12.04.2023 Views

Kupinga ya Kiprotestanti

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Kupinga ya Kiprotestanti

Wapadri wakashtushwa kwa kufikiri kwamba watu wote wangeweza sasa kuzungumza

pamoja nao Neno la Mungu na kwamba ujinga wao wenyewe ungehatarishwa. Roma ikaalika

mamlaka yake yote kuzuia mwenezo wa Maandiko. Lakini kwa namna ilivyozidi kukataza

Biblia, ndivyo hamu ya watu ikazidi kujua ni nini iliyofundishwa kwa kweli. Wote walioweza

kusoma wakaichukua kwao na hawakuweza kutoshelewa hata walipokwisha kujifunza

sehemu kubwa kwa moyo. Mara moja Luther akaanza utafsiri wa Agano la Kale.

Maandiko ya Luther yakapokewa kwa furaha sawasawa katika miji na katika vijiji. “Yale

Luther na rafiki zake waliyoandika, wengine wakayatawanya. Watawa, waliposadikishwa juu

ya uharamu wa kanuni za utawa, lakini wajinga sana kwa kutangaza neno la Mungu ...

wakauzisha vitabu vya Luther na rafiki zake. Ujeremani kwa upesi ukajaa na wauzishaji wa

vitabu wajasiri.”

Kujifunza Biblia Mahali Pote

Usiku waalimu wa vyuo vya vijiji wakasoma kwa sauti kubwa kwa makundi madogo

yaliyokusanyika kando ya moto. Kwa juhudi yote roho zingine zikahakikishwa kwa ukweli.

“Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru; kunamupa mujinga ufahamu.” Zaburi 119:130.

Wakatoliki walioachia mapadri na watawa kujifunza Maandiko sasa wakawaalika kwa

kuonyesha uwongo wa mafundisho mapya. Lakini, wajinga kwa Maandiko, mapadri na

watawa wakashindwa kabisa. “Kwa huzuni,” akasema mwandishi mmoja mkatoliki, “Luther

alishawishi wafuasi wake kwamba haikufaa kuamini maneno mengine isipokuwa Maandiko

matakatifu.” Makundi yakakusanyika kusikia mambo ya kweli yaliyotetewa na watu wa elimu

ndogo. Ujinga wa hawa watu wakuu ukafunuliwa kwa kuonyesha uongo wa mabishano yao

kwa msaada wa mafundisho rahisi ya Neno la Mungu. Watumikaji, waaskari, wanawake, na

hata watoto, wakajua Biblia kuliko mapadri na waalimu wenye elimu.

Vijana wengi wakajitoa kwa kujifunza, kuchunguza Maandiko na kujizoeza wenyewe na

kazi bora ya watu wa zamani. Walipokuwa na akili yenye juhudi na mioyo hodari, vijana

hawa wakapata haraka maarifa ambayo kwa wakati mrefu hakuna mtu aliweza kushindana

nao. Watu wakapata katika mafundisho mapya mambo ambayo yalileta matakwa ya roho zao,

na wakageuka kutoka kwa wale waliowalea kwa wakati mrefu na maganda ya bure ya ibada

za sanamu na maagizo ya wanadamu.

Wakati mateso yalipoamshwa juu ya waalimu wa ukweli, wakafuata agizo hili la Kristo:

“Na wakati wanapo watesa ninyi katika mji huu, kimbilieni kwa mji mwengine.” Matayo

10:23. Wakimbizi wakapata mahali mlango karibu ulifunguka kwao, na waliweza kuhubiri

Kristo, wakati mwengine ndani ya kanisa ao katika nyumba ya faragha ao mahali pa wazi.

Kweli ikatawanyika kwa uwezo mkubwa usio wa kuzuia.

Ni kwa bure watawala wa kanisa na wa serkali walitumia kifungo, mateso, moto, na

upanga. Maelfu ya waaminifu wakatia muhuri kwa imani yao kwa kutumia damu yao, na

75

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!