuwa wagonjwa baada

ya kupata ahueni wanaendelea kuambukiza wengine.

n Baadhi ya watu wanapougua kutokana na Ukimwi wanaamini

wamerogwa, hivyo wanakwenda kwa waganga

wa kienyeji.

Wana ujumbe kwetu!

JIMOWACO wanaamini kwamba

hata wewe msomaji pamoja na watu

waliokuzunguka mnaweza kuanzisha

mkakati kama huu katika eneo lenu.

Siri ya mafanikio ni subira, kujiamini

na kupeana moyo!

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

23

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!