Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Kupinga ya Kiprotestanti

Katika matengenezo adui zake wakashitakiwa maovu ya ushupavu juu ya wale waliokuwa

wakiomba sana kukataa ushupavu. Mwendo wa namna ileile ulikuwa ukifuatwa na wapinzani

wa kazi ya kiadventiste. Hawakutoshelewa na kuzidisha makosa ya ushupavu, wakaeneza

taarifa ambazo hazikuwa hata na uhusiano kidogo wa kweli. Amani yao ilikuwa ikisumbuliwa

na kutangazwa kwa Kristo kuwa mlangoni. Waliogopa ingeweza kuwa kweli, huku

wakatumaini kwamba haikuwako. Hii ilikuwa siri ya vita yao kwa kupinga Waadventiste.

Mahubiri ya ujumbe wa malaika wa kwanza yalielekea mara kukomesha ushupavu. Wale

walioshirikiana kwa kazi hizi kubwa walikuwa katika umoja; mioyo yao ilijazwa na upendo

wa mtu kwa mwenzake na kwa ajili ya Yesu, ambaye walimtazamia kumwona upesi. Imani

moja, tumaini la baraka moja, wakahakikisha ngabo juu ya mashambulio ya Shetani.

Kosa Linasahihishwa

“Basi wakati bwana arusi alipokawia, wao wote wakasinzia na kulala usingizi. Lakini saa

sita ya usiku kulikuwa kelele: Tazama bwana arusi anakuja! tokeni kukutana naye.” Katika

wakati wa jua kali wa mwaka 1844 ujumbe ukatangazwa katika maneno ya Maandiko kabisa.

Kile kilichoongoza kwa maendeleo haya kilikuwa ni uvumbuzi kwamba amri ya Artasasta

kwa ajili ya kurudishwa kwa Yerusalema, ambayo ilisaidia kujua mwanzo wa hesabu ya siku

2300, ikafanyika katika masika ya mwaka wa 457 B.C., na si kwa mwanzo wa mwaka, kama

ilivyoaminiwa. Hesabu kutoka masika ya mwaka 457, miaka 2300 ikamalizika wakati wa

masika ya mwaka 1844. Mifano ya Agano la Kale pia ilielekeza kwa wakati wa masika kama

wakati ambao “kutakaswa kwa mahali patakatifu” kulipaswa kufanyika.

Kuchinjwa kwa Kondoo wa Pasaka kulikuwa ni kivuli cha mauti ya Kristo, mfano

ulitimilika, si kwa tukio tu, bali na kwa wakati. Kwa siku ya kumi na ine ya mwezi wa kwanza

wa Wayuda, siku ile kabisa na mwezi ambapo kwa karne nyingi kondoo wa Pasaka alikuwa

akichinjwa, Kristo akaanzisha karamu hiyo ambayo ilikuwa kwa kukumbuka mauti yake

mwenyewe “Mwana-kondoo wa Mungu.” Kwa usiku uleule akakamatwa kwa kusulibiwa na

kuuawa.

UNABII WA 2300 SIKU / MIAKA

161