Haliuzwi - Femina HIP
Haliuzwi - Femina HIP Haliuzwi - Femina HIP
ISSN: 0856-8995 KATUNI: machi-aprili 2012 Si Mchezo! Haliuzwi MIKOPO imenitoa 1
- Page 2 and 3: Mimi na mamsapu hatutaki utani! Tun
- Page 4 and 5: STORI YANGU Mikopo imenitoa Naitwa
- Page 6 and 7: MAMBO MAPYA Unapofika Kimanzichana
- Page 8 and 9: 8 Si Mchezo! machi-aprili 2012 MAMB
- Page 10 and 11: HADITHI YA PICHA 10 ‘MKOPO WA NGO
- Page 12 and 13: 12 Mungu mkubwa! Japo nina kazi ya
- Page 14 and 15: JE, WAJUA? Kabla ya kukopa jipange!
- Page 16 and 17: TULICHOVUNA Tunajali VICOBA imetuli
- Page 18 and 19: CHEZASALAMA Huyu ndiye mwanamume wa
- Page 20 and 21: BURUDANI Wimbo: Vinapanda bei Msani
- Page 22 and 23: Minyoo bwana! Hahahahaaaa! Watu bwa
- Page 24 and 25: KATUNI upatu au hupati? Wanawake Mt
- Page 26 and 27: 26 Si Mchezo! machi-aprili 2012 Ama
- Page 28 and 29: SAUTI YANGU Si Mchezo! Femina HIP S
- Page 30 and 31: Mila katika kupambana na VVU Unyago
- Page 32: 32 Si Mchezo! machi-aprili 2012
ISSN: 0856-8995

KATUNI:

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

Haliuzwi

MIKOPO

imenitoa

1
Mimi na mamsapu

hatutaki utani!

Tunadunduliza vijisenti

vyetu taratiiibu.

Wenyewe tumejiwekea

malengo. Hata wewe

unaweza.

2 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Ndiyo,

Bamsapu anatunza

funguo, mie natunza

kibubu. Mpo? Zama

ndani ya toleo hili

ujifunze kuhusu vikundi

vya kuweka na kukopa

na hata upatu! Watu

wanafaidika bwana,

asikwambie mtu!

Si Mchezo! Huzalishwa na

kusambazwa.

Si Mchezo! husambazwa.

Lilikozalishwa toleo hili.
Femina

HIP

Mhariri

Majuka Ololkeri

Pendo Mashulano

Mwandishi

Ng’orongo Nyamoni

Washauri

Betty Liduke

Gaure Mdee

Raphael Nyoni

Mkurugenzi Mtendaji

Dr. Minou Fuglesang

Machapisho na Uzalishaji

Amabilis Batamula

Jiang Alipo

Katuni na Usanifu

BabaTau, Inc.

Mpiga Chapa

Jamana Printers Ltd

Shughuli za Nje

Constancia Mgimwa

Nashivai Mollel

Gloria Mkoloma

Christine Bisangwa

Rashid Kejo

Usambazaji

EAM Logistic Ltd

Femina HIP na Washirika

Si Mchezo! limefanyika kwa hisani

kubwa ya Serikali za Sweden (Sida),

Denmark (DANIDA) na Marekani

kupitia USAID kama sehemu ya

ufadhili wa PEPFAR kwa shirika la

FHI360 mradi wa UJANA, PSI mradi

wa HUSIKA pamoja na HIVOS. Toleo

hili limefanyika kwa ushirikiano na

JHU-CCP/TCCP na RFSU.

Yaliyomo humu ndani ni jukumu la

Femina HIP na hayawakilishi maoni

au mitazamo ya wafadhili.

Wasiliana nasi kwa:

S.L.P. 2065, Dar es Salaam

Simu: (22) 212 8265, 2126851/2

Fax: (22) 2110842

email: simchezo@feminahip.or.tz

Si Mchezo! huchapishwa na

Femina HIP.

Sms: 0715 568222

YALIYOMO

4 Stori Yangu: Mikopo imenitoa

6 Mambo mapya:

8 Mambo ya Fedha: Zijue Vicoba

10 Hadithi ya Picha: Mkopo wa ngoma!

14 Je, Wajua: Kabla ya kukopa jipange

16 Tulichovuna: Tunajali Vicoba imetulia!

18 Chezasalama: Mwanamume wa ukweli...

20 Burudani: Vinapanda bei

22 Pasipo na Daktari: Minyoo bwana!

23 Huduma: Walianza kama utani

24 Katuni: Upatu unapogeuka Hupati!

27 Ukweli wa Mambo: Yanawakuta wengi

30 Ujana: Mila katika kupambana na VVU

31 Ushauri

TAHARIRI

Mamboz? Najua umeitikia pouwaaaa! Katika ‘kulipika’ toleo

hili la 59, tuliwazukia wakazi wa Mkuranga. Ingawa tuliweka

kambi wilayani, mishemishe zetu zilikuwa Kimanzichana na

kwingineko vijijini. Tulikula nao stori kibao kuhusu mambo ya

fedha, vikundi vya kuweka na kukopa, hususan SACCOS na

VICOBA. Hatukusahau hata ule ‘mchezo’ wetu maarufu, UPATU!

Nakuacha uzame ndani, nisikuharibie utamu. Kila la kheri!

Pendo

Tuanzie

buku mbili

Ndo

naandika

hivyo..!

“Mmh! sasa

umaskini

baibai”

machi-aprili 2012 Si Si Mchezo!

3
STORI YANGU

Mikopo imenitoa

Naitwa Juma Kapute aka

Chaudele, jina ambalo kwa

Kizaramo linamaanisha

kitindamimba. Kimanzichana

ndo makazi yangu ingawa

asili yangu ni Mngindo kutoka Lindi.

Baada ya kuhitimu elimu ya msingi niliajiriwa

katika mgahawa ambako nilipiga mzigo kwa

miaka minne. Wakati huo nilikuwa nikitunza

kiasi fulani cha mshiko katika mshahara wangu

kila mwezi, hivyo nikawa nimedunduliza hadi

Sh 140,000.

Niliacha kazi na nikaitumia fedha hiyo

kufungua mgahawa wangu na kwa kuwa kwa

mapishi niko juu, pale mgahawani nilikuwa

nikipiga mzigo mwenyewe, ingawa kwa sasa

nasaidiana na mke wangu kwani tuna miradi

mingine kibao.

Niliendesha ‘kijiwe’ hicho huku nikiweka

kiasi fulani cha faida benki, niliamua kujenga

nyumba na kununua samani lakini nikawa na

ndoto ya kupanua biashara.

Wakaja watu wa FINCA ambao walikuwa

wanatoa mikopo kwa wanawake, hivyo mke

wangu alichangamkia mkopo ili afanye biashara

ndogondogo. Kwa kuwa hatukuwa tumejipanga

fresh tulishindwa kurejesha. Ilifika wakati

wakaja kutunyang’anya vitu vyote ndani, hivyo

ikabidi nitumie akiba ya benki kuokoa jahazi.

4 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Ila sikukata tamaa, nilijiunga na Kasi Mpya

SACCOS ili niendelee kufukuzia ndoto

zangu. Nikalipa kiingilio kutokana na faida

niliyokuwa nimeipata tena mgahawani

baada ya sakata la FINCA, nikawa nanunua

hisa kila mwezi hadi ikatimia Sh 70,000.

Nikawa na uwezo wa kukopa sh 300,000

ambazo nilizitumia kununulia mbao na

kuziuza. Nikawa narejesha Sh 50,000 kila

mwezi hadi nilipomaliza deni. Nilikuwa na

mpango wa kukopa tena lakini ikatokea

songombingo, SACCOS ikafa na viongozi

wakasepa na mkwanja wote! Imebaki stori!

Baadaye walikuja watu wa VICOBA,

wakatuhamasisha nami nikachangamkia

fursa kama kawa. Tuliunda kundi la watu
30, tukachanga pesa ikafikia Sh

105,000 na kila mmoja akanunua

hisa kwa kadri awezavyo kwani

aliyenunua hisa nyingi alikuwa

na uwezo wa kukopa pesa nyingi

pia.

Wanasema ng’ombe wa maskini

hazai na hata akizaa huzaa

dume! Hawa nao baadaye

walisepa na pesa za wanachama

na hadi leo kesi iko mahakamani.

Hapa napo nilikula hasara ya Sh

52,000 hivi. Sikuchoka!

Baadaye ilianzishwa SACCOS

inaitwa Belita nikalipa kiingilio na michango

nikawa mwanachama. Nilianza na mkopo wa

Sh 50,000, nikaendelea kupanda na hivi majuzi

nimekopa milioni nne. Narejesha bila tabu kwa

kuwa nimewekeza fedha hizo katika biashara.

Naishukuru mikopo maana imepanua biashara

zangu, hivi sasa namiliki mkokoteni, baiskeli

kumi, bajaj na nina mpango wa kuanza kujenga

nyumba nyingine ya ukweli!

Mkokoteni na baiskeli nakodisha, bajaj pia

inakodishwa kubeba mazao na wagonjwa

na nimepata tenda ya kusafirisha wanafunzi.

Vyote hivi vinalipa kichizi!

Mingo zote hizo zinaniwezesha kurejesha

mkopo na kusomesha watoto wangu watatu

na pesa ya kubadilisha

mboga hainipigi chenga.

Akaunti yangu ya benki

nayo naendelea kuitunisha

kwa faida inayobaki baada

ya kutoa marejesho na

matumizi.

Nitaendelea kukopa,

kuwekeza na kurejesha

kwani mikopo ndiyo

iliyonifikisha hapa. Cha

muhimu ni malengo,

nidhamu katika matumizi

na marejesho na pia

kujiwekea akiba benki.

Nasema tena, NITAKOPA

MPAKA KIELEWEKE!

machi-aprili 2012 2012 Si Si Mchezo!

5 5
MAMBO MAPYA

Unapofika Kimanzichana

ukiulizia watu maarufu

eneo lile wa kwanza

kutajwa ni msanii 20%!

Nasi tukasema si vibaya

‘tukimpaisha’ kwa staili ya

pekee, tukatinga nyumbani

kwao japo kupata picha na

familia yake! Unamuona

mrembo Jema? (wa kwanza

kulia). Huyo ni mtoto wa

20% na aliyeshika majarida

ni mama mzazi wa msanii

20%.

Madogo hawa wanapiga bonge la ‘kolabo’ kulishambulia jukwaa!

Ilikuwa ni katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar huko Mkuranga

ambapo mtoto Ramadhani Kasimu (aliyeshika ‘mic’) alikonga

nyoyo za umati na wimbo “Naenda kusema kwa mama” wa msanii

Asley. Huyo dogo mwingine pichani ni Jaffery A. Jaffery, alikwenda

kutunza akanogewa akabaki uwanjani kumpiga tafu mwenzake!

Naye alitunzwa ‘mshiko’ wa uhakika!

6 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Kibubu bwana!

Hahaha!

Hiki kinaitwa kibubu. Inawezekana

kili’batizwa’ jina hilo kwakuwa ‘hakisemi’,

yaani hakionyeshi kilichomo

ndani yake! Kibubu ni benki kiaina!

Kinunue au kichongeshe uwe nacho

nyumbani, ‘tupia’ humo fedha ndogondogo

kila siku, jiti, bati, jero, buku

na hata msimbazi kadri unavyozisaka.

Baada ya mwaka au muda fulani uliojipangia,

kivunje na utaona maajabu!

Watu wamenunua mashamba kwa

vibubu!
VICOBA, SACCOS

wana mengi ya ziada

Uzuri wa vikundi vya kuweka na kukopa

ni zaidi ya ule tunaoweza kuufikiria kwa

haraka. Kitendo cha kuwa pamoja kinawapa

nafasi ya kufanya mambo mengi mengine

yenye faida kwao binafsi na hata kwa jamii

zinazowazunguka. Tumevitembelea sana

vikundi hivi na tumejionea kwamba baadhi

yao wanapokutana kwa shughuli zao

za msingi, wanatumia mkusanyiko huo pia

kupata elimu ya afya. Mashirika mbalimbali

pia hutoa elimu ya mambo tofauti kwa

vikundi hivi kwani si rahisi kuitoa kwa mtu

mmojammoja. Hakuna anayeweza kubisha

kwamba kuwa pamoja kuna faida lukuki.

Cheza kwa stepu na kutumia nguvu kama

Makhirikhiri ndio staili yake. Si mchezo! Jamaa

naye ‘aliwabamba vya kutosha’ wananchi wa

Mwalusembe kwa staili za kuvutia.

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

7
8 Si Mchezo! machi-aprili 2012

MAMBO YA FEDHA

Vijue Vicoba

Inawezekana wewe na jirani zako mnatamani kuanzisha chama cha kuweka na kukopa lakini hamjui

hata pa kuanzia! Aliadina Peter Rwezaula, Afisa Maendeleo Mwandamizi wa Wilaya ya Mkuranga

anatupiga ‘darasa’ kidogo kuhusu hili:

“Vyama vya kuweka na kukopa viko vya aina nyingi ila maarufu zaidi ni Vicoba na Saccos. Taratibu zake

hazitofautiani sana lakini kwa leo tutajikita katika Vicoba tu. Twende pamoja!

VICOBA ni nini?

Ni kifupi cha maneno ya kimombo, Village

Community Bank, au kwa ‘kibantu’ chetu

tunaweza kusema ‘Benki’ ya Wanakijiji.

Jinsi ya kuanzisha Vicoba

t Mnatakiwa kuwa kikundi cha watu kuanzia

15 hadi 30.

t Siku ya kwanza ya kukutana mnaweza kumualika

Afisa Ushirika au Afisa Maendeleo

ya Jamii ili kupata maelekezo zaidi.

t Mtengeneze katiba (ni vizuri mpate

msaada wa mtaalamu)

t Wakati wa kutengeneza katiba mtakubaliana

kuhusu kiingilio (ambacho hutolewa

mara moja na hakirudishwi), thamani ya

hisa, jinsi ya kununua n.k.

t Chagueni viongozi wa muda (mtabadilisha

viongozi kufuatana na katiba yenu)

J

Vinaendeshwaje?

n Wanachama wanatakiwa wawe wananunua

hisa lakini lazima kuwe na

ukomo wa hisa anazoweza kumiliki

mtu mmoja.

n Kikundi kikutane angalau mara moja

kwa wiki.

n Ndani ya kikundi cha Vicoba inabidi

muwe na vikundi vya watu watano

watano ili kuwekeana udhamini wakati

wa kukopa

n Ni muhimu kuwa na mfuko wa jamii ili

kusaidiana wakati wa matatizo kama

misiba na mikopo ya dharura isiyo na

riba

n Kikundi cha Vikoba kiwe na sanduku

la kuhifadhia fedha na washika funguo

watatu kwa kufuli tatu.

n Kila kikao wanachama wapewe taarifa

ya akiba, mapato na matumizi.

n Kikundi kikikua itabidi kiwe na akaunti

benki ili kutunza fedha

Kumbuka

Ni kinyume cha sheria kwa

mwanachama mmoja kumiliki

zaidi ya moja ya tano ya hisa za

chama na hairuhusiwi mtu kuwa

mwanachama wa Vicoba mbili.
NGUVU ZA MWANAUME

Jogoo halipandi mtungi?

Ili watoto wasielewe wakubwa hupenda kusema ‘jogoo

halipandi mtungi’! Hili ni tatizo la uume kutokusimama au

Kiswahili sanifu, uhanithi. Watu wenye tatizo hili huchekwa

na hivyo kufanya washindwe kutafuta ushauri wa kitaalamu.

Kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi ya afya

ya uzazi.

Tuliteta na Dk Constantine Kibela na Dk Lugano Kiswaga wa

Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kuhusu hili kwani tumekuwa

tukipokea maswali lukuki ya wasomaji.

Kulikoni jogoo kushindwa?

“Hili ni tatizo ambalo mtu anaweza kuzaliwa nalo au

kulipata katika kipindi chochote cha maisha yake.

Linaweza kuwa la kudumu au la muda tu,” anasema

Dk Constantine. Kumekuwa na uzushi kwamba kitovu

cha mtoto kikiangukia kwenye uume mtoto atakuwa

hanithi, jambo ambalo si kweli.

Sababu za uhanithi:

n Karibu 60% ya watu wenye tatizo hili hutokana na

sababu za kisaikolojia, umri, matatizo ya kimazingira

mfano: msongo wa mawazo kutokana na kukosa

kazi, fedha, matatizo ya kifamilia, hofu ya kuambukizwa

magonjwa, hofu ya kutumia kondom nk

n Magonjwa sugu katika mwili, kwa mfano, ugonjwa

wa ini, figo, kisukari, kifua kikuu nk

n Matumizi yaliyokithiri ya dawa za kulevya au

pombe

n Vyakula tunavyokula vinaweza kusababisha uhanithi,

kwani mrundikano wa mafuta katika mishipa

ya damu unasababisha damu kushindwa kufika

vizuri katika uume ili kuuwezesha kusimama.

Tatizo hili halipaswi kuwa la mwanamume

tu bali mwanamke anao

uwezo wa kumsaidia mwenzi

wake katika kutafuta ushauri na

hata kumsaidia kuondoa hofu

aliyonayo.

Je, tatizo hili

linatibika?

Kitu muhimu ni kutambua

chanzo cha tatizo lenyewe

na kujitokeza kupata ushauri.

Wanaume wengi wanashindwa

kutafuta ushauri juu ya suala

kama hili kwa kuona haya eti

“mwanaume mzima ijulikane

mi hanithi!” Wengine hufikia

hatua ya kuigiza kama wana

uhusiano wa kujamiiana

ilimradi tu waonekane rijali.

Kwa hisani ya TMEP,

Mradi unaodhaminiwa na RFSU

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

9
HADITHI YA PICHA

10

‘MKOPO WA NGOMA!’

Mama Mwajei amejaliwa mtoto mmoja

tu, hivyo anamlea kama mboni

ya jicho! Siku ya siku imewadia,

Mwajei kavunja ungo. Ndiyo! Kawa mkubwa

sasa. Kawekwa ndani mwezi, sasa ni wakati wa

kumtoa, wenyewe wanasema ‘kumkogesha maji’.

Amepania kumfanyia bonge la sherehe, tatizo

mshiko. Anafanyaje? Nini kinatokea? Fuatilia….

Imeigizwa na Kimanzichana Vijana Troupe”

Duh! Namie mwezi

ujao nakamata kitita

Sema usemavyo

lakini hapa ngoma

itachezeka na

pombe zitanyweka

mpaka kieleweke

Si Mchezo! machi-aprili 2012

Hongera sana.

Laki tano hiyo,

hesabu

Asante sana

Naona hukataziki,

sasa mie simo na

utakuja kujuta

Mama Mwajei ndo

keshaamua, kila mtu

anamshangaa

Ama kweli

tamaa mbele

mauti nyuma!

Si pale Kibisa Saccos mume

wangu? Mikopo nje nje…

Una akili sana

waifu, kachukue

tufanye biashara

Mungu anipe

nini mimi!

Shughuli ya

Mwajuma

itaacha

historia

Alhamis mwamu, Ijumaa mbiga,

Jmosi mkole, usiku wake rusharoho,

Jpili mwali anatoka. Upo?

Haya jirani, asante kwa

mwaliko, tuko pamoja
Shost, mie nikipata tu

mkopo namtoa mwanangu.

Mzee nshamweka sawa

Niliyopewa haitoshi kwa

biashara. Mie naona

tuitumie kumtoa mwajuma

Chonde chonde!

Itakutokea puani

hiyo! Tena mie

simo kabisaaa!

He! Mumeo kakubali?

Yaani mkopo

umcheze mtoto?

Maspika fanya manne

kama hili. Sitaki

muziki wa kitoto

Usitie shaka,

hapa umefika

Hajakubali shost,

nimemwongopea

wa biashara

Mmh! Hii akili au matope? Umcheze

mtoto kwa mkopo? Utaulipaje?

Ulisema ya biashara,

leo unaniambia ya

ngoma! Sitaki kusikia

Mimi ndo

niliyesaini

na mimi ndo

nitadaiwa

na ndo

nshaamua

Ndo ushakuwa mkubwa, nakupatia

ushanga mweupe na mwekundu,

nitakueleza kazi zake…

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

11
12

Mungu mkubwa!

Japo nina kazi

ya kufagia lakini

nimeacha historia

Jamani, si

mnisikilize

kwanza?

Huu mweupe unavaa

ukiwa vizuri, yaani

kama hauko hedhi…

Hatujaja kwa

mazungumzo. Lete

chetu, vinginevyo

tunazama ndani

Si Mchezo! machi-aprili 2012

Leleleleleleeleleeeeeeeee

Yeleleleleleleleee

TAREHE YA MAREJESHO INANUKIA…

Yaani Mwinyi, wewe wa

kukataa kunikopesha

elfu hamsini jamani!

Aaaah, mkuki kwa

nguruwe eenh? Wewe

mbona nikikuomba

‘vitu’ unabana?

Jamaniii, mume wangu

nitamwambia nini mie

Ona sasa, ndo

tushaaibika

Halohalooooooooooo

Maji ndo yamefika

shingoni, anasaga vumbi

kusaka marejesho

Tupishe hukoooo

Hivi angekufuata

wewe msomaji

katika hatua hii

ungemshauri nini?
Anafurahi

lakini mwisho

wake utakuwa

ni majonzi

Mama Mwajei

katimiza ndoto

yake. Tuendelee!

MAMBO YANAZIDI KUWA MAGUMU…

Nipe thelathini

kwa vyote

Mmmh! Anauza bei

ya kutupa! Sijui ana

shida gani!

Hii aibu tupu!

Mwarabu

mie leo

nimeaibika

mtaani!

Nitafanya nini

mie! Najuta

kutokumsikiliza

mume wangu!

Nema

Mwajuma

nemaaaaaa

Kapendezaaaaaa

Fyokofyoko,

unalia nini sasa,

si nilikwambia!

Jamani mwali

wetu kapendeza

hajapendezaaaaaa?

SIKU YA SIKU IMEWADIA…

Ana vitu

chungu mzima,

tukavibebe tu

tuvinadi

Ndiyo, haiwezekani

mkopo achukue

yeye, tulipe sie

Nisamehe mume

wangu, niko chini

ya miguu yako…

Hivi saa hizi ni usiku

au mchana…?

Mi mgeni mji

huu, sijui

Duh! Muziki wa ukweli,

hajaleta nyenze.

Twendeni jamani,

hakuna kumlegezea

Kama hukujifunza

kwa kisa cha Mama

Mwajei hujifunzi tena!

Ni makosa kutumia

mkopo kwa jambo

ambalo halizalishi.

machi-aprili 2012 Si Mchezo! 13
JE, WAJUA?

Kabla ya kukopa jipange!

Wa kucheka mmecheka, wa kusonya mmesonya,

wa kugomba mmegomba, wa kubishana mmebishana

lakini ukweli unabaki palepale kwamba hapa

Mama Mwajei alichemka!

Hebu tusemezane kidogo: hivi, inakuwaje unakubali furaha

ya siku mbili-tatu ikusababishie majuto kwa miaka? Wapo

waliochukua mkopo, wakafurahia jinsi mifuko ilivyoota ‘vijipu’

ghafla, breki ya kwanza ikawa kilabuni ‘kujenga heshima’!

Wapo pia waliochukua mkopo kwa ajili ya kujipatia ‘jiko’ jipya!

Hawa nao tuwape pole!

Katika sakata la Mama Mwajei tunaweza kuwalaumu na kuwachukia

wanakikundi wenzake kwa kitendo cha kwenda

‘kusafisha’ nyumba ya mwenzao, lakini ilikuwa ni haki kwao

kufanya hivyo kwani vinginevyo lingegeuka kuwa ‘zengwe’ lao

na wangepaswa kulipa fedha hiyo kwani wao ndio waliokuwa

wadhamini wake.

Nema

Mwajuma

nemaaaaaa

Kapendezaaaaaa

14 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Jamani mwali

wetu kapendeza

hajapendezaaaaaa?

Ukweli ni huu

Jamani, si

mnisikilize

kwanza?

Mikopo si kitu kibaya na wala

hatuna sababu ya kuiogopa kwani

wapo wenzetu waliochukua

mikopo wakawekeza katika

biashara, wakajikwamua kiuchumi

kama tulivyoona katika stori

ya Juma Kaputi kwenye kurasa

za Stori Yangu. Cha muhimu ni

kujipanga na kuwa na malengo

yenye tija.
Hatujaja kwa

mazungumzo. Lete

chetu, vinginevyo

tunazama ndani

Tufanyeje?

Ufahamu

n Fanya utafiti na uwe na ufahamu mzuri wa mradi

unaotaka kuufanya kabla ya kuchukua mkopo

n Ni muhimu kufungua akaunti benki ili uziweke fedha

mara tu baada ya kuzipata kwa usalama wa fedha hizo

na pia kuepuka kuwa nazo mfukoni au nyumbani ili

usishawishike kuzitumia kwa mambo ambayo siyo

uliyoyakusudia

n Usimwamini kila mtu kwa ushauri kuhusu matumizi ya

fedha kwani baadhi ya marafiki wanaweza kukushauri

vibaya kwa kuwa ama wanafaidika na ‘matanuzi’

utakayoyafanya au wangependa kukuona ukiumbuka.

Mkopo, kama lilivyo jina lake, ni

fedha ambayo utatakiwa kuirejesha.

Katika vyama vya ushirika, kama

SACCOS, VICOBA na hata katika taasisi

nyingine za fedha, mkopo wowote

utakaouchukua unapaswa kuurejesha

ukiwa na kiasi fulani cha riba, hata kama

utaurejesha baada ya wiki moja tu.

Ili uweze kurejesha mkopo huo pamoja

na riba ni lazima fedha hiyo iwekezwe

katika mradi ambao utairuhusu ‘kutuna’

ili hata utakapokuwa umeirejesha, kiasi

fulani cha faida kibaki kwako kuendeleza

huo mradi uliouanzisha.

Unaporejesha fedha ya mkopo unatoa

fursa kwa wenzako pia kuweza

kukopeshwa na hatimaye watu wengi

zaidi watajikwamua kutoka katika

umaskini.

Kumbuka

J Usichukue mkopo bila

mipango mizuri ya kuwekeza

fedha hiyo

SWALI:

Nini kinasababisha

baadhi ya watu kujikuta

‘wakitumbua’ fedha ya

mkopo?

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

15
TULICHOVUNA

Tunajali VICOBA imetulia

n Wakati wakisubiri wenzao kwa kikao, nasi

‘tukawatwanga’ Si Mchezo! wapate ujumbe’

“likuwa ni Jumatatu tuliiivu majira ya mchana.

Kama tulivyokuwa tumekubaliana, mtu

mmoja baada ya mwingine aliwasili katika kivuli

cha mwembe na hatimaye tukajikuta tumetimia

20. Penye wengi hapaharibiki neno, mmoja

wetu alijitolea kuwa kiongozi wa muda, akatuongoza

katika kuanzisha kikundi chetu”.

Hivi ndivyo ilivyoazishwa Tunajali VICOBA, kikundi

cha kuweka na kukopa cha wanakijiji wa Mwanambaya,

Mkuranga. Kikundi hiki kilianzishwa Juni 28,

2003 na hadi sasa kina wanachama 31, kama anavyosimulia

Katibu wa kikundi hicho, Moshi Mfaume

Manda.

Enhe, mkutano uliendaje?

Huo ulikuwa ni mkutano wetu wa kwanza.

Alikuwepo Afisa Maendeleo wa Kata kushuhudia

kinachoendelea. Tulijiundia katiba,

kisha tukafanya uchaguzi wa viongozi. Tunao

viongozi wanane, Mwenyekiti, Katibu,

Mtunza Hazina, wahesabu fedha wawili na

watunza funguo watatu.

16 Si Mchezo! machi-aprili 2012

n Kama kawa, wana sukari, sabuni ya maji

(kwenye kidumu), midamida ikifika watauziana

Mnapokutana mnafanya nini?

Kila Alhamisi saa nane mchana tunakutana:

l Mwenyekiti anafungua mkutano

l Wanaodaiwa sabuni na sukari wanalipa

madeni (ni mradi wa kikundi)

l Tunachangia Mfuko wa Jamii (kila mwanachama

anachangia sh 1,000 kwa mwezi)

l Tunanunua hisa, yaani akiba (fedha) mtu

anayoamua kuweka (bei ya hisa ni sh 500

na mtu anaweza kununua hadi hisa 5 kwa

wakati mmoja)

l Waliokopeshwa fedha wanarejesha

l Tunasoma barua za maombi ya mikopo

(kama zipo)

l Tunawakopesha wale ambao maombi yao

yamepitishwa na kikundi

l Tunauziana sukari na sabuni (kwa

mkopo)

l Katibu anasoma taarifa ya mapato na

matumizi

l Mwenyekiti anafunga kikao
n Mida ya hisa ilipofika, kila

mwanachama alinunua kadri ya

uwezo wake

Wanachama

wanakopaje?

z Anajaza fomu (tunazo)

z Inasainiwa na wadhamini

wawili ambao lazima wawe ni

wanachama wa kikundi

z Maombi yatasomwa mbele ya

wanakikundi wote tunapokutana

na yatajadiliwa

z Ikipitishwa anakopeshwa, na

kiwango cha juu ni mara tatu

ya hisa alizonazo.

z Anatakiwa kuanza kurejesha

baada ya mwezi mmoja na

katika miezi mitatu lazima awe

amemaliza

z Tunatoza riba ya asilimia 10 ya

mkopo

z Anayeshindwa kulipa tunachukua

hisa zake zote pamoja

na za wadhamini wake

n Wanauziana sukari ili kutunisha mfuko.

Ni kwa mkopo na wiki ijayo kila mmoja

atapaswa kulipa!

Mna vyanzo vingine vya mapato?

n Tuna shamba la kikundi ambapo tunalima mihogo,

matunda na mboga

n Tuna mfuko wa jamii ambao tunachangia wenyewe

kwa ajili ya kusaidia wenye matatizo na kugharamia

shughuli za kikundi

n Tunanunua sukari kwa jumla na kuuziana kwa rejareja

n Tumepata mafunzo ya kutengeneza sabuni, hivyo

tunatengeneza na kuuziana

n Wachelewaji katika vikao tunawatoza faini ya sh 500,

ili kutunisha mfuko

Ujumbe?

n Kikao kimefungwa, Mwenyekiti, Dora

Danda na Katibu wake Moshi M. Manda

wanaweka kumbukumbu sawa.

Ndiyo. Vikundi vya kuweka na kukopa ni vizuri. Tumeshuhudia

wanachama wenzetu wakianzisha biashara na hata kujenga

nyumba za kisasa kwa kuweka na kukopa. Nanyi pia mnaweza

kuanzisha!

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

17
CHEZASALAMA

Huyu ndiye mwanamume wa ukweli

Edna anakonda kwa mawazo! Ana mtoto wa

mchanga na angependa kusubiri japo kwa

miaka mitatu kabla ya kuzaa mtoto mwingine.

Hajui la kufanya. Amesikia stori nyingi za

kutisha kutoka kwa ‘mashosti’ wake kuhusu njia

za kisasa za uzazi wa mpango, hivyo anaogopa

kuzitumia!

Frank, mumewe Edna, yeye ana mtazamo tofauti.

Amewahi kusoma kijitabu kinachoelezea vizuri

njia za uzazi wa mpango na anafahamu kwamba

stori alizozisikia mkewe hazina ukweli wowote.

18 Si Mchezo! machi-aprili 2012

“Twende kliniki mpenzi wangu. Tutapata maelezo

yote na hofu yako itaondoka. Tutachagua njia inayotufaa

na tutafurahia mapenzi yetu bila hofu,”

Frank anamshawishi Edna na taratiibu wanambeba

mtoto wao Alice na kuongozana kuelekea

kliniki.

Frank ni mwanamume wa kipekee mno! Anajali,

anamhurumia mkewe na anaona umuhimu wa

kutumia njia za uzazi wa mpango kwa faida yake

mwenyewe, mkewe na hata watoto. Si mbabe, ni

msikivu. Huyu ndiye mwanamume wa ukweli!
Faida za kutumia njia

za uzazi wa mpango

Kupanga uzazi kuna faida

nyingi kwa mama, baba, watoto

na familia kwa ujumla

Kwa mama:

n Itamsaidia kurejesha afya

baada ya kujifungua

n Inampa nafasi ya kutosha

ya kuonyesha mapenzi kwa

watoto na kwa mumewe

n Inampa mama nafasi ya

kuhudumia familia na

kufanya shughuli za maendeleo

Kwa watoto:

t Mama mwenye

afya huzaa watoto

wenye afya

t Watapata mapenzi

na huduma

ya wazazi kwa

ukamilifu

Kwa baba:

n Anapunguza mzigo wa jukumu

la kuihudumia familia

n Inamsaidia kumudu mahitaji

ya familia (elimu, chakula,

malazi na mengineyo)

n Inampa nafasi ya kutosha

ya kuonyesha mapenzi kwa

watoto na kwa mkewe

n Anapata muda wa kuhudumia

familia na kufanya

shughuli za maendeleo

Chukua hatua!

n Panga pamoja na mpenzi wako,

amueni lini mnataka kuzaa, watoto

wangapi na wapishane kwa umri

gani

n Kwa ushauri wa mtaalam, kubalianeni

njia ya uzazi wa mpango

ambayo inawafaa.

Ni haki na wajibu wa mwanamume

kushiriki katika

kupanga uzazi. Familia bora

hujengwa na mwanamume

na mwanamke pamoja

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

19
BURUDANI

Wimbo: Vinapanda bei

Msanii: Blad Key

Naamka asubuhi ee,

jikoni kwangu kumelala

paka

Namfata mke wangu ee,

amenuna eti anadai talaka

Hataki tuongee,

amenuna eti anataka

kuondoka

Anarudi kiijini,

maisha ya dhiki yeye

amechoka x2

Mie nitafanya nini, na

mfukoni sina hata senti

Kipato changu cha chini,

madukani vitu vinapanda

bei x2

We mama weee!!

Kiitikio

Vinapanda bei,

Kila siku vitu vinapanda

bei,we mama wee.

Vinapanda bei,

Kila siku vitu vinapanda bei

anyokiee.

20 Si Mchezo! machi-aprili 2012

20 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Huu neneee

Nimechelewa kazini, kwa

sababu nauli iko juu

Kutokana na hali duni,

ikabidi nako niende kwa

miguu

Ile nafika kazini, bosi nae

anakuja juu

Anaanza nifokea, hali

iliyofanya nibaki roho juu

Mie nitafanya nini kipato

changu hakikidhi mahitaji

Hali ya maisha ni ngumu

kila siku vitu vinapanda bei

x2

We mama weee!!

Kiitikio

Kibwagizo

We we we we wee

We mama we we we, we

mama. x3
Baunsa noma!

Mshikaji alienda kuiba kwa baunsa. Wakati J

anatoka tu, ghafla akakutana nae. Baunsa

akachukua vile vitu na kuvirudisha ndani

halafu akamshika mkono kama ‘mwana’ vile

na wakaanza kutembea. Mshikaji akajua labda

anapelekwa polisi. Kufika kituo cha polisi

cha kwanza wakapita, cha pili wakapita tena

mmh! Mshikaji akaingiwa na hofu kufika kituo

cha tatu baunsa akawa anapita tena, mshikaji

akamuona afande nje akapiga kelele ‘‘afandee

mimi mwiziii’’

Toto nidhamu sifuri

Mtoto: Baba niletee glasi ya maji!

Baba:: We mtoto una kichaa nini? kachukue

mwenyewe!

Mtoto: Bwana niletee!

Baba: Usinisumbue, ntakuja kukupiga makofi!

Mtoto: Basi ukija kunipiga makofi njoo na glasi

ya maji

J

Hajatulia!

Siku moja, mama

mwenye nyumba alikuwa

akimuuliza msichana wake

wa kazi kuhusu kuisha

haraka kwa vijiti vya

kuchokonoa meno.

Mama:

Hizi “toothpicks” mbona

zimeisha haraka?

Dada wa kazi:

Mimi mwenyewe sijui

labda uwaulize watoto

wako, mimi huwa

nikimaliza kutumia tu,

nazirudisha kwenye kopo

lake!

Mama: Haaaa!!??

J

Yataka moyo kuwa dokta….

Mgonjwa:

Dokta mimi nina tatizo la kusahau, yaani

nikisema neno au ukiniambia hapo hapo

nasahau kabisa.

Dokta: Tatizo lako limekuanza lini?

Mgonjwa: Tatizo gani tena?

Dokta: ???**$!!!

J

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

21
Minyoo bwana!

Hahahahaaaa! Watu bwana! Bila shaka umewahi

kusikia mtu akisema eti binadamu lazima

awe na minyoo! Eti minyoo ina kazi ya kulainisha

chakula katika tumbo la binadamu!

Dokta Lugano Kiswaga wa Hospitali ya

Wilaya ya Mkuranga anasema huo ni uongo

mtupu!

“Minyoo iko ya aina nyingi na hakuna aina

yoyote ya minyoo yenye faida katika mwili

wa binadamu, ila huingia katika mwili wa binadamu

au mnyama kwani ndiyo mazingira

yanayoiwezesha kuzaliana,” anasema.

Mh! Inaingiaje?

“Kuna njia nyingi za kuingia ila kubwa ni

kupitia chakula kisichosafishwa vizuri,

nyingine ni kujipenyeza katika matundu

madogomadogo ya ngozi ya mwanadamu,”

anasema.

“Ukila chochote bila kunawa mikono vizuri

kwa sabuni na maji safi, unaweza kuingiza

minyoo tumboni. Usipoosha vizuri matunda

na mboga za majani zinazoliwa zikiwa

mbichi, mfano kabichi, karoti, nyanya nk,

unaweza kula minyoo”, anasema.

“Minyoo inapopenya katika matundu ya

ngozi, inakwenda katika mishipa ya damu,

kisha kwenye moyo, halafu kwenye mapafu

na hatimaye unaikohoa inaingia katika

utumbo. Inapofika humo huweka makazi,

ikakua, ikataga mayai, kisha ukayatoa mayai

hayo kupitia haja kubwa, yanaanguliwa

nje ya tumbo la binadamu na mzunguko

hujirudia kama kawaida”, anasema.

22 Si Mchezo! machi-aprili 2012

PASIPO NA DAKTARI

Utajuaje kama una minyoo?

n Unaweza kuiona katika kinyesi

n Kukohoa

n Inatoboa utumbo, hivyo unaweza kuona

damu kidogo katika kinyesi

n Kuwashwa sana usiku sehemu ya haja kubwa

(hasa kwa watoto)

n Kukonda

n Kukosa hamu ya kula

n Upungufu wa damu

n Ngozi kupauka

n Ukuaji hafifu (kudumaa – hasa kwa watoto)

Chonde chonde!

Ukiona dalili hizi au hata baadhi yake, kamwone

mtaalam wa afya kwa vipimo na ushauri kwani

linaweza kuwa ni tatizo la minyoo, ambalo

linaweza kuleta athari kubwa kwa binadamu,

ikiwamo upungufu mkubwa

wa damu na hata

kifo! Usimeze dawa za

minyoo bila ushauri wa

daktari. J

Kumbuka

Zingatia usafi

kujiepusha na

magonjwa
HUDUMA

Walianza kama utani!

Siku moja wanawake 30 walikaa kikao ‘wakateta’

jambo. Walichoka kuona jinsi janga la Ukimwi lilivyokuwa

likienea kwa kasi katika jamii. Waliunda

kikundi chao ‘wakakibatiza’ jina la JIMOWACO, yaani

Jipeni Moyo Women and Community Organisation,

kikundi ambacho leo hii ni gumzo kubwa Kisarawe na

Mkuranga.

Hawa, ni wanawake ambao waume zao walikuwa wakifanya

kazi katika mgodi wa chokaa huko Kisarawe na hiyo

ilikuwa ni mwaka 2003. Walichangishana pesa, wapo walioomba

kwa waume zao, wapo waliovunja ‘vibubu’ vyao,

ili mradi wazo lao lifanikiwe!

Wako mbali!

Leo hii JIMOWACO imesimama!

Imeajiri wafanyakazi

12 na tayari imefungua

tawi wilayani Mkuranga,

imeanzisha vikundi 20 vya

kuweka na kukopa katika

jamii, vikiwa na mchanganyiko

wa watu waishio na

VVU na wasio navyo. Wanatoa

mahitaji ya shule na

huduma za afya kwa watoto

wapatao 7,093 na wanatoa

huduma kwa watu

waishio na VVU/Ukimwi

wapatao 1,913 (Mkuranga)

na 1,200 (Kisarawe)!

Ama kweli hata mbuyu

ulianza kama mchicha!

Mambo sio mteremko!

Wana malengo!

“Tulipoanza tulikusudia kusadia

yatima na wanaoishi katika

mazingira hatarishi, wajane,

na waishio na VVU/Ukimwi”,

anasema Flaviana Mlaki, Mratibu

wa Watoto-JIMOWACO.

Mwananchi akifurahia msaada wa sare za

shule kutoka JIMOWACO

Pamoja na mafanikio makubwa waliyoyapata, Flaviana

anasema vikwazo pia vipo:

n Hawana uwezo wa kuwafikia watoto wote wanaohitaji

huduma yao kwani ni wengi sana katika jamii.

n Unyanyapaa nao bado upo na ni kikwazo kwa watu kujitokeza

kwenda kupima VVU.

n Licha ya elimu inayotolewa, maambukizi mapya bado

yanajitokeza kwa kasi kwani waliokuwa wagonjwa baada

ya kupata ahueni wanaendelea kuambukiza wengine.

n Baadhi ya watu wanapougua kutokana na Ukimwi wanaamini

wamerogwa, hivyo wanakwenda kwa waganga

wa kienyeji.

Wana ujumbe kwetu!

JIMOWACO wanaamini kwamba

hata wewe msomaji pamoja na watu

waliokuzunguka mnaweza kuanzisha

mkakati kama huu katika eneo lenu.

Siri ya mafanikio ni subira, kujiamini

na kupeana moyo!

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

23
KATUNI

upatu au hupati?

Wanawake Mtaa wa Sita

ni wachakarikaji haswa!

Asiyeuza juisi anachoma

maandazi, ili mradi mkono uende

kinywani. Siku moja mwenzao,

Mama Semeni, anapata wazo, ‘analiuza’

kwa mashostito nao wanaingia

‘line’. Songombingo linalotokea

baadaye mmmmh, almanusura mtu

asutwe kwa matarumbeta! Kulikoni?

Sitaki kukumalizia utamu! Fuatilia!

Michoro: babatau cartoons 2012

BAADA YA WIKI MBILI

24 Si Mchezo! machi-aprili 2012

MCHEZO UMEANZA
machi-aprili 2012 Si Mchezo!

25
26 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Ama kweli majuto

ni mjukuu!

Kijumbe ndo

keshatoroka na

fedha za mchezo,

ameacha

vumbi tu!

Upatu ni

mzuri. Tatizo

wengi wetu

tunaucheza

kienyeji mno!
UKWELI WA MAMBO

Yanawakuta wengi!

Stori ya Mama Semeni

na wenzake haichekeshi

bali inasikitisha!

Inawezekana hata wewe ama

unacheza upatu au una mpango

wa kucheza. Inawezekana

umeapa kutokucheza tena

upatu kwani yaliwahi kukukuta

yaliyomkuta Mama Havinitishi

na wenzake! Pole!

Sio mchezo mbaya

Upatu au ‘mchezo’ kama

wengi wanavyouita,

si jambo baya. Wengi

‘wametoka’ kwa staili hii.

Utaukuta mitaani, maofisini,

kwa watu ambao ama

wako katika ‘kijiwe’ kimoja

au wanafanya biashara

zinazofanana. Kwa kifupi ni

jambo zuri. Ndiyo, kwani si

kila mmoja ana uwezo wa

kudunduliza vijisenti peke

yake hadi mfuko utune.

Zaidi ya kuwasaidia

watu kuinua mitaji na

kujikwamua kimaisha,

‘mchezo’ huu unawasaidia

watu kuishi kijamaa,

yaani kufahamiana na

kusaidiana katika matatizo

mbalimbali ya kijamii,

wengine wanasema ‘kufa na

kuzikana’.

Tatizo nini?

Tumeshuhudia ngumi zikilika mitaani, watu

wakiporomosheana matusi, wengine wakibubujikwa

machozi baada ya ‘kuingia chaka’, ukiuliza kulikoni

unaambiwa kijumbe ‘kasepa’ na fedha za wanakikundi!

Yote haya yanatokea kwa sababu tunaucheza ‘mchezo’

huu kienyeji mno, kama tunavyoona katika stori ya Mama

Semeni na wenzake.

Walipaswa wakutane, wafanye makubaliano ya kucheza

‘mchezo’, kuwe na orodha ya wanachama iliyoandikwa

na zamu za ‘kupokea’,

wafanye uchaguzi wa

‘kijumbe’ wajipangie

masharti na kuwe

na daftari la kusaini

mwanachama

anapowasilisha mchango

na anapopokea.

J Kumbuka

Ni vizuri muwe ni kikundi

cha watu mnaofahamiana

vizuri kwa makazi, kipato

na tabia, ili kuepusha

mambo kwenda mrama.

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

27
SAUTI YANGU

Si Mchezo!

Femina HIP

SLP 2065,

DSM

Acheni siasa, leteni

maendeleo

Nakereka sana na Baraza la Madiwani

kugombana na Mkurugenzi wa

Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.

Kila siku ni mifarakano isiyokuwa na

tija. Mpaka sasa maendeleo hakuna

na hatupigi hatua yoyote mbele.

Miundombinu ni mibovu, hospitali ya

wilaya hakuna chumba cha kuhifadhia

maiti, vijana hawana ajira na maisha

ni magumu kwa ujumla. Nawaomba

viongozi hawa wakae pamoja na kutatua

tofauti zao, washikamane na kutuletea

maendeleo katika wilaya yetu.

Saidi Juma Aina

Mkuranga

28 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Kama una chochote

unachotaka kusema

tuandikie ili upate

fursa ya kuwaelimisha

wengine

Maoni yaliyotolewa katika ukurasa huu

ni ya wasomaji, si lazima yalingane na

msimamo wa Femina HIP.

Wateja wengine

wa saluni...

Sipendi tabia ya baadhi ya wateja wanaokuja

saluni kupata huduma za urembo wa nywele

na nakshi nyingine. Wengi wanajisahau

kwamba hili ni eneo la biashara na kazi.

Wanajazana na kuanza kupiga umbea, wakati

mwingine nafasi inakosekana kwa wateja

wanaohitaji kupata huduma. Hii ni kero

hapa kwetu na mbaya zaidi wanaume nao

wanashiriki mambo haya. Jamani nendeni

maeneo yenu mkafanye vijiwe vya umbea na

majungu mtuache sisi tufanye kazi.

Marium a.k.a Mama Zai

Kimanzichana-Mkuranga

Acheni kutudharau

Kuna imani kwamba ukifanya

kazi nyumba za kulala wageni

maarufu kama guest house,

baa au ukiwa mhudumu wa

hoteli jamii inakuchukulia

kama mhuni. Hii si sahihi hata

kidogo kwani wanaofanya

kazi hizi wanajiheshimu, kama

yeyote yule anayefanya kazi

katika sekta nyingine. Acheni

kuwashikashika wahudumu.

Jua kwamba wapo kazini na

siyo sehemu ya kuendekeza

mapenzi ya kulazimisha.

Heshimu utu wao.

Judith Macha

Mkuranga-Pwani

Wewe pia unaweza kulonga na vijana

wenzako. Tuandike maoni,

ushauri, vichekesho,maswali

nk, weka anuani yako na tuma

ukiambatanisha na picha yako

kwa Mhariri, Jarida la Si Mchezo!,

S.L.P 2065 Dar es Salaam.

simchezo@feminahip.or.tz

Au tumbukiza katika boksi la Si

Mchezo! kama lipo katika eneo

unaloishi.
januari-februari 2012 Si Mchezo! 29
Mila katika kupambana na VVU

Unyago ni sehemu ya utamaduni wa watu wa Pwani

ya Tanzania kumfundisha mtoto wa kike anapovunja

ungo mambo muhimu yanayohusu afya ya uzazi, usafi

na majukumu mengine yanayomhusu. Utamaduni huu

umesaidia kwa kiasi kikubwa kuweka njia kwa watu

wazima (manyakanga) kuwaandaa wasichana kwa

maisha ya utu uzima. Mwisho wa mafunzo ya unyago

wasichana ambao huitwa wali hutolewa nje kwa sherehe

maalum ya kuhitimu ijulikanayo kama “kunema”.

Hatua zimechukuliwa…

Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya PAYODE

(Partnership for Youth Development)

katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha

iliendesha mafunzo shirikishi kwa

manyakanga kuhusu afya ya uzazi

na kujikinga na maambukizi ya VVU.

Mafunzo haya yalisaidia kuboresha uelewa

wa manyakanga na kuwajengea stadi

za kuingiza elimu hii ndani ya mafunzo

ya unyago. Jumla ya manyakanga 40

wamepata mafunzo kupitia PAYODE

tangu mwaka 2008.

30 Si Mchezo! machi-aprili 2012

Watu wanasemaje?

ZINDUKA

Mtazamo uko hivi…

Wasichana na wanawake

wapo katika hatari zaidi ya

kupata maambukizi ya VVU

ikilinganishwa na wavulana

na wanaume wa umri sawa na

wao. Hata hivyo njia rahisi ya

kuwafikia vijana hasa wasichana

kwa shughuli za uelimishaji

kuhusu ujana na makuzi bado ni

changamoto kutokana na mila

na desturi ya Mtanzania.

Ushuhuda unaonyesha kuwa elimu ya unyago

inayotolewa na manyakanga hawa waliopatiwa

mafunzo imesaidia kupunguza tatizo la

wasichana kuachishwa shule kwasababu ya

ujauzito katika maeneo ya mradi. Jamii na

serikali imefurahishwa na hatua ya PAYODE

kutumia utamaduni wa watu wa Pwani kama

njia chanya ya kufikishia wasichana elimu ya afya

ya uzazi . “Natamani watoto wangu wangeliyajua

haya yote kabla,” anasema mwenyekiti wa

manyakanga, Mama Blandina Mbaji.

USHAURI

Swali

Nina mpenzi ambaye tumekamilisha taratibu zote za ndoa, lakini kabla ya ndoa

akapata ujauzito. Baada ya kuanza huduma za kliniki akaonekana ana maambukizi

ya VVU, na mimi nilipopimwa nikawa salama. Je, mpenzi wangu huyu anafaa kuoa ?

Ushauri tafadhali. Msomaji Si mchezo! Lindi-Pwani

Kama mmepima na ukagundua

mwenzio ana VVU usimuache.

nendeni kwa mshauri nasaha

atawashauri jinsi ya kumkinga

mtoto na wewe mwenyewe

usipate maambukizi na mtaishi

kwa raha.

Amosi

wa Mkuranga

Kama kweli unampenda

mwenzi wako, nakushauri

endelea kuwa naye kama

rafiki yako wa karibu

sana. Pia kuwa mshauri wake katika hali

aliyonayo maana kuwa na VVU siyo kufa

na urafiki au uhusiano usivunjike.

Ibrahim Manjale,

Mkuranga

SWALI LA TOLEO LIJALO

Pole kaka yangu, kama

kweli hiyo mimba ni

yako na unampenda

mkeo nakushauri

umuoe. Kuwa na

VVU siyo mwisho wa

mapenzi na hakuzuii

kuendeleza mipango

yenu. Nendeni

kwenye kituo cha

huduma na tiba kwa

ushauri zaidi.

Hamisi Nuru

Jimowaco-Mkuranga

Kuna binti tumependana na nimependa tabia zake. Yuko tayari

kuoana nami lakini naogopa kwasababu nimetembea na dada

yake ambaye kwa sasa ameolewa. Ila binti huyo sijafanya naye

ngono, anasema mpaka tuoane. Naombeni ushauri wenu. Festo

Mgaya, Songea.

Nawapongeza kwa kupima. Yeyote anayeishi

na VVU ana haki zote za kibinadamu

ikiwa ni pamoja na kuoa/kuolewa, kuwa

na familia n.k. Maamuzi ya kumuoa au

kutokumuoa ni yako na yeye. Katika upimaji

VVU kuna uwezekano kwa sasa ukawa

salama lakini baada ya muda ukakutwa

nawe hauko salama. Nenda katika kituo cha

ushauri nasaha watakupa elimu ya kuishi

na mke mwenye maambukizi ya VVU bila

wewe kupata maambukizi na kupata watoto

wasio na maambukizi.

Asante

Betty Liduke ni rafiki mkubwa

wa vijana, hata wewe unaweza

kulonga naye. Ni msambazaji

mkubwa wa wa Jarida la Si

Mchezo! Mkoani Njombe. Ni

mshauri nasaha na ni mratibu

wa kitengo cha udhibiti

Ukimwi katika Kampuni ya

TANWAT, Njombe.

Mwandikie kupitia

Jarida la Si Mchezo!

Si Mchezo!

S. L. P. 2065

Dar es Salaam

au tuma ujumbe mfupi wa

maandishi kupitia namba

0715 568222 na utuambie

kama ungependa uchapishwe.

machi-aprili 2012 Si Mchezo!

31
32 Si Mchezo! machi-aprili 2012