12.04.2023 Views

Kupinga ya Kiprotestanti

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Kupinga ya Kiprotestanti

Sura 2. Ubatizo wa Moto

Yesu alifunulia wanafunzi wake maarifa ya watu wake tangu wakati ambao alipaswa

kuchukuliwa kutoka kwao, hata kurudi kwake katika uwezo na utukufu. Kuingia ndani sana

ya wakati ujao, jicho lake likaona zoruba kali zilipaswa kupiga juu ya wafuasi wake kwa

miaka iliyokuwa karibu ya mateso. Tazama Matayo 24:9,21,22. Wafuasi wa Kristo

wanapaswa kupitia kwa njia ya namna moja ya laumu na mateso ambayo Bwana wao alipitia.

Uadui juu ya Mkombozi wa ulimwengu ulipaswa kuonekana juu ya wote wanaopaswa

kuamini jina lake.

Upagani ulifahamu kwamba injili ikishinda, hekalu na mazabahu zake yalipaswa

kuondolewa; kwa sababu hii mioto ya mateso ikawashwa. Wakristo walinyanganywa mali

zao na kufukuzwa nyumbani mwao. Hesabu kubwa ya wenye cheo na watumwa, watajiri na

masikini, wenye elimu na wajinga, waliuawa bila huruma.

Ya kianzia chini ya utawala wa Nero, mateso yakaendelea kwa karne nyingi. Wakristo

walitangazwa kwa uongo kuwa ni wao walioleta njaa, tauni, na matetemeko ya inchi.

Wachongezi wakasimama tayari, kwa ajili ya faida tu, kwa kusaliti wasio na kosa kama waasi

na tauni kwa jamii. Hesabu kubwa wakatupwa kwa nyama wa pori ama kuchomwa wahai

katika viwanja vya michezo (amphitheatres). Wengine wakasulubiwa; wengine wakafunikwa

na ngozi za nyama wa pori na kusukumwa kwa nguvu katika uwanja (arena) wa kuchezea ili

kupasuliwa kwa waimbwa. Kwa siku kuu za wote makutano mengi sana yalikusanyika kwa

kufurahisha macho na kusalimia walioumizwa kwa kifo na kuwachekeleya na kushangilia.

Wafuasi wa Kristo walilazimishwa kutafuta maficho katika mahali pa ukiwa na pekee.

Chini ya milima inje ya muji wa Roma, vyumba virefu vilifunuliwa katika inchi na miamba

kwa maelfu ngambo ya pili ya kuta za mji. Ndani ya makimbilio haya ya chini ya udongo

wafuasi wa Kristo wakazika wafu wao, na hapo pia walipaswa kukimbilia, walipozaniwa

maovu na kugombezwa, walipata makao. Wengi wakakumbuka maneno ya Bwana wao,

kwamba kama wakiteseka kwa ajili ya Kristo, inafaa wafurahi sana. Zawadi yao itakuwa

kubwa mbinguni, kwa maana ndivyo walivyotesa manabii waliokuwa mbele yao. Tazama

Matayo 5:11,12.

Nyimbo za ushindi zikapanda katikati ya ndimi za moto zenye kutatarika. Kwa imani

waliona Kristo na malaika wakiwatazama pamoja na usikizi mwingi sana na kutazama

kusimama imara kwao pamoja na kibali. Sauti ikaja kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu:

“Uwe mwaminifu mpaka kufa, nami nitakupa taji ya uzima”. Ufunuo 2:10.

Nguvu za Shetani kwa kuharibu kanisa la Kristo kwa mauaji zilikuwa bure. Watumishi

wa Mungu waliuawa, lakini injili iliendelea kutawanyika na wafuasi wake kuongezeka.

Mkristo mmoja akasema: “Tunazidi kuongezeka kwa hesabu namna munavyozidi kutuuwa,

damu ya Wakristo ni mbegu”.

12

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!