12.04.2023 Views

Kupinga ya Kiprotestanti

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Kupinga ya Kiprotestanti

angeonekana kuja kutakasa dunia kwa kuharibu zambi na wenye zambi, na kubariki watu

wake wanaomungojea kwa kuwapa kutokufa. Siku ya kumi ya mwezi wa saba, Siku kuu ya

Upatanisho, wakati wa kutakaswa kwa mahali patakatifu, ambao katika mwaka 1844

ulianguka kwa tarehe ya makumi mbili na mbili ya Oktoba, ilizaniwa kama ni wakati wa kuja

kwa Bwana. Siku 2300 zingemalizika wakati wa masika, na mwisho ikaonekana kuwa wazi

bila ubishi.

“Kilio cha Usiku wa Manane”

Maneno yakawa na hakikisho la nguvu, na “kilio cha usiku wa manane” kikasikiwa kwa

maelfu ya waaminifu. Kama mawimbi, tukio hili likazambaa kwa nguvu toka mji kwa mji,

kijiji kwa kijiji. Ushupavu ukatoweka kama baridi kali ya alfajiri kabla ya jua kutokea. Kazi

ilikuwa ya namna moja na ile ya nyakati za kurudi kwa Bwana ambako miongoni mwa Israeli

wa zamani walifuata ujumbe wa karipio kutoka kwa watumishi wake. Hapo kulikuwa furaha

nyingi sana, lakini Zaidi uchunguzi mwingi wa moyo, ungamo la zambi, na kuacha dunia.

Hapo kulikuwa kujitoa wakfu kwa Mungu.

Kwa miendo yote ya dini tangu siku za mitume, hakuna mojawapo yaliojiepusha zaidi

kwa upungufu wa kibinadamu na werevu wa Shetani kuliko ile iliokuwa kwa wakati wa

masika ya mwaka 1844. Kwa mwito, “Tazama bwana arusi anakuja,” wale waliokuwa

wakingojea “wakaamka, wakatengeneza taa zao”; wakajifunza Neno la Mungu kwa usikizi

mkuu ambao haukuwako mbele. Hawakukuwa wenye vipawa zaidi, bali wenye kuwa wenye

unyenyekevu zaidi na wenye bidii, waliokuwa wa kwanza kutii mwito. Wakulima wakaacha

mavuno yao katika mashamba, wafundi wa mashine wakaacha vyombo vyao na kwa furaha

wakaenda kutoa maonyo. Makanisa kwa kawaida yakafunga milango yao juu ya ujumbe huu,

na kundi kubwa la wale walioukubali wakajitenga kwao.

Wasiosadiki waliokusanyika kwa mikutano ya Waadventiste wakaona uwezo wa

kusadikisha ukihuzuria ujumbe, “Tazama, bwana arusi anakuja!” Imani ikaleta majibu kwa

maombi. Kama manyunyu ya mvua juu ya inchi yenye kiu, Roho ya neema akashuka juu ya

watafutao kwa bidii. Wale waliotazamia upesi kusimama uso kwa uso pamoja na Mkombozi

wao wakaona furaha kubwa. Roho Mtakatifu akalainisha moyo.

Wale waliokubali ujumbe wakafikia wakati ambao walitumainia kukutana na Bwana wao.

Wakaomba sana mtu kwa mwenzake. Wakakutana mara kwa mara katika mahali pa uficho

kushirikiana pamoja na Mungu, na sauti ya maombezi ikapanda mbinguni kutoka

mashambani na vichakani. Hakikisho la kibali cha Mwokozi yalikuwa ya lazima zaidi kwao

kuliko chakula cha kila siku, na kama wingu lilitia giza katika akili zao, hawakutulia hata

walipoona ushuhuda wa neema ya rehema.

Kukatishwa Tamaa Tena

Lakini tena, wakati wa kutazamia ukapita, na Mwokozi wao hakutokea. Sasa wakaona

kama Maria alivyofanya wakati alipokuja kwa kaburi la Mwokozi na kukuta linapokuwa

164

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!