12.04.2023 Views

Kupinga ya Kiprotestanti

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Kupinga ya Kiprotestanti

Sura 41. Dunia katika Uharibifu

Wakati sauti ya Mungu inapogeuza utumwa wa watu wake, pale panakuwa na muamko

wa kutisha wa wale waliopoteza vyote katika vita kubwa ya maisha. Kupofushwa na

madanganyo ya Shetani watajiri wakajisifu wenyewe kwa ukuu wao kwa wale wasiofanikiwa

sana. Lakini hawakujali kulisha wenye njaa, kuvika wale waliokuwa unchi, kufanya kwa haki,

na kupenda rehema. Sasa wameondolewa vyote vilivyowafanya kuwa wakubwa na

wameachwa ukiwa (maskini). Wanatazama kwa hofu juu ya kuangamia kwa sanamu zao.

Wameuzisha nafsi zao kwa ajili ya anasa ya dunia na hawakuwa watajiri kwa Mungu. Maisha

yao ni ya kushindwa, anasa zao zimegeuka kuwa uchungu. Faida ya maisha yao yote imepotea

kwa wakati moja. Watajiri wanalilia kuangamia kwa nyumba zao kubwa, kutawanyika kwa

zahabu yao na feza, na hofu ya kwamba wao wenyewe wanapashwa kuangamia pamoja na

sanamu zao. Waovu wanaomboleza ya kwamba matokeo ni vile inavyokuwa, lakini hawatubu

kwa maovu yao.

Mhubiri aliyefanya ukweli kwa kafara makusudi ya kupata upendeleo wa watu sasa

anatambua mvuto wa mafundisho yake. Kila mustari ulioandikwa, kila neno lililotamkwa

lililoongoza watu kudumu katika kimbilio la uwongo limetawanya mbegu: na sasa anatazama

mavuno. Bwana anasema: “Ole wao wachungaji, wanaoharibu na kutawanya kondoo za

malisho yangu! ... Angalieni, nitaleta juu yenu uovu wa matendo yenu”. “kwa uwongo

mumehuzunisha moyo wao walio haki, nisiowahuzunisha; nakutia nguvu mikono ya mwovu,

hata asigeuke toka njia yake ya uovu, na kuponyeshwa hai”. Yeremia 23:1,2; Ezekieli 13:22.

Wahubiri na watu wanaona ya kuwa wameasi juu ya Muumba wa sheria yote ya haki.

Kuweka pembeni maagizo ya Mungu kulitoa mwinuko kwa maelfu ya nguvu za uovu, hata

dunia ikawa mfereji moja mkubwa wa zambi. Hakuna lugha inayoweza kueleza tamaa ya

wasiowaaminifu wanapotazama wale walivyopoteza milele--uzima wa milele.

Watu wanashitakiana wao kwa wao kwa ajili ya kuwaongoza kwa uharibifu, lakini wote

wanaunganika kwa kukusanya hukumu yao ya uchungu mkubwa juu ya wachungaji

wasiokuwa waaminifu waliotabiri “maneno ya laini” (Isaya 30:10), walioongoza wasikilizaji

wao kufanya ukiwa sheria ya Mungu na kutesa wale wangeishika kama takatifu.

“Tumepotea”! wameomboleza, “na ninyi ndio munaokuwa sababu yenyewe”. Mikono

iliyowatawaza zamani kwa heshima itanyanyuliwa kwa ajili ya uharibifu wao. Po pote

kunakuwa vita na umwangaji wa damu.

Mwana wa Mungu na wajumbe wa mbinguni wamekuwa katika vita pamoja na muovu,

kwa kuonya, kuangazia, na kuokoa wana wa watu. Sasa wote wamefanya mipango

(makusudi) yao; waovu wameungana kabisa na Shetani katika vita kupigana na Mungu.

Mabishano si ya Shetani peke yake, lakini pamoja na watu. “Bwana ana mashindano na

mataifa”. Yeremia 25:31.

Malaika wa Mauti

267

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!