Kupinga ya Kiprotestanti

newcovenantpublicationsintl
from newcovenantpublicationsintl More from this publisher
12.04.2023 Views

Kupinga ya Kiprotestanti yake wenyewe; na ataleta taabu kwa wengine, na kuongoza watu kuamini ya kama ni Mungu ndiye anayewatesa. Anapotokea kama tabibu mkuu anayeweza kuponya magonjwa yao yote, Shetani ataleta ugonjwa na msiba hata miji ya watu waingie kwa maangamizi. Katika misiba baharini na inchini, katika mateketeo makubwa, katika tufani kali na mvua ya mawe, katika zoruba, garika, kimbunga, mawimbi ya maji kujaa, na tetemeko la inchi, katika namna maelfu, Shetani anatumia uwezo wake. Anaondolea mbali mavuno yenye kukomea yote, na njaa na taabu hufuata. Hugawanya mawaa ya mauti angani, na maelfu huangamia. Ndipo mdanganyifu mkubwa atashawishi watu kutwika taabu zao zote kwa wale wanaokuwa na utii kwa amri za Mungu ni laumu la daima kwa wakosaji. Itatangazwa ya kama watu wanamkosea Mungu juu ya mvunjo wa siku ya kwanza, ya kwamba zambi hii imeleta misiba ambayo haitakoma hata kushika kwa siku ya kwanza kutakapo kazwa kabisa. “Wale wanaoharibu heshima kwa ajili ya siku ya kwanza wanazuia kurudishwa kwa majaliwa ya Mungu na kufanyikiwa”. Kwa hivyo mashitaki yaliyofanywa ya zamani juu ya watumushi wa Mungu yatakaririwa. “Wakati Ahaba alipomuona Eliya, Ahaba akamwaambia: Ni wewe mwenye kutaabisha Israeli”? 1 Wafalme 18:17,18. Uwezo wa kufanya miujiza utatumia mvuto wake juu ya wale wanaomtii Mungu kuliko watu. “Pepo” watatangaza ya kama Mungu amewatuma kusadikisha wanaokataa siku ya kwanza kwa kosa lao. Watalilia uovu mkubwa ulimwenguni na kusaidia ushuhuda wa waalimu wa dini ya kama hali iliopoteza cheo cha mafundisho imaletwa na ukufuru wa siku ya kwanza Chini ya utawala wa Roma, wale walioteseka kwa ajili ya habari njema walishitakiwa kama watenda maovu katika mapatano pamoja na Shetani. Ndivyo hivyo itakavyokuwa sasa. Shetani ataletea wale wanaoheshimu sheria ya Mungu kushitakiwa kuwa watu wanaoleta hukumu duniani. Kwa njia ya kutisha anajaribu kutawala zamiri, anasukuma watawala wa dini na wa dunia kukaza sheria za kibinadamu katika kuasi sheria ya Mungu. Wale wanaoheshimu Sabato ya Biblia watashitakiwa kuwa adui wa sheria na ukimya, kuvunja amri za maana za kijamii, kuleta machafuko ya mambo ya utawala na makosa, na kuita hukumu za Mungu inchini. Watashitakiwa juu ya chuki kwa serekali. Wajumbe wanaokana kanuni ya sheria ya Mungu wataonyesha kwa mimbara shuguli ya utii kwa utawala wa dunia. Katika vyumba vikubwa vya kufanya sheria na baraza za hukumu, wanaoshika amri watahukumiwa. Rangi ya uwongo itatolewa kwa maneno yao; maana mbaya kuliko itawekwa kwa mashitaki yao. Wakuu wa kanisa na serekali watajiiunga kwa kushawishi ao kushurutisha wote kuheshimu siku ya kwanza. Hata katika watawala wa Kiamerika wenye uhuru na wenye kufanya sheria watakubali matakwa ya watu wote kwa ajili ya sheria ya kukaza kushika siku ya kwanza. Uhuru wa zamiri ambao umegaramishwa kwa kafara kubwa hauta heshimiwa tena. Katika kuja kwa karibu kwa shindano tutaona kuonyesha kwa mfano maneno ya nabii, 240

Kupinga ya Kiprotestanti “Joka akakasirikia yule mwanamke, akakwenda zake kufanya vita juu ya wazao wake waliobaki, wanaoshika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo”. Ufunuo 12:17. 241

Kupinga ya Kiprotestanti

“Joka akakasirikia yule mwanamke, akakwenda zake kufanya vita juu ya wazao wake

waliobaki, wanaoshika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo”. Ufunuo 12:17.

241

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!