Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Kupinga ya Kiprotestanti

Waalimu hawa wa bidii wakajifanya wenye kutawaliwa na maono, kuona kuwa kila

mawazo na mvuto kama sauti ya Mungu. Wengine hata wakachoma Biblia zao. Mafundisho

ya Munzer yakakubaliwa na maelfu. Kwa upesi akatangaza kwamba kutii watawala, ilikuwa

kutaka kumtumikia Mungu na Beliali. Mafundisho ya uasi ya Munzer yakaongoza watu

kuvunja mamlaka yote. Sherehe za kutisha za upinzani zikafuata, na mashamba ya Ujeremani

yakajaa na damu.

Maumivu Makuu ya Roho Sasa Yakalemea Juu ya Luther

Wana wa wafalme wa upande wa Papa wakatangaza kwamba uasi ulikuwa tunda ya

mafundisho ya Luther. Mzigo huu hakupashwa lakini kuleta huzuni kubwa kwa Mtengenezaji

kwamba kisa cha kweli kilipaswa kuaibishwa kwa kuhesabiwa pamoja na ushupavu wa dini

wa chini zaidi. Kwa upande mwengine, waongozi katika uasi walimchukia Luther. Hakukana

madai yao kwa maongozi ya Mungu tu, bali akawatangaza kuwa waasi juu ya mamlaka ya

serkali. Katika uhusiano wakamshitaki yeye kuwa mdai wa msingi.

Roma ilitumainia kushuhudia muanguko wa Matengenezo. Na wakamlaumu Luther hata

kwa ajili ya makosa ambayo alijaribu kwa bidii sana kusahihisha. Kundi la ushupavu, likadai

kwa uongo kwamba lilitendewa yasiyo haki, wakapata huruma ya hesabu kubwa ya watu na

kuzaniwa kuwa kama wafia dini. Kwa hiyo wale waliokuwa katika kupingana na

Matengenezo wakahurumiwa na kusafishwa. Hii ilikuwa kazi ya roho ya namna moja ya uasi

wa kwanza uliopatikana mbinguni.

Shetani hutafuta kila mara kudanganya watu na kuwaongoza kuita zambi kuwa haki na

haki kuwa zambi. Utakatifu wa uongo, utakaso wa kuiga, ungali ukionyesha roho ya namna

moja kama katika siku za Luther, kugeuza mafikara kutoka kwa Maandiko na kuongoza watu

kufuata mawazo na maono kuliko sheria za Mungu. Kwa uhodari Luther akatetea injili kwa

mashambulio. Pamoja na Neno la Mungu akapigana juu ya mamlaka ya manyanganyi ya

Papa, wakati aliposimama imara kama mwamba kupinga ushupavu uliojaribu kujiunga na

Matengenezo.

Pande zote za upinzanihuweka pembeni Maandiko matakatifu, kwa faida ya hekima ya

kibinadamu kutukuzwa kawa chemchemi ama asili ya ukweli. Kufuata akili za kibinadamu

kwa kusudi lakuabudu kama Mungu na kufanya hii kanuni kwa ajili ya dini. Kiroma kinadai

kuwa na uongozi wa Mungu ulioshuka kwa mustari usiovunjika toka kwa mitume na kutoa

nafasi kwa ujinga na uchafu vifichwe chini ya agizo la “mitume”. Maongozi yaliyodaiwa na

Munzer yalitoka kwa mapinduzi ya mawazo. Ukristo wa kweli hukubali Neno la Mungu kama

jaribio la maongozi yote.

Kwa kurudi kwake Wartburg, Luther akatimiza kutafsiri Agano Jipya, na injili ikatolewa

upesi kwa watu wa Ujeremani katika lugha yao wenyewe. Ufasiri huu ukapokewa kwa furaha

kubwa kwa wote waliopenda ukweli.

74