28.02.2013 Views

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA MIFUGO

2000

2009

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA MIFUGO

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

S.L.P 9152

DAR ES SAALAM MEI, 2009

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

i

Kimetayarishwa na

© Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi-Dar es salaam

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

S. L. P 9152

Dar es Salaam - Tanzania

Toleo la kwanza 2009

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

ii

ORODHA YA VITABU VINGINE VILIVYOPO

Vipo vitabu vingine ambavyo vimetayarishwa na Wizara kuwasaidia wafugaji, wanafunzi

wa taaluma ya mifugo na wataalam wa mifugo wanaofanya shughuli za ugani. Vitabu

hivyo ni:-

Ufugaji Bora wa Nguruwe (Toleo la tatu) 2009

Ufugaji Bora wa Kuku (Toleo la tano) 1997

Ufugaji Bora wa Ng’ombe wa Nyama 2003

Ufugaji Bora wa Ng’ombe wa Maziwa 2005

Ufugaji Bora wa Kuku wa Kienyeji 2008

Ufugaji Bora wa Nguruwe (Toleo la tatu) 2009

Uzalishaji Bora wa Ngozi 2009

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

iii

WAHARIRI

Walioshiriki kuhariri kijitabu hiki cha Ufugaji Bora ni:-

M. R. Bakuname Idara ya Utafiti, Mafunzo na huduma za Ugani

E. S. Mngulwi Idara ya Utafiti, Mafunzo na huduma za Ugani

H. L. N. Lyimo Idara ya Utafiti, Mafunzo na huduma za Ugani

L. Asimwe Idara ya Uzalishaji Mifugo na Uendelezaji wa Miundombinu

ya Masoko

A. S. Bundala Idara ya Huduma za Afya ya Mifugo

C. J. Ndomba Idara ya Uendelezaji Mifumo ya Ufugaji wa Asili

M. I. Shawala Chuo cha Mafunzo ya Mifugo - Morogoro

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

iv

SHUKRANI

Shukrani ziwaendee watayarishaji wa kijitabu hiki ambao ni wataalam wa Kitengo cha

Ugani na wataalam wengine wote wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi

ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa michango yao mbalimbali

iliyowezesha kufanikisha kazi hii. Waandishi wamezingatia taarifa na takwimu toka

vyanzo mbalimbali ambavyo vyote hivyo wanavitambua na kuvishukuru.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

v

YALIYOMO

SURA UKURASA

JALADA i

WATAYARISHAJI ii

ORODHA YA VITABU VINGINE VILIVYOPO iii

WAHARIRI iv

SHUKURANI v

YALIYOMO vi

DIBAJI viii

UTANGULIZI ix

SURA YA KWANZA 1

1.0 KANUNI ZA UFUGAJI WA NG’OMBE BORA 1

1.1 Banda/Zizi la ng’ombe 1

1.2 Uchaguzi wa ng’ombe wa kufuga 2

1.2.1 Ng’ombe wa nyama 2

1.2.2 Ng’ombe wa maziwa 2

1.3 Utunzaji wa ndama 3

1.4 Utunzaji wa ndama baada ya kuachishwa

maziwa hadi kupevuka (miezi 12 – 18) 4

1.5 Utunzaji wa ng’ombe wakubwa 5

1.5.1 Upandishaji 5

1.5.2 Dalili za ng’ombe jike anayehitaji 5

kupandishwa

1.5.3 Taratibu za uhimilishaji 6

1.6 Matunzo ya ng’ombe mwenye mimba 6

1.6.1 Dalili za ng’ombe anayekaribia kuzaa 6

1.6.2 Matatizo yanayoweza kutokea wakati 6

wa kuzaa

1.7 Matunzo ya ng’ombe anayekamuliwa 7

1.8 Utunzaji wa dume 7

1.9 Uzalishaji wa mazao yatokanayo na ng’ombe 7

1.9.1 Uzalishaji wa nyama 7

1.9.2 Uzalishaji wa maziwa 8

1.10 Ulishaji bora kwa misimu mbalimbali ya

mwaka

1.10.1 Hatua za kukabiliana na tatizo la

8

uhaba wa malisho

1.10.2 Njia za kuhifadhi malisho 9

1.10.3 Vyakula vya ziada 10

1.11 Udhibiti na tiba ya magonjwa ya ng’ombe 10

1.12 Kumbukumbu na takwimu muhimu 11

SURA YA PILI 12

2.0 KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA MBUZI NA

KONDOO

12

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

8

vi

SURA UKURASA

2.1 Zizi au banda la mbuzi/kondoo 12

2.1.1 Vifaa vya kujengea na vipimo vya

banda

13

2.2 Uchaguzi wa mbuzi/kondoo wa kufuga 14

2.3 Utunzaji wa mbuzi/kondoo watoto 14

2.3.1 Matunzo mengine 15

2.4 Utunzaji wa mbuzi/kondoo wanaokua 15

2.5 Utunzaji wa mbuzi/kondoo jike 16

2.6 Utunzaji wa mbuzi/kondoo mwenye mimba 17

2.7 Utunzaji wa mbuzi/kondoo anayenyonyesha 17

2.8 Utunzaji wa dume la mbegu 17

2.9 Matunzo mengine 17

2.10 Udhibiti wa magonjwa ya mbuzi na kondoo 18

2.11 Uzalishaji wa mazao ya mbuzi na kondoo 19

2.11.1 Uzalishaji wa nyama 19

2.11.2 Uzalishaji wa maziwa 19

2.12 Utunzaji wa kumbukumbu za mifugo 19

SURA YA TATU 21

3.0 KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA NGURUWE 21

3.1 Banda la nguruwe 21

3.2 Kuchagua nguruwe wa kufuga 22

3.3 Utunzaji wa watoto wa nguruwe 22

3.4 Utunzaji wa watoto wa nguruwe wiki 1 – 8 22

3.5 Utunzaji wa nguruwe walioachishwa kunyonya 23

3.6 Utunzaji wa nguruwe jike kutoka kupevuka

hadi kuzaa

24

3.6.1 Kutunza nguruwe mwenye mimba 25

3.6.2 Utunzaji wa nguruwe

anayenyonyesha

25

3.7 Utunzaji wa dume 26

3.8 Udhibiti wa afya na magonjwa ya nguruwe 26

3.9 Uzalishaji wa mazao ya nguruwe 27

3.10 Kuweka na kutunza kumbukumbu 27

SURA YA NNE 28

4.0 KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU 28

4.1 Banda la kuku 28

4.1.1 Vifaa vinavyotumika kwa ujenzi wa

banda

29

4.1.2 Ukubwa wa banda 29

4.1.3 Vifaa na vyombo muhimu 29

4.2 Kuchagua kuku bora wa kufuga 30

4.2.1 Kuku wa asili 30

4.2.2 Kuku wa kisasa 30

4.2.3 Kuchagua jogoo 30

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

vii

SURA UKURASA

4.3 Mayai kwa ajili ya kutotoa vifaranga 31

4.3.1 Uchaguzi wa mayai 31

4.3.2 Utunzaji wa mayai 31

4.4 Utunzaji wa kuku kwa makundi 31

4.4.1 Kulea vifaranga kwa kutumia kuku 31

4.4.2 Kulea vifaranga kwa kutumia bruda 32

4.4.3 Kulea kuku wanaokua (wiki 7 - 20) 32

4.4.4 Kuku wanaotaga 33

4.5 Udhibiti na tiba dhidi ya magonjwa ya kuku 33

4.5.1 Dalili za kuku mgonjwa 34

4.6 Ufugaji wa aina nyingine za ndege 34

4.7 Uzalishaji na masoko ya mazao ya kuku 34

4.8 Utunzaji wa kumbukumbu 35

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

viii

DIBAJI

Tanzania ina idadi kubwa ya mifugo, ikiwemo takribani ng’ombe milioni 19.1, mbuzi

13.5, kondoo milioni 3.6, nguruwe million 1.4, na kuku wa asili milioni 33, kuku wa

kisasa milioni 20. Pamoja na kuwa na mifugo mingi kiasi hiki mchango wake katika pato

la taifa bado ni mdogo 4.7% mwaka 2008 kutokana na ufugaji usiozingatia kanuni za

ufugaji bora. Dira ya Sekta ya Mifugo ni kuwa, “Ifikapo mwaka 2025 kuwe na

Sekta ya mifugo ambayo ni shirikishi na inayozingatia ufugaji wa kisasa,

endelevu, inayoendeshwa kibiashara yenye mifugo bora na yenye tija kubwa,

itakayoinua maisha ya Mtanzania kwa kutoa ajira, kuzalisha mali ghafi kwa

ajili ya usindikaji, kuongeza pato la Taifa na kuhifadhi mazingira”. Ili kufikia

malengo ya dira hii, Wizara imeweka mikakati mbalimbali, mojawapo ikiwa ni kuwapatia

wafugaji elimu kuhusu ufugaji bora kupitia machapisho mbalimbali.

Kijitabu hiki ni moja ya machapisho kinachoelezea kanuni za ufugaji bora wa mifugo

hususan ng’ombe wa nyama na maziwa, mbuzi, kondoo, nguruwe na kuku. Kanuni hizi

zimejikita katika uzalishaji, ujenzi wa mabanda, ulishaji bora wa mifugo na upatikanaji

wa maji safi ya kutosha kwa kuzingatia makundi mbalimbali. Aidha kanuni zingine

zilizoainishwa zinahusu udhibiti wa magonjwa na uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko.

Kuna uwezekano mkubwa kwa wafugaji kupata mafanikio makubwa kutokana na

mifugo yao iwapo watazingatia kanuni hizi. Kanuni za ufugaji bora husaidia kuwaongoza

wafugaji kufahamu mambo muhimu wanayotakiwa kufanya ili mifugo yao ikue vizuri,

wapunguze vifo na kupata mazao mengi na yaliyo bora. Pia uzingatiaji wa kanuni hizi

utampunguzia mfugaji gharama za uzalishaji ili kumwogezea kipato.

Kijitabu hiki kimeandikwa kwa lugha nyepesi ili kuwawezesha watumiaji kukielewa

vizuri. Ni matumaini yangu kuwa kijitabu kitakuwa cha manufaa kwa wafugaji na hasa

pale ambapo kuna upungufu wa wataalamu wa ugani. Hata hivyo, kijitabu hiki

hakichukui nafasi ya watalaam wa ugani hivyo wafugaji wanashauriwa kutumia

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

ix

watalaam wa ugani kwa kadri inanavyowezekana. Pia ningependa kutoa mwito kwa

wafugaji kujijengea tabia ya kusoma vitabu kujipatia elimu zaidi na teknolojia ya kisasa.

C. Nyamrunda

Katibu Mkuu 19 Agosti, 2009

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

x

UTANGULIZI

Nchini Tanzania zaidi ya asilimia 80 ya wananchi huishi vijijini na hujishughulisha na

kilimo, ufugaji na uvuvi. Shughuli hizi ndizo uti wa mgongo wa taifa hili na zitaendelea

kutegemewa katika kukuza uchumi. Ufugaji ni moja ya shughuli muhimu inayowapatia

wananchi chakula na kipato ikizingatiwa kuwa asilimia 40 ya kaya za kilimo zipatazo

milioni 4.8 hutegemea ufugaji. Mifugo ambayo inafugwa kwa wingi ni ng’ombe, mbuzi,

kondoo, nguruwe na kuku.

Pamoja na kuwa na mifugo mingi, ufugaji bado haujaweza kumwongezea mfugaji

kipato na kuchangia pato la taifa kwa kiasi cha kuridhisha. Changamoto iliyopo mbele

yetu ni kuongeza uzalishaji na tija ili kukidhi malengo ya Mkukuta, Dira ya Taifa ya

Maendeleo 2025, Malengo ya Milenia 2015 na mwongozo wa Kilimo Kwanza. Sekta ya

mifugo inayo nafasi kubwa katika kuchangia kufikia malengo haya kama kanuni za

ufugaji bora zitazingatiwa.

Madhumuni ya kutayarisha kijitabu hiki ni kuainisha kanuni za ufugaji bora unaozingatia

ufugaji wa kisasa, endelevu, unaoendeshwa kibiashara ili kupata mifugo bora na yenye

tija kubwa, itakayoinua maisha ya wananchi wanaotegemea ufugaji na kuhifadhi

mazingira.

Utayarishaji wa kijitabu hiki unatambua pia kuwepo kwa vitabu vingine vinavyoelezea

kwa kina kuhusu ufugaji wa mifugo mbalimbali. Inatarajiwa kwamba kijitabu hiki

kitatumiwa na wafugaji na wadau wengine kama nyenzo muhimu katika kuboresha

uzalishaji wa mifugo nchini.

Kijitabu hiki kinaainisha mambo ya kuzingatia katika ufugaji wa ng’ombe, mbuzi,

kondoo, nguruwe na kuku wakati wa ujenzi wa mabanda, uchaguzi wa wanyama wa

kufuga, na matunzo yao katika makundi mbalimbali. Aidha kanuni za udhibiti wa

magonjwa, uzalishaji mazao ya mifugo yanayokidhi viwango na mahitaji ya soko na

uwekaji wa kumbukumbu sahihi umeainishwa.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea

kipato

xi

SURA YA KWANZA

1.0 KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA NG’OMBE

Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao

mengine kama ngozi, mbolea na hutumika kama wanyama kazi. Zaidi ya asilimia

95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na

maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa.

Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili, wale

wanaofugwa kwa ajili ya nyama na lingine kwa ajili ya maziwa. Ili kuwawezesha

ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na ngozi mfugaji anapaswa

kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na:-

i) Kwa ng’ombe wanaofugwa kwa mfumo wa ufugaji huria ni muhimu

ardhi hiyo itunzwe kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na

malisho.

ii) Kujenga banda au zizi bora

iii) Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na lengo la uzalishaji (nyama

au maziwa).

iv) Kutunza makundi mbalimbali ya ng’ombe kulingana na umri na hatua

ya uzalishaji

v) Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.

vi) Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalam wa

mifugo.

vii) Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya

soko.

viii) Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango vya ubora na

usalama.

ix) Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.

1.1 Mifumo ya Ufugaji

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

1

Ng’ombe wanaweza kufugwa katika mfumo wa ufugaji huria au kulishwa katika

banda (ufugaji shadidi). Ufugaji huria huhitaji eneo kubwa la ardhi yenye malisho

mazuri na vyanzo vya maji. Pamoja na kuwa na ufugaji huu, ni muhimu ardhi hiyo

itunzwe kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho. Ufugaji wa

shadidi uzingatie uwepo wa banda bora na lishe sahihi

Ufugaji Katika Mfumo Huria

Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora katika ufugaji huria anapaswa

kuzingatia yafuatayo:-

• Atenge eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi ya ng’ombe alionao,

• Atunze malisho ili yawe endelevu na yapatikane wakati wote,

• Awe na eneo lenye maji ya kutosha; na

• Atenganishe madume na majike ili kuzuia ng’ombe kuzaa bila mpangilio.

Matunzo mengine ya ng’ombe yazingatie vigezo vingine muhimu kama umri, hatua

ya uzalishaji na matumizi ya ng’ombe husika.

1.2 Banda/Zizi Bora la ng’ombe .

1.2.1 Banda Bora

Banda lijengwe sehemu ya mwinuko mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na

sifa zifuatazo:-

• Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya mvua, upepo, jua kali na baridi,

• Kuta imara zenye matundu au madirisha kwa ajili ya kuingiza hewa na

mwanga wa kutosha,

• Sakafu yenye mwinuko upande mmoja ili isiruhusu maji na uchafu

kutuama,

• Lijengwe katika hali ya kuruhusu kufanyiwa usafi kwa urahisi kila siku, na

sakafu ngumu ya zege au udongo ulioshindiliwa na kuwekwa malalo,

• Paa lisilovuja na,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

2

• Liwe na sehemu za kulala ng’ombe wa makundi mbali mbali, sehemu ya

kukamulia (kwa ng’ombe wa maziwa), stoo ya vyakula, sehemu ya kutolea

huduma za kinga na tiba, eneo la kulishia na la maji ya kunywa.

1.2.2 Zizi bora

Zizi lijengwe sehemu ya mwinuko isiyoruhusu maji kutuama, mbali kidogo na

makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-

• Liweze kuhakikisha usalama wa ng’ombe,

• Ukubwa wa zizi uzingatie idadi ya mifugo,

• Liwe na sakafu ya udongo ulioshindiliwa vizuri na kufanyiwa usafi mara kwa

mara;

• Zizi la ndama liwe na paa; na

• Lijengwe kwa vifaa madhubuti na visivyoharibu ngozi

1.3 Uchaguzi wa koo na aina ya ng’ombe wa kufuga

Kwa ufugaji wenye tija, mfugaji anashauriwa kuchagua koo na aina ya ng’ombe

kwa kuzingatia malengo ya ufugaji (nyama au maziwa).

1.3.1 Ng’ombe wa nyama

Ng’ombe wanaofaa kufugwa kwa ajili ya uzalishaji nyama ni wale wanaokua kwa

haraka na kuweka misuli mikubwa iliyojengeka vizuri. Baadhi ya koo zenye sifa

hizo ni pamoja na Boran, Mpwapwa (nyama na maziwa), Charlolais, Aberdeen

Angus, pamoja na chotara wao. Hata hivyo, nchini Tanzania ng’ombe aina ya Zebu

(mfano Ufipa, Gogo, Masai, Sukuma, Tarime, Iringa red), Sanga (Ankole) na

chotara wao ndio hutumika kama ng’ombe wa nyama.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

3

1.3.2 Ng’ombe wa maziwa

Sifa za ng’ombe wa maziwa ni zifuatazo:-

Ng’ombe wa nyama aina ya Boran

• Umbo lililopanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea kichwani

• Mgongo ulionyooka kuanzia mabegani kuelekea mkiani

• Miguu mirefu iliyonyooka, minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele

na kwato imara

• Kiwele kiwe kikubwa chenye chuchu nne, ndefu, na unene wa wastani

• Nafasi kati ya chuchu na chuchu iwe ya kutosha

• Endapo ng’ombe anakamuliwa awe na kiwele kikubwa kilichoshikamana

vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye kiwele iliyosambaa

Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian,

Ayrshire, Jersey, Mpwapwa, Simmental na chotara watokanao na mchanganyiko

wa aina hizo na Zebu.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

4

Ng’ombe wa maziwa aina ya ‘Friesian’

1.4 Utunzaji wa Makundi Mbalimbali ya Ng’ombe wa Maziwa

Kulingana na Umri na Hatua ya Uzalishaji

1.4.1 Utunzaji wa Ndama.

Mfugaji anapaswa kutunza ndama vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na

bora kwa ajili ya maziwa. Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama

tangu kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na:

• Kuhakikisha kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini

vya magonjwa kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawajoto (Tincture of

Iodine) mara baada ya kuzaliwa.

• Ndama apatiwe maziwa ya awali yaani dang’a (colostrum) mara baada ya

kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Aidha,

aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa siku 3-4;

• Endapo jike aliyezaa amekufa au hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa

ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a mbadala, ambayo inaweza

kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo:

� Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa wakati huo huo,

� Lita moja ya maji yaliyochemshwa na kupozwa hadi kufikia joto la

mwili,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

5

� Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki (cod liver oil),

� Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3, na

� Yai moja bichi.

Koroga mchanganyiko huo, weka katika chupa safi na ndama anyweshwe kabla

haujapoa. Ndama anyweshwe mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda wa

siku 3 mfululizo na kila mara mchanganyiko uwe mpya. Wakati wa kunyweshwa,

chupa iwekwe juu ya ulimi na kichwa cha ndama kiinuliwe juu kidogo ili asipaliwe;

• Endapo ndama hawezi kunyonya, ng’ombe akamuliwe na ndama apewe

maziwa kwa njia ya chupa kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa,

• Ndama aendelee kupewa maziwa kwa kiasi kama ilivyoonyeshwa kwenye

Jedwali Na. 1,

• Ndama aanze kuzoeshwa kula nyasi laini, pumba kidogo na maji safi wakati

wote kuanzia wiki ya 2 baada ya kuzaliwa; na

• Ndama aachishwe kunyonya au kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi 3.

Mfugaji ahakikishe kwamba ndama anayeachishwa kunyonya ana afya

nzuri.

Jedwali Na. 1: Kiasi cha Maziwa na Chakula Maalum kwa Ndama

Umri (Wiki) Kiasi cha Maziwa kwa Kiasi cha chakula Maalum cha

siku (lita)

ndama kwa siku (kilo)

1. 3.0 0.0

2. 3.5 0.0

3. 4.0 0.0

4. 4.5 0.0

5. 5.0 0.1

6. 5.0 0.2

7. 5.0 0.3

8. 4.0 0.4

9. 3.0 0.7

10. 2.0 1.0

11. 1.5 1.25

12-16 0.75 1.5

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

6

Vyombo vinavyotumika kulishia ndama visafishwe vizuri kwa maji

yaliyochemshwa, sabuni na kukaushwa.

Matunzo mengine ya ndama ni pamoja na:-

• Kuondoa pembe kati ya siku 3 hadi 14 mara zinapojitokeza ili kuzuia

wanyama kuumizana na kuharibu ngozi,

• Kukata chuchu za ziada kwa ndama jike,

• Kuhasi ndama dume wasiozidi umri wa miezi 3 ambao hawatahitajika kwa

ajili ya kuendeleza kizazi ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri,

• Kuweka alama au namba za utambilisho kati ya siku ya kwanza na ya tano,

mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio, kwa ajili ya urahisi wa udhibiti

wa umiliki na utunzaji kumbukumbu; na

• Kuwapatia kinga dhidi ya maambukizi na tiba ya magonjwa wanapougua.

Huduma hizi zifanyike chini ya maelekezo ya mtaalam wa mifugo.

Utunzaji wa ndama baada ya kuachishwa maziwa hadi kupevuka (Miezi

3 – 18)

• Ndama baada ya kuachishwa maziwa apate malisho bora na chakula

mchanganyiko kuanzia kilo 2 - 4 kwa siku kutegemea umri wake,

• Ndama wanapofikia umri wa miezi 18, wachaguliwe wanaofaa kuendeleza

kizazi, wasio na sifa nzuri waondolewe katika kundi.

1.4.2 Utunzaji wa Mtamba

Mtamba ni ng’ombe jike aliyefikisha umri wa kupandwa (wastani wa miezi 18)

hadi anapozaa kwa mara ya kwanza. Ni muhimu kutunza vizuri mtamba ili

kupata kundi bora la ng’ombe. Miezi 3 kabla ya kupandishwa mtamba

apatiwe:-

• Malisho bora,

• Maji ya kutosha,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

7

• Madini mchanganyiko; na

• Chakula cha ziada kiasi cha kilo 2 – 3 kwa siku, ili kuchochea upevukaji

na kuongeza uzito wa mwili.

1.4.3 Utunzaji wa ng’ombe wakubwa

Kundi la Mitamba

Kundi hili linajumuisha ng’ombe wenye mimba, wanaokamuliwa na madume.

Mfugaji anapaswa kutunza vizuri ng’ombe wake wakubwa kwa lengo la kumpatia

mazao mengi na bora. Hili kundi kwa ujumla huhitaji malisho bora na maji safi ya

kutosha kila siku. Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ng’ombe

wakubwa ni pamoja na:

• Ng’ombe apatiwe majani makavu (hei) wastani wa kilo 10 au majani mabichi

kilo 40 kwa siku kutegemeana na uzito. Iwapo malisho hayatoshi hususan

wakati wa kiangazi, apewe masalia ya mazao (viwandani na mashambani)

kama molasisi, mabua, maharage, mpunga n.k,

• Ng’ombe apewe vyakula vya ziada (pumba, mashudu, madini mchanganyiko,

unga wa mifupa na chokaa) kulingana na hatua na kiwango cha uzalishaji; na

• Ng’ombe apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa

mtaalam wa mifugo.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

8

Upandishaji

Mfugaji anapaswa kumpandisha ng’ombe kwa umri na wakati muafaka ili kuepuka

matatizo ya uzazi na pia kuhakikisha anapata ndama bora na maziwa mengi.

Mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja na:

• Mtamba apandishwe akiwa na umri wa miezi 17 -24 na uzito wa kilo 230 -

300 kwa ng’ombe wa kigeni na umri wa miezi 30 – 36 na uzito wa kilo 200

kwa ng’ombe wa asili. (Rejea Jedwali Na 2),

• Ng’ombe aliyekwishazaa apandishwe siku 60 baada ya kuzaa; na

• Siku 18 - 23 baada ya kupandishwa, ng’ombe achunguzwe kama ana dalili

za joto ili apandishwe tena. Iwapo ng’ombe ataendelea kuonyesha dalili za

joto baada ya kupandishwa mara tatu mfugaji apate ushauri wa mtaalam

wa mifugo.

Jedwali Na.2: Umri na Uzito wa Kupandisha Mtamba

Aina ya Ng’ombe Uzito (Kg) Umri (Miezi)

Friesian 240- 300 18 - 24

Ayrshire 230 – 300 17 - 24

Jersey 200 – 250 18 - 20

Mpwapwa 200 – 250 18 - 20

Chotara 230 - 280 18 – 24

Boran 200 - 250 24 - 36

Zebu 200 30 - 36

Dalili za Ng’ombe Anayehitaji Kupandwa

Ni muhimu mfugaji akazitambua dalili za ng’ombe anayehitaji kupandwa ili aweze

kumpandisha kwa wakati. Dalili hizo ni pamoja na:-

• Kupiga kelele mara kwa mara,

• Kutotulia/kuhangaika,

• Kutokwa na ute mweupe usiokatika ukeni,

• Kupenda kupanda wenzake na husimama akipandwa na wenzake; na

• Kunusanusa ng’ombe wengine

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

9

Ng’ombe akionyesha dalili za joto apandishwe baada ya masaa 12, kwa

kuhimilisha au kwa kutumia dume bora (kwa mfano, akionyesha dalili asubuhi

apandishwe jioni na akionyesha dalili jioni apandishwe asubuhi).

Uhimilishaji

Uhimilishaji ni njia ya kupandikiza mbegu kwa ng’ombe jike kwa kutumia mrija.

Faida za uhimilishaji ni pamoja na kusambaza mbegu bora kwa haraka na kwa

gharama nafuu, kupunguza gharama za kutunza dume na kudhibiti magonjwa ya

uzazi.

Ili mfugaji anufaike na huduma hii anapaswa kufanya yafuatayo:-

• Kuchunguza kwa makini ng’ombe mwenye dalili za joto,

• Kumjulisha mtaalamu wa uhimilishaji mapema ili kuwezesha zoezi hili

kufanyika kwa wakati,

• Kuchunguza kama ng’ombe atarudi kwenye joto siku ya 18- 23 baada ya

kupandishwa; na

• Ng’ombe aliyepandishwa apimwe mimba siku 60 hadi 90 baada ya

kupandishwa.

1.4.4 Matunzo ya Ng’ombe Mwenye Mimba

Ng’ombe mwenye mimba huchukua miezi 9 hadi kuzaa. Katika kipindi hicho chote

anastahili kupatiwa lishe bora na maji ya kutosha ili akidhi mahitaji ya ndama aliye

tumboni na kutoa maziwa mengi baada ya kuzaa.

Mambo ya kuzingatia ni pamoja na:

• Ng’ombe apewe lishe bora na maji ya kutosha kipindi chote cha mimba,

• Miezi 2 kabla ya kuzaa apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku,

• Apewe kinga dhidi ya maambukizi na tiba ya magonjwa,

• Ng’ombe anayekamuliwa aachishwe siku 60 kabla ya kuzaa; na

• Ng’ombe anayekaribia kuzaa, hususan mtamba, azoeshwe kuingia kwenye

sehemu ya kukamulia.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

10

Dalili za Ng’ombe Anayekaribia Kuzaa

Mfugaji anapaswa kufahamu dalili za ng’ombe anayekaribia kuzaa ili aweze

kufanya maandalizi muhimu. Dalili hizo ni pamoja na:

• Kujitenga kutoka kwa wenzake,

• Kiwele kuongezeka ukubwa,

• Chuchu kutoa maziwa zikikamuliwa,

• Kutokwa na ute mwekundu na sehemu za uke kuvimba na kulegea,

• Kuhangaika, kulala chini na kusimama; na

• Kati ya saa moja hadi mbili kabla ya kuzaa sehemu ya uke hutokwa na maji

mengi ambayo husaidia kulainisha njia ya ndama kupita.

Huduma kwa Ng’ombe Anayezaa

Ng’ombe anayezaa anahitaji uangalizi wa karibu ili kuhakikisha usalama wa

ng’ombe na ndama anaezaliwa. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na yafuatayo:

• Sehemu ya kuzalia ng’ombe iandaliwe kwa kuwekwa nyasi kavu na laini na

iwe safi,

• Ng’ombe ahamishiwe sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzaa mara baada

ya dalili za kuzaa kuonekana; na

• Ng’ombe aachwe azae mwenyewe bila usumbufu.

Mfugaji apate ushauri/huduma kutoka kwa mtaalam iwapo matatizo yafuatayo

yatajitokeza:-

• Ng’ombe kushindwa kuzaa kwa masaa mawili hadi matatu baada ya

chupa kupasuka,

• Kondo la nyuma kushindwa kutoka masaa sita baada ya kuzaa

• Kizazi kutoka nje; na

• Ng’ombe kushindwa kusimama baada ya kuzaa.

1.4.5 Matunzo ya Ng’ombe Anayekamuliwa

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

11

Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji kupata chakula kwa ajili ya kujikimu na cha

ziada kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa. Ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa

maziwa ng’ombe:

• Apewe chakula cha ziada kwa kiwango cha kilo 1 kwa kila lita 2-3 za

maziwa anayotoa,

• Apewe madini na virutubisho vingine kulingana na mahitaji,

• Apewe maji mengi kwa vile ni ya muhimu katika kutengeneza maziwa,

• Aachwe kukamuliwa siku 60 kabla ya kuzaa. Uachishwaji huu ufanywe

taratibu ili ifikapo siku ya 60 kabla ya kuzaa ukamuaji usitishwe,

• Baada ya kusitisha kukamuliwa, apewe kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku

hadi atakapozaa; na

• Apatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba ya magonjwa

kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.

Uzalishaji wa maziwa

Lengo la ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama

pamoja na mazao yatokanayo na maziwa. Mambo muhimu ya kuzingatia ni:-

• Sehemu ya kukamulia iwe safi na yenye utulivu,

• Ng’ombe awe na afya nzuri, msafi, na kiwele kioshwe kwa maji safi ya

uvuguvugu,

• Mkamuaji awe msafi, kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza,

• Inashauriwa mkamuaji asibadilishwe badilishwe,

• Vyombo vya kukamulia viwe safi,

• Muda wa kukamua usibadilishwe; na

• Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo

maalum (strip cup) ili kuchunguza ugonjwa wa kiwele.

1.5 Uchaguzi na Utunzaji wa Dume Bora la Mbegu

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

12

Dume ndilo linalojenga ubora wa kundi la ng’ombe katika masuala ya uzalishaji

kutokana na uwezo wake wa kupanda majike wengi. Kwa wastani dume moja

linaweza kupanda majike 20-25 wakati wa msimu wa uzalianaji (breeding season).

Ili kundi la ng’ombe liwe bora, mambo yafuatayo yazingatiwe:

• Chagua dume kutoka kwenye ukoo ulio bora kwa kuzingatia kumbukumbu

za uzalishaji wa maziwa au nyama za wazazi wake,

• Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora,

• Lisha dume malisho bora na maji safi ya kutosha. Pia apatiwe chakula cha

ziada,

• Katika ufugaji shadidi, dume la ng’ombe lifugwe kwenye banda imara lenye

sehemu za kuwekea chakula, maji na kufanyia mazoezi,

• Katika ufugaji huria, dume atengewe sehemu na kupatiwa chakula cha

ziada,

• Dume livalishwe pete puani kwa ajili ya kupunguza ukali na kuwezesha

urahisi wa kumshika,

• Dume apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa

mtaalam wa mifugo; na

• Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo katika kuchagua dume bora.

1.6 Utunzaji wa Ng’ombe wa Nyama

Ng’ombe wengi wanaofugwa hapa nchini Tanzania ni wa asili ambao kwa kiwango

kikubwa hutumika kwa ajili ya uzalishaji wa nyama. Hata hivyo uzalishaji wake wa

nyama ni mdogo kutokana na kasi ndogo ya kukua na kuwa na uzito mdogo

wakati wanapopevuka. Hali hii husababishwa na matunzo duni, kwa kuwa

huchungwa/hulishwa kwa kutegemea malisho peke yake ambayo hayawezi

kukidhi mahitaji ya viinilishe vinavyohitajika kwa ng’ombe.

Ili kuongeza kasi ya ukuaji na kuongeza uzalishaji wa nyama, mfugaji anapaswa

kufanya mambo yafuatayo:-

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

13

Ndama:

• Wajengewe banda/boma imara, safi na lisilo na unyevunyevu ilikuepukana

na magojwa kama kichomi na kuhara,

• Waruhusiwe kunyonya kwa muda usiopungua miezi sita, pia wapatiwe

majani laini kuanzia wanapofikia umri wa wiki mbili ili waanze kula

mapema,

• Wapatiwe maji masafi na yakutosha,

• Ndama dume ambao hawatahitajika kwa ajili ya kuendeleza kizazi

wahasiwe wakiwa na umri usiozidi miezi 3 ili wakue haraka na kuwa na

nyama nzuri,

• Wawekwe alama au namba za utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya

tano kwa ndama wote, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio, kwa ajili

ya urahisi wa udhibiti wa umiliki na utunzaji kumbukumbu,

• Ndama wachungwe eneo tofauti na ng’ombe wakubwa kuepuka

maambukizi ya minyoo na magonjwa; na

• Wapatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa na tiba wanapougua.

Utunzaji wa ndama baada ya kuachishwa kunyonya hadi kupevuka

(miezi 6 –24)

Ndama wa umri huu anatakiwa apatiwe:

• Malisho bora na maji safi ya kutosha wakati wote,

• Vyakula vya ziada ili kukidhi mahitaji ya mwili (mifano ya vyakula

mchanganyiko imeonyeshwa kwenye Jedwali Na. 3); na

• Tiba na kinga dhidi ya magonjwa, hususan kinga ya kutupa mimba (S19)

kwa ndama jike watakaotumika kuendeleza kundi.

Katika kipindi cha miezi 6 hadi 24, mfugaji anashauriwa kuchagua ndama

watakaoingizwa katika kundi la wazazi na wanaobaki wawe katika kundi la

kunenepesha kwa ajili ya nyama.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

14

Ng’ombe wa nyama mzazi

Apatiwe:-

• Malisho bora na maji safi ya kutosha wakati wote,

• Vyakula vya ziada (mifano ya vyakula mchanganyiko iliyooneshwa kwenye

Jedwali Na. 3), ili kukidhi mahitaji ya mwili,

• Vyakula vya ziada kiasi kisichopungua kilo 2 kila siku miezi 2 kabla ya

kuzaa,

• Nafasi ya kunyonyesha ndama kwa miezi 6 mfululizo,

• Tiba na kinga dhidi ya magonjwa; na

• Apandishwe kwa kutumia dume bora au kwa kutumia njia ya uhimilishaji

siku 60 baada ya kuzaa.

Unenepeshaji wa Ng’ombe wa nyama

Ng’ombe kwa ajili ya nyama anaweza kuchinjwa akiwa na umri wa kuanzia miezi 3

kulingana na mahitaji ya soko. Kwa kawaida hapa Tanzania ng’ombe huchinjwa

wakiwa na umri wa kuanzia miezi 18 kwa ng’ombe wa kigeni na zaidi ya miezi 36

kwa ng’ombe wa asili.

Ili mfugaji aweze kupata faida kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa nyama

anapaswa afanye yafuatayo:-

• Afuge aina ya ng’ombe wanaokua na kukomaa haraka,

• Anenepeshe ng’ombe kwa muda wa miezi 3 - 6 kabla ya kuchinjwa.

unenepeshaji huongeza ubora wa nyama na kipato kwa mfugaji,

• Awapatie chakula chenye mchanganyiko wenye viinilishe vya kutosha

viinilishe vya kutia nguvu na joto mwilini viwe na uwiano mkubwa kuliko

vingine (Jedwali Na 3),

• Auze ng’ombe mara wanapofikisha umri na uzito unaohitajika katika

soko ili kuepuka gharama za ziada.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

15

Jedwali Na. 3. Mfano wa Mchanganyiko wa Chakula kwa Ajili ya

Unenepeshaji

Aina ya Chakula Kiasi kwa Kilo

Majani makavu ya Mpunga/NganoHey 23.3

Molasis 44.72

Mahindi yaliyoparazwa 18.94

Mashudu ya Alizeti/Pamba 11.4

Madini mchanganyiko 0.7

Chumvi 0.47

Urea 0.47

Jumla 100

1.7 Uzalishaji na Uhifadhi wa Malisho Bora na Vyakula vya Ziada:

Chakula kikuu cha ng’ombe ni nyasi. Vyakula vingine ni pamoja na miti malisho,

mikunde na mabaki ya mazao. Ili kupata malisho misimu yote ya mwaka ni

muhimu kuvuna na kuhifadhi malisho kipindi yanapopatikana kwa wingi.

Inawezekana kupanda malisho mengi kuliko kiasi kinachohitajika msimu

mmoja/wakati wa mvua, kuyavuna yanapofikia hatua ya kutoa maua na

kuyahifadhi (mfano wa malisho yanayoweza kupandwa ni mabingobingo,

guatemala, African fox-tail, desmodium, centrosema, lukina n.k). Malisho ya

kupandwa ni vizuri yawe na mchanganyiko wa jamii ya nyasi, mikunde na miti

malisho.

Masalia ya Mazao Shambani

Masalia ya mazao shambani kama vile mabua, magunzi, majani ya mikunde, viazi,

ndizi, mpunga, na mengineyo yanaweza kukusanywa na kuhifadhiwa vizuri kama

chakula cha ng’ombe.

Malisho ya Miti na Matunda Yake

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

16

Malisho yatokanayo na miti ya malisho na matunda yake yanaweza kutumika

kama malisho ya ng’ombe. Majani na matunda ya miti ya lukina, sesibania,

migunga na mbaazi yanaweza kukaushwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kulisha

ng’ombe.

1.7.1 Vyakula vya Ziada

Ili kukidhi mahitaji ya viinilishe kulingana na kiwango cha uzalishaji, ng’ombe

anatakiwa kupewa vyakula vya ziada. Vyakula hivyo vinatokana na mchanganyiko

wa vyakula mbalimbali. Michanganyiko hii inategemeana na upatikanaji wa

malighafi katika maeneo husika. Mifano ya mchanganyiko huo ni kama ifuatavyo:-

Jedwali Na. 4: Mfano wa Kwanza wa Chakula cha Ziada

Aina ya chakula Kiasi (kilo)

Pumba za mahindi 47

Mahindi yaliyoparazwa 20

Mashudu ya alizeti/pamba 20

Unga wa lukinaa 10

Chokaa ya mifugo 2

Chumvi 1

Jumla 100

Mfano wa pili wa chakula cha ziada ni tofali la kulamba lenye urea ambalo

mchanganyiko wake ni:-

Unga wa mahindi Kilo 1

Pumba za mahindi Kilo 3

Urea kilo 1

Mashudu ya alizeti kilo 2

Chumvi ya kawaida gramu 200

Unga wa mifupa gramu 200

Chokaa ya mifugo kilo 1.5

Saruji kilo 1

Mfugaji anatakiwa kuzingatia yafuatayo ili kupata tija katika ufugaji bora:-

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

17

• Kulisha mchanganyiko wa nyasi, mikunde na mchanganyiko wa madini na

vitamini,

• Kutenga maeneo kwa ajili ya kulisha ng’ombe kwa mzunguko pamoja na

kupanda malisho katika mfumo huria na nusu huria; na

• Kuvuna nyasi na mikunde inapofikia hatua ya kutoa maua na kuyahifadhi

kwa matumizi wakati wa uhaba wa malisho, hususan wakati wa kiangazi.

1.7.2 Njia za Kuhifadhi Malisho

Malisho yanaweza kuhifadhiwa kwa kuyakausha (Hei) au kuyavundika (Saileji).

Hei

Hei ni majani yaliyohifadhiwa kwa kukaushwa baada ya kukatwa au kuachwa

kukauka yakiwa shambani kwa matumizi ya baadaye. Katika kutengeneza hei

yafuatayo yazingatiwe:

Sileji

• Vuna malisho yanapoanza kutoa maua,

• Yaanikwe kwa siku 3 hadi 6 kutegemea aina ya malisho na hali ya

hewa na yageuze mara 1 au 2 kwa siku ili yakauke vizuri,

• Yafungwe katika marobota baada ya kukauka – inawezekana

kutumia kasha la mbao lenye vipimo vifuatavyo:- Urefu sentimeta

75, upana sentimeta 45, na kina sentimeta 35 au mashine na zana

za kufunga marobota ya hei; na

• Hifadhi marobota juu ya kichanja ili kuzuia maji yasiingie, unyevu na

kuharibiwa na wadudu.

Sileji ni majani yaliyokatwakatwa na kuvundikwa. Madhumuni ya kuyavundika ni

kuyawezesha kubaki na ubora wake hadi wakati yatakapotumika. Katika

kutengeneza sileji yafuatayo yazingatiwe:-

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

18

• Tengeneza sileji kwa kutumia majani yenye sukari nyingi kama

mahindi au mabingobingo na mikunde , mabaki ya viwandani kama

molasis,

• Andaa shimo au mfuko wa plastiki kulingana na kiasi cha majani

yaliyovunwa,

• Vuna majani ya kuvundika katika umri wa kuanza kutoa maua.

Endapo majani yaliyovunwa ni teketeke, yaachwe kwa siku moja

yanyauke kupunguza kiwango cha maji,

• Katakata majani uliyovuna katika vipande vidogovidogo,

• Tandaza majani uliyokatakata ndani ya shimo au mfuko katika

tabaka nyembamba na kushindilia ili kuondoa hewa yote,

• Funika shimo ulilojaza majani kwa plastiki ikifuatiwa na udongo,

• Sileji itakuwa tayari kutumika kuanzia siku 21; na

• Sileji iliyofunguliwa kwa ajili ya matumizi ifunikwe haraka

iwezekanavyo ili kuzuia kuharibika.

Sileji inaweza kubaki na ubora katika shimo kwa muda mrefu kama haitafunguliwa

na kuachwa wazi kwa muda mrefu.

1.8 Udhibiti wa magonjwa ya ng’ombe

Magonjwa huweza kusababishwa na matunzo hafifu, lishe duni na visababishi vya

magonjwa kama vile protozoa, bakteria, virusi, riketsia na minyoo. Aidha, wadudu

kama kupe na mbung’o wanasambaza visababishi vya magonjwa.

Afya bora ya ng’ombe inatokana na kuzingatia mambo yafuatayo:-

• Ndama apate maziwa ya awali (dang’a) ya kutosha kwa siku 3-4 baada ya

kuzaliwa ili kuongeza kinga ya magonjwa mwilini,

• Chovya kitovu cha ndama ndani ya madini joto (Tincture of Iodine) mara

baada ya kuzaliwa kuzuia kuvimba kitovu. Ugonjwa huu huwapata ndama

kutokana na kitovu kutokauka au kutohudumiwa ipasavyo mara baada ya

ndama kuzaliwa. Kitovu huvimba na kutoa usaha, hukojoa kwa shida na

wakati mwingine huvimba viungo,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

19

• Ndama apewe dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 kama

atakavyoshauri mtaalam wa mifugo. Minyoo huwashambulia ndama zaidi

hasa wale walioanza kula majani,

• Zingatia usafi wa vyombo na banda, epuka kumpa ndama maziwa

yaliyopoa na machafu ili kuzuia kuharisha,

• Zingatia ujenzi wa mabanda kuruhusu mzunguko wa hewa ili kuzuia ndama

kupata ugonjwa wa vichomi. Vichomi huwapata ndama wa umri wa miezi 5

au zaidi wanaofugwa ndani katika mabanda machafu yasiyo na mzunguko

wa hewa ya kutosha,

• Ogesha ng’ombe kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo ili kuua kupe

wote wanaoleta magonjwa yatokanayo na kupe (ndigana kali na baridi,

kukojoa damu na maji moyo) na mbung’o (ndorobo); na

• Ng’ombe wapatiwe chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali. Chanjo muhimu

ni za ugonjwa wa kutupa mimba, kimeta, ugonjwa wa miguu na midomo na

chambavu.

Mfugaji anashauriwa kutoa taarifa kwa mtaalamu wa mifugo anapoona

ng’ombe wake ana baadhi ya dalili zifuatazo:-

• Joto kali la mwili na manyoya kusimama,

• amepunguza hamu ya kula,

• amezubaa na kutoa machozi,

• anasimama kwa shida na kusinzia,

• anapumua kwa shida na pua kukauka,

• anatokwa na kamasi nyingi,

• anajitenga na kundi,

• anakonda,

• Anapunguza utoaji wa maziwa ghafla.

1. 9 Kumbukumbu na Takwimu Muhimu

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

20

Kumbukumbu ni taarifa au maelezo sahihi yaliyoandikwa kuhusu matukio muhimu

ya kila ng’ombe na shughuli zote zinazohusiana na ufugaji. Mfugaji anashauriwa

kuweka kumbukumbu na takwimu muhimu katika shughuli zake za ufugaji wa

ng’ombe. Kumbukumbu zinamsaidia mfugaji kujua mapato na matumizi na

kufanya maamuzi sahihi kuhusu mifugo husika na mazao yake. Aidha,

humwezesha kuweka mipango ya shughuli zake. Mfugaji anapaswa kuweka

kumbukumbu muhimu zifuatazo:-

• Uzazi (uhimilishaji na matumizi ya dume, tarehe ya kupandwa, kuzaa,

kuachisha kunyonya)

• kinga na tiba

• utoaji wa maziwa

• Ukuaji

• Idadi ya ng’ombe kwa makundi – majike, ndama, mitamba, madume,

maksai.

• Kiasi na aina ya chakula

• Mapato na matumizi

• Kumbukumbu za manunuzi ya vifaa

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

21

SURA YA PILI

2. 0 KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA MBUZI NA KONDOO

Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu na kuishi katika

mazingira magumu kama ya maradhi na ukame ikilinganishwa na ng’ombe.

Kutokana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na pia

wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvukazi na kipato kidogo. Uzao wa

muda mfupi unamwezesha mfugaji kupata mbuzi/kondoo wengi kwa kipindi kifupi.

Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi, sufu na mazao

mengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato. Ufugaji bora wa mbuzi na

kondoo uzingatie kanuni zifuatazo:-

i) Wafugwe kwenye banda au zizi bora,

ii) Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na lengo la uzalishaji

(nyama, maziwa au sufu),

iii) Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili,

iv) Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa kama inavyoshauriwa na

mtaalam wa mifugo,

v) Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za uzalishaji; na

vi) Kuzalisha nyama, maziwa au sufu yenye ubora unaokidhi mahitaji ya

soko

Kondoo Mbuzi

2.1 Zizi au Banda la Mbuzi/Kondoo

Mbuzi/kondoo wanaweza kufugwa katika mifumo ya huria, shadidi na kwa

kutumia njia zote mbili. Zizi hutumika katika mfumo huria ambapo mbuzi/kondoo

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na 22

kujiongezea kipato

huchungwa wakati wa mchana na kurejeshwa zizini wakati wa usiku. Zizi bora ni

lile lenye sifa zifuatazo:-

• Lililo imara linaloweza kumkinga mbuzi/kondoo dhidi ya wanyama hatari na

wezi,

• Lililojengwa mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama,

• Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo. Ni vema mbuzi/kondoo

watengwe kulingana na umri wao; na

• Liruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.

Pale ambapo mbuzi/kondoo wanafugwa kwa mfumo wa shadidi hufugwa katika

banda wakati wote. Banda bora la mbuzi/kondoo linatakiwa kuwa na sifa

zifuatazo:-

• Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa

hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama

hatari,

• Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika

kwa urahisi,

• Lijengwe sehemu isiyoruhusu maji kutuama na liwe mbali kidogo na

nyumba ya kuishi watu. Pia ujenzi uzingatie mwelekeo wa upepo ili hewa

kutoka bandani isiende kwenye makazi,

• Liwe na sakafu ya kichanja chenye urefu wa mita 1 kutoka ardhini (Kwa

banda la mbuzi),

• Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji na mahali pa kuweka jiwe la

chumvichumvi; na

• Liwe na vyumba tofauti kwa ajili ya majike na vitoto, mbuzi/kondoo

wanaokua, wanaonenepeshwa na wanaougua.

2.1.1 Vifaa vya Kujengea na Vipimo vya Banda

Inashauriwa banda la mbuzi/kondoo lijengwe kwa kutumia vifaa vinavyopatikana

kwa urahisi katika eneo husika. Ukubwa wa banda utategemea idadi ya

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

23

mbuzi/kondoo wanaofugwa humo na ukubwa wa umbo kama inavyoonekana

kwenye Jedwali Na. 5

Jedwali Na 5: Eneo la mbuzi/kondoo linalotakiwa

Kundi la Mbuzi/Kondoo Eneo kwa Mnyama Mmoja

(Mita 2 )

Vitoto 0.3

Wasio na mimba 1.5

Wenye mimba 1.9

Dume 2.8

• Paa lijengwe kwa kutumia vifaa kama miti, mbao, na kuezekwa kwa nyasi,

makuti, majani ya migomba, mabati au hata vigae kwa kutegemea uwezo

wa mfugaji,

• Kuta zijengwe kwa kutumia mabanzi, mbao, nguzo, wavu wa waya, fito na

matofali. Kuta ziwe imara zinazoruhusu hewa na mwanga wa kutosha.

Mlango uwe na ukubwa wa sentimita 60 x 150,

• Sakafu inaweza kuwa ya udongo au zege. Sakafu ya kichanja inaweza

kujengwa kwa kutumia miti, fito, mianzi, mbao au mabanzi na iweze

kuruhusu kinyesi na mkojo kupita. Chumba cha majike na vitoto kiwe na

nafasi ya sentimita 1.25 kati ya papi na papi, fito na fito au mti hadi mti.

Chumba cha mbuzi/kondoo wakubwa iwe sentimita 1.9 kati ya mbao na

mbao.

2.2 Uchaguzi wa Mbuzi/Kondoo wa Kufuga

Madhumuni ya kuchagua mbuzi au kondoo wa kufuga ni kuboresha uzalishaji na

kuendeleza kizazi bora. Kuna aina nyingi za mbuzi/kondoo wanaoweza kufugwa

kulingana na mazingira na mahitaji ya mfugaji. Uchaguzi hufanyika kwa kuangalia

umbile, uzalishaji na kumbukumbu za wazazi kama vile umbo kubwa, ukuaji wa

haraka, uwezo wa kutunza vitoto na kutoa maziwa mengi.

Mbuzi wanaofaa kwa ajili ya maziwa ni aina ya Saanen, Norwegian na Toggenburg

pamoja na chotara wao.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

24

Mbuzi wanaofaa kwa ajili ya nyama ni Boer na chotara wao, mbuzi wa asili kama

vile Pare white, Newala na Ujiji. Mbuzi aina ya Malya (Blended) wanafaa kwa ajili

ya nyama na maziwa.

Aidha, kondoo aina ya Black Head Persian (BHP), Masai red, Suffolk na Hampshire

wanafaa kufugwa kwa ajili ya nyama. Merino na Lincoln hufugwa kwa ajili ya sufu,

wakati Corriedale na Romney hufugwa kwa ajili ya nyama na sufu. Hapa Tanzania

kondoo wanaopatikana kwa wingi ni Black Head Persian, Masai Red Dopper na

kondoo wengine wa asili.

Mbuzi/kondoo jike wanaofaa kwa ajili ya kuzalisha maziwa na nyama wawe na sifa

zifuatazo:-

• Historia ya kukua upesi, kuzaa (ikiwezekana mapacha) na kutunza vitoto

vizuri,

• Umbo la mstatili linaloashiria utoaji wa nyama nyingi; na

• Asiwe na ulemavu wa aina yoyote

Sifa za Ziada kwa Mbuzi wa Maziwa

• Awe na miguu ya nyuma iliyo imara na iliyonyooka na yenye nafasi kwa ajili

ya kiwele; na

• Awe na kiwele kikubwa na chuchu ndefu zilizokaa vizuri

Sifa za Dume

Dume bora awe na sifa zifuatazo:-

• Miguu iliyonyooka, imara na yenye nguvu,

• Asiwe na ulemavu wa aina yoyote,

• Mwenye uwezo na nguvu ya kupanda; na

• Mwenye kokwa mbili zilizo kaa vizuri na zinazolingana

Angalizo: Dume lichaguliwe kwa makini kwa sababu “dume ni nusu ya

kundi”.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

25

2.3 Utunzaji wa Vitoto vya Mbuzi/Kondoo

Utunzaji huanza mara tu baada ya kuzaliwa.

Mfugaji ahakikishe:-

• Kitoto cha mbuzi/kondoo kinapata maziwa ya mwanzo (dang’a) ndani ya

masaa 24 tangu kuzaliwa na kwa muda wa siku 3,

• Kama kinanyweshwa maziwa, kipewe lita 0.7- 0.9 kwa siku. Maziwa haya, ni

muhimu kwani yana viinilishe na kinga dhidi ya magonjwa,

• Iwapo mama hatoi maziwa au amekufa, inashauriwa kutengeneza dang’a

mbadala au kama kuna mbuzi/kondoo mwingine aliyezaa anaweza kusaidia

kukinyonyesha kitoto hicho,

• Kitoto cha mbuzi/kondoo kiendelee kunyonya kwa wiki 12 - 16. Wiki 2 baada

ya kuzaliwa, pamoja na maziwa, kianze kupewa vyakula vingine kama nyasi

laini na chakula cha ziada ili kusaidia kukua kwa tumbo. Aidha, kipewe maji

wakati wote,

• Vyombo vinavyotumika kulishia vinakuwa safi muda wote,

• Kitoto cha mbuzi/kondoo kiachishwe kunyonya kikiwa na umri wa miezi 3 hadi

4 kutegemea afya yake; na

• Vitoto vipatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam

wa mifugo.

2.3.1 Matunzo Mengine

Utambuzi

Mbuzi huwekewa alama ili atambulike kwa urahisi na kuwezesha utunzaji wa

kumbukumbu zake. Shughuli hii hufanyika kwa mbuzi/kondoo akiwa na umri wa

siku 3 - 14. Njia zitumikazo ni pamoja na:

• Kuweka alama sikioni kwa kukata sehemu ndogo ya sikio,

• Kumpa jina kwa wafugaji wenye mbuzi wachache,

• Kumvisha hereni ya chuma au plastiki yenye namba kwenye sikio,

• Kumvalisha mkanda wenye namba shingoni; na

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

26

• Kuweka namba kwa kuunguza sehemu ya ngozi ya mbuzi. Pale mfugaji

anapotumia njia hii inashauriwa aweke alama kwenye eneo ambalo

halitaathiri ubora wa ngozi

Kuondoa vishina vya pembe

Mbuzi/kondoo aondolewe vishina vya pembe akiwa na umri kati ya siku 3 hadi 14.

Visipoondelewa hukua na kusababisha kuumizana na kuhitaji nafasi kubwa

kwenye banda. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo.

Kuhasi

Vitoto vya mbuzi/kondoo ambavyo havitatumika kwa ajili ya kuendeleza kizazi

vihasiwe kabla ya kufikia umri wa miezi 3. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo.

2.4 Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo wa Miezi 4 - 8

Mbuzi wa miezi 4 mpaka 8 ni wale ambao wameacha kunyonya mpaka umri wa

kupandishwa kwa mara ya kwanza. Mbuzi wa umri huu wana uwezo wa kula aina

mbalimbali za malisho kama nyasi, mikunde, miti malisho na mabaki ya mazao

wakati kondoo hupendelea zaidi nyasi fupi. Wakati wa kiangazi huhitaji kupatiwa

chakula cha ziada au kupewa pumba za nafaka mbalimbali, mashudu ya alizeti,

pamba na dengu, majani ya mikunde yaliyokaushwa, madini na vitamini.

Katika ufugaji huria ni vema kuzingatia idadi ya mbuzi/kondoo inayoweza

kuchungwa katika eneo, aina na hali ya malisho.

Ili mbuzi/kondoo aweze kukua na kufikia uzito wa kuchinjwa/kupevuka mapema,

mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora zifuatazo:-

• Kumpatia vyakula vya ziada kwa muda wa miezi 2 mfululizo kiasi cha kilo 0.2 –

0.7 kwa siku kuanzia anapoachishwa kunyonya,

• Kumpatia dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 na kutoa kinga za

magonjwa mengine kama itakavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

27

• Kuchanja na kuogesha ili kuzuia magonjwa mbalimbali,

• Kukata kwato mara zinapokuwa ndefu; na

• Kuhasi madume yasiyotumika kuzalisha.

2.5 Umri wa Kupandisha Mbuzi/Kondoo

Mbuzi/kondoo wakitunzwa vizuri wanaweza kupandishwa wakiwa na umri wa

miezi 8 hadi 12 kwa mbuzi/kondoo walioboreshwa na miezi 18 hadi 24 kwa mbuzi

wa asili kutegemea afya yake. Hata hivyo, inashauriwa wapandishwe wanapofikia

uzito wa kilo 12 au zaidi na wasipandishwe mbuzi/kondoo wa ukoo mmoja.

Dalili za joto

Mfugaji anashauriwa asimpandishe jike kabla hajafikisha umri wa kupandwa wa

miezi 8 hadi 12 kwa mbuzi/kondoo walioboreshwa na miezi 18 hadi 24 kwa mbuzi

wa asili hata kama ataonyesha dalili ya kuhitaji dume. Mbuzi/kondoo aliyezaa

anaweza kupandishwa siku 30-60 baada ya kuzaa. Mbuzi/kondoo aliyeko kwenye

joto huonyesha dalili zifuatazo:-

• Hutingisha/huchezesha mkia,

• Hupanda na kukubali kupandwa na wengine,

• Hutoa ute mweupe ukeni,

• Huhangaika mara kwa mara na kupiga kelele,

• Hufuata madume,

• Hamu ya kula hupungua,

• Hukojoa mara kwa mara,

• Uke huvimba na huwa mwekundu kuliko ilivyo kawaida; na

• Kwa mbuzi anayekamuliwa hupunguza kiwango cha maziwa

Mbuzi/kondoo apelekwe kwa dume mara tu dalili za joto zinapoonekana kwani

joto hudumu kwa wastani wa siku 2 (saa 48). Chunguza tena dalili za joto baada

ya siku 19 hadi 21 na kama dalili hazitaonekana tena kuna uwezekano mkubwa

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

28

kuwa mbuzi/kondoo amepata mimba. Mfugaji apange msimu mzuri wa

mbuzi/kondoo kuzaa. Msimu mzuri ni mara baada ya mvua.

2.6 Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo Mwenye Mimba

Kwa kawaida mbuzi/kondoo hubeba mimba kwa muda wa miezi 5. Utunzaji wa

mbuzi/kondoo mwenye mimba ni muhimu kwani ndiyo chanzo cha kupata vitoto

vyenye afya bora. Mfugaji anashauriwa kufuata kanuni zifuatazo:

• Apatiwe vyakula vya ziada kilo 0.2 – 0.7 kwa siku ili kutosheleza mahitaji

yake na kitoto kinachokua tumboni,

• Apatiwe nyasi, miti malisho na mikunde mchanganyiko kilo 1.8 – 2.5 kwa

siku.

Dalili za Mbuzi/Kondoo Anayekaribia Kuzaa

• Huhangaika kwa kulala na kuamka mara kwa mara,

• Sehemu ya nje ya uke hulegea,

• Hujitenga na kundi na hutafuta sehemu kavu na yenye kivuli,

• Hupiga kelele; na

• Hutokwa na ute mzito ukeni.

Mfugaji akiona dalili hizi anashauriwa asimruhusu mbuzi/kondoo kwenda

machungani, bali amtenge kwenye chumba maalum, ampatie maji ya kutosha na

kumuandalia sehemu ya kuzalia.

2.7 Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo Anayenyonyesha

Mbuzi/kondoo anayenyonyesha huhitaji chakula kingi zaidi ili kukidhi mahitaji ya

mwili na kuzalisha maziwa kwa ajili ya kitoto/vitoto. Pamoja na nyasi, mikunde na

majani ya miti malisho kilo 1.8 – 2.5 kwa siku ni muhimu apewe chakula cha

nyongeza kilo 0.3 – 0.8 kwa kila lita ya maziwa inayoongezeka baada ya lita 2 na

maji safi, salama na ya kutosha wakati wote.

Taratibu za Kuzingatia Katika Ukamuaji wa Mbuzi wa Maziwa

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

29

Lengo la ufugaji wa mbuzi/kondoo wa maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na

salama pamoja na mazao yatokanayo na maziwa. Mambo muhimu ya kuzingatia

ni:-

• Sehemu ya kukamulia iwe safi na yenye utulivu,

• Mbuzi/kondoo awe na afya nzuri, msafi, na kiwele kioshwe kwa maji safi ya

uvuguvugu,

• Mkamuaji asibadilishwe badilishwe awe msafi, mwenye kucha fupi na asiwe

na magonjwa ya kuambukiza,

• Vyombo vya kukamulia viwe safi; na

• Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo

maalum (strip cup) ili kuchunguza ugonjwa wa kiwele.

2.8 Utunzaji wa Dume Bora la Mbegu

Dume bora la mbegu ni muhimu litunzwe ili liwe na uwezo wa kutoa mbegu bora,

kupanda na kuzalisha. Dume bora huanza kupanda akiwa na umri kati ya miezi.8 -

10 kwa mbuzi walioboreshwa. Katika msimu wa kupandisha dume moja liruhusiwe

kupanda majike 40 hadi 50. Aidha, inashauriwa madume wenye umri wa miezi 8 –

9 waruhusiwe kupanda majike ambao ndio mara ya kwanza kupandwa.

Dume apatiwe:-

• Malisho ya kutosha na vyakula vya ziada kiasi kisichopungua kilo 0.2 – 0.7

kwa siku na maji ya kutosha,

• Majani ya miti malisho, mikunde na nyasi mchanganyiko na mabaki ya

mazao; na

• Kilo 0.45 hadi 0.9 za chakula cha ziada za nyongeza kwa siku kulingana na

uzito wake na wingi wa majike anayopanda.wiki 2 kabla na baada ya

kuanza kupanda.

2.9 Matunzo Mengine

Kukata Mkia

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

30

Mara nyingine kondoo hukatwa mkia ili kuruhusu mtawanyiko mzuri wa mafuta

katika misuli mwilini. Pia kondoo aliyekatwa mkia huwa msafi. Kazi hii ifanywe

kama itakavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo kwa kutumia vyombo maalum.

Inashauriwa mkia ukatwe urefu wa sentimita 2.5 – 3.8 kutoka kwenye shina la

mkia wakati kondoo akiwa na umri wa siku 3 mpaka mwezi 1.

Kumnyoa Kondoo wa Sufu

Sufu hunyolewa wakati kondoo akiwa hai au amechinjwa. Kwa kawaida

hunyolewa miezi 6 hadi mwaka 1 ambapo sufu huwa imefikia urefu wa sentimita

15 – 20. Vifaa vinavyotumika ni pamoja na mikasi au visu maalum. Uangalifu

unahitajika wakati wa kunyoa ili ngozi ya kondoo isiharibike. Unyoaji ufanyike

wakati wa kiangazi na siyo wakati wa mvua, kondoo akiwa na mimba au kipindi

cha majani kutoa mbegu.

2.10 Udhibiti wa Magonjwa ya Mbuzi na Kondoo

Magonjwa husababishwa na vimelea jamii ya virusi, bakteria, protozoa na riketsia.

Magonjwa mengine husababishwa na upungufu wa viinilishe, vitamini na protini.

Dalili za mbuzi/kondoo mgonjwa ni pamoja na:-

� Manyoya husimama,

� Kuzubaa, kusinzia, kukohoa na kupiga chafya,

� Kukosa hamu ya kula na kunywa maji,

� Kujitenga na kundi,

� Kuvimba taya la chini,

� Kupumua kwa shida,

� Kutokwa na machozi na makamasi,

� Kuwa na upele au uvimbe kwenye sehemu ya mwili; na

� Kutupa mimba.

• Hatua za haraka za kumuona mtaalamu wa mifugo zichukuliwe iwapo

baadhi ya dalili hizi zitaonekana,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

31

• Mbuzi na kondoo wachanjwe dhidi ya magonjwa ya homa ya maapafu.

Ugonjwa huu ni hatari sana na huenea kwa njia ya hewa na unaweza

kusababisha vifo kati ya asilimia 60-100,

• Kila baada ya miezi 6 mifugo ipatiwe kinga dhidi ya ugonjwa wa miguu na

midomo na magonjwa mengine kama Kimeta, bonde la ufa, kutupa mimba

na chambavu (BQ) zitolewe kulingana na ushauri wa mtalaam wa mifugo,

• Kama kuna wanyama walioathirika watengwe kwenye kundi, wasisafirishwe

au kuuzwa,

• Mbuzi/kondoo wapatiwe dawa ya minyoo. Vitoto vya mbuzi/kondoo

vipatiwe dawa ya minyoo vinapofikia umri wa mwezi 1. viendelee kupatiwa

dawa ya minyoo kila mwezi hadi vinapofikia miezi 5 na baada ya hapo

vipatiwe dawa ya minyoo kila baada ya miezi 3 - 4; na

• Zingatia usafi wa banda ili kuwakinga na ugonjwa wa kuharisha na

kuharisha damu na magonjwa mbalimbali.

2.11 Utunzaji wa Kumbukumbu za Mifugo

Kuweka kumbukumbu za mifugo ni muhimu katika uzalishaji kwa ajili ya kutambua

kosaafu, gharama za utunzaji na faida. Pia, humsadia mfugaji kufanya maamuzi

katika uendelezaji wa ufugaji wake. Mtalaamu wa mifugo pia anaweza kutumia

kumbukumbu hizi ili kumsaidia mfugaji kuboresha ufugaji wake.

Kumbukumbu muhimu zinazohitajika kutunzwa ni:-

• Kumbukumbu za idadi na ukuaji wa wanyama waliopo, jinsi zao, uzito wa

mbuzi/kondoo kwa kila mwezi ili kufuatilia ukuaji wake, tarehe ya

kuachishwa kunyonya na idadi ya waliouzwa,

• Kumbukumbu ya uzazi zinazoonyesha tarehe ya kuzaliwa, namba yake, jinsi

yake, aina (breed), namba ya dume/jike, na uzito wa kuzaliwa,

• Kumbukumbu za upandishaji zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo

anayepandwa, tarehe ya joto na ya kupandwa, namba ya dume lililotumika

kupanda, tarehe ya joto la pili kama atarudia na tarehe ya kuzaa,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

32

• Kumbukumbu za chanjo na matibabu zinazoonyesha namba ya

mbuzi/kondoo, tarehe ya matibabu, aina ya chanjo au ugonjwa, dawa

iliyotumika, idadi ya waliokufa na waliopona na jina la mtaalam aliyetibu,

• Kumbukumbu za maziwa zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo, tarehe

ya kuzaa, kiasi cha maziwa kwa siku, na kiasi cha maziwa kwa kipindi chote

cha kukamuliwa, tarehe ya kuacha kukamua na idadi ya siku alizokamuliwa,

• Kumbukumbu za mapato na matumizi zinazoonyesha mapato na matumizi,

vitu vilivyouzwa au kununuliwa kwa siku, kiasi cha fedha unachokuwa

nacho kila wakati, kiasi cha fedha unachodai na kudaiwa.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

33

SURA YA TATU

3.0 KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA NGURUWE

Ufugaji wa nguruwe hapa nchini unaongezeka siku hadi siku kutokana na

kuongezeka kwa walaji wa nyama ya nguruwe. Ili kufuga kwa faida ni vyema

kufuata kanuni za ufugaji bora wa nguruwe.

Nguruwe huweza kufugwa katika mfumo huria au wa ndani (shadidi). Katika

mfumo huria, nguruwe huachwa huru kujitafutia chakula, hivyo ni lazima mfugaji

awe na eneo au ardhi ya kutosha, eneo lililo jitenga mbali na makazi ya watu.

Katika mfumo wa shadidi, nguruwe hufugwa ndani muda wote bila kutoka nje na

kupewa chakula na maji kufuatana na mahitaji ya kila kundi.

Nguruwe jike Nguruwe dume

3.1 Banda la nguruwe

Banda la nguruwe ligawanywe kulingana na makundi mbalimbali yanayofugwa.

Aidha, liwe na sehemu ya stoo na ya kuchanganyia chakula. Banda bora linatakiwa

kuwa na sifa zifuatazo:-

• Lijengwe mahali pasipo na upepo mkali,

• Kuta imara, zinazopitisha mwanga na hewa,

• Liwe na sehemu ya kufanyia mazoezi,

• Liwe kubwa la kutosha nguruwe kuchagua sehemu ya kupumzikia na sehemu

ya mkojo na kinyesi,

• Sakafu imara isiyoteleza, yenye mwinuko (2%) na isiyoruhusu maji kutuama;

na

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

34

• Paa lisilovuja

Vipimo vya wastani vya banda la nguruwe ni kama inavyoonyeshwa kwenye

Jedwali Na. 6

Jedwali Na.6: Nafasi Inayohitajika Kwa Makundi ya Nguruwe.

Sehemu /Kundi Eneo kwa Nguruwe

(Mita 2 )

Chumba cha nguruwe mwenye mimba 1.28

Sehemu ya mazoezi 3 hadi 4

Chumba cha kuzalia pamoja na kreti 6.2

Sehemu ya kunyonyeshea pamoja na sehemu

10

ya watoto

Chumba cha wasionyonyesha:

Sehemu ya kulala 0.4

Sehemu ya mazoezi 0.9

Nguruwe wanaokua (kilo 50 hadi 60) 0.73

Nguruwe wenye uzito zaidi ya kilo 90 0.93

Sehemu ya chakula kwa:

Nguruwe wa kunenepesha 0.2 hadi 0.3

Jike 0.35

3.2 Kuchagua Nguruwe wa Kufuga

Aina kuu za nguruwe wanaofugwa Tanzania ni nguruwe wa asili, Landrace,

Hampshire, Large White, Saddleback na machotara wao. Ili kuweza kupata mazao

mengi na bora ni muhimu kwa mfugaji kuchagua nguruwe wenye sifa zifuatazo:-

Jike:

• Awe na umbile la kumwezesha kubeba mimba na kuzaa kwa urahisi;

• Awe na chuchu zisizopungua 10 – 14 na zilizojipanga vizuri;

• Achaguliwe kutoka kwa wazazi wenye historia ya kuzaa watoto wengi,

kutoa maziwa mengi na utunzaji mzuri wa watoto; na

• Awe na miguu iliyonyooka, yenye nguvu na viungo imara.

Dume:

• Achaguliwe kutoka kwenye ukoo wenye historia ya kutokuwa na magonjwa

au ulemavu,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

35

• Awe na miguu imara, mchangamfu na mwenye afya bora,

• Awe na umbile zuri na misuli imara itakayomwezesha kupanda majike bila

matatizo,

• Awe mwenye kokwa mbili zinazoonekana na zilizokamilika; na

• Awe anayekua haraka.

3.3 Utunzaji wa Watoto wa Nguruwe

Watoto wa nguruwe hutunzwa kulingana na hatua ya ukuaji.

• Mara baada ya kuzaliwa watoto wawekwe mahali penye joto la kutosha na

wanyonye maziwa ya mwanzo. Maziwa hayo ni muhimu kwani yana

viinilishe vya kujenga mwili, kuleta nguvu na kuongeza kinga dhidi ya

magonjwa,

• Kama mama amekufa mara baada ya kuzaa au anakataa kunyonyesha na

hakuna nguruwe mwingine anayeweza kuwanyonyesha, watoto wapewe

dang’a ya ng’ombe au dang’a mbadala,

• Vitovu vikatwe na kuachwa sentimita 5 kwa kutumia vifaa safi, na kupaka

dawa ya joto (Tincture of Iodine) ili kuzuia viini vya magonjwa kupitia

kitovuni,

• Wachomwe sindano ya madini ya chuma au kupaka madini ya chuma

kwenye chuchu za mama wiki ya kwanza kwa kuwa maziwa na damu ya

watoto haina kiasi cha kutosha cha madini hayo muhimu kwa kutengeneza

damu mwilini. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo; na

• Meno anayozaliwa nayo yakatwe kwa kutumia mkasi mkali na safi. Meno

hayo humuumiza mama anaponyonyesha. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa

mifugo.

3.4 Utunzaji wa Watoto wa Nguruwe Wiki 1 - 8

Wiki moja baada ya kuzaliwa watoto wa nguruwe wapatiwe huduma zifuatazo:-

• Waendelee kupatiwa joto la kutosha hasa maeneo ya baridi kwa kutumia

chanzo chochote cha joto kama umeme, taa ya chemli au mkaa,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

36

• Wanyweshwe maji yenye madini ya chuma mililita 1.5 kwa kipindi cha

mwezi mmoja au kuwapa nafasi ya kula udongo msafi au vidonge vyenye

madini ya chuma pale ambapo njia ya sindano au ya kupaka chuchu

haikuwezekana,

• Walishwe chakula maalum cha kwanza cha watoto kidogo kidogo kuanzia

siku ya 10 baada ya kuzaliwa na waendelee kupewa chakula hiki na maji ya

kutosha mpaka siku ya kuachishwa kunyonya,

• Watoto vidume ambao hawahitajiki kwa ajili ya kuzalisha wahasiwe wakiwa

na umri kati ya wiki 3 hadi 6,

• Wawekwe alama za utambulisho kabla ya kuwatenganisha na mama yao

kwa kuwaweka namba kwenye masikio. Mfugaji anashauriwa kupata

ushauri wa mtaalam wa mifugo kuhusu kuweka alama za utambulisho; na

• Watoto waachishwe kunyonya kwa kutenganishwa na mama yao wakiwa

na umri wa wiki 8 kwa kumhamishia mama kwenye chumba kingine na

kuwaacha watoto kwenye chumba walichozaliwa.

3.5 Utunzaji wa Nguruwe Walioachishwa Kunyonya

Baada ya watoto wa nguruwe kuachishwa kunyonya ni muhimu kuzingatia

yafuatayo:-

• Hakikisha watoto wanapewa dawa ya minyoo, wanakingwa dhidi ya

magonjwa na kutibiwa mara wanapougua,

• Nguruwe walioachishwa kunyonya waanze kupewa chakula cha kukuza

kama ilivyoainishwa katika Jedwali Na. 7.

Jedwali Na. 7: Aina ya Chakula cha Kukuza Nguruwe

Aina Kilo

Pumba za mahindi 45

Mahindi yaliyosagwa 30

Mashudu ya pamba au Alizeti 15

Dagaa 3

Damu iliyokaushwa 5

Madini 2

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

37

JUMLA 100

• Badilisha chakula hatua kwa hatua kutoka chakula cha watoto kuingia

chakula cha kukuza. Lisha sehemu 3 /4 ya chakula cha watoto na 1 /4 ya

chakula cha kukuza kwa wiki ya kwanza, ongeza kufikia ½ kwa ½ wiki ya

pili na ya tatu iwe 1 /4 ya chakula cha watoto na 3 /4 ya chakula cha kukuzia.

Wiki ya 4 endelea kulisha chakula cha kukuza pekee.

• Kiasi cha chakula kinachotakiwa kulishwa nguruwe wanaokua ni kama

inavyoonyeshwa katika Jedwali Na. 7

Jedwali Na. 7: Kiasi cha Chakula kwa Nguruwe Wanaokua

Wiki Kiasi kwa siku (kilo)

8 - 12 1.0

12 -18 1.5

18 -23 2.0

23 -30 3.0

• Chakula kigawanywe na kulishwa mara 2 kwa siku pamoja na maji safi ya

kutosha wakati wote,

• Usafi wa chumba, vifaa na mazingira ni muhimu ufanyike kila siku,

• Viwepo vitu vya kuchezea kama minyororo au matairi mabovu ili watoto

waweze kufanya mazoezi, kuondoa upweke na kupunguza kupigana; na

• Mfugaji achague nguruwe kwa ajili ya kuendeleza uzalishaji wakiwa na umri

wa miezi 3 au zaidi. Wale wasiohitajika kuendelea kufugwa wachinjwe kwa

ajili ya nyama na mafuta wakifikia uzito wa kilo 60 hadi 90.

3.6 Utunzaji wa Nguruwe Jike Kutoka Kupevuka Hadi Kuzaa

Aina nyingi za nguruwe hupevuka wakiwa na umri wa miezi 5, hata hivyo si vema

kumpandisha wakati huo kwa kuwa atakuwa hajakomaa vizuri kimaumbile.

Inashauriwa kumpandisha atakapokuwa na umri wa miezi 8 hadi 9.

• Kabla ya kupandishwa nguruwe jike apewe kilo 2.5 hadi 3.0 za chakula kwa

siku,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

38

• Nguruwe jike apelekwe kwa dume pale tu akioonyesha dalili za joto

zifuatazo:-

� Kutopenda kula chakula,

� Kupiga kelele ovyo,

� Kuhangaika kila mara,

� Kupanda au kukubali kupandwa na nguruwe wenzake,

� Sehemu ya uke kuvimba na kuwa nyekundu,

� Kukojoa mara kwa mara na kutoa ute mweupe usiokatika ukeni; na

� Kutulia anapokandamizwa mgongoni.

Dalili hizi siyo lazima zionekane zote wakati mmoja hivyo ni muhimu mfugaji kuwa

mwangalifu na ili aweze kuzitambua kwa urahisi, chumba cha majike

yanayotarajiwa kupandwa kinatakiwa kiwe karibu na cha dume. Dalili hudumu kwa

muda wa siku 2 hadi 3 hivyo nguruwe apandishwe mara anapokuwa kwenye joto

na kurudia tena katika muda wa masaa 12.

3.6.1 Kutunza Nguruwe Mwenye Mimba

Mimba ya nguruwe huchukua miezi 3, wiki 3 na siku 3 (siku 114 hadi 119) hadi

kuzaa.

• Nguruwe jike mwenye mimba awekwe kwenye banda lenye nafasi, hewa na

mwanga na eneo la kutosha kwa ajili ya mazoezi ya mwili. Nguruwe mwenye

mimba anahitaji mazoezi zaidi ili kuimarisha miguu na misuli yake. Sehemu ya

uzio isiwe na unyevu kuepuka magonjwa, ikiwezekana kuwe na kivuli cha

kumkinga na jua kali,

• Chumba cha kuzalia kiandaliwe wiki 2 hadi 3 kabla ya nguruwe kuzaa.

Kiwekwe malalo na itengwe sehemu ambayo itahifadhi watoto wasilaliwe au

kukanyagwa na mama yao,

• Kiwe na sehemu ya kuweka chombo cha kuongezea joto, chakula na maji kwa

ajili ya watoto,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

39

• Nguruwe mwenye mimba anahitaji kupewa chakula kinacholeta nguvu na

kujenga mwili. Katika mwezi wa 1 apewe kilo 2 hadi 2.5 kwa nguruwe

mwenye afya nzuri, akiwa dhaifu apewe kilo 3 kwa kipindi cha wiki 3,

• Kuanzia siku 60 kabla ya kuzaa alishwe kilo 3.5 za chakula kwa siku. Siku ya 3

kabla ya kuzaa, chakula kipunguzwe hadi kufikia kilo 2 kwa siku. Siku ya kuzaa

asipewe chakula, apewe maji tu,

• Wiki 1 kabla ya kuzaa nguruwe aogeshwe vizuri kwa maji safi na sabuni. Baada

ya kuogeshwa anyunyiziwe dawa ili kuzuia wadudu wa ngozi na apewe dawa

ya minyoo; na

• Anapokaribia kabisa kuzaa awekwe kwenye chumba cha uzazi.

Dalili za Kuzaa

Dalili za kuzaa zinapoonekana awepo mwangalizi ili aweze kutoa msaada kama

utahitajika, hasa kwa nguruwe anayezaa kwa mara ya kwanza. Dalili za kuzaa ni:-

• Kiwele na chuchu huongezeka ukubwa kwa kujaa maziwa,

• Njia ya uke huvimba na kuwa nyekundu na mara nyingine hutoa maji

mazito,

• Nguruwe huhangaika na hupumua kwa nguvu,

• Maziwa yanaweza kutoka yenyewe kwenye chuchu,

• Hukojoa mara kwa mara,

• Hukusanya majani na kuandaa mahali pa kuzalia; na

• Tumbo linapwaya na baadhi ya majike hupoteza hamu ya kula.

3.6.2 Utunzaji wa Nguruwe Anayenyonyesha

Nguruwe anayenyonyesha anastahili kupatiwa matunzo muhimu kutokana na

mahitaji ya mwili na utoaji wa maziwa. Ili kukidhi mahitaji hayo mfugaji anapaswa

kuzingatia matunzo yafuatayo:-

• Mara baada ya nguruwe kuzaa ahakikishe kondo la nyuma la uzazi limetoka

lote, kwa kuhesabu vipande kulingana na idadi ya watoto. Endapo idadi

haikulingana, unashauriwa kumwona mtaalam wa mifugo aliyekaribu.

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

40

• Apatiwe chakula kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 8

Jedwali Na. 8: Kiwango cha Chakula kwa Siku

Idadi ya siku baada ya kuzaa Kiasi cha chakula kwa siku (kilo/

1 1

2 2

3 3

4 - 8 4

gram)

Siku ya 9 na kuendelea 3 na gram 333 kwa kila mtoto

Siku ya kuachisha kunyonya (siku ya

60)

• Apatiwe maji ya kutosha wakati wote; na

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

2

• Apunguze chakula mpaka kilo 2 kwa siku anapomtenganisha nguruwe na

watoto na amwongeze hadi kufikia kilo 3 kwa siku kutegemeana na afya ya

nguruwe.

Kumbuka nguruwe akilishwa chakula kingi, atanenepa sana na hatapata

mimba kwa urahisi baadae na akibahatika kupata mimba huweza kuharibika.

Akilishwa chakula kidogo hudhoofika, huzaa watoto dhaifu katika mimba

zinazofuata na hutoa maziwa kidogo.

3.7 Utunzaji wa Dume

Nguruwe dume anaweza kutumika kwa kupanda jike akiwa na umri wa miezi 8

hadi 9. Kwa umri huo anaruhusiwa kupanda jike 1 kwa wiki. Afikiapo miezi 10

anaruhusiwa kupanda majike 2 hadi 3 kwa wiki. Akiwa na umri wa mwaka 1 au

zaidi ana uwezo wa kupanda jike 1 kila siku kwa wiki 2 hadi 3 kisha apumzishwe

kwa muda wa wiki 2. Dume mwenye uzito mkubwa asitumike kupanda jike dogo

kwani anaweza kumvunja mgongo.

41

Katika utunzaji wa dume bora la mbegu ni muhimu kuzingatia yafuatayo:

• Dume aliyechaguliwa kwa ajili ya mbegu, atenganishwe na majike ili

kuepusha kupanda wakati usiotakiwa,

• Dume awe na eneo la mita za mraba 9.3 kwa ajili ya kupata mazoezi ya

mwili,

• Dume aogeshwe kwa dawa zinazoweza kuua wadudu na vimelea

vinavyoweza kusababisha magonjwa,

• Dume wa kupanda asinenepeshwe, hivyo alishwe chakula bora kiasi cha

kilo 2 hadi 3 kwa siku na maji ya kutosha; na

• Dume anayepanda majike chini ya mara 3 kwa wiki, alishwe kilo 2.5 za

chakula na kama anapanda zaidi ya mara 3, alishwe kilo 3 kwa siku.

3.8 Udhibiti wa Afya na Magonjwa ya Nguruwe

Mfugaji anatakiwa kujali afya ya nguruwe ili kupunguza vifo na gharama za

matibabu. Magonjwa yanayoshambulia nguruwe hapa nchini ni pamoja na Homa

ya Nguruwe, Ukurutu, Kichomi, Ugonjwa wa Midomo na Miguu, Kimeta, Mafua,

Ugonjwa wa kuhara hasa kwa nguruwe wachanga na minyoo. Dalili kuu za

nguruwe mgonjwa ni:-

• Hupoteza hamu ya kula

• Kutochangamka

• Kudhoofu

• Kukonda

• Kudumaa

• Kujisuguasugua na kunyonyoka manyoya

Mfugaji akiona mojawapo ya dalili hizo amwone mtalaam wa mifugo.

3.10 Kuweka na Kutunza Kumbukumbu

Kuweka kumbukumbu ni muhimu kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya uzalishaji na

pia humsadia mfugaji kufanya maamuzi katika kuendeleza ufugaji wake.

Kumbukumbu zinazowekwa zionyeshe:-

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

42

• Idadi ya nguruwe wanaofugwa kwa makundi mabalimbali

• Kiasi cha chakula kinachohitajika kwa kila nguruwe

• Uzito kila baada ya wiki 1 hasa kwa wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama

• Kumbukumbu za mapato na matumizi

• Kumbukumbu za uzazi kwa nguruwe jike ni kama:

� Aina ya nguruwe

� Namba ya nguruwe

� Tarehe ya kuzaliwa

� Dume lililotumika

� Tarehe ya kuzaa

� Idadi ya waliozaliwa, wazima na waliokufa

� Uzito wa watoto walipozaliwa, baada ya wiki 3 na baada ya wiki 8

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

43

SURA YA NNE

4.0 KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU.

Kaya nyingi hapa nchini hujihusisha na ufugaji wa kuku kwa lengo la kujipatia

chakula na kipato. Mazao yatokanayo na ufugaji wa kuku ni pamoja na mayai,

nyama, mbolea na manyoya kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Mifumo ya ufugaji

kuku ambayo hutumika hapa nchini ni huria, nusu huria na shadidi. Ufugaji wa

kuku utakuwa endelevu na wenye tija kwa kufuata kanuni za ufugaji bora

zifuatazo:-

• Kufuga kuku kwenye banda bora

• Kuchagua kuku bora wa kufuga

• Kutunza na kulisha kuku kulingana na hatua mbalimbali za ukuaji

• Kudhibiti na kutibu magonjwa ya kuku

• Kutunza kumbukumbu

4. 1 Banda la kuku

Kuku tafuta picha mbadala

Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Banda bora la

kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

• Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa

hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama

hatari,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

44

• Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa

urahisi,

• Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe

mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.

• Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala

• Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu

ya kulelea vifaranga

• Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo

vya chakula na maji

• Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa

wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa

• Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na

sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga

4.1.1 Vifaa vinavyotumika kwa ujenzi wa banda

Vifaa vya kujengea banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo

husika. Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-

• Sakafu Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito

• Kuta Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi,udongo, matofali, mawe,

mabati na wavu

• Paa Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati na vigae.

• Wigo Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi, mianzi, matete, wavu na

mabati

4.1.2 Ukubwa wa banda

Ukubwa wa banda utategemea idadi ya kuku na aina ya kundi la kuku. Kuku

wanahitaji nafasi tofauti kutegemea umri, aina, na njia ya ufugaji. Eneo la mita

moja ya mraba linatosha kwa vifaranga 16 wa umri wa wiki 1 - 4. Hivyo banda

lenye mita za mraba 16 linaweza kulea vifaranga 320 hadi wiki 4. Baada ya wiki 4

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

45

eneo hili liongezwe kutegemea aina ya kuku na njia inayotumika katika ufugaji

kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na. 9

Jedwali Na 9: Eneo Linalohitajika Kufuga Kuku Kwenye Sakafu ya

Umri wa kuku

Matandazo Kutegemea na Umri na Aina ya Kuku

Idadi ya kuku kwa mita 1 ya mraba

Kuku wa mayai Kuku wa nyama

Siku 1 hadi wiki 4 18 18

Wiki ya 5 hadi ya 8 9 9

Wiki ya 9 hadi 20 6 -

Wiki 21 na kuendelea 3 - 4 -

Angalizo:

Mabanda yanayozungushiwa wigo kama ilivyo katika mfumo wa nusu huria, kuku

mmoja huhitaji eneo la wazi lenye ukubwa wa mita za mraba 10. Mfano, kuku

100 huhitaji eneo la mita za mraba 1000

4. 1.3 Vifaa na Vyombo Muhimu

Mfugaji anashauriwa kutumia vifaa na vyombo maalum ili kurahisisha na

kuboresha utunzaji wa makundi mbalimbali ya kuku. Vifaa na vyombo

vinavyohitajika kwa ajili ya kuwekea chakula na maji, kutagia mayai na kupumzikia

vinapatikana kwenye maduka ya pembejeo za mifugo. Aidha, mfugaji anaweza

kutengeneza mwenyewe kwa kutumia malighafi zilizopo kwenye mazingira yake.

4.2 Kuchagua Kuku Bora wa Kufuga

4.2.1 Kuku wa Asili

Aina za kuku wa asili wanaopatikana hapa nchini ni pamoja na Kuchi (Kuza), Poni

(Kishingo), Njachama, Kinyavu, Mbuni na Tongwe (Msumbiji). Mfugaji anaweza

kuongeza uzalishaji kwa kuchagua kuku mwenye sifa zifuatazo:-

• Uwezo wa kutaga mayai mengi (kati ya 15-20) katika mzunguko mmoja wa

utagaji (Jedwali Na 10),

• Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

46

• Uwezo wa kustahimili magonjwa,

• Anayetoka maeneo yasiyo na magonjwa; na

• Umbo kubwa na kukua haraka.

Jedwali Na 10: Masuala ya Kuzingatia Wakati wa Kumchagua Kuku

Mtagaji wa Kienyeji

Viungo vya mwili Sifa

Macho Maangavu, yenye wekundu kwa mbali na makubwa

yamejaa kwenye soketi za macho.

Mdomo Wenye rangi ya njano kwa mbali

Kisunzu/upanga Chekundu, laini, kimelala kidogo upande na

kinang’aa

Shingo Iliyosimama

Umbali kati ya kidari na

nyonga

Upana wa vidole 3-4 vya mpimaji

Upana wa nyonga Upana wa vidole 3 vya mpimaji

4.2.2 Kuku wa Kisasa

Kuku bora wa kisasa kwa ajili ya mayai au nyama ni mwenye sifa zifuatazo:-

• Uwezo wa kuanza kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 5 - 6) kutegemea na

koo,

• Umbo kubwa na anayekua haraka (kilo 1.5-2.0 kwa kipindi cha wiki 8-12)

kutegemea na koo kwa kuku wa nyama,

• Anayetaga mayai mengi (250 au zaidi) kwa kuku wa mayai kwa mwaka; na

• Awe na uwezo wa kutaga katika umri wa miezi 6 - 8.

4.2.3 Kuchagua Jogoo Bora wa Mbegu

Jogoo wa mbegu anatakiwa awe na sifa zifuatazo:

• Achaguliwe kutoka kwenye koo zenye sifa ya kutaga mayai mengi,

• Mrefu, umbo kubwa, miguu imara na yenye nguvu,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

47

• Awe machachari, ushawishi kwa mitetea na ari ya kupanda; na

• Uwezo wa kupanda akiwa na umri wa miezi 7 – 10.

4.3 Mayai kwa Ajili ya Kutotoa Vifaranga

4.3.1 Uchaguzi wa Mayai

Mayai kwa ajili ya kutotoa vifaranga yawe na sifa zifuatazo:-

• Yaliyorutubishwa na jogoo,

• Yasiwe na nyufa,

• Yasiwe na maganda tepetepe,

• Yasiwe na kiini kilichovunjika,

• Yawe na ukubwa wa wastani; na

• Yasiwe yamekaa zaidi ya wiki 2 baada ya kutagwa.

4.3.2 Utunzaji wa Mayai

Mayai ya kienyeji kwa ajili ya kutotoa vifaranga yatunzwe kwa kusimamishwa

wima sehemu iliyochongoka ikiwa imeangalia chini kwa siku 3 za mwanzo na kisha

yageuzwe ili sehemu iliyo butu iangalie chini. Mayai yahifadhiwe kwenye sehemu

iliyo na ubaridi kidogo na giza.

4.4 Utunzaji wa Kuku kwa Makundi

4.4.1 Utunzaji wa Vifaranga

Malezi bora ya vifaranga ni muhimu katika ufugaji wa kuku kwa sababu vifaranga

hawana uwezo wa kustahimili mazingira wakiwa wenyewe mara wanapoanguliwa.

Ukosefu wa malezi bora husababisha vifaranga kuwa dhaifu, kufa kwa wingi na

hivyo kupunguza idadi ya kuku wa baadaye. Malezi ya vifaranga yanaweza

kufanyika kwa kutumia kuku walezi au kutumia vifaa maalum.

Kulea Vifaranga kwa Kutumia Kuku Mlezi

Vifaranga wanaweza kulelewa na mama yao au kuku mlezi. Endapo kuku wengi

wametotoa vifaranga kwa wakati mmoja, achaguliwe kuku mlezi aliye na uwezo

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

48

wa kulea vifaranga wengi kati ya waliototoa aendelee kulea na wengine waliototoa

waachwe huru ili warudi kwenye mzunguko wa kutaga. Kuku mmoja anaweza

kulea vifaranga 20 hadi 25. Mfugaji wa kuku, pamoja na kanuni nyingine,

anapaswa kuzingatia yafuatayo:-

• Kuku anayelea vifaranga atengewe chumba maalum, apewe maji ya

kutosha na chakula chenye virutubishi muhimu,

• Vifaranga wasiachiwe kutoka nje hadi watakapofika umri wa wiki 6,

• Vifaranga watengwe na mama/mlezi baada ya wiki 4 kuruhusu mama

aendelee na mzunguko wa kutaga; na

• Katika maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi vifaranga wacheleweshwe

kutenganishwa na mama/malezi hadi wiki ya 6 au mpaka waonekane

wameota manyoya ya kutosha.

Kulea Vifaranga kwa Kutumia Bruda

Bruda ni chombo/sehemu iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwapatia joto

vifaranga badala ya mama/mlezi. Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa

kutumia bruda ambayo ni mduara unaoweza kutengenezwa kwa kutumia mbao,

karatasi ngumu au kwa kuziba pembe za chumba. Aidha, njia hii hupunguza vifo

vya vifaranga vinavyosababishwa na ndege au wanyama hatari, huruhusu kuku

kutaga mapema zaidi na kuwa na mizunguko mingi ya utagaji (kwa kuku

wanaoatamia). Vilevile, hurahisisha udhibiti wa magonjwa.

Mfugaji anapaswa kufuata taratibu zifuatazo katika kulea vifaranga kwa kutumia

bruda:-

• Kuweka vifaa vya kuongeza joto kwa mfano taa ya umeme, chemli au jiko

la mkaa. Zingatia kiwango cha joto katika bruda kinachohitajika. Wiki ya

kwanza ni 35 o C, wiki ya pili ni 33 o C, wiki ya tatu ni 31 o C na wiki ya nne ni

29 o C,

• Kuchunguza mtawanyiko wa vifaranga ndani ya bruda ili kutathimini hali ya

joto. Wakijikusanya kwenye chanzo cha joto, inaashiria kuwa baridi imezidi

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

49

hivyo joto liongezwe. Wakiwa mbali na chanzo cha joto maana yake joto

limezidi hivyo joto lipunguzwe,

• Bruda iwe na sakafu yenye malalo yatokanayo na maranda ya mbao au

pumba za mpunga. Malalo yabadilishwe endapo yataonekana yameloana,

• Bruda iwekwe vifaa vya maji na chakula. Maji na chakula kiwekwe kabla ya

kuweka vifaranga,

• Vifaa vya joto viwekwe ndani ya bruda masaa 6 kabla ya kuingia vifaranga,

• Vifaranga walishwe chakula cha kuanzia gramu 12 - 15 kwa kipindi cha wiki

ya kwanza na gram 15 - 21 kwa kipindi cha wiki ya 2. Katika wiki ya 3

wapewe gramu 21 - 35 kwa kifaranga na chakula hicho kiwepo muda wote,

• Vifaranga wapatiwe vitamini, madini na dawa za kinga (antibiotics); na

• Vifaranga wapatiwe chanjo kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa

mifugo. Chanjo dhidi ya magonjwa muhimu kwa mfano, Marek’s (mara

anapototolewa), Mdondo (siku ya 3 - 4 na kurudiwa baada ya siku ya 21 na

kila baada ya miezi 3) na Gumboro (siku ya 7 na kurudia tena siku ya 21).

Wapatiwe dawa ya minyoo (wiki ya 8) na Coccidiosis ( wiki ya 3 - 4)

4.4.3 Kutunza Kuku Wanaokua (wiki 8 - 18)

Utunzaji wa kundi hili unategemea mfumo unaotumika.

Kuku Wanaofugwa Katika Mfumo Huria

Kuku wanaofugwa katika mfumo huu wapatiwe matunzo bora yakiwemo

yafuatayo;

• Wapewe chakula cha ziada asubuhi kabla ya kutoka na wanaporudi kwenye

banda. Chakula hicho kinaweza kugawanywa mara 2 kwa siku,

• Wapatiwe maji safi na ya kutosha wakati wote; na

• Wapatiwe chanjo na dawa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.

Kuku Wanaofugwa Katika Mfumo Shadidi

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

50

• Majogoo watenganishwe na mitetea katika wiki 7 hadi 10 ili kuzuia uzaliano

usio na mpangilio,

• Wapewe chakula cha kukuzia kuanzia wiki ya 8 - 15 gramu 55 - 60 na

kuanzia wiki ya 16 gramu 65 - 80 kwa wanaofugwa mfumo huria na gram

120- 125 kwa kuku kwa siku kwa wanaofugwa mfumo wa shadidi,

• Kuku wa nyama wapatiwe chakula cha kuku wa nyama muda wote,

• Wapatiwe maji safi ya kunywa kwa muda wote kwenye vyombo visafi,

• Kuku wachunguzwe dalili zozote za ugonjwa ili waweze kupata tiba sahihi

kutoka kwa mtaalamu wa mifugo,

• Kuku wa wiki 9 - 20 wanahitaji nafasi ya mita za mraba 0.15 kwa kuku na

wiki 21 au zaidi mita za mraba 0.2 kwa kuku,

• Kuwe na vyombo maalum vya kutosha kwa ajili ya chakula na maji

• Wafanyiwe usafi wa banda mara kwa mara ili kuzuia magonjwa

yanayotokana na uchafu; na

• Wakatwe midomo ili kuzuia kudonoana.

4.4.4 Kuku Wanaotaga

Mahitaji ya kuku wanaotaga ni tofauti na ya makundi mengine. Mambo ya

kuzingatia kwa kuku wanaotaga ni pamoja na:-

• Banda liwe na viota vya kutagia mayai (kiota 1 kwa kuku 3 - 5). Viota

viwekwe bandani mara kuku watakapofikisha umri wa wiki 18 ili waanze

kuzoea kuvitumia,

• Wapatiwe chakula na maji safi wakati wote kwa kutumia vyombo maalum

ambavyo ni visafi,

• Kuku wasiotaga waondolewe kwenye kundi. Kuku hao huonekana wasafi na

sehemu ya kutolea yai huwa ndogo na kavu, upanga wake kichwani (comb)

huwa mdogo na mwekundu,

• Wapewe dawa ya minyoo kila baada ya miezi 3,

• Wawekewe fito au ubao mwembamba kama sehemu ya kupumzikia na

mazoezi ili kuzuia kudonoana,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

51

• Mayai yakusanywe mara 4 au zaidi kwa siku ili yasidonolewe na kuku,

• Kuwe na malalo makavu na yabadilishwe mara yanapochafuka,

• Vyombo vifanyiwe usafi kila siku ili kuzuia magonjwa; na

• Watundikiwe majani mabichi aina ya mchicha, papai, alfaalfa, majani jamii

ya mikunde ili kuboresha lishe.

4.5 Udhibiti na Tiba Dhidi ya Magonjwa ya Kuku

Kuku wanaopata lishe bora, kutunzwa vizuri na kupatiwa chanjo dhidi ya

magonjwa yanayotokea mara kwa mara huwa na afya nzuri. Ni bora kuzuia

magonjwa kuliko kutibu ili kupunguza vifo na gharama. Iwapo ugonjwa utatokea

kuku wagonjwa watenganishwe na kuku wasio wagonjwa na wapatiwe tiba.

Kanuni muhimu za kufuata ili kuzuia magonjwa ni:-

• Banda liwe safi muda wote,

• Kabla ya kuweka kuku, banda linyunyiziwe dawa ya kuua wadudu wa

magonjwa mbalimbali,

• Kuku wakaguliwe kila siku ili kubaini wagonjwa au wenye matatizo,

kuwatenga na kutoa taarifa kwa mtaalam wa mifugo,

• Kuku wapatiwe chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali,

• Watu wasiohusika wasiingie eneo la kufugia kuku bila utaratibu,

• Ndege na wanyama wengine wasifike eneo la kufugia kuku,

• Banda la kufugia kuku litenganishwe na mabanda ya mifugo mingine,

• Lango la kuingilia katika banda la kuku liwekewe dawa ya kukanyaga kwa

wanaoingia ndani ili kuzuia kuingiza vimelea vya wadudu wa magonjwa; na

• Vifaa vya chakula na maji viwe safi wakati wote.

4.5.1 Dalili za Kuku Mgonjwa

Dalili za ujumla zinazoonekana kwa kuku mgonjwa ni kama zifuatazo:-

• Kuzubaa,

• Kupoteza hamu ya kula,

• Kujitenga na wenzake katika kundi; na

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

52

• Kupunguza au kusimama kutaga.

Mfugaji anapoona mojawapo ya dalili hizo amwone mtaalam wa mifugo

4.6 Ufugaji wa Aina Nyingine za Ndege

Aina ya ndege wengine wanaofugwa hapa nchini ni pamoja na Bata maji, Bata

bukini, Bata mzinga, Kanga na Njiwa. Ndege hao hufugwa kwa kiasi kidogo

ukilinganisha na kuku kwa kuwa soko lao ni dogo. Utunzaji wao hautofautiani sana

na kuku;

• Wajengewe banda la kuishi ambalo ukubwa wake utategemea idadi ya

ndege wanaofugwa,

• Wapatiwe chakula chenye virutubisho na maji ya kunywa ya kutosha,

• Wapatiwe kinga na tiba dhidi ya magonjwa,

• Bata maji na Bata bukini wajengewe bwawa lenye nafasi ya kutosha kwa

ajili ya kuogelea; na

• Njiwa wajengewe viota sehemu ya juu kama kwenye mapaa ya nyumba.

4.7 Utunzaji wa Kumbukumbu

Utunzaji wa kumbukumbu ni muhimu sana katika ufugaji wa kuku na ndege

wengine wafugwao ili kusaidia mfugaji kujua maendeleo ya ufugaji wake.

Utaratibu wa kuweka kumbukumbu mara tukio linapotokea ni lazima ili kuepuka

kusahau. Mfugaji ahakikishe anaweka kumbukumbu ambazo ni sahihi na

zinazoeleweka.

Aina za Kumbukumbu

Kumbukumbu zinazopaswa kuwekwa ni pamoja na:-

• Aina na idadi ya kuku waliopo kwenye kila kundi (mfano vifaranga, wanaokua,

wanaotaga, majogoo),

• Uzalishaji wa mayai kwa kundi la kuku waliopo,

• Utotoaji wa vifaranga,

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

53

• Kinga na matibabu,

• Mapato na matumizi,

• Utagaji wa kila kuku na utunzaji (kwa kuku wa asili); na

• Kumbukumbu za vifo.

UFUGAJI UNAOTUMIA KANUNI BORA ZA UFUGAJI HUONGEZA TIJA NA

KIPATO CHA MFUGAJI

Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama wa chakula na

kujiongezea kipato

54

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!