Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Kupinga ya Kiprotestanti

Sura 14. Ukweli Unaendelea Katika Uingereza

Wakati Luther alipokuwa akifungua Biblia iliyofungwa kwa watu wa Ujeremamy,

Tyndale akasukumwa na Roho wa Mungu kufanya tendo lilelile katika Uingereza. Biblia ya

Wycliffe ilitafsiriwa kutoka kwa Kilatini, ambamo mulikuwa makosa mengi. Bei ya kurasa

zilizoandikwa ilikuwa juu sana na kwa hiyo mtawanyiko wake ulikuwa wa shida.

Kwa mwaka 1516, kwa mara ya kwanza Agano Jipya likachapwa katika lugha ya asili ya

Kigiriki. Makosa mengi ya tafsiri ya kwanza yakasahihishwa, na maana yakarudishwa vizuri

zaidi. Nakala zile zikaletea watu waliojifunza ufahamu bora kwa kweli na zikatoa mwendo

mpya kwa kazi ya matengenezo. Lakini sehemu kubwa ya watu walikosa Neno la Mungu.

Tyndale alipaswa kutimiza kazi ya Wycliffe katika kutoa Biblia kwa watu wa inchi yake.

Akahubiri bila woga mambo ya hakika yake. Kwa tangazo la Papa kwamba ni kanisa

lililotoa Biblia, na ni kanisa pekee linaloweza kuieleza, Tyndale akajibu: “Kamwe

haukutupatia Maandiko, ni wewe uliyeyaficha kwetu; ni wewe uliyewachoma wale

walioyafundisha, na kama ungaliweza, ungalichoma Maandiko yenyewe.”

Mahubiri ya Tyndale yakaamsha usikizi kubwa. Lakini mapadri wakajitahidi kuharibu

kazi yake. “Ni kitu gani kinapaswa kufanywa?” akapaza sauti. “Siwezi kuwa po pote. Ee!

kama Wakristo wangalikuwa na Maandiko matakatifu katika lugha yao wenyewe,

wangaliweza wao wenyewe kushindana na wenye kutumia maneno madanganyifu hawa. Bila

Biblia haiwezekani kuimarisha watu katika kweli.”

Nia mpya ikaja katika mawazo yake. “Injili haitasema lugha ya Ungereza miongoni

mwetu? ... Kanisa linapaswa kuwa na nuru ndogo kwa wakati wa azuhuri kuliko wakati wa

mapambazuko yake? ... Wakristo wanapashwa kusoma Agano Jipya katika lugha yao ya

kuzaliwa.” Ila tu kwa njia ya Biblia watu waliweza kufikia ukweli.

Mtaalamu mmoja wa Katoliki katika mabishano pamoja naye akapaza sauti ya mshangao,

“Ingekuwa vema kutokuwa na sheria za Mungu kuliko kukosa zile za Papa.” Tyndale akajibu,

“Ninazarau Papa na sheria zake zote; na kama Mungu angenipatia maisha, kabla ya miaka

mingi nitawezesha kijana anayeongoza jembe la kukokotwa na ngombe kufahamu Maandiko

zaidi kuliko ninyi.”

Tyndale Anatafsiri Agano Jipya kwa Kiingereza

Alipofukuzwa nyumbani kwa ajili ya mateso, akaenda Londoni na huko kwa mda

akatumika bila kizuizi. Lakini tena Wakatoliki wakamlazimisha kukimbia. Uingereza wote

ukaonekana wenye kufungwa kwake. Katika Ujeremani akaanza uchapaji wa Agano Jipya

kwa lugha ya kingereza. Alipokatazwa kuchapa katika mji moja, akaenda kwa mji mwengine.

Mwishowe akasafiri kwenda Worms, ambako, miaka michache mbele, Luther alipotetea injili

mbele ya baraza. Katika mji ule kulikuwa rafiki wengi wa Matengenezo. Vitabu elfu tatu vya

Agano Jipya vikachapwa, na mchapo mwengine ukafuata.

97