Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Kupinga ya Kiprotestanti

na ugomvi; lakini kwa namna matisho yao yalizidi, ndipo furaha yangu iliongezeka...

Wamekwisha kuharibu heshima (sifa) yangu na mwenendo wangu. ... Kuhusu roho yangu,

hawawezi kuikamata. Yeye anayetaka kutangaza neno la Kristo ulimwenguni, inampasa

kutazamia kifo wakati wowote.”

Akari ya kufika kwa Luther huko Augsburg kukaleta kushelewa kukubwa kwa mjumbe

wa Papa. Mpinga mafundisho ya dini anayeamsha ulimwengu akaonekana sasa kuwa chini

ya uwezo wa Roma; hakupaswa kuponyoka. Mjumbe alikusudia kulazimisha Luther kukana,

ao isipowezekana alazimishe kwenda Roma kufuata nyayo ya Huss na Jerome. Mjumbe wa

Papa akatuma watu wake kumwambia Lutter afike bila ahadi ya ulinzi salama wa mfalme na

matumaini yake mwenyewe wema wake. Kwa hiyo mtengenezaji akakataa. Hata wakati

alipopata ahadi ya ulinzi wa mfalme mkuu ndipo akakubali kuonekana mbele ya mjumbe wa

Papa. Kama mpango wa busara, watu wa Roma wakakusudia kumpata Luther kwa njia ya

kujioyesha kama wapole.

Mjumbe akajionyesha kawa rafiki mkubwaa, lakini akaomba kwamba Luther ajitoe kabisa

kwa kanisa na kukubali kila kitu bila mabishano wala swali. Luther, kwa kujibu, akaonyesha

heshima yake kwa ajili ya kanisa, mapenzi yake kwa ajili ya ukweli, kuwa tayari kwa kujibu

makatazo yote kuhusu yale aliyoyafundishwa, na kuweka mafundisho yake chini ya uamuzi

wa vyuo vikubwa (universites). Lakini alikataa juu ya mwendo wa askofu katika

kummulazimisha kukana bila kuonyesha na kuhakikisha kosa lake.

Jibu moja tu lilikuwa, “uKane, ukane”! Mtengenezaji akaonyesha kwamba msiimamo

wake unakubaliwa na Maandiko. Hakuweza kukana ukweli. Mjumbe, aliposhindwa kujibu

kwa mabishano ya Luther, akamulemeza na zoruba ya laumu, zarau, sifa ya uongo maneno

kutoka kwa kiasili (traditions), na mezali (maneno) ya Wababa, akikatalia Mtengenezaji

nafasi ya kusema. Luther mwishowe, bila kupenda, akamupa ruhusa ya kutoa jibu lake kwa

maandiko.

Akasema,akiandika kwa rafiki, “Mambo yaliyoandikwa ingeweza kutolewa kwa mawazo

ya wengine; na jambo la pili, mtu anakuwa na bahati nzuri sana ya kutumika kwa hofu nyingi,

kama si kwa zamiri, ya bwana wa kiburi na wa kusema ovyo ovyo ambaye njia ingine

angeshinda kwa kutumia maneno yake makali.” Kwa mkutano uliofuata, Luther akaonyesha

maelezo mafupi na ya nguvu ya mawazo yake, yanayoshuhudiwa na Maandiko. Kartasi hii,

baada ya kusoma kwa sauti nguvu, akaitoa kwa askofu, naye akaitupa kando kwa zarau,

kuitangaza kuwa mchanganyiko wa maneno ya bure na mateuzi yasiyofaa. Sasa Luther

akakutana na askofu wa kiburi kwa uwanja wake mwenyewe--mambo ya asili na mafundisho

ya kanisa--na kuangusha kabisa majivuno yake.

Askofu akapoteza kujitawala kote na katika hasira akapandisha sauti, “ukane! ao

nitakutuma Roma”. Na mwishowe akatangaza, katika sauti ya kiburi na hasira, “uKane, ao

usirudi tena.” Mtengenezaji kwa upesi akaondoka pamoja na rafiki zake, hivyo kutangaza

wazi kwamba asingoje kwake kwamba atakana. Hili si jambo ambalo askofu alilokusudia.

52