Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Kupinga ya Kiprotestanti

kungali Wayahudi, wajinga ambao hawakujua tabia na kazi ya Kristo. Na watoto

hawakufurahia nuru ambayo wazazi wao waliikataa kwa zarau katika mahubiri ya mitume,

Mungu aliwezesha nuru kuangaza juu yao. Waliona namna gani unabii ulitimia, si katika

kuzaliwa tu na maisha ya Kristo, bali katika kifo chake na ufufuo. Watoto hawakuhukumiwa

kwa ajili ya zambi za wazazi; lakini wakati walipokataa nuru ingine waliopewa, wakawa

washiriki wa zambi za wazazi na wakajaza kipimo cha uovu wao.

Wayahudi katika ugumu wa mioyo yao wakakataa shauri la mwisho la rehema. Ndipo

Mungu akaondoa ulinzi wake kwao. Taifa likaachwa kwa utawala wa mwongozi lililo

mchagua. Shetani akaamsha tamaa kali sana na mbaya kuliko za roho. Watu wakakosa akili

wakatawaliwa na nguvu na hasira ya upofu, ya shetani katika ukaidi wao. Marafiki na ndugu

wakasalitiana wao kwa wao. Wazazi wakaua watoto wao, na watoto wazazi wao. Watawala

hawakuwa na uwezo wa kujitawala wao wenyewe. Tamaa ikawafanya kuwa wajeuri.

Wayahudi wakakubali ushuhuda wa uwongo kwa kuhukumu Mwana wa Mungu asiye na

kosa. Sasa mashitaki ya uwongo yakafanya maisha yao kuwa si ya haki. Kuogopa Mungu

hakukuwashitusha tena. Shetani alikuwa akiongoza taifa.

Waongozi wa makundi ya upinzani wakaanguka mmoja juu za mwingine na kuwa bila

huruma. Hata utakatifu wa hekalu haukuweza kuzuia ukali wao wa kutisha. Mahali patakatifu

pakanajisiwa na miili ya waliouawa. Lakini washawishi wa kazi hii ya kishetani walitangaza

kwamba hawakuwa na hofu yo yote kwamba Yerusalema ingeharibiwa! Ulikuwa mji wa

Mungu. Hata wakati majeshi ya Waroma walipozunguka hekalu, makundi yalisimama imara

kwa wazo kwamba Aliye juu angejitia kati kwa kushinda kwa maadui wao. Lakini Israeli

alitupia mbali ulinzi wa Mungu, na sasa hakuwa na ulinzi.

Alama za Musiba

Unabii uliyotolewa na Kristo kwa ajili ya uharibifu wa Yerusalema yalitimia wazi wazi.

Dalili na maajabu yalitokea. Kwa muda wa miaka saba mtu aliendelea kupanda na kutelemuka

katika njia za Yerusalema, kutangaza misiba itakayokuja. Kiumbe hiki cha ajabu kilifungwa

gerezani na kuazibiwa, lakini kwa matusi mabaya hayo akajibu tu, “Ole, ole kwa

Yerusalema”! Aliuawa katika mitego ya maadui aliyotabiri.

“Hakuna Mkristo hata mmoja aliyeangamia katika uharibifu wa Yerusalema. Baada ya

Waroma chini ya uongozi wa Cestius walipozunguka mji, kwa gafula wakaacha mazingiwa

wakati kila kitu kilionekana kuwa cha kufaa kwa shambulio. Mkuu wa Roma akaondoa

majeshi yake bila sababu ndogo wazi. Alama iliyoahidiwa ilitolewa kwa Wakristo waliokuwa

wakingojea. Luka 21:20,21.

Mambo yakafanyika kwa namna ambayo hata Wayahudi ama Waroma hawakupinga

kukimbia kwa Wakristo. Katika kushindwa kwa Cestius, Wayahudi wakafuata, na wakati

majeshi hayo mawili yalipokutana, Wakristo popote katika inchi waliweza kufanya kimbilio

lao bila kusumbuliwa mahali pa salama, kwa mji wa Pella.

8