MAGONJWA MAKUU YA KUKU, TIBA NA KINGA - Research Into Use
MAGONJWA MAKUU YA KUKU, TIBA NA KINGA - Research Into Use MAGONJWA MAKUU YA KUKU, TIBA NA KINGA - Research Into Use
3.1 MAgoNjWA MUHIMU YANAYoSAbAbISHWA NA bAKTerIA 6 Magonjwa Makuu Ya Kuku, Tiba Na Kinga
Maelezo: Bakteria ni vimelea ambavyo havionekani kwa macho. Bakteria wengi huishi katika mimea na wanyama waliohai au waliokufa. Bakteria wanaosababisha magonjwa hupatikana kwenye miili ya kuku wagonjwa, utumbo, makamasi, na vinyesi vyao. Aidha katika mazingira machafu na vyakula, maji, hewa, na vifaa vya kazi vilivyo chafuliwa. Mazingira yenye unyevunyevu na joto ni vichocheo vya kuzaliana na kusambaa kwa bakteria. Magonjwa muhimu yanayosababishwa na bakteria hapa nchini ni pamoja na: Homa kali ya Matumbo, Kuharisha Kinyesi Cheupe, Kipindupindu cha Kuku, Mafua ya Kuku, Ugonjwa Sugu wa Mfumo wa Hewa, Kolibasilosi na Kampilobakta. 3.1.1 HoMA KALI YA MATUMbo (foWL TYPHoID) Maelezo: NI ugonjwa wa kuku unaosababishwa na bacteria na hushambulia zaidi kuku wakubwa pia na vifaranga. Ugonjwa pia hushambulia aina zote za bata, kanga na ndege wa porini. Jinsi Ugonjwa Unavyoenea: Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa. Panya, ndege na wanyama wengine wanaweza kueneza ugonjwa kwa kubeba mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa na kuchafua maji na vyakula. Maambukizi pia yanaweza kupitia katika mayai yanayototolewa na vifaranga kuathirika. Pia mashine za kutotolea zilizochafuliwa zinaweza kuambukiza vifaranga. Dalili Kuku wakubwa • Kuharisha kinyesi cha majimaji na cha rangi ya njano • Vifo vya ghafla • Kupauka kwa upanga na masikio kwa sababu ya kupungukiwa damu Tahadhari: Wageni na wafanyakazi wanaweza kusambaza ugonjwa kutoka shamba hadi shamba au banda hadi banda • Manyoya hutimka, hushusha mbawa, hufumba macho na kuzubaa (kuvaa koti) Magonjwa Makuu Ya Kuku, Tiba Na Kinga 7
- Page 1 and 2: Magonjwa Makuu ya kuku, Tiba na kin
- Page 3 and 4: YALIYoMo DIbAjI iii SHUKrANI iv UTA
- Page 5 and 6: DIbAjI Ndege wafugwao wana nafasi k
- Page 7 and 8: UTANgULIZI Sekta ya ufugaji wa ndeg
- Page 9 and 10: • Hupunguza athari za kiuchumi zi
- Page 11 and 12: Taratibu za Kuzuia Kuenea kwa Magon
- Page 13: Ugonjwa ni nini? Ugonjwa ni mabadil
- Page 17 and 18: Tiba • Yapo madawa mengi aina ya
- Page 19 and 20: Tiba • Yapo madawa mengi aina ya
- Page 21 and 22: Kuku wakubwa • Kuku wakubwa huony
- Page 23 and 24: Dalili Kuku wanaweza wasionyeshe da
- Page 25 and 26: Tiba • Madawa aina ya sulfa na an
- Page 27 and 28: Dalili Ugonjwa huu hushambulia zaid
- Page 29 and 30: Tiba • Madawa aina ya sulfa na an
- Page 31 and 32: Magonjwa Makuu Ya Kuku, Tiba Na Kin
- Page 33 and 34: Maelezo Virusi ni vimelea ambavyo h
- Page 35 and 36: Madoa makubwa ya damu kwenye firigi
- Page 37 and 38: Dalili • Chukua Tahadhari: Wageni
- Page 39 and 40: Kuku wenye mboni ya kijivu Kupooza
- Page 41 and 42: 3.2.4 NDUI YA KUKU (foWL Pox) Maele
- Page 43 and 44: Dalili • Tumbo kuvimba • Kuku k
- Page 45 and 46: Uchunguzi wa Mzoga • Uharo wenye
- Page 47 and 48: jinsi Ugonjwa Unavyoenea Dalili •
- Page 49 and 50: Maelezo Protozo ni vimelea vyenye c
- Page 51 and 52: 3.3.2 HISToMoNASI (HISToMoNIASIS) M
- Page 53 and 54: Magonjwa Makuu Ya Kuku, Tiba Na Kin
- Page 55 and 56: Maelezo Minyoo huishi katika njia y
- Page 57 and 58: Tiba Dawa za Minyoo - kuwekwa kweny
- Page 59 and 60: Maelezo Hawa ni wadudu wanaoishi kw
- Page 61 and 62: Kuzuia na Kinga • Banda (kuta, pa
- Page 63 and 64: Maelezo Magonjwa yatokanayo na upun
Maelezo: Bakteria ni vimelea ambavyo havionekani kwa macho. Bakteria wengi huishi

katika mimea na wanyama waliohai au waliokufa. Bakteria wanaosababisha magonjwa

hupatikana kwenye miili ya kuku wagonjwa, utumbo, makamasi, na vinyesi vyao. Aidha

katika mazingira machafu na vyakula, maji, hewa, na vifaa vya kazi vilivyo chafuliwa.

Mazingira yenye unyevunyevu na joto ni vichocheo vya kuzaliana na kusambaa kwa

bakteria.

Magonjwa muhimu yanayosababishwa na bakteria hapa nchini ni pamoja na: Homa kali ya

Matumbo, Kuharisha Kinyesi Cheupe, Kipindupindu cha Kuku, Mafua ya Kuku, Ugonjwa

Sugu wa Mfumo wa Hewa, Kolibasilosi na Kampilobakta.

3.1.1 HoMA KALI YA MATUMbo (foWL TYPHoID)

Maelezo: NI ugonjwa wa kuku unaosababishwa na bacteria na hushambulia zaidi kuku

wakubwa pia na vifaranga. Ugonjwa pia hushambulia aina zote za bata, kanga na ndege

wa porini.

Jinsi Ugonjwa Unavyoenea: Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa

na kinyesi cha kuku wagonjwa. Panya, ndege na wanyama wengine wanaweza kueneza

ugonjwa kwa kubeba mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa na kuchafua maji na vyakula.

Maambukizi pia yanaweza kupitia katika mayai yanayototolewa na vifaranga kuathirika. Pia

mashine za kutotolea zilizochafuliwa zinaweza kuambukiza vifaranga.

Dalili

Kuku wakubwa

• Kuharisha kinyesi cha majimaji na cha rangi ya njano

• Vifo vya ghafla

• Kupauka kwa upanga na masikio kwa sababu ya kupungukiwa damu

Tahadhari: Wageni na wafanyakazi

wanaweza kusambaza ugonjwa

kutoka shamba hadi shamba au

banda hadi banda

• Manyoya hutimka, hushusha mbawa, hufumba macho na kuzubaa (kuvaa koti)

Magonjwa Makuu Ya Kuku, Tiba Na Kinga

7